FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA KIAFRIKA-1





FASIHI   SIMULIZI  YA  KISWAHILI   NA KIAFRIKA
MODULE   1; UTANGULIZI
 FASIHINSIMULIZI   YA  KISWAHILI

Senkoro   (1988:10-11) Anasema Fasihi simulizi ni ile inayojitambulisha na kujihusisha na utamaduni wa waswahili popote pale walipo ulimwenguni.Utamaduni  wa waswahili ni ule unaohusu desturi na mila za waswahili sayansi,sanaa zao,uchumi wao na maisha yao kwa ujumla.
Hali kadhalika inawahusika ,maudhui,falsafa,mawazo,historia, n.k vinvyofanana na maisha ya waswahili. Kwa upande wa lugha ,Falsafa ya Kiswahili ni ile inayotumia lugha au lahaja ya Kiswahili.
        FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA
     Ni ile inayojitambulisha na kujihusisha na utamaduni  wanaa zao ,siasa na  Afrika kupitia jamii na Lugha zao. Hivyo  utamaduni wa Waafrika ni ule unaohusu mila zao ,siasa na uchumi wao kwa ujumla.
   Hivyo Fasihi simulizi  ya kiafrika ina mawazo ,falsafa,wahusika,maudhui,na dhamira zinazoendana na maisha yao.Imetungwa kwa lugha za kiafrika au lahaja za lugha hizo.
   Maswali hapa ya kujiuliza ni;
Ø  Je fasihi simulizi ni ya kiafrika?
Ø  Je fasihi  simulizi  inayotumia lugha za nje zinazotumika nje ya  Afrika ni ya kiafrika pia?
Ø  Je   fasihi simulizi ya kiafrika inapaswa kuandikwa na nani? Mwafrika au hata mzungu?

FASIHI   SIMULIZI
  Mgullu  (2003 uk  16) anasema Fasihi simulizi ni sanaa itoayo maudhui yake kwa lugha ya maneno ambayo hutamkwa ama hutendwa.
 Ni fasihi inayohusu mkusanyiko wa kazi za kisanaa za binadamu zinazowasilishwa kwa njia ya mazungumzo au utendaji.Siku hizi fasihi  simulizi  huhifadhiwa kwa kuandikwa vitabuni,kanda za video,Redio na santuri.
Mlacha  (1985:16)  Anasema Fasihi simulizi ni Nyanja ya maisha ya jamii ambayo huchangia sana katika kuendeleza na kudumisha historia ya jamii husika.
       Fasihi simulizi  huchangia katika kuelimisha jamii kuhusu asili  yake ,chanzo chake na maendeleo ya utamaduni wake na maisha  ya jamii hiyo tangu zamani .
Wamitila (2003:44) Anasema  Fasihi simulizi ni dhana inayotumika kurejelea kazi ambazo kimsingi hudokeza na kwa njia ya masimulizi ya mdomo.Hutumika katika jamii kama njia ya kupashana maarifa yanayohusu utamaduni fulani,historia fulani ya jamii na matamanio yao.
   OKPEWHO (1992:3) Anasema Fasihi simulizi ni matini bainifu ambazo huvutia fikra zetu au hisia zetu,kama vile hadithi,mashairi na michezo ya kuigiza  na sio kwa matini za kweli kama vile Ripoti za magazetini au rekodi za kihistoria,hata hivyo nazo zikiandikwa kwa kuvutia zinaweza kuwa fasihi.
    Mlokozi (1996:24) Anasema Fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani  na kuwasilishwa  kwa hadhira kwa njia yam domo na vitendo bila kutumia maandishi.
   Hivyo ni tukio linalofungamana na muktadha fulani wa kijamii na kutawaliwa na mwingiliano wa  mambo sita,ambayo ni;
Ø  Fanani (msanii)
Ø  Hadhira
Ø  Fani inayotendwa
Ø  Tukio
Ø  Mahali na wakati
Ø  Fasihi  simulizi inaendana na tukio
SWALI: ‘’Mbali na jitihada za wataalamu mbalimbali katika kufasili fasihi simulizi na fasihi simulizi ya kiafrika mpaka sasa hakuna fasihi  iliyotoshelevu.Jidili  dai hili na pendekeza fasili yako’’
KUFANANA NA KUTOFAUTIANA KWA FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA YA KIAFRIKA
v  Zote zinahifadhi mila ,desturi na historia pamoja na lugha za jamii husika
v  Zote zinahitaji utendaji  ambao unajumuisha vifaa mbali mbali kama vile maleba yaani mavazi maalumu
v  Vipera na tanzu vinaingiliana na kufanana
v  Muktadha na maudhui ya lugha maalum dhana hizi zinajitokeza kote
UTOFAUTI  KATI YA FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA YA KIAFRIKA
Ø  Fasihi simulizi ya kiafrika ni pana sana  lakini fasihi ya Kiswahili ni finyu kwani fasihi  ya Kiswahili huchota vipengele fulani katika fasihi simulizi ya kiafrika.
Ø   Fasihi simulizi ya kiafrika ni kongwe
Ø  Utamaduni wa Fasihi simulizi ya kiafrika ni tofauti na ule wa kiafrika.
   TANZU ZA FASIHI SIMULIZI NA UAINISHAJI WAKE
 Tanzu ni matawi.Uainishaji wa Tanzu za Fasihi simulizi  si jambo rahisi.Wataalamu mbali mbali wamejaribu kuainisha lakini wamepambana na matatizo kdha wa kadha  kwani;
v  Afrika ina utajiri mkubwa wa tanzu za fasihi simulizi.
v  Tanzu hizo zinafanana sana
v  Tanzu hizo zinaingiliana.

