VITABU MBALIMBALI
MAISHA YA UJANA,UTAKATIFU,
CHANGAMOTO ZA KARNE YA 21 NA UTIMILIFU WA DALILI ZA UJIO WA MASIHI
UJANA
Ujana ni kipindi kati ya utoto na
utu uzima.Unaanzia miaka 18 hadi miaka 40.Unaelezwa kama ni kipind cha
maendeleo ya kimwili na kisaikolojia kuanzia mwanzo wa kubalehe kwa ukomavu na
mwanzoni mwa utu uzima.Ukomavu wa mtu binafsi huenda unakosa kuwa sawa na umri
wao kwani watu wasiokomaa hupatikana kwa umri wowote.
Kwa ujumla ujana unahusu wakati
wa maisha ambao si utoto wala utu uzima lakini mahali fulani kati.Hiki ni
kipindi ambacho mtu anakuwa na nguvu ya
kufanya jambo lolote.Kundi hili ndilo
linalotegemewa sana katika kufanya kazi
ya Mungu na ujenzi wa taifa kwa ujumla.
1yohana 2:13-15 anasema ‘’Nawaandikia
ninyi vijana kwasababu mmemshinda yule mwovu,Nimewaandikia ninyi vijana
kwasababu mna nguvu na neno la Mungu linakaa ndani yenu nanyi mmemshinda yule
mwovu’’.
UTAKATIFU
Ni kuishi maisha mbali na dhambi
au ni hali ya kujitenga na dhambi yaani ni hali ya kuwa mkamilifu.Hili ni agizo
ambalo Mungu alitupatia kuwa tuishi maisha matakatifu kama yeye alivyo.
‘’Basi ninyi mtakuwa wakamilifukama
baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu” [Mathayo 5:48]
MAMBO YA KUFANYA ILI UWE MTAKATIFU
{1}Kuacha dhambi au kuzaliwa mara
ya pili
Ili uwe mtakatifu ni lazima uache
dhambi kwani roho mtakatifu hakai mahali
pachafu na Mungu hapendi michanganyo hivyo ni vyema kujitakasa na kuwa safi na
bila hivyo huwezi kuuridhi ufalme wa
milele.
‘’…mtu asipozaliwa mara ya pili
hawezi kuuona ufalme wa Mungu ………………..mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho hawezi kuingia katika ufalme wa
Mungu [Yohana 3:1-6]
{2}Kusamehe ni hali ya kumhurumia
au kumfutia makosa mtu yeyote
aliyekukosea bila kujali umri,kabila,rika,taifa wala ukubwa wa kosa alilokukosea
kwani bila kusamehe na Mungu hawezi kukusamehe wewe pia.
‘’Kwa maana mkiwasamehe watu
makosa yao na baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi,Bali msipo wasamehe watu
makosa ya o wala baba yenu hatawasamehe
ninyi makosa yenu’’[ Mathayo 6:14]
{3}Kutoa sadaka
Ni hali ya kumtolea mungu kwa
vile ulivyojaliwa Sadaka inaweza kuwa pesa,zao kama mahindi,maharage,kadri
Mungu alivyokujalia.Tangu mwanzo kabisa watu walionyesha shukrani yao na
kujitoa kwa Mungu kwa njia ya kumtolea sadaka.Katika sadaka nyingine za shukrani
mtu alimtolea Mungu sehemu za nafaka zake au mifugo ile iliyo bora.’’Nuhu akamjengea
BWANA madhabahu;akamtwaa katika kila mnyama aliye safi na katika kila ndege
aliyesafi,akavitoa sadaka za kuteketezwa
juu ya madhabahu’’[mwanzo 8:20]
Wengine walionyesha ushirikiano
mwema na Mungu na wanadamu wenzao,ambapo mtoaji alikula sehemu ya sadaka yake
katika karamu pamoja na jamaa na marafiki.’’Yakobo akachinja sadaka katika
mlima akawaita ndugu zake waje wale chakula,nao wakala chakula wakakaa usiku
kucha mlimani’’[Mwanzo 31:54]
Sadaka nyingine ilikuwa kwaajili
ya msamaha wa dhambi,ambapo mnyama aliyechinjwa alichukua adhabu ya
mtoaji.’’Basi sasa,jitwalieni ng’ombe waume saba,na kondoo waume
saba,mkamwendee mtumishi wangu ayubu,mjisingezee sadaka ya kuteketezwa;na huyo
mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi;kwa kuwa nitamridhia yeye,nisiwatendee sawasawa
na upumbavu wenu;kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katika habari zangu
kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu’’[Ayubu 42:8]
Lakini Wakati wa agano la kale wapo watu ambao walimtolea Mungu sadaka bila kuhubiriwa bali walimsikiliza roho wa Mungu alipowaambia wafanye hivyo basi walifanya.mfano Kaini na habili[mwanzo 4:4-15] ,Ibrahim alimtoa mwanaye isaka kuwa sadaka bila kuteketezwa bila kuhubiriwa na mtu yeyote bali alimsikiliza roho wa Mungu alivyomwongoza[waebrania 11:17-18]
Mipango ya sadaka za Israel ilikuwa ya aina kubwa tano ingawa zilitofautiana lakini sadaka kuu zilikuwa ni zile za kuteketezwa.Sadaka hizi ziliitwa sadaka za kuteketezwa kwasababu wanyama wote waliteketezwa juu ya madhabahu,
Sadaka ya kuteketezwa ilitolewa kwaajili ya taifa zima na ilichochewa na kuteketea juu ya madhabahu wakati wote pasipo kukoma ikiwa na maana ya kujitoa kwa Mungu bila kukoma’’Basi sadaka utakazozitoa juu ya madhabahu ni hizi;wanakondoo wa mwaka mmoja wawili siku baada ya siku daima,mwanakondoo mmoja utamchija asubuhi;na mwanakondoo wa pili utamchinja jioni…………….’’[kutoka 29:38-42]
Sadaka ya unga pamoja na sadaka ya divai[au ya kinywaji]iliyounganika ilionyesha shukrani kwa Mungu kwaajili ya chakula cha kila siku kilichotoka kwake.Sadaka ya unga na divai haikutolewa peke yake bali siku zote ilitolewapamoja na sadaka za kuteketezwa au za amani.Divai ilimiminwa juu ya sadaka ya mnyama iliyokuwepo juu ya madhabahu,na mkono mmoja wa unga uliteketezwa pamoja nayo.’’Na sadaka ya unga itakuwa sehemu ya kumi na mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta,ni kafara ilisongezwa kwa BWANA kwa moto kuwa harufu ya kupendeza;na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai,robo ya hini’’[Lawi 23:13]
Sadaka ya amani ilionyesha ushirika na uhusiano mwema,yaani jambo lilionyeshwa katika karamu iliyofuatana nayo.Baada ya sherehe ya damu mwanzoni,sherehe ya kuteketeza sehemu yake na kutoa sehemu yake kwa kuhani,mtoaji alishirikiana na familia yake ,marafiki zake na watu wenye dhiki au maskini akla mabaki ya mnyama katika karamu ya furaha.’’……………….na hiyo nyama ya sadaka zake za amani zilizochinjwa kwaajili ya shukrani italiwa siku iyo hiyo ya matoleo yake ,asisaze yoyote hata asubuhi………….’’[Lawi 7:13-15]
Sadaka ya dhambi,hii ni sadaka iliyokuwa inatolewa kwa mtu yeyote ambaye amejitambua kuwa amevunja sheria mojawapo ya Mungu.Kama kwa dhambi za makuhani walinyunyiza damu ya mnyama ndani ya mahali patakatifu,wakateketeza vipande vingine vya nyama katika madhabahu na mabaki wakachoma nje ya kambi na kama dhambi ilikuwa ya raia binafsi,makuhani walinyunyizadamu katika madhahabu wakateketeza vipande vingine juu ya madhahabu hiyo na kula vipande vilivyobaki.’’Na mtu awaye yote katika watu wan chi akifanya dhambi pasipo kukusudia,kwa kufanya neno lolote katika hayo ambayo Bwana alizuilia yasifanywe,naye akapata hatia,atapojulishwa hiyo dhambi yake aliyoifanya ,ndipo atakapoleta mbuzi mke mkamilifu,awe matoleo yake kwaajili ya dhambi yake aliyoifanya……..’’[Lawi 4:27-29]
AINA ZA SADAKA KATIKA KIPINDI
HIKI CHA AGANO JIPYA HADI SASA
{A}Sadaka ya malimbuko
Sadaka hii ni zao la kwanza la
kazi ya mikono yako mfano kama ni mazao basi mazao ya kwanza kabla ya kuanza
kuyatumia,kazi ya sadaka hii ni
Kumheshimu Mungu kwa vile alivyokujalia.”Mheshimu BWANA kwa mali yako,na
malimbuko ya mazao yako yote,Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi
…………………….’’ [Mithali3:9-10 ]‘’ ‘’Atoaye dhabihu za kushukuru ndiye
anayenitukuza’’ Katika kipindi hiki cha agano jipya kuna aina nyingi za sadaka.’’ [Zaburi 50:23]
{B} Zaka{fungu la kumi}
Sadaka hii ni asilimia 10 au moja ya kumi au shemu moja ya Baraka
aliyokupa Mungu.Zaka ilianza zamani sana kabla ya MUNGU hajaweka sheria ya watu kutoa zaka,Wako
watu waliompenda MUNGU kwa mioyo yao walimtolea zaka bila kulazimishwa wala
kuhubiriwa ila walitoa kwa moyo.
‘’Leteni zaka kamili ghalani ili
kiwemo chakula katika nyumba yangu
,mkanijaribu kwa njia hiyo asema BWANA wa majeshi:mjue kama sitawafungulia
madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni Baraka,hata isiwepo nafasi ya kutosha au
la’’ [Malaki 3:10]
{C}Sadaka ya Nadhiri
Ni sadaka ya patano na MUNGU.Hii
hutolewa kipindi mtu anapokuwa katika tatizo na anaahidi zawadi endapo
atatekelezewa.
‘’Na mkaanani,mfalme wa Aradi,aliyeketi upande wa Negebu,alisikia
kuwa Israel amekuja kwa njia ya Atharim;bas akapigana na Israel na watu kadhaa
wa kadhaa miongoni mwao akawateka ,Basi Israel akaweka Nadhiri kwa BWANA Akasema;Kama wewe utawatia watu hawa mikononi
mwangu kweli,ndipo mimi nitaiharibumiji yao kabisa,Basi bwana akasikiza sauti
ya Israel……………’’[ Hesabu 21:1-3]
{D}Sadaka ya Hiari au ya kawaida
Hutegemea mguso na msukumo wa
ndani kutoka kwa MUNGU.Sadaka hii haina kiwango maalumu bali hutegemea mguso wa
roho mtakatifu ndani ya mtu binafsi.
‘’Na
hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao sadaka ikiwa ni
ng’ombe au kondoo wampe kuhani………………..’’[
Mwanzo 18:3-]
‘’Maana
kama ipo hukubaliwa kwa kadri ya alivyo
navyo mtu si kwa
kadri ya asivyo navyo’’[2Wakorintho 8:12]
{E}Sadaka ya shukrani
Hutolewa wakati wa
ushindi,kubarikiwa na hata kuwa mzima.Mara nyingi Sadaka hii huambatana na
Ushuhuda Fulani kutoka kwa mtoaji.
‘’Naye Haruni atawasongeza walawi mbele za
BWANA wawe sadaka ya kutakaswa,kwaajili
ya wana wa Israel ili wawe wenye kufanya
utumishi wa BWANA……………………………umtoe mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA na huyo
wa pili awe sadaka kuteketezwa ,ili kufanya upatanisho kwaajili ya walawi’’
[Hesabu 8:11]
NAFASI YA SADAKA MBELE ZA MUNGU
{A}Sadaka inafanya MUNGU atume
malaika zake wakupiganie.
‘’Apandaye haba atavuna
haba,maana utumishi wa huduma hiihauwatimizii wafatakatifu riziki
walizopungukiwa tu bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani apewazo MUNGU’’[2Wakorintho
9:6-11]
{B}Sadaka zinatoa nafasi kwa
MUNGU awe na sauti juu ya vitu.
‘’Kwa imani Habili alimtolea MUNGU dhabihu
iliyo bora kuliko kaini kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki ;MUNGU
akazishuhudia sadaka zake na kwa hiyo ijapokuwa amekufa angali akinena[
Waebrania 11:4].
{C}Sadaka inatoa nafasi ya
kubarikiwa
‘’Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi tena
nimejaa tele;nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vilivyotoka kwenu,harufu ya
manukato ,sadaka yenye kibali,impendezayo MUNGU ,Na MUNGU wangu atawajazeni
kila mnacho hitaji kwa kadri ya utajiri wake,katika utukufu,ndani ya kristo
Yesu. [Wafilip 4:18-19]
{4}Uongozwe na roho mtakatifu
‘’Lakini mtapokea nguvu akiisha
kuwajilia juu yenu roho mtakatifu;nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalem na katika Uyahudi wote na samaria na hata mwisho wa nchi’’ [Matendo
1:8]
‘’……..kwasababu ya dhambi
aliihukumu dhambi katika mwili ,ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili
bali mambo ya roho.’’[ Warumi 8:1-11]
UTANDAWAZI
Mtumizi ya neno UTANDAWAZI
yalianzia miaka ya 1990.Neno utandawazi lina maana nyingi kutegemeananu
matumizi yanayokusudiwa.
K
wa maana ya kawaida utandawazi ni mfumo wa kuifanya dunia iwe kama kijiji kimoja
kwa mfumo wa teknolojia ya mwasiliano,mtandao siasa,uchumi na utamaduni.
KIBIBLIA UTANDAWAZI
Ni harakati za mfumo mpya wa
kidunia ambao na Mpinga kristo unaowezesha watu wa dunia kuwa na uchumi
mmoja,dini moja raisi mmoja na teknolojia moja.” Naye awanyaye wadogo kwa
wakubwa na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika
mkono wa kuumeau katika vipaji vya nyuso zao, tena kwamba mtu awaye yote
asiweze kununua wala kuuza isipokuwa ana chapa ile,yaani jina la mnyama yuleau hesabu ya jina lak.
Hapo ndipo penye hekim, yeye aliye na akili na aihesabu ya mnyama huyo, maana
ni hesabu ya kibinadamu na hesabu yake ni mia sita sitini na sita”[ Ufunuo
13:16-18 ]
Kulingana na maandiko utandawazi
ulipo leo ni mandalizi tu ya mfumo wa wazi wa Mpinga kristo” Na sasa lizuialo mwaliju, Yule apate kufunuliwa
wakati wake maana ile siri ya kuasi hivi sasa
inatenda kaz,lakini yupo azuiaye sasa, hata atakapoondolewa, hapo ndipo
atakapofunuliwa Yule asi ambaye Bwana Yesu atamua kwa pumzi ya kinywa chake, na
kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake,
Yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake shetani, kwa uwezo wote na
ishara na ajabu za uongo na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea,
kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli wapate kuokolewa”[2 Thesalonike
2:6-10]
Kuna dalili nyingi zinazojitokeza
kudhibitisha ujio wa kumpinga kristo kea uwazi. Baadhi ya dalili hizo ni
kuongezeka kwa maarifa ya utendaji isiyo ya kawaida ya binadamu” Lakini wewe ee Daniel yafunge maneno haya
ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho , wengi wataenda mbio huko na
hukon na maarifa yataongezeka” [ Daniel 12:4]
Karne ya mwishoni mwa karne ya 20
na mwanzoni mwa karne hii ya 21 (sasa) ni kipindi kumekuwepo na mnibuko mkubwa
wa maendeleo ya teknolojia ya sayansi kama vile matumizi ya kitabu cha nyuso
(facebook), Twitter,Ebuddy n.k. mabadiliko haya yameiathiri jamii hasa vijana
kimwili na kiroho moja kwa moja
ATHARI ZA UTANDAWAZI KTK MAISHA
YA KIROHO
1.
Kumzimisha
roho mtakatifu au kupoteza nguvu ya kiroho
Kuna mungu mmoja tu, na mungu huyo siku zote yupo katika utatu wa Baba,
mwana na roho mtakatifu. Kwa hiyo ufahamu wa mwanadamu kuhusu roho mtakatifu
umeunganishwa na ufahamu wake wa utata, na huo tena umeunganishwa na maisha na
huduma ya yesu kristo. Na ufunuo wake ulifikia kilele chake katika yesu kristo.
ROHO MTAKATIFU WAKATI WA AGANO LA
KALE
Watu wa wakati wa agano la kale walipooana dalili maalumu za nguvu na
uwezo wa mungu waliita nguvu hiyo wakitumia neno la kiebrania la “ruach”Neno
hili liitumiwa katika lugha ya kila siku pasipo uhusiano wa pekee na “mungu”
nalo liliweza kuwa na maana ya upepo
Anasema “ Ikawa
muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikanyesha mvua nyingi.
Ahabu akapanda garini akaenda zake yazreeli” pia neno ( ruach) lilikuwa na
maana ya” pumzi” au roho (katika maana ya maisha na hisia za mtu [1Wafalme18:45)
“Wakamwambia maneno yote ya yusufu
aliyowaambia na alipoona magari
aliyoyapeleka yusufu, ilikumchukua, roho
ya yakobo baba ikafufuka.[ Mwanzo 45:27].
