FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA KIAFRIKA
FASIHI SIMULIZI YA
KISWAHILI NA KIAFRIKA
MODULE 1; UTANGULIZI
FASIHINSIMULIZI YA
KISWAHILI
Senkoro (1988:10-11) Anasema Fasihi simulizi ni ile
inayojitambulisha na kujihusisha na utamaduni wa waswahili popote pale walipo
ulimwenguni.Utamaduni wa waswahili ni
ule unaohusu desturi na mila za waswahili sayansi,sanaa zao,uchumi wao na
maisha yao kwa ujumla.
Hali kadhalika inawahusika
,maudhui,falsafa,mawazo,historia, n.k vinvyofanana na maisha ya waswahili. Kwa
upande wa lugha ,Falsafa ya Kiswahili ni ile inayotumia lugha au lahaja ya Kiswahili.
FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA
Ni ile inayojitambulisha na kujihusisha na
utamaduni wanaa zao ,siasa na Afrika kupitia jamii na Lugha zao. Hivyo utamaduni wa Waafrika ni ule unaohusu mila zao
,siasa na uchumi wao kwa ujumla.
Hivyo Fasihi simulizi ya kiafrika
ina mawazo ,falsafa,wahusika,maudhui,na dhamira zinazoendana na maisha
yao.Imetungwa kwa lugha za kiafrika au lahaja za lugha hizo.
Maswali hapa ya kujiuliza ni;
Ø Je fasihi simulizi ni ya kiafrika?
Ø Je fasihi simulizi
inayotumia lugha za nje zinazotumika nje ya Afrika ni ya kiafrika pia?
Ø Je
fasihi simulizi ya kiafrika inapaswa kuandikwa na nani? Mwafrika au hata
mzungu?
FASIHI SIMULIZI
Mgullu (2003 uk
16) anasema Fasihi
simulizi ni sanaa itoayo maudhui yake kwa lugha ya maneno ambayo hutamkwa ama
hutendwa.
Ni fasihi inayohusu mkusanyiko wa kazi
za kisanaa za binadamu zinazowasilishwa kwa njia ya mazungumzo au utendaji.Siku
hizi fasihi simulizi huhifadhiwa kwa kuandikwa vitabuni,kanda za
video,Redio na santuri.
Mlacha (1985:16)
Anasema Fasihi simulizi ni Nyanja
ya maisha ya jamii ambayo huchangia sana katika kuendeleza na kudumisha
historia ya jamii husika.
Fasihi simulizi huchangia katika
kuelimisha jamii kuhusu asili yake
,chanzo chake na maendeleo ya utamaduni wake na maisha ya jamii hiyo tangu zamani .
Wamitila (2003:44) Anasema Fasihi
simulizi ni dhana inayotumika kurejelea kazi ambazo kimsingi hudokeza
na kwa njia ya masimulizi ya mdomo.Hutumika katika jamii kama njia ya kupashana
maarifa yanayohusu utamaduni fulani,historia fulani ya jamii na matamanio yao.
OKPEWHO (1992:3) Anasema Fasihi
simulizi ni matini bainifu ambazo huvutia fikra zetu au hisia zetu,kama
vile hadithi,mashairi na michezo ya kuigiza
na sio kwa matini za kweli kama vile Ripoti za magazetini au rekodi za
kihistoria,hata hivyo nazo zikiandikwa kwa kuvutia zinaweza kuwa fasihi.
Mlokozi (1996:24) Anasema Fasihi
simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia yam domo na vitendo bila
kutumia maandishi.