Wageni walipokuja kama vile Finegan (1970),Matteru (1977),Mlokozi (1996),Catheline, Kitula na king’ei  (2005),Wafula  na Ndungo (1993),Liongo (1972),Wafula na Njogu  (2007) na wengine wamefanya jitihada za kuainisha tanzu za Fasihi simulizi.Si rahisi kuainisha Tanzu kwani hakuna mipaka bayana kati ya Utanzu mmoja na mwingine.Hadithi,methali,Vitendawili na mafumbo vinaweza kuwekwa katika kundi moja.
Ø  Wapo wataalamu walioainisha Tanzu za watoto na tanzu za watu wazima.Mfano Methali ni tanzu za watu wazima.
Ø  Swali; Je ni upi utanzu bora kuliko mwingine?  Baadhi  ya wataalamu walisema methali ni uti wa mgongo wa  mazungumzo.
VIGEZO VYA UAINISHAJI WA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI
Wafula na Njogu wanasema ili tuweze kuainisha tanzu za fasihi simulizi lazima tuwe na vigezo;
v  Majina ya tanzu
v  Miundo
v  Mitindo
v  Wahusika
v  Wakati na mahali pa utendaji
                     Wafula R. na Ndungo .C (1993) wametumia vigezo vifuatavyo katika uainishaji wao;
*      Majina ya tanzu
*      Miundo
*      Mitindo yake
*      Mianzo na miisho  yake
*      Maudhui
*      Kujipambanua kwake kitabaka
*      Jinsia (kuna tanzu za kike na za kiume)
*      Mahali na wakati
*      Wahusika
 Materu (1983) ameainisha tanzu za Fasihi simulizi katika makundi makubwa matatu,ambayo ni;
1.       NATHARI
Ni masimulizi au mazungumzo
·         Ngano
·         Visasili
·         Misendu na n.k
2.      USHAIRI
Ø  Mashairi
Ø  Nyimbo
Ø  Tumbuizo
Ø  Utenzi
Ø  Maghani
Ø  Ghibu
3.      SEMI
·         Mafumbo
·         Misemo ya kilinge
·         Methali
·         Vitendawili
  Kitula king’ei na Catheline Kisovi wametaja makundi  4 ya tanzu ambayo ni;
1.      SEMI
Ø  Misemo
Ø  Methali
Ø  Mafumbo
Ø  Vitanza ndimi
Ø  Utani
2.       Hadithi
v  Ngano/Hekaya
v  Visasili
v  Maghani
v  Visakale
3.      MAIGIZO
*      Michezo ya kuigiza
*      Sarakasi
*      Majigambo
*      Ngomezi
*      Utani
*      Mawaidha
*      Mipasho/Michongoano
*      Ngonjera
*      Vichekesho
4.      USHAIRI
v  Nyimbo kama vile Rege,Chakacha,Nyimbo za harusi,Mbolezi,Wawe,Mkwaju ngoma,Nyimbo za Unyago,Bembelezi,Nyimbo za jandoni n.k
v  Ngonjera
v  Mashairi
v  Tenzi
v  Kirumbikizi
 Mlokozi M.M (1996) ameainisha tanzu kwa kutumia vigezo  vifuatavyo;
Ø  Umbile na tabia ya Utanzu
Ø  Muktadha wa uwasilishaji yaani wakati na mazingira
Ø  Namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira  (Mtindo)
Ø  Dhima ya Fani na utanzu wake.
Mlokozi ameainisha Tanzu za Fasihi simulizi  katika makundi sita ambayo ni ;
1.       MAZUNGUMZO
Utanzu huu una vipera vine,ambavyo ni;
·         Hotuba
·         Malumbano ya watani
·         Mizaha
·         Sala
*      Dua
*      Maapizo
*      Tabano
2.      MASIMULIZI
Utanzu huu una vipera  vitatu,ambavyo ni
Ø  Hadithi za kubuni
*      Vigano
*      Istiara
*      Mbazi
*      Michapo
Ø  Salua
*      Visakale
*      Mapisi
*      Tarihi
*      Shajara
*      Kumbukumbu
Ø  Visasili
*      Visasili vya uzuri
*      Visasili vya ibada na dini
*      Visasili vya miungu na mizimu
3.      MAIGIZO
Utanzu huu unajumuisha maigizo ya watoto,misiba,Sherehe za kidini n.k
4.USHAIRI  SIMULIZI
  Vipera vyake ni;
·         Nyimbo
*      Tumbuizo
-Bembea
-Mbolezi
-Nyiso
*      Tukuzo
-Kongozi
-Nyimbo za dini
-Nyimbo za taifa
*      Chapuzo au kimai
-Nyimbo za kutwanga
-Nyimbo za watoto
-Nyimbo za vita
*      Tenzi na Tendi
·         Maghani
*      Ghani nafsi-kutamba
*      Ghani tumbuizi
*      Sifo-Vivugo (majigambo)
       -Tondozi
*      Maghani simulizi
-Tendi
-Rara
5.      SEMI
·         Methali
·         Vitendawili
·         Mafumbo
-Chemsha bongo
-Fumbo jina
·         Simo/misimo
·         Kauli kaulia
6.Ngomezi

