MADA 1-KISWAHILI 2 : FASIHI KWA UJUMLA

    MADA 1  :  FASIHI KWA UJUMLA
NADHARIA YA FASIHI
Nadharia ni Imani au kanuni zinazofuatwa na watu Fula
ni au jamii katika kushughulikia  jambo Fulani mahsusi.
Nadharia za fasihi ni muongozo au kanuni zinazofuatwa na wataalamu (wanazuoni) mbalimbali katika kuteua fasili/maana halisi ya fasihi.
Fasihi ni nini?
Wataalamu mbalimbali wamefasili/Maana ya dhana ya fasihi, maana hizo ni kama zifuatazo:-
1.      Fasihi ni kioo cha jamii (maisha),Kwa maana kwamba mtu anaweza akajitazama akaona taswira yake na akajirekebisha . Fasihi hii ina udhaifu kwani kioo hakiwezi kumweleza  mtu jambo la kufanya ili hali yake iwe bora zaidi . Pia si sehemu zote takazojiona kwenye kioo(F.Mkwera , 1978)
2.       Fasihi ni hisi,Fasili ina maana kuwa lazima pawe na mguso fulani wa wahusika ndipo mtu aweze kuandika na kueleza jambo fulani,’Sengo na kiango  Wanasema “hisi ni kama kuona njaa, baridi, joto, uchovu pengine kuumwa. Hapa swali la kujiuliza ni kwamba, je fasihi ina maana moja kati ya hiyo? Uamuzi wa kutenda jambo huja wakati umeguswa?. Je hizo hisia ziko wapi? Je mtu ambaye haguswi  sana moyoni hawezi kuwa mwanafasihi  mashuhuri? Je mwanamuziki ambaye huusifu uzuri wa mwanamke anaguswa moyoni? Je mwandishi kama Shaban Robert,  E. Kazilahabi wameguswa mara ngapi? Vile vile kivipi waguswe Zaidi ya wengine?  (Sengo na Kiango) hivyo bado fasili hii ina udhaifu
3.       Fasihi ni mwamvuli wa mtu na jamii na utu na maisha ya hadhi na taadhima.Fasihi  hii ina maana kwamba mwamvuli humkinga mtu katika mvua na jua na fasihi huhifadhi na kukinga amali za jamii zisiharibike maana hii ni nzuri kwani inasisitiza utunzaji wa kile kizuri kwa maana kuwa jamii inachambua kuwa makini na kuona amali za jamii zinazohifadhiwa. Lakini swali la kujiuliza ni  kwamba jamii itasaidiwa?
Jamii haitulii kama maji katika mtungi  bali hubadilika mara kwa mara kutokana na nguvu za migongano, hivyo kitu kipya huzaliwa na cha zamani hufa kwasababu jamii haitulii, hivyo hakuna haja ya kuhifadhi amali za jamii chini ya mwamvuli. Zipo mila na desturi zilizohifadhiwa na makabila mengi ambazo hazina nafasi leo. Hali ya mabadiliko ya jamii kutokana na siasa, utawala, uchumi, elimu, sayansi na teknolojia vyote hivi katika maendeleo vitatoboa mwamvuli na kuziharibu amali zilizohifadhiwa (Sengo na Kiango 1973)
4.       Fasihi ni sanaa ya uchambuzi wa lugha yoyote kadri inavyosemwa,inavyoandikwa na kusomwa,Hii ni kweli kuwa fasihi lazima itumie lugha kwani lugha ndicho chombo muhimu kitumiwacho na fasihi na si fasihi  tu bali taaluma zote hutumia lugha.Udhaifu wa fasili hii ni kwamba maana hii imejikita katika uchambuzi wa Lugha kana kwamba hakuna vipengele vingine vinavyochambuliwa katika fasihi zaidi ya lugha na hii ni sawa na kusema umeme ni waya wa shaba kwa vile umeme umepita kwenye waya huo.Na hii ni si kweli kwani Hisabati,fizikia au historia si fasihi ingawa hutumia lugha.
5.Fasihi ni kielelezo cha hisia za mwandishi juu ya mambo yanayomwathiri yeye,kikundi au jamii nzima anamoishi na kwamba lengo lake ni kustarehesha au kufunza wasomaji.Fasili(maana) hii ni nzuri kwa ujumla lakini mapungufu yake ni kwamba imemuwekea mwandishi kama chanzo pekee cha uumbaji wa Sanaa na hasa akili yake pia maana hii imetokana  na falsafa ya kidhaanifu kwa kuhusisha uchambuzi wa mambo katika fikra bila  kutazama hali halisi ya maisha ya watu na vitu.
   6.    Fasihi ni chombo cha utetezi wa maslahi ya tabaka moja au jingine na kwamba mwandishi ni mtumishi wake anayejijua au asiyejijua atake asitake mwandishi huyu analengo au dhamira fulani anayotaka kuionesha.Wasomaji wanaweza kuyakubali au kuyakataa maudhui ya kazi yake na pengine jamii kufuatana na msimamo juu ya itikadi ya siasa (napengine amali za jamii) inayotawala kwa kipindi kile  na jinsi mwandishi anavyooanisha maandishi yake na itikadi hiyo.
Fasili au maana hii ni nzuri sana kwani kwa kifupi ni kwamba fasihi ni mojawapo ya silaha nyingi zinazotumiwa na tabaka moja kutetea maslahi yake katika mapambano ya kudumu dhidi ya matabaka mengine.
Hitimisho kwa ufupi fasihi ni taaluma inayotumia Sanaa maalumu ya lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii inayohusika.Fasihi hutueleza uzuri wa maandishi au mazungumzo ambayo huonekana katika mashairi ,historia za maisha ya watu ,tenzi,hadithi za kusisimua na insha mbali mbali.

