Miongozo ya Lugha na Fasihi-LINA UBANI
MIONGOZO ya Lugha na Fasihi ni mfululizo uliokusudiwa
wanafunzi na watpenzi wa lugha na fasihi ya Kiswahili. Mfululizo huu umebuniwa
kutokana na lengo la kuwasaidia wanafunzi wa hjjha na fasihi katika ngazi
mbalimbali za taaluma zao, hasa wale wanaojiandaa kwa mitihani ya Taifa.
Mfululizo huu utatoa vijitabu ambaVyo vitakuwa vinasaidia kuchambua vitabu vya
lugha na fasihi ambavyo vimeteuliwa na Wizara ya Elimu vitumike kuwatahini
wanafunzi katika vyuo na sekondari nchini. Kwa hali hiyo, mfululizo huu
utajumuisha uchambuzi wa vitabu vilivyochapishwa na Dar es Salaam Umvereity
Press (DUP) na vile ambavyo vitakuwa vimechapishwa na mashirika raengine.
Uchambuzi wa kila kitabu utazingatia fani na maudhui
yanayojitokeza katika kazi hiyo, na mwishoni kuna maswali ambayo yanamwongoza
mwanafunzi. Miongozo hii imeandaliwa kwa kuzingatia utaalamu wa hali ya juu ili
kurahisisha usomaji wa kitabu kinachohusika. Wanafunzi na wapenzi wa lugha na
fasihi watafaidika mno na mfululizo huu. Mhariri mwanzilishi wa mfululizo huu
anawatakia usomaji mwema.
Namna ya Kuitumia
Miongozo ya Lugha na Fasihi inaweza kuwa ya manufaa kwa
wanafunzi; lakini pia inaweza kuhatarisha juhudi za welewa kwa baadhi ya
wanafunzi. Miongozo ya aina hii inapasa iwe kichocheo kwa wanafunzi katika
kushiriki hisia na mihemko ya mwandishi iliyoko katika kazi ya fasihi
inayohusika. Kutokana na hoja hii, msomaji anatakiwa aione miongozo hii kama
kitu kinachosaidia kuimarisha stadi na welewa wake na sio kibadala cha
kitabu kinaohohusika.
Wakati wa kusoma miongozo hii mambo muhimu yanayotakiwa
kuzingatiwa nipamoja na haya yafuatayo:
· Kabla ya kusoma mwongozo wowote ule, inampasa mwanafasihi asome kwanza kazi ya fasihi inayohusika.· Kilichoandikwa katika mwongozo wowote kisichukuliwe kuwa ni sawa na maandiko matakatifu kama vile Quran Tukufu na Biblia Takatifu. Msomaji una nafasi ya kukubali au kukataa maoni yaliyomo katika mwongozo unaohusika.· Msomaji una nafasi ya kutoa uchambuzi na uhakiki mpana zaidi kuhusu kitabu kilichohakikiwa.· Msomaji ihusishe kazi ya fasihi na mazingira ambamo watu walioandikiwa wanayaishi. Jifanye kama yanakukuta utayatatuajie?
Mwishoni mwa mwongozo wowote kuna maswali ambayo yanasaidia
kupanua welewa zaidi kwa mwanafunzi na msomaji wa kawaida. Msomaji aghalabu yuko
huru kujadili kwa mapana zaidi kazi inayohusika.
I Mwandishi
Penina Muhando ni Profesa na Afisa Mkuu Taaluma wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam. Mchango wake katika fasihi na taaluma ya Kiswahili ni mkubwa
- hasa kwa upande watamthiliya.
Katika tamthiliya, 'mwandishi huyo amepata kutunga Hatia
(EAPH), Tambueni Haki Zetu (EAPH), Pambo (F. Books), Nguzo
Mama (DUP), Harakati za Ukombozi (na wenzake) (TPH) na huu wa Lina
Ubani (DUP). Kazi zote hizo zinajishughulisha sana na maisha ya watanzania
kwa ujumla; kuanzia enzi za ukoloni hadi kipindi tulichonacho. Aidha, Lina
Vbani ni tamthiliya inayoangalia matatizo yanayomkabili mtanzania wa leo
kama tutakavyoangalia katika uchambuzi/uhakiki ufuatao.
II Dhamira Kuu
Maudhui ya Lina Ubani yanaweza kuangaliwa katika nyanja
mbali mbali za maisha ya jamii ya kitanzania. Maudhui hayo yanazungukia dhamira
muhimu ya ujenzi wa jamii tnpya, artbamo ndani mwake kuna vidhamira vingine
vidogo vidogo. Tutazichambua dhamira hizo hapo ehini.
III Maelezo ya Awali na Dhamira Zenyewe
Kwa kipindi cha 'miaka kadhaa nchi ya Tanzania imekumbwa na
msukosuko wa kiuchumi. Kuyumba huko kunatokana na hali halisi kwamba bidhaa zake
zimekuwa zile ambazo hupangiwa bei kutoka kwa wanunuzi wake ambao ni mataifa
makubwa ya dunia ya kwanza.
Pamoja na hali hiyo, nchi ya Tanzania yenyewe ilipopata uhuru
ilidhamiria kujengajamii nlpya anlbayo itakuwa na uhuruwa kweli, haki kwa watu
wake, usawa wa binadamu, uchumi kuwa mikononi mwa umma na mengineyo ya aina
hiyo. Hali hiyo ilianza kutekelezwa, lakini haikufikia hali nzuri kabisa. Hii
ilitokana na kutotekelezwa kwa misingi thabiti iliyotangazwa katika “Azimio
la Arusha” ambalo lilikusudiwa lirekebishe hali mbaya iliyokuwepo nchini.
