MTIHANI WA KUJIPIMA KISWAHILI KIDATO CHA TATU
MTIHANI WA KUJIPIMA KISWAHILI
KIDATO CHA TATU
MUDA: Saa
2:30
MAAGIZO:
·
Mtihani huu una sehemu A, B, C, D, na E.
·
Jibu maswali yote katika sehemu A, B na C. Jibu
swali moja katika sehemu D na maswali mawili katika sehemu E.
·
Majibu yote yaandikwe kwenye karatasi ya majibu
utakayopewa.
·
Zingatia maelekezo kwa makini.
SEHEMU A (ALAMA 10)
UFAHAMU
1.
Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha ujibu
maswali.
Watoto wa baba Kapeto ni mfano wa kuigwa kwenye kijiji cha Sokomoko.
Mama na baba Kapeto ni waajiriwa katika taasisi maarufu ya elimu ya juu iliyopo
katikati ya mkoa wa Nyanda za juu nchini.
Kapeto ni mtoto wa tatu kuzaliwa kwenye
familia yao. Juhudi zake katika masomo zilimfanya kuwa kipenzi cha walimu pamoja
na wanafunzi wa shule ya msingi Sokomoko. Ubunifu wake katika sanaa pamoja na
umahiri wake kwenye riadha ulimpa umaarufu mkubwa hata katika shule za vijiji
vya jirani.
Hali ilikuwa tofauti kwa kitinda mimba wa familia hiyo.
Licha ya kulelewa kwa kupewa huduma zote muhimu na kuengwa engwa kama mboni ya
jicho, hapendeki hakusawiri kabisa tabia za watoto wa kaya hii. Kilichobainika kutoka kwa wakazi wengi wa kijiji
hicho ni masikitiko, na wengine walidiriki kusema “….. ama kweli kwenye miti
hakuna wajenzi.”
Tabia ya kujishirikisha kwenye vikundi
vya watoto watukutu,
haikuacha kudhihirisha ile kawaida ya uozo wa tunda, kuambukiza mengine.
Kwa manung’uniko na majonzi, mama Kapeto
aliwahi kusikika akiukana mtazamo unaoamini kuwa baada ya dhiki faraja, kwa sababu ujauzito wa
mvulana huyu ulimsumbua mama yake kupita kiasi ukilinganishwa na ule wa mwanzo
uliokuwa wa watoto mapacha.
Maendeleo ya kitaaluma yalimomonyoka
taratibu wakati Hapendeki akiwa ukingoni mwa kuhitimu masomo yake. Hatimaye
mwana huyu akawa ni mwanafunzi pekee aliyeshikilia mkia katika matokeo ya
mtihani wa mwisho wa kumaliza elimu ya msingi. Tukio hili halikusita
kuwakumbusha walimu waliokuwa wakiwakumbika vyema wakubwa wake waliopitia shule
hiyo kutokana na historia njema waliyoiacha.
Matumaini ya wazazi kupata muhandisi
yalididimia. Walichoambulia ni madaktari ambao wanajiendeleza kimasomaso huko
ughaibuni, huku kila mmoja akiwa na matarjio ya kubobea katika taaluma ya
kutibu wagonjwa wa jinsia yake. Kapeto naye amefanikiwa kujiunga na masomo ya
mchepuo wa biashara, ambayo nayo yanatoa ishara njema ya kumfanya awe mtaalamu
wa uchumi hapo baadaye. Masikini wee! Nyota ya Hapendeki imezima.
MASWALI
(a) Pendekeza
kichwa cha habari kinachoshabihiana na mambo yaliyoelezwa kwenye kifungu.
(b) Watoto
wote wa familia hii ni wangapi?
(c) Wataje
watoto wote kwa majina yao.
(d) Taja
methali mbili zilizomo kwenye kifungu ulichosoma.
(e) Eleza
maana ya maneno yaliyopigiwa mstari kulingana na yalivyotumika kwenye kifungu.
2.
Fupisha aya ya tatu na ya nne katika kifungu kwa
maneno yasiyozidi thelathini (30).
SEHEMU B (ALAMA 25)
SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
Jibu maswali yote
katika sehemu hii huku ukiwa makini katika kuyaelewa maswali
3.
Tungo sentensi huundwa kwa kuzingatia kanuni na
vipashio vinavyohusika. Tunga sentensi yenye sifa zifuatazo:-
-
Yenye kishazi kimoja
-
Yenye kirai nomino na kirai kielezi
4.
Ichanganue sentensi uliyotunga hapo juu kwa njia
ya kisanduku.
5.
Vitenzi vifuatavyo vikiambishwa vinaweza kuunda
majina ya watu waliobobea kwenye kazi Fulani.
Mfano: Kagua Mkaguzi
(i)
Ugua _______________________
(ii)
Chunguza _______________________
(iii)
Andaa _______________________
(iv)
Pekua _______________________
(v)
Jenga _______________________
6.
(i) Toa fasili ya kielezi.
(ii) Toa mfano mmoja kwa kila
kazi ya kielezi ili kuthibitisha ukamilifu wa fasili yako hapo juu.
7.
Taja aina ya ngeli inayowiana na kila nomino
katika orodha ifuatayo.
NOMINO
|
AINA YA NGELI
|
(i)
Kipofu
|
|
(ii)
Kiti
|
|
(iii)
Ngoma
|
|
(iv)
Mtama
|
|
(v)
Bata
|
|
SEHEMU C : (ALAMA 10)
UANDISHI
8.
Kwa kuzingatia muundo sahihi na mambo muhimu
yanayohitajika mwandikie mzazi wako simu ili umfahamishe kuwa mumeshafunga
shule.
SEHEMU D : (ALAMA 15)
MAENDELEO YA KISWAHILI
9.
“Waarabu hawana mchango wowote katika kukua na
kuenea kwa lugha ya Kiswahili.” Jadili kwa mifano kauli hii.
SEHEMU E (ALAMA 40)
FASIHI
Jibu maswali
mawili tu. Swali la 12 ni la lazima.
VITABU VYA REJEA
TAMTHILIYA
-
Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
-
Orodha - Steve Raymond (MA)
10.
Chagua wahusika wawili kutoka kila tamthiliya
mbili ulizosoma kisha uoneshe jinsi mwandishi alivyowatumia katika kuifunza
jamii maadili mema.
11.
Fani na maudhui huingiliana na kuathiriana.
Jadili kauli hii kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma.
12. Fafanua njia mbali mbali zinazotumika katika ukusanyaji wa fasihi simulizi katika jamii.