DHIMA YA MWANAFASIHI KATIKA JAMII
Maana ya mwanafasihi/mtunzi wa kazi ya fasihi
Ni mtu yeyote anayejishughulisha na uandishi au utungaji wa kazi za fasihi yaani fasihi andishi na fasihi simulizi.
DHIMA ZA MWANAFASIHI
1. .Kuelimisha jamii,Katika kuelimisha jamii mwanafasihi ;
  (a)Huchambua na kuchochea umma kuwafumbua macho,hufichua wazo au uchafu uliomo katika jamii,wagandamizaji hufichuliwa na wagandamizwao hupewa muongozo sahihi ili waitambue hali yao dhaifu.Mfano”Duka la Kaya”imechambua na kuchochea jamii ili iweze kupambana na hali mbaya ya maisha.
(b).Kupiga vita kwa hali na mali mazingira yote ya ujinga,maradhi,njaa na umaskini,Mfano mwandishi wa tamthiliya ya Hawala ya fedha anapambana na maovu kama vile ujinga na uvivu na Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe anajadili na kupiga vita uzembe  na mengineyo.
(c).Kukosoa jamii,Mwanafasihi anaikosoa jamii katika vipengele mbalimbali vya maisha.Mfano riwaya ya “ Vuta n’kuvute”inakosoa mila na desturi zilizopitwa na wakati “Raha karaha na Mashairi ya Chekacheka”mwandishi wa diwani hizi anaikosoa jamii ya Tanzania kwa mapana kama vile Uongozi mbaya,kukithiri kwa rushwa n.k.
(d).Kutia hamasa na kumfanya mtu asikate tamaa,Mfano S.Kandoro anaeleza hamasa ya wananchi waliokuwa wameungana kama “Siafu ili kumtoa nyoka pangoni katika shairi  liitwalo  ‘Siafu wamekazana’’.Mwandishi kwa hamasa amewaita waafrika njooni “au” kwetu ni kwa nini’.Hivyo ni wazi kuwa kazi hizi zinajitahidi kuendeleza mapambano dhidi ya ukoloni  mambo leo.
(e)Mwandisi anadhima kujenga misingi na fikra za usawa na demokrasia miongoni mwa umma wa wakulima na wafanyakazi,Mwanafasihi huyu huwatukuza wakulima na wafanyakazi pamoja na amali zao.
(f) Mwanafasihi hueneza mawazo na falsafa za jamii,Kwa mfano katika shairi na ngonjera za Mathias Mnyapala ametangaza sana siasa ya ujamaa na kujitegemea kwa kutumia ngonjera za UKUTA 1 & 2 vile vile riwaya kama vile mfaa na utu,njozi za usiku,ndoto yandaria ,jero si kitu n.k zimetangaza sana siasa ya ujamaa na kujitegemea hapa nchini Shaban Robert aliwahi kueneza falsafa juu ya kweli kwa kiasi kikubwa katika mashairi yake.
(g)Mwanafasihi hutoa mwongozo kwa kuikomboa jamii kutoka fikra mbovu za kugandamizwa,kunyonywa na kuonewa na kujikomboa ili iweze kupata haki na usawa,Mfano Riwaya ya kiimbila “Ubeberu Utashindwa” na tamthiliya ya E.Mbogo “Tone la Mwisho” G Husseni “Kinjekitile”
2.Kuburudisha,zipo kazi mbalimbali za fasihi zinazoburudisha.Msomaji au msikilizaji wa fasihi huburudisha yaani husisimsha mwili na akili na huvutiwa kihisia na kazi ya fasihi anayoisoma au kusikiliza.Tabia ya msomaji au msikilizaji huweza kujengwa kutokana na mafunzo na mifano bora ya matendo ya kuigwa anayoyapata katika fasihi.
3.Kuhifadhi na kurithisha amali za jamii,Amali za jamii ni pamoja na mila na desturi mtindo wa maisha,Imani, historia jiografia,visasili na visakale ni urithi wa maarifa ya kijadi kwa mfano tiba, sayansi ya kilimo,mbinu za uwindaji,ufundi wa aina zote n.k.Amali hizo huweza kuhifadhiwa na kuendelezwa na mwanafasihi na hivyo kurithishwa kwa vizazi vijavyo.
Kwa mfano tamthiliya ya Kinjikitile inahifadhi mengi kuhusu hali ya maisha wakati wa ukoloni wa kidachi,Kurwa na Doto (1969) ni riwaya yenye kuhifadhi japo kwa kejeli,mila,desturi na itikadi za jadi za waunguja,Riwaya ya Bwana Mnyombokero na Bibi Bugonoka;Ntuhanalwo na Buliwali  iliyoandikwa na Anicet Kitereza imehifadhi mila,Imani,mtindo wa maisha,ufundi na taaluma mbalimbali za jadi za wakerewe mengi yaliyoeleza humo siku hizi hayapatikani popote isipokuwa katika riwaya hiyo, vile vile Mzishi wa Baba ana Radhi (1967) kinaeleza mila na desturi za wapangwa.
Watunzi hasa nyimbo na visasili hukoleza pia shughuli za kijadi za kiutamaduni kwa mfano Ibada,matambiko,sherehe,katika shughuli za aina hiyo nyimbo licha ya kuwa kiburudisho hubeba ujumbe wenye kuhusiana na tukio hilo.
4.Kudumisha na kuendeleza lugha,Kwa kadri lugha inavyotumiwa na kufinyangwa na watunzi ndivyo inavyokuwa na kupevuka.Maneno mengi yatumiwayo leo katika lugha mbalimbali yalibuniwa na kuenezwa na watunzi wa mashairi,riwaya,nyimbo na tamthiliya katika Kiswahili.Mifano mizuri ni maneno mengi yahusuyo Sanaa ya ushairi(vina, mizani, beti, mishororo, miwala, tathlitha, takhimisa, tarbia n.k)
Katika jadi ya ushairi wa kiswahili inadaiwa kuwa ushairi ulikua ni ghala ya maneno.Washairi walitumia maneno magumu au yasiyokuwa ya kawaida makusudi ili kuyahifadhi ysipote.katika tamaduni nyingine kazi hiyo hufanywa na kamusi pamoja na vitabu viitwavyo Hazina ya maneno kwa kuwa waswahili hawakuwa na kamusi kazi ya kuhifadhi maneno ilifanywa na ushairi.
FASIHI NI SANAA.
Sanaa ni uzuri unajitokeza katika umbo lililosanifiwa umbo ambalo mtu hulitumia kuelezea hisia zinazomgusa kwa kutoa kielelezo au vielelezo vyenye maana maalumu.
               Aina za Sanaa
i)        Sanaa za Uonyeshi,ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa na uzuri wake kuonyeshwa wakati wowote. mfano uchoraji, uchongaji, kutarizi, ufinyanzi, n.k. Sanaa ambazo hututolea vitu kama vile picha, vinyago, nguo zilizotarizwa, vyungu n.k.
ii)      Sanaa za Ghibu,ni sanaa ambazo uzuri wake haujitokezi kwenye umbo linaloonekana kwa macho au kushikika bali  katika umbo linalogusa hisia mfano ushairi, uimbaji, upgaji muziki, n.k. Uzuri wa sanaa hizi umo katika kuzisikia.
iii)    Sanaa za Vitendo,ni sanaa ambazo uzuri wake umo katika umbo la vitendo. Uzuri wa sanaa  hizi umo katika umbo la vitendo, na ili kuupata uzuri huu yampasa mtu kutazama vitendo vikifanyika. Umbo hili linalazimisha kuwepo kwa mwanasanaa (mtendaji) na mtazamaji(Hadhira) wa sanaa mahali pamoja kwa wakati mmoja, ama sivyo sanaa haikamiliki. Hali hii ndiyo inayosababisha sanaa hizi za vitendo kuita sanaa za maonyesho kwa sababu lazima wakati zinapototendeka awepo mtu wa kuonyeshwa, maana uzuri wake umo katika vitendo vyenyewe.

SIFA ZA SANAA ZA MAONESHO
-          Dhana ya kutendeka (tendo)
-          Mtendaji (fanani)
-          Uwanja wa kutendea/jukwaa maalumu
-          Watazamaji (hadhira).
Hivyo sanaa za maonyesho ni dhana zilizo kwenye umbo linalotendeka na  ili dhana hii itendeke inahitaji mtu wa kuitenda (mtendaji). Mtendaji huhitaji uwanja wa kutendea hiyo dhana, na wakati akiitenda hiyo dhana wanakuwepo watazamaji.
                     Tanzu za Sanaa za Maonyesho
i)        Tambiko
Ni sadaka inayotolewa kwa miungu au mahoka, mizimu, pepo, n.k.  wakati wa kusalia miungu.
Matambiko yalikuwa na umuhimu mkubwa katika jamii za babu zetu kuliko siku hizi. Jamii ya asili ilipokabiliwa na matatizo yaliyowashinda kama vile magonjwa, ukame, au kukosa mtoto, n.k. walifanya tambiko na kusali ili miungu yao iwasaidie. Wakati fulani walifanya matambiko kwa ajili ya kuomba radhi au kutoa heshima na shukrani.
Mara nyingi matambiko haya huandamana na kafara kama sadaka inayotolewa na jamii kwa wahenga wao. Kafara inaweza kuwa ya kuku, kondoo, ng’ombe, mbuzi au chakula. Katika jamii nyingi za Kiafrika kabla ya ukoloni walitoa kafara ya binadamu.