Kama kwamba hili halikutosha, hali iliongezewa uduni baada ya nchi hii kushiriki
katika vita vya kumng'oa Idi Amini aliyekuwa ameivamia. Tamthiliya ya Lina
Ubani inaisimulia vita hiyo kwa kutumia mbinu za kifasihi simulizi na za
kisasa, kwani mwandishi anatumia masimulizi ya ngano kuhuSu dude lililowavamia
ndege na wanyama katika makazi yao msituni. Baada ya kuvamiwa na dude liitwalo
Dyamini, ndege na wanyama hawa walikimbilia kijiji cha jirarii walikowakuta
binadamu, nao wakawapokea vizuri. Baadaye binadamu na ndege na wanyama
wanashirikiana kupambana na kumfukuza Dyamini, lakini kwa sadaka kubwa ya
uchumi na niaisha ya watu. Tunaweza kuchambua mambo yanayojitokeza katika
tainthiliya hiyo kania ifuatavyo:
(a) Dhana ya Ukale na Usasa
Tamthiliya hii inatumia mbinu za aina mbili katika usimulizi
wake. Kwanza, mwandishi anamtumia mhusica Bibi, ambaye hutamba hadithi ya
Dynamini kwa mtoto Mota - ambaye ni mjukuu wake. Kwa kutamba hadithi, mwandishi
ameonyesha, mbinu za kifasihi simulizi (ukale), na hivyo kufanya kwa mara ya
kwanza pawcpo na jaribio la matumizi ya mbinu za kifasihi simulizi naza kisasa
katika tamthiliya moja. Mhusika Bibi anaonyesha dhana yake ya ukale katika
masuala mbalimbali; yakiwemo:
(i) Suala la Ndoa
Bibi anasema kwamba suala la kuoa bila kufuata ushauri wa wazazi na mababu ni kosa. Mashauri na maelekezo ya wakongwe ni kuwa wanamchagulia mchumba kijana wao, na mara zote wanakuwa wa kabila moja. Bibi analaumu kuwa mtoto wake Huila hakumsikiliza alipomchagulia mchumba na kujiamulia kuoa mwanamke wa Kichusa. Kwa maono ya Bibi, mwanatnke huyu hafai, na mkatili kwa kila hali. Jambo la mtu kujiamulia kuoa anavyopenda linakiuka matakwa ya wazazi katika kabila la Bibi.
(ii) Chakula na Neema Nyingine
Bibi anaonyesha pia kuwa neema ya chakula ilikuwa hapo zamani; siyo sasa ambapo anaona mambo yamebadilika. Bibi anamwelezea mjukuu wake Mota kuhusu kijijini kwao Malolo; kabla ya kuhujumiwa na mwanamke Lijino....mwanamke yule katufanya kitendo. Wenyewe tulistarehe kule kwetu Malolo. Chakula kila aina. Wewe ulikuwa mdogo sana mlipokuja na mama yako, Malolo, Ndizi! Viazi!! Miwa! mmoja humalizi (uk. 17).
Yawezekana lawama nyingine za Bibi kuhusu chakula kwa Huila na
Sara zinatokana na imani ya hali ya maisha aliyoizoea ya kijijini na siyo ile ya
mjini.
(iii) Elimu ya Zamani
Bibi anaona pia hapo zamani mambo yalikuwa mazuri kwa upande wa elimu. Watoto wake, akiwa Daudi na Huila, walipokuwa wakisoma zamani walikuwa wanaimba na kufurahi sana, siyo kama hawa wa sasa, akina Mota. Nyimbo za sasa, Bibi anazionani kelele tu zisizo na msingi. Anaziona shule za siku hizi kuwa duni, kwani zimejaa kelele za ujamaa! ujamaa! tu.
(iv) Mabadiliko ya Kihistoria
Katika hali isiyo ya kawaida tunamwona Bibi akiulizia mabadiliko ya jamii; jambo ambalo katika hali ya kawaida ya ukale wa Bibi tusingelitegemea, Katikatamko hilitunamsikia akisema:
...niambiebasi. Zamani sanaulikuwepo utumwa - nasikia walikuwa wanapita kijijini kwetu wanapelekwa pwani. Utumwaukaisha. Ukaja ukoloni, wazungu wakaja kukaa pale kwetu. Halafu ukoloni ukaisha wazungu wakahama. Halafu ukaja uhuru, wakaondoka machifu. Babu Wa baba yako, huyo Daudi akaambiwa yeye si chifu tena. Halafu Uhuru ukaisha. Halafu ndiyo tukasikia Ujamaa! Ujamaa! Huuujamaa Mwalimu anasema utakwisha lini (uk. 27).
Mawazo ya Bibi katika dondoo hili yanaonyesha anatambua nguvu za
mabadiliko katika jamii. Lakini pamoja na kutambua mabadiliko hayo, inaelekea
Bibi huyo amechanganyikiwa, kwani kuna mawazo ya kukubali mabadiliko na kuna
mawazo yanayopinga mabadiliko ya jamii kama tulivyokwishadokeza.
(v) Fasihi Simulizi
Jambo jingine linalojitokeza ni lile linalohusu Fasihi Simulizi na imani za utambaji wake. Kuna imani miongoni mwa jamii mbalimbali kuwa utambaji wa hadithi unafanywa usiku na siyo mchana. Jamii hizo zilisisitiza jambo hili kufanyika usiku badala ya mchana kwa sababu muda wa mchana watu walilazimika kujishughulisha na kazi kama vile kilimo na usiku wakati wa mapumziko watambe hadithi. Dhana hii inajitokeza pia katika tamthiliya hiyo.
(b) Ukombozi wa Jamii
Dhamira hii muhimu inajadiliwa pia na mwandishi katika
tamthiliya hii. Ukombozi huo tunaweza kuujadili kwa kuzingatia hatua mbili;
kwanza, kwa kutumia ngano ya Dynamini aliyeivamia Tanzania, kuna mapambano ya
kumwondoa adui huyo. Pili, kuna ukombozi wa Watanzania wenyewe na sualala
kuijenga jamii mpya.
