Kiswahili -2-MADA MPYA 3: KUHAKIKI KAZI YA FASIHI ANDISHI





MADA MPYA 3: KUHAKIKI KAZI YA FASIHI ANDISHI
MADA NDOGO-1: MAENDELEO YA FASIHI ANDISHI.
A.Mwelekeo wa kazi za fasihi andishi nchini Tanganyika na Zanzibar wakati wa ukoloni.
Kimaudhui Kazi nyingi za fasihi andishi nchini Tanganyika na Zanzibar zilishughulikia masuala mbalimbali ya kimaisha lakini kazi nyingi zilikuwa na mambo ya mila na tabia kama njia ya kufundisha maadili .vile vile zilishughulikia utamaduni, mawaidha, dini, maadili mema na maonyo na kazi zilizoopinga ukoloni
Senkoro (1976) anaonyesha kuwa maandishi ya kwanza ya nathari yaliyotokana na waafrika wenyewe na kama vile“Uhuru wa watumwa ‘(1934) cha James Mbotela kinashughulikia uhusiano baina ya mataifa ya magharibi na ya Afrika.Katika kitabu hiki mwarabu na muislam wanalaumiwa kwa utumwa uliokuwepo Afrika Mashariki wakati mkoloni anasifiwa kwa kuleta uhuru japokuwa utumwa ulitiliwa nguvu na ukoloni.
Kwa ujumla hadithi ya uhuru wa watumwa inaonyesha ubaya wa biashara ya utumwa iliyoendeshwa na waarabu na papo hapo inaonyesha matukio yaliyowapata watumwa mambo yaliyowaumiza na uchungu ulowapata watumwa hao.
Mwandishi anaeleza mateso ya watumwa kwa watumwa kwa uchungu na mchomo mkali.Pia hadithi hii inawatukuza wakoloni wa Kiingereza, ikijaribu kumfanya mwafrika akubali kutawaliwa.Hadithi hii inausuta utumwa wa kimwili uku ukiusanifu ule wa akili na mawazo ambao ni utumwa ulio mbaya zaidi.
Senkoro anaendelea kusema kuwa baada ya mwaka 1949-1960 kazi nyingi za fasihi za Kiswahili hasa riwaya zilifuata mkondo wa ngano na fasihi simulizi kama za Paukwa pakawa…hapo zamani za kale palitokea kimaudhui fasihi simulizi zilijali maadili ya kufuatwa katika kujenga jamii inayofaa katika maisha.Mfano mzuri wa vitabu hivi ni Adili na Nduguzi (1952) utenzi wa mwanakupona (1858) na Al-inkishafi (1890).
Katika Adili na Nduguze  mwandishi alitumia visasili vya jadi ya kiarabu kama vile matumizi ya majini anaonya dhidi ya uchoyo na kuhimiza moyo wa wema, usamehevu na kutosheka.Katika utenzi wa mwanakupona,mama anatoa mafunzo kwa binti yake.Humo ndani ya utenzi mwanamke anapaswa kujitazama kwa nyenzo tatu
Ø  Yeye ni nyenzo ya starehe ya mume wake hivyo inampasa ajitahidi mno kumfurahisha ili apate rehema zake, kwani Mungu hata acha kumtia hatiani kwa kutotimiza huu mume atakapomkana mbele ya Mungu.
Ø  Inampasa mwanamke awanyenyekee wanaume wote isipokuwa watumwa tu.Aonyeshe kilicho na heshima kubwa kwao.
Ø  Mwanamke ajione kuwa yu mmoja wa matajiri au maskini (watumwa).Binti anayeandikiwa shairi hili ni tajiri naye anaaswa asichanganyike na watumwa, watu duni waliodharauliwa duniani
Shughuli za kisiasa zilizopamba moto miaka ya 1950-1960  ilisababisha kuibuka kwa fasihi ya kisiasa ambayo wasanii wake walizitumia kumpinga mkoloni.
Shaaban Robert  pamoja na matatizo yake yote, alionyesha upinzani wake hasa katika riwaya zake za Kusadikika (1951) na Kufikirika (1967) ambamo zaidi ya kuwatetea wajumbe mbalimbali walikuwa wakiutetea uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Pia mwandishi anaitetea serikali ya kikoloni kwa kejeli kubwa kwani ilikuwa inainyonya Tanganyika na Zanzibar kwa ajili tu ya kukidhi “Uguma na Utasa” wa mfalme na malkia.Ugumba na Utasa ambao Shaaban Robert kautumia kwa ishara tu ya mahitaji ya wakoloni.
Katika “Kusadikika” mwandishi anajali suala la haki ya watu dhidi ya uongozi kandamizi wa kiimla utawala usio na kiasi wala mpaka ni utawala ambao hatimaye hukwamisha maendeleo ya nchi na watu wake.Kwa sababu huwanyima huwanyima watu uhuru wa kufikiri na kuchangia katika maendeleo ya nchi yao kwa kutumia mbinu ya kejeli, tashtiti, misemo, nahau. Mwandishi amejitahidi kufikisha lengo lake la kuonyesha hasara ya kuyakwamisha maendeleo ya nchi.
Ukoloni wa kiutamaduni ni mwanzo tu wa ukoloni wa siasa na uchumi. Hata katika riwaya ya Tafsiri ya hadithi ya ”Chinua Achebe”Shujaa Okonkwo (1932) ambapo wamisionari walitangulia kuja ili baadae watawala waje na kuiteka nchi yote. Hivyo wamisionari walishirikiana na watawala katika kuwanyanyasa na kuwanyonya watu.
Mhusika wa zamani, hasa mhusika mkuu alikuwani halisi mwenye sifa zisizo za kawaida ambaye alisanifiwa na msanii kwa makusudi mazima ya kuumba. Mfano bora wa kuigwa na kumfanya awe kielelezo cha ukweli na ukamilifu wa maisha na mwenye kupigania na kuleta mambo hayo bila kuwa na dosari. Mhusika mkuu wa zamani alitafakari maisha ya jamii kwa njia ya matendo makubwa na lugha teule. Mhusika huyo japo kuwa alijitokeza  kuwa mtendaji mkuu kiasi hicho lakini hakuwa na saikolojia wala hisia. Sifa hizi za upungufu wa saikolojia na hisia katika mhusika mkuu wa zamani ndizo zilizomtofautisha na mhusika mkuu wa kisasa.
Tofauti nyingine ya msingi ni ile inayohusu uhusianao kati ya mhusika mkuu huyo na wakati. Mhusika mkuu wa zamani kama vile wa kwenye hadithi ya kifasihi alijitokeza kama mhusika mkuu wa wa wakati wote. Kwa msanii wa namna hiyo ya wahusika, dhana za wakati na ukweli uliokamilika zilikuwa katika hali ya kutobadilika wakati na ukweli vilikuwa na vitu vilivyotitia pamoja.
Kwa jinsi hiyo maandishi ya kisanii yaliyopewa jukumu la kuzibeba sifa hizo yalilengwa kuwa ni ya wakati wote, yasizeeke. Lakini kinyume chake mhusika mkuu wa kisasa anayaona maswala yasiyotulia bali ni maswala ambayo yana badilika pamoja na jamii. Na baadhi ya wasanii wa kisasa wanaona kuwa, swala la ukweli uliokamilika kwa kiasi kikubwa ni ndoto iliyomo katika vichwa  vya watu tu, na wala si maisha halisi.
Mhusika mkuu wa kisasayuko katika wakati maalumu wa kihistoria ambapo anayazamia maisha kwa undani na kuyatafakari. Lakini kadri Shaban Robert alivyozidi kuandika kama Maisha yangu na baada ya mwaka Hamsini(1966) Wasifu wa Siti binti Saad(1967) Siku ya utenzi wote(1968) ndivyo alivyozidi kuwapa wahusika wake sifa zinazokaribia au zinazoelekeana katika hali halisi ya maisha. Hii ina maana kwamba mkabala wake ulizidi kuelekea katika hali ya kueleza ukweli kwa kutumia mbinu za kisanii ambazo hazikutenga kazi ya Sanaa kwa kiasi kikubwa na uyakinifu wa maisha.
Kwa ujumla fasihi Andishi ya awali ilihusu zaidi maadili na masuala ya kidini kama katika”Adili na nduguze”.
Pili mvutano ulikuwepo baina ya wakoloni na waafrika, Ulikuwa unadhihirishwa katika baadhi ya kazi za fasihi Andishi za awali.Pia maandishi mengine ya fasihi yalihusu matarajio ya jamii itakiwayo baada ya ukoloni, kama katika kufikirika na kusadikika, katika kipindi hiki tanzu za fasihi andishi zilizokuwapo ni riwaya na ushairi. Baada ya uhuru, tamthiliya zote za Kiswahili zilizochapishwa zilikuwa zimeandikwa na wakenya, watanzania, hawakujitokeza katika uwanja huu hadi baada ya uhuru.
B: Mwelekeo w kazi za fasihi Andishi nchini Tanzania baada ya uhuru
 Baada ya uhuru kulikuwa na fasihi mchangamano ambayo ni vigumu kuainisha hadi tukio kuu la kutangazwa kwa Azimio la Arusha, kabla ya hapo fasihi kwa kiasi kikubwa, ilikuwa ya kushangilia uhuru uliopatikana hasa katika magazeti ambako mashairi na hadithi nyingi zilionyesha hoi hoi ya lelemama za uhuru.
Kwa upande wa mashairi, vitabu kama vile Utenzi wa uhuru wa Tanganyika(1967) na utenzi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania(1968) viliandikwa wakati huo. Ni kipindi hicho cha uhuru utanzu wa tamthiliya ulijitokeza kwa mara ya kwanza kwa upande wa Tanganyika na Zanzibar.
Mwandishi maarufu wa tamthiliya aliyejitokeza kipindi hicho Ebrahim Hussein ambaye tamthiliya yake ya kwanza “wakati ukuta”(1969) ilichapishwa ikifuatiwa na tamthiliya ya “Kinjekitile”(1969)
Fasihi ya Kiswahili imepevuka zaidi kwenye miak ya 1970. Mulokozi(1996) anasema karibu tanzu zote za fasihi Andishi ya Kiswahili zimepata wawakilishi. Hali hii imejitokeza fasihi za mokondo mbali mbali.
Kimaudhui, fasihi andishi nchini Tanzania baada ya uhuru imejadili dhamira mbali mbali ambazo zinatokana na matukio  mbali mbali ya kihistoria yaliyojitokeza katika jamii yetu ya Tanzania.
Kipindi maalumu cha maisha kina matukio yake maalumu ambayo huigusa jamii kwa uzuri au ubaya na kuwa dundo la moyo la kipindi hicho ndichi kinachojenga kilele. Aidha tukio linapokuwa dundo la moyo la kipindi fulani cha maisha huwa pia mada kuu(muhimu) ya wakati huo kwa jamii inayohusika.Mada hiyo uweza kujitokeza kinagaubaga katika taaluma mbali mbali za jamii na fasihi ikachukua nafasi muhimu.
Kihistoria masuala makuu ya miaka   ya 1960 yalikuwa ni ukombozi wa bara la Afrika na ujenzi wa jamii mpya baada ya uhuru. Masuala haya makuu yaliyojitokeza  katika fasihi andishi ya Tanzania wakati huo. Hivyo palitokea fasihi andishi za kisiasa na kifalsafa zilizojadili kuhusiana na  maisha, utawala na ujenzi wa jamii mpya.Kazi nyingi za fasihi zilipingana  na ukandamizaji, ubinafsi na pamoja na unyama mwingine uliokuwa unafanywa.Pia zilieleza mkondo wa ubanadamu usawa na ustawi. Baadhi ya kazi hizo ni za Shaaban Robert, Utu bora mkulima (1987) na siku ya watenzi wote(1968)
Kwa upande wa ukombozi, riwaya ya kiimbila “Lila na Fila” (1966) iligusa dhamira hiyo kiishara na  Tamthiliya ya E. Hussein”Kinjekitile” (1969). Katika kipindi cha miaka ya sitini ilitokea fasihi ya tabia na maadili ambayo imejadili  maadili mema na maonyo.
Fasihi hii ya tabia na maadili inawakilishwa na J.M Somba “kuishi kwingi kuona mengi”(1968) “Alipanda upepo akavuna tufani” (1968) Mathias Mnyapala “Diwani ya mnyapala(1965) S.A Kandoro “Mashairi ya Saadan”(1972), Akili mali “Dwani ya Akili Mali”(1967)
Aina nyingine ya fasihi iliyojitokeza katika kipande hiki ni ile riwaya na hadithi fupi za upelelezi na za mapenzi. Fasihi ya aina hii ilizuka kutokana na nguvu mbali mbali za jamii.
Katika Tanzania, aina hii ya fasihi ililetwa kwa mara ya kwanza na M.S Abdulla alipoandika riwaya ya “Mzimu wa watu wa kale”(1959) na miaka ya 1960 aliandika riwaya ya “kisima ch giningi”(1968) akafuatiwa na katalumbwa aliyeandika kitabu cha “Simu ya Kingo”(1965)
Mwisho kazi za fasihi zilijitokeza miaka ya sitini ni fasihi ya mila na utamaduni inayowakilishwa na M.S Farsy “Kurwa na Dotto”(1960) F.Nkwera “Mzishi wa baba ana radhi zake” (1968)
Mwaka 1967, Azimio la Arusha lilitangazwa. Azimio hilo lilionekana kwa wanasiasa na wananchi wengi kuwa ndio dira ya kuitetea jamii ya Tanzania katika maisha bora ya ufanisi na maendeleo kwa hiyo kipindi cha miaka mitano  hivi baada ya Azimio la Arusha kilikuwa na fasihi ambayo ilitukuzwa maadili na awali zilitokana na tamko la Arusha.
Maudhui yaliyotawala fasihi ya kipindi hiki ni ujenzi wa jamii mpya kwa kupitia nguzo ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kazi hizi zilizosisita mabadiliko ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, zilizopigania jamii mpya Ijapokuwa bila kuonyesha kimantiki (kiyakinifu) vipi jambo hilo lingewezekana. Mfano wa kazi hizi ni:-Mashairi ya miaka kumi ya Azimio la Arusha (1977),Mashairi ya Azimio la Arusha  (1970),Utenzi wa zinduko la ujamaa (1972),Utenzi wa kumbukumbu za Azimio la Arusha (1970),Matunda ya Azimio la Arusha (1980),Liwazo la ujamaa (1978),Mtu ni utu (1971),Ndoto ya Ndana (1976),Njozi za usiku (1970),Kijiji chetu (1971) n.k
Pia kutokana na Azimio la Arusha pamoja na  siasa yake iliyosisitizakuhusu umuhimu wa vijiji na umuhimu wa kilimo, zilitokea kazi za fasihi ambazo zilihubiri kuhusu maisha bora wa vijiji yaliyo linganishwa na yale ya mjini.
Suala ambalo liliwahi kuangaliwa na Shaaban Robert katika riwaya yake ya “Utubora Mkulima”(1968). Sasa ilipata damu mpya katika kazi kama za Penina Muhando,”Hatia” (1971) Balisidiyo Shida (1975) Mnyampala, Ngonjera za ukuta  (1968) Mbogo “Giza limeingia”(1980) mashairi mbali mbali katika magazeti n.k katika kazi hizi mvutano baina ya mji na kijiji ambao ulileta matatizo ya wizi, ujambazi, umalaya na mengine ya aina hiyo yalitolewa dawa moja, kurudi vijijini. Jawabu hili halikuwa sahihi kwani linakwepa kiini hasa cha tatizo  na  lilipotosha maana halisi ya kijiji na kilichotakiwa kuundwa katika jamii ya Tanzani.Kijiji kilionekana kuwa mahali pa kuwalundika wahuni walioshindwa maisha ya mjini.
Katika kipindi hiki cha 1970-1980  zilijitokeza kazi ambazo zilitazama suala lakujenga jamii mpya kwa kutafakari na kujiuliza na hata kwa mashaka na wasi wasi pia. Hususani baada ya kubaini utata, migongano ya kitabaka na ukuaji wa haraka wa ubepari wa kimji. Mfano Kiu (1972) Kichwa maji (1974),Gamba la nyoka (1979),Nyota ya Rehema (1978) Dunia uwanja wa fujo (1979)  ( Madumulla 1988)
Kwa ujumla miaka ya 1980 riwaya ya Kiswahili imeshuhudia jaribio la muundo wa riwaya ya kifalsafa. Lakini kama ilivyogusiwa kwa kiasi kikubwa mikondo ya riwaya imeendelea kuwa ile ile ya miaka ya sabini. Riwaya ya ukasuku katika upande wa riwaya dhati imepotea. Badala yake kuwa riwaya inayopevuka nakutumia ukweli wa mambo. Inayojaribu kubainisha migongano ya kijamii katika vipengele mbali mbali vya maisha hususani vya kiuchumiu ijapokuwa waandishi wanafanya hivyo katika mkabala au mitazamo ya maisha inayotufautiana,mikabala hiyo ni kama vile;Mfumo wa vyama vingi,Utandawazi
Kipindi hiki mfumo wa chama kimoja ulifutika na mfumo wa vyama vingi ukaanzishwa hapa nchini ambapo uliambatana na kuanzishwa kwa utitiri wa vyama vingi. Fasihi andishi iliyojitokeza kipindi hiki ilizungumzia mfumo wa vyama vingi na athari zake kwa jamii yake. Mfano wa kazi hizo ni riwaya ya “Nyuma ya pazia” (1996), na mashairi mbali mbali yaliyokuwa yanaandikwa kwenye magazeti.
Kwa upande wa utandawazi ambao unaenda sambamba na ubinafsishaji wa soko huria umewaathiri sana waandishi wa fasihi ya Kiswahili. Katika fasihi ya Kiswahili  utandawazi umesababisha kuzuka kwa fasihi mpya ya Kiswahili ambayo imezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 1990, muda mfupi baada ya neno utandawazi kuingia masikioni na kuzama akilini mwetu kuanzia 1980.
Utandwazi ni neno dhahania lenye maana nyingi tata kutegemea msisitizo wa anayelitumia. Pamoja na tofauti za maana na matumizi ya neno hili wataalamu wakubliana kwamba ni neno linaloelezea mfungamano na uhusiano uliojitokeza katika miaka mingi iliyopita, hasa katika biashara na uchumi. Lakini pia katika utamaduni, miongoni mwa jamii tofauti za dunia zimekuwa na mfungamano na uhusiano uliojitokeza katika miaka mingi iliyopita hasa katika biashara na uchumi,na kiutamaduni. Mfungamano na uhusiano huu unaotofautishwa  na uhusiano mwingine wa aina hii uliojitokeza kabla, kwasababu utandawazi umepata kazi kubwa ya kuwekeza mitaji na kuvuna faida kubwa kiuchumi kiutamaduni, ikisaidiwa na maendeleo makubwa ya kiteknolojia yaliyopatikana karibuni hasa ya vyombo vya habari vya masafa marefu. Utandawazi unahusishwa na kuenea kwa tamaduni za kimataifa (Marekani na Ulaya) kwa njia ya biashara (kama vile vinywaji vya Cocacola, bia na pombe kali ambazo zamani zilikuwa hazijulikani). Mtiririko wa muziki na taswira kupitia video,luninga,mitandao ya kompyuta/Tanakilishi na simu,CD, DVD na VCD.Mfano wa fasihi ya Kiswahili ni kama vile Nagona(1990), Mzingile(1990), Zirani na zraili(1999), Babu alipofufuka(2001). Makundi wa soko huria(200), Baria- Adam(2002), Dunia yao(2005), Mkamaduma(2005) zimeathiriwa sana na utandawazi wa kimagharibi, sifa moja kubwa ya kimaudhui miongoni mwa kazi hizi ni ile ya kushughulikia kwa kina matatizo ambayo yana kabili ulimwengu wetu leo. Ingawa bado riwaya hii inajishughulisha kwa kiwango fulani na matatizo ya ndani ya nchi na jamii husika kwa kiasi kikubwa imekiuka mipaka ya kitaifa na kuenea kwa kiasi kikubwa inachunguza si jamii ya Tanzania tu bali dunia yote huku ikionyesha athari za utandawazi kwa jamii hizo.
Katika Babu alipofufuka (2001), Dunia yao(2003) na hata Bina- Adamu (2002), Suala zima linaloshughulikiwa kifalsafa ni siasa. Nini maana ya kuishi? Nini maana ya uhuru? Nini maana ya maendeleo? Nini maana ya uraia wa mtu? Nini maana ya uzalendo? Kwanini kikundi kidogo cha watu wapange maisha ya watu wengi katikavjamii fulani nan je ya jamii hiyo? Kuna dunia ngapi katika dunia moja ya jamii fulani?  Mipaka ya dunia hizo ni miembamba au mipana kwa kiasi gani? Nini maana ya kijo? Nini maana ya kuishi? Inawezekana mtu anayeishi akawa amekufa? Nguvu zipi zinaongoza limwengu wetu? Zinaongoza kwa mslahi ya nani na kwa taathira?.Athari hizi za utandawazi katika jamii na maisha halisi zimehitimishwa na Chachage, ambaye riwaya yake ya “Makuadi wa soko huria”(2002) inavua nguo na kusambaratisha utandawazi na utetezi wake wa ndani.
Kwa jumla maendeleo ya fasihi Andishi nchini Tanzania baada ya uhuru ni makubwa sana ukilinganisha na wakati wa ukoloni. Tanzu zote za fasihi  Andishi, riwaya, hadithi fupi ushairi na tamthiliya zimepanuka sana. Vile vile kama waandishi wengi sana wa tanzu hizo na uandishi wao umekuwa ukibadilika kulingana na mabadiliko mbali mbali yanayoitokeza katika jamii. Kila tukio la kihistoria lililotokea katika jamii limezaa kazi zake za fasihi.
MADA NDOGO 2; KUHAKIKI USHAIRI
USHAIRI
 Ushairi ni Sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalumu wa maneno fasaha na yenye muwala,kwa lugha ya mkato, picha au sitiari au ishara katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo ili kueleza tukio, wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisi fulani kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.Kutokana na maana hiyo kuna mambo muhimu yanayojitokeza katika ushairi:
Ø  Ushairi ni Sanaa yaani kazi iliyobuniwa na mtunzi mahususi.
Ø  Ushairi una ufungamano na hisia.
Ø  Ushairi una mpangilio wa aina fulani kuanzia kiwango cha sauti, neno, sentesi hadi ubeti.
Ø  Ushairi huchota hisia na tafakari zake kutoka katika ulimwengu halisi wa maisha ya jamii na mara nyingi hufungamana na falsafa ya jamii fulani.
Ø  Ushairi hutumia lugha ya mkato yenye kueleza mambo mengine kwa maneno machache kwa kutumia mbinu za taswira na tamathali za semi.
Ø  Ushairi huzingatia sana dhana ya urari (ulinganifu wa vitu) kimuundo.
Ø  Ushairi una uhusiano na muziki (nidhimu) ngoma na uchoraji (mchoraji) hutumia rangi na brashi mshairi hutumia taswira na maneno.
AINA (KUMBO) KUU ZA MASHAIRI YA KISWAHILI
MULOKOZI(1996) Ameainisha aina tatu za ushairi waKiswahili.Aina hizo ni:-
I)                    USHAIRI WA KIMAPOKEO
Ni mashairi na tenzi za kijadi zenye kufuata kanuni za urari wa mzani na mpangilio wa vina vya mwisho au kati.Katika ushairi wa kimapokeo kuna mambo ya msingi ambayo yanasemekana kuwa ni mti wa mgongo wa ushairi wa Kiswahili.
Kwa mujibu wa wanamapokeo.Shairi la Kiswahili lazima liwe na vina na mizani,mistari ubeti na kituo.
Katika utenzi (aina pia ya ushairi wa kimapokeo) kuna kuwa na bahari katika mstari wake wa mwisho.
Ushairi wa kimapokeo unaweza kugawanyika katika sehemu kuu mbili yani Tenzin na Mashairi
a)      TENZI
Ni utungo ambao kimaudhui huelezea tukio fulani linalotokea katika jamii au liliwahi kutokea.Pengine huweza kuwa maelezo juu ya wasifu wa mtu fulani, jambo fulani la kihistoria au jambo lolote zito linaloelezwa kwa maelezo marefu.Utenzi ni masimulizi marefu juu ya jambo fulani maalumu
Katika upande wa fani utenzi una sifa za pekee kabisa
v  Utenzi unakuwa na beti nyingi kuliko yalivyo mashairi au aina nyingine yoyote ya ushairi.Beti hizi zaweza kuwa 100, 200, 300 au zaidi kutegemeana na ufundi wa mshairi mwenyewe.
v  Utenzi huwa hauna mizani ndefu,tenzi zilizo shamiri sana katika jamii hii ni zile zenye mzani nane nane katika kila mistari zaweza pia kwenda zaidi ya nane kufikia kumi na moja lakini hazuii zaidi ya hapo
v  Katika utenzi kila ubeti huwa na mistari minne, mistari mitatu ya kwanza ikiwa ina vina vyenye urari sawa na ule wa mwisho ikiwa na kina tofauti ingawa vina vya mistari mitatu ya kwanza huwa na vina vyenye urari sawa lakini vina hivyo hubadilika badilika toka ubeti mmoja hadi mwingine.
v  Katika utenzi kina cha mwisho katika msitari wa mwisho wa kila ubeti huwa hakibadiliki badiliki, kina cha mwisho wataalamu wengi wa ushairi hukiita bahari kwa sababu huwa kimetenda na kuongelewa katika utenzi mzima   Mfano wa tenzi:   S.Robert, Mapenzi bora,A.Abdilatif, Utenzi wa maisha ya Adam na Hawa (1971)   J.K.Nyerere, Utenzi wa Injili kadiri ya utungo wa Luka (1996).Mfano Utenzi wa Fumo Liyongo (13 BK)
          Ubeti 6: Liyongo Kitamkali
                  Akabalighi vijali
                  Akawa mtu wa kweli
                 Na hiba huongeya
Ubeti 7: Kilimo kama utukufu
              Mpana sana mrefu
               Majimboni yu maarufu
               Watu hujakumwangalia
Ubeti 10: Sultani pate Bwana,
               Papo nae akanena,
              Wagala mumemwona,
              Liyongo kuwatokeya
b)     MASHAIRI
Shairi kama sehemu ya ushairi, ni utungo ambao huelezea kwa ufupi mambo fulani kuhusu binadamu na mazingira yake.Aghalabu mashairi huelezea mambo yanamhusu binadamu na maisha yake ya kila siku.Mashairi ya kimapokeo yanapoandikwa hufuata kanuni za vina, mizani, mistari, ubeti na kituo mfano:-
    KUNTU SAUTI YA KIZA (FUNGATE YA UHURU-UK 38)
Nyuki ni mtanashati, umbo na zake tabia,
Yeye yu kila wakati, vichafu huvikimbia,
Mchana na kulati, hatui kwa kukosea,
Kuntu sauti za kiza, Nyuki hapendi vichafu.

