4. VIPENGELE VYA FANI KATIKA HADITHI FUPI ZA KISWAHILI

Cover Image

4. VIPENGELE VYA FANI KATIKA HADITHI FUPI ZA KISWAHILI


Sura ya Nne
KATIKA sura hh nyadala wetu utazingatia uchambuzi wa vipengele vya fani ns kuonajinsi gani vinaleta athari mbalimbali katika hadithi fupi za Kiswahili. Tutaangalia sifa muhimu zinazohitajika katika ujenzi wa fani ya utanzu huu wa hadithi fupi. Ni muhimu kusisitiza hapa kuwa fani itakayojadiliwa hapa ina uhusiano mkubwa na maudhui, na kwamba hapa vimetenganishwa kwa ajili ya uchambuzi tu.
Vipengele vitakavyojadiliwa na kuchambuliwa ama kuchanganuliwa hapa ni wahusika, lugha na matumizi yake, muundo, mtindo na mandhari. Katika mjadala wetu tutaangalia jinsi vipengele hivyo vinavyotegemeana na kuhusiana katika kuandaa ama kuunda na kuikamilisha fani ya hadithi fupi ili iweze kutoa maudhui yanayoihusu.
Wahusika: Uumbi ama Ujenzi Wake
Wakati wa kuelezea maana ya hadithi fupi, tulisema kuwa wahusika, (pamoja na mengineyo, k.v. tukio) ni muhimu katika kuiunda kazi ya kifasihi ya hadithi. Lakini hatukuwa tumeelezea maana y'a wahusika hao katika kazi hiyo ya hadithi fupi. Pia hatukuwa tumeelezea mbinu za uumbi au ujenzi wake na jinsi wahusika wanavyoathiri mkondo wa hadithi kutokana na ujenzi wake. Katika sehemu hii tutavichambua vipengele hivyo kwa mapana.
Kwanza kabisa tuanze kwa kufafanua kwa nini wahusika wamewekwa kama sehemu ya fani na sio sehemu ya maudhui. Ukweli ni kwamba kuna hoja ambazo zimetolewa na baadhi ya wataalamu kuwa wahusika ni sehemu ya maudhui. Hawa wana sababu zao. Nia ya kuwaweka wahusika upande wa fani si kwa sababu hawachangii katika maudhui. Uamuzi wa kuwaweka upande wa fani unatokana na sababu kadhaa. Kwanza, tumefikiria, ujenzi wa wahusika m muhimu katika kutoa maudhui kwa hadhira. Mhusika hujengwa kwa namna mbalimbali-ikiwemo jinsi aonekanavyo, atendavyo na kusema. Kwa kuwa fani ni jinsi kazi ya faaihi ilivyojengwa, tunafikiri wahusika watafaa kuwa sehemu hii ya fani.
Kwa upande mwingine, wahusika ni muhimu sana katika kutoa na kufikisha dhamira kwa hadhira. Kutokana na nafasi muhimu ya wahusika katika kazi ya kifasihi, na kutokana na ukweli kwamba umuhimu wake uko' katika upande wa fani na maudhui, labda mahali panapostahili pangekuwa katikati ya pande hizo mbili-ambazo kimsingi hazipo. Tunafikiri upande wa fani ndio unaostahili kuwekwa wahusika.
Baada ya maelezo hayo mafupi, sasa tuangalie maana ya wahusika katika kazi ya- kifasihi. Wahusika katika kazi yoyote ya sanaa itumiayo lugha ni watu, wanyama ama vitu. Wahusika hao husawiriwa kisanaa na mwandishi ili waweze kuwakilisha dhana mbalimbali za maisha katika jamii. Kwa hiyo, mwandishi huwasawiri wahusika kwa wasomaji wake kwa kutumia sifa pambanuzi walizo nazo, naimna gani walivyo, mambo gani hawayapendi na yapi wanayapenda, maisha yao n.k. Wahusika hao hutumia misemo, nahau, tamathali za usemi, na methali, katika mazungumzo yao tli kujenga tabia na hali ya kisanaa.
Wahusika wa kazi za sanaa huwa na tabia zinazotofautiana kati yao kwa sababu mbalimbali. Kwanza kabisa, inategemea mwandishi ana lengo gani analotaka kulionyesha katika kazi yake ya sanaa. Pili, aina ya kazi ya sanaa inaweza kuathiri aina ya wahusika: jinsi walivyosawiriwa, kuaminika kwao, wanavyohusiana wao kwa wao, uwakilishi wao na majina yao. Wahusika katika hadithi ni mhimili mkubwa katika fasihi andishi na hata simulizi.
Utofauti mwingine wa wahusika katika hadithi unatokana na mbinu za uumbi wao, ambao kwa upande mwingine unategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wa usanii alionao mwandishi pamoja na dhamira anayoielezea kama tulivyosema.
Msanii anaweza kuamua kuwa anataka wahusika wanaowakilisha tabia na matendo fulani tu katika jamii na kwa hiyo atawaumba wahusika hao ili kukamilisha nia na lengo lake. Katika kuzipata tabia na hali za wahusika, msanii analazimika kutumia mbinu za kuwapa majina wahusika wake, kama wakati mwingine anavyofanya Shaaban Robert katika baadhi ya vitabu vyake kama vile Kusadikika1 na Adili na Nduguze2 Katika kazi hizo za Shaaban Robert, majina yanaonyesha moja kwa moja tabia ya mhusika mwenye jina linalolingana na tabia ambayo mwandishi anataka kuielezakwajamii. Wakati mwingine mwandishi anaweza kuwaelezea wahusika jinsi walivyo.
Penina Muhando na Ndyanao Balisidya3 wanasema kifupi tu kuwa wahusika wanaweza kuumbwa kinafsia, kiakili na kimwili. Kutokana na ujenzi wa aina hii, mhusika huonyesha wasifu wake wa ndani na nje, au anaweza kuonyesha mabadiliko yake kila anapokutana na mazingira tofauti. Hii inamaanish a kuwa mhusika ataonyesha mabadiliko na ataonekana katika uhalisia wake kwa kuzingatia nguvu zinazomzunguka kama vile za utamaduni, siasa, uchumi na kadhalika.
Ikibidi wakati mwingine, mwandishi anaweza kumjenga mhusika mmoja kwa njia ambayo ni tofauti na mhusika ama wahusika wengine katika kazi yake ili aweze kuijenga dhamira iliyokusudiwa. Kwa kuzingatia sababu hiyo, mwandishi analazimika kuwatumia vyema wahusika wake.
Hii vilevile madhihirisha kuwa mwandishi huyapisha mawazo aliyonayo juu ya ulimwengu kwa wahusika wake. Mwandishi anayo nafasi ya kuwajenga wahusika wake kadiri anavyopenda, lakini ana mipaka katika utanzu huu wa hadithi fupi kama ilivyodokezwa hapo awali.
Kila msanii kimsmgi ana mbinu za kuumba wahusika wake. Anaweza kutumia mbinu ya aina moja, au anaweza kutumia mbinu mbalimbali katika kazi moja.
Mbinu za kuwaumba wahusika zinategemea pia uwasilisho wake kwa wasomaji. Katika kuwawasilisha wahusika kwa wasomaji, msanii anaweza kutumia njia mbalimbali. Kwanza, anaweza kuwawasilisha kwa kuwaumba kidhahiri (exposition). Katika mbinu hii sifa na matendo ya mhusika yanaelezwa waziwazi. Njia hii ya kuwaumba wahusika husaidia kumfanya msomaji asipate taabu katika kutambua kiini cha kisa, wazo au dhamira. Msanii hapa anamjenga na kumtumia mhusika huyo kutoka mwanzo hadi mwishoni mwa hadithi yake. Uwasilishaji dhahiri kwa upande mwingine huambatana na mbinu nyingine za usimuliaji wa hadithi. Kwa kawaida uwasilishaji dhahiri hutokea wakati hadithi inaposimuliwa na mhusika au msimulizi wa nafsi ya kwanza. Mfano wa hadithi zenye aina hii ya usimulizi zinaweza kupatikana katika kitabu cha Nitakuja kwa Siri.4 Katika usimulizi wake, mhusika mwenyewe huelezea kila kitu anachokitenda.
Udhahiri pia unajitokeza wakati hadithi inaposimuliwa na msimulizi Mmaizi. Msimulizi Mmaizi ni wa nafsi ya tatu ambaye anazijua siri zote za wahusika wote. Huyo ni msimulizi anayeweza kuwako kila mahali kwa wakati mmoja na anayejua tangu mwanzo mambo yote katika dunia yake ya h dithi. Uumbaji huu unaweza kutumia utangulizi ambao mwandishi anaweza kuuweka mwanzoni mwa hadithi yake
Msanii anaweza pia kumwuumba mhusika kimatendo na kumwasilisha kwa hadhira yake. Katika aina hii ya uwasilishaji msanii hutumia ufafanuzi mchache wa maoni yake na sehemu kubwa humwachia msomaji anayetakiwa afasiri maana na sifa za mhusika aliyeumbwa kutokana na matendo yake. Msanii huwaumba wahusika kwa kutoa matendo nusunusu, hafcoi maelezo juu ya matendo yote kwa mara moja.
Msanii anaweza pia kumwasilisha mhusika kwa kutumia mbinu za kihisi. Mawazo au hisi hizo hutokana na nafsi ya mhusika huyo5 Wakati mwingine msanii hutumia mbinu za mazungumzo baina ya wahusika wake, yaani wahusika huwekwa wazungumze wao kwa wao. Hapo kadiri wanavyoendelea, wazo la mhusika pamoja na tabia yake hujulikana taratibu katika kazi hiyo. Kwa kuyaunganisha mawazo, matukio na matendo ya mhusika huyo tabia na pengine maumbile ya mhusika katika hadithi hudhihirika.
Aina ya Wahusika
Katika hadithi fupi kuna wahusika wakuu na wahusika wasaidizi ama wadogo. Hebu tuwaangalie wahusika hao kwa undani.
Wahusika Wakuu
Wahusika wakuu kwa kawaida ni mmoja ama wawili katika hadithi fupi. Wahusika hao hujitokeza kutoka mwanzoni hadi mwishoni mwa hadithi. Mara kwa mara wahusika wa aina hii hubeba kiini cha dhamira kuu na maana ya hadithi yote. Vituko na matendo yote hujengwa kuwahusu ama kutokana nao.
Kwa kawaida, wahusika hao huonyesha mabadiliko mengi ikiwa ni pamoja na kupoteza nafasi kubwa kama walikuwa nayo: mhusika hufikia kilele, anaanguka. Au inawezekana mhusika akaibuka ghafla mwishoni mwa hadithi na kuonekana kuwa ni mtu maarufu baada ya kuwa duni katika hadithi akionyesha tabia mbalimbali.
Wahusika wa hadithi fupi hawasawiriwi kwa mapana kutokana na sababu ya mawanda. Mawanda ya hadithi fupi si mapana kama yale ya tamthiliya ama riwaya.
Wahusika wakuu wanaweza kuwakilisha vikundi mbalimbali katika jamii, au wanaweza kuwakilisha tabia za mtu binafsi, n.k. Ikitokea labda mhusika mkuu amekufa wakati hadithi haijafikia mwisho, itambidi mwandishi kumleta mhusika mkuu mwingine atakayebeba uzito wa mhusika aliyekufa. Kama hafanyi hivyo, hadithi italazimika kuishia pale ilipofikia.
Wahusika Wasaidizi
Katika hadithi fupi, wahusika wadogo sio muhimu sana kama wahusika wakuu, na hujitokeza hapa na pale katika hadithi inayohusika. Wakati mwingine wahusika wa namna hii hujengwa sambamba na mhusika mkuu, huku wakihusishwa na migOngano mbalimbali. Mbinu ya aina hii ya kuwasawiri wahusika inajitokeza sana katika hadithi fupi za kisasa.
Ukiwalinganisha wahusika wadogo (wasaidizi) na wahusika wakuu hawa sio muhimu sana, lakini kuwako kwao kunasaidia kufafanua dhamira za hadithi na kuipa mwelekeo muhimu wa kisanaa na kimaudhui. Wahusika hao hujitokeza mara moja moja. Kwa ujumla wahusika wote katika hadithi wanahusiana. Wahusika wasaidizi wanasaidia kukuza, kudumaza au kufanya maamuzi muhimu ya hadithini.
Katika makundi mawili ya wahusika tuliyoyaona hapa juu, tunaweza kuwa na aina tatu nyingine za wahusika muhimu. Wahusika hawa ni bapa, duara (mviringo) na wahusika wafoili(shinda).
Wahusika Bapa
Wahusika bapa huwakilisha aina moja tu ya tabia kutoka mwanzo hadi mwisho wa hadithi. Wahusika hao wanazingatia kuishi katika wazo moja kuu waliloanza nalo kutoka mwanzo hadi mwisho. Wahusika bapa hawawezi kubadilishwa na mazingira au na matukio ya wakati wanayokutana nayo. Wala uhusiano wao na wahusika wengine wa hadithini haubadiliki kutoka mwanzo hadi mwisho. Kwao, inategemea wameanza na uhusiano wa aina gani.
Kimsingi, wahusika bapa wanatumika kama chombo maalumu kilichoan-daliwa rasmi na msanii ili kutimiza lengo fulani bila ya kujali hali za kawaida za maisha ya binadamu. S.A.K.Mlacha6 anawagawa wahusika hawa katika mafungu mawili, wahusika bapa-sugu na wahusika bapa-vielelezo.
Wahusika bapa-sugu ni wale ambao wanaonyesha msimamo wao kutokana na maelezo ya msanii. Wanakuwa sugu katika hali kwamba hawabadiliki, kila wanapoonekana, hali zao huwa ni zilezile, hawahukumiwi bali wao huhukumu tu, hawashauriwi bali wao hushauri tu, hawaongozwi bali wao huongoza tu. Wanakuwa kama madikteta!
Wahusika bapa-vielelezo kwa upande mwingine ni wale ambao pamoja na kutobadilika kwao, wamepewa majina ambayo humfanya msomaji aielewe tabia na matendo yao. Mfano wa wahusika hao ni ule wa majina kama Boramimi, Majivuno, Karama n.k. Shaaban Robert anatumia sana mtindo huu.