Katika kuhusianisha na mungu neno
“ruach” liliweza kuwa na maana ya upepo ambaomungu aliutumumia ili kuongeza
maendeleo ya hali ya ulimwengu
Anasema “Na mungu akamkumbuka
Nuhu na kila kilicho hai na wanyama wote waliokuwa pamoja naye katika safana,
Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua, chemichemi za vilindi
zikafungwa [Mwanzo 8:1]. ‘’Bwana akageuza
upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi ambao uliwaondoa wale nzinge na
kuwapeleka katika bahari ya sham, hakusalia hata nzinge hata mmoja ndani ya
mipaka ya misri “ Na vilevile “ruach” ilikuwa na maana ya
“pumzi ya pua au kinywa” cha Mungu ambayo kwa njia yake alifanya mambo makuu au
ya roho wake ambayekwa njia yake alikuwa na nguvu, matendo na hisia za kiumbe hai.[ Kutoka 10:19]
“Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika,
na jeshi lake lote kwa pumzi ya kuinywa chake” [Zaburi 33:6]
“Ndipo ilipoenekana mikondo ya
maji, misingi ya ulimwengu ikafichuliwa
ee Bwana, kwa kukemea kwako kwa mavuno
ya pumzi ya puani mwako”[ Zaburi 18:15]
Katika matukio maalumu roho huyo wa
mungu (au nguvu ya mungu ) alikuja juu ya watu walioteuliwa kwaajili ya
makusudi maalumu
“Roho ya Bwana ikamjilia juu
yake, nawe akawa mwamuzi wa Israel, akatoka kwenda vitani “[Waamuzi 3: 10]
“ Akajibu akaniambia akasema,
Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, si kwa nguvu, bali ni kwa roho
yenuasema Bwana wa majeshi” [Zakaria 4: 6 ]
Matokeo ya nguvu yanaweza kuwa
uongozi wenye, ushindi, nguvu isiyo ya kawaida ya binadamu au uwezo wa ufundi
maalumu.
“Nami nimemjaza roho ya
Mungu,katika hekima na maarifa na ujuzi na mambo ya kazi ya kila aina” [Kutoka
31:3-5]
Mara nyingine matokeo yake
yalikuwa matendo au tabia isiyo ya kawaida. Siku zote kazi yake ilikuwa upande
wa haki na kupinga maovu.
” Lakini wakaasi wakamhuzunisha roho yake
mtakatifu kwa hiyo akawageuzia akawa adui akapigana”
Nguvu ya kiroho au roho mtakatifu hupokelewa na mtu
yeyote pale anapookoka inaweza kuambatana na kunena kwa lugha na inaweza isiambatane
hii inategemeana na mtu. Hii ni ahadi ambayo Yesu aliwaahidi wanafunzi wake
kabla ya kupaa[ Isaya 63 : 10]
“
Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu roho mtakatifu, nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika yerusalemu na katika
uyahudi wote na samaria na hata
mwisho wa nchi” [Matendo 1:7]
Mtu aliyeokoka anapokuwa na roho mtakatifu au nguvu ya roho kiwango
cha kiroho hushuka pale anapokengeuka/anapotenda dhambi. Roho mtakati alifanya kazi mbalimbali wakati wa agano la kale kama ifuatavyo;
KAZI
ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA AGANO LA KALE
A.
Alihusika
katika uumbaji
“ Hapo mwanzo Mungu aliimba
mbingu na nchi,naye nchi ilikuwa ukiwa, tena
utupu na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho ya Mungu
ikatulia juu ya uso wa maji”[ Mwanzo 1:1-2]
Mungu alitumia roho mtakatifu
(neno) katika uumbaji wala hakushika jembe,udongo,maji wala kifaa chochote
B.
Alihusika
kutoa unabii tangu Isaya hadi Zakaria. Wakati wa agano la kale manabii waliotoa
unabii walinena kwa roho mtakatifu.“ Alitazama juu akawaona waisraeli
wamepiga kambi kila kabila mahali pake,
kisha roho ya Mungu ikamjia naye
akatamka kauli hii ya mwenyezi Mungu ………………….” [Hesabu 24:2-3]
“ Siku hizo Hezekia aliugua akawa
katika hatari ya kufa na Isaya nabii, mwana wa Amosi akaenda kwa mfalme
akamwambia Bwana akasema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa
wala hutapona.[Isaya 38 :1-2]
C.
Alihusika
kuwapa watu maarifa,wakati wa agano la kale Roho mtakatifu aliwapa watu maarifa
ya kufanya mambo mbalimbali.
“ Bwana akanena na
Musa na akamwambia, Angalia nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwanawa Uri, mwana
wa Huri, wa kabila la Yuda, nami nimemjaza roho ya Mungu katika hekima na
maarifa na ujuzi wa mambo ya kazi ya kila aina”[ Kutoka 31: 1-2]
D.
Alitoa
hekima ya kuongoza kwa viongozi. Yusufu alitoa tafsiri mbele ya Farao lilikuwa
tendo jema likashamngaza Farao na wengine
“Farao akawambia watumwa wake,
Tupate wapi mtu kama huyu mwenye roho ya Mungu ndani yake. Farao akamwambia
Yusufu kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote hapana mwenye akili na hekima
kama wewe. Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu na kwa neno lako watu wangu
watatawaliwa katika kiti cha enzi tu, itakuwa
mkuu kuliko wewe.[ Mwanzo 41: 38-40]” “Nami nitashuka niseme
nawe huko, nami nitatwaa sehemu ya roho iliyo juu yako na kuiweka juu
yao nao watachukua mzigo wa watu hawa pamoja na wewe, ili usiuchukue wewe peke
yako” [Hesabu 11: 14-17]
Mungu aliahidi kuwa siku ingekuja
ambapo siyo watu walioteuliwa tu bali watu
wa Mungu bila kujali hali yao,
kwa kuwa wanaume na wanawake wangekuwa
na roho wa mungu ambaye angemiminwa juu yao.
” Hata itakuwa baada ya hayo ya
kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili, na wana wenu waume kwa wake , wakatabiri wazee wenu wataota
ndotona vijana wenu wataona maono”[ Joeli 2: 28-29]
ROHO MTAKATIFU KATIKA AGANO JIPYA
Yesu
kristo alipofika duniani watu walipokea ufunuo wazi zaidi kuhusu roho wa MUNGU
.Watu hawakutambua jambo hili kila wakati lakini kila
lilipotendeka mioyoni mwa watu ilikuwa
ni kwaaili ya kuwaleta watu kwa MUNGU kwa mara ya kwanza au kuumba tabia mpya
ndani.Hii ya ajabu ote ilifanywa na roho
wa MUNGU asiyeonekana.
Katika maonesho ya ajabu ya MUNGU, roho wa MUNGU alikuwa anakuja kwa
watu walioteuliwa kwaajili ya kazi
maalumu.Yesu alikuwa na roho asiyekuwa na mipaka au kikomo.Yesu aliishi na
kutimiza kazi yake kwa njia ya nguvu isiyo na kikomo yaani ya roho wa MUNGU
aliyefanya kazi ndani yake kila wakati.
;Basi litatoka chipukizi katika shina la yese
,na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda,Na roho ya Bwana
atakaa juu yake,roho ya hekima na ufahamu,roho ya shauri na uweza ,roho ya
maarifa na ya kumcha’’.
Watu walipata ufahamu kuhusiana na roho mtakatifu,Ufahamu huu ulianza
kuonekana wakati wa ubatizo wa Yesu,Mungu baba,alikuwa Mbinguni,Mungu mwana
alikuwa duniani ambaye ndiye YESU,Mungu roho alikuja kutoka Mbinguni na kudhihirisha ukuu kwa kumkalia
Mwana. [Isaya 11:1-2]
‘’Naye yesu alipokwisha kubatizwa
mara akapanda kutoka majini,na tazama mbingu zikamfunukia,akamwona roho wa
MUNGU akishuka kama hua akija juu yake,na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema Huyu ni mwanangu mpendwa
wangu ninayependezwa naye’’ [ Mathayo 3:16-17]
ROHO MTAKATIFU NA KANISA LA
KWANZAKwa njia
ya Yesu kristo ,MUNGU alitaka kuwapa
waamini wote roho mtakatifu,Yesu alipaswa kutimiza kazi ambayo baba alimpa
kabla waamini hawajampokea roho mtakatifu.
Mungu alitaka kuonyesha ukuu na kuridhika
kwake na kazi ya Yesu na alimfufua kutoka kwa wafu na kumpa utukufu.
Baada ya utimizaji huo wa ushindi wa
huduma ya Yesu kristo duniani Baba angewapa wengine Roho.Hivyo Yesu aliwaahidi
wanafunzi wake wangoje Yerusalemu baada ya kupaa kwake nao wangempokea roho
mtakatifu kama alivyowahidia.
‘’Hata alipokuwa amekutana nao
aliwaagiza,wasitoke Yerusalemu bali wangoje ahadi ya baba ambayo mlisikia
habari zake kwangu,ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji,bali ninyi mtabatizwa
kwa roho mtakatifu baada ya siku hizi chache’’[Matendo 1:4-5]
Mungu alitimiza ahadi siku ya Pentekoste,Siku ambapo Mungu alimimina
roho juu ya wanafunzi wa Yesu.
‘’Kukawatokea ndimi
zilizogawanyika kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao,Wote wakajazwa
roho mtakatifu,wakaanza kusema kwa lugha nyingine,kama roho alivyowajalia
kutamka.’’[ Matendo 2:3-5]
Hata sasa Mungu anamimina roho wake juu ya waamini bila kujali hali
yao,umri wao,jinsia,wala kabila.Wanaookokaau wanomkiri Yesu wanajazwa roho
mtakatifu katika mazingira tofauti na wakati tofauti kama vile wakati wanabatizwa,baada
ya kufundisha somokuhusu roho mtakatifu n.k
ILI KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU
-lazima umpokee yesu kuwa Bwana
kuwa mwokozi wamaisha yako
-Lazima uitake Baraka
hii kwa bidii
-Uwe na kiu
ya kiroho
‘’ Hata siku ya mwisho,siku ile kubwa ya sikukuu,yesu akasimama,akapaza sauti yake
akisema,mtu akiona kiu na aje kwangu anywe,………………na neno hilo alilisema katika
habari ya roho ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye’[ Yohana 7:37]
-Tubu toba ya kweli
‘’Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake
Yesu kristo,mpate ondoleo la dhambi zenu,nanyi mtapokea kipawa cha roho
mtakatifu’’ [Matendo 2:38]
-Tumia imani katika kumpokea roho mtakatifu
‘’
Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vilivyo vyema,je
baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa
roho mtakatifu hao wamwombao?’’ [Luka 11:13]
JINSI YA KUJAZWA ROHO
MTAKATIFU
1/Omba kwaajili ya kumpokea roho
mtakatifu,omba kwa kumaanisha na kwa bidii.‘’.Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua
kuwapa watoto wenu vipawa vyema,jebaba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa
roho mtakatifu hao wamwombao?’’[ Luka
11:9-13]
2/Wasamehe waliokukosea na tubu
dhambi zako,kwani dhambi ni hufanya mtu asipokee roho mtakatifu.‘’’……tubuni mkabatizwe
kila mmoja kwa jina la Yesu kristo,mpate ondoleo la dhambi zenu,nanyi mtapokea
kipawa cha roho mtakatifu’’ [Matendo
2:38]
3/Onyesha kiu ya kumpokea na
andaa moyo wako kwaajili ya kumpokea Roho mtakatifu ’’ Na neno hilo alilisema
katika habari ya roho mtakatifu ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye’’
[Yohana 7:37-39]
4/Anza kumsifu MUNGU mpaka unapokea upako wa roho mtakatifu
‘’Wakamwabudu;kisha wakarudi
Yerusalemu wenye furaha kuu.Nao walikuwa daima ndani ya hekalu,wakimsifu
Mungu’’[ Luka 24:52-53]
Wakati wa agano jipya roho mtakatifu alikuwepo, na yupo lakini
anafanya kazi tofauti na kipindi cha
agano la kale.Katika kipindi hiki cha agano jipya wanaomwamini Mungu wanampokea
roho mtakatifu na huondoka pale muumuini anapokengeuka na si lazima ahusike
katika kutabiri au kutoa unabii,lakini katika agano la kale alihusika zaidi
katika kutoa unabii na kuongoza kwa ujumla.
KAZI ZA ROHO MTAKATIFU
KATIKA AGANO JIPYA
{A}Hutufundisha yote aliyoagiza
kristo
Roho mtakatifu akikaa ndani ya
mtu humfundisha yale tunayopaswa kutenda.
‘‘Lakini huyo msaidizi,huyo roho mtakatifu
ambaye baba atampeleka kwa jina langu atawafundisha yote na kuwakumbusha yote
niliyowaambia.’’[Yohana 14:26]
{B}Hutuongoza
Roho mtakatifu akikaa ndani
mwamini humuongoza katika mambo mbali mbali ya kimwili na kiroho.Mfano mtu
mwenye roho mtakatifu kuwahi ufika Ibadani si lazima agongewe kengele bali roho
humuongoza na kumkumbusha.
‘’Lakini yeye atakapokuja huyo
roho wa kweli,atawaongoza awatie kwenye kweli yote kwa maana hata nena kwa
shauri lake mwenyewe ,lakini yote atakayo atayanena na mambo yajayo atawapasha
habari yake.’’[ Yohana 16:13]
{C}Hutuombea
Katika kuomba muombaji anapoomba hadi
kufikia kunena kwa lugha roho mtakatifu hutusaidia kwa kuugua kusikokuwa kwa
kawaida.
‘’Kadhalika roho naye hutusaidia
udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba jinsi ipasavyo,lakini roho mwenyewe
hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkika.’’[ Warumi 8:26]
{D}Roho mtakatifu anakaa ndani ya
muumini ,mwamini akiwa na roho mtakatifu atakuwa safi katika mwenendo na
matendo yake kwani atamshuhudia juu uhusiano wake na MUNGU.
‘’Lakini ikiwa roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu,yeye aliyemfufua kristo Yesu
katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa kwa Roho wake
anayekaa ndani yenu’’. [Warumi 8:11]
Mwamini anaweza kupoteza Nguvu ya kiroho au
roho mtakatifu kutegemeana na hali ya
maisha au tabia mbali mbali mbaya ambazo hutawala maisha ya mtu kama vile
kuangalia michezo ya luninga akili hutawaliwa na kufahamu wahusika wa michezo
hiyo na n.k humpa ham mtazamaji ya kuangalia
kila wakati na hivyo hupoteza
hamu ya kusoma biblia.
Kuangalia filamu chafu huvuta fikra za mtazamaji na kumfanya afikiri kila
wakati kufanya tukio halisiau kufanya jaribio la kuiga mitindo mbali mbali
mibaya aliyoiona hivyo huteka fikra za
mtazamaji na humfanya afunguwe milango ya kuingiwa na pepo la uzinzi,mwisho huishia kuingia
katika dhambi ya uzinzi.
{E}Hutapatia uhakika juu ya
wokovu wetu
‘’Roho mwenyewe hushuhudia pamoja
na roho zetu,ya kuwa sisi tu watoto wa MUNGU’’ [Warumi 8:16]
{F}Hutupatia nguvu ya kuishi
maisha matakatifu
‘’Lakini yeye atakapokuja huyo
roho wa kweli ,atawaongoza awatie kwenye kweli yote;kwa maana hata nena kwa
shauri lake mwenyewe’’ [Yohana 16:13]
{G}Huleta uwezo na nguvu ya
kumsifu MUNGU katika ibada na kuabudu katika roho na kweli.
‘’…..maana sisi tu
tohara,tumwabuduo Mungu kwa roho,na kuona fahari juu ya kristo yesu,wala
hatuutumainii mwili.’’
[Wafilip 3:3]
‘’Mungu ni roho,nao wamwabuduo
yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli’[ Yohana 4:24]
{H}Anaweza kuruhusu jambo Fulani
lifanywe au lisifanywe kutegemeana na muktadha au mazingira au hali halisi ya tukio hilo
‘’Wakapita
katika nchi ya Frigia na Galatia,wakikatazwa na roho mtakatifu wasilihubiri
lile neno katika Asia’’ [Matendo 16:6]
MADHARA YA
KUMPOTEZA ROHO MTAKATIFU
{i}Kufa kiroho au Kuwa na imaniisiyona
matendo
Mtu yeyote
asipokuwa na roho mtakatifu hata katika imani atakuwa na imani haba sana.Imani
yake huwa ni ya mdomoni na si matendo.Anaweza kuwa mhudhuriaji wa ibada kama
picha lakini moyoni amepooza au amekufa kiroho.
‘’Maana
kama vile mwili pasipo roho umekufa ,vivyo hivyo na imani pasipo matendo
imekufa’’.[ Yakobo 2:26]
‘’Na kwa malaika wa kanisa lililoko sardi andika,Haya ndiyo anenayo yeye aliyena
hizo roho saba za Mungu na zile nyota saba,Nayajua matendo yako ya kuwa unajina
la kuwa hai nawe umekufa’’.[ufunuo 3:1-3]
{ii}Kukosa
au kutokuwa na maono au kutojua mambo yajayo katika ulimwengu wa roho.