Ni inzi na sio nyuki, Nadhafa hajazoea,
Kwa uchafu ni ashiki, hawezi kuuachia,
Vianzavyo humiliki, fahari hujonea,
Kuntu Sauti za kiza, Nyuki hanyoni vichafu.
U WAPI UZURI WAKO
U wapi uzuri wako, haupo umepotea,
Ya wapi maringo yako, na hashuo za dunia,
Leo upo peke yako, sote tumekukimbia.

Sasa ni chano cha maji, watu wajichanyatia,
Umekwisha ujuwaji, haya zimekupatia,
Yale usoyatarajia kwako yamekuhamia.
DAFINA
Paa ni kuruka angani, kama ndege wa tiara
Paa ni mnyama porini, ni mwenye nyingi, Papara
Paa ni kuteka mengine, moto uwako imara
Paa ni toa migombani, Samaki atie sura
Paa Pia ni la nyumba, makuti au kurara
Mgodi wa Kiswahili ni dafina isiyokwisha

2. USHAIRI WA MAIGIZO
Ushairi huu unahusisha ngonjera na ushairi wa kidrama
v  NGONJERA
Ni ushairi wa majibizano ulioanzishwa na Mathias Mnyapara miaka 1960 ili kueleza siasa ya ujamaa na kujitegemea kabla ya hapo ulikuwepo ushairi wa majibizano lakini ulikuwa unatambwa tu.
Ø  Katika ngonjera kuna pande mbili zinazojibizana kuhusu mambo fulani upande mmoja huwa sahihi na wa pili huwa umepotoka.
Lengo la mabishano ni kuushawishi upande uliopotoka ukubaliane na upande wenye msimamo sahihi baada ya kuelimishwa. Hili linapotokea ngonjera huwa imefikia kilele chake. Mfano wa ngonjera ni Ngonjera za ukuta 1 na 2 (Mnyapara 1970-1972)
Ushairi wa kidrama ni ule unaotumika katika baadhi ya tamthiliya. Ushairi huo ni sehemu tu ya mchezo wa kuigiza ni mtindo wa kuandika mazungumzo ya wahusika katika tamthiliya hivyo hauwezi kutenganishwa na hiyo fani ya tamthiliya. Kwa mfano tafsiri Shaspare, Mabepari wa Verusi Julius Kaizari (Nyerere) 1969, Mfalme Epidope (Mushi 1971)
Mfano:
Juma: Naam na nitampa bure bila ya fidia
              Pokeeni na Jeshika kutika kwa Myahudi
              Hati maalum ya hiba, baada ya kifo chake
              Ataacha kwenu nyingi, kila atakachokiacha

Baraka: Mabibi wema, mwaonyesha maana kwa walagai

Neema: Kunakaribia kucha, lakini nina hakika
               Bado hamjaridhika, kabisa na mambo hayo
               Kwanza na twendeni ndani, kisha huko tuhajiri
               Nasi tutawajibuni, mambo yote sawa sawa
             (W. Shakespare, Mabepari wa virusi 1969)
Katika mfano huu ushairi huu una mizani 16 kwa mshororo bila urari wa vina, kanuni ya utoshelezi imekiukwa wazo la mshororo mmoja linaendelezwa katika mshororo unaofuata.
3.      USHAIRI WA MLEGEZO / KISASA / MASIVINA
Ni mashairi yasiofuata urari wa vina na mizani, Vina vinaweza kutoka lakini si lazima katika mistari. Pia mapigo yanaweza kuwa sawa kwa idadi katika mfululizo wa vipande kadhaa lakini si katika tungo nzima.
Mfano:
CHAI YA JIONI
Wakati tunywapo chai hapa upenuni
Na kuwatazama watotowetu
Wakicheza bembea kwa furaha
Tujue kamba ya bembea yetu
Imeshalika na imeanza kuoza
Na bado kidogo tutaporomoka

Kulikuwa na wakati uinisukuma juu
Nikaenda zaidi ya nusu duara
Kulikua na wakati nilidaka
Ulipokimbia na kuanguka

Sasa tukisubiri ndoto tusizoweza kutekeleza tena
Tumalize machicha ya chai yetu ya jioni
Bila kutema tena na kuwa tabasamu
Baada ya hapo tujilambe lambe utamu utamu
Uliobakia kwenye midomo yetu
Tukikumbuka siku ilee ya kwanza
Tulipoutana jioni chini ya mwembe
Tukifunga bembea yetu
Naye umbwa samba akikusubiri

Lakini kabla hatujaondoka kimya kimya
Kukamilisha nusu duara iliyobakia
Tuhakikishe vikombe vyetu visafi
(Kazilahabi 1988)

VIJENZI VYA USHAIRI WA KISWAHILI
Ushairi wa Kiswahili unajengwa na vipengele vifuatavyo:-
1.      Mpangilio wa maneno
Maneno ya ushairi hupangwa ili kuleta maana fulani, sauti za aina fulani au urari fulani wa mizani.
Katika shairi la Kazilahabi “Kisu mdomoni” , kisu mdomoni (kiuchumi) uk 10 kuna mstari ufuatao.
“Ya nyuma sana nisijali ya mbele sana niyakabili. Hapa neno “sana” limewekwa makusudi kati ya “nyuma” na “nisijali” ili kupata maana mbili. Mambo ya zamani sana (ya nyuma sana) na kutojali jambo neno (sana nisijali) kama neno sana kinga kuja baada ya nisijali maana hizo mbili zisingalitokeza. Vivyo hivyo uwili huu wa maana tunaupata katika kipande cha pili cha mstari huo “ya mbele sana niyakabili” kutokana na mpangilio wa maneno.
2.      Takriri na Ridhimu au wizani
Takriri ni mbinu ya kurudia rudia jambo kwa kusudi maalumu, vina na urari wa mizani ni aina ya takriri. Mtunzi anaweza pia kurudia rudia maneno fulani au silabi fulani kwa shabaha malumu. Kwa mfano katika shairi la “ Kufa moyo” Shaaban Robert anatumia mbinu ya takriri kwa kurudi rudia kifungu cha maneno “ siku ya ………. Kwa msisitizo:-
Siku ya panga kufuta, mashujaa kwenda kona
Siku ya kuja matata, kwa damu kwenda mdundo
Siku ya watu kuteta, kufa moyo mfundo
Siku ya kung’ara nyota za watenzi wa mtindo
      (Shaaban Robert 1991 : 48-49)
Takriri hutumika sana katika nyimbo na mashairi ili kutia msisitizo.
Ridhimu ni mapigo asili ya lugha , kila lugha ina mapigo yake. Mawimbi ya sauti yenye kupanda na kushuka na yanayofunga maana na mfuatano wa sauti usio na maana yoyote.
Ridhimu ya ushairi wa muziki hutokana na mlingano wa vipande vya mapigo ya lugha au sauti . Katika muziki vipande hivyo vya mapigoni lazima vilingane kabisa katika ushairi.Vinaweza kupitana kidogo ili kupunguza maudhi masikioni.
3.      Taswira au Picha
Taswira ni mbinu ya kuumba picha ya jambo katika mawazo ya msomaji au msikilizaji wa tungo hilo kwa kutumia maneno. Picha ya maneno ikichorwa vizuri mtu huweza kuhisi, kuona, na hata kunusa kile kinachozungumzwa.
Mfano:
Amina umejenga, umekufa umetangulia
Kama ua umefunga, baada ya kuchanua
Nakuombea mwanga, peponi kukubaliwa
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
(S. Robert Amina 1966: 3)
Katika ubeti huu, mshairi analinganisha maisha ya mauti ya Amina kwa njia ya picha na ua mbalo limekuwa likichanua na kisha likafunga au kunyauka.
4.      Tamathali za Semi
Tamathari ni umithilishaji yaani uwakilishaji wa jambo kwa kulinganisha au kulifananisha na jingine.Kwa mfano badala ya kusema “Juma alikuja mbio sana” Mshairi atasema “Juma alikuja kama umeme” Tamathari nzuri hupanua, huyadumisha na huipa uhai na uhalisia zaidi dhana inayoelezwa, huburudisha na kuzindua akili ya msomaji au msikilizaji wa shairi na athari ya kudumu katika hisia na mawazo yake.
Tamathari zinazotumika zaidi katika ushairi ni Tashbiha, tafsida, tashhisi, mbalagha, kejeli, sitiari n.k.
5.      Hisia za kishairi
Hisia hizi hutokana na msukumo wa ndani wa moyoni alionao mshairi wakati anapotunga shairi lake na hujidhihirisha katika uteuzi na mpangilio mzuri wa maneno yenye kuwakilisha maudhui husika kwa mfano, maudhui ya huzuni hudhihirika katika maneno yanayotumika ambayo aghalabu yanadokeza hali ya huzuni, vina vyenye sauti ya kilio.Mfano ee, lel, lel, lel, ea, aa, ya n.k.
Mfano mzuri ni shairi la Shaaban Robert la AMINA ambazo linaomboleza kifo cha mkewe.Hisia za furaha pia huweza kuwasilishwa kwa njia hizo hizo
   Mfano:-Shairi la Cheka kwa furaha
            Dhiki ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?
              Haya cheka ha! ha!, ndio ada duniani,
              Basu cheka kwa! kwa!, usifike moyo wako.
              (Robert, kielelezo cha fasihi 1968:16)
6.      Lugha ya mkato.
Shairi huzungumza mambo wa ufupi kuliko ulivyo katika maongezi ya kawaida. Hivyo ni muhimu kwa mtunzi kujua namna ya kueleza jambo kwa Lugha ya mkato.Hii inawezekana kwa kutumia taswira na tamathali badala ya maelezo marefu.
7.      Mchezo wa maneno
Mbinu ya kuchezea maneno hutumiwa na washairi ili kutoa maana ya kile kisemwako na kuongeza utamu wa usemaji mara nyingi maneno yenye umbile moja lakini maana tofauti hutumiwa kwa ajili hii mfano katika Shairi la M.Mulokozi la “wale, wale” maana tatu za neno wake (yaani kundi la watu na hao watafune na kumeza chakula “na” “wale”wale” kwa maana ya “hao hao” si wengine zinachezewa ili kuleta ujumbe fulani.Mshairi anaona kuwa hakuna mabadiliko ya msingi yaliyotokea .Kundi lile la walaji limerejea katika madaraka kadharika maneno “kura” na “kula” yamewekwa sambamba ili kuonyesha uhusiano uliopo kati ya uchaguzi (kupiga kura) ulaji.
              Wale wale
              Wale wale ndiyo wao
              Bado wapo palepale
              Wao wale wenye vyao
              Na vya kwao vile vile
              Wala kale wala leo
              Kura huko kule kule
              Mwendo huu ndiyo huo
              Bado tupo pale pale
              (Mulokozi 1990)

