MJENGO WA TUNGO
SURA YA PILI
MJENGO WA TUNGO
MAANA YA TUNGO:
Neno tungo ni kipashio ambacho ni
matokeo ya kupanga au kuweka pamoja vipashio sahili ili kupata kipashio
kikubwa zaidi. Tungo ni neno au mpangilio wa maneno unaodokeza taarifa
fulani ambayo yaweza kuwa kamili au isiwe kamili.
Mfano:
1. wana cheza
2. mwezi uliopita
3. kijana atakayeondoka
4. mara kwa mara
5. shangazi yake
6. mchezaji
Mifano yote hiyo hapo juu ni tungo lakini viwango vya kukamilika kwa taarifa zake vinatofautiana.
MJENGO WA TUNGO
Tungo za Kiswahili zinajibainisha katika makundi matatu yaani
a) virai
b) vishazi
c) sentensi
1. Virai
kirai ni. neno au mpangilio wa maneno ambao una
neno kuu moja na unatoa taarifa fulani. Kimsingi neno kuu ndiyo
hutupatia aina ya kirai. Mfano kama neno kuu ni nomino tunapata kirai
nomino.
Mfano:
a) mara kwa mara
b) mtu mweusi mweusi hivi
c) yule mwerevu
d) chakula kilichopikwa
e) jana jioni
f) mpungufu wa busara
AINA ZA VIRAI
1. Virai nomino
Virai hivi vimekitwa katika mahusiano ya nomino na maneno mengine.
Miundo ya virai nomino
(i) Muundo wenye nomino moja peke yake
Mfano:
(a) Mtoto anacheza
(b) Shangazi amewasili
(c) Vijana walisoma
(ii) Muundo wenye nomino mbili
(a)Mwalimu na wanafunzi ni wavumilivu
(b) Mwenyekiti na wajumbe walikutana
(c) Juma na Asha wamepigana
ZOEZI
Pigia mstari virai nomino katika sentensi zifuatazo.
1. Mlima unapendeza sana
2. Juma amenunua kitabu
3. Mvua imenyesha usiku kucha
4. Mwalimu amefundisha vizuri
5. Dada anaimba wimbo
2. VIRAI VIWAKILISHI
Ni virai vinvyoundwa na viwakilishi badala ya nomino
Mfano:
a) Huyu anacheza vizuri
b) Mimi ninapenda ubwabwa
c) Lile si mali yake
d) Mkali amepigwa
e) Warefu wakae mbele
Kumbuka :
Maneno yaliyopigiwa mstari ndio virai viwakilishi
3. VIRAI VIVUMISHI
Ni neno au mpangilio wa maneno yanayo fanyakazi ya kuvumisha nomino ama viwakilishi .
Mfano
a) Lile la kijani linauzwa
b) Maandazi ishirini yanauzwa
c) Chakula kilicholetwa hapa hakifai
d) Mtu wa siasa amewasili
e) Mfano mwingine ni huu
4. VIRAI VIELEZI
Hivi hudokeza namna au jinsi, mahali, wakati na kiasi cha utendekaji wa jambo.
Mfano:
a) Vijana wameimba usiku kucha
b) Wametembea harakaharaka
c) Amepanda juu ya mti
d) Tutawasiliana badae
e) Anaishi Dar es saalam
A. ZOEZI
Ainisha virai katika sentensi zifuatazo.
1. Tuliyopewa na kiranja yanafaa
2. Watoto walioandikishwa wameanza masomo
3. Wa mlango upo
4. Dada anampenda mdogo wake
5. Majani yameota kila mahali.
B. Kwa kutumia mifano iliyopo hapa chini Eleza sifa na tabia za virai.
(b) Msichana yule mzuri
(c) Mwalimu wetu
(d) Askari hodari
(e) Mwanafunzi na mwalimu
SIFA ZA KIRAI
1. Kirai hakina muundo wa kiima- kiarifu ambao
unahusisha mtendaji wa tendo na tendo
linalotendwa.