FASILI YA DHANA MBALI MBALI ZA FASIHI
v  Mazungumzo
Ni mazungumzo yenye sanaa ndani yake yaliyosheheni mbinu za kifani (Fani na Maudhui).
Mfano Tamathali za semi  kama vile sitiari,Tashibiha n.k
v  Mbazi
Ni hadithi fupi zenye lengo la kuonya
v  Salua
Ni hadithi zinazosimulia matukio ya kihistoria / ya zamani .
v  Visakale
Ni visa vya kimapokeo vya mashujaa
v  Mapisi
Ni historia ya matukio ya kweli
v  Tarihi
Ni maelezo au jedwali la matukio muhimu na tarehe zake.
v  Visasili
        Ni hadithi za kale zinazozungumzia asili ya kitu au imani ya mtu.mfano asili ya binadamu.
v  Mbolezi
Ni nyimbo za kuliwaza katika msiba.
v  Nyiso
Ni nyimbo  za jandoni na unyago.
v  Wawe
Ni nyimbo za kazi
v  Kongozi
        Ni  nyimbo za kuaga mwaka,mara nyingi zinaambatana na tambiko.
v  Tenzi
Ni utungo unaozungumzia tukio fulani.
v  Tendi
Ni utungo unaozungumzia tukio la kishujaa
v  Sifo
Ni nyimbo za kusifu
v  Tondozi
Ni tungo za kusifu wanyama n.k
v  Rara
Ni maghani ya kusimulia tukio fulani la kihistoria na huenda sambamba na ala za mziki.
v  Fumbo jina
Ni mafumbo ya yanayotaja majina .mfano  Mwamvua alizaliwa kipindi cha mvua
v  Lakabu
Kupewa jina kulingana na tabia mfano Mwl J.K Nyere-Baba wa Taifa
v  Kauli Taulia
Ni kauli zenye mfuatano wa sauti


Powered by Blogger.