FANI NA MAUDHUI
Ushairi kama Sanaa hujengwa na mambo mawili ambayo ni fani na maudhui.Maudhui ni mambo yaliyomo (yanayozungumzwa) ndani ya shairi na fani ni njia anazozitumia mtunzi kuyasawirisha maudhui yake kwa hadhira yake.Fani na maudhui huingiliana hutegemeana na kukamilishana.Ni mambo ambayo hayatunganiki, fani hubeba maudhui, na maudhui huathiriwa na fani.Uwiano wa fani na maudhui ndiyo kigezo bora cha ndani cha ubora wa shairi.
Katika fani kuna mambo yafuatayo:- Muundo, mtindo, matumizi ya lugha na jina la kitabu katika kipengele cha lugha kuna mpangilio wa maneno, tamathali za semi, methali, misemo, picha n.k.
Maudhui ni mawazo yanayosemwa ndani kazi ya Sanaa.Mada kuu inayayozungumziwa katika shairi huitwa dhamira.Dhamira inapounganishwa na mtazamo wa mtunzi, Shabaha na ujumbe hupatikana yanaweza kuhusu jambo lolote linalohusika.Maudhui yanaweza kuhusu jambo lolote linalomkera mwanadamu kwa mfano maana ya maisha, mapenzi, mauti, ndoa, elimu, kazi, dini, ukombozi, usaliti n.k.
UHAKIKI WA VIPENGELE VYA FANI
a)      Mtindo wa mashairi
Masharti ya Kiswahili yana mtindo mingi sana katika utungaji wake kwa hakika si rahisi kutambua ama au idadi ya aina za utungaji wa ushairi, kwani hii hususani kutegemeana sana na ufundi wa mtungaji mwenyewe.Baadhi ya mtindo ya utungaji wa ushairi ni kama ifuatavyo
a)      Mtindo wa pindu
Katika utungaji wa aina hii silabi mbil za mwisho wa mstari hurudiwa rudiwa kwa mfano: kama mstari wa kwanza uliishia na neno “fahamu” basi mstari wa pili utaanza na silabi mbili za mwisho, yaani “hamu” wakati mwingine huitwa “Mkufu”
Mfano:   Zipokeeni Salamu, lamu kila na mvita,
              Vita kwa wanadamu, damu zinawezachonyota,
          Nyota njema ni agumu, gumu jema kulipata,
               Pata kwa kuyafuata, fuata mambo mazuri.
         
               Zuri katika dunia, nia mama yanaleta,
               Leta kila la sheria, ria huleta matata,
          Tata watu hujifia, fia ipo kwa kupita,
               Pita usije kupita, pita katika mazuri.
(waniitila, kichocheo cha fasihi simulizi na andishi Uk 224)
b)     Mtindo wa msisitizo
Kuna msisitizo wa aina mbili, kuna msisitizo wa wima na msisitizo wa ulalo
Msisitizo wa wima ni kule kuwa na neno moja likawa linatokea mwanzoni na linarudiwa katika kila mistari wa shairi zima
Mfano:    Ua langu la moyo, nitunzo nipowe
               Ua langu usinitunze, ua nitunze nitowe
               Ua nikae shingoni, ua usinichambue
               Ua la moyo ua, Ua lichanue kwangu
          (Diwani ya Akilimani 1973:63)
Msisitizo wa ulalo ni ule wa kutumia kibwagizo kama kiini cha habari yote inayozungumziwa katika shairi lote na ikawa hicho kibwagizo cha rudiwa rudiwa katika kila ubeti wa shairi
Mfano:    Kokoni kucha kuchile, risala enenda hima,
               Kufika similatile, ulitimavu si mwema,
               Kumbe nao watambule, haya ninayoyasema,
               Iwapo kimya si chema, na maneno hayafai.

               Sipendelei kusudi, na manji mno kusema,
               Nendapo hijitahidi, kimya change hatuzamu,
               Kanama sio mwadi, watu wengine si wema,
               Iwapo kimya si chema, na maneno hayafai.
            (fani na taratibu za ushairi wa Kiswahili 1939:18)
c)      Mtindo wa beti kubadilisha vina.
Iwapo katika ubeti wa kwanza kina cha kati kilikuwa “na” na ile ile cha mwisho kilikuwa “ma” basi katika ubeti unaofuata kina cha kati kitakuwa “ma” na kile cha mwisho kitakuwa “na”.
Mfano:    Kila shairi nalia, chozi latoka machoni,
               Na ninyi mwangalia, wala hamniponzeni,
               Mpenzi kankimbia, naudhika simwoni
               Nirudie we mwandani, roho ipate tulia.

               Nakuomba samahani, magoti nakupigia,
               Nisamehe nuksani, zote nilo kutendea,
               Naapa kwa yangu dini, kamwe sitayarudia,
               Narudia we mwandani, roho ipate tulia.
d)      Mtindo wa kubadilisha vina vya kati toka ubeti ili hali vile vina vya mwisho katika ubeti vikibaki vile vile
Katika ubeti wa kina kina cha mwisho kilikuwa “za” basi kina hicho kitaendelea kujitokeza ubeti mmoja hadi ubeti mwingine wakati vile vya kati vitaendelea kubadilikabadilika.
Mfano:     Jalali wangu mchunga, nikidhi yako rehema,
                Niweke natangatanga, nitabaruku kwa wema,
                Niweke kwenye kiunga,cha malisho ya uzima,
          Na majani ya rehema, na vijito vyenye raha.

                   Tabaruku moyo wangu, nisifikwe na zahama,
                 Pasinifike machungu, kwani u mwenye hunena,
                 Nakutegemea tangu, wala sinayo tahuma,
                 Uniongoze kwa wema, nami nitakutukuza.
           (fani na taratibu za ushairi wa Kiswahili 1986:38-39)
e)      Mtindo wa kidato
Katika muundo huu baadhi ya mistari na maneno yake au silabi zake zina maneno machache au zimefupishwa tofauti na mistari mingine ambayo huwa na silabi au maneno mengi.Ufupishaji huu wa maneno au silabi katika baadhi ya mistari hufanywa kwa lengo maalumu.
Mfano:Tohara, kwa wanawake ni hatari
                Madhara, kwa wake uke, hushamiri
                Hasara, ya peke yake, hudhurika
                Zinduka
              (Wasakatonge 2004:02)
f)       Mtindo wa kuhoji
Huu ni mtindo unaotumiwa na mwandishi wa kuuliza maswali ambayo aidha majibu yake yako wazi au hayako wazi hivyo mtindo huu unaweza kutumika kama tashtiti.
Mfano:     Si wewe?
                Ukinijia mapema kama ukidayatema,
                Nikawa kama wako baba na mama,
                Kakulea kwa ugonjwa na uzima,
                Ni wewe uso hisani.

                Si wewe?
                Niliyekunyima chungu kukutafutia tamu,
                Kila kichota hakisishi hamu,
                Ukazoa bila kufahamu,
                Kuhujua kuichota,
                Ni wewe ujilaumu.
         (Fungate la uhuru 1996:42-43)
g)      Mtindo binafsi
Huu ni mtindo ambao mwandishi anaweza kutumia nafsi ya umoja au wingi au nafsi kundi kila nafsi ina maana yake kimaudhui.Nafsi moja huzungumzia mambo fulani yanayomkabili mtu mmoja tu.Mara nyingi huwa ni maonyo, mawaidha au sifa.
Mfano:     Umeshapwelea nchi kavu,
                Wako werevu umekwisha,
                Sasa tunatweta,
                Utaabani,
                Ni wewe ulo mrafi,
                Si wewe?
         (Wasakatonge 2004:21-22)
Nafsi nyingi hutokea pale mashairi anapozungumzia na kundi fulani la watu huku na yeye akiwa mmojawapo.
Mfano:     Hatukubali tena,
                Kwetu kurudisha ubwana,
                Kwetu kuurejesha utwana,
                Kwetu kuurejesha utumwa.
                Hatukubali katu,
                Ndani ya nchi yetu.
                Hiyo huru.
          (Wasakaonge 2004:30-31)
Lakini nafsi kundi hutoka pale ambapo mwandishi au msanii anapozungumza na kundi la watu huku yeye akiwa ama msimulizi.Hutoa masimulizi kama hadithi au hotuba fulani.
Mfano:     Jua kali ni wasakatonge.
                Wao ni wengi ulimwenguni
                Tabaka lisilo ahueni
                Siku zote wako matesoni
                  Ziada ya pato hawaoni
               Lakini watakomboka lini?
                (Wasakatonge 2004:5)
h)     Mtindo ambao unaruhusu kipande kizima cha mstari wa mwisho wa ubeti kuweza kurudiwa, kikiwa ni chanzo cha huo ubeti unaofuata:-
Iwapo mstari wa mwisho wa ubeti wa kwanza ulikuwa kama “Uwanjani nayanena, leo wote wataona” Basi ule mstari wa kwanza na ubeti wa pili utaanza na “leo wote wataona”
Mfano:    Chochote ulichonacho, kilikuwa kwa mwenzako,
               Leo yeye hako nacho, kimesha hamia kwako,
               Huenda utokwe nacho, kiende kwa mwingine huko,
               Kiumbe wacha vituko, sione ulichonacho.

               Sione ulichonacho, ukaendesha vituko,
          Na upambwe chokochoko, mwishowe ni pukutiko,
               Malao akupambacho, kilipambiwa mwenzako
               Kiumbe wacha vituko,sione ulichonacho.
         (Sheria za kutungo mashairi na Diwani ya Amri 1967:30)
Kimsingi mitindo katika ushairi ni mingi sana na hutegemea ufundi wa mshairi katika kuunda mashairi yake na ushair unaweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa.
ii)  Miundo ya Mashairi
Muundo ni neno pana ambalo hujumlisha mjengo wa shairi yaani jinsi ulionekana.Mashairi yana mundo mbalimbali kutegemea ufundi wa mshairi mwenyewe kimsingi Shairi linaweza kuwa la kimapokeo au likawa Shairi huni (kisasa) Shairi la kimapokeo huwa na mpangilio maalumu wa vina na mizani, silabi, vituo, beti n.k.Idadi ya mistari huzaa aina mbalimbali za mashairi.
a)      Muundo wa Tarbia         
Kila ubeti wa shairi huwa na mistari mine na kila mstari huwa na mizani kumi na sita (16) vile vile katika muundo huu kila mstari unakua umegawanika katika viande viwili vilivyo na mizani sawa kila kipande kukiwa na mizani nane.
Mfano:     Amkeni kumekucha, wakubwa hata wadogo,
                 Wadoho siku waacha, kwa kuogopa kinyongo,
                 Kinyongo sikuficha, kukificha ni uongo,
                 Mnapowacha madogo, na makubwa mtawaacha.

                 Na wakubwa mtawaacha, mnapoacha madogo,
                 Mfano kama kuchacha, chakula japo kidogo,
                 Kidogo kinapochacha, kikubwa hakina kingo,
                 Mnapowacha madogo, na wakubwa mtawaacha.
      (Masahiri ya Saadani 1972:25)
b)     Muundo wa Tathnia
Kila ubeti wa shairi huwa na mistari miwili muundo huu unatiwa zaidi katika nyimbo si muundo ambao hutumika sana katika mashairi ya kawaida ya kusomwa kam mashairi au ya kuimbiwa.
Mfano:    Mjamzito, umelazwa “Thieta”
                  Lazima kupasuliwa
                 Chake kitoto tumbo kinatweta
                  Hawezi kujifungua
                 Mwili u moto, tumbo linamkeketa
                  Kwa kite anaunguwa
                 Jasho na Joto, kiungo cha mpwita
                  Na mauti yanamwita
                 Ni jambo zito, daktari kufata
                  Wauguzi waameitwa
(Fungate la uhuru 1988:08)
c)      Muundo wa Tathilitha
Kila ubeti wa shairi unakuwa na mistari mitatu
Mfano:    Kujitawala si kwema, kuliko kutawaliwa,
                Kujitawala ni umma, kila yao kuamua,
                Kujitawala si kama, wanguzi na rushwa.


                Kujitawala khatamu, na umma kushikiliwa,
                Kujitawala hukumu, makosa kushitakiwa,
                Kujitawala si sumu, mara kwa mara kuuwa.

                Kujitawala kisomo, kupiga kubwa hatua,
                Kujitawala kilimo, njaa na kuondoa,
                Kujitawala si somo, njiani kusimuliwa.
d)     Muundo wa Takhimisa
Kila ubeti wa shairi unakuwa na mistari, mitano
Mfano:     Hao nyani wanaruka, mara hapa mara kule,
                 Hao nyani wanabweka, hawaoni soga mbele,
                 Hao nyani wanaanguka, waingiwa na ndwele, 
                 Nyani wanababaika,misitu una upele
                 Msitu haukaliki, nyani wanahangaika.

                 Msitu wawaka moto, kufukuzwa hao nyani,
                 Umeligundua pato, la nyani lenye utani,
                 Moto waziona kwato, zilizoko mapangoni,
      Nyani watupa watoto, hawakubaliki mwituni
                 Msitu haukaliki, Nyani wanahangaika.
e)      Muundo wa Sabilia
Katika muundo huu mtunzi au mshairi anakuwa na uhuru wa kuweka zaidi ya mistari mitano katika kila ubeti, ubeti unakuwa na mistari sita na kuendelea
Mfano:     Mmea unapokuwa, huifurahisha mvua.
                 Lakini siposogea, hulisingizia jua
                 Uliamini ni mola, hata maji kukupatia
                 Ulikubali kabila, haliishi bila mila
                  Mwanadamu kadhalika, kukua kufurahika
                 Huupenda uhakika, wa nyota yake kufika
                 Umri wa kuridhisha, huhitaji kujitwisha
                 Hapa, ukiufikisha, huona, kufanikiwa
                 Maisha ya hupenda, ni, mazuri ya kwenda
          Na siyo yenye kupinda, haya daima hupenda
                         (Diwani ya Mloka 2002:18)
f)       Muundo wa mistari mine
Muundo huu unaweza kuwa na mizani nane au pungufu.Muundo huu ni wa Abdilatifu Abdalla (1973) mfano ametumia katika mashairi yake ya “Kamili wazi” “mnazi” “Jana na leo na kesho” na “Njia panda” mara nyingi huo mstari wa mwisho kina chake huwa ni sawa na kina cha mwisho wa mstari mwingine katika ubeti wao
Mfano:     Kimbunga mji wa Siyu, kilichowahi kufika.
                 Si kwa yule wala huyu, ilikuwa patashika
                 Kimeingoa mibuyu, minazi kunusurika
                 Nyoyo zilifadhaika
                 (Kimbunga 1995:01)
iii)   Matumizi ya Lugha.
Hiki ni kipengele muhimu sana katika kazi yeyote ile ya Sanaa ya kifasihi. Matumizi ya Lugha ndiyo yanayofanya kazi fulani ionekane tofauti na nyingine au itofautishe kazi ya Sanaa ya kifasihi na ile isiyo ya kifasihi.Luha ndiyo mzizi wa kazi ya fasihi kwani fasihi ni kazi ya Sanaa inayotoa maudhui ya kutumia Lugha ya maneno.Matumizi ya Lugha katika kazi ya fasihi yako ya aina mbalimbali
a)      Methali, misemo na nahau
Mhakiki anapaswa avifahamu na ajue kuvichambua katika ushairi.Vipengele hivyo vina kazi ya kufafanua maudhui ya kazi ya fasihi

METHALI
Ni kazi ya Sanaa ya kifasihi inayotumia mafumbo kwa kwaida semi zote zina hakima ndani yake.Ubora wa hekima hiyo hutegemea muktadha hali ambapo methali hutumika.Methali pia ina kazi ya kufurahisha, kutisha, kuonya nakadhalika, waandishi hutumia methali katika kazi zao nani jukumu la mhakiki kuzitambua hizo

MISEMO NA NAHAU
Matumizi ya misemo na nahau hushabihana na yale ya methali.Misemo, misimu na nahau huzaliwa, hukua nap engine hufa
      -Sekela amenipaka mafuta kwa mgongo wa chupa (sekela amenipa sifa zilizostahili)
      -Juma katutangulia (Juma amekufa)
b)     Tamathali za Semi
Mulokozi & Kahigi wanasema kuwa tamathali za semi ni maneno, nahau au semi ambazo hutumiwa [H1] na waandishi wa fasihi ili kutia nguvu na msisitizo katika maana, mtindo, na pengine sauti katika maandishi hayo.Tamathali za semi zinatumiwa pia [H2] kuipamba kazi ya Sanaa ya kifasihi kwa kuongeza utamu wa Lugha.
Baadhi ya tamathali za semi ni:-
Ø  Tashbiha
Hii ni tamathali ya ufananisha au mlinganisha wa vitu viwili au zaidi katika tashbiha kama ilivyo katika sitiari huwa kuna vitu vitatu vinavyofananishwa ambavyo wataalamu wameviita kuzungumzwa, kufananisha na kiungo.Katika tashbiha hakuna maana dhahania bali kuna ulinganishaji wa vitu viwili vilivyobayana.
Mfano:     Kweli ni sawa na radi, inapotoa kauli…
          Kweli kinywnani ikiwa sawa na moto wa nili
                 Kweli kama msumeno hukoreza sawa kweli
Ø  Tashhisi (uhaishaji)
Washairi mara nyingine huweza kukipa kitu kisichokuwa na uhai sifa za kitu chenye uhai, hasa sifa za binadamu, kisanaa maelezo ya kitashhisi huwa na upekee unaomwingia msomaji akilini haraka, kwani si jambo a kawaida, mathalani kuona mti “Ukimpungia mtu mkono” au “nyumba ikimkodolea macho mgeni”
Mfano:     kimya hakineni jambo si kimya chawatazama…
              Kimya chajazua mambo, pasiwe mwenye kusema.
              Kimya kipimeni sana, msione kutosema.
              Kimya hakichi kunena, kitakapo kusimama.
              Kimya chaja watukana, na kizuwe yalozama.
Katika ubeti huu “kimya” (ambayo ni nomino dhahania) kimepewa sifa za binadamu kinaweza kunena, kutazama, kuzua mambo, kusimama na kutukana.