Katika aina hii ya wahusika, msanii anatilia mkazo katika aina moja ya tabia inayotawala, na ambayo anataka iwafikie wasomaji kiasi ambacho sehemu nyingine zote za sifa za mhusika huyo hazionyeshwi. Wahusika bapa hawawakilishi hali halisi ya tabia za watu wanaoishi. Kwa kawaida huonyesha kipengele kimoja tu cha tabia hata kama wanakutana na mazingira mbalim-bali.
Wahusika Duara
Wahusika wa aina hii vilevile huitwa wahusika mviringo. Hao wanaonyesha tabia mbalimbali kila wakiwepo katika hadithi Wahusika hao ni hai zaidi na wanavutia kisanaa. Kwa kawaida mhusika mmoja anajengwa akionyesha tabia mbalimbali kila anapokutana na mazingira fulani, japokuwa tabia hizo nazo haziwi zote. Ni wahusika wenye kubadilika kitabia, kimawazo, kisaikolojia, n.k. Wahusika wa aina hii hukua, huugua, hufa hucheka, hununa n.k., kila paaapopaaa. Kwa hakika wahusika hao wanawakilisha maisha ya watu katika uhalisi wake. Wahusika duara' wanavutia kisanaa ukiwalinganisha na wahusika bapa tuliok wisha kuwaona hapa juu. Kila tukio watendalo wahusika duara hufanya hadithi ijisogeze mbele kisanaa na kidhamira, na huifanya badithi ikubalike katikajamii na kuaminikajuu ya ukweli wa kutendeka kwake. Vwezekano wa kuwaonyesha wahusika duara kwa mapana katika riwaya ni mkubwa sana kuliko katika hadithi fupi.
Wahusika Wafoili
Wahusika wa aina hii wapo katikati ya wahusika duara na wahusika bapa. Hawakujaa kama wahusika duara, lakini ni hai zaidi kuliko wahusika bapa.
Wahusika wafoili wakati mwingine hujulikana kama wahusika shinda, Ili waweze kujengeka vizuri, wahusika hao huwategemea wahusika duara na wahusika bapa. Wanaendeshwa na mawazo ya wengine.
Kwa kawaida wahusika hao wana tabia na matendo ama msukumo wa nafsi ulio tofauti na wahusika wakuu ama wahusika wengine muhimu katika kazi ya sanaa. Mwandishi huwajenga na kuwatumia wahusika hao ili kupambanua zaidi sifa pekee walizo nazo wahusika wakau ama wahusika muhimu katika kazi ya sanaa inayohusika. Kwa mfano, weupe wa nguo uaavyojitokeza ukiwa katikati ya nguo nyeuni, au nguo nyeusi hiyo inavyojitokeza ikiwa katikati ya nguo nyeupe. Mguo nyeusi itakuwa nyeusi zaidi ikiwa katikati ya nguo nyeupe, na nguo nyeupe itakuwa nyeupe zaidi ikiwa katikati ya nguo nyeusi.
Ujengaji huu wa wahusika unafanywa na msanii ili kuipa nguvu zaidi kazi ya kisanaa inayohusika. Wahusika kama vile wababe, wapinzani, n.k. wanaweza kuwako katika kundi hili pia.
Wahusika wafoili (au hata wahusika wengine) sio lazima wawe katika kila hadithi fupi (ama hadithi kwa ujumla). Hadithi inaweza kuwa na wahusika wale ambao msanii ameamua wawe katika kazi yake.
Aina za wahusika zilizojadiliwa hapa juu zinaathiriwa katika ujenzi wake na matakwa ama uamuzi wa msanii mwenyewe katika kuwajenga wahusika hao. Msanii waweza kuamua kuonyesha kuwa wahusika wake wanawakilisha utaifa fulani: Mwafrika, Mwingereza, Mmarekani, Mrusi, Mchina na wengineo. Au, mhusika anaweza kuwakilisha hali yake katika jamii: Bachela, na wengineo. Mwisho, anaweza kuwakilisha tabia mbalimbali: jasiri, kichaa, mwisi na nyinginezo.
Hata hivyo, wahusika hao wote wana jambo moja mahimu: kwamba si watu halizi wanaoishi, bali ni mkusanyiko wa tabia za watu halisi wanaoishi, walioishi au watakaoishi siku sijazo na kujazilizwa kwa wahusika hao ili waweze kujenga dhaaa fulani anayoitaka msanii.
Kutokana na umuhimu wa wahusika katika hadithi fupi (na hata katika kazi nyingine za kisanaa za fasihi) msaii yapasa afanye uchunguzi mkubwa kabla ya kufanya uchaguzi wa wahusika anaotaka kuwatumia katika kazi yake ya sanaa. Jambo litakalomwongoza, pamoja na mengine, ni dhamira aliyoichagua, mbinu za uwasilishaji anazotaka kutumia, usisimko wa aina ya kazi anayoisanii n.k. Mbinu hizo zitamfanya mhuaika kuwa mzuri au duni kisanaa. Wahusika katika ujumla wao, huarifu, hufundisha, hufurahisha, au vyote hufanywa kwa pamoja.
Kuaminika na Kutoaminika kwa Wahusika
Katika kazi ya sanaa, mhusika anayeaminika m yule ambaye masimulizi yake katika hadithi yanaaminika kutoka mwanzo hadi mwisho. Hata hivyo, kuna baadhi ya usimulizi katika hadithi unafanya masimulizi yake yasiwe ya kuaminika. Mara nyingi wahusika wa kuammika ni wa aina mbili: Msimulizi Mmaizi wa nafsi ya tatu ambaye katika usimulizi wake anaelekea kujua kila kitu. Pia, msimulizi wa nafsi ya kwanza naye ana nafasi ya kuaminika.
Mwandishi anawajenga wahusika wa kuaminika nje au ndani ya hadithi yake kwa madhumuni maalumu wakati mwingine. Kuaminika kwa wahusika kutakuwa ni kule kukubalika kwao kimatendo katika mkondo wote wa hadithi yenyewe au maisha ya kawaida ya binadamu.
Wakati mwingine msanii huwajenga wahusika wake visivyoaminika kwa makusudi ya kuonyesha dhamira na lengo fulani, au kwa kutodhamiria na kutokuelewa jinsi ya kuwajenga wahusika wake.
Aidha, maelezo mengi yaliyotolewa kuhusu wahusika yanahusu pia wahusika wa riwaya. Wahusika wa hadithi fupi wanatakiwa wawe wachache sana na wajengwe kifupi na kirahisi, tofauti na riwaya.
Matumizi ya Lugha
Majadiliano na maelezo juu ya maana ya lugha yamekwisha fanywa na wataalamu mbalimbali. Lugha, kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu "ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa taifa au kabila fulani kwa ajili ya kuwasiliana."7 Tutaitumia maana hii katika auala lote la mjadala wetu kuhusu lugha katika kazi ya sanaa. Hata hivyo, japokuwa Lugha inatumika kama chombo cha mawasiliano, mawasiliano hayo yanatofautiana kulingana na mazingira. Kuna mawasiliano rasmi ambayo hufanywa sehemu fulani fulani, na kuna mawasiliano ya kisanaa ambayo hufanywa katika kazi za sanaa. Katika sura hii tutajadili zaidi juu ya mawasiliano ya kisanaa. Tutaangalia matumizi ya lugha katika hadithi fupi, na kwa kiasi fulani katika kazi nyingine kila tutakapoona kuwa ni muhimu kupambanua matumizi ya Lugha katika hadithi fupi. Vinginevyo, kazi za lugha hazihesabiki, na wala hatuwezi kuzieleza zote hapa.
Lugha katika hadithi fupi ya Kiswahili ni mtindo anaoutumia msanii kujieleza kimaandishi. Kwa hiyo, tutakapojadili matumizi ya lugha katika hadithi fupi za Kiswahili, tutazingatia mbinu mbalimbali zitumikazo katika kusanii maneno ambayo yanaleta athari matika maana iliyokusudiwa na watumiaji wake.
Lugha kama kiini cha mawasiliano huifanya hadithi iwe hai na iweze kuelezea dhana mbalimbali katikajamii. Hadithi fupi nzuri inakuwa na lugha yenye mpangilio maalumu, lugha ya ujazo. Uzuri wa lugha hapo unazingatia ukamilifu wake katika sarufi, mofolojia (maumbo), fonolojia (umbosauti) na umbo maana katika uchangamano wake.
Msanii mzuri hutumia lugha kwa tahadhari kubwa. Katika usanii wake, msanii atalazimika kutumia lugha fasaha ambayo ina tamathali mbalimbali za usemi, methali, nahau, n.k. Tutazijadili semi na tamathali hizo kwa urefu hapa chini.
Methali na Misemo
Methali ni semi zinazotokana na ujuzi, sheria na tabia za jamii ambazo kwa kawaida hushauri na kufundisha mambo mbalimbali. Kwa muda mrefu methali zimekuwa zikihifadhiwa na fasihi simulizi kwa manufaa yajamii nzima. Ili kufanikisha mawasiliano na uhusiano katika jamii, methali hufuatilia maisha ya jamii ya kila siku na kujihusisha na upinzani ama usuluhishi mbalimbali. Kwa vile methali zinajitokeza katika vipengele vingi mno vya maisha yajamii tutazijadili hapa kwa kirefu kidogo ili kutoa tahadhari kwa watumiaji wake katika ujenzi na uandishi wa hadithi fupi za Kiswahili.
Mwandishi anapotumia methali katika hadithi ni vyema ajue kuwa licha ya uzuri wa kisanaa utokanao na matumizi mazuri ya methali, methali zina kazi nyingine zaidi hasa kwa upande wa maudhui.
Kutokana na kuhifadhiwa kwake kwa njia ya simulizi kwa kipindi kirefu, methali, zimekuwa na dhima ya kuueleza utamaduni kwa kupitia mifumo mbalimbali ya tamaduni na historia kwa jumla. Ni muhimu kwa mwandishi kufahamu matumizi ya kila methali anayoitumia. Kwa mfano, methali ya "Maskini na mwanaye, tajiri na mali yake," inayoonyesha kiburi cha walionacho cha kutojali wale ambao hawanacho kitu. Kiburi hicho kimeandamana na kebehi. Methali, hiyohiyo inawakatisha tamaa wale wasiona-cho! Methali ya "Kidole kimoja hakivunji chawa," au "Jiwe moja haliinjiki chungu, "inaonyesha umuhimu wa ushirikiano katika utendaji wa kazi katika jamii. Yawezekana kabisa kuwa methali hiyo imechimbuka wakati wa ujima, wakati ambapo kazi zilifanywa kwa pamoja na kwa manufaa ya watu wote. Uchambuzi ukifanywa kwa uangalifu, utaweza kueleza migongano au migogoro inayokuwepo miongoni mwa jamii, na kwa hiyo utumiaji wa methali hizo unaweza kulengwa kwenye dhima ya kuichambua na kuitatua migogoro na migongano hiyo.
Msanii anapozitumia methali katikajamii, awe na uhakika juu ya maana ya methali hizo. Baadhi ya methali zikitumiwa bila uangalifu zitaonyesha nadharia ya utengano ambayo inaweza kupotosha maana na kuleta athari isiyokusudiwa. Baadhi ya methali hueleza matatizo katika jamii tu, hazitaji chimbuko la matatizo hayo. Kwa mfano, methali, "Mkaidi huliwa na nzi... Mkaidi mngoje siku ya ngoma... Mkaidi hafaidi mpaka siku ya Iddi," ni ile inayosema tokeo la "ukaidi," lakini hatuambiwi kwa nini huyu "mkaidi" aliamua kuwa mkaidi. Pengine mkaidi alikataa kutii kwa sababu alitaka kulinda maslahi na maisha yake. Je, ni nani asiye na haki ya kulinda uhai wake? Wasanii wanashauriwa kwa hiyo wawe waangalifu wakati wa kuzitumia methali hizo ili ziweze kuleta maana inayokusudiwa.
Kwa upande mwingine, methali zimekuwa na matazamo muflisi wa udhanifu - mtazamo kama ule usio wa kisayansi. Katika dini ya Kikristo kwa mfano, kuna amri isemayo kuwa "usiibe." Lakini haielezwi kwa nini huyu mtu anaamua "kuiba". Hivyo ndivyo ilivyo kwa baadhi ya methali, kwamba haziangalii kiini cha tatizo kilichosababisha mtu kuleta "tatizo," bali zenyewe zinaonya au kukemea tu. Athari ya jambo kama hili ni kuwa hata ikisemwa namna gani, "wizi" au "tatizo" litaendelea kuwepo, mpaka pale kiini cha shida zilizosababisha wizi au tatizo kitakapotatuliwa. Tunategemea methali kama hizo zingechambua kiini cha matatizo na pengine kuonyesha uwezekano wa kutatuliwa kwa matatizo yanayosibu. Uchambuzi na uwasilishi wa namna hii m wa manufaa kuliko kutoa vitisho visivyosaidia.
Mwelekeo na mtazamo wa mjadala wetu hapa unatupa dhana moja muhimu. Dhana hiyo ni ile inayoifanya methali ionekane kama ni sanaa tegemezi ambayo matumizi na ukweli wake hutegemea muktadha (context). Kwa msingi huo, ni vigumu kupata methali ambayo ni "kweli" tu, au ni "uongo" tu wakati wote.
Jambo la mwisho kulitaja hapa ni kuhusu dhima ya methali kama kiungo au kichocheo muhimu cha kisanaa katika hadithi fupi. Kwa hakika methali na misemo hupamba hadithi kama matumizi yake yakiwa mazuri. Tuone mfano ufuatao:
GONZA KWAHERI
Gonza, tazama sasa giza limekufika! Umelala, umekufa, unadai machozi yetu ambayo hatuna hiyari ya kuyatoa. Uliponenewa ukishikwa shikamana hukusikia, na wala hukujali! Kwako, mwanzo na mwisho uliviweka pamoja. Watu husema, ukiona kongoni ana pembe uzeeni ujue amejitunza. Gonza, umeufikia mwisho kwa hiyari isiyo hiyari, huna mwanzo wala mwisho tena, bali litakutanda giza la milele. Ulitakiwa ujue kuwa anayekuzidi nguvu hukupiga na fimbo yako mwenyewe (...). Gonza! Mkaidi huliwa na nzi! Mbuku, kwa sababu ya ujinga wake hachagui vya kumeza (...) Funo kukuza pembe zake si ufahari bali ni kuepuka mitego ya wawindaji!8