(i) Mapambano ya Kumwondoa Mvamizi
Ingawa katika ngano inayojadiliwa, Dyamini ndiye dude vamizi,
lakini katika hali halisi, Idi Amini ndiye aliyeivamia Tanzania mwaka 1978.
Uvamizi huo wa Amini ulifanywa kwa madai kwamba alikuwa akiwasaka wapinzani
“Guerrillas” ambao ilidaiwa walitokea Tanzania. Baada ya uvamizi huo
wa Amini, kulifuatiwa na mapambano makali yaliyofanywa kwa hatua.
- Hatua ya Kwanza
Hii ilihusu kupambana ili kupata nafasi ya kujenga daraja ya
Kyaka katika mto Nile upya. Baada ya ujenzi huo wa daraja, kulikuwa na kuvuka
kwa majeshi na vifaa vya kivita.
- Hatua ya Pili
Kupambana ili kumwondoa kabisa Idi Amini kutoka ardhi ya
Tanzania. Hii ilifanyika kwa muda usiopungua majuma mawili.
- Hatua ya Tatu
Mapigano kuhamia Uganda. Haya yalidumu hadi kukombolewa kwa
Uganda na Amini kukimbia kabisa.
Pamoja na kuikimbia Uganda, na pamoja na kuwa Tanzania ilikuwa
imeshinda vita, kulikuwa na madhara ambayo yalitokana na vita hiyo.
- Upotevu wa Maisha ya Watu
Kulikuwa na vifo vya watu wengi, askari nawananchi.
Kulikuwanawengi waliopata vilema vya maisha.'Katika tamthiliya hii tunaambiwa
kuwa Daudi, mtoto wa Bibi alikufa vitani, kitendo ambacho yaelekea kiliwehusha
akili yake.
- Kutetereka kwa Uchumi
Uchumi wa Tanzania ulitetereka kwa kiasi kikubwa. Inasemekana
vita hiyo ilikuwa inatumia T.Shs.7,000,000.00 kwa siku moja na hivyo kudhoofisha
kabisa uchumi wa Tanzania ambao ulikuwa tayari umeanza kuimarika kwa wakati huo.
Aidha, tatizo la uchumi nchini linatokana pia na hali ya uchumi duniani.
- Wizi wa Fedha za Umma
Kuna methali inayosema “Kufa Kufaana!” Vita hivyo
vimeleta tabia ya wizi kwa baadhi ya maofisa wajeshi na hata wa kawaida.
Kwaupandewa maofisawajeshi, baadhi yaowalikuwaamawanaiba fedha,
au wanazitumia vibaya fedha walizokuwa wamepewa kwa ajili ya vita.
Pensheni ya wanajeshi waliofia vitani kama vile Daudi wa
tamthiliya haikuwafikia, wamekula “wakubwa”. Waliopoteza viungo vyao
wakati wa mapigano pia hawakulipwa.
Maofisini, watu mbalimbali walikuwa wameiba fedha kwa kisingizio
cha vita.
Kuliibuka matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi na kila tatizo
ilisemwa ni kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi iliyokuwa imetokana na vita vya
kumwondoa Amini. Kimsingi, hivyo vilikuwa visingizio tu. Kutokana na hali
ilivyokuwa, kuna baadhi ya watu wanaona ni afadhali kama Tanzania isingeingia
vitani - kwani imeleta hasara zaidi kuliko faida. Lakini Amini angekaa hapa hadi
lini?
(ii) Ujemi wa Jamii Mpya
Dhamira hii imekuwa ikijitokeza katika kazi nyingi za kifasihi
toka kutangazwa kwa “Azimio la Arusha” ambalo ndilo lilikuwa nguzo ya
ujenzi wa jarnii mpya iliyokusudiwa. Jamii mpya kimsingi ilipasa kuzingatia
mambo kama vile usawa wa binadamu, haki miongoni mwa watu wajamii,
uongozi safi, niakazi bora na chakula cha kutosha. Mwandishi wa
tamthiliya ya Lina Ubani amechambua matendo ya wanajumuia na kuyatafiti
kwa undani.
- Suala la Haki
Mwandishi anaiona jamii kukosa kuWatendea haki watu kama
wanavyostahili. Katika kuilalamikia jamii, mwandishi anatumia mifano mbalimbali,
lakini ya msingi hii inayotajwa hapa chini:
I. Kuhamia Vijijini
Miaka ya 1970...; Tanzania iliamua kuwahamishia watu katika
vijiji vya maefndeleo. Mipango ya kuwahamishia watu katika vijiji haikutekelezwa
vyema. Watu walihamishwa kutoka sehemu nzuri na kuwekwa nyikani kama mhusika
Bibi anavyosema; na kulalamikia uamuzi wa Lijino hivi:
Basi kaja huyo Lijino huyo! Mfflh! Mwanamke yule! Nasikia ana watoto lakini utafikiri hakuzaa. Mtahama! Amri moja! Kwa hiyari mmekataa. Sasa amri moja. Mmh! Basi kwenda kutuweka nyikani....Huu ni mfano mmoja wa kunyimwa haki kwa bitiadamu.