Ø  Metonumia
Hii ni tamathali inayotumia neno (au semi) kuwakilisha neno, kitu, mtu au dhana nyingine yenye kuhusiana nalo neno hilo huweza kutumiwa kwa kuwa dhana inayozungumziwa au kwa kuwa linataja ktu ambacho ni sehemu na kuwakilisha cha kitu kingine kikubwa zaidi.
Mfano neno “kitambi” huweza kutumiwa kuwakilisha tajiri au kabila “meno” huweza kuwakilisha kicheko

Ø  Mubalagha
Ni matumizi ya lugha yaliyotiwa chumvi ili kuongeza utamu na kuleta athari fulani katika ushairi wa majigambo, tamathili hii hutumika sana maana huo ni ushairi wa kujitapa na mtu mwenye kujitapa aghalabu hujilimbikizia sifa. Mara nyingi mubalagha hutumika katika tenzi zenye kusimulia habari za mashujaa.
Mfano: katika utenzi wa fumo Lyongo kuna mfano unaokusudiwa kuonyesha ukubwa wa (kimo na umbo) na nguvu za Lyongo.
              “Ruhu zikienda kishindo
                Zima zao hukoma ondo
                Huyo ni bwana wa kondo
                Ashindaye jeshi miya
Ingawa wagala wanajulikana kuwa ni watu warefu akini vimo vyao vilifika magotini tu (ondo) pia Lyongo

Ø  Kejeli
Ni usemi ambao maana ya ndani ni kinyume cha maanayake halisi. Ni usemi wa kebehi ambamo kisemwacho na msemaji. Pia kejeli ni tukio ambalo ni kinyume cha lile linatazamiwa au lililotakiwa na ambalo kutokea kwake huwa ni namna ya dhihaka
Katika shairi la “Ibada na Haki” Shabaan Robert anatumia usemi wa kejeli kukebehi watu wanothamini fedha kuliko dini.
Anasema hivi:    Huifanya fedha mungu wao
                         Itazame adha na Imani yao!
                         Na mwenye akili kama hana fedha
                         Hatajwi mahali ila kwa rakadha
                         Na kuadhiriwa kuwa mtu chini,
                         Tazama dunia ilivyo na dini
Katika mstari wa pili “Itazame adha na Imani yako!” kuna kejeli, mshairi anachotaka kutuambia ni kwamba watu hao hawana adha wala Imani katika mstariwa mwisho “Tazama dunia ilivyo na dini” Anakusudia kutuambia
“Tazama dunia ilivyo na dini kwa hiyo semi hizo ni kejeli kinachosemwa ni kinyume na maana yake halisi kadha toka alama za mshangao!) zimetumika kusisitiza hali ya kejeli.
                                         
            MBINU ZA KISANAA
Kuna mbinu mbalimbali za kisanaa ambazo hutumika katika kazi za kifasihi ya ushairi na ambazo mhakiki atatakiwa azitambue na kuzifafanua mbinu hizo ni kama vile
Ø  Takriri
Ni kurudia rudia neno, sauti, herufi au wazo katika kazi ya Sanaa ya kifasihi.
Mfano:     kweli kito mhabubu, mwenyezi nijaze kweli
              Kweli siri ya ajabu, huwapa watu fadhili
                Kweli chimbo la johari, linahimili la kweli
                Kweli inatafakari, husema na kujadili
Katika ubeti huu neno “kweli” limerudiwa rudiwa. Neno hili linasisitiza wazo kuu la mwandishi
Ø  Onomatopea
Ni mwigo wa sauti. Hutumiwa na washairi kutoa picha au dhana ya kile kinachowakilishwa au kupambanuliwa na sauti hizo. Mfano tukisema “maji yalimwagika mwaaa!” neno mwaaa! Ni onomatopea linawakilisha sauti au kishindo cha maji yanayomwagika. Baadhi ya onomatopea ambazo zimekwisha kuwa sehemu za msamiati wa kawaida. Mfano: pikipiki, bomboni, kata n.k.
Katika shairi la “Cheke kwa furaha” Shabaan Robert ametumia onomatopea ili kuleta dhana ya kucheka
               “Dhiki ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?
                 Haya cheka ha! ha! ha! Ndiyo ada duniani
                 Basi cheka kwa! kwa! kwa! Usafike moyo wote
                 Pamoja na malaika, wema mbinguni waliko
Maneno ha! ha! ha! na kwa! kwa! kwa!  Ni onomatopea yanayotoa sauti ya kusikika ya sauti ya mtu anayecheka. Huu ni mpangilio maalumu wa sauti ili kutoa picha ya kusikika ya dhana inayozungumzwa
Ø  Mjalizo
Ni kuunganisha maneno yanayofwatana bila kutumia viunganishi mfano: bila kutumia “na, kwa” n.k. Mfano:  Nilikaa, nikashangaa, nikachoka
                    Niliimba, nikanuna, nikacheka
Ø  Mdokezo
Hii ni mbinu ya kisanaa ambapo mwandishi anaukatiza usemi fulani na kumuacha msomaji. Aghalabu pana vielekezi vinavyoweza kumsaidia msomaji katika kukamilisha.
Mfano:     wimbo la mauaji limezidi
                Mashaka…ah! Shida tupu
                Maneno…tena anyway…
                Labda tusubiri.
Ø  Tashtiti 
Ni matumizi ya maswali ambayo majibu yake kwa kawaida yanakuwa yameeleweka. Swali hili linakuwa yameeleweka. Swali hili linakuwa kwa ajili ya msisitizo tu au mshangao.
Mfano:  Mtu anayemfahamu amekufa anauliza
               -Adela ameachana nami?
            Au mtu anayemfahamu amekutembelea
             - Jamani hata Luiza naye kaja?
             -Aisee ni wewe?
Ø  Usambamba
Ni takriri ya sentensi au kifungu vya maneno vyenye kufanana kimaana au kimuundo. Usambamba huonekena sana katika ushairi simulizi
Shabaan Robert amekitumia kipengele hiki mara kwa mara atika mashairi yake katika shairi lake “kinyume” anasema
            Tulifululiza mwendo lakini sana twasita
            Tulikwenda kwa mshindo lakini sana twanyata
Katika mistari yote miwili wazo linalosisitiza ni moja maneno tu ndiyo yanabadilika uwezo wao wa zamani katika utendaji mambo unalinganishwa na udhaifu “wao” wa sasa.
c)      Taswira au Picha
Dhana hii hutumiwa kueleza neno, kirai au maelezo ambayo yanaunda picha fulani katika akili ya msomaji. Taswira zinaweza kuwa za kimaelezo (yaani maelezo fulani yanaunda picha) au za ki-ishara (zinazounda picha ambayo inaashiria jambo fulani au imeficha ujumbe mwingine). Taswira huweza kuundwakwa matumizi ya tamathali za semi hasa tashbiha na sitiari.
Kimsingi taswira nyingi ni taswira za uoni (yaani zinamchochea msomaji kuona picha fulani)
Mfano:     Neno lenye mzunguko, halipatikani mwisho,
            Wa huku hafiki huko,wala halina matisha.
                Halishibishi huchosha, wala hapati utuvu,
                Heri ya mtu ni kwenda, njia iliyonyooka.

                Na milima akapanda, apendako akafika,
                Mabondeni akashuka, mwituni akatumbua,
                Na mzunguko wa dira, mwisho wake ni dinani
                Hupati kupenda bara, na hushuki baharini
                Tazama mashaka gani, njia ya dira si njia
Katika shairi hili tunapewa picha tatu mahususi picha ya kwanza ni neno linalozunguka mshairi anatuambia kuwa neno ambalo halifuati njia iliyonyooka neno lenye mzunguko halifiki mwisho wake na halileti mradi uliokusudiwa “Halina malisho”
Hapa neno limefanya kuwa kitu chenye uwezo wa kutembea na kuzunguka

Picha ya pili ni ya mtu aendaye safari ngumu kwa ujasiri na moyo wa dhati akipanda milima na kushuka na mabonde akipenya misitu na kuvuka mito hadi kufika kule anapokwenda. Huyu ni mtu asiyeogopa matatizo anayeshikilia njia ngumu lakini nyoofu, alimradi anajua kuwa itamfikisha kwenye lengo lake. Ni mtu anayepamana na matatizo badala ya kuyakimbia mtu wa kwenda njia iliyonyooka

Piha ya tatu ni dira, dira ni chombo kitumiwacho na mabaharia na wasafiri wengine kusahihisha majira yao, wasipotee njia. Dira ni chombo cha mviringo na mshale wake aghalabu huzungukia palepale ulipo, katu hautoki nje ya dira. Picha hii inasisitiza wazo la mwandishi kuwa njia yenye kuzunguka haiwezi kumfikisha mtu kwenye lengolake. Mshale wa dira huzunguka daima lakini haufiki kokote.
Picha hizi tatu kwa pamoja zimefaulu kufikisha ujumbe wa mwandishi kuhusu maisha na namna ya kuyakabili tuyakabili kwa juhudi na ujasiri na nia.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu ni vyema liwiane na yale yaliyomo ndani ya kitabu hicho. Mfano: “Fungate la uhuru” (1988) jina hili linawiana vipi na yale yaliyomo ndani ya kitabu hicho?
PICHA YA JALADA KATIKA UCHAMBUZI
Kazi ya kifasihi kuwa na picha au michoro fulani kwenye majalada yao. Inawezekana majalada hayo yakawa na uhusiano fulani na dhamira na maudhui ya kazi zinazohusika. Picha hizi huweza kuwa kielelezo muhimu cha fani kwenye uchambuzi wa kazi ya kifasihi. Hata hivyo si kazi zote za kifasihi ambazo zinaonyesha uwiano kati ya majalada yake na yaliyomo.
UHAKIKI WA VIPENGELE VYA MAUDHUI
Maudhui katika mashairi hupatikana baada ya mhakiki kupitia beti zote za shairi lile ili kupata ujumbe wa shairi lazima itambidi mhakiki ajumlishe yaliyo katika beti mbalimbali za shairi lile.
Kwa ufupi katika ushairi uchambuzi wa maudhui mhakiki anapaswa kuangalia:
Ø  DHAMIRA
Ni wazo kuu katika kazi ya fasihi.
Ø  UJUMBE
Ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazifulani ya fasihi.
Ø  FALSAFA YA MWANDISHI
Ni wazo ambalo mtu anaamini lina ukweli fulani unaitawala maisha yake.
Ø  MSIMAMO WA MWANDISHI
Ni hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili linaweza kuwa halikubaliki na wengi, lakini yeye atalishikilia tu.
Ø  MTAZAMO WA MWANDISHI
Ni hali ya kuyaona mambo katika maisha kwa kuzingatia mazingira aliyonayo msanii mwenyewe

HATUA ZA UCHAMBUZI WA USHAIRI
Katika uchambuzi huu wa vitendo, kielelezo tutatumia shairi la “Wauwaji wa Albino wapigwe vita” Shairi hilo linasema hivi:
Kwa kweli inashangaza, ni mambo hufikirika,
Ukijaribu kuwaza, wenzetu wanatutukana
Albino wanaweza, kifo kimeshawafikia
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

Ni unyama wa kuzidi, albino kuwashika
Huu wote ni ukaidi, utajiri kuusaka
Tena ni kwa makusudi, maovu umeyashika
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

Mikononi wanawakata, kwa mashoka na mapanga
Kuwasema sita sita, huu wote ni ujinga
Kwa vitisho wajikita, kusikiliza waganga
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

Albino tuwalinde, wamekuwa almasi
Wasakwa kila upande, sababu ya ibilisi
Yatupasa tuwalinde, binadamu kama sisi
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

Majumba kuyabomoa, pande zote kuzunguka
Damu isiyo hatia, kwa wingi inamwagika
Mola inamlilia, hukumu ipo hakika
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

Albino ni wenzetu, uzao wao ni halisi
Acha tofauti zetu, tena tuwape nafasi
Tujenge taifa letu, tuuache ukakasi
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

Ujinga na upumbavu, kuwaua albino
Wajawa maumivu, mikono na visigino
Sahitaji utulivu, upole mshikamano
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

Zamu yako inakuja, mwisho wao utafika
Wenyewe watajitaja, tena bila ya mashaka
Sote tuwe na umoja, kufungua mashtaka
Kuwasaka wauwaji, kusudi wahukumiwe.


HATUA ZA KUCHAMBUA SHAIRI
1.      Lisome shairi zima toka manzo hadi mwisho ili upate picha ya jumla, kimaana na kiumbo ya shairi hilo. Katika hatua hii kama shairi ni gumu linaweza lisieleweke, kwa bahati shairi la “wauwaji wa albino wapigwe vita” linaeleweka bila tatizo
2.      Rudia kulisoma tena shairi hilo polepole, andika maana ya jumla unayoipata. Unaweza kupata maana zaidi ya moja katika “Wauwaji wa albino wapigwe vita” maana ya jumla inayojitokeza ni maombolezo ya mauwaji ya Albino
3.      Huku ukiwa na kalamu yako ya risasi, rudia kulisoma tena shairi hilo mstari baada ya mstari. Pigia kila neno usemi, sentensi au kipengele kinachoelekea kuwa na umuhimu au dhima maalumu ya kifani au kimaudhui.
Katika shairi ili pengine utayapigie mstari mafungu ya maneno yafuatayo:
            -Albino wanaweza kifo kimeshawafikia
            -Ni wauwaji wabaya vikali walaaniwe
            -wasakwa kila upande sababu ya ibilisi
            -damu isiyo hatia kwa wingi inamwagika
            -Albino ni wenzetu uzao wao ni halisi
4.      Jaribu kufanya kisisisi maneno hayo yalyopigiwa mstari au kuorodheshwa katika hatua ya tatu bila shaka yapo mambo ambayo undani wake hutauelewa katika hatua hii, hivyo aghalabu itabidi
a)      Urejee mambo hayo yalivyotumika
b)      Urejee katika muktadha wa shairi hilo kama una ufahamu kwa upande wa wauwaji wa Albino wapigwe vita, muktadha huo ni mauaji ya Albino
Jiulize semi, sentesi hizi zinasema/zinaonyesha au zinadokeza nini? Kwa nini mtunzi kaamua kutumia maneno hayo na si mengine? Je yanahusiana vipi na maana ya jumla uliyopata katika hatua ya pili.
5.      Chunguza vipengele vingine vya kisanaa na kimuundo alivyovitumia mtunzi. Jiulize kama vinaoana na madokezo ya maana uliyoyapata katika hatua ya nne. Vipengele unavyoweza kuchunguza katika hatua hii ni muundo wa shairi, vina, mizani, wizani, takriri, milio ya maneno, tamathali n.k. kwa mfano hadhihirika kuwa muundo wa shairi ni kijadi ambao hautuambii lolote kuhusu maana ya shairi hili vifanye uchambuzi vipengele vya kisanaa ulivyovipambanua
6.      Husisha ufafanuzi wake hadi hatua hiina maana ya shairi iliyokwisha kujitokeza kuona kama mambo hayo yanaoana barabara au bado kuna pengo au mkinzano.
Baada ya hatua hii utakuwa umepata maana kamili ya shairi ambayo unaweza kuitetea kifasihi kwa kurejea katika shairi lenyewe si lazima maana unayopata/unazopata ioane/zioane na maana watakazopata wengine jambo muhimu ni kuwa na ushahidi wa kutosha kuweza kutetea hoja zako.
Maana ambayo umepata hadi sasa yaweza kuelezwa iwe:
Mshairi anaomboleza mauaji ya Albino ambayo yanafanywa na  watu mbalimbali kwa Imani za kishirikina anaonyesha kuwa kuua binadamu wenzetu ni unyama na ni ukatili. Anamwomba Mungu awaepushie Albino na mates ohayo.
7.      Hadi hatua hii umepata maana ya shairi lakini bado hujapata maudhui yake. Ili kupata maudhui unatakiwa upambanue dhamir kuu ya/za shairi hili na uonyeshe mtazamo wa mshairi kuhusu dhamira hizo. Katika shairi hili ni dhahiri dhamira kuu ni “Mauaji ya Albino” mtunzi anasawiri tukio la mauaji ya Albino mwandishi anaonyesha kuwa mauaji ya albino ni tukio lenye kuleta majonzi na kilio. Mtazamo wake kuhusu mauaji ya Albino ni kwamba wanaofanya hivyo hawana utu hivyo ni sawa na wanyama wa porini na anaonyesha kuwa kuwaua albino ni kinyume cha utu
Mtunzi anazungumzia pia dhamira ya ujinga. Mwandishi anaonyesha kuwa ujinga ni kikwazo cha maendeleo ya jamii kwani wote wanaojihusisha na mauaji ya albino ni wajinga na wanataka kupata utajiri kwa njia za mkato.
8.      Katika hatua hii mchambuzi ana uhuru wa kuithamini kusifu au kwaani. Baada ya kulichambua na kulielewa vizuri shairi hilo katika hatua saba zilizotangulia sasa unaweza kulitolea tathmini ya kifani na kimaudhui katika kufanya tathmini ni muhimu kuzingatia muktadha wa wakati lilipotungwa na wakati wa leo.
Tathmini yako itazingatia muktadha yote miwili unaweza kusema kuwa, shairi hilo lilipotungwa ulikuwa na umuhimu wake leo labda umepungua kwa kuwa muktadha huo wa vifo vya Albino umepita. Hata hivyo labda shairi limebaki na umuhimu wa kihisia na kifalsafa kuhusu tatizo la maisha na mauti na ufumbuzi wake.