Kifungu hiki kimetumia methali kadhaa zilizoko katika msisitizo ambazo zinaibusha'bisia kali kwa wasomaji na kuwafanya waathirike kwa viwango mbalimbali wasomapo kifungu hiki. Fani hapa imeongezewa uzito wa kisanaa ambao huzalisha taharuki na hisia kadiri ya matakwa ya msanii mwenyewe.
Matumizi ya methali wakati mwmgine huambatana na misemo kama vile misimu na nahau. Misimu na misemo kimsingi haihesabiwi kuwa m fasaha wala ya kufaa. Nahau kwa mfano hutumia maneno ya kawaida, lakini, yamesetiri maana iliyo tofauti na ni nzito katika maana. Angalia mifano ifuatayo kwa ufafanuzi zaidi:
a - Chichi ana mkono wa birika
b - Asha ana ulimi wa nge
c - Diana amevaa miwani
d - Leonila ana mate ya fisi
e - Zeituni ametutoka angali mbichi
Hivyo ndivyo ilivyo misemo ya kinahau. Katika misemo ya kawaida nahau hizi zingeweza kutamkwa kama ifuatavyo:
a - Chichi ni mchoyo/mnyimi
b - Asha ana maaeno makali sana
c - Diana amelewa (pombe)
d - Leonila anapenda nyama sana
e - Zeituni amekufa bado akiwa na umri mdogo sana
Tamathali za Usemi
Baada ya kuangalia matumizi ya methali na nahau ama misemo katika hadithi fupi, sasa tuangalie kipengele kingine cha semi na tamathali katika kuunda fani ya hadithi fupi. Umuhimu wa kipengele hiki ni kusaidia katika kutofautisha kazi ya sanaa itumiayo lugha na ile isiyo ya kisanaa kama vile hotuba n.k. Semi na tamathali zinaweza kugawanywa kama vile alivyofanya Casmir Kuhenga9 Aidha, tunatahadharisha kuwa tamathali za usemi ziko nyingi, na hapa tunazijadili baadhi yake tu.
Tamathali za Mafumbo
Fungu hili lina tamathali kama vile dhihaka, kyembe, tasifida na nyinginezo kama tutakavyoziona hapo baadaye. Kama tulivyokwis'ha kudokeza, tamathali hizo zinatumika kwa madhumuni maalumu. Tuiangalie kila tamathali peke, yake.
Dhihaka
Aina hii ya tamathali ni ya dharau na ina lengo la kumweka mtu katika hali duni kupita kiasi, lakini kwa mbinu za kifumbo. Mara nyingine mtu anayed-harauliwa hujifahamu, lakmi mara nyingi huwa hajifahamu. Wanaomsema kwa kawaida hujua bezo zote juu ya mtu huyo.
Mwandishi wa hadithi fupi anaweza kutumia tamathali za aina hii ili kuonyesha ubingwa wake katika sanaa anayoisanii. Matumizi bora ya sanaa yanategemea sana uwezo na ujuzi alionao msanii. Misemo kama hii huijenga hadithi inayohusika kimaudhui na kifani. Angalia mfano ufuatao kwa ufafanuzi:
Adella alikuwa msichana msafi mno. Ndiyo maana kila mara alipata kupaka mafuta yaliyonulda na kukaribisha nzi walioleta matatizo makubwa.10

Katika mfano tuliouona hapa juu, Adella anasemwa kuwa ni msafi sana kwa kuwa anapaka mafuta yanayokaribisha nzi kwa matatizo. Kusema kweli hii ni dhihaka, kwani hali ilivyo nzi hufuata uchafu mara nyingi. Au angalia mfano mwingine hapa chini:
Bwana Bwanyenye, wewe ni miongoni mwa matajiri nchini Tanzania. Ama labda nikuite kabaila. Nanyi makabaila wa siku hizi mu wakarimu sana. Juzi umetoa shilingi moja kama dawa ildwa ni mchango wako kusaidia ujenzi wa makao makuu ya TANU.11

Katika kifungu tulichokiona hapa juu, Bwanyenye anasifiwa kuwa m "mkarimu," na amepata kutoa shilingi moja katika mchango wake wa kusaidia ujenzi wa jengo la TANU. Shilingi moja kutoka kwa Bwanyenye ni kichekesho na dhihaka tupu!
Tasifido
Tamathali bu iko katika kundi la "adabu," ama "ficho." Yako baadhi ya maneno fulani katika maandishi yanakiuka misingi ya utamaduni wa jamii. Maneno hayo hujulikana kama Lugha safihi. Maneno hayo hayapendezi kusikika hadharani, hasa ikiwa hadhara hiyo ni ya makundi ya watu mbalimbali. Ashakum, tuangalie mifano kadhaa ili kupata ufafanuzi zaidi wa suala zima la tamathali hiyo. Katika mfano huo, mwanafunzi anataka kwenda haja. Anamwendea mwalimu wake anayemfundisha kwa muda huo na kumwambia akiomba aruhusiwe kwenda nje kwa shughuli hiyo. Anasema:
a - Mwalimu naomba kwenda haja
b - Mwalimu naomba kwenda kujituma
c - Mwalimu naomba kwenda kunya
d - Mwalimu naomba kwenda kukojoa
Katika mifano minne iliyotolewa kuna aina ama namna mbili ya kusema jambo lililomsibu mwanafunzi huyo aliyeko darasani kwa sasa. Mifano a na b imekuwa ya "adabu" au "ficho" kuhusu shughuli anayotaka kufanya mwanafunzi huyo nje ya darasa. Lakini mifano c na d haina "adabu" na kusema kweli haipendezi kusikika masikioni. Tasifida ni tamathali inayosema kitu, tamathali inayoambaa kitu ili kupunguza ukali wake kama ilivyofanywa hapa juu. Mifano zaidi imetolewa hapa chini.
a
-
Mariamu ni mwizi
a1
-
Mariamu ana mkono mrefu



b
-
John amekufa
b1
-
John ameaga dunia
b2
-
John ametutupa mkono
b3
-
John amefariki dunia
b4
-
John amerudisha namba kwa Mungu
b5
-
John ametutoka
b6
-
John si mwenzetu tena
b7
-
John ametutangulia
b8
-
John ameitikia mwito wa Bwana Mola wetu
b9
-
John amefumba macho
b10
-
John amesafiri njia ya wote