Hivyo ni tukio linalofungamana na
muktadha fulani wa kijamii na kutawaliwa na mwingiliano wa mambo sita,ambayo ni;
Ø Fanani (msanii)
Ø Hadhira
Ø Fani inayotendwa
Ø Tukio
Ø Mahali na wakati
Ø Fasihi simulizi inaendana na tukio
SWALI: ‘’Mbali na jitihada za wataalamu mbalimbali katika kufasili fasihi
simulizi na fasihi simulizi ya kiafrika mpaka sasa hakuna fasihi iliyotoshelevu.Jidili dai hili na pendekeza fasili yako’’
KUFANANA NA KUTOFAUTIANA KWA FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA YA KIAFRIKA
v Zote zinahifadhi mila ,desturi na
historia pamoja na lugha za jamii husika
v Zote zinahitaji utendaji ambao unajumuisha vifaa mbali mbali kama vile
maleba yaani mavazi maalumu
v Vipera na tanzu vinaingiliana na
kufanana
v Muktadha na maudhui ya lugha maalum
dhana hizi zinajitokeza kote
UTOFAUTI KATI YA FASIHI
SIMULIZI YA KISWAHILI NA YA KIAFRIKA
Ø Fasihi simulizi ya kiafrika ni pana
sana lakini fasihi ya Kiswahili ni finyu
kwani fasihi ya Kiswahili huchota
vipengele fulani katika fasihi simulizi ya kiafrika.
Ø Fasihi simulizi ya kiafrika ni kongwe
Ø Utamaduni wa Fasihi simulizi ya
kiafrika ni tofauti na ule wa kiafrika.
TANZU ZA FASIHI SIMULIZI NA UAINISHAJI WAKE
Tanzu ni matawi.Uainishaji wa Tanzu za Fasihi simulizi si jambo rahisi.Wataalamu mbali mbali
wamejaribu kuainisha lakini wamepambana na matatizo kdha wa kadha kwani;
v Afrika ina utajiri mkubwa wa tanzu za
fasihi simulizi.
v Tanzu hizo zinafanana sana
v Tanzu hizo zinaingiliana.
Wageni
walipokuja kama vile Finegan (1970),Matteru (1977),Mlokozi (1996),Catheline,
Kitula na king’ei (2005),Wafula na Ndungo (1993),Liongo (1972),Wafula na
Njogu (2007) na wengine wamefanya
jitihada za kuainisha tanzu za Fasihi simulizi.Si rahisi kuainisha Tanzu kwani
hakuna mipaka bayana kati ya Utanzu mmoja na
mwingine.Hadithi,methali,Vitendawili na mafumbo vinaweza kuwekwa katika kundi
moja.
Ø Wapo wataalamu walioainisha Tanzu za
watoto na tanzu za watu wazima.Mfano Methali ni tanzu za watu wazima.
Ø Swali; Je ni upi utanzu bora kuliko
mwingine? Baadhi ya wataalamu walisema methali ni uti wa
mgongo wa mazungumzo.
VIGEZO VYA UAINISHAJI WA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI
Wafula na Njogu wanasema ili tuweze
kuainisha tanzu za fasihi simulizi lazima tuwe na vigezo;
v Majina ya tanzu
v Miundo
v Mitindo
v Wahusika
v Wakati na mahali pa utendaji
Wafula R. na Ndungo .C
(1993) wametumia vigezo vifuatavyo katika uainishaji wao;
Majina
ya tanzu
Miundo
Mitindo
yake
Mianzo
na miisho yake
Maudhui
Kujipambanua
kwake kitabaka
Jinsia
(kuna tanzu za kike na za kiume)
Mahali
na wakati
Wahusika
Materu (1983) ameainisha tanzu za Fasihi
simulizi katika makundi makubwa matatu,ambayo ni;
1. NATHARI
Ni masimulizi au mazungumzo
·
Ngano
·
Visasili
·
Misendu
na n.k
2. USHAIRI
Ø Mashairi
Ø Nyimbo
Ø Tumbuizo
Ø Utenzi
Ø Maghani
Ø Ghibu
3. SEMI
·
Mafumbo
·
Misemo
ya kilinge
·
Methali
·
Vitendawili
Kitula king’ei na Catheline Kisovi wametaja makundi 4 ya tanzu ambayo ni;
1. SEMI
Ø Misemo
Ø Methali
Ø Mafumbo
Ø Vitanza ndimi
Ø Utani
2. Hadithi
v Ngano/Hekaya
v Visasili
v Maghani
v Visakale
3. MAIGIZO
Michezo
ya kuigiza
Sarakasi
Majigambo
Ngomezi
Utani
Mawaidha
Mipasho/Michongoano
Ngonjera
Vichekesho
4. USHAIRI
v Nyimbo kama vile Rege,Chakacha,Nyimbo
za harusi,Mbolezi,Wawe,Mkwaju ngoma,Nyimbo za Unyago,Bembelezi,Nyimbo za
jandoni n.k
v Ngonjera
v Mashairi
v Tenzi
v Kirumbikizi
Mlokozi M.M (1996) ameainisha tanzu kwa
kutumia vigezo vifuatavyo;
Ø Umbile na tabia ya Utanzu
Ø Muktadha wa uwasilishaji yaani wakati
na mazingira
Ø Namna ya uwasilishaji wake kwa
hadhira (Mtindo)
Ø Dhima ya Fani na utanzu wake.