HISTORIA NA MAENDELEO YA KISHAIRI WA KISWAHILI
Wataalamu wengi wanakubali kuwa ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi hasa ngoma na nyimbo. Kabla ya karne ya 10 BK ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa na kugharura kwa ghibu bila kuandikwa.
Kuanzia mwaka 1000 B, mambo mawili yaliletwa na kuathiri ushairi, mambo hayo ni Dini ya kiislamu na Uandishi wa hati ya kiarabu waswahili wengi walijifunza kusoma na kuandika hati za kiarabu, hali hiyo ilienda sambamba na ustawi wa miji ya Pwani katika biashara na majengo ya mawe mashujaa mashuhuri wa miji ya Pwani wanokumbukwa katika tendi na masimulizihuenda waliishi katika hicho ni Fumo Lyongo wa Shangapate kaskazini mwa upwa wa Kenya kati ya karne ya 8 na 9
Katika kipindi hiko washairi wengi walitunga mashairi mengi kwa ghiba kwa sababu hayakukusudiwa kuhifadhiwa kwa maandishi kwa kipindi kirefu ni tarihi na baadhi ya mswada hiyo imepotea. Tungo zilizosalia ni Fumo Lyongo ambayo ilandikwa 1500 BK kutoka katika mapokeo ya mdomo.
-“kumswifu” yanga au suifa ya mwana ning utingo wa mwanzo kuhifadhiwa kwa maandishi.
Mwaka 1500-1700 BK kulikuwa ni kipindi cha uvamizi wa maneno katika kipindi hicho tungo chache zilihifadhiwa zikiwasifia maneno mashairi yaliyo wasifia wareno> mfano
            -mzungu mgeli} 1630
            -Portugezi Afala} 1630
Lakini tungo mashuhuri za wakati huo ni:
·         Utendi wa Hamziyya (Seyyid Aidamis bin Athumani 1652)
·         Siri lasirari (Binti Lamba 1668)
·         Utendi wa Tambika (Taboka) {Mwango bin Athumani 1728}
·         Siri Lasirari ni kisa cha kubuni
·         Hamliyya ni tafsiri ya utendi wa kiarabu kuhusu maisha ya Mtume Muhamadi
·         Tabuta (tambuka) ulihusu vita kati ya waislamu na warumi walikuwa chini ya mfalme Hela kali
1750-1900 kipindi cha waarabu
Sehemu kubwa za tendi mashuhuri za wakati ambazo mpaka leo zipo ni:
·         Tendi za dini na vitu
-          Utenzi wa Shufaka
-          Utenzi wa masahibu
-          Utenzi wa kijamaa
-          Utenzi wa mayasa na mikidadi
-          Utenzi wa Ras L Ghuli (unahusu vita vya waarabu kati ya waislam na makafiri-{1855})
·         Tungo za kitamaduni, mawaidha na Tumbuiza
Tungo hizi zilikuwa nyingi na zilikuwa katika maandishi na zilihusu (maudhui yake) kueleza mandhari ya Afrika Mashariki mfano tungo hizi ni:
-          Utenzi wa Inkishafi (1810)
Mtunzi: Seyyid Abdallah bin Nasri.
Utenzi huu unazungumzia matokeo ya uvamizi wa waarabu na wareno ambapo matokeo yake ni kuporomoka kwa mji wa Pate.
-          Utenzi wa Mwana kupona (1858)
Unahusu utamaduni na misingi ya Dini. Utenzi huu uliandikwa kama wosia kwa binti yake na kwa kiasi kikubwa unahusu unyumba pia ndani yake kuna mafundisho ya unyago kwa watu wa Pwani.
Kundi jingine kubwa ni mashairi ya siasa kundi hili liliwakilisha/lilisimamiwa na akina Muyaka bin Haji wa Mombasa. Huyo alitunga mashairi ya kupinga waarabu wa Oman mfano;Suid bin Said (1810-1876),Kibabina (1776-1834) na wengine.
Wote hawa walitunga mashairi yaliyohusu harakati za kisiasa na kijamii za wakati huo, wa baadhi yao walifungwa au kuuwawa gerezani kwa sababu ya kupinga kutawaliwa. Mchango mkubwa wa hawa ni kuendeleza mashairi ya unne (tarbia)
Kwa ujumla katika kipindi hiki mambo yaliyojitokeza katika maendelezo ya ushairi ni manne:
i)        Umbo la tarbia (unne) ulifika kilele
ii)      Utendi
iii)    Kanuni ya utunzi ziliwekwa wakati huo
iv)    Hati ya maandishi (Kiswahili n kiarabu) ilisanifiwa kuzingatia sauti za lugha ya Kiswahili.
1885-1918 USHAIRI WAKATI WA UKOLONI WA KIJERUMANI
Ushairi wa wakati huo unaweza kugawanyika katika makundi matatu.
i)        Ushairi wa kawaida-mashairi haya yalihusu mawaidha, mapenzi na dini.
ii)      Ushairi wakusifu wakoloni- huu uliandikwa kwenye magazeti na vitabu mfano kitabu maarufu cha Dr. C
Velter (1907) Prose and Poesie der Sua heli
Kitabu hiki kilisifu utawala wa kidachi
iii)    Ushairi wa upinzani.
Huu ulipinga utawala wa kikoloni.
Mfano: utenzi wa vita vya wadachi (H.Abdallah)
            Utenzi wa vita vya majimaji
Katika kipindi hiki mambo matatu yalitokea katika ushairi kwa upande wa Tanzania.
a.      Kuandika kwa kutumia hati ya kirumi hati hii ulienea kwa kupitia Elimu kanisa na ilianza kutumiwa na watunzi baada ya hati ya kirabu
b.      Utafiti kuhusu ushairi ulianza wakati huo na wachambuzi maarufu walikuwa C.Velter Buttner na K.Mein holf n.k
Hawa walisaidiwa na waafrika kama vile Mohamed Kajunwa, utenzi wa Fumo Lyongo Rev.Taylor ndiye aliyekusanya mashairi ya Fumo Lyongo.
1918-1961 UKOLONI WA KIINGEREZA
Kipindi hiki kiliambatana na mambo matatu mapya:-
a)      Elimu .Hii ilieneza lugha ya Kiswahili na ushairi katika maeneo ya bara kupitia shuleni maarifa ya kusoma na kuandika. Hati ya maandishi ya kirumi ilienea kupitia elimu
b)     Kuanzishwa kwa mashirika ya uchapishwaji.Katika kipindi hiki magazeti mengi yalichapwa kwa lugha ya Kiswahili na kusambazwa. Baadhi ya magazeti yalikuwa na kurasa maalumu ya ushairi ambapo ulisaidia kuwakutanisha watunzi kutoka Afrika Mashariki.
Mfano: Gazeti la “Mambo leo” 1923 kupitia gazeti hilo watunzi maarufu kama S.Robert, Mdanzi Hamasa, Mzee Waziri (kijana) walipata umaarufu kupitia mambo leo
Pia kuanzishwa kwa shirika la wachapishaji vitabu Afrika Mashariki (E.A.L.B) kulisaidia sana kukuza na kueneza Sanaa ya ushairi.
c)      Shughuli za siasa za kudai Uhuru ziliibua ushairi wa kisiasa mnamo mwaka 1950-1960.
Mfano: S.Kandoro alitunga mashairi mengi pia kipindi hicho ushairi ulikuwa wa aina.
1.      Mashairi yaliyosaili mfumo wa uchumi wa kikoloni. Matatizo ya kazi, umanamba, mshahara mdogo n.k haya yote yalitolewa na gazeti la mamba leo.
2.      Mashairi yaliyohusu utaifa yalianza miaka 1930. Haya yalijiuliza mwafrika ni nani? kwa nini mzungu yupo hapa?
Mfano:     S.Robert- mashairi ya kutetea weusi mfano Shairi la Rangi zetu,S.Kandoro kwetu ni kwao kwa nini
 Pia kulikuwa na mashairi ya kutetea Lugha mfano S.Robert (Titi la mama li Tamu)  S.Kandoro (Kitumie Kiswahili)
3.      Mashairi ya kisiasa ambayo yalihimiza watu waungane ili waweze kujitawala wenyewe S.Kandoro shairi la siafu wamekazana
4.      Pia kipindi hiki walitokea wachunguzi wengi sana wa ushairi wa Kiswahili.
Mfano:     Withchens (1930), A.Wine, B.E.Damman (1930-50) Lumbart, H.Cory W.Whitely n.k. “wazungu”. Waafrika Sr. Mbarak Hisway, Hamis Kitumbey
USHAIRI BAADA YA UHURU
Baada ya uhuru ushairi ulisambaa zaidi kutokana na msukumo wa kisiasa fani mpya mfano Ngonjera na mtiririko au tungo huru zilizanziashwa ili kuzingatia mahitaji mapya ya kisiasa na kisanaa. Ushairi wa Kiswahili baada ya uhuru ulikuwa wa aina kuu mbili
1.      Mashairi ya kawaida: Haya yalitungwa sana magazetini na vitabu vya mashairi mbalimbali vilichapishwa ambapo Dhamira za malezi, mapenzi , dini, mawaidha n.k.
o   Akilimali snow- white
o   Mwinyi khatibu- Mohamed
o   Andanenga
o   S.Kandoro
o   S.Robert
2.      Mashairi ya kisiasa: Hapa kuna makundi mbalimbali ya mashairi ya kushangilia Uhuru.
Mfano: Utenzi wa uhuru wa Tanganyika
             Utenzi wa jamhuri wa Tanzania
             Utenzi wa uhuru wa Kenya.
a)      Mashairi yanayojadili dhamira ya ujenzi wa jamii mpya. Katika mashairi yao walisisitiza watu wafanye kazi ili kuinua pato.
Mfano: S.Kandoro katika shairi la kujitawala
            J.K.Nyerere-chombo cha taifa letu
b)      Mashairi ya Ujamaa
Hayo yalitokea baada ya Azimio la Arusha ambalo yalisisitiza siasa ya ujamaa na kujitegemea, ambapo walipinga unyonyaji, ukupe, ukabila na ubepari. Walitukuza kilimo na kuwashawishi watu kurudi shamba (kijijini)
Mfano: Mashairi ya Azimio la Arusha (kamaji), Ngonjera za Matias Mnyapara, Mashairi ya miaka 10 ya Azimio la Arusha (    Abdulah)
Tatizo kubwa lilijitokeza katika hiki ni ukasuku ambapo waandishi wengi walikariri hotuba za viongozi bila kuzifanyia uchambuzi na kuziandikia mashairi.
c)      Mashairi yaliyohakikii siasa yaliyokuwepo na hawa walikuwa na mitazamo mbalimbali.
·         Wanauhalisia
Walihakiki dhana ya ujamaa na ukombozi na kuchambua mafanikio ya matatizo yake hasa katika utekelezaji wa malengo ya Azimio la Arusha. Waandishi hao ni E.Kezilahabi, E.Husein, Z.Mochiwa na T.A.Mvungi.
·         Washairi wa Malengo wa kushoto
Hawa walikuwa na mambo yafuatayo walichukua msimamo wa kufanya kazi na mkabala wa kitabaka katika kutolea tungo zao
·         Waliona usoshalist kama suluhisho la matatizo yao.
Ili usoshalist upatikane waliona ni lazima kumwaga damu (kutumia nguvu). Kundi hili lilikuw na K.Kahigi, na M.Mulokozi, Ally Salehe, M.S.Khatibu, A.Abdullah na S.A.Mohamed.
Hivyo Sanaa hii ambayo ilianza upwa wa Kenya na Tanzania katika kare ya 10-15 sasa imeenea Afrika Mashariki nzima hadi Rwanda, Burundi na Kongo
MGOGORO KUHUSU USHAIRI WA KISWAHILI
Mgogogro huu ulianza mwisho mwa miaka ya sitini (1968) na mwanzoni mwa miaka ya sabini. Mgogoro ulihusisha pande mbili washairi wa kimapokeo (wasiokubali mabadiliko hawa walisisitiza kuwa vina na mizani ni uti wa mgongo wa shairi la Kiswahili) wanamabadiliko waliona kuwa si lazima shairi liwe na vina na mizani.
Sababu kuu zilizozua utata ni mbili
          i.            Maana ushairi kwa ujumla
        ii.            Maana ya shairi la Kiswahili
Mvutano huu unahusisha na mabadiliko ya kidunia yaliyotokea miaka ya Sitiari na Sabini katika Nyanja mbalimbali za maisha hata kupelekea washairi nao kuhitaji mabadiliko katika tasnia ya ushairi kwa upande wa fani
Msukumo huu wa kuleta mabadiliko katika tasnia ya ushairi uliletwa na wanazuoni akina E.Kezilabahi, Jared Angira na E.Husein wasomi hawa walijishughulisha na utunzi wa mashairi hivyo baada ya kusoma fasihi za nchi mbalimbali waligundua kuwa vina na mizani ni wazo zilizofuatwa na washauri wote duniani hivyo waliamua kuasi sharia hizo ili kuleta mabadiliko ya kuondoa minyororo iliyowafunga kuhusu utungaji wa shairi la Kiswahili kwa pamoja waandishi hawa waliweza kutunga mashairi mengi au tungo zisizofuata niaza ya vina na mizani na pia waliungwa mkono na watunzi wengi kama vile M.M.Mulokozi, K.K.Kahigi miaka ya themanini washairi wengi waliibuka kuungana na kundi hilo. Mfano: Henry MhanikanaT.Mvungi
Madai ya wana mabadiliko kutunga tungo zao yalikuwa kama ifuatavyo:
1.      Mbinu na njia za kutunga mashairi ya Kiswahili zilikuwa chache mno.
2.      Kutunga kwa kufuata taratibu za muundo wa tungo za Kiswahili (mapokeo) kuliwanyimia uhuru walidai kuwa hakuna sharia za utunzi wa mashairi katika (diwani ya Amri) (sharia za kutunga mashairi).
3.      Muundo wa tungo zao zisizofuata kaida ni wa kiasilia. Hii ina maana kwa ushairi wa mwanzo haukuwa na mizani wala vina.
Kwa namna nyingine tunaweza kusema kuwa mgogoro huo ulijitokeza baina ya wazee akina Kuluta Amri Saadam Kandoro, Ustadhi, Andamenga, Shihabdini chira hdin n.k na vijana akina E.Kezilahabi na Uanza.

   MADA NDOGO ;KUHAKIKI  RIWAYA
Riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye mawaidha, lugha ya nathari, mchanganyiko wa visa, wahusika kadhaa na matukio yaliyosukwa kimantiki yenye kufungamana na wakati na kushabihiana na maisha halisi.
SIFA ZA RIWAYA
1.      Urefu, Riwaya kwa kawaida huwa ndefu ikilinganishwa na tanzu nyingine za kinathari kama vile hadithi fupi. Mfano wa Riwaya ya Bwana Mnyombokera na Bibi Bagomoka (198 ) iliyoandikwa na Kiterezi, Hii ina mamia ya kurasa
2.      Matukio,Riwaya humulika hali halisi ya maisha ya binadamu ingawa matukio ya riwaya si lazima yawe ya kweli yametokea, yanaweza kupatikana katika ulimwengu halisi wa binadamu matukio kama vile rushwa, wizi wa mali ya umma, matabaka, uongozi mbaya, athari za pesa katika ndoa na mapenzi na tatizo la usafiri Dar-es-salaam katika “Pepo ya mabwegwe” (1981) iliyoandikwa na Mwakyembe, mambo yaliyoandikwa yamo katika jamii yetu kwa sasa.
3.      Muundo,Riwaya huwa na miundo changamano ukilinganisha na kazi nyingine za kinathari. Riwaya inaweza kua na muundo wa msago, rejea au rukia, wakati mwingine inaweza kuwa na muundo changamano yaani inakuwa na muundo miwili katika kazi moja.

4.      Mandhari yake ni pana
Mandhari ya riwaya ni mapana na kikamilifu kwani riwaya hushughurikia mawazo mengi, hujishughulisha na vipengele vingi vya maisha ambavyo hupatikana katika nyakati na mahali tofauti kama vile shuleni, mijini, vijijini, nyumbani, barabarani n.k. ili kushughulikia mazingira mapana mwandishi hutumia kipindi kirefu cha wakati ikilinganishwa kazi nyingine kama vile hadithi fupi ambayo huweza kuchukua kipindi kimoja tu kukuamilika.
5.      Wahusika ,Wahusika wa riwaya ni wengi na waliokuwa zaidi. Riwaya hushughulikia masuala mengi huwa na wahusika wengi wanaomwezesha mwandishi kukidhi haja hiyo kuna wahusika wanaobadilika kwa lengo la kuonyesha hali halisi ya maisha kuna wale wasiobadilika ili kutumiwa kukashifu au kuhimiza hali fulani n.k. Riwaya ya Ziraili na Ua la faraja na Mkufya na Makuadi wa Soko Huira iliyoandikwa na Chacha Gezina wahusika wengi.
6.      Mtindo,Riwaya hutumia mtindo wa wasimulizi, monolojia au dayolojia na nafsi zote tatu. Mwandishi anaweza kuwa ndiye msimulizi au mhusika fulani akawa ndiye anayesimulia au wahusika wakawa wanajibizana wao kwa wao.
Mfano: Njama (1981), Uchu (2000), Kikosi cha Kisasi(1979) vya musiba ametumia zaidi mtindo wa monolojia na dayolojia kidogo.
AINA/TANZU ZA RIWAYA
Kuna michepuo miwili ya riwaya  ambayo ni;
A.     RIWAYA YA DHATI
Riwaya dhati ni riwaya yenye kuchambua masuala mazito ya kijamii, kutafuta sababu zake athari zake na ikiwezekana ufumbuzi wake. Ni riwaya inayokusudiwa kumkera na kumfikirisha msomaji, sio kumstarehesha mtu.

