MITIHANI
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
MAPAMBANO OPEN
SCHOOL
JARIBIO LA MAALUM
WIKI
KIDATO CHA
TANO
KISWAHILI-2
MUDA : SAA 2:30 Oktoba,12,2018
MAELEKEZO
1. Karatasi
hii ina
jumla ya maswali tisa (9)
2.
Jibu swali moja kila sehemu na kila
swali lina alama 20
3.
Soma swli kwa mkini kabla ya kuanza kujibu
4. Andika jina lako vizuri na mchepuo
wako
SEHEMU A
(Alama 20)
FASIHI KWA UJUMLA
1.
‘Dhana
ya uhuru wa mwandishi wa kazi ya fasihi kwa nchi za Afrika bado ni
kizungumkuti’.thibitisha dai hili kwa kutoa hoja (nne)mifano ya waandishi
mbalimbali pamoja na kazi zao
2.
“Wasanii wengi wa
fasihi hutumia wahusika wasio binadamu kwa lengo la kisanaa’’.Kwa hoja mifano
onesha sababu za kutumia wahusika wasiobinadamu katika kazi ya sanaa.
SEHEMU B (
Alama 20 )
Usiku
Utakapokwisha -Mbunda Msokile
Mfadhili -Hussein Tuwa
3.
“Wasanii wengi hubuni jina la kitabu
linalosawiri yalioyomo ndani ya kitabu husika”.Kwa kutoa hoja nne kwa kila
riwaya jadili dai hili kwa kurejelea Tanzania ya leo,tumia riwaya mbili.
4.
Wasanii
wa kazi ya fasihi hutumia mbinu za kifani ili kujenga ,kuzipa mvuto na kuleta
radha tamu kwa wasomaji wa kazi zao.Fafanua mbinu tano ( 5 ) za kifani
zilizotumika katika kila tamthiliya ,tumia tamthiliya mbili ulizosoma.
SEHEMU C
(Alama 20)
TAMTHILIYA
Morani -E.Mbogo
Kivuli
Kinaishi
-S.Mohamed
Nguzo Mama -P.Mhando
5.“Suala la ujenzi wa nchi yenye haki na usawa si suala lelemama”. Thibitisha dai hili kwa hoja nne (4) kwa kila Tamthiliya,Tumia tamthiliya
mbili ulizosoma.
6 . Ubunifu wa kisanaa ni nguzo muhimu sana katika kufikisha ujumbe kwa jamii yeyote ile.Kwa kutumia Tamthiliya mbili ulizosoma jadili vipengele vya fani vilivyotumiwa na mwandishi kufikisha ujumbe.
SEHEMU E
(Alama 20 )
USANIFU WA
MAANDISHI
7.Soma
habari ifuatayo kisha eleza mbinu za kisanaa zilizotumika;
Kulikuwa kimya kwa muda.Wote wakanyamaza.Lakini ghafla
mtu mwingine akashtuka na kusema, “Hawana shida bwana…..”Uzuri wote wa UDA
ulisahauliwa huko.Maskini UDA! Gari halikutokea.Baada ya muda kidogo ikasikika
sauti kali “pyaaaa!” Aligeuza shingo nyuma hakuna kitu.Kulia,hapana.Ni Kushoto
mwa kijumba kimoja karibu na kituo cha
basi waliposimama.Kuna mtu mmoja alikuwa anagalagala,baiskeli kule!! Mguu
juu!!.
Ondoa injinikiuno yako we! Blad ful!” Alisikia
mtu mwenye gari lililomgonga akifoka.Akalikodolea macho kwa nguvu na hasira
gari hilo lililokuwa likilamba lami na kuyamaliza magurudumu yake .Limekwenda halina
namba.Hakujua……
Mhuni mmoja naye akamshambulia aliyegongwa
,Mwanaharamu we!!.Huangalii unapopita?.Eee? Unafikiri mkokoteni huo?,Ungefia
mbali huko.Stupid!” Lupyana,akaguna akashangaa…….machozi yakamtwaa machoni. Kila mtu ana matatizo
yake”,aliwaza.Mji una namna mbalimbali ya kuwachachia watu.Simba akizidiwa hula
majani.Hatimaye gari la UDA
la kwanza lililotarajiwa kuwachukua watu kutoka kona ya Dzengelendete
kuwapeleka Lupembe mjini
likaja.Mikikimikiki ikaanza! Watu walisukumana! Kila mtu aligombea nafasi
mithili ya mbuzi wanaoswagwa kuingia zizini.Katika harakati hizo,mtu mmoja
alichukuliwa fedha kutoka mfukoni.
“Nimeporwaaaaaa-aa-aa,nimeporwa,jamani”.Watu
hawakujali.Ooooh. Unaleta gozigozi?.Watakuiba hata wewe mwenyewe! Bwege
wewe’’.Kondakta wa basi hilo
alifoka.Kama ilivyo ada sikio halilali njaa.Mtu mwingine akadakia.
“Aaah,shauri yako we mshamba wa
kijijini’’.Lupyana aliwaza kidogo aliposikia hayo.“Dunia tambara bovu kweli”
alijisemea.
Wakati huo huo,kuna mtu alikuwa anapanda
basi kupitia dirishani,na alimkanyaga
Lupyana begani.Lupyana akasonya lakini hakuna aliyemjali.Kwa
hakika,asingethubutu kuparura mkono wake
juu ya hili jitu la miraba minne kwani lingemcharanga na kumtafuna mbichi
mbichi.Hofu ikatawala moyoni mwake
tena.Watu wengine walitaka kushuka.Oya we mama toa makalio yako njiani
tunashuka’.Kijana mmoja alionekana
amenyoa nywele kama ugiligili wa jogoo alibwatuka…!Mama naye kumbe mtata!Akamjibu,Shuka zenyewe ziko wapi? Peleka fito zako huko.Watu
walicheka kwenye basi wakampongeza mama kwa kumunyoosha huyo kijana mkosa
adabu.
Vituko vya UDA viliendelea.Baada ya dakika chache akaja mama mmoja
mgonjwa.Yeye aliomba msaada kuwa apite mlango wa mbele karibu na kule anapokaa
dereva.Akasukumwa kwa nguvu na kondakta,akaanguka huku akifokewa kuwa hii siyo
gari ya wagonjwa. “Soma juu ya mlango”. Kwa kweli,”Asiyekujua
hakuthamini!”.Zimwi likulalo hadi mwisho
halikujui.
Kwa mbele kulikuwa kijana mwingine aliyetaka
kushuka.”Pisha…..pisha!” Waliokuwa karibu nae walimwita lukwalakwala.Lakini lukwalakwala akalalamika
kwa nguvu,Musee ona kwisa kanyaga mimi?,Dunia musima inasangilia amani wewe
inakanyaga?”.We lukwalakwala toa kelele zako hapo unafikiri basi hili la baba ako?’’.Kijana
mwingine alidakia.Lukwalakwala alikunja uso ukawa na makunyanzi kama goti la mbuzi
na kufoka, “Siku mingine tafyeka koromeo lako”.Watu walicheka kwenye basi na
hapo Lupyana naye akaangua kicheko