Fani katika Tambiko
Ø  Sanaa
Katika tambiko sanaa inayotendeka ni ule ufundi wa kutenda vitendo kwa ukamilifu kwa kutambika kwa kutumia ufundi wa aina fulani.
Ø  Wahusika
Wahusika wa tambiko ni wale wazee maarufu walioteuliwa na jamii kuendesha shughuli hizi za matambiko. Si watu wote katika jamii huhusika.
Ø  Mazingira (Mahali)
Tambiko linaweza kufanyika porini, makaburini, njia panda, kwenye mti mkubwa au mahali popote kutegemeana na aina ya tambiko lenyewe.
Umuhimu wa Tambiko
1)      Hujenga imani kama chombo cha kutatulia matatizo ya jamii. Jamii ya asili ilipokabiliwa na matatizo ilifanya tambiko na kusali ili miungu iwasaidie kuondokana na tatizo hilo.
2)      Tambiko husaidia kuendeleza mila na desturi za jamii.
3)      Tambiko hujenga na kuimarisha mahusiano miongoni mwa wanajamii.
4)      Matambiko huiongoza jamii katika mapambano dhidi ya matatizo mbalimbali yanayowakabili.
Hasara za Tambiko
1)      Hujenga dhana potofu katika jamii kwani watu huamini nguvu fulani bila kuwa na uhakika au uthibitisho wa kisayansi.
2)      Huleta hasara kubwa kwa jamii kwani kafara ya tambiko inahitaji mnyama au chakula, ambapo watu hutumia hela nyingi kuvipata vitu hivyo.
ii)       Mivigha
Ni sherehe zinazofanywa na jamii katika kipindi maalumu cha mwaka. Mivigha hufanywa  kwa lengo la kufundisha jambo fulani maalumu kwa maisha ya jamii. Sanaa za maonyesho katika kundi hili zinahusu kuingizwa kwa mwanajamii kwenye kundi la watu wa aina fulani kutoka kundi la watu wa aina nyingine. Mfano jando na unyago, harusi, kutawazwa chifu, n.k.Katika jando na unyago mtu hutoka kundi la watoto kuingia kundi la watu wazima, mtu aliyeoa anatoka kundi la makapera kwenda kundi la waliooa au kutawazwa chifu, mtu anatoka kundi la raia na kuingia kundi la watawala n.k.
Kutoka kundi moja kuingia kundi jingine ni hatua iliyopewa umuhimu mkubwa katika jamii ya asili. Umuhimu huu uliambatana na madaraka mapya yaliyo mkabili mwanajamii kuingia katika kundi jipya. Kila kundi la watu lilikuwa na madaraka fulani mbayo kutekelezwa kwake ndiko kulikoleta maendeleo ya jamii .
                              Fani katika  Mivigha
Ø  Sanaa
Sanaa katika mivigha ni ule ufundi wa kutenda kikamlifu na kiufundi katika kudhihirisha yale yanayotendeka.
Ø  Wahusika
Katika mivigha wahusika ni wa aina tatu:
a)      Mtendaji/watendaji,ni wale wote wanaoshiriki kutenda ile dhana ya kuwatoa watu kutoka kundi moja na kuwaingiza katika kundi lingine. Vitendo hivyo huambatana na nyimbo, michezo mbalimbali n.k.
b)      Watazamaji ,ni wale wanaoingia kutoka kundi moja na kwenda kundi lingine. Hawa ndio watazamaji, kwa sababu maneno, nyimbo, vitendo, ngoma, n.k. vyote vinafanyika ili wao wavione na wajifunze na baadae watekeleze yale waliyojifunza.
c)       Waangaliaji, ni wale wanaoangalia mambo yanayotendeka bila wao kushiriki katika kucheza au kuimba au kutoa mafunzo, wanaangalia tu. Hawa kwa upande wa sanaa za maonyesho sio watazamaji kwa sababu yale yafanywayo hayawasilishwi kwao. Wakiwepo au wasiwepo bado vitendo vinatendeka tu bila maana yake kupotea. Hawa wanaitwa “waangaliaji”
    (d)  Mahali /Mandhari,kwa upande wa mivigha uwanja wa kutendea ni mahali sherehe zinapofanyika. Inaweza ikawa ndani ya nyumba, au porini, kwenye uwanja wa nje ya nyumba,milimani au mapanngoni, n.k.
Umuhimu wa mivigha
1)      Mivigha hufundisha umuhimu wa kazi kama vile kilimo, uwindaji, uhunzi, ufinyanzi, ushonaji, n.k.
2)      Mivigha huhimiza umuhimu wa ujasiri katika maisha.
3)      Mivigha  hufundisha suala zima la unyumba na malezi kwa ujumla mfano  umuhimu wa uzazi na malezi bora.
4)      Mivigha husisitiza umuhimu wa umoja na ushirikiano katika jamii.
                                    Hasara za Mivigha
1)      Hugharimu pesa nyingi sana ambapo huwaacha wenye sherehe kwenye madeni makubwa.
2)      Sherehe huweza kusababisha ugomvi, chuki, dharau, tamaa, n.k.
3)      Huleta ushindani na matokeo yake husababisha baadhi ya watu wasio na uwezo hujiingiza katika wizi, utapeli, ujambazi, n.k.
                                          3. Majigambo
Ni masimulizi ya kujigamba kwa mtu kuhusu mambo ya kishujaa aliyopata kuyatenda maishani mwake. Majigambo hayo husimuliwa katika lugha ya kishairi na masimulizi yake huambatanishwa na vitendo vya mjigambaji mwenyewe.
Mtambaji anapotamba katika sanaa hii, kwa kawaida huwa na tabia ya kujivuna au kujitapa kuwa yeye ni bora kuliko wengine wote.
Wakati wa utambaji mazingira humtawala fanani. Pengine fanani alikuwa akitamba kuonyesha utukufu wake kwa mfalme wao. Au alikuwa akitamba wakati wa kujiandaa kwenda vitani.
Fani katika Majigambo
Ø  Sanaa
Sanaa katika majigambo ni ule ufundi anaoutenda mjigambaji, kwa kujigamba kwa ufundi huku akionyesha vitendo waziwazi alivyopata kuvitenda maishani mwake.
Ø  Wahusika
Hapa kuna mtendaji na watazamaji
·         Mtendaji ,ni yule anayejigamba mbele ya wenzake, yaani Yule anayejigamba kuhusu mambo yake ya kishujaa aliyoyatenda maishani mwake.
·         Watazamaji,ni wale wanaotazama vitendo vinavyotendwa na mtendaji.
Ø  Mahali/Jukwaa maalum
Uwanja wa kutendea ni mahali popote ambapo majigambo yanaweza kufanyikia. Hapa inaweza kuwa kwenye uwanja mkubwa ambapo sherehe hizo zinafanyikia au kwenye ukumbi.
Ø  Matumizi ya Ngoma katika Majigambo
Majigambo vile vile yaliambatana na ngoma, wakati mwingine ngoma zilichezwa na katikati ya ngoma mjigambaji mmoja alijitokeza na kuanza kujigamba, alipomaliza alirudi kucheza ngoma na mwingine alijitokeza tena.
      Umuhimu wa Majigambo
1)      Hudumisha utu wa mwanaume katika jamii.
2)      Hudumisha ari ya kuwa wakakamavu, shujaa na jasiri katika jamii.
3)      Huburudisha jamii yaani mtendaji na wasikilizaji.
Hasara za Majigambo
1)      Hukuza na kuendeleza ubinafsi kwani fanani huonekana ni bora zaidi kuliko watu wengine.
2)      Mkusanyiko wa hadhira hutumia pesa au vyakula kwa wingi, hivyo husababisha umasikini .
3)      Majigambo husababisha unafiki kwa sababu fanani huonyesha mafanikio yake tu na sehemu alizoshindwa hagusii kabisa, kitu ambacho si cha kweli katika maisha ya mwanadamu.
4         .Michezo ya Watoto
Ni mchezo mbalimbali inayochezwa na watoto, na michezo hiyo hufungamana na hali ya utamaduni, uchumi na siasa ya jamii inayohusika. Mchezo hii husaidia watoto waweze kujifunza mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii yao. Kwa njia hii watoto hujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji kama vile kilimo, kupika chakula, kuwinda, n.k. Vile vile hucheza mchezo wa baba na mama. Hapa mtoto mmoja anakuwa mama, mwingine baba na wengine watoto. Mchezo huu huakisi mambo halisi ya nyumbani.
                              Fani katika Michezo ya Watoto
Ø  Sanaa
Sanaa katika michezo ya watoto wadogo ni ule ufundi wa kutenda vitendo kikamilifu na kuonyesha ujuzi mkubwa katika utendaji huo
Ø  Wahusika
Kuna watendaji na watazamaji. Watendaji ni watoto wenyewe wanaocheza michezo hiyo, yaani wavulana na wasichana. Idadi ya watendaji inategemea aina ya mchezo wenyewe.Watazamaji ni wale wanaotazama mchezo huo. Hapa  wanaweza wakawa watoto wenyewe ambao hawachezi au jamii inayowazunguka watoto hao.
Ø  Mahali
Uwanja wa kutendea michezo ya watoto ni sehemu yoyote itakayochaguliwa na watoto wenyewe kulingana na michezo unaohusika. Kwa mfano, wanaweza kucheza uwanjani, chini ya mti, barabarani, chumbani, sebuleni, kando ya nyumba, n.k.

Umuhimu wa Michezo ya Watoto
1)      Huwasaidia watoto wadogo kujifunza mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii yao. Kwa njia hii watoto hujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji mali, utamaduni na siasa ya jamii yao.
2)      Huwasaidia watoto kujifunza kuwa na ujasiri, ushujaa, udadisi wa mbinu mbalimbali za kupambana na matatizo yanayojitokeza katika jamii.
3)       Hurithisha amali za jamii toka kizazi kimoja hadi kizazi kingine. Michezo hii hurithisha mila na desturi za jamii fulani kwa kucheza michezo hiyo.
4)      Michezo hiyo huburudisha watoto. Katika kucheza michezo hiyo, watoto huburudika na kustarehe.
5)      Huwasaidia watoto huimarisha viungo vya mwili kwa watoto wanaocheza michezo hiyo.
Hasara za Michezo ya Watoto Wadogo
Ø  Watoto huweza kuumizana kutokana na michezo hii.
Ø  Ikiwa wazazi wa watoto hawa wana tabia chafu kama ile ya kugombana, kutukanana ovyo, vivyo hivyo watoto hawa watarithi tabia chafu kutoka kwa wazazi wao na wanaweza kuwaambukiza wenzao.
5. Utani
Ni hali ya kufanyiana mizaha pasipo kuogopa na kushtakiana au utani ni uhusiano wa kutaniana au kufanyiana masihara ambao ni tofauti na desturi za kutokuheshimiana. Madhumuni yake makubwa ni kupunguza na kuondoa kabisa uhasama na chuki iliyokuwepo baina ya makundi fulani ya watu.
Fani katika Utani
Ø  Sanaa
Sanaa katika utani ni ule ufundi na uwezo wa kutaniana baina ya wahusika wanaohusika na utani huo.
Ø  Wahusika
Katika utani, washiriki wanaweza kuwa mtu na mtu, familia na familia, kabila na kabila, ukoo na ukoo au nchi na nchi.
Ø  Mahali
Uwanja wa kutendea inaweza kuwa mahali popote ambapo utani unaweza kufanyika. Inaweza ikawa kwenye harusi, msibani, kwenye pombe wakati watu wanakunywa, n.k.
Umuhimu wa Utani
1)      Kutoa maadili na mafunzo fulani kwa jamii.
2)      Kuimarisha umoja na ushirikiano miongoni mwa wanajamii (kujenga undugu)
3)      Kuhimiza ujasiri na juhudi katika maisha.
4)      Kuhimiza upendo katika maisha.
5)      Hukuza na kuimarisha mila na desturi za jamii.
Hasara za Utani
1)      Husababisha ugomvi katika jamii.
2)      Huleta hasara za kuchukuliana vitu bila malipo.
3)      Huvunja au kuvunjiana heshima miongoni mwa wahusika.
Kazi za fasihi zipo katika nyanja zifuatazo uchoraji, ususi, fasihi, ufinyanzi, muziki, ufumaji, utarizi na maonesho.Nyanja hizi za Sanaa zinaweza kuonyeshwa kwenye kielelezo hiki:-