MATAWI YA RIWAYA YA DHATI
1.      Riwaya ya kijamii
Ni riwaaya inayosawiri maisha na matatizo ya kawaida ya jamii. Matatizo haya huweza kuwa ya kifamilia, kiuhusiano wa kitabaka ya kisasa ya kiutamaduni n.k. Utanzu huu ndiyo wenye idadi kubwa zaidi ya riwaya.
Mfano:                -Shabaan Robert “Siku ya watenzi wote” (1968)
                -M.S.Moamed “Nyota ya Rehema” (1978)
                -S.A..Mohamed “Dunia mti mkavu” (1980)
                -E.Kezilahabi “Rosa mistika” (1971)
                -J.N.Somba “Alipanda upepo Akavuna Tufan” (1969)
                -Alex Banzi “Titi la mkwe” (1972)
2.      Riwaya ya kisaikolojia
Ni riwaya inayododosa nafsi ya mhusika, fikra, hisia, mawazo, Imani, hofu, mashaka na matumaini na matamanio yake binafsi na athari za mambo hayo kwake binafsi na labda jamii yake. Baadhi ya watunzi waliojipambua katika utanzu huu ni
                -E.Kezilahabi “Kichwa maji” (1974)
                -M.S.Mohamed “Kiu” (1972)
                -S.A.Mohamed “Tata za Asumini” (1990)
                -K.G.Mkangi “Ukiwa” (1973)
3.      Riwaya ya kitawasifu
Ni riwaya ambayo husimulia habari za maandishi tangu kuzaliwa kwakwe hadi pale inapokomea au hadi kufa.
Mfano:     -Shabaan Robert “Maisha Baada ya miaka Hamsini” (1966)
                -Maisha ya Hemed Bin Muhamed “Tipu Tipu” (1950)
4.      Istiara
Ni riwaya ya mafumbo ambayo umbo lake la nje ni ishara au kuwakilisha tu cha jambo jingine.
Mfano:   -Riwaya ya Nathanuel Swift (1926)
              -Safari za Gulliver (Mfasiri F.Johnson) (1945)
              -Shamba la wanyama (Msafiri F.Mkwegere)
Ni ishara ya mfumo wa utawala wa dikteta wa kisovieti wa enzi za Staliri. Yaelekea pia riwaya Shabaan Robert (1951) kusadikika ni ishara kuhusu utawala na mabavu wa kikolono.
5.      Riwaya ya kigano
Ni riwaya yenye umbo la mtindo wa ngano mathalani huweza kuwa na wahusika wanyama, visa vya ajabu ajabu, mandhari ya kubuni na visa vyenye kutendeka nje ya wakati wa kihistoria.
Mfano:    -Shabaan Robert (1952) “Adui na nduguze”
               -J.K.Kimbila (1966) “Lila na fila”
6.      Riwaya teti
Ni riwaya inayosimulia vituko na masahibu ya watu, wapuuzi, walaghai, wajanja na kwa njia inayosisimua na kuchekesha. Aghalabu hao huwa ni watu wanaovutia wa tabaka la chini na bapa. Matukio ya Riwaya hii hayana msukumo ulioshikamana vizuri shabaha yake mojawapo ni kuziteta na kuzikejeli tabia za matabaka na watu mbalimbali katika jamii.
Mfano:    -Hadithi za “Hekaya za Abunuasi na Hadithi nyingine (1915) imefanana na vituko vya riwaya teti.
7.      Riwaya ya wasifu
Ni riwaya inayoandikwa na mtu mwingine kuhusu maisha ya mtu mwingine tangu kuzaliwa hadi kufa kwake.
Mfano:   -J.Makabarah “Maisha ya Salum Abdallah” (1975)
              -S.Robert “Wasifu wa Siti bint Saad” (1967)
8.      Riwaya chuku
Ni riwaya ya vituko na masaibu yasiyokuwa ya kawaida ni riwaya isiyozingatia uhalisia mara nyingi masaibu ya Riwaya chuku huambatana na mapenzi, mfano; baadhi ya hadithi za Alfu-lela-Ulela (1929) ni chuku katika fasihi ya Kiswahili. Riwaya za Shabaan Robert za “Adili na Nduguze” (1952) na “Kusadikika” (1951) zinaingia katika kundi hili.
9.      Riwaya ya kihistoria
Hii huchanganya historia halisi na Sanaa kwa makusudi ili kutoa maudhui fulani. Mara nyingi riwaya hii hujikita kwenye matukio makuu ya kihistoria yalioathiri mwenendo na mwelekeo wa jamii au taifa linalohusika na historia ya kubuni, matukio ya kweli na ya kubuni. Hata hivyo riwaya hiyo inazingatia zaidi namna matukio makuu ya kihistoria yalivyomwathiri na yalivyoathiriwa na matendo ya mtu binafsi aliyeyashiriki baadhi watunzi mashuhuri wa riwaya za kihistoria ni
Mfano:    -Olef Msewa “Kifo cha ugenini” (1977)
               -M.Karuthi “Kaburi bila msalaba” (1971)
               -S.A.Shafi “Kuli” (1979)
               -A.Lihamba “Wimbo wa Sokomoko” (1990)
               -B.Mapalala “kwa heri iselemaguzi” (1992)
               -G.Ruhumbika “Miradi Bubu ya wazalendo” (1992)
10.  Riwaya ya kimaadili.
Ni riwaya inayowapa watu maadili mema na wengine maadili hayo ni ya kidini wausika wanakuwa na sifa za kudumu kama vile upendo wa ukarimu.
Mfano:    -Shabaan Robert “Adili na Nduguze” (1952)
               -M.Mnyapala “Mrina Sali na wenzake wawili” (1961)
               -G.Mhina “Mtu ni Utu” (1971)
11.  Riwaya ya kimapinduzi
Ni riwaya inayojadili matatizo ya kisiasa katika jamii. Riwaya hii ni mwelekeo fulani wa kuleta mabadiliko ya kisiasa katika jamii.
Mfano: wa riwaya hizi ni “kuli” (1978), Kabwela (1978), Mzalendo (1977) Ubeberu Utawashinda (1971) n.k.
12.  Riwaya ya kifalsafa
Ni riwaya zinazojadili migogoro ya kimaisha kifalsafa. Riwaya hizi hujuliza maswali kama vile
-          Ukweli ni nini?
-          Maisha ni nini?
-          Kifo ni nini?
-          Kuwepo na kutokuwepo ni nini? n.k
Muundo wa riwaya hizi ni wa kimchangamano au a mviringo na wahusika huvunjwa vunjwa hivyo mhusika wa riwaya hizi ni wazo tu au hawapo kabisa
Mfano:     E.Kezilahabi- “Nagona” (1987) Mzingile (1991)
                S.Mohamed- “Kiza katika nune” (1988)
                K.G.Mkangi- “Mafuta” (1984) n.k
13.  Riwaya Barua
Ni riwaya ambayo sehemu yake kubwa husimuliwa kwa njia ya barua wanazoandikiana baadhi ya wahusika.
Mfano:     -Mariam Ba “Barua ndefu kama hii “(1980) Msafiri Maganda
                -Walter Tribisch “Nampenda mvulana. Barua ya siri” (1964)
14.  Riwaya ya vitisho
Ni riwaya yenye visa vya kutisha na kusisimua damu mara nyingi visa hivyo huambatana na mambo ya ajabu au miujiza
Mfano:    -C.Mung’ong’o “Mirathi ya Hatari” (1977)
               -N.J.Kuboja mbojo Simba-mtu (1971)
15.  Riwaya pendwa
Ni riwaya iliyokusudiwa kuwastarehesha na kuburudisha msomaji tu lengo hili kulihimiza kwa kusawiri visa na vituko vya kusisimuwa damu
Mfano: Vituko vya majambazi na uhalifu, ususi na mahaba ya waziwazi.
Riwaya pendwa huwa na mafunzo kidogo kama lengo la ziada katika Tanzania aina hii ya riwaya ililetwa kwa mara ya kwanza na Abdull alipoandika riwaya ya “Mzimu wa watu wa kale“ (1957/8) na miaka ya 1960
-           Katalambwa (1965) simu ya kifo
SIFA ZA RIWAYA PENDWA
1.      Matumizi makubwa ya taharuki na utendaji
Taharuki hutumika kuelezea hamu kubwa anayokuwa nayo msomaji katika kujua yatakayotokea katika hadithi fulani. Taharuki hutokea pale ambapo msomaji ana hamu kubwa au anajua yanayoweza kutokea laikini hajui jinsi yatakavyotokea.
Riwaya pendwa ni riwaya ya taharuki kwa sababu ya kimsingi ya fani yake hujiweka katika mbinu ya kisanaa ya taharuki. Taharuki imepewa nafasi kubwa katika aina hii ya riwaya kwa njia ya vituko vya kusisimua vinavyojibainisha kwa njia ya mkingano iliyosukwa kwa namna ya ufundi usiokuwa wa kawaida.
Kwa upande wa utendaji wahusika wake n hodari sana katika kutenda, katika kuwindana, kupigana kwa silaha na mikono mitupu na kufanya matukio yake utendaji unaojitokeza humu unaziteka nafsi za wasomaji wake.
2.      Hutumia wahusika walewale.
Riwaya pendwa inasifa ya kutumia wahusika walewale hivyo ikawa na uwezo wa kujiendeza katika vijitabu kadhaa. Karibu kila mwandishi maarufu wa aina hii ya riwaya ameandika vitabu zaidi ya kimoja. Sifa hiyo ya kuwatumia wahusika walewale imefanya kijitabu kimoja katika mfuatano wa vitabu kadhaa vya mwandishi mmoja kionekane kama tukio linalojitegemea katika mfululizo wa matukio. Ili kuustawisha na kuwisisitiza mfuatano huo, baadhi ya waandishi wameweza hata kudondoa kazi za nyuma katika kazi zao za baadae mfano Abdallah “Kosa la bwana Musa”,Hofu (1988) musiba,Salamu Toka Kuzimu (1993) Mtobwa,Tutarudi na roho zetu?? (1987)
3.      Mhusika mkuu hupewa sifa zisizo za kawaida
Mhusika mkuu ameumbwa juu ya wahusika wengine anatawaliwa, hivyo ana sifa ya ubabe sifa ya kuwa kielelezo chenye ukamilifu, yaani kutokana na dosari.
Mfano:            Abdallah “ Kosa la Bwana Musa”
Mhusika mkuu ndiye mshindi hata apitapo katika taabu na mashaka ya aina gani tunajua hatimaye ni mshindi katika mambo yake. Wahusika hawa wakuu hutenda na kuendesha mambo yao kama miungu wadogo pasi na kukosea hata wakawa wasioaminika.
4.      Mandhari yake huundwa kwa namna ya pekee
Wasanii wa riwaya pendwa wanatumia mandhari ya kitanzania au kiafrika, lakini sehemu kubwa ya matukio ama imo ndani ya vichwa vya wasanii au filamu za upelelezi, uhalifu na mapenzi za kigeni.
5.      Upangaji holela wa matukio
Katika riwaya pendwa kuna upangaji wa haraka wa mtiririko wa matukio kiasi kwamba sehemu zingine zinakosa upatanifu na mantiki.
6.      Kuenzi jinsia ya kike kama chombo cha anasa na uhalifu.
Riwaya pendwa hua zina mapenzi ndani yake kana kwamba upelelezi au shughuli inayofanyika haiwezi kusisimua bila mapenzi, yaani hazina dawa, dawa ya kazi ni mapenzi.
7.      Hutumia lugha ya kila siku
Mara nyingi riwaya pendwa hutumia mitindo wa masimulizi na monolojia na kwa kiasi kidogo dayolojia. Lugha yake ni rahisi ya mazungumzo ya kila siku.

ATHARI ZA RIWAYA PENDWA
1.      Hudumaza vipaji vya waandishi wetu kwani huiga kila kitu.
Kazi hizi zinadhihirisha jinsi gani fasihi pendwa za kigeni pamoja na filamu zinaathiri waandishi wetu. Riwaya pendwa ni matokeo ya mwigo ambayo yameathiri uasili wa waandishi wetu katika ubunifu kimaudhui na kifani kazi hizi zinashindwa kabisa kudhihirisha umahiri wa waandishi wetu katika kubuni kazi na sanaa zenye mawazo yao wenyewe.
2.      Hufundisha majangili na wahalifu mbinu mpya katika shughuli zao za kufanya uhalifu.
Riwaya pendwa husababisha uhalifu katika jamii.Mfano: Athari mbaya za tamaduni za kigeni zinazokuja kwa njia ya filamu na riwaya pendwa ni kama vile kuzuka kwa makundi ya kiharamia hapa nchini ambayo yanavamia benki, baa, maduka na kuwaibia watu kwa kutumia silaha mbalimbali.
3.      Hazichambui kwa undani misingi ya matatizo ya jamii.
Riwaya hizi haziingi kwa undani katika misingi ya matatizo ya jamii kama kuna tatizo linalosababisha upelelezi je kiini chake ni nini? Riwaya hizi zinataja juu ya wivu, tamaa, uovu wa aina hiyo bila kuyahusisha vilivyo mazingira ya jamii (mfano filamu zinaitwa 24)