2. Chaweza kuwa na hadhi ya kishazi (kishazi tegemezi vumishi kinaposhushwa hadhi)
3. Kirai kina dhima nyingi
4. Chaweza kuwa neno moja au zaidi
5. Chaweza kutokea upande wa kiima au kiarifu.
6. Hutambulika kwa kuwa na neno kuu moja
6. Hutambulika kwa kuwa na neno kuu moja
KISHAZI
Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza
kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa
na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe.
Mfano
(i) Mzee analima
(ii) Mzee aliyekuja jana
Tofauti za vishazi (i) na (ii) hapo juu ni kwamba,
kishazi (i) kina kitenzi kinachojitosheleza chenyewe kwani kinakamilisha
ujumbe ulio dhamiriwa na mzungumzaji. Kwa upande mwingine kitenzi cha
kishazi (ii) hakimtoshelezi msikilizaji kwa sababu hakimkamilishii
ujumbe na kwa hali hiyo humfanya atake maelezo zaidi kutoka kwa
mzungumzaji. Mzee aliyekuja jana amefanya nini? Au anataka nini?
Kutokana na maelezo hayo hapo juu hufanya kuwe na aina mbili za vishazi ambazo ni vishazi huru na vishazi tegemezi .
AINA ZA VISHAZI
1. KISHAZI HURU
Ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kikuu
ama kitenzi kishirikishi ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe kamili
usiohitaji maelezo zaidi ya kuikamilisha maana
Mfano:
(i)Mzee analima
(ii)Watoto wanaimba vizuri
(iii) Bibi anasuka mkeka
(iv ) Wembamba si hoja
(v) Juma alikuwa anaimba.
Kila kishazi huru kina hadhi ya sentensi sahili kwa hiyo
tungo hizi twaweza kuziita pia sentensi kwani kila moja inajitosheleza
kimaana.
ZOEZI
1.Tunga sentensi 5 ukionesha vishazi huru (kwa kupigia mstari)
2.Tungo kuwa na kitenzi kikuu, na kutoa taarifa kamili je, huweza kufanya
tungo hiyo kuwa kishazi huru?
3 .Tunga sentensi tatu kila sentensi ioneshe muundo wa kishazi huru(onesha (i) t, (ii) Ts na (iii) T)
2. KISHAZI TEGEMEZI
Ni kishazi ambacho hakitoi taarifa kamili na
hujibainisha na kiambishi cha -O-Rekeshi kilichomo katika kitenzi na
maneno mengine yanayodokeza utegemezi.
.
Mfano:
(i)Mzee uliyemwona jana
(ii)Nyumbu aliyepigwa risasi
(iii)Mbwa aliyepata kichaa
(iv) Kwakuwa huna pesa
(v) Kama hatachelewa
Tungo hizi hapo juu hazijakamilisha maana,
zinahitaji kishazi huru ili zikamilishe maana iliyokusudiwa na
mzungumzaji.
Angalia mifano ifuatayo:
(i)Mzee uliyemwona jana ni babu yangu
(ii)Nyumbu aliyepigwa risasi amekufa
(iii)Mbwa aliyepata kichaa mwogope
(iv)Kwa kuwa huna pesa nitakununulia chakula
(v) Kama hatachelewa hataadhibiwa
Tungo hizi zimetoa taarifa kamili baada ya
kuambatanisha vishazi viwili, kishazi tegemezi na huru. Kishazi tegemezi
na kishazi huru vinapoambatana hujenga sentensi changamano.
SIFA ZA KISHAZI TEGEMEZI
1. Kishazi tegemezi hakiwezi kutoa maana kamili ikiwa hakijaambatana na kishazi huru.
Mfano:
(i)Yule kijana tuliyekuwa naye jana
(ii)Ndama aliyezaliwa
(iii)Mbuzi aliyenunuliwa juzi
2.Kishazi tegemezi kinaweza kutambulika kwa kuwa na
viambishi rejeshi vinavyoambatanishwa kwenye kitenzi na maneno
yanayodokeza utegemezi.