Mtu yeyote
aliyeokoka akimpoteza roho mtakatifu hawezi au nguvu ya kiroho hawezi kujua mambo ya rohoni kwani unakuwa umejiondoa katika ulimwengu wa
roho. Kuishi bila roho mtakatifu ni sawa
na meli isiyo na nahodha baharini.Mara nyingi hukosa mambo mazuri na hupatwa na
mabaya kwani hukosa taarifa katika rohoni kuwa aombe.
‘’…Lakini
yote atakayo yasikia atayanena,na mambo yajayo atawapasha habari yake’’ [Yohana
16:13]
‘’Siku hizo
Hezekia aliugua akawa katika hatari ya kufa ;na Isaya nabii,mwana wa Amozi
akaenda kwa mfalme ,akamwambia Bwana asema hivi,Tengeneza mambo ya nyumba yako
maana utakufa wala hutapona…………’’[Isaya 38;14]
{iii}Kuwa
mropokaji,
Mtu yeyote
aliyeokoka akimzimisha au asipokuwa na roho mtakatifu mara nyingi huwa
mropokaji kwani hakuna roho inayomwongoza azungumze nini,wapi na atumie maneno gani.
{iv}Kuenenda
kwa mwili ,
Mtu yeyote
akimpoteza roho mtakatifu kila anachoona anaweza kukifanya bila kufikiri kitu
hicho kina madhara gani,au lip jema na lipi si jema hivyo hukengeuka moja kwa
moja.
{2}Kuingiza mitindo mbali mbali
ya uimbaji wa kidunia makanisani.
Kutokana na maendeleo ya sayansi
na teknolojia waumini hasa vijana waliookoka wanachukua au wanaiga mitindo
mbalimbali ya uimbaji wa kidunia na kuingiza kanisani kama vile mitindo ya
dansi,rapu,lege, n.k wanaitumia moja kwa moja katika uimbaji makanisani.Uimbaji
huu huambatana na uigaji wa mitindo ya kucheza,mavazi na n.
Mitindo hii inapotosha ua
inaondoa ushuhuda kwa kanisa na uwepo wa Mungu pia.Hali hii imewafanya ambao
hawajaokoka kutamka dhahiri kuwa walokole wa sasa wamechakachuliwa.
Mfano;Baadhi ya vijana huimba Hip
Hop makanisani wakiwa na uvaaji unaosawili waimbaji wa hip hop wa kidunia kama
vile kushika shika suruali,na kuvaa milegezo.Mitindo hii ya uimbaji inaigwa
kutoka magharibi[ulaya].Kwa ujumla haifai Hip hop kuimbwa kanisani au eneo
lolote la ibada hata kama nyimbo hizo zitamtaja Mungu kwani zinabadili maana
halisi ya ibada na kanisa kwa ujumla.Ni vyema
tujue kuwa nyumba ya ibada inapaswa kuheshimiwa ili kurejesha heshima
kwa Mungu wetu.
Mara nyingi watu wanaposikia
nyimbo hizi wakiwa kanisani hukumbuka kipindi kabla hawajaokoka hivyo huangalia
namna waimbaji wanavyocheza na sii kisikiliza ujumbe,Hatimaye huvutiwa
kusikiliza na kucheza na mwisho wa yote huzifuata disco ambako zinaimbwa kwa
wingi zaidi na baadaye kunogewa na starehe na kuacha wokovu.Ni wajibu wa kila
mmoja kutafakari na kuangalia mienendo yake ya wokovu na si kuangalia
mabadiliko ya dunia kwani Yesu au Mungu wetu habadilishwi na chochote.
[3]Kuoa na Kuolewa
Katika karne ya 21 suala la ndoa au
kuoa na kuolewa limekuwa na changamoto kubwa.Hii ni kutokana na uwepo wa njia
tofauti wanazotumia watu kutafutana na kuombana uchumba kama vile kwa kutumia
kitabu cha nyuso[Facebook],simu,twiter,skype na n.k
Kwa sasa vijana wanatamaniana
hivyo wanatafutana si kwaajili ya kuoana au kuolewa au kwa kuzingatia vigezo
kama vile umri na uhitaji wa kuwa na mwenza au familia n.k bali huoana kwaajili
ya kuzitimiza tamaa zao za mwili na si kupendana kwa dhati.
Vijana Wengi wanapofikia hatua hii hukengeuka na kumwacha
Mungu kutokana na kupumbazwa na pressure ya mapenzi na waliokwisha ingia huogopa kuchwa au
kusitisha uhusiano wao.Mara nyingi mabinti hulazimishwa kufanya mambo mengi
maovu na wapenzi wao,kwa woga huwa wanatii na kusahau kuwa wanamkosea
Mungu.Mabinti wengi hulazimishwa kufanya uzinzi na matokeo yake huishia
kuathirika na gonjwa hatari na kupata mimba zisizotarajiwa na waliowapa
huwakataa.
Hii ni kwasababu vijana wengi
huliangalia suala la ndoa kwa wepesi zaidi bila kutambua kuwa katika ndoa ikiwa
Mungu hatahusishwa huwa na matatizo.Ni vyema kujua kuwa mtu yeyote au mchumba
huwa na muonekano huu;
Unapofikiri kuoa ni vyema utambue
kuwa unayemchagua atakuwa mwenzi wa maisha milele hivyo haitoshi kuangali umbo
la nje tu kwani linaweza kubadilika.Zingatia sana mahitaji ya nafsi na rohoni
ndiko yanakotoka mambo mazuri na vigezo vingine ni ziada.
-Zingatia sana mapenzi ya Mungu
katika maisha yako na kati ya wengi una chumbia mmoja,na katika kufanya maamuzi
kabla ya kuanza kuchumbia mshirikishe Mungu.
“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala
usizitegemee akili zako mwenyewe’’[mithali 3:5]
-Imani moja kwani ndoa ni
muunganiko wa watu wawili hadi kifo hivyo ili muunganiko uwe imara lazima
uhusishe na masuala ya imani.
’’Msifungiwe nira pamoja na
wasioamini,kwa jinsi isivyo sawasawa;kwa maana pana urafiki gani kati ya haki
na uasi?Tena pana ushirika gani kati ya nuru na giza?Tena pana ulinganifu gani
kati ya kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja nay eye
asiyeamini?’’.[2wakorintho 6:14-15]
-Usiangalie sura,umbo au
umbile,elimu n.k kwani Mungu ndiye muumbaji pia ndiye anayetoa hivyo hata
akikupa mke au mume mwenye sura ya tofauti na matarajio pokea na ushukuru kwani
yeye anamjua kila mtu kwa namna au jinsi alivyo.
‘’Nyumba na mali ni urithi apatao
mtu kwa babaye,bali mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana’’[Mithali 19:14]
MTU/MCHUMBA
-Jinsi ulivyomuona[muonekano wa nje]
-Jinsi alivyo[moyoni]
-Jinsi atakavyokuwa[baada ya kuoa
au kuolewa]
Angalizo kwa vijana wa sasa ni
kosa kuchumbia bila kumuomba Mungu kwani,unapoamua kwenda kutoa posa unakuwa
umeridhika na muonekano wa nje bila kujua jinsi alivyo moyoni na jinsi
atakavyokuwa baada ya kuolewa.Ni vyema kumuomba Mungu kwani yeye anajua akupe
mke yupi atakayefanana na wewe kimwili na kiroho.
Hata hivyo katika jamii,tumegawanyika katika makundi mawili ambayo ni;
[A] INTROVERT
Ni aina ya watu ambao ni watulivu
wasiopenda kukaa na watu au ni aina ya watu wanaopenda kukaa peke yao kila
wakati.
[A quite person who prefers to be
alone than with other people]
SIFA ZAO
-Ni watulivu
-Ni wataratibu
-Hawapendi kujionyesha na si waongeaji bali wana maneno machache.
-Ni watu wasiomkosea Mungu nani wepesi kuepuka dhambiya
uongo,usengenyaji na n.k
-Mara nyingi hupenda kujihusisha na shughuli moja tu na si kuchanganya mfano kama
ni mfanyakazi basi hawezi kujihusisha na biashara na n.k hivyo ni vigumu kwao
kupata maendeleo.
-Hata akiwa na wazo zuri anachelewa kufikiri
na kufikia muafaka au kumweleza mtu mwingine ili amusaidie.
[B]EXTROVERT
Ni aina ya watu wanaopenda kuchangamana na watu wengine.
[A person who is full confident,
full of life and who prefers being with
other people]
SIFA ZAO
-Ni wacheshi
-Ni wepesi kufikiri jambo kwa
haraka na kulitafutia ufumbuzi
-Ni wepesi kumkosea Mungu na
kuomba toba
-Ni waongeaji sana hivyo ni
vigumu kuepuka dhambi kama vile udanganyifu,usengenyaji.
Kutokana na uwepo wa makundi haya ni
vigumu kujua ni yupi anayefaa kuwa mke mwema hivyo bila kumuomba Mungu unaweza
kupata ubavu usio wako.Vijana tunapaswa kumuomba Mungu ili aseme na Yule
unayemtaka lakini endapo Mungu atakujibu ni vyema kufuata utaratibu maalum
uliowekwa na kanisa au jamii kwa ujumla ili kuepuka udanganyifu na ukengeufu
kwani sii kila binti anafaa kuwa mke na sii kila kiajana anafaa kuwa mume wa
mtu ‘’MUNGU ndiye anayejua kukuchagulia’’
’’Mfalme suleman akawapenda
wanawake wengi wageni,pamoja na binti yake Farao,wanawake wa wamoabi na waamoni
na waedomi nawasidoni na wahiti na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa
Israel,msiingie kwao wala wasiingie kwenu;kwa kuwa wataigeuza mioyo yenu kuifuata
miungu yao’’ [ 1Wafalme 11:1-3]
[4]Kushindwa kutambua karama
uliyonayo.
Mungu humuumba kila mmoja kwa makusudi maalum,humpa kila
mtu karama au huduma yake na idadi ya karama hutofautiana kati ya mtu mmoja na
mwingine.Wengine wana karama ya kuimba,wengine kushuhudia,kuhubiri na n.k
Changamoto kubwa kwa vijana wa leo wengi
hawajui karama zao na hawamuombi Mungu
ili awafunulie karama hizo.Kutokana na kutojua karama hali inawafanya
kutoshiriki au kutofanya kazi yeyote kanisani bali wanabaki kuabudu kama
desturi.Kama Mungu ndiye muumba wa vyote ni vyema ujiulize maswali,kwanini
asingekuumba kunguni,ng’ombe,bata au mnyama mwingine yeyote?Ni vyema mwanadamu
ujue kuwa lipo kusudi la wewe kuumbwa kama mwanadam hivyo ni vyema umuombe
Mungu ili akufunulie karama au huduma yako ili uifanyie kazi katika kuujenga
ufalme wa mbinguni.
”Naye alitoa wengine kuwa mitume
na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu,kwa kusudi la
kukamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa kristo
ujengwe’’ [Waefeso 4:11-12]
Wakati Fulani Mungu anaweza kumpamtu karama
kwa mda maalum na kwa kusudi maalumu la wakati
huo,mfano karama ya unabii .Katika kanisa si lazima karama zifanane kwani
Mungu humpa kila mtu kwa namna yake na kulingana na Mungu anavyotaka mtu awe au
atumike katika kanisa.
‘’Basi pana tofauti za
karama;bali roho ni yeye yule,tena pana tofauti za huduma na Bwana ni yeye
yule,kisha pana tofauti za kutenda kazi bali Mungu ni yeye Yule azitendaye kazi
katika wote.Lakini kila mmoja hupewa
ufunuo wa roho kwa kufaidiana Maana mtu
mmoja kwa roho apewa neno la hekima;na mwingine neon la maarifa,apendavyo roho
yeye yule……………………’’ [1Wakorintho
12:4]
Hivyo mnaweza kuokoka kwa siku moja,mkabatizwa
kwa wakati mmoja,na mkajazwa roho mtakatifu wa wakati unaofanana lakini kila
mmoja akawa na karama yake tofauti kadri Mungu atakavyo mjalia na hata katika
kanisa karama mbali mbali hufanya kazi kwaajili ya kulijenga kanisa na kutimiza
kazi ya Mungu.
Mungu humuumba kila mtu kwa kusudi maalum,Hakuna mtu ambaye Mungu
alimuumba awe mwizi,jambazi,mlevi,mzinzi na n.k bali shetani huwadanganya watu ili apate wafuasi wa kwenda naye
jehanamu.Ni vyema wanadamu tujiulize kama Mungu ndiye aliyeumba vitu vyote je
kwa nini asingekuumba panya,paka,kuku,bata n.k hivyo lipo kusudi la kumuomba
Mungu ili anene na wewe nini kusudi la kuumbwa kwako.
KAZI ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTOA UNABII
Katika lugha ya kisasa maneno
‘’Unabii au Nabii’’ kwa kawaida yana maana ya kutabiri mambo yajayo.Maana hii
haikuwa ya msingi katika huduma ya unabii wakati wa agano la kale.Wakati ule
maana yake ilikuwa kujulisha mapenzi ya Mungu yaani nabii alikuwa msemaji wa
Mungu.
{A}Kufundisha mafundisho ya
kiroho ndani ya mtu
”Basi
tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji,bali ninyi ni wenyeji pamoja na
watakatifu,watu wa nyumbani mwake Mungu,mmejengwa juu ya msingi wa mitume na
manabii,naye yesu kristo mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni’’ [Waefeso 2:19-20]
Mara nyingi unabii hulenga
kufundisha mafundisho ya msingi katika kanisa ili kulipatia kanisa msingi ulio
imara.
{B}Kubomoa na kuharibu kazi za
shetani na kupanda roho ya Mungu ndani ya mtu.
Yeremia 1:5-10 anasema ‘’Kabla sijakuumba
katika tumbo nalikujua na kabla hujatoka tumboni
nalikujua,nalikutakasa;nimekuweka kuwa nabii wa mataifa,Ndipo niliposema,aa
Bwana Mungu,Tazama siwezi kusema;maana mimi ni mtoto,Lakini Bwana akaniambia
,Usiseme mimi ni mtoto mdogo;Maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekuamuru
kwake,nawe utasema kila neno nitakalo kuamuru ……………………..Ndipo Bwana akaunyosha mkono wake akanigusa kinywa
changu,Bwana akaniambia,Tazama nimetia maneno yangu kinywani mwako angalia
nimekwenda leo juu ya mataifa na juu ya falme ili kung’oa na kubomoa na kuharibu
na kuangamiza ili kujenga na kupanda’’
{c}Kuonya
‘’Akaniambia mwanadamu nakutuma kwa wana wa Israel,kwa mataifa wanaoasi
mimi;wao na baba zao wamekosa juu yangu,naam hata hivi leo,Na wana hao wana
nyuso zisizo na haya na mioyo yao migumu.Mimi nakutuma kwa hao;nawe utawaambia
Bwana Mungu asema hivi,Na kwamba watasikia {maana ndio nyumba ya kuasi hao)
hata hivyo watajua yakuwa nabii amekuwako miongoni mwao “[Ezekiel 2:3-5]
{d}Kufariji, kutia moyo, nakuthibitisha
kile ambacho Mungu amekwisha kusema na
wewe.
“Bali yeye ahutubuye asema na watu maneno ya
kuwajenga na kuwafariji na kuwatia moyo , yeye anenaye kwa lugha hujijenga
nafsi yake; bali ahutubuye hulijnga kanisa ………..”[1Wakorintho 14:3]
Hata leo manabii wapo ila
wanafanya kazi katika nafasi na kazi zao tofauti na za wale manabii wa agano la
kale.
“Naye alitoawengine kuwa mitume na wengine
kuwa manabii na wengine kuwa wainjlisti na wengine kuwa wachungaji na walimu “[Efes
1 Yohana 4:1-4 anasema “wapenzi msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho
kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu
manabii wa uongo wengi wametokea duniani” [1Yohana 4:1-4]. Katika hili mwajua roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu
Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu; na kila roho isiyomkiri Yesu
haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba
yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
SIFA ZA UNABII WA KWELI
I.Huambatana na upako au nguvu za
Mungu(spiritual power).
“Mkijua neno hili kwanza ya kwamba hakuna
unabii katika maandalizi upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu Fulani tu, maana
unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya binadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka
kwa Mungu wakiongozwa na roho mtakatifu”.[2 petro1;20-22]
II.Huambatana na matendo halisi
Mara nyingi unabii wa kweli
huambatana na utokeaji au utendekaji wa tendo halisi
“ Basi tulipokuwa tukikaa huko
siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka uyahudi alipotufikia
akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono akasema roho mtakatifu asema
hivi, Hivyo ndivyo wayahudi watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu nao watamtia
katika mikono ya watu wa mataifa…….” [Matendo
21:9-14]
Haya yalitabiriwa juu ya Paulo na
yalitokea wakati wake ulipofika(matendo 21;29-40) hivyo utabiri wa kweli ni ule
unaotimia.