II. Kunyimwa Vitu/Vyeo Wasomi
Jambo jingine muhitnu linaloonyesha kukosekana kwa haki kwa watu
m kule kuwapa vyeo wasiosoma, na wasomi kuwatUmikia wasiosoma. Imeelezwa kuwa
wale waliosoma wanakosa hata gari la kutembelea wakati wale wasibsoma ndio wenye
kustarehe. Tazama Bibi anavyosema kuhusu suala hilo:
.... Kumbe vyeo wanakuja kupata wasiosoma. Baba yako kasoma, kasoma miaka na miaka. Sasa mie namuuliza, 'hivyo mwanangu kusoma kote kule hata gari unashindwa kununua?' Akaniambia eti magari hayaruhusiwi. Mbona barabarani yamejaa?. Eti hayo ni ya wakubwa. Hao wasiosoma hao! Ningejua wanangu wasingesoma. Wamesoma nimepata faida gani? (uk. 33 - 34).
Mwandishi anaichambua jamii ya Tanzania katika uhalisi wakc. Kwa
muda mrefu sasa watu ambao elimu yao si ya juu sana, au hata wale wasiosoma
kabisa, wamekuwa ndio wanaoteuliwa kuwa viongozi. Wamekuwa wakitembelea magari,
na wameruhusiwa kununua magari. Hali hii imekuwa ikikatisha tamaa watu wengi, na
hivyo wakati mwinginp kuathiri utendaji kazi wa wasomi mbalimbali.
Katika utendaji kazi, tumeona kuwa wakati mwingine kumekuwa na
chuki kati ya wasomi na wasiosoma, na kwa sababu hii; wasiosoma wamekataa
kushauriwa nawasomi. Mfano mzuri hapa niwa Zoersi na Huila.
Huila ni mtaalamu na ni msomi wa kiwango chajuu. Kila mara
amekuwa akijitahidi kutoa ushauri kwa mwanasiasa mashuhuri, lakini aliyekosa
busara na welewa Bwana Zoeni. Zoeni, kama zilivyo tabia za baadhi ya wanasiasa,
amekuwa akidharau kabisa mawazo ya mtaalamu Huila. Kisingizio kikubwa cha Zoeni
ni kuwa SERA ya CHAMA haiwezi kujadiliwa na wataalamu. Matokeo ya dharau ya watu
wa aina hii ni kuanguka kwa uchumi wa nchi na kufanya mikataba ya kuifilisi
nchi. Iko mifano kadhaa katika tamthiliya hiyo.
- Zoeni anagongana kimawazo na Huila wakati anapotoa ushauri wa
kitaalamu. Zoeni anaona Huila anamfundisha kazi, na hivyc anamfokea:
...sihitaji ushauri wako. Kazi yako ni kutekeleza. Sera siyo kazi yako. Ondoka ofisini kwangu... (uk. 25).
- Zoeni anafanya mikataba kwa niaba ya nchi ambayo inahatarisha
kabisa uchumi wa nchi. Kwa mfano kuna mikataba inayohusu nishati katika nchi
nzima. Kwa sababu ya kutokuwa na upeo mkubwa vva kitaalamu, tunaambiwa Zoeni
aliwekeana mikataba na nchi zilizoendei 'a ili kupata mitambo ya nuklia ambayo
haikutakiwa kwa wakati huo nchini. Zoeni anamkebehi mtaalamu na kumdharau, kwa
mfano anasema;
.... Tujadili sera? Unazungumza nini bwana mtaalamu? Sera inajadiliwa?.... Ulipokuwa unasomea huo utaalamu hawakukufundisha kuva sera ikishapitishwa haijadiliwi?.... Ninyiwataalamukwaninimnapendakuchezeaakilizawatu. Pesa zote tunapoteza kusomesha watu, utaalamu wenyewe ndiyo huu... (uk. 24 - 25).
Iko pia miradi mbalimbali inayotekelezwa bila mpango maalumu
kama vile kuanzishwa kwa “windmills” katika kila kijiji (jambo
ambalo haliwezekani), kushughulikia mti wa 'Hanga' unaotoa mafuta ambao Zoeni
amepata habari kuwa Philippines kuna mti huo ambao yawezekana upo pia nchini.
Bila kufanya tathmini, inaamriwa rnradi uanze mara moja! Hili ni jambo la hatari
na linaonyesha hali halisi ambayo imekuwa ikitokea nchini. Miradi mingi
imeanzishwa na kufa bila mafanikio kutokana na kutosikiliza maoni na ushauri wa
wataalamu wetu. Muda umefika wa kubadilisha hali hii.
- Suala la Makazi Bora
Jamii ya Tanzania ilikusudia kujenga makazi bora kwa wananchi
wake, hasa baada ya kutangazwa kwa “Azimio la Arusha”. Ingawa wazo
lilikuwa zuri, utekelezaji wake haukuridhisha kwa kiwango kikubwa. Yaelekea
vyombo vya dola vilitumia vibaya madaraka yake na hivyo kuwatesa wananchi bila
sababu za msingi. Kuna watu waliobomolewa nyumba zao eti kwa sababu zilikuwa nje
ya kiwanja kilichopimwa, lakini ilikuwa katika eneo lililotakiwa; kama Bibi
anavyolalamika:
...Mh! Tuna taabu. Huyo Kibwana Kata! Mmh! Shoga yangu Mama Senga nyumba yake maskini: 'Bomoa! Haiko kwenye kiwanja'. Tumetutika maji sie! Tukasema: hela Senga kaleta, maji tutashindwa kuteka nyumba ijengwe? Hata! Basi kila kukicha ndoo kichwani. Halafu Kibwana Kata anakuja: 'Bomoa!' Tukadhani anatania. Wakabomoa... (uk.12)
Hali hii inaonyesha kwamba watu wengi waliathiriwa na
“Operesheni Vijiji” ya miaka ya mapema ya sabini. Wananchi wengi
waliteseka. Kuonyesha kwamba kulikuwa na utekelezaji mbaya wa Operesheni hiyo
hivi sasa baadhi ya watu waliohamishwa wakati huo wameruhusiwa kurudi kwenye
vijiji vyao vya zamani.