Mfano:
(i)Mzee uliyemwona ni babu yangu
(ii)Nyumba iliyoungua juzi imebomoka
(iii)Vyombo vilivyopotea vimepatikana
(iv) Kama atakuja tutamuona
(v)Ngoma hailii vizuri kwakuwa imepasuka
3.Kishazi tegemezi kinaweza kufutwa katika sentensi bila kuharibu maana ya sentensi nzima
Mfano:
(i) –Nyumba iliyoungua juzi imebomoka
-Nyumba imebomoka
(ii) –Vyombo vilivyopotea vimepatikana
-Vyombo vimepatikana
(iii) -Ndama aliyezaliwa amekufa
-Ndama amekufa
4.Kishazi tegemezi vilevile kinaweza kutambulika kwa
kuwepo vishazi, kama vile :- ‘ingawa’, ‘kwamba’, ‘ili’, ‘kwasababu au
mzizi wa ‘AMBA-’
mfano:
(i)Mwalimu amesema kwamba wanafunzi wengi ni watoto
(ii)Mwanafunzi ambaye hayupo ataadhibiwa
5.Kishazi tegemezi kinaweza kutanguliwa au kufuatiwa na kishazi huru.
Mfano:
(i)Nilimwona Rehema nilipokwenda mjini
(ii)Nilipokwenda mjini nilimwona Rehema
DHIMA NA HADHI YA VISHAZI
Kishazi huru kina hadhi ya sentensi (sahili )
lakini kishazi tegemezi hakina hadhi hii. Vishazi tegemezi ambavyo
hutegemea vishazi vingine katika tungo hushuka daraja na kuchukua dhima
ya kikundi.
Baadhi ya vishazi tegemezi huchukua dhima ya
vivumishi katika tungo ambayo kwa kawaida ni dhima ya kikundi au neno .
Vishazi hivi huvumisha nomino iliyo katika tungo hiyo. Vishazi hivi
huitwa “vishazi tegemezi vivumishi”.
Mfano:
(i)Ng’ombe aliyezaa amekufa
(ii)Kalamu iyopoteaimepatikana
Baadhi ya vishazi tegemezi hufanya kazi ya
vielezi viwapo katika tungo sawa na vikundi vielezi. Kutokana na hali
hii vishazi hivi navyo, huwa pia vimeshushwa hadhi kwani vimeteremshwa
daraja kutoka kishazi kuwa sawa na kikundi ambacho kwa kawaida kina
hadhi ndogo kuliko kishazi. Hivi huitwa “vishazi tegemezi”
AINA ZA VISHAZI TEGEMEZI
1.Kishazi tegemezi vumishi ( βv)
Hivi huvumisha jina lililo katika tungo
mfano:
(i)Chakula kilichopikwa leo kimeliwa chote
(ii)Wimbo unaoimbwa ni mzuri
(iii) Samaki aliyeoza ananuka
2.Kishazi tegemezi kielezi ( βE)
Hiki hutoa maelezo zaidi kwa kitendo kilicho katika tungo.
mfano:
(i)Mama alichukia aliposengenywa
(ii)Sisi tulimhurumia alivyolia
(iii)Walimu walitufukuza walipotuona
(iv) Gari lilipinduka lilipo gonga mti.
ZOEZI
1.Andika vishazi tegemezi sita kisha onesha viangama vya utegemezi
2.Kamilisha vishazi tegemezi vya swali la kwanza kwa kuongezea vishazi huru.
3.Ainisha vishazi katika tungo zifuatazo kwa kupigia
mstari na kuweka alama “ Ktg”kama ni kishazi tegemezi na” Khr”
kwa vishazi huru.
(a)Hizi ndizo kalamu ulizoagiza
(b)Viti vilivyovunjika vipelekwe kwa fundi
(c)Watu wanaofanya kazi kwa bidii watapata maendeleo haraka.
(d)Leo nitakiona kilichomtoa kanga manyoya.
SENTENSI
Sentensi ni kifungu cha maneno kuanzia neno
moja na kuendelea chenye kiima na kiarifu na kinaleta maana kamili.