III.Hutimia kwa maombi
“Elia alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na
sisi akiomba kwa bidii mvua isinyeshe na mvua haikunyesha juu ya nchi kwa muda
wa miaka mitatu na miezi sita,akaomba mvua inyeshe tena na mbingu zikatoa mvua
nayo nchi ikazaa matunda yake” [Yakobo
5:17-18]
5/ Mmomonyoko wa maadili
Kwa sasa suala la mapenzi
linaonekana kama suala la msingi (current issue), kwaani vijana hat watu wazima
wamekuwa wakijihusisha na kwa namana
moja ama nyingine, maendeleo ya sayansi na teknolojia kama vile facebook,twitter pamoja na ofa
mbali mbali zinazotolewa na mitandao ya simu za mikononi imefanya watu kuingia
katika mahusiano yasiyo ya msingi. Mitandao hii imevunja ndoa kwa baadhi ya
wanandoa, imewafanya waliookoka kutomtafakari Mungu na kusoma biblia bali sasa
wameingia kufanya mawasiliano(kuchati)
na facebook, twitter kuangalia michezo ya luninga isiyo na maana picha
chafu(pornography) na kuwasikiliza wasanii mbali mbali wanoima nyimbo za
kidunia. Matokeo yake wengi wameingiwa
na pepo la uzinzi(ngono) na kufa kiroho. Wengi wamemsahau Mungu na kuyaenzi
mapenzi.
“ Nawasihi enyi binti za
yerusalem kwa paa na kwa ayala za porini,msiyachochee mapenzi wala
kuyaamusha…..” [Wimbo uliobora 3:5]
6/ Kukosa msimamo
Watu wengi kwa sasa wamekosa
msimamo kiimani wengi wanatamani mafanikio kuliko kwenda mbinguni. Hali hii
imewafanya waumini wengi hasa
vijana kutanga tanga huku na huko
kiimani. Hawapendi watumishi wa hubiri kuhusiana na kuacha dhambi bali
wanapenda mahubiri yahusuyo kubarikiwa au namna ya kupatafedha na mali.
Wakati kama hu vijana au waumini
tunapaswa kuamka na kutambua kuwa
tumeokoka ili twende mbinguni hivyo tuwe
na msimamo dhabiti.
“Lakini sisi hatumo miongoni mwao
wasitao na kupotea bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kuokoa roho
zetu’’.[Waerania
10:39]
ATHARI ZA UTANDAWAZI KATIKA
MAISHA YA KAWAIDA
1.Tamaduni za kigeni
Kwa sasa utamaduni wa kigeni
umeanza kuenea sanaAfrika na umewaathiri
vijana katika mavazi. Vijana wameiga uvaaji mbaya kama vile kuvaa suruali
mlegezo hata matumizi ya lugha kwa
vijana yamekuwa ya kihuni sana. Vijana
wameiga mambo mbali mbali yanayofanywa
na waimbaji wa hip hop,dansi blues n.k wa ulaya kama vile vijana wa
kiume kusuka nywele kuva heleni na
mabinti kuvaa mavazi ya kiume kamavile suruali pamoja na mavazi yanayobana
ambayo yanawavutia na kutoa ushawishi kwa vijana wa kiume. Mavazi haya ni
chukizo kwa Mungu viongozi wa dini serikali wazazi na walezi wameshindwa
kukemea na matokeo yake mavazi
yamechochea ubakaji n.k hadi sasa mavazi haya yanavaliwa hata kanisani
Watumishi wengi hushindwa
kuwakemea waumini wao kwa kuhofia kuwapoteza au kuwakatisha tama katika maisha
ya wokovu. Baadhi ya watumshi kuhofia kukosa waumini wanasahau kuwa kutokemea
ni kuwapoteza kabisa kwani hali hii inaharibbu
ushuhuda kwa kanisani kufanya
wengine wasiokoke(wasimpokee Yesu).
” Mwanamke asivae mavazi
yampasayo mwanaume wala mwanamume asivae mavazi yampasayo mwanamke kwa maana
kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana Mungu wako”.[Kumbu kumbu la
tarati 22:5]
Hivyo viongozi wa dini naomba
msimame kwenye nafasi zenu na kukemea uovu bila woga ili kulijengakanisa na
kufanyawote tufike mbinguni, vinginevyo wokovu wetu utaishia hapa hapa duniani.
2.Mahusiano
Suala la mawasiliano kwa sasa
limeshamiri sana katika jamii. Mika iliyopita masuala ya mahusiano yalitazamwa
kwa jicho la tofauti kwani ilikuwa ni aibu wachumba (wapenzi), kutembea
pamoja ikiwa bado hawajawa wanandoa na vijana wadogo hawakujihusisha katika
mahusiano wala hawakujua chochote
kuhusiana na mapenzi.
Kwa sasa mahusiano kwa watoto
wadogo na vijana imekuwa changamoto
kubwa. Kutokana na utata wa vijana kushindwa kujua n umri upi binti
na kijana waingie katika mahusiano na ni umri upi binti achumbiwe na
kijana achumbie?
Changamoto hii imetokana na
watoto wadogo wanaosoma shule za msingi
na sekondari wanaojiingiza katika mahusiano na kudanganyana au kuahidiana kuoana bila kujua ni kipi kifanyike kati ya kusubiri
wakati wao ufike au kuingia kwenye mahusiano ndipo wamwombe Mungu. Vijana
wanaanza kama marafiki na kuwa wachumba
kwa wakati mmoja ndipo wanamwomba Mungu, wanasahau kuwa Mungu ndiye mwenye
kuianzisha safari lakini wao
wanamshirikisha wakiwa wamesha patina.
Kama kweli kijana amedhamilia kupta
mchumba anapaswa kumwomba Mungu kwani
ndiye mpaji nasi kuchagua
kwani mke si nguo wala sura, bali ni tabia na ajuaye hayo ni Mungu pekee.
“ Je mmekuwa wajinga namana hii?
Baada ya kuanza katika roho mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?[Wagalatia 3:3]
Vijana wengi waamekuwa wakihusiha
katikamapenzi wakiwa na umri mdogo na
matokeo yake wameishia kuathirika na ugonjwa wa ukimwi, magonjwa ya
zinaa,kupata mimba zisizotarajiwa wanafunzi wengi wamefukuzwa shule,kupiga
punyeto kwa vjana wa kiume na usagaji kwa mabinti. Hili ni chukizo kwa Mungu
kwani mwili wako ni hekalu la roho
mtakatifu.
“ ……lakini mwili si kwa znaa, bali ni kwa
bwan, naye Bwana ni kwa mwili aye Mungu alimfufua Bwana na tena atatufufua na sisikwa uwez wake. Je
hamjui ya kuwa miiliyenu ni viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya
kahaa? Hasha! Au hamjui a kuwa yeyee aliyeungwa na kahaba
ni mwili mmjoa naye? Maana asema
wale wawili watakuwamwili mmoja
lakini yeye aliyeungwa na Bwana
ni roho moja naye. Ikimbieni zinaa kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje yamwili wake ila
yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu
ya mwili wake mwenyewe au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la roho
mtakatifu? Aliyendani yenu mlipewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe
maana mlinunuliwa kwa thamani …..”[1 wakorintho 6:13]
Wazazi wengi na walezi wengi wamezembea kaatika suala la malezi
na baadhi yao wamekengeuka na
kuonesha mahusiano yao batili ( nje ya
ndoa) hadharani mbele ya watoto, jambo
ambalo ni kinyume na maadili
yakidini na kiAfrika pia. Wazazi
wamekuwa wakienda dico na kujihusisha
katika mapenzi na vijana wadogo, wengi wakishaingiwa na pepo la uzinzi
na uasherati ni vigumu kujinasua
hubaki wanatapatapa namwishoni
huambuliamauti.
“ Hamjui ya kuwa ninyi ni hekalu
la Mungu nay a kuwa roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu
hekalula Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu
abalo ndilo ninyi”.[1wakorintho
3:16-1]
Wakati umefika vijana kujitambua
, tuamke tujitambue tuache kufuata
mkumbokwani ukimwi na magonjwa ya zinaa vitatumaliza hivyo ni bora kuoa kuliko kufanya zinaa
“Basi kwa habari ya mambo yale
mliyoandika, ni heri mwanaume asimguse mwanamke lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake
mwenyewe na kila mwamanmke na awe
na mme wake mwenyewe”.[1wakorintho
7:1-2]
Kupiga punyeto, kuwa na girl friend au boy
friend si njia ya kuepuka kifo bali
njia pekee ni “kuacha dhambi”.
NI UPI WAKATI MZURI WA
KIJANA(MTU)KUMPATA MWENZA AU MCHUMBA?
Uchumba ni uhusiano kati ya mume na mke wenye lengo la kuishi pamoja kama wanandoa.Hii ni kiwango cha juu sana cha
urafiki kati ya msichana na mvulana ambao wameweka ahadi ya kuoana.Watu wengi
huchumbia ovyo kutokana na kutomruhusu roho mtakatifu ahusike.Usimchumbie binti
kwa kumdanganya ili ukubaliwe,ni vyema kumweleza dhahiri ili ajue hali halisi.
‘’Maana mtu mwenye kukubaliwa si yeye
ajisifuye,bali yeye asifiwaye na Bwana’’[2wakorintho 10:18]Mara nyingi binti
unayeletwa na Mungu hana maswali mengi.
Aina za uchumba
1.Uchumba wa siri (secret
courtship)
Ni uchumba ambao wachumba
wawili wanakubaliana kwa siri bila kushirikisha jamii. Aina hii ya uchumba inafanywa
kiholela, wachumba hao huchangamana na hutambuana vyema. Ila wachumba hao
wasipokuwa makini wataanguka katika
dhambi ya uzinzi na kusalitiana. Aina hii ya uchumba mara nyingi hutumiwa na vjana ambao umri wao haujafikia kuoa wala kuolewa.
2.Uchumba wa wazi(open courtship)
Ni ule uchumba
ambao unafahamika na kanisa au
jamii kwa utaratibu wa makanisa mbali mabali uchumba huu huambatana na kuvishana pete rasmi inayoitwa pete ya uchumba inayoshuhudiwa na mashahidi.
Kilele cha hatua hiii ya uchumba nindoa. Ndoa
ni makubaliano baina ya watu wawili ya
kuisi pamoja kama mume na mke. Ndoa ni
mpango wa Mungu toka mwanzo na
mwanzilishi ni Mungu mwenyewe lakini ili ndoa iwe ndoa ni vyema
ipitie hatua hii ya uchumba .“ Kwa hiyo mwanaume atamwacha
baba yake na mama yake naye
ataambatana na mkewe, nao
watakuwa mwili mmoja” [Mwanzo 2:24-25]
Kipindi cha uchumba nikipindi
kigumu wahusika wanapaswa kuwa makini kwani wanaweza kumkufuru Mungu na
kuanguka katika dhambi bila kujua wakati mwingine uchumba unaweza kuvunjika bila kufikia kilele(ndoa).Changamoto kubwa
kwa vijana huwa ni naye anayestahili kuwa mwenza maana mabinti ni wengi. Vijana wengine hukosea katika kufanya
maamuzi sahii kutokana na kushindwa kujua Mungu kwao. Hii hutokana na wahusika kutafutana bilia kumwomba Mungu na wengine
huanza kuomba wakiwa wameshapatana, wakati mwingine kijana anamwomba Mungu akiwa na sura ya binti au
kijana Fulani anayempenda, hili ni
tatizo kubwa kwa vijana wengi vijana wanapaswa kutambua kuwa ukiingia kwenye uchumba ni vyema
kufiia kilele chake yaani ndoa na
ukiingia kwenye ndoa hupaswi kumwacha mkeo
au mumeo hivyo ni vyema kumwomba
Mungu vya kutosha kabla ya kuchumbia
au kuchumbiwa.
“ Lakini wale waliokwisha
kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi ila Bwana ; mke asiachane na
mumewe lakini ikiwa ameachana naye
na akae asiolewe au apatane na
mumewe ; tena mume asimwaache mkewe”. [1 wakorintho 7:10-11]
Angalizo: si kila wakati unaweza
kuchumbia au kuchumbiwa bali
kuna muda maalumu
“Kwa kila jambo kuna wakati na
majira yake, na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu.[Mhubiri
3;1]
Hivyo ni dhahili kwamb kuna muda
maalum ambao kijana anweza kuchumbia au
kuchumbiwa kwa kawaida baada ya
kutoa pos hapo ndipo uchumba
unapotambliwa rasmi.
DONDOO
Kwa kijana wa kiume kuanzia miaka
25 lakini mazingira ya kiuchumindiyo
yanayoamua
Kwa binti inategemea
maumbile anaweza kuchumbiwa kuanzia miaka20
Kwa anayesoma bila kujali umri
wake anashauriwa kutojiingiza suala la
kuoa au kuolewa bila kumaliza elimu ya awali yaani kidato cha nne na cha
sita
Usiingize suala la kuoa au
kuolewa kama unajua akili yako haijatuliwa
kwaniutaingia katika ndoa bila
kutarajia hasa kwa kusukumwa na tama ya
mwili.
Ujitazame kiwango chako cha
elimu kazi n.k vinaweza kupelekea kuchumbia au kuchumbiwa.
SIFA ZA KIROHO KWA BINTI NA
KIJANA ANAYECHUMBIA AU KUCHUMBIWA
Lazima awe ameokoka na awe
anaishi maisha matakatifu
Zaburi 119:9 anasema
“ Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? kwa kutii akilifuata neno lako.
Aliyejaa neno la Mungu,“Moyoni
mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi’’ [Zaburi 119:11]
Anayejua nini maana ya ndoa kwa
mtazamo wa kiMungu
“Hata wamekuwa si wawili tena,
bali ni mwili mmoja,basi aliowaunganisha Mungu mwanadamu
asiwatenganishi’’[Mathayo 19:3-6]
Anayejua kuwa ndoa ni agano la
kufungamana na bila ya kuachana hivyo
lazima ufikiri kwanza kabla ya kuingia .
“Kwa maana mwanamke aliyena mume amefungwa na
sheria kwa Yule mume wakati anapokuwa yu
hai;bali akfa Yule mume , basi wakati awapo
hai mumewe ,kama akiwa na mume
mwingine huitwa mzinzi” [Warumi
7;2-3]
Ni vyema anayechumbia
au kuchumbiwa ajue kuwa ndoa ni ya watu wawili na sio zaidi kwani bila
kujua hayo matokeo ni mzozo na kuachana au
kupigana kila kukicha.
SIFA ZA KIMWILI ZA KIJANA
Aliyetoka utotoni
Mwenye uwezo wa kuwa mume
Mwenye uwezo wa kuwa baba yaani
kimajukumu awe na uwezo kulisha familia.
Anayejua mkewe anapendelea vitu
gani na je kinachomsukuma kuoa ni nini?
Pressure ya mwili, wakati au umri hasa anapaswa kuwa na hitaji toka moyoni
Anayejijua jinsi alivyo kitabia
kama vile mkimyautapata shida kwani
hakuna hata anyeweza kukaribisha mgeni.
Anayejitambua kitabia uwezo
kielimu kwani si vyema mke akawa juu kielimu kuliko mume.
SIFA ZA KIMWILI ZA BINTI
Aliyetoka utotoni yaani
aliyevunja ungo
Mwenye uwezo wa kuwa mke
Anayejitambua umri wake elimu
yake tabia n.k
Mwenye mawazo yasiyo ya kitoto
na mwenyeuwezo wa kuwa mama
Aliyekomaa viuongo vyake
SIFA ZA KIJANA ANAYESTAHILI KUOA
NA BINTI ANAYESTAHILI KUOLEWA.
Anayemcha Mungu
“kumcha Bwana ni chanzo cha
maarifa,bali wapumbavu hudharau hekima na adabu”.[Mithali1:7]
Unayemfahamu vizuri na kwa muda
wa kutosha historia yake hali yake ya
kiimani n.k
“Nami nitakuapisha kwa Bwana
Mungu wa mbingu na Mungu wan chi kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti
za wakaani ambao nakaa kati yao bali enenda hata nchi yangu na kwa jamaa zangu
ukamtwalie mwanangu Isaka mke”[Mwanzo 24:3]
Kama kuna utofauti wa kiimani
kati yenu ni vyema ukawa makini kujua hali halisi ya kifikra ni yupi
atakayebadili msimamo wake na
kumfuata mwenzie. Ni vyema sana
mkifanana kiimani kabla ya kuoana kwani
usuluhishi wa matatizo ya wanandoa wenye
msimamo tofauti huwa ni mgumu kuisha na hata malezi kwa watoto yanakuwa
magumu kwani baba atawapeleka huku na mama atawapeleka kwake mwisho
watakosa msimamo.
Lakini kama hamjafahamiana kwa muda wa kutosha (mrefu)hakikisha Mungu
anahusika.
Ni vyema kufahamiana viwaango vya
elimu uwezo wa kiuchumi hata viwango vya rohoni , kwani kama viwango vyenuu vya kiroho wote mpo chini
baada ya kuoana mnaweza kupoa kiroho na kuwa wakengeufu.
Anayejituma katika kazi ya Mungu
mwenyewe ,mwenye tabia njema hata kama ana sura ya tofauti na
ulivyotarajia.
Aliyemnyenyekevu, mkarimu au
mtoaji.
Aliyeokoka vizuri na unayempenda
kwa dhati msionane kwa kuoneana huruma kwani baadaye huleta madhara na majuto.
VITU MUHIMU KWA KIJANA KABLA YA
KUCHUMBIA
-Hakikisha una shughuli yeyote
yakuingiza kipato
-Hakikisha una mahali pa kuishi
yaani umejenga nyumba au umepanga zaidi ya chumba kimoja.
-Hakikisha una kitanda godoro
zuri na vyombo vya kupikia viti (kochi au sofa) n.k
-Uwe na mipango endelevu ya
kimaisha na kiuchumi ambayo utamshirikisha
hata mwizi.