- Mipango Mibaya ya Maendeleo
Tumeidokeza dhamira hii pale awali. Lakini pengine hapa
tungezungumzia tatizo la mipango mibaya ya maendeleo na utekelezaji wake. Mfano
wa maelezo ya jambo hili nl ule wa Talafa aliyegeuzwa shingo “uso ukawa
nyuma”. Inasemekana aliwalazimisha wananchi walime pamba ambayo
haikuchukuliwa/kununuliwa na serikali kwa vile hapakuwa na daraja la mto
uliokitenga kijiji hicho. Mwaka uliofuata inasemekana wananchi waliamua kulima
fiwi badala ya pamba. Jambo hili linaonyesha pia mpango mbaya wa utekelezaji wa
sera za kiuchumi nchini na kusema kweli matukio ya aina hii nimengimno.
Kuna Ubani
Huo wote ni mvundo ambao si sawa na ule wa “La kuvunda
halina ubani”, bali “La kuvunda lina ubani!” Hakuna tatizo hata
moja kati ya yaliyosemwa ambayo hayawezi kutatuliwa. Kuna ubani.... Matatizo
haya yana dawa. Ni suala la kuamua tu. Mifano michache imeanza kuonekana katika
baadhi ya taasisi zetu: Kwa mfano, hivi sasa Waziri wa Mambo ya Ndani
anajitahidi kuisafisha jamii. Rais na Waziri Mkuu wamemwunga mkono. Ili
kufanikisha jambo hili, ni lazima watanzania wote tumwunge au tuunge
mkono juhudi hizo za kuleta “ubani” utakaoondoa “mvundo”
kama vile uzembe, wizi, uvivu na ufujaji wa mali ya umma na pia unyimaji wa haki
kwa watu.
(c) Dhamira Nyingine
Pamoja na dhamira hizo tulizoziona, kuna dhamira kadhaa ambazo
ingefaa zijadiliwe hapa. Tuziangalie dhamira hizo.
(i) Imani ya Ushirikina na Uchawi
Jamii nyingi zina imani hizo za uchawi na ushirikina. Nchini
Tanzania imani hizo pia zipo; na kimsingi zilipata kujitokeza wakati wa
“Operesheni Vijiji” ambapo inasemekana baadhi ya watendaji wake
walikumbana na matatizo mengi. Uchawi na ushirikina wakati mwingine vimetumika
kama nguzo ya wanyonge ya kujitetea dhidi ya tabaka tawala. Hatuna ushahidi wa
kufanikiwa kwake, lakini kuendelea kutumiwa kama nguzo na baadhi ya jamii ni
dalili kuwa huenda kuna mafanikio.
Katika tamthiliya ya Lina Ubani tunaambiwa kuwa Talafa
aliyekuwa msumbufu kwa wanakijiji walioktiwa wamelima fiwi badala ya pamba
aligeuzwa shingo, uso umetazama mgongoni! Jambo hili ni la kutisha. Linaweza
kubadilisha nia ya afisa yeyote mtendaji ambaye atakwenda kijijini hapo.
(ii) Elimu na Nafasi Yake
Tumetaja hapo awali kuwa Bibi alisifia elimu ya zamani. Lakini
hakujadili mchango ama nafasi yake katikajamii.
Tamthiliya hii inaonyesha umuhimu wa elimu katika jamii na
hasara zinazoweza kutokea kama elimu haithaminiwi. Kutothaminiwa kwa wasomi wetu
kunaweza kuleta madhara makubwa.
Elimu ya jadi pia imedokezwa kwa namna fulani katika tamthiliya
hii. Elimu hii inatolewa kwa kizazi kipya kupitia hadithi kama vile Bibi
anavyofanya kwa Mota. Elimu zote zinaweza kuwa za manufaa katika jamii
zikitumiwa vyema.
(iii) Nafasi ya Mwanamke katika Jamii
Mwanamke katika tamthiliya hii ana nafasi za msingi mbili:
mwanamke mzazi na mwanamke mfanyakazi.
- Mwanamke Mzazi
Mwanamke katika kipengele hiki amejengwa akiwa na nafasi yake
kama mama watoto. Hapa tunawaona akina mama wawili: Sara akiwa na mtoto wake
Mota. Pili kuna Bibi ambaye ana watoto Daudi na Huila. Seti mbili za akina mama
na watoto hao zinakamilishwa kwa dhana muhimu ya malezi. Mama,
inakubalika na kueleweka kuwa ni mwalimu wa kwanza wa mtoto. Kwa hiyo nafasi
yake kama mlezi ni muhimu sana katikajamii. Malezi mema huzaa chema. Malezi
mabaya huzaa kibaya. Tumeonyeshwa katika tamthiliya hii mbinu na watu mbalimbali
walio muhimu katika malezi, msingi wa kwanza akiwa ni mama.
- Mwanamke Mfanyakazi
Mwanamke huyu ni msomi. Hapa tuna mfano wa Sara na Lijino.
Hakuna tatizo kubwa linalojitokeza kwa Sara, lakini tunaambiwa na Bibi juu ya
mwanamke Lijino kuwa alikuwa mkatili, kama kwamba hakuzaa. Usemi huu
unasisitiza ukatili wa Lijino.
Kutokana na hali hii, tunaweza kusema kuwa tabia haitegemei
jinsi-nafsi. Mwanamke ana uwezo sawa tu na mwanaume kama akipewa nafasi
inavyotakiwa.
(iv) Mjadala Kuhusu Ushairi
Suala la ushairi wa vina na mizani (kimapokeo) na
ule wa masivina linaelekea kujitokeza katika tamthiliya hii. Mota katika
tamthiliya hiyo anatunga “ngonjera” ambayo “haina” vina na
mizani.