Sentensi ndio kipashio cha juu kabisa katika daraja ya vipashio katika
lugha
MUUNDO WA SENTENSI
Sentensi ina sehemu kuu mbili, yaani kiima na kiarifu
1.KIIMA (K)
Kiima ni sehemu ya sentensi inayotaja nomino ambayo
inahusika na utendaji au utendekaji wa jambo. Nomino hiyo
inaweza kutajwa bayana au isitajwe kwa kuwa inaeleweka kulingana
na muktadha au mazungumzo ya awali. Kiima hutokea kushoto mwa kitenzi
mfano:
K
(i)Mwalimu / anafundisha vizuri
K
(ii)Deo / alikuwa anacheza
K
(iii) / Anaimba.
VIPASHIO VYA KIIMA
Kiima huundwa na
(i)Jina (N) moja
K
-Juliana/ anafua nguo
(ii)Jina na Jina (N+N)
K
- Sahani na vijiko / vimo kabatini
(iii)Jina na kivumishi (N+V)
K
- Kijana mwerevu / amefaulu
(iv)Kiwakilishi peke yake
- Wachache / watazawadiwa
k
(v)Kitenzi – jina na kivumishi
K
- Kuimba kwa vijana / kunafurahisha
(vi) Kitenzi jina
K
-Kucheza kwake / kunapendeza
(vii) Jina na kishazi tegemezi vumishi
K
-Mwanafunzi aliyeshindwa mtihani / amejinyonga
(viii) Kiwakilishi na kivumishi
K
-Sisi sote / tunapenda kuimba
2.KIARIFU (A)
Ni sehemu ya sentensi inayojazwa na maneno yanayoarifu
tendo lililofanywa, linalofanywa au litakalofanywa. Kiarifu ndio
sehemu muhimu zaidi katika sentensi ambayo wakati mwingine huweza
kusimama pekee bila kiima kwani wakati mwingine huchukua
viwakilishi vya kiima.
VIPASHIO VYA KIARIFU
(i)Kitenzi kikuu ( prediketa)
Mfano
:
A
-Juma / anacheza
A
-Maria / anakula
A
-Juma / alikuwa anacheza
A
-Mtoto / alitaka kwenda kusoma
A
-Kuku / ni ndege
A
-Popo / si ndege
(ii) Shamirisho
Ni jina au kikundi jina kinachojaza nafasi ya mtendwa.
katika sentensi.Shamirisho hutokea baada ya kitenzi kikuu au
baada ya kitenzi kishirikishi.Shamirisho hujibu swali Fulani (mtenda)
ametenda nini?
Mfano:
-Mwahija amembeba / mtoto
sh
-Babu amefuga / ng’ombe wengi
sh
(iii) CHAGIZO(ch)
Ni neno au kikundi cha maneno kinachojaza nafasi ya
kielezi katika tungo. Chagizo huweza kutokea mara baada ya kitenzi
kikuu au baada ya shamirisho.
Mfano:
-Mama anasoma kitabu pole pole
ch -Binti anaimba vizuri sana
ch
ZOEZI
Tenga kiima na kiarifu katika sentensi zifuatazo.
1.Watachezea kwenye chumba kilicho safishwa
2. Magari ya megongana
3. Hawa ndio wazazi wangu
4. Chakula kilicholetwa hakifai
5. Nia yetu ni kuoana
AINA ZA SENTENSI
1.Sentensi sahili
Hii ni sentensi yenye kishazi huru kimoja tu. kishazi hicho
kinaweza kuwa na kifungu tenzi kimoja kifungu tenzi hicho kinaweza kuwa
kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi au kitenzi kishirikishi.
Mfano:
(i)Yule ni mwalimu wetu
t
(ii) Twiga wanaishi porini
T
(iii)Vipofu walikuwa wanaomba msaada
Ts T
Muundo wa sentensi sahili
(i)muundo wa kitenzi kikuu peke yake(T)
Mfano:
-Anaimba
-Wanacheza
-Tutalima
Katika muundo huu vitenzi husimama peke yake kama sentensi sahili.Vitenzi hivi ndivyo huwa kiini cha sentensi sahili.
(ii)Muundo wa kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu.
Mfano:
-Alikuwa anasoma
Ts T
-Alikuwa anataka kukimbia
Ts Ts T
-Tulikuwa tunataka kwenda kuimba
Ts Ts Ts T
(iii)Muundo wa kitenzi kishirikishi.