Ufumaji

Muziki

Utarizi
                                          

Uchoraji
 



     SANAA

        Fasihi
                                                                                   

Ufinyanzi
FASIHI                                  SANAA
                                                                                           

        Uchongaji

Maonyesho

Ususi
 




Kila kipengele cha Sanaa kinatofautiana   na kingine kwa umbo na matumizi. Fasihi ni kipengele cha Sanaa kinachotumia maneno kuumba huo uzuri wa kisanaa.
TOFAUTI KATI YA FASIHI NA TANZU NYINGINE ZA SANAA
1.       Lugha , kazi zote za kifasihi zinaundwa kisanaa kwa kutumia lugha inayotumika au kuandikika. Lugha hiyo hubeba maana Fulani (ujumbe) kwa jamii Fulani.Hivyo lugha ndiyo inayotufautisha fasihi na Sanaa nyingine. Kwa mfano, uchoraji kipengele chake muhimu kalamu, rangi na kipande cha nguo au karatasi. Ufinyanzi lugha yake ni udongo , uchongaji wa vinyago lugha yake ni gogo la mti n.k. Fasihi si maelezo ya kawaida kawaida kama vile matangazo, taarifa ya habari au barua, fasihi ni maelezo yenye mguso kisanaa. Kazi za kifasihi, huumbwa kimafumbo hutumia nahau au misemo , methali, tamathali za semi, taswira na ishara mbali mbali. Kazi za fasihi hufikirisha mtu huweza kutumia akili ili aweze kugundua kazi ya kifasihi aliyosoma au kuisikia kuwa ina maana gani.
2.       Wahusika,kazi yeyote ya fasihi inakuwa na wahusika wake ambao matukio mbali mbali yanayohusu jamii huwazungukia wahusika ni watu ama viumbe, waliokusudiwa wawakilishe tabia za watu katika kazi za fasihi. Kwa upande mwingine wahusika ni muhimu sana katika kutoa na kufikisha dhamira kwa hadira iliyokusudiwa na mwandishi.
3.       Mandhari, kazi ya fasihi inakuwa na mandhri ambayo huonyesha tukio linaponyika. Mandhari hiyo inaweza kuwa ya kubuni au ya kweli.Mandhari husaidia kujenga hisia inayokusudiwa na mwandishi.
4         . Utendaji, utendaji hasa katika fasihi simulizi hushirikisha fanani na hadhira kwa wakati mmoja. Vile vile utendaji humfanya fanani aweze kuonyesha baadhi yamatendo katika usimulizi wake.
5         Fani na maudhui,kazi za fasihi zina sehemu mbili yaani fani na maudhui na sehemu hizi zinafungamana. Maudhui ni kile kinachosemwa na fani ni namna kinavyosemwa. Kazi nyingine za Sanaa vile vile zinafanikisha ujumbe kwa hadhira lakini mbinu na vifaa vinavyotumika ni sehemu ya fasihi. Kwa ujumla kazi za kifasihi, fani na maudhui yake ni ya hali ya juu sana ukilinganisha  na Sanaa nyinginezo.
KWA VIPI FASIHI NI SANAA ?
    Usanaa wa fasihi hujitokeza katikavipengele mbali mbali kama ifuatavyo:-
1.       Mtindo, Sanaa katika fasihi hujidhihirisha katika namna kueleza jamii (mtindo) katika kueleza jambo kunakuwa na aina fulani ya kiufundi ambao mwanafasihi huutumia katika kufikisha ujumbe kwa jamii yake. Taarifa inayotolewa inaweza kufichwa katika fumbo, shairi, kitendawili, tamthiliya au hadithi.
2.       Muundo (mpangilio maalumu wa matukio),katika kazi ya fasihi, matukio yanapangwa kiufundi ili yaweze kuwasilishwa vizuri kwa jamii husika. Matukio hayapangwi ovyo ovyo tu bali yanakuwa na mpangilio maalumu.
3.       Utenzi mzuri wa lugha iliyojaa nahau, misemo, methali, tamathali za semi,taswira na ishara mbali mbali unaonyesha wazi usanaa wa fasihi. Lugha itumikayo katika fasihi ni ya kisanaa. Ni lugha iliyopambwa na inayokusudiwa kuibua hisia za namna Fulani kwa hadhira yake. Lugha hiyo inaweza kuchekesha, kukejeli, kubeza, kuchokoza, kutia hamasa au kushawishi. Matumizi ya lugha yako ya aina tofauti, kuna tamathali za semi, misemo, nahau, methali. Lugha ya wahusika hasa lahaja zao, uchaguzi wa msamiati,ufundi wa kutoa maelezo hasa ya wahusika ya mandhari na matukio, uteuzi wa lugha yenyewe itumiwayo.
4.       Uundaji wa wahusika, wahusika huwa na tabia zinazotofautiana kati yao. Wanaundwa kiufundi sana na msanii anaweza kuamua anataka wahusika wanaowakilisha tabia na matendo fulani tu katika jamii na kwa hiyo atawaumba wahusika hao ili kukamilisha nia na lengo lake.Katika kutofautisha tabia na hali za wahusika, mwandishi analazimika kutumia mbinu ya kuwapa majina wahusika wake. Wahusika wanaweza kuumbwa kinafsi au kiakili na kimwili. Kutokana na ujenzi wa aina hii mhusika huonyesha wasifu wake wa ndani na nje au anaweza kuonyesha mabadiliko yake kila anapokutana na mazingira tofauti.
5.       Ujengaji mzuri wa Mandhari, fasihi hujengwa katika mazingira maalum. Mandhari husaidia sana kujenga hisia inayokusudiwa na mwandishi. Mandhari yanajengwa kiufundi na mwandishi ili yasaidie katika kujenga kazi nzima ya fasihi.