c
-
Hamida amezaa mtoto wa kiume
c1
-
Hamida amejifungua mtoto wa kiume
c2
-
Hamida ameshusha tumbo lake
Katika mifano iliyotolewa hapa juu, misemo a,b, na c ni mikali. Lakini misemo a1, b1 - b10, na c1 - c2 ni misemo ambayo ina adabu.
Matumizi mazuri ya semi kama hizo yanaweza kuiweka hadithi kuwa bora zaidi. Hata hivyo baadhi ya wataalamu wanaona hali ya kutumia tasifida kuwa ni upungufu fulani katika kazi ya sanaa. Mmoja kati ya wanataaluma hao ni C.H. Holman12 ambaye anasisitiza kuwa wasanii wawe na mtazamo wa kuyatamka mambo kihalisia kama vile yalivyo bila ya kujali yanaumiza ama kufurahisha. Inadaiwa kwa ujumla kuwa mtazamo wa fasihi ni kuelekea kwenye uhalisia, na kwamba mambo yanatakiwa yasemwe bila ficho - yasemwe waziwazi.
Shitizai (Kinaya au Kejeli)
Tamathali hii imekusudiwa kuleta maana iliyo kinyume na ile iliyokusudiwa ama kinyume na ukweli ulivyo. Lengo hasa la shitizai ni kujaribu kuzuia matatizo na migongano pindi itumikapo kwa lengo maalumu la kufundisha na kuasa. Tazama mifano ifuatayo kwa ufafanuzi wa kauli hii:
a
-
Mtu ni mchafu, lakini anaambiwa
a1
-
Sijamwona mtu msafi kama wewe
b
-
Mtu ni bepari, lakini anaambiwa
b1
-
Wewe ni mjamaa ambaye hajapata kuonekana
c
-
Mtu ni adui. lakini anaambiwa
c1
-
Wewe ni rafiki mpenzi, (cf Raisi Nyerere alimwita Fashisti Idd Amin Dada rafiki yake wakati anatangaza vita mwaka 1978).
Katika mfano wa kwanza mtu "mchafu" anayesifiwa anaridhika, haleti matata. Ni hivyo pia katika mifano mingine ya b na c. Wakati mwingine, kejeli pia ina maana ya kuchekelea mtu, kumdharau na kumchusha kwa mzaha. Ni usemi ambao maana yake ya ndani ni kinyume chake, na inabeua maana yake halisi. Ni kebehi, ambamo kisemwacho sicho kikusudiwacho.
Innuendo (Kijembe)
Huu ni usemi wa mzunguko, ni usemi wa kifumbo na humsema mtu kwa ubaya. Katika kusemwa kwa mhusika fulani, msemaji mmoja hudokeza kidogo tu hali ya ubaya juu ya mwmgine. Kunakuwa na hali ya tafakari baina ya wahusika, na halafu hufanya hukumu juu ya mambo muhimu katika hadithi. Maamuzi mara nyingi yanakuwa katika hali ya ubaya.
Tamathali za Mlinganisho
Katika kundi la tamathali tulilolijadili hapa juu tumeona kuwa kundi hilo linatumia mafumbo katika tabia mbalimbali. Kundi tunalolijadili hapa linahusu tamathali za ulinganisho. Kama lilivyo kundi jingine tuliloliona, kundi hili ni muhimu katika ujenzi wa fani ya hadithi fupi za Kiswahili. Tamathali kama vile sitiari, tashibiha, tashihisi, na nyinginezo zinajumuishwa katika kundi hili. Tuangalie baadhi ya mifano ya tamathali hizo hapa chini:
Sitiari
Hii m tamathali ya usemi ambayo kwa kawaida inahusisha matendo, kitu au tabia ya vitu vyenye maumbile tofauti. Ulinganisho huu unazingatia misingi au sifa inayopatikana au zinazopatikana katika vitu vyote viwili, lakini sifa hizo haziwi wazi kati ya kitu na kitu. Angalia mifano ifuatayo:
a - Maisha ni moshi
b - Mtu kinyonga
c - Ana mwendo wa kobe
d - Mchuzi wa kukata na shoka
e - Mwogafisi John
f- John alikuwa mbogo
g - Wakati wa vita alikuwa simba
h - Mwatumu ana jicho la kinyonga
i - Ulimi wako Maria Magge ni ua la waridi
j - Petro ni mwamba, juu yako nitajenga imani yangu
k - Lydia amekuwa sungura
l - Salma ni mbwa kabisa
Katika mifano hiyo, mfano (a) kwa mfano umefananishwa maisha na moshi. Moshi ni kitu kinachodumu kwa muda mfupi sana toka pale unapojitokeza. Kwa hiyo, "mtu" ambaye amefichwa katika neno "maisha" anaishi kwa muda mfupi sana kama vile maisha ya moshi yalivyo. Mfano wa (b) unamlinganisha "mtu" na "kinyonga." Kinyonga ni mnyama aliye na tabia ya kubadili rangi kila awapo katika mazingirs. mapya. Kutokana na dhana hii, mtu anafikiriwa kuwa kinyonga kw» sababu hatabiriki, wakati wowote anaweza kubadilika na kwenye mazingira yoyote yale. Katika mfano wa (c) kobe anatembea polepole. Mtu mwenda pole hulinganishwa na kobe, ndipo tunapopata methali ya "Taratibu ya kobe humfikisha mbali." Kwa kufuata utaratibu huo, sitiari nyingine zote zilizolinganishwa hapa juu zinaweza kufafanuliwa vile. Ni muhimu kusisitiza bapa kuwa sitiari ni tamathali ya usemi ilinganishayo vitu bila kutumia viunganishi kama vile: mithili ya, mfano wa, sawa na, kama kwamba, na kadhalika.
Tashibiha au Mshabaha
Tamathali ya aina hii hutumia mhnganisho wa mambo ama vit.u kwa kutumia viunganishi: "kama," "mfano wa," "mithili ya," "sawa na," "mfano wa," n.k. M.M. Mulokozi na K.K. Kahigi,13wakijadili tashibiha katika ushairi wanasema kuwa katika tashibiha, kama ilivyo katika sitiari, kuna vitu vitatu vinavyofananishwa ambavyo wataalamu wameviita kizungumzwa, kifananishina kiungo. Kizungumzwa ni kitu halisi ambacho huzungumzwa na kitu kinachofananishwa kwa fumbo. Kifananishi kipo katika mawazo na huzingatia maana dhahnia. Kiungo m sifa zipatikanazo katika kitu kinachozungumziwa na hivyo kuhusisha vitu vyote viwili. Maelezo kama hayo pia yanaelezwa na wataalamu wengine kama vile Walter Blair14 na wenzake. Kwa kutumia tashibiha, msanii wa hadithi fupi anaweza kuifanya sanaa yake kuwa bora na nzuri. Mifano ifuatayo inaonyesha tamathali za kitashibiha.
a - Alikuwa mweusi kama mpingo
b - Ana sauti tamu sawa na ya chiriku
c - Kiuno chake ktnatetemeka kama cha mbuni
d - Mwantumu, akiwa amechukia mithili ya mbogo, alinitupia shoka
e - Alianza kukoroma kwa kunguruma mfano wa radi
Katika mfano (a) mtu anasemekana yuko mweusi. Ufafanuzi zaidi wa weusi huo unaelezwa uko kama mpingo. Mpingo ni mti mweusi sana na unapatikana katika sehemu kadha wa kadha za Afrika. Kutokana ua sifa hii ya weusi sana, ndipo inaposemekana kuwa mtu ni mweusi kama mpingo. Kwa maelezo ya kawaida tungeaema hivi:
a - Alikuwa mweusi sana
b - Ana sauti nzuri sana
c - Alichukia (Mwantumu) sana
e - Alinguruma sana
Ukilinganisha semi zile za awali na hizi za pili, hali ya kisanaa imejitokeza sana katika semi za awali kuliko hizi za pili.
Tashihisi au Uhaishaji
Tamathali hii ni ile ya kunafsisha vitu, yaani kufanya vitu viwe na maumbile na kusema au kutenda kama mtu. Katika tamathali ya aina hii vitu kama mimea, maji, moto vinapewa uwezo wa kimtu. Angalia mifano ifuatayo:
a - Chtriku mpenzi usilie! Nibusu mashavu yote ili nafsi yako itakatike.
b - Ua, langu, sema kauli ya mwisho ili nami nitulie.
c - Ningekuwa na uwezo, ningekuamuru nyota ua waridi langu ufunue ktdari changu ili ujionee mwenyewe jinsi ulivyofotolewa na papi za moyo wangu mchanga!
d - Kimya kiliukumbatia moyo wa Maria Florence, msichana msomi wa Jangwani, Dar es Salaam, uliokuwa ukivuja machozi mazito ya damu kwa mapenzi.
e - Kiburi husafiri juu ya mgongo wa ngamia kwa furaha na shangwe, lakini hurudi kwa 'aibu kikitembea kichwa chini na kuomba mahali pa kujisetiri.
f - Mauti u kttu gani wewe? Kwa nini huwezi kuamua, unakuwa hujali nani au nani. kila mtu unamchukua tu? Hata mtoto unamchukua tu? U kitu gani wewe usiyejali umri7

Maneno yaliyo kwenye italiki hapa juu yamepewa uwezo wa kutenda ua kusimama badala ya binadamu.
Mifano mingi ya aina hii inajitokeza katika hadithi za masimulizi za mapokeo. Angalia kifungu cha hadithi ifuatayo:
Hapo zamani palikuwa na Chura na Nyigu. Chura alimwuliza Nyigu. Kwa nini una kiuno chembamba vile? Nyigu akajibu. Ni kwa vile miye sili, chakula chote wakimaliza weye! Ndiyo maana mimi ni mwembamba vile.

Katika mfano uliotolewa hapo juu, Chura na Nyigu ni kiwakilisho cha binadamu wenye uwezo wa kufanya mazungumzo kama hayo yaliyoonyeshwa.
Lakabu
Aina hii ya semi huelezea kitu kwa ubadilisho wa sifa. Uhusiano wa maneno mawili kisarufi hugeuzwa na pengine huwekwa kinyume na taratibu za kisarufi zilivyo. Angalia hapa chini.
a
-
Baridi kali ilimkaribisha
(Lakini mtu ndiye mwenye uwezo wa kukaribisha)
b
-
Giza nene lilimmeza
(Lakini mtu ndiye anayemeza)
c
-
Alididimia katika mawimbi ya furaha
(Lakini kudidimia mahali ni kupotea, si furaha kama ulivyosemwa hapa)
Tamathali za Msisitizo na Nyinginezo
Kundi la tamathali za aina hii husisitiza mambo mbalimbali katika hadithi na hata kazi nyingine za sanaa. Katika kundi hili tuna mubaalagha, metonumia, majazi, na nyingine kama tutakavyoziona hapa chini.
Mubaalagha
Hii m tamathali ya chuku. Tamathali hizo hutia chumvi katika maelezo yanayofanywa katika kazi ya sanaa hususan hadithi fupi. Lengo la matumizi ya tamathali za aina hii ni kufurahisha, kuchochea, kuchekesha au kusisitiza hoja. Hoja mara nyingine zinaweza kujitokeza zile za kuibua hisia za kuchoma moyo, kuchochea furaha, huzuni n.k. Angalia kwa mfano semi zifuatazo:
a - Uso wake ulikuwa ua mito ya machozi ya uchungu baada ya mume wake kushikwa na askari wa usalama wa taifa.
b - Mwangalie alivyo na mlima wa matiti! Amebeba mzigo wa matiti!
c - Watu walijaa chumbani hadi chumba kikatapika.
d - Ana ana tani za mapesa.