Mfano:
-Mama ni mwalimu
t
- Huu sio mti wa dawa
t
- Yeye angali masomoni
t
- Ana alikuwa mwizi.
t
SIFA ZA SENTENSI SAHILI
(i)Ina kiima ambacho kimetajwa wazi au kimeacha kutajwa kwa kuwa kinaeleweka wazi.
(ii)Ina kiarifu kilichoundwa na kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kikuu nakitenzi kisaidizi au kishirikishi.
(iii)Haifungamani na sentensi nyingine na hivi inajitosheleza kimuundo na kimaana
2.SENTENSI CHANGAMANO
Hii ni sentensi iliyojengwa kwa kutumia kishazi huru kimoja na kishazi tegemezi kimoja au zaidi
mfano:
Sherehe iliyotangazwa imeahirishwa
Kishazi tegemezi (k/tg) – sherehe iliyotangazwa
Kishazi huru (k/hr) – sherehe imeahirishwa
Sifa ya sentensi changamano
Sentensi changamano ina kishazi tegemezi ambacho
hutegemea kishazi kingine huru ndani ya sentensi hiyo. Hivyo
msingi muhimu wa uhusiano ndani ya sentensi hizi ni ule wa kishazi
kimoja kutegemea kingine
Miundo ya sentensi changamano
Miundo ya sentensi changamano hutofautiana kutegemea
jinsi vishazi tegemezi vilivyoundwa ndani yake. Kutokana na
hayo kuna miundo ifuatayo ya sentensi changamano.
(i)miundo yenye vishazi – virejeshi
Miundo hii ni ile ambamo kirai – nomino hubeba kishazi – kirejeshi
Mfano:
-Mtoto aliyekuja jana anaumwa
-Mbuzi aliyenunuliwa juzi jioni amechinjwa leo asubuhi
Katika sentensi hizi uchangamano unaingizwa na vishazi
tegemezi rejeshi vilivyopigiwa mstari. Vishazi hivi vimebebwa na virai
nomino kiima katika sentensi husika.
(ii)Miundo – yenye vishazi vielezi.
Vishazi hivi ni vishazi vinavyoeleza hali ya vitenzi katika vishazi huruvinavyoandamana navyo ndani ya sentensi
Mfano:
-Mimi niliwaona walipoiba mahindi
-Mimi sikuvutiwa alivyosoma
-Maria alikimba aliponiona
Maneno yaliyopigiwa mstari ni vishazi vielezi katika
kila sentensi kila kishazi kama hicho hueleza hali katika kishazi
kilichoandamana nacho.
ZOEZI
1. “Si kila tungo ni sentensi “ Fafanua kauli hii kwa hoja za kutosha ili kubainisha tofauti zake.
2. Kwa kutumia mifano eleza maana ya istilahi zifuatazo
(a) Kiima
(b) Kiarifu
(c) Sentensi
(d) Shamirisho
(e) Chagizo
(f) Sentensi sahili
3. Nini tofauti kati ya
(a) Sentensi sahili na sentensi shurutia
(b) Sentensi ambatano na sentensi shangamano
4. Kwa kutumia mifano eleza wazi muundo wa sentensi sahili, changamano na ambatano.
3. SENTENSI AMBATANO
Ni aina ya sentensi ambayo hujengwa na
sentensi mbili au zaidi zilizounganishwa kwa kutumia viunganishi kama
vile na, lakini, wala, au, tena wakati mwingine alama ya mkato (,)
hutumiwa badala ya viunganishi
Mfano:
-Mwalimu anafundisha na wanafunzi wanasikiliza
-Juma ni mrefu lakini Hamisi ni mfupi
-Ni mkatili tena hana huruma.
Miundo ya sentensi Ambatano
(i)Miundo yenye sentensi sahili tu
mfano:
-Baba analima na mama anapika
-Siogopi wala sitishiki
(ii)Miundo yenye sentensi sahili na changamano
Mfano:
-Wanafunzi waliofika jana wamekwenda darasani lakinimwalimu wao hakufundisha.