NINI KIJANA AFANYE KABLA YA KUCHUMBIA
Fanya maombi ya kutosha, ni
vyema yakawa maombi ya kufunga kwani yanakupa nguvu,kuvuta uwepo wa Mungu na
kumtafakari Mungu zaidi. Usiombe kwa Mungu
ukiwa na sura ya mtu Fulani.
Anza kuomba kabla hujapata wala
kufikiria sura ya mtu fulani kwani Mungu
ndiye kuchagulia na kuidhihirisha.
Omba ushauri kwa wachungaji au watu waliooa kabla ya
kuchukua hatua yeyote.
Endapo Mungu akisema na wewe
juu ya mtu fulani usifanye haraka ili upate muda wa kujiridhisha
Mungu akikudhihirishia kuwa ni yeye
tafuta muda au fuata hatua zinazofaa
ili mzungumze ikiwezekana inaweza kuwa
kanisani, nyumbani kwa mchungaji au mzee wa kanisa na unapoongea naye epuka kushawishi au
kumtongoza kwani mnaweza kuoana kwa kuoneana huruma kwani kuna madhara makubwa mbeleni.
NINI BINTI AFANYE ANAPOCHUMBIWA
Mwombe Mungu vya kutosha,ni
vyema kufanya maombi ya kufunga ili kuvuta nguvu na uwep[o wa Mungu.
Usifanye haraka kujibu “ndiyo
nimekubali”
Mshirikishe mama mchungaji au
mzee wa kanisa atakushauri pia ataomba na wewe
Endapo Mungu atakupa kibali mpe
majibu kwa heshima
Endapo hukupata kibali mjibu kwa
heshima ili usimkwaze,kwani ukimjibu vibaya anaweza kuacha wokovu.
Kama limepata kibali anza kufanya maandalizi mapema na jitahidi kuwa
karibu na akina mama
MAMBO YA KUEPUKA WAKATI WA
UCHUMBA
-Epuka mahusiano yenye lengo baya
-Anza mahusiano kwa mawasiliano kwa tahadhari na epuka zawadi fedha n.k huleta athari
kubwa baadaye
-Ukaribu usiokuwa na kiasi kama
vile kukaa pamoja kuongea pamoja kila
wakati na kuongozana au kutembea
pamoja huleta anguko dhambini.
-Msionyeshane matendo ya mapenzi wakati wa uchumba iwe kwa
message au kwa maongezi.
“……msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha hata yatakapoona vema yenyewe” [Wimbo uliobora 3;5]
-Epuka kukaa muda mrefu
katika uchumba ni vyema uchumba wenu usizidi mwaka mmoja.
3.suala la elimu
Vijana wengi wamejikita katika masuala mbali mbali kama vile uimbaji wa
mziki ya hip hop dansi wavipa
kipaumbele. Hata katika shule mbali mbali za sekondari wanafunzi wengi hutumia
daftari za darasani kuandika nyimbo za hip hop badala ya kuandika masomowanayofundishwa. Hali ii
imewafanya vijana wengi watakuwa waimbaji(wasanii)
Wamesahau kuwa hata kuwa msanii
unapaswa uwe umesoma. Ili mwanafunzi afaulu ni vizuri darasani anapaswa
kuwa na utii heshima na adabu na
anapaswa kumcha Mungu kwani ndiye mpaji
nani cha maarifa.
“ Kumcha Bwana ni chanzo cha
maarifa bali wapumbavu hudharau hekima na adabu”.ni vyema vijana
tujitambue na tujue kuwa Mungu anatuwazia mema hata katika mambo ya
kitaalamuma tunasisitizwa kusoma kwa bidii.[Mithali 1:7]
“Mkamate sana elimu wala usimwache aende zake
maana yeye ni uzima wako”.[Mithali
4:13]
Vijana tuzingatie elimu na tutumie muda vizuri kusoma na kupata
elimu mbal mbali kama vile kujifunza
kuhusu ujasilia mali n.k hii itatusaidia
kujikwamua kiuchumi tuache uzurulaji na kukaa vijiweni bila kazi.
4.Matumizi ya muda
Ni changamoto kubwa na hasa kwa
vijana wengi wa karne hii ya 21. Vijana wengi wanamwomba Mungu ili awafanikishe
katika mambo mbali mbali laikini wakishafanikiwa wanakuwa wazembe kutekeleza maono wanayopewa. Vijana wengi wanaendekeza
usingizi na uzembe katika masomo na katika kazi. Wanafunzi wengi hawasomi
wabidii analala sana na matokeo yake
anafeli mitiani inakuwa hasara kwake na kwa wengine na kuharibu ushuhuda.
Vijana wakati umefika tuamke tufanye
shughuli za maendeleo tusome kwa bidii
tuache kuwa na fikira potofu ili kufikia malengo yetu.
“ Usipende usingizi usije ukawa
maskini, fumbua macho yako nawe utashiba chakula”.[Mithali 20:13]
5/UGUMU WA MAISHA
Maendeleo ya sayansi na
teknolojia yamewaathiri vijana moja kwa moja kwani yamepelekea vijana kukosa
ajira kwani baadhi ya kazi ambazo zilikuwa
zinfanywa na watu hapo awli kwa
sasa zinafanywa na mashine . hali hii
inawasababshia vijana wengi kuwa na maisha magumu
na matokeo yake wanaingia katika
vitendo viovu kama wizzi uporaji
ujambazi utapeli na uvutaji wa madawwa
ya kulevya na mabinti wanajiingiza kufanya ufuska(kujiuza) vitendo hivi
vinahatarisha maisha pia ni dhambi.Hali ngumu ya maisha hijaanza sasa hata wakati wa Yesu ilikuwepo ilipelekea hata yuda kupokea vipande 30 vya pesa na hata vipande
hivyo hakuvitumia.
“Akavitupa vile vipande vya fedha
katika hekalu akaondoka; akaenda akjinyonga”.[Mathayo 27:5]
Suala la maisha magumu haliwezi
kuisha kwa vijana kujihusisha
katika uzinzi(kujiuza) bali ni
kwakomba kwani Mungu wetu anatuwazia
mema.
“Unikumbushe na tuhojian; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako”.[Isaya 43; 26]
“Niite nami nitakuitikitia, nami nitakuonyesha mambo makubwa ,magumu
usiyoyajua”.[Yeremia33:3]
Matokeo yake vijana wengi wanajihusisha na vitendo viovu wamefungwa jera wengine wameuawa na wengine wameathirika
kwa magonjwa.vijana tumwombe Mungu na tufanye kazi kwa bidii ili
tujikwamue kwani vijana wakipukutika
nani atahubiri injili nani atalijenga
taifa?
T u f u n g u k e sasa.
MBINU ZA KUZIKABILI CHANGAMOTO ZA
KARNE YA 21ST C
A.KIMWILI
Vijana wanpaswa kujishughulisha
na kufanya shughuli Mbali mbali ili
kujikwamua na ugumu wa maisha
Vijana wanapaswa kuepuka kuangalia picha
chafu kama vile filamu chafu na kujiingiza
kwenye mahusiano kabla ya wakti na hata
wakati ukifika ni vyema kkumwomba
“Mungu” na si kuingia bila utaratibu.
“Lakini mambo yote na
yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu”.[1wakorintho 14;40]
Kuwa makini na marafiki au kuacha kufuata mkumbo kwani baadhi yaani marafiki wanakupotosha.
“Enendeni pamoja na wenye hekima nawe utakuwa na hekima rafiki wa
mpumbavu ataumia.[Mithali13:20]
Kuachana tamaa ya pesa au mafankio kkutokana
na tama vijana wengi wameingia kutafuta utajiri
kwa njia zisizohalali kama vile
njia za kishirikina na
wengine wamejiingiza katika wizi
ujambazi ubakaji, mauaji n.k bali wapaswa kutulia na kutafakari kuhusu maendeleo na vyema
kuridhika na vile ambavyo
Mungu amekujalia.
“Usiwe na tabia ya kupenda fedha mwe radhi na
vitu mlivyonavyo kwa kuwa yeye mwenyewe amesema sitapungukiwa kabisa wala sitakuacha kabisa”.[Waebrania 13: 5]
B.KIROHO
-Kumcha Mungu kwa bidii
“Kesheni basi kwa maana hamjui ni
siku ipi atakayokuja Bwana wenu lakini fahamuni neon hili kama mwenye nyumba
angalijua ile swala asingeliacha nyumba
yake kuvunjwa.[Mathayo
24:42-43]
“Dumuni sana katika kuomba
mkikesha katika kuomba huku na kushukuru”.[Wakolosai 4:2]
-Ukiomba usipojibiwa au Mungu akichelewa kujibu usimkasirikie wala kumwazia
kwa upmbavu tene usiwaonee wivu wenzako wanaojibiwa maombi yao
maana Mungu humjibu kila mtu kwa wakati wake kwani si kila ombi hujibiwa
kama mwombaji anavyotaka.
-Ukiwa na shida usitoke rohoni na
kuingiamwilini na kuanza kutafuta majibu ya tatizo lako
“ Basi sarai mkewe Abrahamu hakumzalia mwana naye alikuwa
na mjakazi mmisri jina lake
hajiri sarai akamwambia
Abram basi sasa Bwana amenifunga
tumbo nisizae,umwingilie mjakazi wangu
labda nitapata uzao kwa yeye .Abram akasikiliza
sauti ya srai sarai mkewe Abramu
akamtwaa hajiri mmisri mjakazi wake baada ya kukaa Abram katika nchi ya kanaani
miaka kumi akampa Abram mumewe awe mkewe, asi akamwingilia hajiri naye akapata
mimba naye alipoona ya kwamba amepata
mimba bibi yake alikuwa duni machoni
pake….. sarai akamtesa naye akakimbia
kutoka mbele yake”[Mwanzo 16:1-4]
-Kuzishinda tamaa za mwili na
kuepuka maneno machafu. Vijana wanapaswa
kujizuia na si kujiendekeza lakini njia ya kuyashinda ya dunia ni
kwa maombi maana shetani
amepandikiza roho za uzinzi na
uasherati kwa vijana na kuwafanya
vijana kuangamia kwa
magonjwa kama vile ukimwi, kaswende kisonono pangusa n.k
“ Na hao walio wa Kristo Yesu
wameusulubisha mwili pamoja na mawazo
yake mabaya na tama zake………”.[Wagalatia
5:24-25]
“Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kutakaswa
kwenu mwepuke na uasherati”[Wathelonike
4:3]
-kujipambanua nafsi
vijana wanapaswa kujitambua wewe
ni nani na wajibu wako ni nini? Na umeumbwa kwa kusudi gani/
“ lakini kama tumejipammbanua
nafsi zetu tusingehukumiwa,ila
tuhukumiwapo tunarudiwa na Bwana isije ikatupasa adhabu”.[1wakorintho 11;31]
-Vijana hawana budi kutambua hatima ya maisha yao hapa duniani
“ Kwa jasho la uso wako utakula
chakula hata utakapoirudia ardhi ambayo
katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u
mavumbi wewe nawe mavumbini utarudi”.[Mwanzo 3:19]
-Kuwa na msimamo thabiti na
kusoma neno la Mungu na kulitendea kazi
-Vijana wanapaswa kuwa na imani
thabiti isiyo na mashaka kwani
Mungu hapendezwi na watu wenye mashaka.
‘’Basi imani ni kuwa na hakka ya mmbo
yatarajiwayo ,ni ayana ya mambo yasiyoonekana…… kwa imani twafahamu ya kuwa
ulimwengu ulimbwa na Mungu kwa neon
la Mungu hata visivyoonekana”.[Waebrania 11:1]
kama umeamua kuokoka basi
okoka kweli hata ujaribiwe usirudi
nyuma bali mllie Mungu kwani yeye
ndiye muwez a wa yote.
‘’Maana kama vile mwili pasipo na roho umekufa vivyo hivyo na imani
pasipo matendo imekufa”.[Yakobo
2:26]
MADHARA YA UTANDAWAZI KWA KANISA LA LEO
-Mmomonyoko wa maadili
-Kanisa limekuwa la kisasa mno
yaani roho mtakatifu haachiwi nafasi ya
kuongoza.
UTIMIILFU WA UNABII WA UJIO WA
MASIHI
Ujio wa Masihi ulitabiriwa
toka kipindi cha agano la kale. manabii wengi walitumiwa na Mungu
kutabiri dalli na matukio
kadhaa wa kadhaa yatakayotoke.
kwa wakatii ule unabii uliilenga zaidi miji mbali mbali ya Israel iliyokuwepo wakati ule lakini pia
ulilengasiku za mwisho.
KUZALIWA KWA YESU
Yesu alizaliwa Bethelehem ya
uyahudi mji ambao mwanzoni ulikuwa mdogo kilometa chache kusini ya yerusalem.
Ulikwisha kuwa mji wakati wa yakobo
jirani na mji huo kulikuwa na mahali ambapo yakobo alimzika mke wake rahel.
“Akaja rahel akazikwa katika njia
ya efrathi ndiyo bethelehem, yakobo akasimamisha nguzo ya kaburi la raheli hata leo”.[Mwanzo 35:19-20]
Mji wa bethelehem ulikuwa katika
eneo la kabila la yuda. Nchi yake ilikuwa ya milima lakini ilifaa kwa kulima nafaka
na kufuga kondoo
‘’Ikiwa zamani za waamuzi walipoamua
kulikuwa na njaa katika nchi. Akaondoka mtu mmoja akaenda mi wa bethelehem ya yuda akaenda
kukaa nchi ya moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili”.mfalme mkuu wa Israel
Daudi alitoka bethelehem [Ruth 1:1]
“ Basi Daudi alikuwa mwana wa yule mwefrathi wa bethelehem ya yuda
aliyeitwa jina la yese; naye huyo alikuwa
na wana wanane; nay eye mwenyewe
alikuwa mzee siku za sauli na mkongwe miongoni mwa watu”.[1 samwel 17:12]
Hata Masihi aliyeahidiwa alizaliwa
huko; manabii wengi walitabiri kuwa
Masihi yaani yes Kristo attazaliwa huko.
“Bali wewe bethelehem efrathi
aliyemdogo kuwa miongoni mwa elfu za yuda; ktoka kwako wewe utanitolea mmmoja atakayekuwa mtawala katika Israel; ambaye matokeo yake
yamekuwa tangu zama za kale tangu milele”.[Mika 5:2]
Wakati wa utimilifu wa unabii huu
wa kuzaliwa kwa Masihi “Mungu”
aliwataarifu mamajusi pamoja na wachungaji wa makondeni na walikwenda
kumsujudia Yesu bethelehem,hivyo basi Mungu akitaka akutumie haangalii sura
mazingira wala kabila wala elimu bali
utayari wako. Kwa wakati ule
wachungaji waa makondeni walikuwa
ni watu wa hali ya chini. Walikuwepo wasomi kama waandishi na mafarisayo lakini Mungu hakuwa taarifu hao kwanza.
YESU
KRISTO
Jina la Yesu lilikuwa ni jina la
kwaida la kiyahudi nalo lilionekana katika
lugha ya kiyunani ya agano jipya likiwa sawa na jina la “Yoshua” la
kebrania katika agano la kale. Maana ya jina la “Yesu” ni “Yahweh” (YEHOVA) ni
mwokozi wetu na hivyolilifaa kuwa
jina kwa yeye ambaye aliokoa watu wake yaani wenye dhambi.
“Naye atazaa mwana nawe utamwita jina lake
Yesu, maana yeye ndiye atakayewa okoa watu
wake na dhambi zao”.[Mathayo
1:21]
Kristo lilikuwa neno la kiyunani
lililokuwa sawa na neno kiebrania Masihi
MASIHI
Neno Masihi linatokana na lugha
ya kiebrania na maana yake ni mpakwa mafuta. Wana wa Israeli wakati wa agano la
kale walifanya sherehe ya kukupakwa mafuta kwa mfaime. Makuhani na marunyinoine
kwa manabii kwaajili ya kuwaweka raomi katika huduma zao. Katika sherehe za
namna hiimafuta ya pekee ya kazi hiyo yalimiminwa kichwani pa mtu akiwa ishara
ya kuwa tumon wakati huo alikuwa na haki
na madaraka ya kutekeleza huduma
iliyolingana na wito wake .
“Mwite huyo
nduguyo Haruni na wanawe nao
mavazi hayo nawe watie mafuta na kuwaweka kwa kazi takatifu na kuwatakasa ili
kunitumikia mimi katika kazi yaukuhani”.[Kutoka
28:41]
“Na Yesu mwana wa Nimoihi mtie mafuta awe
mfalme wa Israel. Na Elisha mwana shafati wa Abel mehola mtie mafuta awe nabii
mahali pako”.[1Wafalme
19.16]
Wakati wa agano jipya nchi
zilizokuwa zinatumia lugha ya kiyunani neno la kiebrania kreno nalo pia lilikua na maana ya mpakwa mafuta
WAKATI WA AGANO LA KALE
Wakati wa agano la kale neno
mpakwa mafuta lilitumiwa zaidi kwa mfalme wa Israel ambaye ambaye mara
nyingi aliitwa mpakwa mafuta
“Tazama leo hivi macho yako
yanaona jinsi Bwana alivokutia mikononi mwangu pangoni na watu wengine
wakaniambia nikuue; lakini nikakuacha ;
nikasema sitaki kunyoosha mkono wangu
juu ya Bwana wangu; kwa maana yeye ni “Masihi” wa “Bwana”.[1Samwel 24.10]
Katika kipindi cha kwanza taifa
la Israel lilikuwa kama ukoo mkubwa tu. Mungu alionyesha kwamba
uongozi wa taifa kwa wakati wa usoni ungekuwa katika kabila la Yuda. Kutokana na kabila hilo angepatikana ambaye angetawala Taifa na kwa amani mafanikio na
furaha tele.
