Wema Sepetu AIPASUA CCM Singida......Mwenyekiti Atishia Kuhama Chama Iwapo Wema Sepetu Atapitishwa
Kinyang'anyiro
cha ubunge wa viti maalum katika mkoa wa Singida kimeibua mapya, baada
ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT)
Wilaya ya Ikungi, Christina Hamis, kutishia kususia kuingia kwenye ofisi
za jumuiya hiyo na kuhama chama.
Mwenyekiti
huyo anakusudia kuchukua uamuzi huo kwa madai kuwa Katibu wa CCM wa
wilaya hiyo, Aluu Segamba, anamlazimisha amuunge mkono mgombea ubunge wa
Viti Maalumu (CCM), Wema Sepetu.
Alisema
atachukua maamuzi ya kuhama chama na kujiunga na Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) kutokana na vitendo anavyofanyiwa na baadhi ya
viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na Mkoa wa Singida kwa sababu hamuungi
mkono msanii huyo wa Bongo movie na Miss Tanzania 2006.
Christina
alisema pamoja na kwamba yeye ni Mwenyekiti wa UWT wilaya, jambo
linalomshangaza ni kuona mambo yasiyoridhisha yakifanyika ndani ya
nyumba za mawakala wa mgombea ubunge huyo.
Alisema
tangu mchakato umeanza amekuwa akipokea kauli za kashfa na matusi
kutoka kwa watu wa karibu wa Wema akiwamo mama yake, Mariam Sepetu,
kutokana na kutomuunga mkono mtoto wake.
Mariam
Sepetu alipoulizwa kuhusu kutoa maneno ya kashfa kwa Mwenyekiti wa UWT,
alisema hawezi kujibu mambo yoyote kuhusu kiongozi huyo.
Christina
alisema kwa mara kadhaa amewasilisha malalamiko yake kwa Katibu wa CCM
wilaya ya Ikungi, Segamba kuhusu matusi, kashfa na vitisho anavyopata,
lakini hapewi ushirikiano.
“Nimemweleza
Katibu wa Wilaya mambo nayofanyiwa, lakini niliishiwa kuambiwa siwezi
kupata msaada wowote kwenye ofisi hiyo na kwamba niachane na Wema kwa
sababu ameletwa na kiongozi mmoja mkubwa wa serikali, mawaziri na mtoto
wa kigogo agombee ubunge,” alisema.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti huyo, maamuzi ya kugombea ubunge kwa Wema
kumetokana na kushawishiwa na vigogo wa serikali na kwamba viongozi
waliopo mkoani hapa wanatakiwa kumuunga mkono.
Christina
alisema baada ya kuona hasaidiwi, aliwasilisha malalamiko kwa Katibu wa
UWT Mkoa wa Singida, Anjela Mirembe, lakini jibu alilopatiwa ni kwamba Wema ameletwa na wakubwa na hivyo aachane naye.
Alipotakiwa
kuzungumzia malalamiko ya mwenyekiti huyo wa UWT wilaya ya Ikungi,
Mirembe alithibitisha kupokea malalamiko hayo kwa maneno, badala ya
maandishi kama taratibu za kiutendaji wa kazi za kiofisi zinavyoelekeza
na hivyo kushindwa kuyafanyia kazi.
Katibu
wa UWT wilaya ya Ikungi, Yagi Kyaratu, alisema alipokea malalamiko hayo
kutoka kwa mwenyekiti wake na kuyawasilisha kwa Katibu wa UWT mkoa wa
Singida.
Katibu
wa CCM wilaya ya Ikungi ambaye pia ni kaimu katibu wa CCM Mkoa wa
Singida, Segamba, alipotafutwa ili aweze kujibu tuhuma zilizoelekezwa
kwake alijibu kuwa yupo kwenye kikao.
Kwa
upande wake, Wema alipotafutwa jana, simu yake hukupatikana na hata
alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi, hakujibu hadi tunakwenda
mitamboni.