(iii)Miundo yenye sentensi changamano tu
-Mzee aliyefika asubuhi ameondoka na mzigo aliokuja nao ameuacha
(iv) Miundo yenye vishazi visivyounganishwa kwa viunganishi
vishazi vyote vinavyohusika katika miundo ya aina hii
vina virai– vitenzi vyenye kiambishi tamati. Kiambishi
hiki kinaeleza hali ya nia ya kutenda jambo. Kila kishazi katika miundo
kama hii kikiondolewa katika muktadha wa sentensi kubwa kinakuwa
sentensi inayojitegemea. Isitoshe, miundo kama hii haihusishi njeo.
Mfano:
-Mwambie, aondoke,
-Mwombe, akupe
-Mfundishe, aelewe
miundo hii mara nyingi huwa imeelekezwa kwa nafsi ya pili umoja na wingi.
4. Sentensi shurutia.
Hizi ni sentensi zinazoonesha kutegemeana na
matukio mawili. Sentensi shurutia zimejengwa kwa vishazi tegemezi
viwili vinavyoonesha kuwa tukio moja lilitazamiwa litokee au lisitokee
ili la pili litokee au lisitokee. Utegemezi huo huoneshwa kwa mofimu za
masharti: ‘nge’, ‘ngali’, ‘ngeli’ na ‘ki’
Mfano:
-Angewahi kuja tungekwenda kufua
-Angelisoma kwa bidii angelifaulu mtihani
-Akija nitakuita
Sentensi shurutia zenye viangama ngeli, ngali, nge daima
huwa katika wakati uliopita. Pia kiangama kimoja kama vile
‘nge’ kikitumika katika kishazi cha mwanzo sharti kishazi cha pili
kitumie kiangama hicho hicho. Hali kadhalika‘ngeli’, ‘ngali’,
ZOEZI:
Ainisha sentensi zifuatazo .
a) Haya ni maelezo ya mtu mwingine.
b) Mbuzi aliyenunuliwa juzi amechinjwa leo asubuhi.
c) Nitakuja lakini nitachelewa
d) Angeondoka mapema asinge chelewa
e)Ng’ombe aliye nunuliwa amechinjwa ili wananchi wapate kitoweo.
UCHANGANUZI WA SENTENSI
Kuchanganua sentensi maana yake ni kufafanua vipengele vinavyojenga sentensi katika madaraja mbalimbali.
Kila sentensi huweza kufafanuliwa au kuchanganuliwa na kubainishwa vipashio vinavyoijenga.
Hatua za uchanganuzi wa sentensi
(i)Kutaja aina ya sentensi, yaani kama ni sentensi ambatano, sahili, changamano au shurutia
(ii)Kutaja sehemu kuu za sentensi yaani kiima na kiarifu
(iii)Kutaja vipashio vya kiima na kiarifu yaani vikundi nomino,vikundi tenzi ,vikundi vielezi nk
(iv) Kutambua vijenzi vikuu vinavyounda sentensi hiyo yaani vishazi vyake
(v)Kutaja aina zote za maneno yaliyomo katika sentensi.
Vifupisho vitumikavyo katika uchanga nuzi.
S – Sentensi K - Kiima
A- Kiarifu KN- kikundi nomino
KT- Kikundi tenzi KE- Kikundi kielezi - Kapa
Njia za uchanganuzi wa sentensi.
a) Njia ya jedwali/ Visanduku
b) Njia ya matawi / Miti.
c) Njia ya mishale
d) Njia ya maelezo.
Katika kidato cha tatu,hata hiyo tutatumia njia ya jedwali na matawi peke yake.
Mfano: 1.
K A
Ng’ombe huyu/ anakula majani makavu
N V T N V
usiku na mchana .
E
Njia ya jedwali
.
S SAHILI
| |||
K
|
A
| ||
KN
|
KT
|
KN
|
KE
|
N V
|
T
|
N V
|
E
|
Ng’ombe huyu
|
anakula
|
Majani makavu
|
Usiku na mchana
|
Njia ya matawi.