Katika ngonjera yake anawakashifu Madyamini ambao yeye anawaona
wako hata sasa:...hapa hapa shuleni, kama yulefulani anakaa deski la mbele,
kachukua machungwa ya wenzake... (uk. 55). Hapa dhana ya Madyamini
imepanuliwa na kuwa wabaya wote.
(v) Ulevi na Ukweli wa Maisha
Mwanahego ni mtu aliyechorwa kuwa ni mlevi ambaye anaonekana
kuwa na akili zake zenye ukweli mtupu. Maneno anayoyasema Mwanahego si ya mlevi,
bali ni mtu ambaye ameamua kuserna ukweli, lakini baada ya kujifanya mlevi. Kwa
upande mwingine, tukubaliane na hali hii ya ulevi, je, Mwanahego anaelewa juu ya
suala la umoja? Anaelewa umuhimu wa fedha za kigeni? Kuna utata.
Ni vyema kuelewa kwamba mlevi mara nyingi hakumbuki
anayosema. Mlevi ni tofauti na mnywaji. Tunafikiri Mwanahego ni kipaza sauti cha
mwandishi ambaye amedhamiria kuihakiki jamii yake.
Mwisho, tunaweza kusema kuwa hizo ni baadhi tu ya dhamira za
Lina Ubani. Wasomaji wana nafasi ya kufanya utafiti zaidi na kugundua
dhamira zaidi.
IV Vipengele vya Fani
Fani na maudhui ni pande mbili za sarafu moja. Lazima vitu hivyo
viangaliwe katika mchangamano. Lakini hapa tumetenganisha kwa ajili ya
majadiliano tu. Majadiliano yatazingatia muundo na mtindo, ujenzi wa wahusika,
mazingira au mandhari, na hatimaye matumizi ya lugha.
(a) Muundo na Mtimdo
Tamthiliya hii inatumia mbinu za aina mbili za kimuundo. Mbinu
hizo ni za kifasihi simulizi na zile za kidrama ambazo ndizo wasanii wengi wa
tamthiliya huzitumia hivi sasa.
Katika kuineemesha, mwandishi anatumia (viingizi vya) nyimbo na
maombolezo, ambavyo au huletwa na watambaji wanaounda sehemu ya wahusika na
wahusika wengine kama vile Bibi.
Kimtindo, tamthiliya hii inatumia masimulizi ya ngano
katika kuelezea ukweli wa namna fulani wa kifasihi. Aidha, kuna mbinu za kisasa
za kidrama pia. Hali hii huunda michezo miwili katika mmoja.
Wachezaji muhimu wa mchezo ule wa kifasihi simulizi ni Bibi na
Mota, wakisaidiwa na watambaji. Wale wanaotumika katika mchezo wa kidrama ambao
ni wa kisasa ni pamoja na Zoeni, Huila na wale watu wa mataifa ya kigeni.
Michezo yote miwili huenda sambamba na kuunganishwa na
watambaji. Watambaji katika tamthiliya hii ni muhimu kwani wao wanasaidia
kupambanua zaidi dhana muhimu ya ukale na usasa.
Maombolezo katika tamthiliya hii yanaletwa na Bibi (ambaye kwa
kweli kwa namna fulani analeta kero). Maombolezo hayo ni mengi, na tunadiriki
kusema kuwa hii ni tamthiliya ya kwanza ya aina yake. Haijawahi kutokea
tamthiliya ya aina hii, na Profesa Muhando anastahili pongezi.
Suala la matumizi ya nyimbo na ngoma limejitokeza katika
tamthiliya hiyo. Wasomaji hufurahia kuisoma lakini wakati huo huo kuwa makini
katika kutoa uhakiki wake.
(b) Wahusika
Kama tulivyodokeza sehemu nyingine hapo awali, wahusika ni watu,
wanyama, vitu na mahali. Vitu hivi pamoja na viumbe hai vinaweza kutumika katika
kazi ya fasihi kwa pamoja, au vinaweza visitumike vyote kwa mara moja. Hapa
tutachambua wahusika muhimu tu - wakiwemo Mtambaji, Bibi, Huila, Zoeni, Mota,
Daudi, Mwanahego, Lijino, Dyamini na wengineo.
(i) Bibi
Miongoni mwa wahusika muhimu wa tamthiliya hii ni Bibi. Kupitia
Bibi, mwandishi anatoa dhamira mbalimbali ambazo zinaihusu jamii nzima. Bibi
mwenyewe aghalabu anaonyesha tabia za aina yake pia.
- Ni mlalamishi. Ana uchungu wa kufiwa na mtoto wake kipenzi
Daudi.
- Kiungo muhimu katika dhamira ya ukale na usasa.
Msisitizo wake wa kutaka mtoto wake achaguliwe mchumba wa kabila lake, kusifia
kwa nyimbo za zamani, kutamba hadithi ni miongoni mwa vitu vinavyothibitisha
dhana ya ukale na usasa.
- Amechanganyikiwa. Tabia zake katika hadithi ya
tamthiliya hii inashindwa kueleweka. Je, ni nini hicho anachodai kiteremke toka,
mawinguni? Kuna nyakati tunafikiri labda ni utawala/viongozi u(wa)lio juu na
wanalazimishwa kuteremka. Aidha, kuna wakati inajionyesha tabiayawehu.
- Ni mtu asiye na shukrani.
Haridhiki kwa huduma anayopewa na mke wa Huila. Hampendi Sara - anamwita mchawi.
Haridhiki kwa huduma anayopewa na mke wa Huila. Hampendi Sara - anamwita mchawi.
- Ili kuonyesha uzee wake, Bibi amepewa sifa zote za kizee.
- Mhakiki muhimu wa jamii, kwani anazungumzia matatizo ya
kuhamia vijijini yaliyotokana na utekelezaji mbaya, matatizo ya ndoa za mseto wa
makabila na kadhalika.