Mifano hii inaonyesha dhana ya chuku tuliyokwisha kuitaja hapa juu. Katika mfano (a) imeelezwa kuwa "mtu" alilia hadi kuunda mito ya machozi. Sote tunafahamu mto ulivyo na maji mengi. Na mto kuwa usoni mwa binadamu ni jambo lisilo la kawaida, na kusema kweli hili haliwezi kutokea. Hii ni chuku, ni usemi uliotiwa chumvi nyingi mno. Mfano (b) tunaambiwa "mtu" ana "mlima" wa matiti. Amebeba "mzigo" wa matiti. Kwa mara nyingine tena, sote tunaufahamu mlima ulivyo na jinsi binadamu asivyoweza kuubeba kifuani pake! Au mzigo ukiwa ni mkubwa sana, ni vigumu pia kuubeba. Kuhusu chumba kujaa hadi kutapika hii nayo ni chuku pia. Anayetapika ni mtu aliyeshiba sana. Ikiwa hii imesemwa kwa dhana ya kuwa kulikuwa ua watu wengi katika chumba kinachohusika, basi hii imetiwa chumvi nyingi mno!
Aidha, semi hizo zote zikichunguzwa hapa, zinaleta dhana ya kufanya kitu na kuvuka mpaka wa kawaida. Hii ni kufanya kitu kupita kiasi.
Metonumia (au Taashira)
Neno la Kiingereza la metonymy ni la asili ya Kigiriki lenye maneno mawili: meta na onyma yenye maana ya badiliko lajina la kitu. Katika Kiswahili, bado neno hili linadumisha asili yake ya Kigiriki na kubaki linaitwa "metonumia," kwa dhana ileile. Kwa kuzingatia hilo, tunaweza kusema kuwa metonumia ni tamathali itumiayo maneno kuwakilisha dhana, kitu n.k. Tamathali hii hutumia hasa ishara (ndiyo maana huitwa pengine taashira) kama alama ya kuwakilisha tukio fulani. Kwa mfano:
a - Kutabasamu huwakilisha furaha
b - Kitambi huwakilisha utajiri
c - Kukonda huwakilisha umaskini
d - Taji huwakilisha ufalme
e - Jembe huwakilisha ukulima
f - Mvi huwakilisha uzee
Majazi
Msemo huu huashiria maana ya kitu kizima mara ikitamkwa sehemu tu ya kitu hicho. Majazi na metonumia kimsingi ni tamathali zinazofanana, tofauti iko katika msisitizo tu. Ni aina ya sitiari, ambapo pia kitu kizima kikitajwa huwakilisha dhana ya sehemu ya kitu hicho. Angalia mifano ifuatayo:
a - Mbuzi: Mnyama/chombo
b - Paa: Mnyama/sehemu ya nyumba/tendo
c - Roho: Mtu
Tunaweza kufafanua tamathali hiyo kwa kutoa mifano ya sentensi mbal-imbali hapa chini.
a - Mbuzi amekataa kukuna nazi
b - Paa aliweza kuhangaisha umma
c - Roho yake imehama leo asubuhi
Taniaba
Huu ni usemi unaoonyesha kuwa kitu fulani ni badala ya kitu kingine. F.E.M.K. Senkoro anasema kuwa taniaba ni tamathali ambayo jina la mtu binafsi hutumiwa kwa watu wenye tabia, mwenendo na kazi ya mtu anayefanan-ishwa. Halafu anatoa mifano ya tamathali hiyo kuwa ni:
a
-
Yesu: Dhana ya mkombozi
(Raisi Nyerere ni Yesu wa Tanzania)
b
-
Voster: Dhana ya ubaguzi
(Mavoster ni wengi katika Afrika hii)
c
-
Amini: Dhaaa ya ujambazi
(Ma-Amini wanapatikana sehemu nyingi hapa Afrika)15
Msisitizo Bayani
Hii ni tamathali inayoonyesha ushindani wa mawazo. Ni tamathali inayosisitiza maana ya sentensi kwa kutumia kinyume. Kwa mfano tazama tungo zifuatazo:
a - Mwanadamu hupanga, Mungu hupaagua
b - Waitwa ni wengi, lakini wateule ni wachache
c - Tabia yake si mbaya, ni nzuri
d - Zeituni si mweusi, ni mweupe
Ritifaa
Hii ni tamathali ya usemi ambayo kwayo mtu huzungumza na kitu au mtu asiyekuwepo ambaye husikiliza katika fikra tu. Angalia mifano ifuatayo:
a
-
Ewe mwanangu Atuyane Tugalile! Lala vyema humo tumboni mwa mama yako Diana. Napenda akuzae siku zako zikifika. ili uje tnishi sote katika mtaa huu wa Takadiri hapa Magomeni!
b
-
Ewe marehemu babu yangu unayelala mbele yangu kwa uchungu nakuhurumia. Sit.wamba sioni uchungu kwa hilo lililonisibu, na natambua hungesita kusimama na kunituliza kama ungekuwa na uwezo huo. Lakini babu... tangulia... labda tutaonana wakati wangu ukifika. Msalimu marehemu mke wako, bibi yangu Bibiana.
c
-
Baba yetu marehemu Amani, Salaam sana. Habari za siku nyingi toka ututoke ghafla hapo mwezi Mei. Sisi uliotuacha nyama hatujambo. Vipi waliotangulia kabla yako? Je, mtoto wako Ignacio ulimkuta ana wajukuu? Na jee mdogo wake Ja-mir aliyekufa mwaka 1984 naye wameungana na mume wake baada ya kuachana katika kufa kwa mwaka mmoja na nusu? Siku hizi hawagombani tena? Je, yule mdogo wetu Joel naye ulimkuta anakaribia kuoa? Au ameoa? Ana wajukuu wake huko akera? Je, kawa majirani zetu waliokufa. kabla yako nao hawajambo?
Tana hamu ya kukueleza machache ya. huku duniani. Kwanza kabisa, mtoto wako wa kiume yule mwalimu anayefundisha. pale Chuo cha Ualimu Songea ameendelea kudhibiti mali safi ua mama. Yule mtoto wako anayefundisha Chuo Kikuu, ambaye ulimwacha amechumbia sehemu za Mbangamao uchumba umevunjika. Hii ni kazi ya majirani zetu, hasa huyu mjukuu wa Ndenda, anayefanya kazi pale Songea. Madai yao hasa m kuwa mtoto wako Shitete wanadai ni mhuni, eti aaa wasichana wengi ua anatunga vitabu vya kihuni na ha-dithi sa kihuni. Jambo hili Ulimwudhi sana Shitete, alikuwa amepanga kufanya mauaji makubwa. Kwanza angemng’oa yule wa Lindi ua kumalizia na huyu. Lakini ushauri wa mama umesaidia na kumrudisha nyuma. Shitete kwa sasa ameoa huko sehemu za Mpapa... Huwezi kuamini, LAKINI mtoto wako Shitete sasa ana maisha mazuri. Watoto wako wengine wote ua wajukuu zako hawajambo.
Mwisho, tunakuomba uendelee kutukumbuka kwa kuja katika njia za ndoto. Sisi kama kawaida, tutakutambikia pale ktiegeoni kila baada ya miezi sita. Tafadhali tusalimie marehemu babu zetu Manyuka aa Msokile. Tusalimie bibi zeta Bibiana Kuhangaika na Kilwambo Kitunda. Tusalimie ndugu zetu wote«walioko huko. Tutakutana sisi tutakapobadilisha maisha yet«kwa kifo. Tunakutakia heri!
Familia yako
Kijijini Mtakanini
Mifano hii yote inajaribu kufafanua mjadala wetu kuhusu tamathali hiyo ya kiritifaa iliyotajwa hapajuu. Pengine tungeona tena mfano mmojajuu ya suala hilohilo. Mfano huu ni wa shairi la Shaaban Robert liitwalo AMINA aliloliandika kumlilia mke wake baada ya kufariki dunia.
AMINA
Amina umejitenga., kufa umetangulia
Kama ua umefunga, baada ya kuchanua
Nakuombea mwanga, Peponi kukubalika
Mapenzi tuliyofunga hapana wa kufungua
Nilitaka unyanyuke, kwa kukuombea dua
Sikupenda ushindike, maradhi kukuchukua
Ila kwa rehema yake, Mungu amekuchagua
Mapenzi tuliyofunga kapana wa kufungua
Majonzi hayaneneki, kila nikikumbukia
Nawaza kile ua hiki, naona kama ruia
Mauti siyasadild, kuwa mwisho wa dunia
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Nasadiki haziozi, roho hazitapotea
Twafuata uokozi, kwa mauti kutujia
Nawe wangu mpenzi, Peponi utaingia
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Jambo moja nakumbuka, sahihi ninalijua
Kuwa sasa umefika, ta'bu isokusumbua
Kwayo nimefurahika, nyuma nilikobakia
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Ninamaliza kutunga, kwa kukuombea dua
Vumbi tena likiunga, roho likirudishiwa
Mauti yakijitenga, mapenzi yatarejea
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Usomapo shairi hili mtu unaweza kuona picha ambayo inajitokeza mbele ya Shaaban Robert ya marehemu mke wake Amina. Maneno hayo ya kishairi yanasemwa kana kwamba Shaaban Robert mwenyewe angetaka Amina amjibu na kumsemesha. La! Imeshindikana... Shairi hili liko kwenye tamathali ya kiritifaa.
Tabaini
Huu ni usemi unaosisitiza jambo kwa kutumia maneno ya ukinzani. Angalia mifano ifuatayo:
a - Amekuwa mrefu si mrefu, mfupi si mfupi, ni wa kadiri.
b - Hali yake ni ya ugeugeu, nzuri si nzuri, mbaya si mbaya.
c - Binadamu kinyonga, atakusemesha mazuri, kumbe rohoni. kweusi!
d - Usimwamini mtu. Yu acheka machoni, rohoni ana mabaya juu yako.
e - Ngamia afe, mzigo wa bwana ufike.
f - Sura inacheka, moyo unalia.
g - Yanga si timu mbaya, wala Simba si timu mbaya.
h - Hatukuwa tusio na furaha kwa kuondoka jioni hiyo.
Mbinu Nyingine za Kisanaa
Kimsingi, tamathali za usemi huambatana na matumizi ya mbimu nyingine za kisanaa ambazo hutunuwa na wasanii. Mbinu hizo kwa baadhi wameziweka katika kundi la tamathali za usemi. Hapa tumeziweka katika kundi hili kwa msingi kwamba mambo yanayojitokeza siyo ya ulinganisho katika zote, bali husisitiza ua kupamba kazi ya sanaa. Katika kundi hili kuna takriri, tashtiti, mjalizo, mdokezo, na kadhalika.
Takriri
Takriri ni urudiaji wa maneno, silabi au sauti zinazolingana katika kazi ya sanaa. Mwandishi huamua kwa makusudi kurudiarudia maneno au vipengele hivyo kwa lengo maalumu la kulisisitizajambo ama kulitia mkazo jambo linaloelezwa. Angalia hapa chini kwa ufafanuzi zaidi.
Maria Magge aliamua tena kumfuata Manda. Alikwenda, hakufika. Jua lilizidi kunyonya maji ardhini. Jua lilinyonya, likanyonya ua mvutano ukazidi. Hakukata tamaa. Alikwendambele hakufanikiwa. Hakukata tamaa, alikwenda mbele tena ajaribu bahati yake. Mwisho alifika ukingo wa tumaini lake. Hakufantkiwa! Alimwomba Mungu mchana na usiku, hakufanikiwa. Imani juu ya Mungu ikapungua. 'Mwisho alitoa sauti ya kukata tamaa iliyojaa masikitiko akisema: "Mwalimu wangu mpenzi, usiponioa nitakufa ... Nitakufa ningali mbichi usiponioa mwalimu wangu! 16

Maneno yote ya msisitizo yameandikwa kwa italiki. Tunaweza kufafanua zaidi kwa mifano mingine kama inavyoonyeshwa hapa chini:
a - Haba na haba hujaza ki baba
b - Baraka haraka haina baraka
c - Padogo pako si pakubwa pa mwenzio
Katika methali hizi tatu tunaona takriri katika maneno na herufi zilizo kwenye italiki. Ukichunguza zaidi, utaona kuwa methali hizo zina takriri za aina nyingi.
Ukariri wa sauti au silabi pia unaweza kuonekana katika mfano ufuatao wa shairi la Abdilatif Abdalla:
Kuno kunena kwa nini
Kukanilomeya kuno
Kwani kunena kunani
Kukashikwa kani vino
Kani isiyo na kiini
Na kuninuya mno
Kanama nako kunena
Kwaonekana ni kuwi17
Katika andiko hili takriri inajidhihirisha kwenye silabi - ku -, herufi - k -, - n -, - m -, n.k.
Mtindo huu wa msisitizo una lengo la kufanya jambo limwingie msomaji vyema. Aidha, takriri pia inatumiwa kupambanua dhamira zilizoko katika hadithi. Wakati huohuo pia takriri inapamba hadithi kisanaa na kusaidia kuweka kumbukumbu ya baadhi ya mambo muhimu. Takriri pia hutumika kwa nia ya kutaka kukazia jambo fulani, ikiwa jambo hilo litatajwa mara nyingi na kurudiwarudiwa kirefu, ama kutajwa peke yake.
Mdokezo
Wakati mwingine hutokea kuwa mwandishi anamjenga mhusika wake akisema mawazo yake kwa njia ya mdokezo. Kuna mifano mingi katika kitabu hiki, hasa katika sehemu ya pili ya kitabu hiki. Mifano michache imetolewa hapa chini:
Ah! Naye asijaribu kukuvika kilemba cha ukoka! Kwani... Mwanaume hanalo moja likuaminishe! Na ukimpa ndiyo yako; nakuambia, ah! ... na tukae tu... Tusubiri ukweli wa historia usiopingika...18

Tashtiti
Huu ni mkazo wa maneno yasemwayo ama kuaadikwa. Katika mbinu hii, mwandishi hutumia mbinu za kuuliza maswali kwa jambo ambalo anafahamu jibu lake. Msanii hufanya hivyo kwa lengo la kusisitiza jambo, kuleta mshangao, n.k. Angalia mifano michache inayofuata:
a
-
Msickana Diana amefariki. Jambo hili linamshtusha msichana Luiza, kwa hiyo anataka kujua zaidi kitu anachokijua. tayari. Anasema kwa mshangao mkubwa ua kujiuliza:

Diana na uzuri wake amekufa? Looh! Sadakta! Ametu-toka? Hatakuwa nasi tena! Masikini...



b
-
Jambazi limekatwa mguu hapa kijijini wakati lilipokuwa likiiba mali ya kijiji. Baadhi wamepata habari na wala hawaamini kuwa tukio hili ai la kweli. Kwa hiyo wanasisitiza kwa kuuliza maswali mbalimbali.
Jitu limekatwa mayu? Masalale! Shaash...! Bughudha sasa imekwisha? Hatuonewi tena na jitu? Na tuone...
Ukiangalia maswali yale yanayoulizwa katika mifano iliyotolewa hapo juu, majibu yake ni wazi na yanafahamika vyema kabisa kwa yule anayeuliza maswali hayo. Kitu ambacho anachokitaka hapo ni msisitizo tu utakaotokana na kujibiwa kwa maswali hayo. Mifano mingine ni kama hii inayofuata:
a
-
Saumu malaika Aziz muhibu wa moyo wangu! Looh! Nikupe nini uniamini kuwa kwato niko radhi kujitosa ba harini nikikukosa? Sadakta!



b
-
Astaghafirulahi! Mwanaharamu maluuni huyu jizi asiyejua kupenda! Limekwenda na kila kitu changu? Ole! Litanikoma.
Nidaa
Huu ni msemo ambao unaonyesha kushaogazwa kwa jambo fulani. Misemo ya aina hii huambatana na matumizi ya alama za mshangao, kukubali jambo, kuchukia ama kuonyesha heshima maalumu. Angalia misemo inayofuata:
a
-
Ah, maskini moyo wake, mbona nakupenda vile?
b
-
Zeituni mpenzi wangu! Ningekuwa. na uwezo ningekuandalia harusi ya ndovu kumla mwanawe!
c
-
La! Hasha! Puka chaka! d - Lahaulaa! Alaaa! Ama!