“………………………………….fimbo ya enzi
haitaondoka katika yuda wala mfanyashria kati ya miguu yake, hata atakapo kuja yeye
mwenye milki ambaye mataifa watamtii
atafunga punda wake katika mzabibu mzuri amefua nguo zake kwa mvinyo
na mavazi yake kwa damu a zabibu”
karne kadhaa baadaye Mungu alikutekeleza
unabii huo kwa kumwahidi mfalme
Daudi (aliyekuwa mtu wa kabila la yuda) ufaalme wa ttofauti yake ambao ungekuwa ufalme wa milele.[Mwanzo 49:10]
‘’Na nyumba yako na ufalme wako
vinathibitishwa milele mbele yakonacho kiti chako kitafanywa imara milele
kwa maeno hayo yote ndiyo na maneno hayo yote,ndiyo nathani alivyonena
na Daudi”[2Samwel
7:16-17].
WaIsrael waliishi kwa kutazamia
wakati ambapo maaui wote wangeangamizwa
na mfalme bora angetawala kwa
amani na haki ulimwenguni kote. Mfalme na mwokozi Yule angeitwa “MASIHI”
Mungu alipomwahidia Daudi ufalme
wa pekee pia aliahidi kwamba angemtendea
mwana na mfuasi wa Duadi kama
mwanawe yeye Mungu
“Mimi nitakuwa baba yake atakuwa
mwanangu;akitenda maovu nitamwadhibu kwa
fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu”[2 samwel7;14]
Wa Israel waliona kuwa kila
ushahidi juu ya maadui zao kama mfan wa ushindi
muu wa ushindi mkuu wa Masihi na uwekaji wa ufalme wake. Waliwasifu wafalme wao katika lugha ilivyokuwa
ya hali ya juu. Zaidi hata iwe kweli kwa wafalme waliohusika. WaIsrael waliyatazamia mambo
makuu katika ufalme wao.lakini kwa
utimilifu wake ulimhusu mfalme
mkamilifu yaani “Masihi”.
TAFSIRI MBALI MBALI ZILIZO MHUSU
MASIHI
Utabiri Uliotabiriwa na Manabii
haukutimilizwi katika ufalme wowote
wa kipindi cha mfalme wa Daudi katika agano la kale lakini jambo
hili haliku wakatisha tama siku zote walitazamia Yule
ambaye angekuwa “ Daudi” mkuu wa wakati ujao
“………maana kwa ajili yetu mtoto
amezaliwa,tumepewa mtoto mwanamume; na
uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
naye ataitwa jina lake mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu, baba wa milele mfalme wa amani maongeo ya enzi yakena amanii hayatakuwa na mwisho kamwe, katika kiti cha
enzi cha Daudi na ufalme wake……”[Isaya 9: 2-7]Mfalme huyo alikuwa
Yesu Kristo
“Kitabu cha ukoo wa Yesu
Kristomwana wa Daudi mwana wa Ibrahimu”[Mathayo 1:1]
Wayahudi waliitafsiri
zabuburi ya 110 wakati wa Yesu kuwa
zaburi hiyo ilimhusu Masihi ingawa waliukataa. ‘ Umasihi wa Yesu “ kwa kuwa
mfalme wa zaburi 110 pia alikuwa kuani Yesu hakuwa mfalme wa Umasihi
tu bali pia kuhani wa umasihi.
‘’Bwana ameapa, wala hataghairi
ndiwe kuhani hata milele, kwa mfano wa melkizedeki’’ [Zaburi 110:4]
Utawala wa Yesu wa muungano wa
ukuhani na ufalme wa unabii uliotabiriwa katika kitabu cha nabii Zakaria.
“Ukamwambie ukisema Bwana wa majeshi anasema
hivi yakwamba tazama mtu huyu ndiye ambaye jina lake chipukizi naye atakuwa
katika mahali pake naye ataliinua hekalu
la Bwana, naamu yeye atalinoa hekalu la Bwana. Naye atachukua huo utukufu
ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi na kuta kuwa na kuhani katika kiti
chake cha enzi na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili”.[Zakaria 6:12-13]
YESU NA WAYAHUDI
Yesu alikuwa Masihi kakini
hatangaza uMasihi wake hadharani kwani wayahudi wakati ule walikuwa na uelewa kinyume kuhusu Masihi wayahudi hawa kujali
sana kazi ya kiroho ya Masihi kwani wao hawa kutazamia kiongozi wa kiroho
ambaye ange waokoa watu kutoka katika utumwa wa adui shetani na kuwaweka chini
ya utawala wa Mungu. Badala yake walitazamia kiongozi wa siama ambaye
angewaokoa kutoka katika malaka ya warumi na kuleta ufalme mpya na uhuru waa
Israel ambao ungekuwa wa amani , uliuvu na mafanikio.
“ basi walipo kutanika
wakamuuliza wakisema je’ Bwana wakati huu ndipo utakapo waludishi Israel ufalme
akawaambia si kazi yenu kujua nyakati wa majira, baba aliyo yaweka katika
mamlaka yake mwenyewe’’[Matendo 1:6-7]
Aidha kama Yesu angetangaza
hadharani kuwa ndiye Masihi kabla ya kuonyesha uMasihiwake angewavuta wafuasi
wengi wa aina kinyume
Yesu haku kataa jina la Masihi
lakini alipendelea kulikwepa alipo sema
habari ya nafsi yake alipendelea kujiita mwana wa adamu wayahudi wengi walifiri
analitumia kumaanisha ni yeye tu kumbe jina hili lilikuwa na maana ya pekee tu
kwa wale waliokolewa halihlisi ya ukweli wa Yesu Kristo pamoja na umasihi wake
Lengo la Yesu kujiita mwana wa
adamu nikuwafanya watu wafkiri sana nafsi yake na ujumbe wake ulikuwa juu ya
nini.
“Basi makutano wakajibu sisi tumesikia katika
toraiti yakwamba Kristo adumu hata
milele nawe wasemaje imempasa mwana wa adamu kuuliwa, huyu mwana wa adamu ni nani
[Yohana 12: 34]
Jina mwana wa adamu,linatokana na
unabii uliotolewa na nabii Danieli wakati wa agano la kale,“Nikaona katika
njozi za usiku natazama mmoja aliye mfano mwanadamu akaja pamoja namawingu ya
mbingu,akamkaribia huyo mzee wa siku wakamleta karibu naye akapewa mamlaka na
utukufu na ufalme ili watu wa kabila zote na taifa zote na lugha zote wamtumikie,.mamlaka
yake ni mamlaka ya milele ambayo hayata pita kamwe na ufalme wake ulio wezwa
kuangamizwa [Danieli 7. 13:14] Maana ya mwana wa adamu uliunganishwa ni ile ya
ufalme wa Mungu na jambo hili lilikuwa msingi wa maneno ya Bwana Yesu kujiita
mwana wa adamu.Yesu alipofika duniani ufalme ulifika duniani. (Ulimwenguni)
nakuonekana dhahiri kwa watu wakati huo ulimwengu ulikuwa chini ya nguvu za
shetani.
“Ambao ndani yao Mungu wa dunia
hii amepofusha fikra zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake
Kristo aliye sura yake Mungu”.[2Wakorintho
4:4]Lakini Yesu aliwaweka watu wote
waliokuwa wamefungwa na shetani
pamoja na wagonjwa aliiwaweka huru.
Hii ilikuwa ishara ya kuwa utawala na mamlaka ya ufalme wa Mungu huweza kuwaweka watu huru kutoka katika mamlaka ya shetani.
“ Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote akifundisha katika masinagogi yao na na kuihubiri habari njema ya ufalme na kuponywa ugonjwa na udhaifu
wa kila namana katika watu”.[Mathayo 4:23-24]
Pia mathayo 12: 28 anasema “
Lakini nikitoa pepo kwa roho wa Mungu , basi ufalme wa Mungu umekwisha
kuwajilia”.Ufalme wa Mungu utadhihirishwa
dhahiri na kupata maana
halisi kwa wasioamini wakati Yesu
atkaporudi ili ahukumu uovu na waovu na kumwondoa shetani ili
kusimika utawala wa Mungu uliyo
wa haki.
“ Basi kama vile magugu
yakusanywapo na kuchomwa motoni; ndvyo
itakavyokuwa katika wa dunia. Mwana wa
Adamu atawatuma malaika zake nao watakusanya kutoka katika ufalme
wake maachukizo yote na hao
watendao maasi na
kuwatupa katika tanuru ya moto
ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Ndipo wenye haki watakapo ng’aa kama jua katika ufalme
wa baba yao mwenye masikio na asikie”Mathayo 13:40-43]
Lakini maono ya Daniel
yanaonyesha kuwa “ mwana wa Adamu “ atashiriki ufalme wake
na watu wake.
“ Na ufalme
na mamlaka na uku wa ufalme
chini ya mbingu zote watapewa
watu watakatifu wake aliyejuu; ufalme wake ni ufalme wa milele
na wote wenye mamlaka watamtumikia
na kumtii”.[Daniel
7:27]
Wakati mwana wa Adamu yupo
duniani aliwaahidi wale waliomfuata
kwa kutenda matendo mema
kuwaatashrikiana nao katika ufalme wake.
“Yesu akawaambia amini nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya
atakkapoketi mwana wa Adamu katikakiti
cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi
katika viti kumi na viwili mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israel”[Mathayo 19;28]
MAISHA YA YESU KRISTO
Waandishi wa injili walitoa maelezo zaidi kuhusianana namna Yesu
alivyoishi na kufundisha lakini
hawajaeleza mfululizo maalmu
wa maisha yake. Waandishi hao
waliandika katika vipindi tofauti
na sehemu a miktadha(mazingira)
mbali mbali.
“Basi kuna ishara nyingi alizozifanya
Yesu mbele ya wanafunzi wake
zisizoandikwa katika kitabu hiki, lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, mwana wa Mungu na kwa kuamini mwe na
uzima kwa jina lake”[Yohana 20:30-31].
Katika mandishi yao waandishi
wote hawajatofautiana katika kueleza nafsi
ya Yesu kadri walivyotaka kuionesha. Yesu ni Mungu
pia ni bawana na mwokozi wa ulimwengu.
Masimulizi mbali mbali ya
maisha ya Yesu katika injili
nne za mwanzo tunaweza kuyagawa katika
sehemu tatu kama ifuatavyo;-
1. Kuzaliwa kwake na utoto wake
2. Huduma yake ya hadharani kama
vile mafundisho yake uponyaji miujiza na
mambo mengine yaliyomhusu Yesu.
3.Matukio ya mateso kifo na
kufufuka kwake.
Masimulizi kuhusu Yesu
alivyozaliwa katika biblia takatifu yanachukua nafasi kubwa. Wandishi wa injili hawajaeleza
kuhusu utoto wake mpaka alipopata umri wa miaka 12. Lakini hata kipindi akiwa na umri mdogo Yesu alijua na kujitambua dhahiri kuwa alikuwana uhusiano wa pekee na Mungu kwa sababu alikuwa mwana wa Mungu.
“ Na alipata umri wake yapata miaka kumi namiwili walipanda kama
ilivyodesturi ya sikukuuna walipokwisha kuzitimiza siku wakati wa kurudi kwao, Yule mmtoto Yesu
alibaki nyuma hhuko Yerusalemu, na wazee
wake walikuwa hawana habari…….. nao wote waliomsikia walistaajabu
fahamu zake na majibu yake ….”[Luka
2:42-49]
Pia waandishi wa injili
hawajaeleza juu ya miaka 18 iliyofuata katika
maisha yake. Walianza kueleza
alipokuwa na miaka 30
“ Naye Yesu mwenyewe alipoanza kufundisha alikuwa amepata umri wake
kama miaka 30 ….”[Luka
3:23].Pale mto Yordan Yesu alibatizwa naaliyembatiza alikuwa ni Yohana
mbatizaji, Yesu alibatizwa na kuanza huduma yake hadharani. Ubatizo wa
Yesu ulionesha mambo
makubwa mawili;-
1.Alikuwa tayari kutekeleza
makusudi aliyotumwa na Mungu.
2.Alikuwa na uhusiano na alijiunganisha dhahiri
na watu ambao alitaka kuchukua dhambi zao.
Ili kuthibitisha hayo Mungu
alimtuma roho mtakatifu kama njiwa (hua)
juu yake
Hii ilikuwa ishara ya wazi
kuwa alimpa uwezo wa
kuitenda(kuifanya) kazi aliyomtuma.
Mara baada ya Yesu kupokea uwezo
wa pekee kutoka kwa Mungu Yesu
alijaribiwa na shetani ili atumie uwezo
wake pasipokuunganishwa na baba yake
lakini Yesu alishinda jaribu hilo.
“ Kisha Yesu alipandishwa na roho nyikani ili ajaribiwe na ibilisi akafunga siku arobaini mchana na
usiku mwisho akaona njaa……… ukiwa ndiwe mwana wa Mungu amuru kwamba mawe haya
yawe mkate………..imeandikwa mtu hataishi kwa mkate tu ila kwa kila neon litokalo
katika kinywa cha Mungu………ukiwa mwana wa Mungu jitupe chini
kwa maana imeandikwa;atakuagiza malaika zake na mikononi mwao
watakuchukua………….”[Mathayo
4:1-11]
Baada ya Yesu kushinda jaribu
hilo alianza moja kwa moja kufanya kazi aliyokabidhiwa na baba yake.Huduma
ya Yesu ilichukua miaka mitatu na nusu.
Yesu alifanya huduma zake nyingi galilaya kwa sasa ni sehemu za kaskazini mwa
Palestina. Alikutana na upinzani mkubwa kutoka maeneo ya kusini mwa
uyahudi(uyahudi kusini) hasa mjini yerusalem mji ambao yalikuwa makao makuu ya mamlaka ya dini ya
kiyahudi.Viongozi wa kiyahudi waliona kuwa Yesu
kuitwa mwana wa Mungu kama ni kufuru hivyo walipinga asiitwe masihi.
‘’mbona asema hivi?Anakufuru.Ni
nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmojandiye Mungu?”[Marko 2:7]
Yesu aliijua kuwa mwisho wa
huduma yake angeuawa na wayahudi wa Yerusalemu; lakini alitambua kuwa alipaswa
kumaliza kazi aliyotumwa na Mungu(baba
yake) na baada ya kumaliza kazi ile kwa wakati maalumu uliopangwa na baba (Mungu) ulipofika aliacha wayahudi
wamkamate na kumsulubisha.
“Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu
aliyenyoosha mkono wake ili kumshika
kwani sababu saa yake ilikuwa haijaja bado”.‘[’Yohana 7: 30]
KUFA KWA MASIHI NA KUFUFUKAKWAKE
Wanafunzi wa Yesu hawakuelewa
kuwa Yesu alipaswa kufa na hata wayahudi
wengi walijua unabii wa agano la kale kuhusu
mtumishi wa Mungu aliyeteswa sawa
sawa na walivyojua unabii kuhusu Masihi
wa Mungu lakini hawakuunganisha mambo yote
mawili yaani unabii wa mwana wa
Mungu aliyeteswa na unabii wa Masihi.
“ Tazama mtumishi wangu
alitenda kwa busara, atatukuzwa na
kuinuliwa juu naye atakuwa juu sana”.[Isaya
52: 13]. Yesu alidhihirisha dhahiri “
kuwa yeye alikuwa yote yaani mtumishi aliyeteswa na Masihi
wa Mungu. Aliwambia wanafunzi wake
kuwa alikuwa Masihi na alipaswa kufa.“ Ila nawaambia ya kwamba Elia
alikwisha kuja, wasitambue lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo mwana
wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao”[Mathayo 17:12]
Kusulubiwa kwa Masihi ilikuwa
kinyume cha imani ya kawaida ya wayahudi kwani kwao waliamini kuwa “Masihi” ni mbarikiwa wa Mungu kuliko watu
wote na mtu aliYesulubiwa waliamini
alilaaniwa na Mungu.“ Kristo alitukomboa
katika laana ya torati kwa kuwa alifanywa
laana kwa ajili yetu;maana imeandikwa, amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya
mti”.[Galatia
3:13]Hivyo imani ya wa kristo ya kumwamini
Yesu aliYesulubiwa ikiwa ni
mwokozi na Masihi ilikuwa kikwazo kwa wayahudi.