(ii) Zoeni
Huyu ni mwanasiasa ambaye kimsingi amepewa tabia nyingi
zinazoudhi. Tabia hizo ni kama zifuatazo:
- Ana dharau na hajasoma elimu ya kisasa. Haambiliki.
- Ana kiburi. Yeye ni mhusika muhimu ambaye anakuwa nguzo ya
mchezo katika tamthiliya hiyo yenye mbinu za kidrama.
- Mwanasiasa asiye makini. Hajali utaalamu wa wasomi kama vile
Huila.
- Ni mpenda rushwa na hongo. Aidha, ni mzembe! Hali hii
inajitokeza wakati anapokwenda mkutanoni kuiwakilisha nchi naye analala katika
chumba cha mkutano.
- Ni mbadhirifu wa mali ya umma kwa shughuli zake za binafei.
- Hana adabu kwa wafanyakazi wengine. Anawatukana na kuwaaibisha
mbelezawatu.
(iii) Huila
Tofauti na mhusika kama Zoeni, Huila ni msomi, ambaye ana tabia
zifuatazo:
- Ni mtulivu namvumilivu mkubwa.
- Nimchapa kazi, na ana juhudi kubwa.
- Hakatitamaa upesi.
- Ni mtetezi wahakiza binadamu.
- Ana ushirikiano mkubwanawafanyakaziwenzake.
- Anajalifamilia yake wakati wote.
- Nimchapa kazi, na ana juhudi kubwa.
- Hakatitamaa upesi.
- Ni mtetezi wahakiza binadamu.
- Ana ushirikiano mkubwanawafanyakaziwenzake.
- Anajalifamilia yake wakati wote.
(iv) Mwanahego
Miongoni mwa wahusika airibao wamechprwa kuwa wazembe, lakini ni
muhimu sanani Mwanahego.
- Ni msema ukweli
- Nimcheshi
- Anawahakiki viongozi wazembe katika J'amii.
- Nimcheshi
- Anawahakiki viongozi wazembe katika J'amii.
(v) Sara
Ni mke wa Huila. Anamsaidia sana mume wake katikakumfariji
anapokuwa namatatizo.
(vi) Mota
Huyu ni mtoto wa Huila na Sara. Anakuwa kiungo muhimu cha
rtiaelezo kuhusu malezi ya kizazi kipya.
- Mota anatumika kuelezea migogoro kati ya ushairi wa mapokeo na
masivina.
- Ni mwelezaji wa hali ya ubaya miongoni mwa watu: Kwamba kila
mahali kuna wabaya (Madyamini).
- Ni msikivu. Ni mtulivu. Ana akili bora.
(vii) Daudi
Kakake Huila ambaye alifia vitani; wakati wa kumfukuza Dyamini.
(viii) Dyamini
- Mvamizi.
(ix) Watambaji
Wanaisimulia hadithi na kuiunga kati ya hadithi ya
kingano na ile ya kisasa.
(x) Wahusika wengine
Lijino, Katibu Kata, Katibu Tarafa na wengine wanasiasa.
(c) Mazingira/Mandhari
Mazingira ya tamthiliya hii ni ya kitanzania. Ni mazingira ya
baada ya Azimio la Arusha na vita ya kumwondoa Idi Amini. Japokuwa hadithi
(sehemu kubwa) inasimuliwa kingano, hadithi hiyo inaihusu Tanzania.
(d) Matumizi ya Lugha
Lugha ni chombo cha mawasiliano miongoni mwa jamii. Matumizi ya
lugha hutofautisha kazi - kazi ya kisanaa na isiyo ya kisanaa.
Katika tamthiliya hiyo, mwandishi ametumia lugha vyema katika
kuwajenga wahusika wake. Tuchambue matumizi yake.
(i) Lugha ya Kikabila
Mwandishi amemjenga mhusika muhimu sana, Bibi, kwa kutumia lugha
za aina mbili: lugha ya Kiswahili fasaha na lugha ya kikabila - Kikaguru. Jambo
hili limesaidia kwa namna moja katika kuumba hali halisi aliyokuwa nayo Bibi.
Lakini pia, tahadhari ni kuwa baadhi ya mambo ambayo hayakutafsiriwa kwa
Kiswahili yatashindwa kufikisha ujumbe ipasavyo.
(ii) Lugha za Kigeni
Yako matumizi ya lugha za kigeni, zikiwemo Kifaransa,
Kiingereza, Kijerumani n.k. katika kuwajenga wahusika wanaohudhuria mkutano wa
kimataifa. Hali hii inaweka mazingira ya tamthiliya iwe karibu na uhalisia wa
mambo yanayozungumzwa.
(iii) Kiswahili Fasaha
Lugha hii imetumiwa na msanii pia. Pamoja na lugha hii, kuna pia
matumizi ya lugha iliyo sanifu.
(iv) Matumizi yu Methali, Misemo na Nahau,
Mwandishi ametumia misemo na nahau, pamoja na methali pia katika
kuimarisha kazi hii. Angalia kwa mfano;
- Penye wema(...) ubaya huzengea (uk. 36)
- La kuvunda lina ubani (uk. 58).
- La kuvunda lina ubani (uk. 58).
(v) Tamathali za usemi.
Mwandishi ametumia tamathali mbalimbali za usemi. Tamathali hizo
ni pamoja na sitiari, tamathali ambayo hulinganisha mambo/vitu viwili au
zaidi vyenye sifa tofauti, lakini haitumii maneno ya viungo kama
tashbiha. Mfano wasifa tofauti ni huu ambao ni kilio cha Bibi.
“Aliyeua Daudi (Kaua jembe langu)”
.........
(Kaua kuni zangu)
.........