  MADA NDOGO; MAENDELEO YA FASIHI
  CHIMBUKO LA FASIHI NA SANAA.
Kuna mitizamo mikuu minne  ya kiulimwengu inavyotokeza katika suala la chimbuko la fasihi .Mitazamo hiyo ni  kama ifuatayo;
1.       Mtazamo wa kidhanifu.
Mtazamo wa kidhanifu wa misingi yake katika kudhani tu kwa hiyo kufuatana na mtazamo huu inaaminika kuwa fasihi na Sanaa kwa ujumla kutoka kwa Mungu kwa hiyo mwanasanaa huipokea ikiwa imekwishapikwa na kuivishwa na Mungu huyo.
Mtazamo wa namna hii ulijitokeza tangu zamani sana wakati wanafalsafa wa mwanzo wa kigiriki na kinenzi kama vile Socrafes Plato na Anstotle,walipoanza kuingia katika ulimwengu wa nadharia ya Sanaa. katika uwanja wa nadharia ya fasihi/Sanaa ya Kiswahili kuna mifano mingi ya wahakiki wa mwanzo waliokuwa na mitazamo sawa naya wanafalsafa hao mfano F.Nkwera (1970),  insha yake ya fasihi inadhihirisha uaminifu wake wa mawazo ya kidhanifu kwa kudai “fasihi ni Sanaa ambayo huanzia kwa muumba humfikia mtu katika vipengele mbalimbali -ni hekima ambayo mtu ameshirikishwa apate kumtambua muumba  wake”.
Nkwera ameungwa mkono na wahakiki wengine ambao wanasisitiza mtazamo huu kwa kusema
“Mtengenezo ya Sanaa huonekana kuwa ni shughuli ya kiungu yenyekumwiga Mungu ambaye ndiye msanii wa kwanza”
John Ramadhani pia katika makala yake ya fasihi ya Kiswahili anasisitiza kuwa.
Zaidi ya kwamba fasihi ni hisia vile vile kitengo cha mtu cha kubaini kazi ya Sanaa ni uigaji wa Mungu ambaye ndiye mfalme wa Sanaa zote”.
Mawazo haya ya akina Nkwera,John Ramadhani na wengine yamejaa   mwangwi tu wa mawazo yaliyochakaa ambayo yalikwisha kutajwa na kushughulikiwa  na wahakiki wa zamani tuliowataja kwa msimamo huu wa kidhanifu,Sanaa au fasihi havijifinyangwi kwa jitihada za akili za mikono ya mtu   bali hupokelewa kutoka katika mikono mbayo mtu hana uwezo wa kuiona.
Udhaifu, mtazamo  huu  umepotosha maana halisi kwa kuchanganya Imani na taaluma,pia unajaribu kumtenganisha msanii na jamii yake kwani unatoa nadharia inayomwinua msanii na kufanya aonekane kuwa  mtu wa ajabu aliyekaribu na Mungu kuliko watu wengine wa kawaida.
2.       Mtazamo wa kiyakinifu
Kulingana na mtazamo huu Chanzo cha fasihi  ni sawa na chanzo cha binadamu wenyewe yaani Binadamu na mazingira yake ndio Alfa na Omega ya fasihi.Iwe kwa kuumbwa au mabadiliko kuanzia chembe hai ambayo imepitia maendeleo kadha ya makuzi hata kufikia mtu binadamu alioanishwa na kazi ili kuyabadili mazingira yake.Katika harakati zake za kujiendeleza kiuchumi kila mara alijaribu hiki na kile alichokiona kinafaa alikiendeleza Zaidi na kukidumisha katika hali hii hadithi(ngano),methali,vitendawili,nyimbo,tenzi(mashairi) n.k vyote hivyo vilitungwa na kusimuliwa kwa madhumuni  ya kufunza,kukosoa,kuadhibu,kuchokoza fikra na kuliwaza jamii baada ya kazi.
Sanaa hii ilirithishwa toka kizazi hadi kizazi kwa njia ya masimulizi na binadamu alivyozidi kujiendeleza kisayansi na kiteknolojia akahifadhi taaluma hii katika maandishi.Ndiyo sababu tunasema chanzo cha fasihi ni sawa na chanzo cha binadamu mwenyewe na jinsi binadamu alivyozidi na atakavyozidi ndiyo taaluma hii ilivyokuwa na kuendelea.
3.       Fasihi inatokana na sihiri,Istilahi Sihiri’ ina maana ya Uwezo au nguvu ya kimiujiza inayotumiwa na watu kusababisha matokeo fulani.Watalaam  hawa wanadai kuwa  chimbuko la fasihi ni haja ya mwanadamu kukabiliana na  kujaribu kuyathibiti mazingira yake. Haja hiyo haikutimilika ipasavyo katika hatua zake za mwanzo  za maendeleo ya mwanadamu kwani uwezo wa kisayansi na kiteknolojia wa mwanadamu wa wakati huo bado ulikuwa kiwango cha chini sana.Hivyo Imani au miujiza ilichukua nafasi ya sayansi na ugunduzi.Fasihi ilichimbuka kama chombo cha sihiri  hivyo katika kujaribu kuyashinda mazingira,Mfano Wawindaji walichora picha ya mnyama waliyetaka kumuwinda kabla ya kwenda kuwinda,kisha walichoma mkuki au mshale kwa kuamini kuwa kitendo hicho kitatokea kuwa kweli watakapo kwenda kuwinda. Nyimbo walizoimba wakati wa kufanya sihiri hiyo ndiyo fasihi ya mwanzo.
Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba inachangnya dhima na chimbuko kwani kutumika kwa nyimbo au ushairi katika sihiri hakuthibitishi kuwa sihiri ndiyo chimbuko lake.Sihiri ni amali moja tu kati ya amali nyingi za wanadamu wa mwanzo zilizotumia ushairi.
4.       Nadharia ya Mwigo,Wataalam wa nadharia wanadai kuwa Fasihi imetokana na mwigo(Uigaji),Katika nadharia hii inaeleza kuwa mwanadamu alianza kuwa mbunifu kwa kuiga maumbile yaliyomzunguka.Hivyo sanaa za mwanzo mara nyingi zilijaribu kusawiri vitu vilivyomo katika mazingira ,mfano wanyama,ndege,miti,watu.
Nadharia hii ni kale,ilianzisha na wataalamu wa kiyunani  na walioieneza zaidi ni Plato (Republic) na Aristotle (Poetics)  Plato anahusisha mwigo na dhana ya uungu.Anaeleza kuwa Maumbile na vilivyomo ni mwigo tu wa sanaa ya kiungu.Sanaa ya Mwanadamu (Hususani ushairi) ambayo huiga tu mambo hayo yaliyomo  katika maumbile haiwezi kuwa na ukweli  au uhalisi wa kuwa inaiga maumbile ambayo na yenyewe  yanaiga kazi ya Mungu.Hivyo alishauri aina fulani za ushairi zipigwe marufuku kwa sababu zinapotosha ukweli.
   Udhaifu wa nadharia hii  ni kwamba inasisitiza mno uigaji na kusahau suala la ubunifu katika sanaa na fasihi.Kama wasanii wangeig maisha na mazingira tu,sanaa yao ingepwaya sana na haingekuwa tofauti na picha ya fotografia au maelezo ya matendo ya mazingira na matendo ya kila siku ya mwanadamu.

