FORM 3-KISWAHILI-MADA 3-MJENGO WA TUNGO

MJENGO WA TUNGO
Sentensi
Maana ya sentensi
Sentensi ni kifungu cha maneno kuanzia neno moja na kuendelea chenye muundo wa kiima na kiarifu na kinacholeta maana kamili.
Sifa za sentensi
Sentensi lazima iwe na mpangilio wa maneno ambao unakubalika na wazungumzaji wa lugha husika.
  • Sentensi lazima ikamilike kimaana, kimuundo na kisarufi.
  • Sentensi huwa na muundo wa kiima na kiarifu /huwa na kirai nomino na kirai kitenzi.
  • Sentensi huweza kuwa na zaidi ya kiima kimoja na kiarifu zaidi ya kimoja.
  • Sentensi inaweza kuundwa na kitenzi kikuu kimoja au zaidi.
  • Sentensi inaweza kuundwa na kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi.
  • Sentensi huonyesha hali mbalimbali, kama vile amri, ombi, mshangao, swali n.k
Muundo wa sentensi
Muundo wa sentensi kimapokeo/kikazi/kidhima
Muundo wa sentensi kimapokeo/kikazi/kidhima unakuwa na vipengele vifuatavyo:
  • Kiima: Ni sehemu katika sentensi ambayo hujaza sehemu ya mtenda au mtendwa wa jambo linaloelezwa. Katika tungo kiima hutokea kushoto mwa kitenzi.
  • Kiarifu: Ni sehemu katika sentensi inayojazwa na maneno yanayo arifu tendo lilofanywa, linapofanywa au litakapofanywa. Kiarifu ndiyo sehemu muhimu zaidi katika sentensi ambayo wakati mwengine huweza kusimama pekee, kwani wakati mwingine huchukua viwakilishi vya kiima.
Vipashio vya kiima
  • Nomino peke yake
  • Nomino, kiunganishi na nomino
  • Nomino na kivumishi
  • Kivumishi na nomino
  • Kiwakilishi peke yake
  • Kiwakilishi na kivumishi
  • Nomino na kishazi tegemezi vumishi
  • Kitenzi jina
  • Nomino na vivumishi zaidi ya kimoja
  • Kitenzi jina na nomino
  • Umbo kapa
Taarifa zitolewazo na kiarifu kuhusu kiima
  • Kiima ni nani
  • Kiima kina nini
  • Kiima hufanya nini
  • Kiima kinahisi nini
Sifa za kiarifu
  • Huwa na kitenzi na pengine huambatana na maneno mengine.
  • Kiarifu kwa kawaida huja baada ya kiima
Vipashio vya kiarifu
  • Kitenzi kikuu peke yake.
  • Kitenzi kisaidizi au vitenzi visaidizi vilivyosambamba na kitenzi kikuu.
  • Kitenzi kishirikishi na kijalizo
  • Yambwa (shamirisho)
  • Kijazalio
  • Chagizo
Sifa za chagizo
  • Chagizo kwa kawaida huwa ni kielezi au kirai husishi ambacho kinafanya kazi kama kielezi.
  • Kwa kawaida ni vipashio vya ziada. Si lazima viwepo katika sentensi ili ijisimamie.
  • Huwa cha lazima ikiwa kinafuata kitenzi kishiriki. Hali ikiwa hivyo, kinafnaya kazi kama kijalizo.
  • Hutumika kufafanua kitenzi/kivumishi /kielezi.
  • Hutumika kujaliza kiima/kama kijalizo.
Aina za sentensi
Uainishaji wa sentensi
Aina za sentensi kimuundo ni pamoja na hzi zifuatazo
Sentensi sahili
Ni sentensi ambayo huundwa na kishazi huru kimoja. Sentensi ya aina hii huwa inaelezea taarifa moja tu. Mfano; Wanafuzi wanafanya mtihani; Walinzi walitaka kunizuia nisiingiendani.
Miundo ya sentensi sahili
  • Muundo wa kitenzi kikuu peke yake. Mfano: Gari limeanguka
  • Muundo wa kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi. Mfano: Mgosiyuda alitaka (TS) nisipate (T) utajiri
  • Muundo wa vira-vitenzi vilivyokitwa katika kitenzi ‘kuwa’. Mfano: John amekuwa akiangaliaTV kwa muda mrefu sana.
  • Muundo wa kitenzi shirikishi. Mfano: Kiswahili ni tunu ya Taifa
Sifa za sentensi sahili
  • Ina kiima ambacho kimetajwa wazi au kimeachwa kutajwa kwa kuwa kinaeleweka.
  • Ina kiarifu ambacho kimeundwa na kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi au kitenzi kishirikishi na kijalizo na chagizo.
  • Haifungamani na sentensi nyingine na hivi inajitosheleza kimuundo na kimaana.
Sentensi changamano
Hii ni sentensi yenye kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi. Sifa moja kubwa ya sentensi changamano ni kuwa na kishazi tegemezi ambacho hutegemea kishazi kingine huru ndani ya sentensi hiyo. Msingi muhimu wa uhusiano ndani ya sentensi hizo ni ule wa kishazi kimoja kutegemea kingine
Sentensi changamano ina muundo wenye vishazi virejeshi. Mfano: Gari liliopinduka jana jioni halikuharibika hatata kidogo.
Sentensi ambatano
Hii ni sentensi inayojengwa na sentensi mbili au zaidi zilizounganishwa kwa kutumia viunganishi kama vile likini, wala, au, na, nakadhalika.
Miundo ya sentensi ambatano
  • Miundo yenye sentensi sahili tu. Mfano: Mwalimu anafundisha wakati wanafunzi wanapiga kelele.
  • Miundo yenye sentensi sahili na changamano. Mfano: Walinzi waliposhindwa polisi waliwasaidia lakini hawakuweza kuwakamata majambazi.
  • Miundo yenye sentensi changamano tu. Mfano: Barabara zilizojengwa na wakoloni zimedumu hadi leo wakati zile zilizojengwa na Wachina hata mwezi hazifikishi.
  • Miundo yenye vishazi visivyounganishwa kwa viunganishi.
Uchanganuzi wa sentensi
Kubainisha uchanganuzi wa sentensi
Uchanganuzi wa sentensi ni mchakoto unaohusika na kuchanganua vipashio vyote vinavyuonda sentensi kuanzia ngazi ya kategoria ya neno. Katika kipengele hiki utaweza kujifunza hatua muhimu za kuzingatia wakati wa uchanganuzi wa sentensi. Pia utajifunza njia mbalimbali zinazotumika katika uchanganuzi wa sentensi.
Hatua za uchanganuzi wa sentensi
  • Kutaja aina ya sentensi, yaani kama ni sahili, changamano au ambatano.
  • Kutaja sehemu zake kuu, yaani kiima na kiarifu au kirai nomino na kirai kitenzi.
  • Kutaja sehemu kuu za kiima na kiarifu au sehemu kuu za kirai nomino na kirai kitenzi.
  • Kutaja sehemu zote za maneno yaliyomo katika sentensi hiyo.
Powered by Blogger.