NOMINO ZALIKA/UNOMINISHAJI

NOMINO ZALIKA/UNOMINISHAJI
Unominishaji kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2007) wanasema ni hali ya kuunda nomino kutoka katika kategoria nyingine ya neno. Kategoria hizi zaweza kuwa kitenzi, kivumishi au hata nomino yenyewe.
Ø Kwa hiyo vinominishi (o, i) vinaweza kunominisha vitenzi vya Kiswahili katika mazingira yafuatayo: Tukianza na kinominishi (o); kinominishi “o” huweza kunominisha vitenzi vya kibantu vinavyoishia na kiambishi tamati “a”.
            Kwa mfano: tenda→ tend-o
                  Andika → andik-o
                  Piga → pig-o
                  Pata → pat-o
                  Jenga → jeng-o
                  Fundisha → fundish-o
                  Ona → on-o
                  Pamba → pamb-o

Ø Hata hivyo kuna baadhi ya vitenzi vya kibantu vinavyoishia na kiambishi tamati “a”ambavyo havinominishwi na kinominishi “o” mfano wa vitenzi hivyo ni kama lowa, tembea nk.
Ø Pia kinominishi “o” huweza kunominisha vitenzi kwa kuambatana na vinyambulishi (-i-) au (-li-) katika baadhi ya vitenzi.
            Kwa mfano: kaanga→ kaang-i-o
                     Chuja→ chuj-i-o
                     Pamba → pamb-i-o
                     Fua → fu-li-o
                     Kaa → ka-li-o
Ø Mazingira mengine ambamo kinyambulishi nominishi “o” huweza kunominisha kitenzi ni pale ambapo huambatana na mofimu (-e-)
            Mfano: Chekecha → chekech-e-o
            Fyeka → fyek-e-o
            Zoa → zol-e-o
Ø Vilevile kinominishi “o” huweza kunominisha kitenzi kwa kushirikiana na viambishi awali vinominishi.
            Mfano: Lima → ki-lim-o
            Soma → ki-som-o
            Kula → m-l-o
            Lia → ki-li-o, m-li-o
            Penda → u-pend-o
            Cheza → m-chez-o
Ø Pia baadhi ya vitenzi huweza kuondolewa irabu ya mwisho na kubakiwa na kinyambulishi “o” kama kinominishi.
            Mfano: toboa→ tobo
Ø Vilevile unominishaji huweza kufanyika katika vitenzi vya utendewa na utendeshwa kwa kuondoa mofimu (-w-a).
            Mfano: somwa → som-o
            Pigwa →pig-o
            Lishwa → lish-o
            Tendwa →tend-o
Ø Kwa upande wa kinominishi “i” pia huweza kunominisha kitenzi katika mazingira tofautitofauti kama ilivyoonyeshwa hapa chini.
Kinominishi “i” huweza kunominisha kitenzi kwa kusaidiana na viambishi awali vinominishi.
            Mfano: soma → m-som-i
            Soma → u-som-i
            Chunguza → u-chunguz-i
             Chokoza → u-chokoz-i
Ø Kinominishi “i” huweza kuchukua nafasi ya kiambishi tamati “a” katika kitenzi na kunominisha kitenzi hicho.
            Mfano: Sema → sem-i
Ø Vilevile kinominishi “i” huweza kuambatana na vinyambulishi vingine ili kunominisha kitenzi.
            Mfano: Chuja → chuj-i-o
            Pita → pit-i-o
Habwe na Karanja (2007:45) wanasema kinominishi “i” kinapotumika kunominisha mizizi inayoishia na konsonanti, mfano; (pik) na (jeng). Mofimu “i” inapopachikwa kwenye mizizi hubadili na kuifanya kuwa nomino.
            Mfano:
Kitenzi

Unominishaji

Nomino      
Pika

mu+pik+i

mpishi
Jenga

mu+jeng+i

mjenzi
Iba

mu+ib+i

mwizi
Ø Vilevile kinominishi “i” huweza kunominisha shina la kitenzi cha mnyambuliko.
             Mfano: tembeza→ m-tembez-i
             Kimbiza → m-kimbiz-i
             Tapisha → ma-tapish-i
·      Kivumishi cha sifa kikiongezwa irabu “u” mwanzoni mwa kivumishi husika huunda nomino zalika:       mfano: baya        ubaya, zuri       uzuri, vivu        uvivu
·     Nomino zinazotokana na kuongeza kiambishi “ki” mwazoni na “o”mwishoni mwa kitenzi. Mfano: soma – kisomo, apa – kiapo, piga –kipigo, ziba – kizibo, lia – kilio.
·     Nomino zinazotokana na kuongezwa kwa kiambishi “m” mwanzoni mwa silabi na “ji” mwishoni mwa kitenzi. Mfano: chora – mchoraji, cheza – mchezaji, baka – mbakaji, kamua – mkamuaji, fagia –mfagiaji.
·   Nomino zinazotokana kwa kuongeza viambishi awali “m” na “u”mwanzoni mwa kitenzi au kiambishi tamati “vu” au “zi” mfano: legeza – ulegevu (hali), mlegevu (mtu), teleza – utelezi (hali),mtetezi (mtu), kakamaa – ukakamavu (hali), mkakamavu (mtu).
·    Kwa kuambatanisha maneno mawili. Mfano: uambatanishaji wa jina kwa jina: askarikanzubatamzingaafisakilimo,
·      Jina na kivumishi: mjamzito.
·     Kitenzi na jina: chemshabongochangamoto.
Jina tegemezi na jina huru: jinategemezi hutokana na kitenzi na linahitaji jina huru ili maana ikamilike. Mfano: mpigambizikitindamimba,kifunguakinywakifunguamimba, nk.
Powered by Blogger.