FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA KIAFRIKA MODULE 1; UTANGULIZI FASIHINSIMULIZI YA KISWAHILI
SUALA
LA UTENDAJI KATIKA FASIHI SMULIZI
Katika fasihi simulizi utendaji ni uti wa mgongo
yaani ni suala la msingi.
Mulokozi (1996:24) Fasihi
simulizi ni tukio na linafungamana na matukio ya kijamii na hutawaliwa na
fanani (msanii au mtendaji)
Ø Fanani ni mtendaji au mwasilishaji na
mtunzi wa kipera,fani husika kwa hadhira katika muktadha wa tukio fulani ,kazi
yake yaweza kuwa kichwani au akatunga
papo kwa papo.
Ø Fani inayotendwa au kipera
Ø Hadhira/wasikilizaji,washiriki,wachangiaji
,wahakiki,watazamaji hawa huangalia uzuri au ubaya.
Ø Tukio-ni shughuli yoyote ya kijamii
ambayo ndio muktadha wa utendaji.mfano msiba,ibada,harusi,sherehe,n.k
Ø Mahali –eneo mahsusi ambapo sanaa
hiyo inatendwa.
Ø Wakati na muda maalum au majira
maalum ya utendaji .Vipera vingi vina
wakati wake.mfano Sifo huimbwa wakati wa kuomba.Mwingiliano huu wa vipengele
hivi ndiyo unaoamua fani hiyo iwasilishwe vipi.
OKPEWHO (1992) Anasema
Utendaji unaotofauta kutokana na sababu
mbali mbali kama vile;
Ø Umri wa fanani
Ø Umri wa hadhira
Ø Nguvu ya fanani,baadhi ya vipera
vinahitaji fanani awe na nguvu mfno majigambo
Ø Tukio husika mfano Msiba hauwezi kufanana
na sherehe
Ø Aina ya mandhari au jukwaa maalum la kutendea yaani pale
inapotendewa.
Ø Vifaa ambatani vinavyotumika na
fanani katika utendaji mfano maleba,mkuki
Ø Idadi ya fanani
Pia utendaji unatokana au unatawaliwa na;
Ø Dhima ya kipera( tukio ),muktadha wa
uwasilishaji na namna ya uwasilishaji hutegemea dhima ya kipera katika jamii.
Ø Muda na mahali,ni muhimu kuzingatia kwa kipera chochote
hutegemea au husukumwa na muda na mahali.mfano matambiko yanafanywa muda gani?
Ø Mila na utamaduni ,kila jamii ina
mila na utamaduni wake na hivyo huathiri
utendaji wa vipera husika.mfano Mavazi au maleba maalum ya kisanaa yaani kipera
hiki kinahitaji aina ipi ya maleba?
Ø Sifa za wahusika au watendaji wa
kipera fulani wanapaswa wawe akina nani?
SWALI; JE UTENDAJI NI NINI?
Muluka (1999) anasema Utendaji ni uwasilishaji
wa hadithi au ngano unaofanywa na
msanii kwa hadhira kwa kutumia mdomo na
kuambatana na matendo ya viungo mbalimbali
vya mwili na ishara uso.Hivyo
kila kipera kipo kwaajili ya kutendwa.
UTENDAJI KATIKA VIPERA MBALI MBALI
Finnegan
(1970) ‘’Oral Literature in Africa’’ anasema kuwa katika utendaji kuna kanuni maalum,jamii
nyingi zina utamaduni wake.Hadithi ni utanzu muhimu katika jamii za
kiafrika.Hadithi ni utanzu wa jioni na mtambaji
anazungukwa na hadhira.
SWALI; Je kwanini hadithi inatambwa jioni?
Ø Kwasababu mchana mtambaji anakuwa katika utafutaji
yaani katika shughuli zake za kila siku.
Ø Hadithi ina fomula zake za kuanza na
kumalizia yaani mianzo na miisho maalum ya kihadithi.
Ø Katika kutamba hadithi fanani habanwi kutumia vipera vingine
katika utendaji wake.
Ø Katika kutamba hadithi msimuliaji hatakiwi
kukalili ila anapaswa kuleta upya fulani wa utendaji wa hadithi hiyo.
Ø Mtambaji anapaswa kutumia sauti vizuri na
iendane na utanzu wenyewe.