Ufunuo wa YesuKristo ulileta sura
mpya naya tofauti kwani kitendo
cha kusulubiwa lilionekana tatizo kubwa. Hata wanafunzi wake hawakuelewa
alipowatabiria kuhusu ufunuo wake. “ Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake mwanan wa Adamu yuaenda
kutiwa katika mikono ya watu nao watamwua; hata akiisha kuuawa baada
siku tatu atafufuka, lakini hawakulifahamu neon lile wakaogopa kumwuliza”.[Marko 9:31-33].Alipofufuka
alithibitisha tosha kuwa Yesu alikuwa “mwana wa Mungu” na “mpaka mafuta” wa
kweli toka kwa Mungu.“Yeye mwenyewe alitangulia kuyaona haya alitaja habari za
kufufuka kwake Kristo ya kwamba roho yake haikuachwa kuzima wala mwili wake
haukuona iharibifu”.[Matendo
2:31]
UJIO WA MASIHI WALIVYO CHUKULIA
WAKATI WA AGANO LA KALE
Wa Israel wa wakati wa agano la kale
walitazamia siku ambbayo Mungu
angechukua hatua katika mambo yote ya wanadamu akitengeneza yaliyo kinyume na
kuimarisha utawala wake
duniani waliita tukio hilo “ Siku ya ya Bwana” ingawa siku ya Bwana kwa kawaida ilifikiriwa kuwa jambo la kutisha waIsrael
mara nyingi waliitazamia kwa
sababu maadui zao na kuwaletea waIsrael wakati wa Baraka kubwa.
“ Hivyo siku ya Bwana ilivyo kuu
i karibu, nayo inafanya haraka sana;
naam sauti ya siku ya Bwana shujaa hulia
kwa uchungu mwingi huko! Siku ile siku ya ghadhabu,siku ya
fadhaa na dhiki, siku ya uharibifu na ukiwa, siku ya giza na utusi tusi, siku ya mawingu na giza
kuu”.[Sefania 3;14-15].Lakini walishindwa kutambua
kuwa siku hiyo Mungu angewaadhibu
wenye dhambi wote pamoja na waIsrael na kuokoa wote walio waaminifu bila kujali
taifa lao wala hali yao katika jamii.“Ole wenu ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani
siku ya Bwana; ni giza wala si nuru”.[Amosi
5:18]
Mambo mbali mabali ya kutisha
kama vile mafiriko
ya naji njaa kali vita waliita
siku ya Bwana. Lakini maarifa kama hayo
yalikuwa ni utangulizi wa siku ile kubwa
na ya mwisho.‘’Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu
na katika dunia,damu na moto na minara ya moshi. Jua litageuzwa kuwa
giza na mwezi kuwa damu kabla haijaja
siku ya Bwana iliyo kuu itishayo. Na
itakuwa kwamba mtu awaye yeyote atakayeliita jina la Bwana
ataponywa; kwa kuwa katika mlima sayuni na katika yerusalem watakuwako watu
watakaookoa kama Bwana alivyosema; na katika mabaki hao awaitao Bwana”.[Yoel 2;30-32]
KURUDI KWAKE KRISTO KWA SHANGWE
NA USHINDI
Kurudi au ujio wa Kristo mara ya
pili ni kilele cha mambo yote
aliyoyafanya wakati yupo duniani na huo ndio utakuwa utimilifu wa mambo yote yaaani ushindi juu ya dhambi mauti na shetani
wokovu wa wandamu kipawa cha uzima wa milele uponyaji wa ulimwengu wa viumbe
vinvyoonekana na kusimamishwa kwa ufalme wa Mungu“ Na hao watakwenda zao
kuingia katika Adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa
milele.[Mathayo
25;46]
Kurudi kwa Yesu (Masihi)mara ya
pili “siku ile ya Bwana ya mwisho”
ambayo kilele cha historia ya ulimwengu.“Naye
Bwana atakuwa mfalme juu ya nchi yote;
siku hiyo Bwana atakuwa mmoja na jina lake moja. [Zakaria 14:9]
Wakati wa agano la kale na agano jipya manabii walitabiri kuharibiwa kwa miji
tofauti ya wakati ule ambayo ilikuwa
imejaa uasi na dhambi kama vile kuangamizwa kwa Yerusalemu. Nji
wayerusalem ulikuwepo tangu miaka mingi
na katika kiindi hicho Yerusalemu
ilibadilka mara nyingi mabonde yalijazwa
milima ilichonga milima
mingine ilitokea kutokana mafungu ya
kifusi na takataka na mipaka
ya Yerusalemu ilibadilika kutoka
kizazi kimoja na kingine. Lakini sura ya
mji uliojengwa juu ya mwinuko usio sawa uliendelea vile vile tangu
wakati wa biblia.
Hapo mwanzo mji wa Yerusalemu
ulijuulikana kwa jina lake fupi la
“Salemu” nao ulikuwa mji wa melekizedeki aliyekuwa mfalme na kuhani wake.“ Na melkizedeki mfalme
wa salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliyejuu sana”[Mwanzo 14:18]
WaIsrael wlipoingia kanaani mji huo ulikuwa na wayebusi
nao uliitwa yebusi. Mara ya
kwanza waIsrael waliuteka mji huo
pamoja na maeneo yake, baada ya
muda mfupi wenyeji wa asili waliuteka tena. Nji huu ulikuwa katika eneo la urithi la Benyamini lakini wayebusi
waliumiliki mpaka wakati wa enzi ya Daudi.“ Tena katika habari ya
wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa yuda hawakuweza kuwatoa; waliokaa pamoja na wana wa yuda huko Yerusalemu hata hivi
leo”.[Yoshua 15: 63]
Mfalme Daudi alikuwa na makusudi
mbali mbali yaliyopelekea kuuteka mji wa
Yerusalemu na kuuweka uwe makao maku ya
ufalme wake. Na kwa wakati huo Yerusalemu ni nji ambao haukumilikiwa na kabila
lolote la Israel.Wayebusi walidhani mji wa Yerusalemu usingeweza kutekwa lakini mashujaa wa Daudi waliuteka kwa mashambulizi ya kushtusha. Waliingia Yerusalemu kwa kuitia
kwenye pango ambalo wayebusi walilitumia
kwa kuleta maji mjini kutoka nje ya ukuta wa mji.“ Lakini Daudi aliipiga
ngome ya
sayuni; huu ndio mji wa Daudi .
naye Daudi alisema siku hiyo
yeyeatakatewapiga wayebusi na apande
kwenye mfereji wamaji na kuwapiga
na hao vipofu ambao roho yake Daudi inawachukia. Kwa sababu hii watu
husema wapo vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani. Basi Daudi akaa
ndani ya ngome hiyo akaiita mji wa Daudi
kasha Daudi akajenga toka
milo na pande za ndani….”[2samwel 5: 7-10]
Malengo ya Daudi yalikuwa kufanya
Yerusalemu kuwa makao makuu ya
serikali na dini pia. Aliweka sanduku
la Agano katika hema la pekee
alilokuwa ameliweka mjini kwajili
ya makusudi hayo.“Wa kaliingiza sanduku la Bwana na kuliweka
mahali pake katikatiya hema,aliyoipiga Daudi kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za
amani milele mbele za Bwana”.[2Samwel 6:1-17].Daudi
alifanya mpango kwa ajili ya mwanawe ambaye angerithi kiti chake
cha enzi ili ajengehekalu la kudumu.
Baada ya sulemani kurithi kiti cha enzi cha
mfalme Daudi aliufanya nji wa Yerusalemu
uwe nji wa ufahari uletao sifa kwa
taifa lote na alijenga jengo kubwa la
kifalme na majengo mengine yenye
ufahari. Lakini siasa yake ya kunyanyasa watu kuwalazimisha kufanya kazi bila malipo yeyote
na walipe kodi nyingi alijenga mawazi
ya uasi miongoni mwao matokeo yake
makabila mengi ya Israel
yalijitenga na Yerusalemu
baada kufa kwake Sulemani.
“Baba yako alifanya zito kongwa letu basi sasa
utupunguzie utumwa mzito tuliotumikishwa na baba yako na lile kongwa zito
alilotutwika nasi tutamtumikia……….”[1falme 12:1-19]
Makabilamawili tu yalisalia na
uaminifu wao kutoka kwa mfalme Daudi kwa
pamoja yaliitwa ufalme wa yuda na mji
wao mku ulikuwa Yerusalemu kama ilivyokuwa awali.Makabila menginekumi yalijiita Israel
yakaimarisha utawala wao kaskazini
wakiwa na mji wao mkuu pamoja na
kanuni na dini zao.
Mwaka 605 Kabla ya Kristo(KK) mji
wa Yerusalemu uliwekwa chini ya
utawala wa Babeli na baada ya kufanya maasi mara kwa mara mi wa Yerusalemu ulibomolewa na wababeli
mnamo mwaka 587 Kabla Kristo.Ikawa katika mwaka wa kenda wa kutawala kwake,
katika mwezi wa kumi na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebu kadreza mfalme wa
Babeli akaja yeye na jeshi lake
lote kupigana na Yerusalemu
akapanga hema zake kuukabiili…… basi nji huo ulihusuriwa hata mwaka wa
kumi na moja wa mfalme sedekia’’[2
Wafalme 25:1-12]
Mwaka wa 539 Kabla Kristo waajemi
waliwashinda na kuwapindua wababeli wakawapa wafungwa wote uhuru. Wayahudi
walirudi katika nchi yao wakaanza kujenga Yerusalemu
kwa upya.“ Kisha nikawambia mnaona hali hii dhaifu tuliiyonayo jinsi
Yerusalemu ulivyo hali ya ukiwa na
malango yake yalivyoteketezwa kwa moto;
haya na tuujenge tena ukuta wa
Yerusalemu ili tusiwe shitumu tena”.[Nehemia 6:17]
Miaka michache
baadaye(iliyofuata) wayahudi walijenga
hekalu upya pamoja na mji wenyewe na kuta
zake kama ilivyooneshwa
hapo juu. Nehemia alipomaliza kazi yake
historia ya Yerusalemu katika Agano la kale ilifikia mwisho wake. Mwaka 333 Kabla Kristo Iskanda
mkuu alishinda mfalme wawaajemi na
mwaka uliofuata aliikuwa mtawala
mkuu wa Yerusalemu lakini baada ya miaka
michache tu ufalme wa uyunani
uligawanyika. Upande wa mashariki kullikuwa nasehemu mbili yaani misri na
shamu(syria) hivyo palestina ilitawaliwa na wamisri mpaka mwaka 198Kabla Kristo
na baadaye Shamu.
Mwaka wa 168Kabla Kristo mapigano yalitokea miongoni
mwa makundi mbali mbali ya wayahudi wa Yerusalemu
mtawala wa shamu Antioko IV
Epifania alitumia nafasi ile
kushambulia Yerusalemu na kuua wayahudi
wengi lengo lake ilikuwa aharibu dini ya
kiyahudi. Baada ya kujenga madhabahu ya kiyunani katika hekalu la wayahudi alichukua wanyama walikuwa najisi na haramu
kwa wayahudi na kuwatoa sadaka kwa miungu ya kiyunani.Wayahudi walikuwa
chini ya uongozi wa wamakadayo walikusanya jeshi la kumpinga Antioko. Baada ya
miaka 3 ya vita vya kupigania uhuru,
wayahudi walipata uhuru wakidini
wakatakasa hekalu upya.
Mwaka 165 Kabla Kristo wamakabayo waliendelea
kupigania uhuru mpaka miaka 20 baadaye wakapata uhuru kamili.Miaka 80 iliyofuata
Yerusalemu uliendelea kuwa uhuru
lakini migongano ya wayahudi kwa
wayahudi mwishoni ilileta warumi ambao
mwaka 63Kabla Kristo walibomoa hekalu na kuchukua utwala
wa Yerusalemu.warumi walimweka mtawala juu ya Palestina aliyeitwa Herode ambaye alisaidiwa na serikali ya Rumi kufanya kazi ya
kujenga upya mji wa Yerusalemu kwa muda mfupi kabla ya wakati wa agano la jipya.Kwa wayahudi kazi yao kubwa ilikuwa
ujenzi wa hekalu jipya baada
ya kubomolewa kwa hekalu
la zerubabeli na warumi mwaka wa
63 KK lilijengwa mahali pa mahekalu yaliyotangulia lakini lilikuwa kubwa na zuri
zaidi. Kazi yake ya ujenzi ilichukua
zaidi ya miaka 40 muda mrefu baada ya kufa HERODE.
“ Basi wayahudi wakasema , hekalu
hili lilijengwa katika muda wa
miaka arobaini na sita nawe utalisimamisha kaika siku tabu”.[Yohana 2:20]
HISTORIA FUPI YA YERUSALEMU YA HIVI KARIBUNI
Mwaka 66 KK kulikuwa na maasi
dhidi ya warumi yaliyoendeshwa na kundi
la wachokozi wa kiyahudi matokeo yake
warumi walishambulia Yerusalemu kwali
ukali wa kijeshi. Mwaka 70 Baada Kristo sehmu kubwa ya nji pamoja na
hekalulibomolewa kama yeru alivyokuwa ametabiri.
“Alipofika karibu aliuona mji akaulilia akisema laiti ungelijua
hatawewe katika siku hii yapasayo
amani!lakini sasa yamefichwa machoni
pako. Kwa kuwa siku zitakuja adui zako watakapokujengea boma.likuzunguke
watakuzingirana kukuhusuru pande zote watakuangusha chini wewe na watoto
wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya
jiwe kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako”.[Luka 19:41-44 ]
Warumi walijenga Yerusalemu upya
mwaka 132 Baada ya Kristo wakatangaza
uwe mji wa kitaifa ambamo wayahudi
hawakuwa na ruhusa ya
kuingia.Kostantino alipokuwa kaisari wa warumi mwaka 313 Baada ya Kristoalitangaza
Yerusalemu uwe uwe mji wa Kristo. Mwaka
wa 637 Baada Kristo waislamu waliuteka mji wa Yerusalemu
na mwaka 691BK walijenga msikiti wao mahali pale pale ambapo kwanza palikuwa na hekalu la kiyahudi.Mwaka 1542 Baada ya Kristo mtawala
wa waislamu alijenga kuta za mji upya zilizopo mpaka leo. Mji wa Yerusalemu
ulendelea kuwa chini ya utwala wa waislamu
mpaka mwaka 1967 BK ambapo
waIsrael walichukua mji wao tena. Msikiti juu yya kilima cha hekalu mpaka sasa
upo.
Kurudi kwa Yesu Kristo duniani ni sehemu ya
mpango wa Mungu kuhusu
wokovu wa wanadam. Wakati wa Yesu wanafunzi
wake walidadisi sana
na walitaka kujua lini hasa
atakaporudi tena mwana wa Adamu, Mafarisayo waliamini hasa juu
ya kiama
ya wafu ila walihitaji
mtu sahihi ambaye anaweza
kuelezea zaidi au kutoa ufafanuzi juu ya
kutokea kwake.Bwana Yesu alidokeza
juu ya dalili za kutokea kwake
na kwa sababu alikuwabado
yupo duniani alitamka
dhahili au wazi kuwa mipango tote ilikuwa mikononi mwa
baba yake.“Si kazi yenu kujua nyakati wala majira baba aliyoweka katika
mamlaka yake mwenyewe”.[Matendo 1:7]
Wayahudi wengi hawakuamini kuwa Yesu ni Masihi wengi waliogopa kushushwa vyeo vyao hasa watawala kwani walifikiri utawala wake
ni wa dunia hii.‘’Basi
walipokusanyika wakamwuliza wakisema je!
Bwana wakati huu ndipo unaporudishia Israel ufalme?”.[Matendo 1:6]Lakini Yesu alieleza
kuwa ufalme wake si wa dunia hii,mapokeo ya yesu yalikuwa ya
tofauti kwani wengi walijua anakuja kuwarudishia Israeli utawala toka kwa
warumi.
SABABU ZA KURUDI KWA YESU AU MASIHI
1.Kulichukua kanisa au
kuwachukua wateule wake
“Kwa maana waitwao ni wengi bali wateule ni
wachache”[Mathayo
22:14]
2.Kuamua vita
“Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu
lile lililonenwa na nabii Daniel
limesimama katika patakatifu asomaye na afahamu ndipo walio katika uyahudi na
wakimbilie milimani”.[Mathayo
24:15]
Nabii Daniel unalenga kutekwa kwa
mji wa Yerusalemu hapo ndipo vita itakapozuka duniani na vita hiyoatakayekuja kuiamua ni
Yesu pekee.