Mjalizo
Wakati mwingine mwandishi huaadika sentensi zake bila kutumia viunganishi kama vile: "ya", "na" "wa" '"kwa" n.k. Hii ni mbinu mojawapo ya kisanaa ambayo wasanii hupenda kuitmnia katika kuongeza uzuri wa kisanaa katika kazi zao. Tazama mifano ifuatayo:
a - Niliimba, nikanuna, nikachoka,
b - Nilivuna, nikatuta, nikashindwa
c - Mwenye kusamehe, asiye ua kinyongo
d - Fundi wa kuogelea, moyo usio woga, mwenye kupenda kusaidia, tayari, kujitoa mhanga
Wigo
Mbinu za aina hii huiga sauti ama milio mbalimbali katika kazi za sanaa. Mwandishi huwa na juhudi ya kujaribu kuiga kitu kama kinavyojitokeza katika mazingira ya kawaida. Katika fungu hili tuna mbinu za matumizi kama vile onomatopeia, mwigo-lafudhi, n.k.
Onomotopeia av Tanakali-sauti
Katika aina hii ya wigo mwandishi hujitahidi kuiga sauti za milio mbalimbali. Milio hii m ya wanyama, magari, simu, n.k. Tazama mifano hapa chini:
a - Alitumbukia bwawani, "Chubwi"
b - Alidondoka chini "pu!"
- Chura alilia, "Korodoodoo! Mungu mkubwa!"
Maneno chubwi!, pu! korodoodoo! m onomatopeia. Mifano ya namna hii pia tunaweza kuipata katika methali za Kiswahili.
a - Chururu si ndo! ndo! ndo!
Hivyo ndivyo yanavyoigwa maji yadondokavyo katika ndoo. Na mchanja kuni naye anapobanda vibanzi kwa shoka hujipa tumaini kuwa:
b - Bandu! bandu! huisha gogo!
Hii ni baadhi tu ya mifano ya tamathali hizo zinazoiga sauti. Bado kunaweza kuwa na mifano mingi mingineyo kama tutataka kuisema na kuitambua ili itumike katika kazi zetu za sanaa.
Onomatopeia au tanakali sauti ina kazi kadhaa. Pamoja na kazi nyinginezo, kwanza ni kukaziajambo linalosemwa limetendeka. Kazi nyingine ya onomatopeia m kukomaza kitendo kinachoelezwa. Mwisho, huvutia usikivu katika taaluma za hotuba.
Tanakali- lafudhi
Hutokea pia kuwa mwandishi katika kusanii kazi yake huiga sauti ya lafudhi ya lugha fulani fulani katika taifa ama mataifa. Angalia mfano huu ufuatao:
"Watataka kwenda kunizika mtu wao. Watakuwa tayari kulipia gharama zote.
"'Tukupe ngapi?" atauliza mmoja kumwuliza yule mlinzi wa maiti wa kabila la Kimakonde. Naye atajibu:
"Kupungua kabati tu, nataka njulupu mia unusu yake!
Uchilete nchezo njomba. Tapachali kweli wewe tapachali."19
Maneno ya lafudhi ya Kimakonde yameandikwa kwa italiki ili kuonyesha tanakali lafudhi tunayoisema.
Usambamba
Huu ni mtindo wa maelezo ambapo kauli zenye kufanana kimaana au kisarufi huwekwa pamoja - huwekwa sambamba. "Kukinzana" katika usambamba hutokea mara chache sana. Angalia mifano ifuatayo:
a - Kikubwa kikipinduka na kifupi huwa kirefu
b - Mwanadamu hupanga, Mungu hupangua
c - Wengine wakicheka, yeye ananuna
Ukiangalia mifano yote hii, utaona kuwa inafanana na tamathali zile zina-zozingatia dhana ya kinyume au msisitizo bayani, tuliyoiona hapajuu.
Tauria (Mchezo wa Manena)
Hii ni mbinu pia ya kisanaa ambayo kwayo msanii hupenda kutumia maneno ya tahajia moja. Tahajia huwa katika herufi, vina, n.k., lakini maana ya maneno hayo huwa ni tofauti. Maneno hayo aghalabu huwa yamepangwa vizuri katika sentensi moja. Tazama kwa mfano sentensi zifuatazo:
a - Kaa alikalia kaa la moto
b - Paa alipaa juu ya paa la nyumba
c - Chungu alifia kwenye chungu
d - Mbuzi alikalia mbuzi ya kukunia nazi
e - Meza alimeza dawa iliyokuwa juu ya meza
- Alimfinya kucha usiku kucha
g - Ana ana kichwa kidogo
Matumizi ya Ucheshi
Mbinu hii imejadiliwa kirefu sana ua F.E.M.K. Senkoro katika kitabu chake kiitwacho Fasihi.20 Hatutajadili hapa kwa urefu kuhusu mbinu hii. Isipokuwa tunasema kuwa mtu mcheshi si msununu, ua msanii anapoingiza mbinu hii katika kazi ya sanaa ana malengo mengi. F.E. M.K. Senkoro anataja faida za ucheshi kama: husaidia kuondoa uchovu, huburudisha, husaidia kujenga taswira, hufuta uchovu.
Hii ni baadhi ya misemo, tamathali za usemi ua mbmu za kisanaa ambazo zikitumiwa katika kazi za sanaa na msanii ubora wake huongezeka. Sehemu hii imejadili matumizi ya tamathali mbalimbali katika kazi ya sanaa. Inasisitizwa kuwa hizi ni baadhi tu ya semi zinazoweza kutumika katika kazi za sanaa. Utafiti zaidi ukifanywa zinaweza kupatikana tamathali nyingine nyingi ambazo ni muhimu na zinaweza kutumika katika kazi za sanaa.
Ishara
Waandishi pia wanaweza kutumia mbinu hii katika kujenga taswira na picha mbalimbali katika kazi zao za kifasihi. Ishara kwa kawaida katika fasihi ni za aina mbili. Kwanza kuna zile ambazo zinahusu maana ya kitu kinachoelezwa, yaani kama kinavyojitokeza katika akili za msomaji ama msikilizaji wa kazi ya sanaa pamoja na mtazamaji. Lakini pia ishara inaweza kuwa na maana ya kitu kingine kabisa katika mazingira ya jamii. Ishara ya safari kwa mfano inaweza kuwa ua maana iliyo tofauti na safari yenyewe. Inategemea msanii anaitumia vipi ishara hiyo ya safari.
Katika fasihi kwa mfano, mhusika anaweza kujengwa akitoa ishara fulani - kama kukonyeza. Mtazamaji atapata wazo na kutenda kufuatana na kukonyeza huko. Au anaweza kutoa ishara inayoonyesha kumeza kitu. Maana yajambo hilo halitakuwa kumeza pengine, bali litakuwa na maana ya kushikwa na njaa kali.
Katika hali zote hizo, ishara bado zinatumika katika kujenga picha mbalimbali ambazo hatimaye huibua hisia kwa wasomaji wa kazi za kifasihi zinazohusika.
Mitindo ya Hadithi Fupi
Baadhi ya wataalamu na wananadharia wanaona mtindo kuwa ni mchanganyiko wa mambo makubwa mawili. Mambo hayo ni wazo (maudhui) la msanii linaloelezwa najinsi wazo hili linavyoelezwa na msanii. Nadharia hii inauangalia mtindo kama kitu chenye mchanganyiko uelezao uhusiano uliopo kati ya mfanyakazi (nisimuliaji/msanii/mwandishi) na kazi anayoifanya21 Jinsi jambo linavyosemwa husaidia kuelezea ua kufafanua maana ya kile kinachosemwa.
Mtazamo huu umepata pia kuelezwa na H.J.M. Mwansoko22 wakati anapochunguza mitindo mbalimbali ya uandishi.
Katika uandishi wa kifasihi, mtindo pia unaweza kuwa ni tabia ya uandishi katika kipindi cha mfumo fulani wa maisha ya mtu. Kwa mfano mwandishi aliyekuwa akiandika kwa Kiswahili karne ya 17 - 18 alikuwa akitumia mtindo ulio tofauti na huu wa sasa. Hii inatokana na hali, mfumo, kanuni ua taratibu za maisha zilizokuwapo kwa wakati huo na zile ambazo ziko kwa sasa ambazo zinaonyesha ukweli kuwa maisha ya jamii yanabadilika kulingana na historia. Ni wazi kuwa mambo yalivyokuwa yakielezwa kama yalivyotendeka kwa wakati huo yatakuwa tofauti na jinsi yanavyoelezwa kwa sasa.
Wakati mwingine mtindo unaangaliwa kama tabia ya mtu binafsi juu ya ufundi, umahiri na hisia za kibinafsi katika kutenda mambo yake anayokutana nayo. Kwa mfano kama kuna wachezaji wawili wa timu ya mpira, nao wana-toka katika timu moja, wanatumia mtindo mmoja wa kucheza wakiangaliwa kama watu wanaotoka katika timu moja. Lakini pia kila mchezaji kutoka katika timu hiyohiyo moja ana mtindo wake wa kucheza. Ndivyo ilivyo katika suala la uandishi. Waandishi wanatofautiana katika mitindo kwa kuzingatia utofauti wa dhamira, nafsi ya msanii na kipindi alichoandikia hadithi ama kazi yake ya sanaa. Ingawa waandishi wa Kiswahili wanatumia lugha ya Kiswahili, kila mwandishi ana mtindo wake wa kuyaelezea mambo yake.
Kwa upande wa mwandishi, mtindo unatawaliwa na mambo kadhaa. Kwanza, ni nia ama lengo lake mwandishi. Pili, ni mtazamo na msimamo wa mwandishi. Mtazamo wa mwandishi unahusu maono yake juu ya suala zima au masuala anayoyaangalia katika kazi yake. Wako waandishi wenye mtazamo wa kidhanifu (ambao msingi wake wa mtazamo ni kudhani) ambao hawakubaliani katika mabadiliko ya kisayansi. Waandishi hao wanaangalia ulimwengu kwa kuhusishwa ua nguvu za Mungu, miungu, n.k. Kutokana na jambo hilo kila mtu anachokieleza mwandishi huyo kitakuwa na udhanifu mwingi.
Mtazamo wa kisayansi ru tofauti na huu. Mtazamo huu huuangalia ulimwengu kuwa ni kitu kinachobadilika kufuatana na historia ya wakati, mahali, n.k. vikitawaliwa ua kanuni za asili zinazotawala maisha ya binadamu. Mtazamo huu ni wa kihalisia unaogusa maisha ya mtu ya kila siku.
Wakati mwingine mtindo unaweza kutokana na mazingira yake ya kielimu. Katika suala kama hili, inategemea mwandishi amepata elimu ya aina gani? Amepata elimu ya vitendo ama nadharia tu? Makusudio ya elimu hiyo ni yepi? Kiwango cha elimu pia kinaweza kuongeza ufanisi wa uandishi wa hadithi fupi. Mwandishi, kwa kutumia stadi alizojifunza katika elimu yake, anaweza kuziandika hadithi vizuri.
Kwa kuhitimisha maelezo hayo yajumla kuhusu mtindo, tunaweza kusema kuwa mitindo inahusu mambo mengi. Kama H.J. M. Mwansoko23 anavyosema kuwa, "mitindo m mifumo ya zana za kilugha inayotokana na maendeleo ya kukua kwa lugha ambayo hutofautiana kufuatana na kutumiwa kwake katika mawasiliano yahusuyo nyanja mbalimbali za kazi ua shughuli za jamii."
Kutokana na fasiri hii ni wazi kuwa kutakuwa na tofauti ya mitindo kati ya utanzu na utanzu, kati ya mtu ua mtu, dhamira ua dhamira, n.k.
Vipengele vya Mitindo
Uchaguzi wa Maneno
Suala hili limekwisha gusiwa hapo mapema kwenye vipengele tofauti tofauti. Ukweli ni kuwa matumizi ya mambo kama tamathali za usemi na misemo mingine, matumizi ya methali n.k. ni mambo yanayokwenda pamoja na jinsi mwandishi anavyochagua maneno katika uandishi wake.
Hiki m kipengele cha lugha kijumla. Unapozungumzia mtindo wa kazi ya sanaa tunazungumzia matumizi ya lugha, kile kinachosemwa kinaweza kilazimishe aina ya matumizi ya maneno. Kwa mfano, mwandishi anapoelezea jambo fulani anaweza kuamua atumie maneno yenye maana nasibishi tu. Maneno ya aina hii yana maana inayofananishwa ua maana halisi ya jambo lililotajwa. Kwa mfano maana nasibishi ya bendera ni uhuru, uzalendo n.k. Maana yake halisi m kipande cha nguo kinachotundikwa ulingoni kikapepea. Maneno yenye maana halisi yanapotumiwa yanaeleza uwazi wa kile kinachoelezwa.
Suala la uchaguzi wa maneno ni la muhimu kwa sababu kila neno linavyotumika lina athari zake mbalimbali katika kulela maana inayokusudiwa.
Kukiwa na uchaguzi mzuri wa maneno, kitu kinachofuatia ni jinsi mwandishi anavyopanga maneno yake. Pengine mwandishi hupanga maneno kwa kutumia sarufi sanifu. Lakini pia anaweza atumie mbinu ngeni kabisa; ambayo haizingatii misingi ya kisarufi. Angalia mfano hapa chini.
a - Twakiacha kiza kitumeze?
b - Kiza kitumeze twakiacha?
c - Kitumeze twakiacha kiza?
d - Hukiogopi kiza kati yetu?
e - Kiza kati yetu hukiogopi?
f - Kati yetu hukiogopi kiza?
g - Yetu kati, kiza hukiogopi?
h - Kikatapika, chumba kilijaa!
i - Chumba kilijaa kikatapika!
j - Kilijaa kikataika chumba!
Mifano hii inaonyesha mipangilio mbalimbali ya maneno katika sentensi. Iko mipangilio ambayo ni ya kawaida ua iko isiyo ya kawaida katika usemaji na uandishi wa lugha ya Kiswahili. Kila mpangilio hapa una athari zake katika kuleta maana ya hadithi.