FASIHI KAMA CHOMBO CHA UKOMBOZI
Ukombozi ni harakati za jamii yoyote zenye lengo la kuitoa jamii hiyo kwa nguvu (kwa silaha) au kwa mazungumzo kutoka katika makucha ya watumwa kisiasa,kiuchumi,kimawazo na kiutamaduni.Jamii inaweza kuwa ni ya kitumwa kisiasa ikiwa haitakuwa na fursa ya kushika hatamu ya uongozi wao na badala yake ikategemea uongozi kutoka kwa jamii nyingine jamii itaitwa ya kitumwa ,kiuchumi,ikiwa haitakuwa na haki ya kuendesha njia mbalimbali za uzalishaji mali.Pia jamii isiyoweza kufikiri na kuamua wala kutokuthamini mawazo yake yenyewe na badala yake ikawa katika mgawanyiko wa ibada na itikadi za kigeni ni jamii isiyo huru kimawazo vile vile jamii haitakuwa huru kiutamaduni ikiwa itakosa kuthamini uaminifu,uumbaji na ugunduzi wake yenyewe badala yake ikasujudu amali zilizo na chimbuko kutoka nje.Nyanja za ukombozi wa jinsi fasihi ya Kiswahili ilivyozitazama mpaka leo
(a)Kisiasa
Ukombozi wa kisiasa unapatikanaje?
Unapatikana tu baada ya kupigania uhuru wa bendera kuwa ndio wa kwanza kupatikana kwa nchi ambayo iko katika harakati za kujikomboa.Katika maandishi ya mengi fasihi ukweli huu unajitokeza kwa mfano katika utenzi wa uhuru wa kenya msanii anatuonyesha  juu ya vita vya kumng’oa mkoloni kutoka katika kiti cha uongozi kwanza baada ya mwafrika kupandisha bendera yake mambo mengine yafuate vilevile katika utenzi wa uhuru wa Tanganyika na utenzi wa jamhuri ya Tanzania “mwandishi anasisitiza  uhuru wa bendera ukielezwa kuwa kabla ya ukombozi wa aina nyingine kufuata.
Kwa hiyo ukombozi huu wa mwanzo (uhuru wa bendera) husababisha uhuru wa kisiasa wanchi kisha uhuru wa kisiasa huwa ni jukwaa la ukombozi wa uchumi na mambo mengine,vitabu vingine vinavyozungumzia ukombozi wa kisiasa ni mzalendo,F.E.MK Senkero) Ubeberu Utashindwa(J.K Kiimbila),Tone la Mwisho(E.Mbogo),Kinjikitile na Mashetani(E.Hussein),Nuru mpya(R.Rufeshobya)
(b)Kiuchumi
Uhuru wa bendera ni sehemu ya mwanzo tu wa ukombozi wa jamii nchi zinaweza kujidai ni huru kumbe uchumi wake bado ungali mikononi mwa nchi nyingine.Nchi nyingi zinazoendelea bado ziko katika harakati hii ya kutaka kujikomboa kiuchumi.Waandishi wengi wa fasihi ya Kiswahili  wamezungumzia sana suala la uchumi katika  mfano ‘’Mashairi ya Azimio la Arusha’’ mwandishi anaonyesha na kushambulia unyonyaji ambao ni adui wa uhuru wetu.
Vilevile waandishi wanasisitiza kufanya kazi kama njia ya kuimarisha uchumi.Pia wameeleza kuwa unyonyaji unaweza kukomeshwa kwa kutaifisha njia zote za uzalishaji mali na kuwa mikononi mwa umma. Pia Katika tamthiliya ya “Bwana Mkubwa” (J.P Mbonde) mwandishi ameonesha kuwa kwa sasa shabaha yetu sisi ni kupigana na ukoloni mambo leo ili kupata uhuru kamili.Ukoloni mambo leo ni kikwazo cha ukombozi wa kiuchumi. Kwa sababu ya ulegevu wa uhuru wa kisiasa nchi inaweza kuwa na mali  lakini ikizembea kufanya kweli ipasavyo yaweza kufanyiwa njama na ukoloni ndio maana upo umuhimu wa bidii katika kazi na uzalishaji wa mali kisha linafuata swala la ulinzi wa mali hiyo.
Kuzikomboa njia za uzalishaji mali hakutoshi kwani kila hila zao zisizoisha wakoloni wanaweza wakatupora mali hiyo tunapaswa kuwa macho.Katika utenzi wa “Zindiko la ujamaa” mwandishi anaeleza utaifishaji wa njia kuu za uchumi na uhalali wa utaifishaji huo. Mwandishi anaonyesha kuwa utaifishaji huo ulifanywa si kwa kuwaona wakoloni kuwa wanadhuluma bali kama njia moja wapo ambayo itaongeza kwenye ukombozi wa kiuchumi katika jamii. Lengo moja ni kufuta ubinafsi ambao unapelekea tofauti za kitabaka na badala yake manufaa ya umma kwa ujumla.
Ukombozi wa kiuchumi si utaifishaji wa njia za uzalishaji mali tu na wala si kukomesha ukabaila na ubepari bali ni kuongeza juhudi katika kazi mbali mbali ili kuongeza kiasi cha pato la kitaifa. Waandishi wengine wanazungumzia ukombozi wa kiuchumi ni kama vile, “Nuru mpya” (G. R. Ruteshubya) “Mashetani” (E. Hussein) “Sauti ya dhiki” (A. Abdallah) “Kasri ya mwinyi fuad” (Shafi Adam Shoji) Zetu bora mkulima na wasifu wa sili binti saad(S. Robert).
C) Kimawazo
Ukombozi wa kimawazo ni uhuru wa mtu katika upeo wa fikra pasipo kutegemea mtu mwingine. Hapa mtu aliye huru awe anajiamini mwenyewe na awe mtu kama watu wengine. Awe mwenye uwezo wa kuwaza, kuamua na kutenda, kuchanganua na kupanga kama watu wengine. Mtu aliye mtumwa wa kimawazo anaweza kufananishwa na mnyama wa kufugwa. Mnyama wa kufugwa daima ni mtumwa na bwana wake wakati wote huongojea amri kutoka kwa bwana wake.
Maandishi ya fasihi yanazungumziakwa upana swala hili la uhuru wa mawazo . Katika riwaya ya “Njozi za usiku” dhana hii ya utumwa wa kimawazo ipo ndani ya watu wengi ambao wanashikilia hasa baada ya maajilio ya elimu iliyokuja pamoja na ukoloni na ikatumika kwa upotofu. Katika riwaya hii msanii anaonyesha kuwa wale waliosoma walidharau kazi zote za mikono, walifikiri kuwa kazi za mikono zinafaa kwa wale ambao hawakusoma. Wao wanafikiri kuwa kazi ya mtu aliyesoma ni kushika kalamu na kuandika tu au kuwasimamia ambao hawakusoma.Tangu uhuru wa Tanzania kumekuwa na harakati za kufutilia mbal ukanganyifu wa namna hii katika mawazo ya watu. Mawazo ya namna hii ndio yamekuwa yakiwafanya watu wengi wa hali ya chini waamini kuwa uchumi walionao wamepewa na Mungu.
Vile vile kimawazo watu waliamini kwamba kila jambo lilitokana na watawala wa kizungu lilikuwa ni bora kabisa. Kwa mfano hata majina yliletwa toka Ulaya  nay a kwetu ya asili kuachwa. Haya yanajadiliwa wazi katika tamthiliya ya “Bwana mkubwa” (J. P. Mbonde)
Katika ukombozi wa kimawazo kuna swala la ukombozi wa mwanamke na swala la dini.Katika suala la ukombozi wa mwanamke watu wengi wanalitazama kirahisi jambo hili. Wengi wanadhani kuwa mwanamke hana haki ya kujibagua kutoka kwa wanaume na kujipigania haki yake. Watu hawa hawaelewi ni mapinduzi gani ambayo hawa wanapigania.Katika fasihi ya Kiswahili Shaban Robert amewatetea wanawake katika kazi zake mbali mbali ikiemo Diwani ya”Wasifu wa siti binti saad” na siku ya watenzi wote. Shaban Robert amemtazama mwanamke kama mtu anayestahili  utu kama watu wengine wowote wale.
Katika kitabu cha “Wasifu wa Siti binti Saad” msanii au mwandishi anaeleza wazi jinsi jamii ilivyomfanya mwanamke kama chombo cha kutunzwa utawani ili kiwe kizuri kipate kuwavutia wanaokitafuta na baada ya kutoka utawani kikawa mikononi mwa mwanaume kikamtegemea kwa hiyo mwanamke alikuwa ni mtu aliyechukuliwa kama hana wajibu wowote wa maana Zaidi ya kuwa mtegemeaji. Lakini Shabn Robert aliona kuwa ( uk 23) “Ukimdumisha mtu leo utamuona juu ya kilele cha utukufu kesho.
Mawazo ya mwandishi ni kwamba wanawake ni vyema watazamwe katika hali zao za maisha katika ubaya na uzuri kama wanaume. Kuhusu suala la dini linajitokeza katika riwaya ya “Kichwa maji” ambapo mwandishi anaona dini imeanzishwa na waoga ambao hutawaliwa na milango yao ya fahamu badalaya kutawaliwa na akili au bongo zao.
Jambo muhimu katika kumkomboa mtu kimawazo ni kwamba ikiwa dini itaendelea kuwepo isiwe na mtazamo duni na finyu na athari zake ambazo alikuja nazo mkoloni akidai kuwa tamaduni zetu ni za kishenzi. Sharti elimu ndiyo iwe ya kutafakari na kugeuza mfumo wa maisha ya jamii.
Katika dini pia kuna madhehebu mbali mbali ambayo kati yao kuna uhasama mkubwa, muislamu anadai kuwa yeye ni bora Zaidi kuliko mkristo na mkristo anajiona yeye ni bora kuliko muislamu. Madhehebu yote haya yamechimbuka huko mashariki ya kati…….katika kitabu cha “Bwana mkubwa” (uk 18-19”)……kwanini basi mlitutenganisha katika vikundi vidogo vya madhehebu tofauti kati ya wakristo na waislamu iwapo Mungu ni yule yule mmoja leo mnatueleza tuombe kuungana, utengano alianzisha nani? na kwa faida ya nani?........mbona babu zetu walimwabudu Mungu wao toka zamani kabla ya ujio wa wazungu.
Kwa ujumla dini imechangia kwa kiasi kikubwa sana katika kudumisha mtu kimawazo na kumfanya atumie fahamu tu kwa hiyo katika kumkomboa mtu kimawazo sharti suala la dini litupiwe jicho kali fasihi inazidi kuona jicho lake.
(d)Kiutamaduni.
Kwa ujumla utamaduni wanchi zilizotawaliwa na ukoloni umeathiriwa sana na ukoloni huo watu wa nchi hizo wanazipoteza kidogo kidogo thamani za utamaduni zao.Katika fasihi ya Kiswahili ukweli huu wa mambo yameoneshwa  katika kitabu cha “Njozi za Usiku” mwandishi wa riwaya hii ameelezea namna vijana wote hasa waliosoma hawataki kabisa kusikia kuhusu mila na desturi zao (uk 51).Hadi leo vijana wengi wakiwa kwao (vijijini) na ikatokea kwamba kuna ngoma za kienyeji zinachezwa wao husimama mbali au kando wakitazama kwa dharau mambo yanayotendeka mbele yao.Wanaamini kabisa kuwa ngoma hizo ni za kishenzi ngoma ambazo zinafaa kuchezwa na watu wasiosoma watu wasio staarabika.
Katika riwaya ya “Kichwa maji” mwandishi ameonesha jinsi isivyo  kawaida kwa msomi au watu wenye cheo serikalini kucheza ngoma za kienyeji lakini vijana hao hao mwanzoni wasomi wenye mwazo ya kisiasa wakisikia sehemu fulani kuna mziki au disko watajitahidi sana ili wasikose kufika huko.Kwa sasa kuna mtindo mwingine wa kupaka madawa ya kujichubua ngozi waonekane weupe na wengine huvaa nywele za bandia au maiti ili kuficha nywele zao za kipilipili.Huu wote ni utumwa wa kimawazo kwa upande fulani watu hawa wanaamini kuwa uzungu ndilo shina la maarifa, watu hawa hawajui kwamba kuna wazungu wengine ni maskini zaidi hata kuliko sisi wenyewe.
Hivyo ili tujikomboe katika nyanja hizi ni lazima tuondoe ubinafsi, uroho wa madaraka na ulevi wa madaraka hapa nchini.