AINA ZA RIWAYA PENDWA
1.      Riwaya ya Mahaba
Ni riwaya yenye kusawiri uhusiano wa kimapenzi kati ya mvulana na msichana au mwanaume na mwanamke. Siku hizi zipo zenye kusawiri mapenzi haramu pia.Kwa mfano: Mapenzi baina ya watu wa jinsia moja (mashoga)
Mfano:            J.Simbamwene “Mwisho wa mapenzi” (1972),J.D.Kiango “Jeraha la moyo” (1974),S.M.Komba “Pete” (1978),J.Simbamwene “Kweli unanipenda” (1978)
2.      Riwaya ya Uhalifu/Ujambazi
Ni riwaya zinazosimulia vituko vya uhalifu. Mfano: wizi, ujambazi, uuaji, magendo, utapeli, n.k. Aghalabu polisi huhusishwa katika kuwasaka na kuwadhibiti wahalifu hao.
Mfano:J.Simbamwene (1972) “Kwa sababu ya pesa”,H.Katalambula (1975) “Buriani”,L.O.Omolo (1970) “Mtu mwenye miwani meusi”,S.J.Chadhoro (1972) “Kifo change ni fedheha”,Hammie Rajab (1979) “Ufunguo wa Bandia”
3.      Riwaya ya Upelelezi
Riwaya hii huelezea mambo mawili kosa au uhalifu na upelelezi wa uhalifu huo hadi mwalifu anapopatikana.
Hivyo wahusika wake ni wahalifu, wadhulumiwa (waliotendewa kosa) na upelelezi wakiwemo polisi. Mtunzi wa kwanza wa riwaya ya upelelezi nchini Tanzania ni mfano;M.S.Abdallah na riwaya zake ni:-Mzimu wa watu wa kale (1958),Kisima cha giningi(1968),Duniani kuna watu (1973),Siri ya sifuri (1974),Mwana wa yungi Hulewa (1976),Kosa la Bwana Musa (1984),Watunzi  wengine wa riwaya ya upelelezi ni:-H.Katalambwa na E.Ganzile,Simbamwene (1984) “Dimbwi la Damu”,E.Ganzele (1980) “Kijasho chembamba”
4.      Riwaya ya Ujasusi
Ni riwaya ya upelelezi wa kimataifa majasusi ni wapelelezi wanaotumwa na nchi, serikali au waajiri wao kwenda katika nchi nyingine kuchunguza siri zao hasa siri za kijeshi (silaha walizonazo) siri za kisayansi na kiuchumi n.k ili taarifa hizo ziwanufaishe waliowatuma wakati Fulani hutumwa kwenda kuharibu silaha zao au nyenzo za uchumi na maadui
Mfano wa riwaya za ujasusi ni:-E.Musiba (1979) “Kikosi cha kisasi”,E.Musiba (1981) “Njama”,K.M.Kassani (1982) “Mpango”,Mtobwa (1987) “Je tutarudi na roho zetu?”,Hammie Rajab (1984) “Roho mkononi”
UHAKIKI WA VIPENGELE VYA FANI
Vipengele vya fani ni kama vile:-
a)      Muundo
Muundo hutumika kueleza mpangilio wa kazi ya kifasihi. Mpangilo huu hujionyesha kwenye maumbo ya kazi za kifasihi kama hadithi fupi au riwaya. Muundo ni namna au jinsi kazi za fasihi inavyoonekana yaani umbo lake, ilivyogawanyika. Mfano sura, mfuatano wa matukio yake (mtiririko wa matukio), msuko n.k. matukio yanaweza kufuatana kwa njia sahihi nay a moja kwa moja (msuko sahahi) au yakawa na uchangamano ambao unahusisha kwenda mbele na kurudi nyuma (msuko changamano)
b)      Mtindo
Ni jumla ya mbinu au sifa zinazomwezesha mandishi kuwasilisha ujumbe wake.Mtindo huelezea jinsi mwandishi anavyoiunda kazi yake.Dhana hii inarejesha sifa maalumu za mwandishi au mazoea ya mwandishi fulani ambayo hujionyesha kwenye fani yake. Mazoea hayo ya mwandishi yanapambanua msanii huyu na wenzake kiasi kwamba msomaji anaweza kusema hii ni kazi inayoandikwa na fulani kwa kusoma tu katika mtindo wa riwaya kuna vipengele vifuatavyo
·         Matumizi ya Lugha
·         Usimulizi wa nafsi (Msanii anaweza kusimulia matukio kwa kutumia nafsi ya 1,2 na ya 3)
·         Matumizi ya masimulizi (msanii hutoa masimulizi yake juu ya mfululizo wa matukio kama yalivyotokea katika kipindi fulani cha maisha ya wahusika. Msanii husema nini kilitokea jinsi gani kilitokea na mahali ambapo hayo yalitokea
·         Matumizi ya monolojia ni masimulizi yanayofanywa na mhusika mmoja katika hadithi au kazi nyingine za kisanaa katika mbinu hii, hadithi inayojitokeza kama inasimuliwa na mhusika aliye hadithini. Mwandishi anaonekana kuwa hayupo. Pia hadithi inaweza kujitokeza ikisimuliwa katikaa nyakati mbalimbali.
·         Matumizi ya dayolojia, ni mazungumzo baina ya wahusika wawili au zaidi katika riwaya.
·         Matumizi ya tanzu nyingine za kifasihi simulizi kama vile nyimbo, mashairi, majigambo, hadithi matumizi ya barua n.k.
·         Uteuzi wa wahusika na ujengaji wa mandhari.
c)      Wahusika
Ni viumbe wa sanaa wanabuniwa kutokana na mazingira ya msanii. Hatua ya kwanza katika utungaji wa kazi ya sanaa ni wazo, wazo kutokana na hali halisi anayoiona msanii ili kueleza fikra rai au falsafa yake kuhusu kile akionacho anaichukua Lugha na kuifinyanga.
Wahusika wake pia huwaweka katika mandhari yatakayomsaidia kuwakilisha hoja zake kutokana na vitendo, maingiliano na fikra zao kuna wasanii wanaotumia wanyama au wadudu kama wahusika kwa lengo la kufikisha maudhui fulani kwa jamii au dhamira, mitazamo yao, kwa jamii.
d)      Mandhari
Ni mahali au makazi maalumu yaliyojengwa na mtunzi na yanamatokeo, matukio mbalimbali ya fasihi. Mandhari ni mazingira ya wahusika na matukio na inahusu mahali wanamokaa wahusika na kuingiliana, mazingira ya kijamii na kiuchumi ya wahusika hao na nafasi zao za kitabaka kufahamu mandhari kunatusaidia kuelewa hisia, imani, tabia, na maumbile ya wahusika. Mandhari hutupatia mwelekeo kuhusu maudhui.
e)      Matumizi ya Lugha
Lugha ina nafasi kubwa sana katika fasihi kwa kuwa fasihi yenyewe ni sanaa ya lugha. Lugha hiyo ndiyo nyenzo inayotofautisha fasihi na sanaa nyingine kama uchoraji, ufinyanzi, udarizi n.k
Lugha ni nguzo kuu ya kazi za kifasihi na uchunguzi wowote wa kazi hizo hauna budi kuangalia suala la lugha kazi ya kifasihi  huyawasilisha  maudhui yake, dhamira yake kwa kutegemea lugha. Baadhi ya wahakiki wa fasihi wa kwanza kuwa  fasihi hutumia lugha kwa namna maalumu, inayozoea lugha ambayo inajulukana kama lugha ya kifasihi. Katika matumizi ya lugha kuna vipengele kama:-
Tamadhali za semi, kama vile tashibiha, sitiari, tafsida, tashihisi, kejeli, mubalagha, dhihaka n.k
·         Mbinu nyingine za kisanaa ni kama vile takriri, tanakali sauti, mdokezo, tashititi, mjalizo n.k
·         Matumizi ya majali maana ya watu aghalabu huwa na maana. Wasomaji wa riwaya ni vyema tuyachunguze majina na kuyahusisha na matukio, dhamira, maudhui na ujumbe wa riwaya husika. Mfano wa riwaya ni “Adili na Nduguze” (1952) mhusika Adili ni mwadilifu
·         Matumizi ya jazanda au Taswira ni mafumbo ambamo ndani maana ya kitu imejificha na mfano katika riwaya ya “Dunia mti mkavu” (1980) mvua inatumiwa kama jazanda na matumizi ya nguvu dhidi ya wananchi.
·         Uteuzi na mpangilio wa maneno. Lugha ni nyenzo ya kimsingi ya msanii na jinsi anavyotumia huathiri jinsi msomaji atakavyoisoma, kuielewa na kuathiriwa na riwaya fulani mfano wa matumizi ya miundo fulani huweza kuathiriwa na maswala yanayozungumzwa.
·         Matumizi ya semi, kama vile methali, misemo, nahau, misimu mafumbo n.k vipengele hivi vina kazi ya kufafanua maudhui ya kazi ya fasihi
·         Matumizi ya taharuki. Hii ni mbinu inayotumiwa na watunzi wa kazi za kubuni ili kutetea hisia na hamu ya msomaji ili kujenga taharuki. Mtunzi husuka matukio yenye mshikamano na kutiririka kwa muwala ambao unamfanya msomaji asiitue kazi hiyo hadi kikomo chake kazi yenye taharuki haichoki kuisoma bali inaburudani ndani yake.

JINA LA KITABU
Jina la kitabu ni vyema lisadifu yale yaliyomo ndani ya kitabu. Mfano Je Shetani msalabani (1982) linasadifu vipi yale yaliyomo ndani ya riwaya hiyo?
UHAKIKI WA MAUDHUI
Maudhui ya riwaya kama kazi yoyote nyingine ya fasihi yaweza kuwa kitu, mtu, tukio au jambo lolote katika maisha yetu. Maudhui hudhihirika baada ya kuangalia mambo mengi, mathalani tukio mbalimbali
Kwa ujumla, maudhui ni muhimu katika riwaya hasa ndiyo msingi wa riwaya kwa hivyo ni lazima tutegemee mambo yaliyojitokeza katika ile riwaya yaani maudhui lazima itoke ndani ya riwaya na sio nje.
Katika bahari hii ya maudhui, hatuna budi  kuichunguza jumuiya iliyozungumzwa. Matokeo yote katika utunzi ule yatapimwa kwa mujibu wa hali ya jumuiya. Mhakiki astahili kuichunguza jumuiya ili kuweza kuhukumu kama mtunzi amezingatia kutoa hali halisi ya jumuiya yake.
Maudhui huwa ni ya aina mbalimbali kwa ujumla huwa yanalenga migogoro na mikinzano katika jamii. Baadhi ya maudhui ya kazi zote za riwaya na sanaa kwa jumla ni kama vile:-
-          Mgongano wa tabaka kati ya watawala na watawaliwa
-          Migongano kati ya wenye elimu na wasiopata elimu
-          Migongano kati ya walio na mali na wasionayo
-          Migongano kati ya mwenye kupigania usawa kati ya mume ne mke na wenye kupinga usawa huu n.k
Kwa ujumla maudhui hutupa mafunzo, ujumbe na kutufahamisha falsafa
MADA NDOGO ;UHAKIKI WA TAMTHILIYA
Tamthiliya ni utungo wa kidrama ambao ni aina mojawapo ya maandishi ya sanaa za maonyesho. Ni sanaa inayoonyeshwa kwa vitendo katika sanaa hii ili mtu apate maadili au utamu uliomo katika sanaa mpaka asome vitendo vya wahusika waliotumiwa na msanii na kuvitafakari kwa makini.
Tamthiliya huonyesha matendo ya wanajamii kwa njia ya kuigiza, maigizo ambayo hatimaye huweza kuonyeshwa kwenye majukwaa katika sanaa za maonyesho wahusika wake huonyesha matendo waziwazi kwa njia ya kuigiza. Wausika hawa huzungumzia nafsi zao wakati zamu zao za kuongea zinapowafikia ili mradi kila mmoja hujaribu kuonyesha waziwazi kuridhika au kutoridhika kwake kufutana na nafasi anayoiwakilisha katika jamii inayohusika.
Sifa za tamthiliya
Tamthiliya huwa na sifa za kawaida za sanaa za maonyesho, sifa hizo ni:
·         Dhana inayotendeka
Dhana inayotendeka ni kile kinachoongelewa katika tamthiliya na kinaweza kuwa cha kubuni au cha kweli. Dhana inayotendeka kwa kawaida huhusu mzozo fulani unaohusisha pande mbili. Kwa mfano, katika tamthiliya ya “Kilio chetu” (1995), dhana inayotendeka ni “Vita dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI”
·         Kuwepo kwa mtendaji
Hapa ni wale wanaotenda ile dhana, yaani wahusika. Ili tamthiliya ikamilike lazima wawepo wale wanaotenda lile tendo ambao wanaitwa wahusika. Kwa mfano, katika tamthiliya ya “Mashetani” (Hussein) watendaji wakuu ni: Juma na Kitaru na watendaji wadogo ni: Mama Kitaru, Baba Kitaru, Daktari, Bibi, Mama Juma, n.k
·         Kuwa na uwanja maalumu wa kutendea
Tamthiliya huigizwa sehemu fulani. Hapa kuna jukwaa ambako wahusika wanaingiliana katika uigizaji wao. Ukubwa au upana wa eneo hilo ni muhimu sio tu kwa athari, bali pia kwa kuupitisha ujumbe fulani.
·         Kuwepo kwa watazamaji
Hawa hutazama dhana inayotendeka. Kwa tamthiliya iliyoandikwa, watazamaji hapa ni wasomaji, yaani wale wanaosoma kazi hiyo ya sanaa. Kwa hiyo, tamthiliya inaingizwa mbele ya watazamaji (hadhira).
·         Kusudio la kisanaa.
Hili hutupa uhakika kuwa kinachotendeka hapo kimedhamiriwa kuwa sanaa na si kitu kingine kwa mujibu wa kanuni za jamii inayohusika.


vi.                Muktadha wa kisanaa
Ni sifa nyingine ya tamthiliya. Muktadha  wa kisanaa unafafanua mazingira ya tukio hilo. Kwa mfano, ugomvi wa walevi kilabuni au baa si sanaa za maonyesho kwa sababu muktadha wa tukio hilo haulipokei kama sanaa.
vii.              Tamthiliya ni kazi ya kubuni kama kazi nyingine za kifasihi.
Hii ni muhimu ili kutofautisha kati ya tendo la dhati katika maisha na tendo la sanaa.
viii.            Matukio ya tamthiliya huigizwa kwa hadhira hai.
Hapa basi pana mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wahusika, ambao ni vipaza sauti vya mtunzi na hadhira.
ix.                 Tamthiliya, hadithi yake imegawika kimuundo katika matendo na maonyesho
Matendo na maonyesho huonyesha matukio mbalimbali. Kila tendo huzingatia tendo moja kuu ndani ya mchezo; na hugawanyika katika sehemu ndogo ziitwazo maonyesho. Onyesho moja kwa kawaida huwasilisha tuko moja linalotendeka mahali pamoja.
x.                   Mgogoro wa tamthiliya huwa mwanzoni
Mwandishi hana wakati wa kutoa maelezo mengi. Kwa mfano, katika tamthiliya ya “Kifo Kisimani “ ya Kathaka wa Mberia, mgogoro kati ya Mtukufu Bokona na wanyonge unajitokeza mwanzoni