Ø Kuna wasimuliaji wazuri na wabaya au
wasiowazuri
Ø Msimuliaji awe mbunifu ili kunogesha
hadithi
Ø Katika utendaji msimuliaji aoneshe
hisia zake.
UFALAGUZI
Ni uwezo alionao fanani katika kuunda
kutunga ,kugeuza na kuiwasilisha kazi ya fasihi simulizi papo kwa papo bila ya
kujifunga na muundo asilia au na muundo uliozoeleka. Hivyo katika utendaji wa kipera fulani kuna
utungaji mpya kutokana na mbinu fulani unazotumia.
Ø Hivyo
hadithi moja inaweza simuliwa tofauti na wasimuliaji tofauti.Utendaji wa
kipera hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine.
SIFA ZA FANANI BORA
Senkoro anasema Fanani bora anatakiwa afanye kazi ya ualimu
,awe mtoa maoni,msanii,mburudishaji,muigizaji
Ø Fanani aifanye hadithi ionekane
mpya kila mara anaposimulia.
Ø Fanani aifurahie na kujivunia fani anayoitenda,kuisimulia
ipasavyo.
Ø Fanani awe mbunifu na awe na
kumbukumbu.
Ø Suala la utamaduni katika utendaji
fanani azingatie utamaduni wa kipera
anachotamba.
Ø Fanani awe tajiri wa lugha yaani ajue
kutumia mbinu mbalimbali za lugha
kama vile nahau,semi,n.k.
Ø Fanani asiwe na aibu katika utendaji
atumie vema lugha na viungo mbali mbali.
Ø Kujua mambo ya kihistoria kwani
Fasihi inapitia vipindi mbalimbali.
UTENDAJI WA KIPERA CHA SEMI
1. METHALI
Ni usemi mfupi wa
kimapokeo unaodokeza mafumbo mazito au fikra zinazotokana na uzoefu wa jamii
husika.Katika utendaji unaweza
kutofautiana na vipera vingine kwani utendaji wa methali lazima unajitegemeza
wakati wa kutenda fani nyingine mfano mkutano,maongezi ya kawaida,majadiliano,hadithi,wakati
wa kukanya mtu n.k.
Kimsingi watambaji wa
methali ni watu wazima (wazee) kutokana na kuishi kwao katika jamii kwa muda
mrefu.
2.VITENDAWILI
Utendaji
katika vitendawili si tegemezi kama methali bali kitendawili kinasimama chenyewe kwa kufuata kanuni zilizowekwa na
jamii husika.Mfano katika kabila la wajaluo
ukishindwa kutegua unaombwa mke au mme na katika jamii nyingine unapewa mji.
2. MAJIGAMBO
Katika Jamii ya wahaya ni jamii
ambayo ni maarufu kwa majigambo.Huu ni utafiti wa kitaaluma uliofanywa na Rubanza
(2004) na Method Samwel ,hawa wote wameangalia jamii ya wahaya.
Katika jamii ya wahaya majigambo
yalikuwa na muktadha wake maalum walikuwa wanatamba mbele ya mtemi kabla
ya kwenda vitani au baada ya kurudi toka vitani n.k
Ø Kwa wahaya mjigambi hujigamba mbele ya
watu ,sherehe ambayo inahudhuriwa na mtemi na kuna namna ya kuanza na kumaliza.Mfano wakati wa kuanza mjigambi anaweza kuanza kwa
kujitambulisha kwa kujigamba na anaweza kumalizia kwa shukrani au heshima kwa
mtemi au kiongozi aliyepo pale.
Ø Katika majigambo ,mjigambi yupo huru
kutumia lugha ya kujikweza akiwa amevaa maleba maalumu mfano katika kujigamba mjigambi anavaa kanzu ndefu au nguo za majani
ya migomba na hushika silaha kama vile mkuki ,panga,n.k
Ø Pia majigambo huambatana na ngoma
yenye mapigo ya pekee na maandamano
fulani.
Ø Katika majigambo kuna zawadi,shujaa
aliyeshinda au aliyerudi toka kuwinda ,vitani n.k hupewa zawadi kama pombe.
Ø Wale walioenda vitani au kuwinda wakashindwa zawadi yao
ilikuwa maji ya kunywa na kinyesi cha ng’ombe.Hii ilikuwa inaleta umakini kwani
kurudi na kinyesi ilikuwa ni aibu.
Miaka ya 1960 utendaji katika majigambo uliathiriwa sana kutokana na
mabadiliko ya kijamii na kiutawala