MADA NDOGO; UHURU WA MWANDISHI/MTUNZI WA KAZI ZA KIFASIHI
Dhana ya uhuru wa mwandishi ni pana sana na inatazamwa kwa kuangalia vipengele kadhaa kama ifuatavyo:
    Mosi,uhuru wa mwandishi uko katika utashi,Bila utashi mwandishi atakuwa mwoga na mwepesi wa kukata tamaa.Atayumbishwa haraka kutoka kwenye msingi wa falsafa yake na Imani aliyo nayo juu ya mabadiliko yatokeayo katika jamii.Makombora ya wahakiki na wanasiasa huweza kumyumbisha, lakini kwa mwandishi mwenye utashi makombora hayo humkomaza.
Baadhi ya waandishi walioonyesha utashi wao katika Afrika ni ‘Ole Sanyika na Ngugi wa Thiongo waandishi hawa wameshambuliwa sana na wahakiki, lakini misimamo yao ni ile ile, pia wamewahi kufungwa na walipotoka kifungoni hawakubadili misimamo yao na wamekuwa hivyo kwa sababu ya utashi wa falsafa zao katika fasihi ya kiswahili, waandishi wenye utashi wapo na msingi wa kuwepo kwao ni kutoyumbishwa na matamshi ya jukwaani na wahakiki ambao hawajapevuka.
Pili,uhuru wa mwandishi umo katika kuwa na falsafa moja inayoeleweka, Falsafa ifanyayo  maandishi ya mwandishi moja yawe na kitu kijulikanacho kama lengo.Waandishi waliotajwa hapo juu yaani Ole Sanyika na Ngugi wa Thiongo ndio wanaongoza kuwa na falsafa zao zinazojulikana. Katika fasihi ya Kiswahili tunaona waandishi wachache wenye falsafa zao inayojulikana wengi tulio nao wanaandika kufuatana na jambo fulani au tukio la wakati huo bila kulinganisha leo ataandika juu ya mapenzi, kesho juu ya upelelezi na kesho kutwa mapinduzi mwishowe anakuwa na orodha ndefu ya vitabu visivyokuwa na lengo.Waandishi wachache tulio nao ambao wameelekea kuwa na falsafa inayoongoza maandishi yao ni kama Shaban Robert, G.Kezilahabi na Mohamedi Suleiman.Bila kuwa na falsafa maalumu ni rahisi  sana mwandishi kuyumbishwa.
Tatu,uhuru wa mwandishi umo katika kuitawala vema Sanaa yake,kama unaandika riwaya na hujui misingi ya Sanaa ya aina hiyo atajikuta katika kikwazo,utajikuta uhuru wa kisanaa unaweza kujaribu, lakini kazi utakayoitoa itakuwa hafifu.Kazi nzuri ya kisanaa ni ile inayounganisha vema ubunifu na uhalisia.Mwandishi akielemea sana katika ubunifu anazua matatizo mengine kazi ngumu aliyonayo mwandishi ni katika kupata barabara msitari huo.Mwandishi mwenye vitabu vingi anaweza kuwa na kitabu kimoja tu kilichoupatia vema mstari huo. Katika fasihi ya Kiswahili waandishi walioupatia msitari huo tunao ni kama vile Ebraim Hussein,Penina Mhando,Mohamed Suleiman, C.G Mng’ong’o na J.A.Safari.Msanii anayeweza kuitawala  vema Sanaa yake anaunganisha vizuri Sanaa na maudhui yake.
Mwisho, uhuru wa mwandishi umo katika lugha anayotumia,ili msanii atawale vema Sanaa yake nilazima ajue lugha anayotumia.Lugha ndicho kiungo maalumu kati ya Sanaa na kazi ya kifasihi mwandishi kama hajui vema lugha anayotumia atajikuta hana uhuru wa kukisema anachotaka kwa hiyo lugha ndiyo nguzo ya nne katika uhuru wa mwandishi, waandishi wa Kiswahili  waliokwisha kutajwa wanakitawala Kiswahili sanifu,Kiswahili sanifu ndiyo msingi wa fasihi ya Kiswahili.
Ni kweli kuna uhuru wa mwandishi?
Uhuru wa mwandishi ni nini?
Ni ile hali ya mwandishi wa fasihi kuwa huru na wazi katika kutoa mawazo au hisia zake kwa jamii.Ni uhuru wa kuandika na kulikosoa tabaka lolote katika jamii bila kupata matatizo yoyote.
Mwandisihi ni nani?
Ni mtu yoyote atumiaye muda wake mwingi  kuandika na kuzungumzia jamii yake kwa njia ya maandishi.
Je kuna uhuru wa mwandishi?
Kwa ujumla uhuru wa mwandishi ni uhuru ikiwa hakufaulu kudhuru tabaka tawala hii ni kwa sababu suala la uhuru wa mwandishi ni la kitabaka na lilianza pale jamii ilipogawanyika katika matabaka kwa maana hii uhuru wa mwandishi unaamuliwa na tabaka tawala
Kuanzia enzi za utumwa, maandishi ya liyovumbuliwa katika  fasihi andishi ya mwanzo ilikuwa ya wateule wachache tu na wenye vyeo vyao.Hao mabwana, wamwinyi na mabepari walihakikisha kila mbinu inatumika ikiwemo ya udhibiti wa maandishi ili kuendeleza na kulinda utawala wao.
Naye B.Goya (1974-78) anasema kuwa mwandishi hana uhuru kwa vyovyote vile kwa sababu yeye ni tokeo la jamii Fulani, kila jamii ina mipaka yake ambayo mtu hatakiwi kukiuka kwa vyovyote vile mwandishi huyu amebanwa na mipaka hiyo asivuke.Pindi avukapo mipaka hiyo atapambana na jamii hiyo (tabaka tawala) vitabu vya mwandishi huyo vitapigwa marufuku au vitabu vikitolewa havitanunuliwa au serikali itavikusanya na kuvifanyia mipango mwingine. Katika Afrika  kuna mifano mingi ya udhibiti wa waandishi mfano mzuri ni mwandishi maarufu wa Kenya Ngugi wa Thiongo ambaye kazi zake hasa ya “Ngaahika Ndeenda”(I will marry when I want)- Nitaolewa Nitakapotaka, ilimgombanisha na vyombo vya dola hadi akawekwa kizuizini, Ngugi ni mwandishi wa kwanza kufichua siri za mfumo wa kibepari kwa watu wanyonge aliliuzi tabaka tawala la jamii yake ambalo halikusita kutumia udhibiti na vyombo vyake vya Mabavu.
Baada ya uhuru vitabu vingi sana viliandikwa kwa kudhibitisha maandishi mbalimbali uliojitokeza waziwazi E.Kazilabi aliandika riwaya “Rosa mistika”(1971),kitabu hiki kilipigwa marufuku kisitumike mashuleni na wala kisiuzwe waziwazi madukani.Ilidaiwa na waliokipiga marufuku kuwa kilikiuka maadili ya jamii kwa kueleza mambo ya aibu kwa wazi.Sura ya kumi ndiyo hasa ilitolewa mfano wa uchafu wa kitabu hiki.Udhibiti huo ulifanywa na Wizara ya Elimu na ulizusha maswali mengi kwa wasomaji.Wasomaji walianza kujiuliza, Je si kweli uchafu uelezwao katika “Rosa mistika” umo ndani ya jamii ya Tanzania? Je upotofu na uongozi mbaya ulifuchuliwa na riwaya hiyo hii si upo kati yetu? Kwa baadhi ya wasomaji ilielekea kuwa suala la uchafu wa maelezo yatokeayo kitandani baina ya wakuu wa chuo na wanafunzi wao lilitumika kama kisingizio tu cha kudhibiti ukweli wa masuala mengine nyeti yaliyowagusa viongozi yaliyowakilishwa na watu kama vile Bwana Maendeleo Deogratius anayeshiriki katika kuwaharibu vijana.
Vitabu vingine ambavyo havieleweki vinasema nini, maudhui, falsafa na ujumbe wa mwandishi ni mashetani(E.Hussein) “Aliyeonja Pepo”(F.Topan) na “Ayubu” Paukwa theatre Association.Na hivi viko kwa kukwepa mkono mrefu wa tabaka tawala.
DHIMA YA UHURU WA MWANDISHI.
·         Mwandishi atakuwa huru kuikosoa jamii au tabaka lolote litakaloenda kinyume na utaratibu wa jamii bila matatizo.Mwandishi atakuwa huru kuonyesha dhuluma, ukatili na ujangili unaofanywa katika jamii na tabaka lolote bila matatizo yoyote.
·         Kukiwa na uhuru wa mwandishi, msanii atakuwa na falsafa inayoeleweka pamoja na utashi wake.Hii itamfanya mwandishi awe na msimamo unaoeleweka.Msimamo  wake utamsaidia kuifundisha na kuielimisha jamii bila uoga.Ataijiulisha jamii hali yake na ataonesha jamii njia za kufikia haja na kutatua matatizo ya jamii bila uoga
·         Mwandishi atakuwa huru kutoa mwongozo katika jamii kwa kuikomboa jamii kutoka katika fikra mbovu za kugandamizwa,kunyonywa na kuonewa na tabaka tawala ili jamii ipate haki na heshima bila woga wa kuliondoa tabaka ambalo ndilo lenye mamlaka yote katika jamii.
·         Uandishi wa kikasuku utapungua, waandishi au wasanii huacha tabia ya kuwa vipaza sauti vya tabaka fulani katika jamii, wasanii makasuku huandika mambo bila kufikiri na kurudiarudia  mawazo yaliyokwisha semwa na wanasiasa majukwaani bila fikra mpya kwa hali hii hupotosha jamii.Hivyo kunapokuwa na uhuru wa mwandishi wa kutosha hali hii haiwezi kutokea kwa sababu mwandishi ataandika mambo mbalimbali yanayojitokeza katika jamii na hataweza kujikomba au kujipendekeza kwa tabaka tawala lenye mamlaka yote katika jamii.
·         Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi fasihi inakuwa chombo cha kuikomboa jamii kiuchumi,kisiasa, kiutamaduni na kifikra (kimawazo). katika jamii ya kitabaka fasihi ni mali ya tabaka tawala na hutumia fasihi kutetea na kulinda maslahi yao.Hivyo inapokuwa mali ya jamii nzima inatumiwa na jamii hiyo katika kuwakomboa wanajamii wote.
·         Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi, mwandishi anakuwa huru kuichokoza na kuisukasuka (kuichochea) jamii bila matatizo yeyote. Mwandishi atachokoza jamii ya wakulima na wafanyakazi kufikiri ili waweze kulichunguza tabaka tawala kwa jicho pevu na kutoa hadharani uozo uliopo katika kunyonywa, kupuuzwa,kuonewa, kugandamizwa na kunyanyaswa na tabaka tawala
·         Mwandishi atakuwa huru kuelimisha na kuishauri jamii katika mambo muhimu yanayojitokeza katika jamii bila woga.Mwandishi ataishauri jamii kuhusiana na mambo kama vile afya, elimu na ichague mambo gani yanafaa kuhifadhiwa na yapi hayafai vile vile msanii anakuwa huru kuirekebisha jamii bila woga kwa kuangalia yapi ni mazuri na yapi ni mabovu yanayotendeka katika jamii  