SAHILI
Ngo,mbe huyu anakula majani makavu usiku na mchana
S . SAHILI
K A
KT KN KE
KN
N + V T N + V E
Ng,ombe huyu anakula majani makavu
Usiku na mchana
Mfano:2
K A
Samaki aliyeletwa / amechina kabisa
N V T E
S . CHANGAMANO
JEDWALI
S CHANGAMANO
| ||
K
|
A
| |
KN
|
KT
|
KE
|
N+V
|
T
|
E
|
Samaki aliyeletwa
|
Amechina
|
Kabisa
|
MATAWI:
CHANGAMANO:
S. CHANGAMANO:
K A
KN KT KE
N + V T E
Samaki aliyeletwa amechina sana
3. Mfano:
Wanafunzi wanasoma sana lakini wanacho kisoma hawakizingatii.
AMBATANO:
S1. Wanafunzi wanasoma sana.
S2. Wanafunzi wanacho kisoma hawakizingatii.
JEDWALI
S AMBATANO
| |||||
S1. K
|
A
|
S2. K
|
A
| ||
KN
|
KT
|
KE
|
KN
|
KT
| |
N
|
T
|
E
|
U
|
W
|
T
|
wanafunzi
|
wanasoma
|
sana
|
lakini
|
Wanacho kisoma
|
Hawakizingatii.
|
MATAWI:
AMBATANO
S. AMBATANO
S1 S2
K A
K A
KN KT KE
KN KT
N T E U W T
Sana lakini hawakizingatii
wanachoikisoma
Wanafunzi wanasoma
4. Mfano:.
A
K/Ondoka hapa S. SAHILI
T E
JEDWALI
S SAHILI
| ||
K
|
A
| |
KT
|
KE
| |
T
|
E
| |
Ondoka
|
hapa
|
MATAWI:
S. SAHILI
K A
KT KE
T E
O ndoka hapa
K A
5. Mimi / niseme kitu gani sasa. SAHILI
W T N V E
JEDWALI:
S . SAHILI
| |||
K
|
A
| ||
KN
|
KT
|
KN
|
KE
|
W
|
T
|
N+V
|
E
|
Mimi
|
niseme
|
Kitu gani
|
Sasa.
|
MATAWI:
S. SAHILI
K A
KN KT KN KE
W T N+ V E
Mimi Niseme kitu gani sasa
K A
6 . Haya/ni maelezo ya mtu mwingine
W t N V
JEDWALI :
S. SAHILI
| ||
K
|
A
| |
KN
|
KT
|
KN
|
W
|
t
|
N+V
|
Haya
|
ni
|
Maelezo ya mtu mwingine
|
MATAWI
S. SAHILI
K A
KN KT KN
W t N + V
Haya ni maelezo ya mtu mwingine
K A
7.Mwalimu wetu/ angali anafundisha vizuri SAHILI
N V Ts T E
S. SAHILI
| ||
K
|
A
| |
KN
|
KT
|
KE
|
N+V
|
TS + T
|
E
|
Mwalimu wetu
|
Angali
anafundisha
|
Vizuri
|
MAJEDWALI:
S. SAHILI
K A
KN KT KE
N + V TS + T E
Mwalimu wetu angali
Anafundisha vizuri
ZOEZI
.
1.Changanua sentensi zifuatazo kwa Njia ya matawi na majedwali
(a) Maria ni mwalimu wetu.
(b) Mtoto aliyeanguka jana usiku na Kuvunjika mkono
amelazwa Hospitali.
.
(c) Bosi aliyefukuzwa kazi amekufa
(d) Katika nchi ya vipofu chongo ni Mfalme.
(e ) Huko shinyanga misitu Imeyeyuka kama siagi.
( a ) CHATI (Chemsha Bongo)
1 2 3 4 5 6 7
1
| ||||||
3
| ||||||
5
|
Kwenda Chini
1. Majengo ya kusomeshea Wanafunzi.
3. Malipo kwa huduma fulani
5. Sikukuu ya Waislamu
7. Sehemu ya Wizara au Kampuni
Kwenda Kulia
1. Mtu anayetoa maelezo ya kuthibitisha
3. Lia kama fahali
5. Kuwa juu ya maji bila kuzama.