MITIHANI

 


WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

MAPAMBANO   OPEN    SCHOOL

JARIBIO LA MAALUM  WIKI

KIDATO   CHA   TANO

KISWAHILI-2                                                                 

 MUDA : SAA  2:30                                                          Oktoba,27,2018

                             MAELEKEZO

1. Karatasi hii  ina  jumla ya maswali  tisa (9)

2. Jibu swali  moja kila sehemu na kila swali lina alama 20

3. Soma swali kwa mkini kabla ya kuanza kujibu

         4. Andika jina lako vizuri na mchepuo wako

                    SEHEMU   A   (Alama  20)

                           FASIHI KWA UJUMLA

1.    ‘Dhana ya uhuru wa mwandishi wa kazi ya fasihi kwa nchi za Afrika bado ni kizungumkuti’.thibitisha dai hili kwa kutoa hoja nne na  mifano ya waandishi mbalimbali pamoja na kazi zao

 

2.    Wasanii wengi wa fasihi hutumia wahusika wasio binadamu kwa lengo la kisanaa’’.Kwa hoja mifano onesha sababu za kutumia wahusika wasiobinadamu katika kazi ya sanaa.

                         SEHEMU   B  ( Alama 20 )

                           Usiku Utakapokwisha      -Mbunda Msokile

                            Mfadhili                            -Hussein  Tuwa

3.     Wasanii wengi hubuni jina la kitabu linalosawiri yalioyomo ndani ya kitabu husika”.Kwa kutoa hoja nne kwa kila riwaya jadili dai hili kwa kurejelea Tanzania ya leo,tumia riwaya mbili.

4.    Wasanii wa kazi ya fasihi hutumia mbinu za kifani ili kujenga ,kuzipa mvuto na kuleta radha tamu kwa wasomaji wa kazi zao.Fafanua mbinu tano ( 5 ) za kifani zilizotumika katika kila tamthiliya ,tumia tamthiliya mbili ulizosoma.

 

                          SEHEMU    C    (Alama   20)

                                            TAMTHILIYA

                                Morani         -E.Mbogo

                   Kivuli Kinaishi                         -S.Mohamed

                   Nguzo  Mama                         -P.Mhando

5.“Suala la ujenzi wa nchi yenye haki na usawa si suala lelemama”. Thibitisha  dai hili kwa hoja nne  (4) kwa kila Tamthiliya,Tumia tamthiliya mbili ulizosoma.

 

6 . Ubunifu wa kisanaa ni nguzo  muhimu sana katika kufikisha  ujumbe kwa jamii yeyote ile.Kwa kutumia  Tamthiliya mbili   ulizosoma jadili vipengele vya fani  vilivyotumiwa na mwandishi kufikisha ujumbe.

 

                        SEHEMU     E   (Alama  20 )

                        USANIFU  WA  MAANDISHI

7.Soma habari ifuatayo kisha eleza mbinu za kisanaa zilizotumika;

Kulikuwa  kimya kwa muda.Wote wakanyamaza.Lakini ghafla mtu mwingine  akashtuka na kusema, “Hawana shida bwana…..”Uzuri wote wa UDA ulisahauliwa huko.Maskini UDA! Gari halikutokea.Baada ya muda kidogo ikasikika sauti kali “pyaaaa!” Aligeuza shingo nyuma hakuna kitu.Kulia,hapana.Ni Kushoto mwa kijumba kimoja  karibu na kituo cha basi waliposimama.Kuna mtu mmoja alikuwa anagalagala,baiskeli kule!! Mguu juu!!.

 Ondoa injinikiuno yako we! Blad ful!” Alisikia mtu mwenye gari lililomgonga akifoka.Akalikodolea macho kwa nguvu na hasira gari hilo lililokuwa likilamba lami na kuyamaliza  magurudumu yake .Limekwenda halina namba.Hakujua……

 Mhuni mmoja naye akamshambulia aliyegongwa ,Mwanaharamu we!!.Huangalii unapopita?.Eee? Unafikiri mkokoteni huo?,Ungefia mbali huko.Stupid!” Lupyana,akaguna akashangaa…….machozi  yakamtwaa machoni. Kila mtu ana matatizo yake”,aliwaza.Mji una namna mbalimbali ya kuwachachia watu.Simba akizidiwa hula majani.Hatimaye  gari  la UDA  la kwanza lililotarajiwa kuwachukua watu kutoka kona ya Dzengelendete kuwapeleka  Lupembe mjini likaja.Mikikimikiki ikaanza! Watu walisukumana! Kila mtu aligombea nafasi mithili ya mbuzi wanaoswagwa kuingia zizini.Katika harakati hizo,mtu mmoja alichukuliwa fedha kutoka mfukoni.

 “Nimeporwaaaaaa-aa-aa,nimeporwa,jamani”.Watu hawakujali.Ooooh. Unaleta gozigozi?.Watakuiba hata wewe mwenyewe! Bwege wewe’’.Kondakta  wa basi hilo alifoka.Kama ilivyo ada sikio halilali njaa.Mtu mwingine akadakia. “Aaah,shauri  yako we mshamba wa kijijini’’.Lupyana  aliwaza kidogo  aliposikia hayo.“Dunia tambara bovu kweli” alijisemea.

 Wakati huo huo,kuna mtu alikuwa anapanda basi  kupitia dirishani,na alimkanyaga Lupyana  begani.Lupyana  akasonya lakini hakuna aliyemjali.Kwa hakika,asingethubutu  kuparura mkono wake juu ya hili jitu la miraba minne kwani lingemcharanga na kumtafuna mbichi mbichi.Hofu ikatawala moyoni mwake  tena.Watu wengine walitaka kushuka.Oya we mama toa makalio yako njiani tunashuka’.Kijana mmoja alionekana  amenyoa nywele kama ugiligili wa jogoo alibwatuka…!Mama naye kumbe  mtata!Akamjibu,Shuka zenyewe  ziko wapi? Peleka fito zako huko.Watu walicheka kwenye basi wakampongeza mama kwa kumunyoosha huyo kijana mkosa adabu.

  Vituko vya UDA viliendelea.Baada ya dakika chache akaja mama mmoja mgonjwa.Yeye aliomba msaada kuwa apite mlango wa mbele karibu na kule anapokaa dereva.Akasukumwa kwa nguvu na kondakta,akaanguka huku akifokewa kuwa hii siyo gari ya wagonjwa. “Soma juu ya mlango”. Kwa kweli,”Asiyekujua hakuthamini!”.Zimwi  likulalo hadi mwisho halikujui.

 Kwa mbele kulikuwa kijana mwingine aliyetaka kushuka.”Pisha…..pisha!” Waliokuwa karibu nae walimwita  lukwalakwala.Lakini lukwalakwala akalalamika kwa nguvu,Musee ona kwisa kanyaga mimi?,Dunia musima inasangilia amani wewe inakanyaga?”.We lukwalakwala toa kelele zako hapo  unafikiri basi hili la baba ako?’’.Kijana mwingine alidakia.Lukwalakwala alikunja uso ukawa na makunyanzi kama goti la mbuzi na kufoka, “Siku mingine tafyeka koromeo lako”.Watu walicheka kwenye basi na hapo Lupyana  naye akaangua kicheko

Powered by Blogger.