MADA NDOGO;MASUALA YA KIITIKADI NA DHANA YA UDHAMINI KATIKA KAZI ZA FASIHI
Maana ya Itikadi
Itikadi ni Imani ya watu au jamii fulani juu ya kitu fulani. Itikadi kisiasa ni mfumo wa mawazo na Imani ambao umewekwa na tabaka tawala/ tawaliwa au tabaka lolote lenye nguvu katika jamii inayohusika ikiwa na lengo la kulinda, kutetea na kuendekeza matakwa na maslahi yake. Utaratibu huo unaambatana na umilikaji wa njia kuu za uchumi na umilikaji wa mapato ya ziada yatokanayo na jasho la wazalishaji mali hizo, nyenzo za kitaaluma kama vile elimu ni nyenzo zisaidia kuimarisha itikadi kama vile dini vinatumika kutetea utaratibu uliowekwa na tabaka tawala.
Kimsingi kuna mitazamo miwili ya kiitikadi:-
i)                    Itikadi inayotetea na kulinda maslahi ya watu wchache tu katika jamii (utumwa, ukabaila na ubepari)
ii)                   Itikadi inayotetea na kulinda maslahi na matakwa ya watu wengi katika jamii (ujima na ukomunisti).
Vile vile tunapojadili juu ya itikadi katika fasihi na usemi kwa ujumla pia tunaongelea juu ya utabaka uliopo katika jamii inayohusika . Kuna matabaka ya aina mbili:-
a)      Tabaka tawala
b)      Tabaka tawaliwa
v  Tabaka tawala linamiliki vyombo vya dola na kwa kutumia vyombo hivyo na kwa kutumia waandishi, tabaka tawala linaunda, linaendeleza na kutetea maslahi yake.Vile vile tabaka tawala lina nguvu za kiakili na za kielimu kwa manufaa yao. Mwandishi kwa ujumla hawezi kuepukana na mfumo huo wa kitabaka. Tabaka fulani huwadhamini waandishi kwa njia mbali mbali.
 UDHAMINI
Ni hali ya watu au shirika fulani kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia kitu fulani . Mdhamini au wadhamini ni kundi la watu wenye shabaha zinazofanana wenye kusimama kama ufadhili wa mradi fulani. Katika fasihi hawa ni wale wanaosimamia makundi maalumu kipropaganda na kiitikadi.
AINA ZA UDHAMINI
Kuna udhamini wa aina mbili:-
i)                    Udhamini wa ushawishi
ii)                   Udamini wa nguvu
Ø  UDHAMINI WA USHAWISHI
Ni aina ya udhamini ambao mdhamini huwashawishi na kuwanunua waandishi au wasanii. Matokeo yake ni kwamba msanii anafungwa na matakwa ya mdhamini.
Ø UDHAMINI WA NGUVU
Huu ni udhamini unaotumia vyombo vya dola kama vile jeshi, polisi, magereza kumdhamini mtunzi au mwandishi n.k.Hakuna hiari katika udhamini wa nguvu, kila kitu kinaendeshwa kama vile mashine tu. Kwa ujumla mwandishi akidhaminiwa kwa nguvu za serikali huwa kama kasuku aimbaye na kuutukuza mfumo wa maisha uliopo katika jamii hata kama roho na moyo wake viko mbali sana na mfumo huo. Lakini msanii anapodhaminiwa kutetea umma, lazima kutakuwa na madhara yake katika jamii yake inayohusika.
Mwandishi wa fasihi katika kila nchi atakuwa na udhamini unaolingana na mazingira yake kwa mfano katika nchi ya Tanzania, mwandishi anaweza kuandika kwa udhamini wa jamii yake inayohusika.Mdhamini anaweza kuwa mtu binafsi mwenye fedha, shirika, chombo cha serikali, chama fulani au kundi la mataifa kwa ushirikiano. Pia mdhamini ni mwakilishi wa wenye mamlaka juu yake, kwa mfano katika serikali yaTanzania chuo kikuu ni mwakilishi wa serikali na serikali ni mwakilishi wa tabaka tawala. Hivyo msanii anayedhaminiwa na chuo kikuu ambacho ni chombo cha serikali hatimaye anajikuta anafanya kazi ili kuendeleza maslahi ya tabaka tawala.
SABABU ZA UDHAMINI
Ø  Uhaba wa fedha kwa waandishi za kuendeshea shughuli zao za uandishi katika uandishi wa kazi za fasihi. Pesa zinahitajika kwa ajili ya kununulia karatasi, kalamu, uchapaji n.k.
Ø  Kulinda na kutetea maslahi yawadhamini wao. Hii inatokea zaidi kama mdhamini ni wa tabaka tawala. Kama tabaka linalo tawala ni la mabepari kazi za fasihi zitatetea tabaka hilo.
Ø  Kujulikana au kuipendekeza. Baadhi ya waandishi hudhaminiwa kwasababu ya kutakakujulikaa na kwa upande mwingine mdhamini anawadhamini waandishi kwa lengo hilo.
Ø  Kupata fedha za haraka. Hawa huandika vitabu vyenye kujaa wahusika wakuu, mafundi wa kufanya mahaba, kutumia madawa ya kulevya na kufanya mapenzi kwa kutumia mipira ya kiume na kike bila kujali staha utamaduni wa jamii yake. Mwandishi anachojali hapa ni pesa na sio matakwa ya jamii yake.
Ø  Kulazimishwa na tabaka tawala. Waandishi hawa wanakubali udhamini huo kwa kuogopa udhabiti wa kazi zao na tabaka tawala. Waandishi hawa wakikataa udhamini huo kazi zao zitadhibitiwa na kupigwa marufuku zisisomwe au kuchapishwa kabisa.
ATHARI ZA UDHAMINI
Ø  Mwandishi anayedhaminiwa anatakiwa kuandika yale tu ambayo mdhamini wake anayataka. Msanii hatakuwa na uhuru wa kuandika kitu chochote na kwa njia anayotaka.
Ø  Mapana ya uandishi wake kidata, kigiografia na kimaudhui huamuliwa na mdhamini na kutegemea mahitaji yake na kiwango cha fedha alichonacho mdhamini.
Ø  Ufafanuzi wa data na maudhui ya kazi ya fasihi lazima ulingane na mtazamo wa itikadi ya mdhamini.Hii ina maana kuwa mwandishi wa kazi ya fasihi hawezi kufanya ufafanuzi wa data na maudhui mwenyewe bila kumshirikisha mdhamini.
Ø  Matokeo ya uandishi wa kazi za fasihi mara nyingi ni mali ya mdhamini na hutumia kuendeleza maslahi yake mabayo sio lazima yalingane na malengo ya mwandishi.
Ø  Wasanii au waandishi wengi kutokana na kudhaminiwa huanza kuandika kazi zao kwa kupenda pesa hii huwafanya waandishi kuwa makasuku kwasababu ya kuandika yale tu yasemwayo na mdhamini wake bila kuyafanyia uchambuzi wa kina.
Ø  Udhamini hukuza utabaka katika jamii, hapa tunakuwa na tabaka la wenye nacho (mdhamini) na tabaka la wasionacho (msanii) mdhamini humnyonya msanii.
Ø  Kuzuka kwa fasihi pendwa (riwaya ya pendwa).Hapa waandishi huandika kazi zao kwa lengo la kupata pesa za haraka, huandika riwaya pendwa ambazo zina soko kubwa hapa nchini hasa kwa vijana na wakati huo huo riwaya hizo hazifunzi lolote jamii Zaidi ya kuburudisha.
Ø  Huchochea rushwa, hii ni kwa sababu waandishi wengi wanataka udhamini huo na matokeo yake wale wanapata udhamini huo lazima watoe chochote (rushwa) kwa mdhamini.
               UMUHIMU WA UDHAMINI
·         Husaidia waandishi chipukizi katika kuchapisha kazi zao.
·         Husaidia waandishi katika kufanya utafiti wa mambo mbalimbali yatakiwayo katika Sanaa hiyo ya fasihi.
·         Husaidia jamii kupata kazi mbali mbali za kifasihi.
·         Husaidia kuleta ushindani wa ubora wa kazi katika soko la kazi za fasihi.
·         Husaidia kuinua vipaji hasa vya waandishi chipukizi.



Powered by Blogger.