Winga Ngassa apewa mkono wa heri Yanga

Dar es Salaam. Baada ya mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa kugoma kumwaga wino wa kuichezea klabu hiyo msimu ujao, uongozi wa klabu hiyo umepa mkono wa kwaheri.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu mkuu wa Yanga, Jonas Tibohora alisema kuwa uongozi wao tayari kumlipia Ngassa deni lake lake la Sh45 milioni analodaiwa na benki kwa sharti la kumwongezea mkataba wa miaka miwili.
“Kwa kumsaidia tumempa mkataba asaini kwa miaka miwili amekataa, sasa sisi tutamfanyaje kama mtu hataki, basi, tutaachana nae afanye anavyotaka yeye.”alisema Tibohora na kuongeza:
“Ni wapi Ngassa alisani mkataba na viongozi kuwa watamlipia deni, hivi hela achukue yeye, atumie yeye halafu uongozi umlipie hivi hivi bure.”
“Hizi hela alitakiwa akatwe mara alipokopeshwa zile fedha, lakini sekretarieti iliyokuwepo awali ilikuwa ikimpa Ngassa mshahara wake mkononi, hivyo akabweteka akawa hapeleki deni kule CRBD, mwaka jana ilipoingia sekretarieti mpya ndiyo ikaanza kumkata deni hilo na hapo ndipo mgogoro ulipoanza.”
Hata hivyo, habari ambazo gazeti hili limezipata zinasema kuwa tangu Novemba mwaka jana, Ngassa amekuwa akikatwa Sh1 milioni kulipia deni la Sh45 milioni anazodaiwa na CRDB ambazo klabu hiyo ya Jangwani ilimdhamini na kuchukua kiasi hicho cha pesa na kuilipa Simba.
Baada ya makato hayo amekuwa akibakiwa na Sh2.5 milioni kwa mwezi.
“ Kwa kweli, fedha anazopata Ngassa ni nyingi, lakini kwa vile ana mambo mengi amejikuta hata hizo zinazobaki hazimtoshi. Ngassa ni mchezaji mzuri, lakini amekosa mtu wa kumsimamia na kumuongoza kimaadili kwenye matumizi,”kilisema chanzo cha habari kutoka Yanga.
Hadi sasa, Ngassa hajasaini hati aliyotakiwa kusaini alipiwe deni hilo, maana yake kuna hatari uongozi wa klabu hiyo ukamruhusu kwenda kuchezea klabu yoyote aitakayo.
POSTED THURSDAY, APRIL 16, 2015 | BY- MWANDISHI WETU, MWANANCHI
Powered by Blogger.