AINA ZA TAMTHILIYA
1.      Tanzia
Tanzia ni ile inayohusika na mambo yenye uzito, kifikirika na kihisia katika maisha ya binadamu. Mhusika mkuu ambaye hupewa sifa nyingi zinazovutia, hukabiliwa na shida au tatizo;tatizo ambalo linaweza kumkabili mtu yeyote. Lakini namna anavyojitahidi kulitanua tatizo hili, namna anavyopigana vita kushinda shida inayomkabili, hali ya ulimwenguni na tabia za binadamu, zinamfanya asiweze kufaulu na mwishowe anashindwa katika vita hii. Kwa mfano, tamthiliya ya “Mzalendo Kimathi” (1978) “Kinjekitile” (1969), “Pungwa” (1988), “Kilio cha haki” (1981) ni mfano wa tanzia. Katika tamthiliya zote hizi mhusika mkuu anashindwa na hata anakufa au anauawa, lakini kifo chake si kile cha ajali barabarani, bali ni kifo kinachokuja baada ya mapambano marefu, mapambano yanayochepuza hisia za ushujaa wa binadamu
2.      Ramsa (komedia)
Ramsa ni ile inayokusudiwa kufurahisha au inayochekeshachekesha na yenye mwisho mwema. Aina hii ya tamthiliya ni kwamba hutuchorea picha yakini ya maisha yetu, huwa haijaribu kuisawiri picha hiyo kwa undani na uzito kama uleunaojitokeza katika tanzia. Mfano wa ramsa ni tamthiliya ya Aliyeonja Pepo (1973)
3.      Melodrama na vichekesho
Melodrama inafanana sana na tanzia, ingawa mara nyingi mhusika mkuu wa meleodrama humaliza kwa ushindi, matokeo yake huwa yanasisimua sana, na mwendo wa msuko wake huwa ni wa harakaharaka zaidi.
Vichekesho, kwa upande mwingine; huwa  vinakusudia kutuonyesha vituko vitakavyotuchekesha tu. Ujenzi wa wahusika huwa ni muhimu, matukio huwa hayawekewi sababu zozote au sababu za kuturidhisha na msuko wake huwa hauna uchangamano mzuri. Tamthiliya nyingi zinazoonyeshwa katika televisheni ni vichekesho.
4.      Tamthiliya ya kihistoria
Hii ni aina ya tamthiliya inayoelezea tukio fulani la kihistoria katika jamii fulani. Msomaji wa tamthiliya hii huweza kukutana na sifa za tanzia pamoja na tamthiliya chekeshi. Mhusika mkuu wa tamthiliya hii mara nyingi huwa ni shujaa aliyejitoa mhanga kuipigania na kuitetea jamii yake ili iweze kuondokana na matatizo yanayoiandama, hususani ya kisiasa na kiuchumi.
Tukio la kihistoria linaloelezewa kwenye tamthiliya hii huwa limeiathiri jamii husika kwa kiasi kikubwa na hivyo huwa si rahisi kusahaulika. Vitabu vya tamthiliya vinavyoelezea matukio ya kihistoria ni kama vile Kinjekitile, Mzalendo Kimathi, Mkwawa wa Uhehe (1979) pamoja na Tone la Mwisho.
UHAKIKI WA VIPENGELE VYA FANI
Uhakiki wa tamthliya kimsingi huzingatia kanuni na misingi ileile ya uhakiki wa Riwaya. Kuna mambo ya msingi yz hizo tanzu mbili kufanana na kutofautiana. Mambo muhimu yanayochunguzwa wakati wa kuhakiki fani ya tamthiliya ni:
a)      Utendaji/tukio/tendo.
Kitu muhimu sana katika ujenzi wa tamthiliya ni tukio. Kutokana na tukio moja, msanii anao uwezo wa kuibua dhamira mbalimbali. Wataalamu wa taaluma hii husisitiza umuhimu wa tendo au tukio katika tamthiliya kwa kusema “drama ni tendon a wahusika ni tendo”
Tendo huanza pale mhusika anapoulza, “Ninataka nini? Je, lengo langu ni nini?” Kwa kawaida, aina ya tendo/tukio litaathiri matokeo ya tamthiliya itakayoandikwa.
Mwandishi mwenyewe anapaswa kuamua juu ya aina ya tamthiliya anayotaka kuandika, lugha, mtindo, wahusika au mandhari anayotumia. Kwa hali hiyo, uteuzi wa tendo/tukio la kuandikia tamthiliya lazima uende pamoja na uteuzi mzuri wa vipengele vingine vya kisanaa kama vile lugha, wahusika, mandhari, n.k.
b)      Lugha
Lugha ndiyo nyenzo kuu ya kazi ya fasihi. Dhamira na maudhui ya kazi ya kifasihi haziwezi kuwasilishwa na kuwafikia wasomaji bila ya kuwako kwa lugha. Uchunguzi wa matumizi ya lugha ni muhimu katika uhakiki wa tamthiliya. Je, mambo gani ya kuchunguza hapa? Hapa tunachunguza:
-          Matumizi ya nahau na misemo.
-          Uteuzi na mpangilio wa maneno/msamiati.
-          Tamathali za semi. Kwa mfano, sitiari, tashibiha, tafsida, tashihisi, n.k.
-          Mbinu nyingine za matumizi ya lugha. Kwa mfano, takriri, tanakali sauti, majazi, mdokezo, mjalizo n.k.
-          Matumizi ya taswira na ishara mbalimbali.
-          Matumizi ya mkopo na kutohoa.
c)      Wahusika
Katika tamthiliya, wahusika ni nguzo muhimu sana. Wahusika si watu halisi bali ni watu wa kubuniwa, wenye sifa muhimu za binadamu. Wahusika huwa na athari kubwa kwa hadhira kutokana na sababu mbalimbali:-
-          Wahusika wanabebeshwa sifa nyingi tofauti ambazo zinawakilisha maisha halisi ya watu hai.
-          Mwandishi wa tamthiliya hulazimika kumjenga mhusika mmoja kwa kuvutia na kumpa mbinu za ki-drama, mambo ya kushangaza au mbinu yoyote ile anayoichagua mwandishi. Kama tamthiliya inaigizwa jukwaani, wale waongozaji wa tamthiliya hiyo wanaweza kuathiri mchezo huo pia. Kama ilivyo katika riwaya, tamthiliya huwa na wahusika wakuu na wahusika wadogo.
d)      Muundo wa tamthiliya
Muundo katika tamthiliya humaanisha msuko wa vitendo na mgogoro kuanzia mwanzo wa mchezo, kuingia kwenye kilele (upeo) na kuhitimisha kwenye ufumbuzi/masuluhisho ya mchezo huo (mwisho). Kwa upande mwingine, muundo huonyesha mpangilio wa maonesho kutoka mwanzo hadi mwisho wa tamthiliya.
Kwa ujumla, tamthiliya inakuwa na mwanzo unaomwelekeza msomaji kwenye wahusika na migogoro au mkinzano unaokuwa na kufikia upeo kasha msuko wa aina fulani kabla ya kufikia ufumbuzi. Muundo unaweza kuwa wa moja kwa moja au muundo wa rejea.
e)      Maelekezo ya jukwaani
Haya ni yale maelezo ambayo huandikwa kwa mabano katika tamthiliya na huandikwa kwa hati ya mlazo. Je, maelezo hayo hufanya kazi gani?
-          Hueleza mienendo na miondoko ya wahusika.
-          Hutoa maelezo kuhusu wasifu wa wahusika, mavazi, lugha ya ishara za uso, n.k.
-          Hutoa maelezo kuhusu mandhari au mahali pa mchezo.
-          Hufafanua matendo mbalimbali yanayotokea jukwaani.
-          Hueleza wasifu wa mazingira na hata malebaya wahusika.
-          Hutoa vielekezi vy jinsi ya kuandaa jukwaa kwa ajili ya uigizaji
-          Hutoa tathmini ya matendo ya wahusika au lugha; kwa kuonyesha wapi pana kinaya, n.k
f)       Mandhari
Madhari hutumiwa kuelezea sehemu ambako tendo fulani hutendeka. Neon hili huweza kutumiwa kwa mapana kuelezea pia mazingira ya kisaikolojia ya tendo fulani. Mandhari huweza kurejelea yale mazingira ya jukwaani na hata wakati wenyewe katika tamthiliya. Mandhari yanaweza kuwa ya kubuni au ya kweli (halisi)
g)      Upeo/kilele
Upeo ni sehemu ya tamthiliya ambamo taharuki  na matamanio ya hadhira hufikia kilele.sehemu ambapo hadhira huanza kupata suluhisho la mgogoro uliomo katika tamthiliya. Peo katika tamthiliya ni za aina mbili upeo wa juu na wa chini
                                i.            Upeo wa juu ni ule ambao unakidhi haja za hadhira au jamii inayoipokea. Katika sehemu hii, jamii hupata majawabu muhimu ambayo tamthiliya huwa imeyachelewesha kwa kutumia mbinu kama vile za taharuki, mbinu rejeshi, mtindo telezi, n.k. Sehemu hizi mara nyingi husisimua hadhira kwa hali ya juu sana.
                              ii.            Upeo wa chini ni ule ambao haukidhi haja ya wasomaji wa tamthiliya inayohusika. Katika baadhi ya kazi za tamthiliya upeo wa chini huonyesha udhaifu wa kazi ya sanaa ya msanii anayehusika. Wakati mwingine upeo wa chini umekusudiwa na msanii na huutumia sana katika hadithi fupi na lengo kubwa huwa ni kuipa hadhira mshangao.
h)      Jina la kitabu na jalada lake
Kama ilivyo kwenye uhakiki wa riwaya, katika tamthiliya vilevile tunaangalia uhusiano wa jian la kitabu na yaliyomo katika kitabu, hali kadhalika jalada na uhusiano wake na maudhui ya kazi inayohusika.
i)        Mtindo katika tamthiliya.
Tamthiliya yoyote hupambanuliwa kwa mtindo wake ambao ni mazungumzo au dayolojia. Mazungumzo/dayolojia hutumiwa kuelezea majibizano baina ya wahusika wawili au zaidi waliopo kwenye jukwaa au katika tamthiliya maongezi au majibizano si kwa ajili ya kujibizana tu. Hata hivyo ni muhimu kutambua kuwa, mazungumzo hayo si mazungumzo tu, lazima yaendeleze tendo kuu katika tamthiliya. Mazungumzo ndiyo nguzo ya kukuza dhamira na maudhui.
-          Mazungumzo mazuri yana uhalisia na uthabiti.
-          Mazungumzo sio maelezo tu bali yanaonyesha matendo ya ndani.
-          Mazungumzo mazuri hukuza na kuendeleza tendo kuu na msuko
-          Mazungumzo sio maongezi yanayovutia tu, lazima yawe na lengo.
-          Ikiwa mazungumzo yanakuza na kuendeleza tendo kuu, basi yanatekeleza jukumu la kidrama.
-          Mazungumzo yanaweza kutokea sambamba; kwa kuwako kwa wahusika kadhaa jukwaani.
-          Mazungumzo na uzungumzi nafsi wa wahusika huchukuliwa kama sehemu ya mazungumzo ya tamthiliya kwa sababu ya kuliendeleza tendo kuu.
-          Mazungumzo huweza kuonyesha sifa zisizokuwa za kawaida katika maongezi ya kila siku ikiwa mwandishi anataka kulimulika jambo fulani.
-          Mazungumzo ya mhusika yanaweza kuyavunja mtarajio fulani wa wasomaji au hadhira katika hali fulani kwa ajili ya kupitisha ujumbe fulani.
-          Mazungumzo ndiyo njia kuu ya kuindeleza hadithi iliyopo katika tamthiliya kwa kuwa mwandishi hana uhuru wa kutumia mbinu za usimilizi, isipokuwa katika maelezo ya jukwaani. Tamthiliya yoyote hupambanuliwa kwa mtindo wake ambao ni dayolojia.
Dayolojia ndiyo mtindo mkuu wa tamthiliya nyingi.
Dayolojia ni majibizano baina ya wahusika wawili au zaidi, ambao hujadili jambo fulani.
UHAKIKI WA MAUDHUI
Maudhui hutujulisha lile lililomgusa mwandishi mpaka kuunda ile kazi yake. Hili linaweza kuwa ni wazo tu au aliloshuhudia au hata likawa ni jumuisho la mambo mengi.
Maudhui pia hutuangazia jinsi jumuiya ya mwandishi ilivyo kwa kuwa fasihi ni kioo cha jamii. Kupitia maudhui, tunaweza kugundua mazingira ya mwandishi yalivyo.
Mwandishi hutumia maudhui yake kutudhihirishia mivutano, misuguano na pia maendeleo ya jamii yake. Maudhui ndiyo lengo la mwandishi. Ndicho chombo chake  cha kutuonyesha furaha na matatizo ya jumuiya iliyomzingira na kuwathiri kimawazo. Kuathirika huku kwa mwandishi hasa hujitokeza zaidi baada ya kusoma kazi zake nyingi.
Kwa hivyo, basi maudhui ya kazi yoyote ile ya fasihi yatahusu mambo ambayo yalimsukuma mwandishi hadi akaiunda kazi ile. Pia yatahusu mafunzo ambayo mwandishi aliliengea hadhira yake. Zaidi ya haya, kwa kuwa maudhui hayatenganishwi na mazingira na jamii, itambidi mwenye kuyachambua ayalinganishe na hali ya jamii ya mwandishi katika vipengele mbalimbali vya maisha. Mathalani, itambidi achunguze siasa, uchumi, utamaduni, n.k.
Mwanafasihi mmoja, Senkoro (1981), amefafanua maudhui kama yanayojumlisha mawazo nap engine mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma mtunzinama msanii hadi akatunga kazi fulani ya sanaa. Huwa msanii huyo amekusudia hadhira yake ya wasomaji, wasikilizaji ama watazamaji wayapate mawazo au mafunzo hayo. Kwa hiyo, haya twaweza kuyaita kuwa ni lengo la msanii kwa hadhira. Mawazo na mafunzo haya hayazuki hivi hivi tu. Kwa hiyo, kuna umuhimu wakati wa kuyachambua na kujadili yahusishwe na hali halisi ya jamii.
Mhakiki anachunguza maudhui ya kazi ya fasihi anaweza kuongozwa na maswali yafuatayo:-
-          Je, wazo kuu la msanii n nini?
-          Je, msanii ametazamia hadhira ya aina gani?
-          Je, kuna kundi lolote analoliunga mkono?
-          Je, kuna kundi analolibeza?
-          Je, msanii ameipa hadhira yake mbinu zipi za kuitatua migogoro aliyoichunguza?
Katika tamthiliya ya Kiswahili, kuna dhamira mbalimbali ambazo waandishi wamezishughulikia kwa mujibu wa Mulokozi (1996). Dhamira hizo ni:-
1.      Migongano ya kiutamaduni
Hizi zinonyesha mvutano kati ya utamaduni wa jadi wa Kiafrika na utamaduni wa Kizungu au kati ya mji na shamba. Suala hili limejadiliwa kwa dhati zaidi katika
-          E.Hussein “Wakati Ukuta” (1969)
-          E.Hussein “Kwenye Ukingo wa Thim” (1989)
-          P.Mhando “Hatia”
-          J.Ngugi “Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi” (1961)
-          H.M.Liyoka “Dunia Imeharibika” (1978)
-          C.Riwa na M.S.Masanja “Damu Imemwagika na Paulo! Paulo!”  (1976) n.k
2.      Matatizo ya kijamii
Kwa mfano, mapenzi, ndoa, ufukara na urithi. Karibu  tamthiliya zote za mawazo zilihusu kipengele hiki. Kwa mfano, Nakupenda Lakini…(1957) na Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (1961), zilizungumzia matatizo ya mapenzi yanayokumbana na vikwazo vya kiuchumi na vinginevyo. Tamthiliya za Hyslope zilihusu matatizo ya urithi, rushwa, fitina na tama. Tatizo la mimba limejitokeza katika Hatia, katika Mke Mwenza (1982), tunakutana na tatizo la wivu katika ndoa za mitala.
3.      Dini
Hizi ziko katika makundi mawili:
·         Tamthiliya za kanisani zenye kufundisha dini. Kwa mfano, zile tamthiliya zinazoingizwa kanisani kukiwa na shughuli au sherehe fulani.
·         Tamthiliya zinazochambua na kuhakiki asasi na maundisho ya dini kifasihi. Hizi ni kama vile
-          F.Topan “Aliyeonja Pepo” (1973)
-          Muba-“Maalimu” (1980)
-          Mulokozi “Mkwawa wa Uhehe” (1979).
Hawa wanaonyesha mikinzano iliyomo ndani ya mafundisho ya kidini, hasa pale mafundisho hayo yanapogongana na maisha halisi, sayansi au mantiki. Tamthiliya nyingine zinazoonyesha mgongano huo ni Kinjekitile (1969) na Njia Panda (1981).
4.      Ukombozi
Hizi zinazungumzia juu ya harakati za kumwondoa mkoloni hapa Afrika. Mfano wa tamthiliya hizo ni Nkwera “Mkwawa Mahinya” katika “Johari Ndogo” (1968), E.Hussein “Kinjekitile” (1969) na “Mashetani” (1971), M.Mulokozi “Mkwawa wa Uhehe” (1979), E.Mbogo “Tone la Mwisho” (1981), P.Muhando, N.Balisidya na A.Lihamba “Harakati za Ukombozi” (1972) na M.S.Masanja “Damu Imemwagika na Paulo! Paulo!” (1976), n.k. Tamthiliya hizi licha ya kujadili ukombozi wa kisiasa, vile vile zinajadili ukombozi wa kiuchumi na kiutamaduni.
5.      Ujenzi wa jamii mpya
Baadhi ya tamthiliya zinazojadiliwa zinazojadili suala hili ni za Ngahyoma “Kijiji Chetu” na M.Rutashobya “Nuru Mpya” (1980). Hawa walipendekeza marekebisho katika mfumo uliopo. Baadhi wameonyesha tu kuwa mambo siyo sawa. Mfano: Mbogo- Giza Limeingia (1980) na Hussein- “Mashetani” (1971) na wengineo wanalitazama suala hili kitabaka na kuhimiza mapambano ya wafanyakazi dhidi ya mabepari na ubepari- Kahigi na Ngemera- “Mwanzo wa Tufani” (1976) na Mazrui “Kilio cha Haki” (1981).
6.      Uke na matatizo ya kijinsia
Hawa wanaonyesha hali duni ya mwanamke katika jamii ya sasa, kutafuta sababu za hali hiyo na kupendekeza ufumbuzi. Baadhi ya tamthiliya hizo ni P.Muhando-“Nguzo Mama” (1982), Ngozi-“Machozi ya Mwanamke” (1977), Mulokozi-“Mkwawa wa Uhehe” (1979), Mazrui “Kilio cha Haki” (1981), E.Mbogo “Tone la Mwisho” (1981), E.Hussein “Kwenye Ukingo wa Thim” (1989).
7.      Uchawi, uganga na itikadi za jadi
Suala hili limejitokeza katika tamthiliya kadhaa. Kwa mfano, Mhanika-“Njia Panda” (1981), Mbogo “Ngoma ya Ng’wanamalundi” (1988), Hussein “Kinjekitile” (1969) na Kitsao “Mfarakano” (1975). Kwa ujumla, uganga na itikadi za jadi katika tamthiliya hizi husawiriwankama amali muhimu za jamii zifaazo kutatua baadhi ya matatizo ya kimaisha.
8.      Tatizo la ugonjwa wa UKIMWI
Hawa wanaonyesha madhara yanayotokana na ugonjwa wa UKIMWI kwa jamii. Tamthiliya hizo ni Ushuhuda wa Mifupa (1990), Mwalimu Rose (2007), Orodha (2006) na Kilio Chetu (1995).

TOFAUTI KATI YA TENZI NA MASHAIRI
Tenzi na mashairi hutofautiana, hasa katika vipengele muhimu vifuatavyo:
1.      Muundo,tenzi hutumia muundo wa tarbia tu katika beti zake ambapo mashairi yana uhuru wa kutumia miundo mingine tofauti kama vile tathlitha, takhmisa n.k
2.      Urefu,tenzi kwa kawaida huwa ni  ndefu kwa vile hutokea zikiwa katika mtindo wa usimulizi, na hivyo kuwa na beti nyingi sana ili kkamilisha usimulizi wa kisa ambapo mashairi kwa kawaida hutumia beti chache
3.      Vina,tenzi zina vina vya mwisho tu; hazina vina vya kati ambapo mashairi yana vina vya kati na vya mwisho.
4.      Urefu na mistari ,tenzi mistari yake ni mifupi; haigawanyiki katika nusu ya kwanza nay a pili, mashairi yake ni mirefu; na hugawanyika mara mbili, nusu ya kwanza na nusu ya pili (huitwa vipande).
5.      Idadi ya mizani, tenzi  katika mistari yake huwa na mizani nane tu, mashairi huwa na mizani 16 katika mistari yake.
6.      Kituo,kituo cha tenzi hubadilikabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Kituo cha shairi kinaweza kubadilika au kutokubadilika.
KANUNI ZA UTUNZI WA NGONJERA
Ngonjera ni tungo za kishairi zinazowasilishwa kwa kutumia mazungumzo ya majibizano baina ya watu wawili au zaidi. Mazungumzo hayo huwa na mjadala wa malumbano yenye lengo la kutoa ujumbe maalumu kwa wasikilizaji
Katika majibizano hayo, mhusika mmoja hueleza jambo fulani kwa ubeti mmoja, mhusika wa pili naye hujibu kwa kupinga au kuunga mkono hoja za mhusika aliyetangulia. Mwishoni mwa ngonjera wahusika hao huwa wanaondoa tofauti zao na kuwa na msimamo mmoja. Hali hiyo hutokea pale mhusika mmoja anakubali kulegeza msimamo wake na kukubaliana na mtazamo wa mwenzake.
Kanuni za utungaji wa ngonjera hazitofautiani na kanuni za utungaji wa mashairi ya kimapokezi. Ngonjera sharti iwe na kichwa, beti, vina, mizani, muwala, utoshelezi, kituo na urari wa mistari ya beti. Ngonjera pia, hutakiwa kutumia lugha ya kisanaa kama ilivyo kwa mashairi.
Mfano wa ngonjera: Mwenye nyumba na mhitaji  
MWENYE NYUMBA:  Nakwambieni jamaa, vya nyumbani mwangu visa,
                                   Mpangaji amekaa, huu mwezi wa tisa,
                                   Mpangaki ana baa, atoapo zangu pesa,
                                   Hivi sasa nimenusa, nataka kumfukuza.
MHITAJI:                    Taibu maneno yako, yananipata kabisa,
                                   Mimi mhitaji kwako, chumba sina nimekosa,
                                   Sema kodi iliyoko, unayopokea sasa,
                                   Name nitakupa pesa, upate kumfukza.
MWENYE NYUMBA:  Kwa hesabu iliyoko, mimi sipati halasa,
                                  Thelethini ndizo ziko, alipazo Bwana Musa,
                                  Kinipa sitini zako, atatoka hivi sasa,
                                  Himiza unipe pesa, nipate kumfukuza.

MHITAJI:                   Sitini ni hizi hapa, pokea ni kama posa,
                                  Na kodi hasa talipa, daima bila kukosa,
                                  Tena Wallahi naapa, kulipa sitakutesa,
                                  Nenda kafanye mkasa, upate kumfukuza.
                                        (Kutoka: Ngonjera za UKUTA, uk 86-87)
TOFAUTI KATI YA NGONJERA NA MASHAIRI
Ngonjera hutofutiana na mashairi katika vipengele vine, navyo ni wahusika, namna ya uwasilishaji, kituo, na matumizi ya lugha.
1.      Wahusika,ngonjera hutumia wahusika wanaojibizana. Wahusika hao wanaweza  kuwa wawili au zaidi, ambapo shairi hutumia mhusika mmoja tu anayezungumza au anayetoa mawazo yake pasipo kujibizana na mtu.
2.      Uwasilishaji, ngonjera huwasilishwa kwa njia ya uzungumzaji wa kujibizana, mashairi huwasilishwa kwa njia ya uimbaji.
3.      Kituo,ngonjera huwa na vituo tofauti kwa vile kila mzungumzaji huwa na ktuo chake, lakini shairi huwa na kituo kimoja tu na hata kama kitabadilikabadilika huwa hakilengi kuonyesha mtazamo wa ukinzani wa mada inayojadiliwa kama ilivyo kwa vituo vya ngonjera.
4.      Matumizi ya lugha, ngonjera hutumia sana lugha rahisi lakini mashairi hutumia sana lugha ya kuzama.








 [H1]


 [H2]
Powered by Blogger.