(Kaua nguozangu) (uk.2)
Kwa upande wa tashibiha, hizo nazo zimetumiwa katika tamthiliya
hii. Tunamsikia Bibi akisema:
....Basi kupaka tu wacha iniwashe. Inachonyota kama upupu Kaja Talafa, Mkali kama pilipili
Tunaweza kupata picha ya sabuni hiyo inayosemekana
inachonyota kama upupu. Lazitna iwe sabuni mbaya! Halafu tunamfikiria
huyu Katibu Tarafa aliye mkali kama pilipili. Hapana shaka huyu ni mtu
mkatili na hana utu wala ubinadamu.
Matumizi ya tamathali za tabaini yapo pia. Tabaini ni
mtindo wa uneni wa fasaha ambao kwayo msemaji husisitiza kauli kwa kutumia
maneno yenye ukinzani, aghalabu neno si. Tunamsikia Bibi akimlalamikia au
kumsema mtoto wake aliyeamua kuolewa na Mchusa aliyemwelezea ukatili wake kuwa
alikuwa, “Mbogo si mbogo, Kifaru si kifaru”. Matokeo yake?
Inasemekana Melina “akakonda akawa mifupa mitupu”. Kwa mara
nyingine tena tabaini hapa imeimarishwa na tamathali ya sitiari.
Kumekuwa na matumizi pia ya tamathali ya kiritifaa.
Ritifaa ni mbinu ya aina ya semi ambazo kwazo (i) mtu aliyekufa huombolezwa
na kuliliwa kama vile angali hai. (ii) vitu visivyokuwa ulimwenguni kwa sasa,
husimuliwa au husifiwa kama viumbe katika hali ya maisha ya duniani. Katika
tamthiliya ya Lina Ubani Bibi analia na kaomboleza mara kwa mara kuhusu
mtoto wake Daudi. Tena pia tunamsikia akimlaumu Dyamini na kumkashifu kutokana
na ubaya wake. Pamoja na tamathali hizo, kuna matumizi machache ya
dhihaka na kejeli.
Licha ya tamathali tulizozisema, mwandishi artietumia pia mbinu
nyingine za kisanaa. Mbinu hizo kwa mfano ni takriri mbalimbali.
Takriri ni mbinu ambayo husisitiza jambo kwa kulirudiarudia. Ziko
takriri za aina mbalimbali: takriri-imundo, takriri-neno na kadhalika.
Katika tamthiliya hii takriri zinazojitokeza mara nyingi ni zile za maneno.
Angalia kWa mfano Mota anavyoyalalamikia Madyamini - ambayo anayaona kuwapo:
“Madyamini shule, Madyantini vijijini, Madyamini
mijini”. Neno Madyamini limerudiwa ili kusisitiza dhana anayoitaka
msanii. Hakika mbinu hizi ni nyingi mno na zinasaidia sana kuimarisha kazi hii.
Matumizi ya mdokezo yapo pia kwa wingi. Hii ni tobinu ambayo kwayo
mwandishi husema na kukatiza maneno na kumwachia msomaji au msikilizaji ahisi
yeye binafsi mwisho wa maneno hayo. Kwa mfano Huila anasikika kwenye simu:
“Haloo... Oh! Dr. Matayo...eeee... ndiyo...mama...ee?Vipitena...?eeh? (uk.
57). Maneno hayo yanaonyesha hamu ya kujua nini kipo upande wa pili. Mbinu ya
mjalizo imetumika pia. Mbinu hii huunga vifungu vya'maneno kwa kutumia
mikato, kwa mfano, kama Huila anavyolalamika kuwa.... “Nimekwenda kote
huko! Ugawaji, Usagishaji, Biashara” (uk. 36). Tashtiti, hali ya
kuuliza na kushangaa mambo yanayofahamika imetumiwa vyema na mwandishi wa
Lina Ubani. Mifano iko mingi. Pamoja na tashtiti kuna pia matumizi ya
nidaa. Nidaa m aina au namna ya msemo wa msisimuo au sauti ya mshangao
atoayo mtu kudhihirisha maono yake ya ndani au kilio cha moyo wakati apatwapo na
mgutusho ghafla wa furaha, hasira, huzuni, chuki na kadhalika. Nidaa
imetumiwa sana na mwandishi wa Lina Ubani. Sara, kwa mfano anapomwona
Bibi analia na kuendelea kuwa mlalamishi anasema: “Ee Mungu wangu!”
(Anatoka) (uk. 32). Msemo huu unaonyesha nidaa. Tamathali na mbinu za
kisanaa zimesaidia katika kuijenga taswira pia.
Hizo ni baadhi tu ya mbinu za kisanaa katika tamthiliya hii ya
Lina Ubani. Utafiti zaidi unaweza kuzifafanua nyingine.
V Mwisho
Profesa Penina Muhando anlefanya jaribio ambalo halijawahi
kufanywa katika uandishi wa tamthiliya za Kiswahili. Jambo hili limefanya
tamthiliya hii kuwa na hadhi ya aina yake rta ya kipekee kuliko zile alizopata
kuziandika mwenyewe. Aidha, kwa rtsomaji wa kawaida anaweza kujikuta katika
matatizo ya kushindwa kuufuatilia vema mchezo huu kutoka mwanzo hadi mwisho.
Vinginevyo, hiini kazi bora, tunampongeza Profesa kwa kazi nzuri hii.
VI Maswali
1. Ni kwa vipi dhamira ya kisiasa imejitokeza katika Lina
Ubani.
2. Eleza maana ya muundo na mtindo katika kazi ya fasihi. Je,
Lina Ubani ina muundo na mtindo gani?
3. Chambua dhamira za Lina Ubani, kishajadili kufanikiwa
au kutofanikiwa kwa mwandishi.
4. Jadili wasifu wa wahusika Zoeni, Bibi, Sara na
Huila.