Matumizi ya Taswira na Ishara (Jazanda)
Picha ama taswira ni kiwakilisho cha kitu kwa maneno au kitu halisi, na kiwakilisho hicho chaweza kufahamika kwa mtu mmoja au watu wengi zaidi. Kimaandishi, kiwakilisho hicho kinapambanuliwa kwa matumizi mazuri ya lugha. Picha za kisanaa zinajitokeza kwa misingi kuwa vitu vinavyowakil-ishwa kipicha vinafahamika. Kwa msingi huo picha ni kitambulisho maalumu cha lugha ya kisanaa. Athari za lugha humfikia msomaji kwa njia ya kusikia, kuona, kunusa ama kugusa. Kutokana na picha, msomaji anaweza kuathirika kwa furaha, kusisimka, kuogopa, kuvutika, kuchukia n.k.
Kwa kutumia lugha ya kisanaa, msanii anaweza kuwasilisha uzoefu wake kwa kiasi kikubwa, hisia zake n.k. lakini kwa njia ambayo ni tofauti ua ile ya kitaaluma. Picha si pambo tu, bali ni kitu muhimu katika kuleta maana ya dhamira mbalimbali zinazojitokeza katika kazi za sanaa.
Picha zinajitokeza kwa dhana mbalimbali. F.E.M.K.Senkoro24 na E. Kezilahabi25 wanaziainisha picha hizo kuwa ni za hisi, picha za maumbile na zile za matendo. Tena ziko picha ambazo zinaeleweka moja kwa moja na ziko nyingine ni ngumu kueleweka kirahisi.
Kwa picha zinazoeleweka kirahisi, wengi wanaosoma kazi za sanaa za kifasihi wanaweza kupata picha ya jumla. Lakini kwa zile picha ambazo ni ngumu kueleweka na zinategemea hali ya kimazingira, zinajitokeza katika kazi za sanaa na kutoa maana kufuatana na muktadha - hali ambapo hiyo kazi ya sanaa inasomwa. Picha za aina hii zinaweza kufasiriwa ama kutafsiriwa na msomaji kwa maana mbalimbali.
Jinsi ya Kusema Jambo
Njia zitumikazo zinatofautiana, na ukweli ni kuwa inategemea na nia ya mwandishi - anataka kusema nini, kwa nani na kwa jinsi gani? Njia muhimu ni pamoja na maelezo, masimulizi na kuhoji.
Maelezo
Aina hii ya maandishi hushughulikia mambo kama yanavyoonekana. Ni ufafanuzi wa maelezo kama mambo yalivyo. Kazi kubwa ya maelezo ni kufahamisha jinsi mambo yalivyo. Angalia mfano ufuatao kutoka kitabu cha Zaka la Damu.
Lyanda alikuwa mtu mwenye umbile kubwa sana, tena mnene kabisa mwenye tumbo kubwa mno. Lyanda maana yake tumbo kubwa sana. Kumbe ni jina alilopewa na Wafakiri. Macho yake yana njaa ya kitu fulani, siyo chakula bali kitu kingine, yana tamaa ya kitu fulani. Mgongo wake umepinda kidogo lakini hayo siyo maumbile yake ...
Pale alipokuwa amekaa Ndatu alianza kuchunguza mazingira. Kwa upande wa magharibi wa ukumbi, palikuwa na meza moja kubwa ambayo ilifunikwa kitambaa kizuri chenye maua ya dhahabu na viti vikubwa sita vilivyozunguka meza hiyo. Hapana shaka ilikuwa ikitumiwa kwa maakuli...26
Ukichunguza maandishi hayo unaweza kugundua mambo mengi yanay-ofanya kazi iwe ya pekee kwa kuweka vivumishi au maneno yanayosifia mambo mbalimbli.
Kwanza, tukimchunguza Lyanda, tunaona picha ya mtu mkubwa - mwenye umbile kubwa tena mnene... na t.umbo kubwa sana. Tunaambiwa kuwa nyumba yake ni kubwa na nzuri - ukwasi uliomo na jinsi nyumba hiyo ilivyopangwa. "...upande wa magharibi... (pana) meza moja kubwa (yenye) kitambaa kizuri, chenye maua ya dhahabu, viti vikubwa sita vilizunguka meza hiyo.
Mfano huu unaonyesha kimsingi mbinu za maelezo ambazo hutumiwa na waandishi kwenye kazi zao za sanaa za kifasihi. Mwandishi wa hadithi fupi za Kiswahili anaweza pia kutumia mbinu hii ya maelezo katika kuelezea ayatakayo.
Masimulizi
Katika mbinu hii ya uandishi, msanii hutoa masimulizi yake juu ya mfululizo wa matukio kama yalivyotokea katika kipindi fulani cha maisha ya wahusika. Mwandishi husema nini kilitokea, jinsi gani kilitokea na mahali ambapo hayo yalitokea. Je, mambo hayo yalipotokea kati ya A na B kulikuwa na nini? Angalia mfano ufuatao kutoka Thamani ya Ukubwa.
Ninapoyaona maandishi hayo, ninatambua mara moja kuwa hii ni kazi ya Mama Tusi, mama ambaye ni majuma mawili tu yaliyopita amein-gizwa kwenye darasa la Kiingereza la masomo ya kujiendeleza ya Watu Wazima, baada ya kufuzu uzuri mtihani wa kisomo chenye manufaa katika hatua yake ya nne. Kwa mbali namwona mtu mwingine ambaye anafanya shughuli nisizozielewa. Anatembea polepole na kimya kimya kutoka kwenye mlango wa jengo hili ambapo nimejibana. Mara anatulia Halafu anaendelea tena...27
Katika kusimulia, yako mambo ya msingi ambayo huangaliwa sana na wasanii. Kwanza kuna yielezi. Matumizi ya vielezi yafanywe kwa uangalifu, kwani huathiri mfululizo wa masimulizi. Tazama.kwa mfano kifungu kifuatacho kutoka hadithi ya Wasubiri Kifo.
Mkoromo huu ulipoacha, mgonjwa alianza kuhema tena upesi upesi ua macho yake ambayo sasa yalionyesha majilio ya kifo takuwa sasa hayatembei ua kope zake zilikuwa hazipepesi. Lakini alikuwa bado akihema. Waliokuwepo walijua fahamu zake zilikuwa zimepotea.28
Jambo jingine muhimu ni kuwa mwandishi anatakiwa azingatie matumizi ya nyakati mbalimbali katika kazi yake ya sanaa. Baadhi ya wasanii hutumia muda uliopita, wengine muda uliopo. Nyakati zote zinaruhusiwa; jambo la muhimu m kuwa msanii ajue kuzitumia vizuri nyakati hizo.
Msimulizi wa hadithi anatakiwa kimsingi kuzingatia mantiki ya hadithi yake anayoisimulia. Mtiririko wa matukio ni muhimu ufuatane.
Katika kujenga mtiririko wa vituko, mwandishi anaweza kuweka hadithi ndani ya hadithi, barua, nyimbo na mashairi na kadhalika. Au hadithi yaweza kuwa mwisho-mwanzo, mwanzo-mwisho, mwisho-kilele, kilele-mwisho n.k. Masimulizi kimsingi hutawaliwa ua mazingira ya tukio linalosimuliwa, mwendo wa tukio (movement), wakati wa kutendeka tukio (time) na maana ya tukio (meaning).
Kuhoji
Hii ni mbinu ambayo kwayo mwandishi hujenga nyadala wake kwa kutumia hoja maalumu kuonyesha imani na msimamo alionao juu ya masuala kadhaa. Katika kufanya hivyo, mwandishi husimama upande mmoja. Au hutokea pia mwandishi husimama katikati, asijipambanue ua upande wowote ule.
Kazi za aina hii hutofautiana ikiwa mwandishi atajishirikisha upande mmoja.
Katika kuhoji, mwandishi atatumia lugha ya kumfanya msomaji aafiki mawazo ya msanii/mwandishi. Ni muhimu kwa mwandishi kuwa mchaguzi wa maneno vyema ili kuipa nguvu kazi yake, Mfano wa andiko la kuhoji ni hili lifuatalo; kutoka Ufakamu wa Lugha ya Kiswahili.
Zamani watoto wetu walisoma kipepepe wakavalishwa kipepepe, wakaiga mambo yote ya kipepepe kusoma, kula, mavazi, mila na hata tabia... Kwa hiyo, kale ikawa imepita na mambo yake. Tatizo likaletwa kwa kuwa watu wa vizazi hivi viwili - yaani watoto waliozaliwa wakati wa utawala wa mkoloni na dahari yetu tulipozaliwa; lazima kukaa pamoja...29
Mbinu hizi zikitumiwa, kazi ya kisanaa huimarishwa na kuwa bora zaidi.
Kuna mbmu mbili zaidi zitumikazo katika kusimulia ua kuelezea jambo. Mbinu hizi ni za matumizi ya monologia na matumizi ya dialogia.
Mbinu za Kimonologia
Monologia ni masimulizi yanayofanywa na mhusika mmoja katika hadithi au kazi nyingine za kisanaa.
Katika mbinu hii, hadithi, inajitokeza kama inasimuliwa na mhusika aliye hadithini. Mwandishi anaonekana kuwa hayuko. Pia hadithi inaweza kujitokeza ikisimuliwa katika nyakati mbalimbali.
Wakati mwmgine, mwandishi anaweza kujitokeza mara chache chache ili kumfafanua mhusika anayesimulia hadithi hiyo ya kimonologia. Angalia mfano huu ufuatao:
AFRIKA
Niko nikiishi kwa matumaini ya kuona siku moja Afrika iko huru. Siku hiyo, nitafurahia kuuona uhuru wa Afrika! Siktt hiyo, siku ambayo Afrika yote itakuwa huru, nitaimba nyimbo za kufurahia uhuru kwa shangwe ua vingorimbo! Nitacheza ngoma zetu! Siku hiyo ni taimba nyimbo kwa Lugha zetu zote za Afrika! Nitaamuru Mandela ua wenzake watolewe kifungoni Robben (kisiwam) ili waje waungane ua familia zao ambazo wametengana nazo kwa siku nyingi. Pia, nitamwomba Mungu huku kunakosemekana kupo awafufue machujaa wa Afrika walioanzisha vita vya ukombozi ili waje wafurahie uhuru wao walioupigania hata wakafa. Nitataka Mkwawa afufuliwe! Nitataka. pia Chabruma, Makita, Mputa, Songea wafufuliwe... Nitataka Kinjeketile, Isike, Milambo, Ng'wanamalundi, na wengine wafufuliwe!! Wakisha fufuliwa, nitaomba waniamuru niwasomee risala yangu. Nami nitai soma: Mababu zetu. Tunayo furaha kuwa pamoja, nanyi. Kazi mliyotuachia tumeimaliza. Tutalinda uhuru wetu! Mababu hawa watanipongeza na kusema... Wanetu wa Afrika, kumbukeni kuishi katika umoja unaounganishwa ua damu yetu. Lakini hili ni jambo kubwa! Epukeni kuuana wenyewe kwa wenyewe kama wanyma mwitu. Tunaahidi kuja kusherehekea siku ya MUUNGANO WA AFRIKA." Nitashukuru.30
Katika kifungu hiki kumekuwa na mbinu ya Kimonologia ikiwa na ufafanuzi uliotolewa pale awali. Aidha, uandishi wake hapa umekuwa u wa kawaida sana, hasa kwa vile umetumia wakati uliopita kidogo ua sehemu kubwa ni wakati unaokuja. Uandishi wa aina hii si wa kawaida sana katika hadithi za Kiswahili. Mpaka sasa (1990), ni hadithi moja tu katika Kiswahili imetumia maelezo yake kwa kuzingatia wakati unaokuja. Hadithi hiyo imeandikwa na J.R.R. Mkabara na inaitwa Mbio za Kipofv.31 Ni muhimu pia kusema hapa kuwa Monologia hutumia nyakati mbalimbali kama vile, muda uliopita, muda uliopo, na muda unaokuja.
Mbinu za Kidialogia
Dialogia ni mazungumzo ya watu wawili au zaidi yanayowakilishwa kimaan-dishi katika kazi za sanaa zitumiazo lugha, hususan, hadithi fupi. Kwa kawaida, dialogia haitumiki katika kazi za kitaaluma kama vile Fizikia, Hisabati, Jiografia, Historia n.k. Taangalie mfano ufuatao unaoonyesha matumizi ya dialogia ulioandikwa na E. Kezilahabi.
Rosa alijipaka mafuta Iddogo. Baada ya muda mfupi taa ilizimishwa. Giza liliingia. Rosa alikaa juu ya kitanda. Thomas alisikia kitanda idnalia. Rosa alikuwa Jdtandani. Thomas, akiwa na shauku kubwa alimtu-pia mkono. Aliona kwamba Rosa hakuwa na nguo hata moja. Thomas alimvuta ili amsogeze karibu. Mara moja mkono wake ulishikwa ua kurudishwa kwa nguvu.
"Si kawaida yangu," Rosa alisema
"Kwa nini?"
"Huwa sipendi. Si leo siku ya kwanza."
"Sasa!"
"Tuzungumze tu."
"Mpaka lini?"
"Mpaka mimi nipende.''
"Utapenda lini?"
"Vumilia kidogo."
"Haiwezekani."
"Kwa nini huwezi?"
"Mwenzio sijiwezi. Lakini kwa nini hupendi?"
"Hali yangu hainiruhusu."
"Hali gani?"
"Mimi mwanafunzi wako."
"Sahau uanafunzi."
Thomas alimtupia mkono tena. Rosa aliurudisha.
"Basi mimi nakwenda kulala kitanda kingine."32
Katika mfano huu, maelezo machache yanatangulia dialogia kali inayofanywa na watu wawili, Rosa Mistika na Mwalimu Thomas, Mkuu wa Shule aliyokuwa akisoma Rosa Mistika.
Dialogia inavyotumiwa na waandishi wengi ina kazi mbalimbali muhimu za kisanaa katika hadithi. C.H. Holman anazitaja kazi hizo kuwa ni:
a
-
Kusaidia kuyasukumia matukio upande ule ambao mwandishi ameukusudia. Mbinu hii hutumika pia kama pambo la hadithi kisanaa.



