FORM 3-KISWAHILI-Kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania katika enzi ya Wajerumani

MAENDELEO YA KISWAHILI
Ukuaji wa Kiswahili nchini katika Enzi za Wajerumani
Fafanua ukuaji wa Kiswahili nchini katika enzi za Wajerumani
Wajerumani waliingia katika pwani ya Afrika Mashariki katika miaka ya 1875, walifanya kila jitihada kuwatawala Waafrika ambapo katika utawala wao walifanya biashara, waliendesha shughuli za kiutawala, za kidini na kielimu. Katika shuguli zote hizo Kiswahili ndio ilikuwa lugha ya mawasilino hivyo kukikuza na kukiendeleza Kiswahili
Walipongia katika pwani ya Afrika Mashariki walikuta Kiswahili kimekwisha enea kwa kiasi kikubwa. Kuna mambo waliyoyafanya ambayo yalisaidia kukua na kuenea kwa Kiswahili kama ifuatavyo:
Kutoa mafunzo ya lazima ya lugha ya Kiswahili kwa wafanyakazi wa serikali
Waliwalazimisha wafaanyikazi wote wa serikali kujifunza kiswashili, kwa sababu sheria ilikuwa ni kwamba pasipojua Kiswahili huwezijiriwa katika serekali ya mjerumani. Kwa hiyo saula hili lilisababisha watu kujifunza lugha ya Kiswahili ili waweze kuajiriwa. Wafanyakazi ambao ilikuwa ni lazima wajifuze Kiswahili ni pamona na maakida.
Wajerumani wenyewe walilazimika kujifunza kiswahili ili waweze kuwasiliana na wenyeji kwa urahisi na hivyo kurahisisha shuguli zao za kiutawala.
Ujenzi wa shule
Shule zilifunguliwa kufundisha watu weusi ili waje wawe wasidizi wao katika utawala wa wajerumani, na lugha iliyokuwa ikitumika kufundisha masomo ilikuwa ni lugha ya Kiswahili
Kuenea kwa utawala wa Wajerumani nchi nzima
Utawala wa wajerumani ulikuwa kwenye kila kona ya nchi. Na kwa kuwa wafanya kazi wa serikali ya wakati huo ilikuwa ni lazima wafahamu Kiswahili, kwa hiyo kila sehemu palipokuwa na ofisi za serikali nchi nzima kulizungumzwa Kiswahili.
Shughuli za kiuchumi
Pia katika shuguli za mashamba, wajerumani walichukua vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi, na kwa kuwa kila mmoja alikuwa na lugha yake tofauti, kwa hiyo lugha pekee iliyowaunganisha katika mawasiliano kwenye eneo la kazi ilikuwa ni Kiswahili.
Kwa hiyo kutokana na sababu kwamba utawala wa kijerumani ulitoa msukumo mkubwa katika matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye shughuli zao za kiutawala, hivyo suala la ueneaji wa Kiswahili lisingeepukika.
Ueneaji wa Kiswahili nchini Tanzania katika Enzi za Wajerumani
Elezea ueneaji wa Kiswahili nchini Tanzania katika enzi za Wajerumani
Wajerumani walichangia kwa sehemu kubwa kuenea kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania enzi za utawala wao. Mambo yaliyochangia kuenea kwa lugha ya Kiswahili enzi za utawala wa Wajerumani ni pamoja na dini, elimu, shughuli za utawala na shughuli za kiuchumi kama vile kilimo.
Powered by Blogger.