MTIHANI WA KUJIPIMA KIDATO CHA SITA KISWAHILI - 2
MTIHANI
WA KUJIPIMA
KIDATO
CHA SITA
121/2
KISWAHILI - 2
Muda:
Saa 3:00
Maelekezo
1. Karatasi hii ina
maswali kumi (10) katika sehemu A,
B, C, D na E.
2. Jibu maswali matano (5) kwa kuchagua swali moja (1) kutoka kila sehemu.
3. Kila swali lina
alama ishirini (20).
4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.
5. Vikokotozi haviruhusiwi katika chumba cha mtihani.
6. Swali lisilo na namba halitasahihishwa.
SEHEMU A (Alama 20)
FASIHI KWA UJUMLA
1. “Mhakiki
wa kazi za Fasihi Andishi ni mnyonyaji wa mwandishi asilia.” Kubali au kataa
dai hili kwa hoja tano.
2. Fafanua
kwa hoja nne (4) juu ya nadhariya za chimbuko la sanaa na fasihi kwa ujumla.
SEHEMU
B (Alama 20)
USHAIRI
Kimbunga –
Haji Gora Haji
Mapenzi Bora
– Shaaban
Robert
Chungu
Tamu –
Theobald A.
Mvungi
Fungate ya
Uhuru - Mohamed
S. Khatibu
3. “Mshairi
ni mwalimu wa jamii kwani hugusa nyanja zote zinazohusu maendeleo ya jamii.”
Thibitisha kwa hoja tatu toka kila diwani miongoni mwa vitabu viwili
ulivyosoma.
4. Jadili
dhamira ya mapenzi kama inavyojitokeza katika vitabu viwili kati ya
vilivyoorodheshwa hapo juu. Toa hoja tatu kila diwani.
SEHEMU
C (Alama 20)
RIWAYA
Usiku
Utakapokwisha – Mbunda
Msokile
Kufikirika - Shaaban Robert
Mfadhili - Hussein
Tuwa
Vuta N’kuvute - Shafi Adam Shafi
5. “Kuwepo kwa fasihi katika jamii ni tarajio la
kimsingi, inapokosekana jamii hupungukiwa katika ukamilifu wake.” Kwa kutumia
vitabu viwili ulivyosoma kubali au kataa kauli hii ukitoa hoja tatu toka kila
riwaya.
6. Jina
la kitabu husadifu yaliyomo ndani ya kitabu. Thibitisha kauli hii kwa hoja tatu
toka kila kitabu miongoni mwa riwaya mbili ulizosoma.
SEHEMU
D (Alama 20)
TAMTHILIYA
Kwenye
Ukingo wa Thim – Ebrahim
Hussein
Morani – Emmanuel
Mbogo
Kivuli
Kinaishi – Said
Mohamed
Nguzo
Mama – Penina
Muhando
7. Miongoni mwa majukumu ya msanii ni kuzungumzia matatizo mbalimbali yanayoikumba
jamii. Thibitisha kauli hii kwa hoja tatu toka kila kitabu ukitumia tamthiliya
mbili kati ya ulizosoma.
8. Waandishi
wa Tamthiliya kwa kawaida hawatenganishi Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi.
Jadili ukitoa hoja tatu toka kila kitabu miongoni mwa tamthiliya mbili
ulizosoma.
SEHEMU
E (Alama 20)
USANIFU
WA MAANDISHI
9. Soma
shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata:
Soma mtoto wa kike,
soma usitetereke,
Soma usishawishike,
hadi mwishoni ufike,
Soma nyadhifa ushike,
nchi hii utumike,
Soma nakutegemea, soma
mtoto wa kike.
Soma usibabaike,
mafudisho uyashike,
Soma nami nifurahike,
vishawishi uepuke,
Soma kisha utumike,
katu usihangaike,
Soma nakutegemea, soma
mtoto wa kike.
Soma na ufundishike, na
vikwazo uvivuke,
Soma nami niridhikr,
moyo nisisononeke,
Soma kesho unizike,
mahali papa niweke,
Soma nakutegemea, soma
mtoto wa kike.
Soma usirukeruke, bongo
zako zichemke,
Soma yote ukumbuke,
masomo yasiponyoke,
Soma usirubunike,
mwanangu usipotoke,
Soma nakutegemea, soma
mtoto wa kike.
Soma usipaparike, raha
zina muda wake,
Soma nisifesheheke,
wenzangu wasinicheke,
Soma nami nitukuke,
Unasi niheshimike,
Soma nakutegemea, soma
mtoto wa kike.
Soma nisinyanyasike,
wenye wivu watapike,
Soma nami ninyanyuke,
wenzangu wasinicheke,
Soma nisiwe mpweke,
tamati nitamatie,
Soma nakutegemea, soma
mtoto wa kike.
MASWALI:
(a) Kwa
sentensi moja eleza ujumbe anaoutoa mshairi.
(b) Mwandishi
ana maana gani kusema, “…..soma usirubunike, mwanangu……”
(c) Kituo
cha shairi hili ni nini?
(d) Mshairi
asemapo: “Soma nisifedheheke, wenzangu wasinicheke.” Haya maneno yanaelekezwa
kwa nani?
(e) Je,
hili ni shairi la mkabala gani?
10.
Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha eleza mbinu za kifani zilizotumika
kufikisha ujumbe.
Mjomba!
Mjomba! Mjomba angalia kule wale ni wanafunzi wamemzingira mama muuzaji wa
mihogo. Wafanyaje? Hawana jinsi, ni mihogo tu wanayoweza kununua kwa shilingi
mia moja walizopewa na wazazi wao. Ndiyo, ndiyo mjomba hali ni ngumu.
Mjomba
angalia kule unaona njaa, vifo…….kila kitu kimezingira wazazi wa wanafunzi,
maisha kama vita. Kila mtu anapambana. Maisha safari, kila mtu anasafiri.
Mjomba
hali imekuwa mbaya. Watu wanajadiliana kila leo mtaani. Wanajiuliza na kuuliza
maisha maswali magumu.
Watu:
Maisha
wapi unatupeleka?
Maisha:
Hamna
haki ya kuuliza hilo swali.
Watu:
Lakini
tulipoanza safari tulikubaliana kuwa utatupa taarifa ya kila
tuendako.
Maisha:
Nakumbuka
tulikubaliana lakini haki hiyo imefutwa. Haipo tena. Kwa
hiyo, fungeni midomo na mikanda
msonge mbele.
Watu:
Jamani
tumegeukwa! Tumegeukwa! Tunanyanyaswa! Tunaonewa! Tumekwisha!
Mjomba sikia, siku zinakuja na siku
zimefika ambapo mawe yanasema; jamani! Ee tulikuwa tumelala, tumeamka sasa
mtatutambua; Tunakuja, Tusubirini…..
Mjomba unawaona walimu, waangalie wale
pale wameegesha magari yao ya kifahari. Waone wanaondoa magari yao kwa kasi ya
ajabu kurejea nyumbani kwao baada ya kazi. Wanaelekea Masaki, Mikocheni,
Msasani, Mbezi Beach, Kinyerezi. Naam, ndiko wanastahili kuishi. Ndiko kwenye
hadhi yao. CHANZO>>>>>>