Mlokozi ameainisha Tanzu za Fasihi
simulizi katika makundi sita ambayo ni ;
1. MAZUNGUMZO
Utanzu huu una vipera vine,ambavyo
ni;
·
Hotuba
·
Malumbano
ya watani
·
Mizaha
·
Sala
Dua
Maapizo
Tabano
2. MASIMULIZI
Utanzu huu una vipera vitatu,ambavyo ni
Ø Hadithi za kubuni
Vigano
Istiara
Mbazi
Michapo
Ø Salua
Visakale
Mapisi
Tarihi
Shajara
Kumbukumbu
Ø Visasili
Visasili
vya uzuri
Visasili
vya ibada na dini
Visasili
vya miungu na mizimu
3. MAIGIZO
Utanzu huu unajumuisha maigizo ya
watoto,misiba,Sherehe za kidini n.k
4.USHAIRI SIMULIZI
Vipera vyake ni;
·
Nyimbo
Tumbuizo
-Bembea
-Mbolezi
-Nyiso
Tukuzo
-Kongozi
-Nyimbo za dini
-Nyimbo za taifa
Chapuzo
au kimai
-Nyimbo za kutwanga
-Nyimbo za watoto
-Nyimbo za vita
Tenzi
na Tendi
·
Maghani
Ghani
nafsi-kutamba
Ghani
tumbuizi
Sifo-Vivugo
(majigambo)
-Tondozi
Maghani
simulizi
-Tendi
-Rara
5. SEMI
·
Methali
·
Vitendawili
·
Mafumbo
-Chemsha bongo
-Fumbo jina
·
Simo/misimo
·
Kauli
kaulia
6.Ngomezi
FASILI YA DHANA MBALI MBALI ZA FASIHI
v Mazungumzo
Ni mazungumzo yenye sanaa ndani yake yaliyosheheni mbinu
za kifani (Fani na Maudhui).
Mfano Tamathali za semi kama vile sitiari,Tashibiha n.k
v Mbazi
Ni
hadithi fupi zenye lengo la kuonya
v Salua
Ni hadithi
zinazosimulia matukio ya kihistoria / ya zamani .
v Visakale
Ni
visa vya kimapokeo vya mashujaa
v Mapisi
Ni historia ya matukio ya kweli
v Tarihi
Ni
maelezo au jedwali la matukio muhimu na tarehe zake.
v Visasili
Ni hadithi za kale zinazozungumzia
asili ya kitu au imani ya mtu.mfano asili ya binadamu.
v Mbolezi
Ni
nyimbo za kuliwaza katika msiba.
v Nyiso
Ni
nyimbo za jandoni na unyago.
v Wawe
Ni nyimbo za kazi
v Kongozi
Ni
nyimbo za kuaga mwaka,mara nyingi zinaambatana na tambiko.
v Tenzi
Ni
utungo unaozungumzia tukio fulani.
v Tendi
Ni
utungo unaozungumzia tukio la kishujaa
v Sifo
Ni
nyimbo za kusifu
v Tondozi
Ni
tungo za kusifu wanyama n.k
v Rara
Ni
maghani ya kusimulia tukio fulani la kihistoria na huenda sambamba na ala za
mziki.
v Fumbo jina
Ni
mafumbo ya yanayotaja majina .mfano
Mwamvua alizaliwa kipindi cha mvua
v Lakabu
Kupewa jina kulingana na tabia mfano
Mwl J.K Nyere-Baba wa Taifa
v Kauli Taulia
Ni kauli zenye mfuatano wa sauti