CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA KITIVO CHA SANAA NA SAYANSI ZA JAMII OSW 122: HISTORIA YA KISWAHILI NA LAHAJA ZAKE JARIBIO KUU (MAALUMU
CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
KITIVO CHA SANAA NA SAYANSI ZA JAMII
OSW 122: HISTORIA YA KISWAHILI NA LAHAJA ZAKE
JARIBIO KUU (MAALUMU)
TAREHE: 2Julai, 2012
MAELEZO
- Jaribio hili lina sehemu A na B.
- Jibu maswali mawili (2) kwa kuchagua swali moja (1) kutoka kila sehemu
SEHEMU A: HISTORIA YA KISWAHILI
1. Kiswahili ni Kiarabu kwa jina lake lakini Ni Kibantu kwa sifa zake. Fafanua kauli hii kwa kutumia hoja za kiisimu
2. "Mafanikio ya ukuaji na ueneaji wa Kiswahili yanatafautiana kati ya
nchi na nchi miongoni mwa nchi tatu za Afrika Mashariki tokea
enzi za ukoloni." Jadili sababu zilizosababisha kutokea kwa
tafauti hizo.
SEHEMU B: LAHAJA
3. Kwa kutumia mifano halisi toa maelezo mafupi juu ya dhana zifuatazo
(i) lugha
(ii) lahaja jiografia
(iii) Atlas lahaja
(iv) lahaja jamii
4. Usanifishaji wa lahaja moja huua lahaja nyingine za lugha husika.
Jadili ukihusisha na lugha ya Kiswahili