3.Kuwahukumu walio hai na wafu
“Kisha nikaziona mbingu zimefunuka na
tzama farasi mweupe nay eye aliyempanda aitwaye mwaminifu na wa kweli naye kwa
haki ahukumu………”[Ufunuo
19:11]WaKristo wa kipindi cha Agano la kale
hawakuwa na ujuzi wowote
kuhusu uzima wa milele ingawa mara nyingine walionyesha
matumaini yao ya ufufuo ambao kwa njia yake wangeokolewa kutoka mautini. Pia walitazamia ufufuo kwa
ajili ya watu waovu ambao wangehukumiwa na kupata adhabu “Tena wengi wa hao walalao
katika mavumbi ya chi wataamuka wengine
wapate uzima wa milele wengine aibu
na kudharauliwa milele”[Daniel
12:2]
Wakati wa agano la kale
hawakuelewa kuhusu uzima wa milele kwa
sababu Yesu alikuwa bado
hajazaliwa. Lakini kwa njia ya
Yesu Kristo Mungu alivunja nguvu za
mauti na kudhihirisha hali ya uzima wa ufufuo. “ Basi kwa kuwa
watoto wameshiriki damu na mwili yeye
naye vivyo hivyo
alishiriki yayohayo ili kw
njia ya mauti amharibu
yeye aliyekuwa na nguvu za mauti yaani ibilisi awaache huru wale
ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya
mauti walikuwa katika hali ya utumwa”.[Waebrania 2:14-15].Wayahudi wachache yaani
masadukayo walikataa kuamini habari yeyote
kuhusiana na ufufunuo.“Siku ile
masadukayo watu wasemao kwamba hakuna kiyama ….”[Mathayo 22: 23]
Wokovu ni ufufuo wa kimwili kwa
maisha mapya Yesu alishinda
dhambi na mauti na kwa sababu hii mtu
amwaminiye Yesu anaweza
kutazamia wokovu kutoka
katika dhambi na mauti. “Lakini tukiwa tulikufa pamija na Kristo
twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye, tukijua
ya kuwa Kristo akiisha kufufuka
katika wafu hafi tena, wala
mauti haimtawali tena maana kwa
kule kwake , aliifia dhambi mara
mojatu, lakini kwa kule kuishi kwake
alimwishia Mungu”.[Warumi
6:8-10]
Mungu alimwumba mwanadamu awe mkamilifu na
hivyo anashughulika naye katika umoja
wa ukamiilifu wake Mungu
hadanganywi na mwanadamu
katika sehemu ya kimwili
na kiroho. Makusudi ya Mungu
kumwuumba mwanadamu ni ya milele wala
hayakuunganishwa na kufa bali na ufufuo wa kimwili pamoja na uzima wa
milele.“Tena wengi wa hao walalao katika mavumbi ya chi wataamuka
wengine wapate uzima wa milele
wengine aibu na kudharauliwa
milelena walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao
wengi kutenda haki watang’aa kama nyota
milele na milele”.[Daniel 12:2]
DALILI ZA UJIO WA MASIHI
1. Chapa 666 au kuuza na kununua
kwa kutumia namba 666
Unabii huu ulinenwa na nabii yohanakuwa siku za mwisho kutakuwa na
utaratibu wa kufanya biashara kwa kutumia electronic (eletroniki) badala ya
pesa taslimu kutakuwa na mfumo huu kila mtu atapewa
nmba itakayo mhusu yeye binafsi
na inayiendana na jina lake
na bila namba hiyo hutaweza
kununu kitu chochote.
13/3/2013 marekani walianza kutumia kitu kiitwacho cheaply ambacho mtu
anakivaa kidoleni au sehemu yeyote ya mwili
kazi yake ni kupata punguzo
kwenye maduka makubwa
pia matumizi ya ATM kadi
visa kadi n.k ni utimilifu wa unabii
huo.
“ Naye awafanya wote wadogo kwa wakubwa
na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa watiwe chapa
katika mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yeyote asiweze kununua wala kuuza isipokuwa ana chapa
ile yaani jina la mnyama
Yule au hesabu ya jina lake”.[Ufunuo
13: 16-17]
2. Kuanzishwa kwa taifa la
Israel,Mnamo mwaka 597 KK Mungu alimpa nabii Ezekiel ujumbe ufuatao;“ Ukawambie Bwana Mungu asema
hivi; tazama nitawatwa wana wa Israel toka kati ya mataifa walikookwenda
name nitawakusanya pande zote
na kuwaleta katika nchi yaowenyewe”.[Ezekiel 37:21]
Pia Ezekiel 38:8 anasema “ Na baada ya siku
nyingi utawajiliwa;katika miaka ya mwisho
utaingia nchi uliyorudishiwa hali yake ya kwanza baada ya kupigwa kwa upanga, iliyokusanywa
toka kabila nyingi za watu wa milima ya Israel……”
Unabii huu ulitimia mwaka 1948
ambapo kwa mara ya kwanza wayahudi
kutoka katika pande zote za dunia walirudi
na kuingia katika nchi yao na kuanza
kudai kuwa umoja wa mataifa uwatambue kama taifa. Baada ya
kuingia katika nchi yao ilichukua
miaka isiyozidi ishirini kwa Israel kuwa taifa mashuhuri lenye nguvu katika masuala ya kisiasa kijeshi na kiuchumi katika mashariki ya kati.
Hata sasa ni taifa lenye nguvu.
3. Maarifa kuongezeka ,Mnamo
miaka ya 605Kabla ya Kristo na 539 Kabla ya Kristo nabii Daniel alitabiri baada
ya kuwa ametoka kifungoni ujumbe ufuatao; “Lakini wewe ee Daniel, yafunge
maneno haya ukakitie mhuri kitabu hata wakatiwa mwisho; wengi wataenda mbio
huko na huko na maarifa yataongezeka”.[Daniel
12:4]
Mungu alimtumia nabii Daniel
kunena kuhusu kuongezeka Kwa marifa Kama dalili mojawapo ya siku za
mwisho.katika karne hii ya 21 maarifa yameongezeka kwa kiwango kikubwa mno.
Ongezeko la maarifa limefanya ulimwengu uchanganyikiwe Sana. Baadhi ya vitu
ambavyo vimeongeza maarifa ni
pamoja na kama vile computer luninga
tovuti kittabu cha nyuso(facebook) hivi vyote
tunaviingiza katika mfumo
mzima wa utandawazi . Lakini utabiri huu
ni uthbitisho kuwa hizi ni siku za mwisho.
4.Vita kati ya taifa moja na
jingine
Kabla ya Yesu kuondoka duniani
alinena ishara ya vita kali kati ya mataifa mbali mbali kuwa itaibuka. Katika karne ya 20 yaani
kuanzia mwaja 1900 hadi sasa vita na uhasama
ulimwenguni umezidi kuwa mkubwa
sana. Uhasama huo ndio uliosababisha
hata kutokea kwa vita ya kwanza
na ya pili ya dunia
mnamo 1914-1918 na 1939-1945. Hata sasa vita na uhasama vinaendelea
kwa kasi mfano marekani na
korea kaskazini piaa Israel na
palestinahiyo ni dhahili kuwa kurudi
kwake kumekaribia.
“Ninyi
mtakaposikia habarrir za vita na
fitinamsitishwe maana hayo hayana budi kutukia kwanza lakini ule
mwisho hauji upesi kisaha aliwaambia
taifa litaondoka kupigana na taifa nyingine na ufalme kupigana na ufalme”.[Luka21:9-12].Utokeaji wa vita na uhasama ni
,maandalizi ya siku ya mwisho.
5.Ishara ya juu,anga na mwezi na
nyota. Nabii Yoel alitabiri miaka ya 835-830 Kabla ya Kristo kuwa kutakuwana
ishara ya jua kabla ya ujio wa Masihi
(Yesu) mara ya pili lakini hata
Yesu alipokwepo duniani aliwaeleza wanafunzi wake uwepo wa
ishara katika jua na mwezi na nyota; na
katika chi dhidi ya mataifa wakishangaa kwa
uvumi wa bahari na msukosuko wake waatu wakivunjika mioyo kw hofu na kwa kutazamia mambo yatayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika.” Unabii huu
ulianza kutimia kkuanzia karne ya 18 yaani kuanzia miakka ya 1700.
19/5/1780 ni siku ya ajabu na yenye tukio la
aina yake kwani “Anga” lote la kaskazini mashariki mwa amerika lilikuwa giza
tupu.3rd Januari 1833 vimondo vilianguka marekani na anga lote lilijaa vitu vya kung’aa
kuanzia saa nane usiku hadi
mapambazuko anga liling’ara na kuwaka.Mwanzoni
mwa mwaka 1900 kimondo kilianguka nchini Tanzania katika mkoa wa Mbeya,kimondo
hicho kipo hata sasa.Miaka ya 1990s jua na mwezi vilipatwa mchana saa nane ,anga zima lilijawa
mwanga mkali nchini Tanzania watu
wengi walihamaki mno.Mwaka 1999 dunia ilihamaki na watu wengi walitegemea mwaka 2000 ni mwisho wa dunia wengine
walijiua lakini haikuwa mwisho wa dunia ila Yesu mwenyewe alisema japo matukio haya yalitokea
ila mwisho hautakuja haraka,hivyo mfululizo wa matukio haya dalili tu za siku
za mwisho.
.6.Utengenezaji wa mabom ya atom
na silaha za nyuklia.Nabii petro alipewa ujumbe na Mungu mnamo miaka 68 baada ya Kristo petro alieleza kuhussu kurudi kwa Yesu ili kuwapa uhakika wale waliokuwa
wanadharau habari hizo waaminio na kumgeukia Mungu.
“Lakini siku ya Bwana itakuja
kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu na viumbe
vya asili vitaunguzwa na kufumuliwa na nchi na kazi zilizomo ndani yake
zitateketea”.[2Petro
3:10-12]
Kuchelewa kurudi kwa Yesu Kristo ni kwa lengo
la kuwapa nafasi wenye dhambi ili watubu na kuepuka hukumu hiyo. Hivyo waKristo ni vyema
tukaetayari kumlaki akirudi kwa
sababu kila mmoja akatoa hesabu yake mwenyewe . kwa sasa silaha na mabomu yanatengenezwa sana hivyo unabii unatumia kwani mwisho wa
silaha hizo ni uharibifu. “ Bwana hakawii kutimiza ahadi yake kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali
huvumilia kwenu maana hapendi mtu yeyote apotee bali wote wafikirie toba”.[Luka
3:9]
7.Kuanzishwa kwa umoja wam mataifa,Kitabu
cha ufunuo kiliandikwa na yohana .alipofungwa
katika cha patmo si mbali na
pwani ya efeso magharibi ya asia ndogo yohana alipokea maono
yake katika maandiko ya kiufunuo. Mungu anatoa ufunuo wake kwa watu kwa njia ya maono ya ajabu yanayoelezwa na malaika . baada ya kuandika yahana alituma mjumbe
katika miji ya bara ili
akapeleke kwa makanisa saba ya asia ndogo.
Katika kitabu cha funuo Mungu ameeleza
kuhusiana na kuanzishwa kwa utawala wa
dunia nzima utakao tokea wakati wa siku za mwisho.ufunuo 13: 3-8 anasema “
nikaona kimoja cha vichwa vyake kana
kwamba kimetiwa jeraha la mauti na pigo
lake mauti likapona. Dunia yote
itastaajabia mnyama Yule
wakamsujudu Yule joka kwa sababu
alimpa huyo mnyama uwezo wake ;
nao wakamsujudu Yule mnyama wakisema
ni nani afananaye na mnyama huyu?
Tena ni nani awezaye kufanya vitu naye? Naye akapew kinywa cha kunena
maneno makuu ya makufuru akapewa iwezo
wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua na na kulitukana jina lake
na maskani yake nao wakaao
mbinguni”.Ukitazama kwa undani
umoja wa mataifa na miundo yake ya kijeshi
kiuchumi mashirika ya fedha duniani
ulimwengu mzima unausujudia umoja wa mataifa kiuchumi
haata kisiasa pia hivyo hali hii
inatu eleza kuwa na utawala momoja ni utimilifu wa dalili za ujio wa Masihi.
8.Kuhubriwa kwa injili kila
mahali ulimwenguni,Kutokana na kukua au kuongezeka kwa maarifa (utandawazi)
imepelekea injili ya Kristo kufika kila
mahali kwa njia mbali mbali kama redio, luninga, tovuti n.k,“Tena habari njema
itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa
ushuhuda kwa mataifa yote hapo ndipo
ule mwisho utakapo kuja”[Mathayo
24:14].Hivyo uenezwaji wa neno la Mungu kila mahali ni utimilifu wa wa dalili za ujio wa Masihi na hata atakuja Masihi hakuna
atakayejitia kuwa siksia
9.Kupoa kwa upendo nawatu kupenda
fedha kuliko kumpenda Mungu. “ Lakini ufahamu wa neon hili ya kuwa siku za
mwisho kutakuwako nyakati za hatari maana watu watakuwa ni wenye kujipenda wenyewe wenye kupenda fedha……………”.[2Timotheo
3:1-6],Watu wengi wana muasi Mungu kwa sababu ya fedha na hata viongozi wa makanisa wanagombana kwa ajili ya fedha. Wengi wanafanya huduma kwa kuangalia
fedha kuliko Mungu hivyo ni vyema tujue
kuwa ule mwisho upo karibu.
Hadi sasa ishara iliyobaki ni
moja tu kutekwa kwa mji wa Israel
kwaani baada ya kutekwa kwa Israel
mataifa mbali mbali yataingia kupigana na menginekulisaidia taifa hilo vita itazuka ulimwengu mzima na ndipo “mwana wa Adam atakaporejea kuamua
vita ya ulimwengu mzima.“Lakinimtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na
majeshi ndipo jueni ya kwamba uharibifu
wake umekaribia ……….wataanguka kwa makali ya upanga na watatekwa nyara na kuchukuliwa katika
mataifa yote na Yerusalemu utakanyagwa na mataifa hata majira ya mataifa
yatakapotimia”.[Luka
21:20]
Ni wajibu wa kila mmoja wetu
watoto vijana wazee kufikiri
namna ilivyotabiriwa hapo awali na
utimilifu wake. Ni vyema kila mmoja
ajiulize moyoni mwake je (Yesu)Masihi akirudi leo nitakwenda mbinguni au nitakuwa upande gani? Kuchelewa kurudi ni nafasi yetu mimi na wewe kutubu na kutengeneza mambo yetu
ili ajapo atukute tukiwa tayari hivyo tujiulize
na tuchukue hatua ya kutubu mapema.
MAMBO YATAKAYO TOKEA YESU
(MASIHI) ATAKAPORUDI MARA YA PILI.
1.Kunyakuliwa kwa kanisa,Baada ya
ishara zote kukamilika za siku za mwisho Yesu Kristo atarudi duniani na kuja kwake
kutakuwa kwa awamu kuu mbili;-
(a)Unyakuo wa kanisa
(b)Ufufuo wa wafu
“Kwa sababu Bwana mwenyewe
atashuka kutoka mbinguni pamoja na
mwaliko na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya Mungu.nao waliokufa katika Kristo
watafunguliwa kwanza kasha sisi tulio hai tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu,ili tumlaki Bwana
hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno
hayo”.[1Wathesalonike
4:16-18]
Kunyakuliwa kwa kanisa litakuwa
tukio la mara moja yaani la haraka na si
watu wote duniani watakaoliona na kuelewa kwa undani utokeaji wake. Unyakuo ndio
utakao watenganisha waamini na wasio
amini na baada ya kuwatenganisha
yatatokea mateso ambayo hayajawahi kutokea ulimwenguni.Wale watakao
kutwa duniani wakiwa hai watabadilishwa na kupaa kwenda mbinguni wakiungana na
watu waliofufuliwa ambao walikufa katika Bwana. Baada ya unyakuo watakao baki ni wale tu waliokataa kumwamini Yesu Kristo.
2.Dhiki “ Kwa kuwa wakati huo kutakuwako
dhiki kubwa ambayo haijatokea tangu mwanzo wa ulimwengu hata sa”.[Mathayo 24:2].Baada ya
kunyakuliwa kwa waumini safi wasio na dhambi
kipindi cha dhiki kuu
kitaanza na kitaambatana na uanzishwaji wa wazi wa utwala wa mfumo wa kifalme. Utawala huu utjulikana kwa alama ya namba 666 na
utaongozwa na mpinga Kristo ataitawala
dunia kwa ukatili kwa kipindi cha miaka
saba(7).
3. Ufufuo wa wasioamini, “Tena
wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka wengine wapate uzima wa milele wengine aibu na kudharauliwa milele”[Daniel 12:2].Ufufuo wa watu ambao
hawakumwamini Kristo wao hawatapewa miili ya kiroho isiyokuwa na uharibifu.
Matokeo ya ufufuo wao siyo uzima bali
hukumu, kuadhibiwa na kuangamizwa milele.
“Nikawaona wafu wakubwa kwa wadogo wamesimama
mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa na kitabu kingine kikafunguliwa
ambacho ni cha uzima na hao wafu
wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa
katika vile vitabu sawasawa na
matendo yao, bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na mauti na kuzima zitawatoa wafu waliokuwamo ndani
yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.Ufunuo 20:12-15]
4.Utawala wa Kristo wa miaka
elfu(1000) au millennia, Kwa lugha nyingine jina la ufalme huo ni millennium na maana yake ni miaka elfu.
Ingawa jina hili katika biblia halionekani sana lakini linahusika sana na utwala wa miaka 1000
uliotajwa katika maono ya kitabu cha
ufunuo.“Hao wafu waliosalia hawatakuwa hai,hata itimie ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri
na mtakatifu ni yeye aliye wa kwanza;
juu yah u mauti ya pili haina nguvu bali
watakuwa makuhani wa munngu na wa Kristo, nao watakatifu pamoja naye hiyo miaka
elfu”.[Ufununo
20:4-6].Utawala huu utakuwa baada ya
ushindi wa Kristo katika
vita kuu ya tatu ya dunia ufalme wake utaanza hapa duniani.
5.Kubadilishwa kwa mbingu na
dunia ,Baada ya kukamilika kwa matukio yote niliyotangulia kuyaeleza mbinguu na
dunia zitapitishwa katika moto na kasha Mungu ataumba mbingu mpya na nchi mpya
mahali ambapo kweli na amani zitatawala
milele.Mahali hapa palipo na raha isiyo na kikomo ndipo yatakapokuwa maskani ya
milele ya wale wote watakaomkubali Yesu Kristo kuwa mwana waMungu na kumpokea
maishani mwao kama Bwana na mwokozi wao.