OSW 223: MOFOLOJIA YA KISWAHILI (OUT)

CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
KITIVO CHA SANAA NA SAYANSI ZA JAMII
OSW 223: MOFOLOJIA YA KISWAHILI
MTIHANI WA MWAKA
TAREHE:  11 Juali 2012
MAELEKEZO:
  • Jibu maswali manne (4) tu
1 (a) Mofolojia ni nini?
   (b) Eleza uhusiano uliopo kati ya taaluma ya mofolojia na:
        i. Fonolojia
       ii. Semantiki
2. (a) "Mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha lugha chenye maana ya kisarufi au ya kimsamiati."             Fafanua udogo wa mofimu ni upi?
     (b) Ainisha kazi za mofimu ki zilizopigia mstari katika sentensi zifuatazo.
      i. Anaendesha gari kizembe
     ii. Akijitahidi atafanikiwa
    iii. Hii ni ramani ya kijiji chetu
    iv. Chama chetu hakitasusia uchaguzi mkuu
    v. Hiki ni kisiwa cha amani
    vi. Wakimbizi wameharibu mazingira
    vii. Wasikilizaji wamekipenda kicheko chako
3. "Kujua dhana ya neno ni kujua taarifa nne muhimu kuhusu neno; taarifa ya kifonolojia,taarifa ya         kimofonolojia,taarifa ya kisintaksia,taarifa ya kiamali na taarifa ya kimaana." Fafanua kauli hii           kwa kutumia mifano kutoka lugha ya Kiswahili.
4. Kwa kutumia mifano hai kutoka lugha ya Kiswahili, eleza kwa ufupi njia zifuatazo katika uundaji       wa maneno.
    (i)  Urudufu  (ii) Uhulutishaji  (iii) akronimi  (iv) Uambishaji  (v)  kutohoa
5. (a) Nini maana ya mofofonolojia?
    (b) Eleza tofauti iliyopo kati ya kanuni za kimofofonolojia na kanuni za kifonolojia
6. Ainisha na eleza kazi ya kila mofimu katika maneno yafuatayo:
    (i) utauua  (ii) mpakani  (iii) walipotukosesha  (iv) matamanio
Powered by Blogger.