HISTORIA YA HADITHI FUPI (Wamitila, 2002:66)

HISTORIA YA HADITHI FUPI (Wamitila, 2002:66)Kihistoria, wahakiki Edgar Allan Poe na Brander Matthews ndio wanahusishwa nakuanzishwa kwa utanzu wa hadithi fupi katika fasihi andishi katika mataifa ya Magharibi.Edgar ndiye aliyelitumia neno la Kiingereza la ‘Short story’ kwa mara ya kwanza (Henry,1995). Baadaye utanzu wa hadithi fupi ulienea na kuingizwa katika fasihi andishiza lughanyingine za huko Ulaya.Katika fasihi andishi ya Kiswahili, utanzu wa hadithi fupi umechipuka baada ya majilio yawakoloni katika Afrika ya Mashariki. Hii ni kwa sababu ujuzi wa kusoma na kuandikaumekuja na wageni kutoka bara Asia na Uropa.Hata hivyo, kama anavyobainisha Wamitila(2008:185), utanzu wa hadithi fupi kama ulivyotamthilia ya Kiswahili una historia ndefu katika fasihi ya Kiswahili na ya Kiafrika kwaujumla. Hii inatokana na uhusiano mkubwa uliopo baina ya tanzu hizi na zile za fasihisimulizi. Utanzu wa tamthilia katika fasihi andishi una misingi yake katika utanzu wamaigizo katika fasihi simulizi.Kwa upande wake, hadithi fupi inafanana sana kiumbo nangano(hurafa, hekaya na ngano za mtanziko) katika utanzu wa hadithi/masimulizi katikafasihi simulizi ya Kiswahili. Uchunguzi wa mitindo ya hadithi fupi nyingi za Kiswahiliunaonyesha sifa nyingi za ngano katika fasihi simulizi. Kwa hivyo ukuaji wa utanzu wahadithi fupi katika fasihi ya Kiswahili kwa kiasi fulani umewekewa misingi na kuwepo kwautanzu wa masimulizi/hadithi katika fasihi simulizi(Wamitila,uk. 186).Mbali na hayo ni bayana kuwa historia ya ukuaji wa hadithi fupi katika fasihi nyingi zaulimwengu inafanana. Yaani ina mianzo inayoshabihiana na kuleta sifa za ubia.Tukirejeleahadithi fupi ya Kiswahili tunaona kuwa watunzi wengi wa hadithi fupi walianza kuandikahadithi zao na kuzichapisha magazetini. Wamitila(2008:185) anasema kuwa utanzu wahadithi fupi ulikua sambamba na maendeleo ya utungo wa gazeti katika karne ya ya kumi natisa.Mathalan baadhi ya hadithi za E. Kezilahabi kama vile: “Cha Mnyonge utatapika Hadharani”,“Mayai Waziri wa Maradhi” na “Magwanda Kubilya na Vyama Vingi” awali zilichapisheamagazetini. Hadithi nyingine zilishiriki katika mashindano ya uandishi na hadithizilizosomwa katika idhaa za BBC na hatimaye kuchapishwa katika mifululizo yaMapenzi niKikohozi,Kinywa Jumba la ManenonaPavumapo Palilie.Diwani hizi ndizo ziliweka msingi wa kuandikwa na kuchapishwa kwa hadithi fupi. Mnamomiaka ya sabini, diwani zingine za hadithi fupi kama vile:Pepeta(Yahya).Zaka la Damu naHadithi Nyingine(BAMITA)Parapanda na Hadithi NyinginenaUwike UsiwikeKutakucha(Ruhumbuka)zilichapishwa.Diwani zilizochapishwa katika miaka ya themanini ni:Si Wazimu si Shetani(S.A. Mohamed)Dhuluma na Hadithi Nyingine(Y.Barshad),Twenzetu Ulaya na Hadithi Nyingine(F.
Powered by Blogger.