b
-
Dialogia inazingatia tabia, hali, uhusika na ujumla wa ujenzi wa mhusika katika hadithi fupi (na hadithi kwa ujumla). Kama mhusika anaanza ua tabia fulani, ataonyeshwa na tabia hiyo, labda kama mwandishi anaibadilisha tabia kwa makusudi maalumu ya kutaka kupata athari fulani. Wahusika hao watahusiana na pia kuonyesha tofauti kati yao, wataonye-sha tofauti ya kitabia, kitaifa, kitabaka, kila mhusika ataionyesha rejesta au lahaja yake, kazi yake na uwezo alionao.



c
-
Dialogia hujaribu kuiga hali halisi ya maisha kimazungumzo kama ilivyo katika jamii.



d
-
Dialogia huonyesha uhusiano mkubwa wa kimawazo uliopo kati ya watu wanaozungumza au kujibizana katika hadithi huku wakitoa dhamira na maudhui muhimu yaliyokusudiwa na jamii.



e
-
Dialogia kati ya watu wawili au zaidi hujengwa na mwandishi ili waweze kutofautiana kimaumbile na ki-mazungumzo. Mwandishi huwaonyesha wahusika hao kwa kuzingatia utabaka wao. Mambo kama maneno, ridhimu na mwendo wa sentensi na matamshi pia yanatofautiana.



f
-
Kwa wasomaji wa hadithi, mbinu hii husaidia kupunguza uchovu wakati wa kuisoma hadithi.
Mbinu hii ya kidialogia inachanganya nyakati kama tulivyoona katika Monologia. Aidha, mbinu hizi zote hutumiwa na mwandishi akihoji, aki-fafanua au akijadili masuala mbalimbali katika jamii.
Msuko au Muundo wa Matukio Katika Hadithi Fupi
Muundo au msuko wa matukio ni kipengele kingine muhimu katika kuiangalia fani ya hadithi fupi za Kiswahili. Wanataaluma, baadhi yao, walioelezea maana ya muundo wamekubaliana kuwa msuko nijumla ya mpangilio, uteuzi na uelezeaji wa vipengele mbalimbali vya matukio katika kazi ya kubuni ya sanaa, hususan hadithi fupi. Muundo huipa kazi ya sanaa fani na umoja wa kimantiki, kama anavyosema Walter Blair33 na wenzake. Wakati mwingine, vitu kama lugha itumikayo, utanzu utumikao, aina ya sentensi, huelezwa kama violezo vya kimuundo. Mfuatano au mtiririko wa vituko vinavyojenga mgogoro katika hadithi unatakiwa uunde mantiki na mafundisho kwa jamii.
Aidha, wakati wakiangalia hadithi kwa ujumla, Penina Muhando na Ndyanao Balisidya34 wameijadili misuko ya hadithi ndefu na kuitaja kuwa ni Msuko wa Kioo, Msuko wa Msago (Msuko wa moja kwa moja), n.k. Japokuwa misuko au miundo hii imetajwa kuwa ni ya riwaya, kwa upande mwingine inatumiwa na hadithi fupi pia. Tofauti muhimu kimatumizi ipo katika upana wa mawanda. Misuko katika hadithi fupi inaambaa katika mawanda yasiyo mapana, na kwa hiyo huifanya hadithi isiwe na uwanja mpana wa kuelezea vituko na vitukio vyake. Tuangalie misuko hiyo ya hadithi kwa undani kidogo.
Msuko wa Msago
Katika aina hii ya msuko, matukio yanasimuliwa na kuonyeshwa kuwa yanafuatana na kuhusiana kimantiki kutoka mwanzo hadi mwisho. Matukio hayo yanakwenda sambamba na wakati. Kila tukio katika msuko au muundo huu linafanyika mahala pake na kwa wakati wake. Angalia Kielelezo Na. 3.

Kieldezo 3: Msuko wa Msago
Katika kielelezo hiki, hadithi inaanzia penye A. Wakati unaonyesha baada ya saa moja. Hadithi inaendelea ua kufikia upeo B wakati muda unaonyesha saa sita. Kisha hadithi maendelea na kufikia mwisho penye C wakati muda unaonyesha saa kumi na mbili.
Msuko wa Kioo
Katika msuko huu, matukio yanasimuliwa kutoka mwanzo kwa kutumia kanuni na taratibu za miundo mingine kama vile Msuko Msago, Mwanzo-Kati, Kati-Mwisho, Mwisho-Mwanso, n.k. Katika usimulizi wake, msuko huu husimulia matukio kwa kurudia jambo lililowisha kuelezwamwanzo. Ni matukio ya kudakiyana. Baadhi ya wanataaluma, kama vile F.E.M.K.Senkoro,35wameutaja msuko huu kawa unatumia mbinu za viona nyuma na viona mbele. Wengine kama vile F.V. Nkwera36 wanauelezea msuko huu kuwa ni wa rukia Angalia Kielelezo Na. 4.

Kielelezo 4: Msuko wa Kioo
Hadithi inaanza penye A. Matukio yake yanasimuliwa kwa kudakiyana kupitia B hadi mwisho C. Ukichunguza kwa makini utaona muda wa matukio hauoam vyema ua mwendo wa matukio kama ilivyo katika Msuko Msago. Msuko huu umechangamana.
Msuko Mwisho-Kati-Mwanzo
Msuko huu huanza na matukio ambayo m ya kumalisia hadithi, au yale ambayo yangepaswa yawe mbele zaidi mwa hadithi.
Msanii akisha yaeleza matukio hayo yaliyotakiwa yawe mwisho mwanzoni, halafu huelezwa matukio ya katikati, hatimaye huelezwa yale ambayo yangepaswa yawe mwaazoni. Wakati mwingme mwandishi huelezea. matukio yanayomalizia hadithi kama mwanzo, baada ya kuendelea na hadithi huelezwa baadaye kidogo. Kisha hadithi hiyo huendelezwa na ifikapo nwisho, inarudia tena kueleza yale matukio yaliyoelezwa mwanzo. Baadhi ya wataalamu wameuita msuko huo kisengerenyuma37 Tazama Kielelezo Na. 5.
Mfano wa hadithi kama hu ni ile ya Mzimu wa Watu wa Kale38 ily otungwa na M.S. Abdulla.
Msuko Mwanzo-Kipeo
Mwandishi maweza kuandika hadithi asifikie mwisho, bali kileleni. Hadithi kama hii kwa kawaida hutumia taratibu za msuko wa kawaida, yaani msuko wa msago ama wa moja kwa moja. Mwandishi huionyesha hadithi yake ikikua huku mhusika wake mkuu akionyesha mambo na matendo muhimu yanayozidi kuijenga dhamira muhimu aliyoikusudia. Mara hadithi ikifikia kileleni inakatishwa ghafla ua kumwacha msomaji katika taharuki kali. Tazama Kielelezo Na. 6(a) kwa ufafanuzi.

Kielelezo 5: Msuko Mwisho-Kati-Mwanzo
Katika hali ya kawaida sehemu BC ilipaswa isimuliwe, lakini katika hadithi hii inaonyesha haikusimuliwa. Badala yake iko sehemu AB tu!
Aidha, badala ya kuanza mwanzo kama ilivyoonyeshwa katika Kielelezo Na. 6(b) hadithi yaweza kuanza na kilele hadi kufikia mwisho.
Katika kielelezo hiki sehemu AB ilipaswa iwe imesimuliwa kabla ya BC. Sehemu BC imeanza na kipeo B, na halafu hadithi husimuliwa hadi mwisho.
Tunaweza kuhitimisha sehemu hii inayohusu misuko ya hadithi kwa kusema kuwa kimsingi, mwandishi anaweza kuwa na mpango wa msuko wa hadithi yake ambao atautumia katika kuelezea mwendo au maendeleo ya matukio katika hadithi nzima. Aidha, msuko wa mwandishi unaweza usitumie kila tukio analolifanya mhusika wa hadithi anayokusudia kuielezea kama inavyoonyeshwa katika Kielelezo Na. 7.
Matumizi ya Mashairi na Nyimbo
Katika kuimarisha kazi ya fasihi mwandishi anaweza pia kutumia nyimbo ama mashairi katika hadithi fupi. Jambo hili linasaidia katika kujenga fani ya aina fulani na kutoa ufafanuzi zaidi wa maudhui. Kwa upande mwingine hilo huingilia utaratibu wa msuko wa hadithi ambao hujikuta umetengeneza vifungu mbalimbali vinavyofanana na vidato katika hadithi nyingine.

Kielelezo (6a: Msuko Mwanzo-Kipeo)

Kielelezo 6b: Msuko Kipeo-Mwisho
Kilele na Mpomoko katika Hadithi fupi
Kilele katika hadithi ni mabali ambapo panaonyesha mabadiliko katika mkondo mzima wa hadithi. Ni mahala ambapo mkwezo wa mawazo yanayosimuliwa katika hadithi hufikiwa kilele. Kwa mfano katika hadithi fulani-labda ya kukata mkonge kulikuwa na tatizo ama mgogoro juu ya vijana kukimbia kufanya kazi ya kukata mkonge, sasa hawakimbii tena kwa sababu labda wamepewa vivutio. Au katika hadithi ya mapenzi, kama kulikuwa na watu wawili: msichana na mvulana waaataka kuoana, pale wanapokubaliana kuoana patakuwa ni kipeo au kilele.

Kielelezo 7: Uteuzi wa Matukio katika Uandishi wa Hadithi
Wakati mwingine huwa si suala la mgogoro kuchukua upande wa pili, bali kipeo paweza kuwa mahali popote ambapo migogoro ya kazi ya sanaa ya kifasihi inayohusika inaonyesha maana kamili. Kwa hiyo kilele kinaweza kiwe mwanzoni niwa hadithi - hasa katika msuko wa hadithi wa kioo - au kinaweza kuwa katikati ya hadithi au hata mwishoni mwa hadithi. Kwa ujumla hii itategemea na mawazo ya msanii mwenyewe.
Kimsingi, kilele wengine huita kipeo na ni vitu vinavyohusiana katika hadithi. Kuna aina mbili ya vilele: kilele chajuu ua kilele cha chini. Tumetaja na kujadili kilele cha juu hapo awali. Tuone kilele cha chini ni nini? Kilele cha chini kinaonyesha tabia iliyo tofauti au iliyo kinyume na ile ya kilele cha juu. Kilele hiki ni mashuko ya mawazo, mahali ambapojambo au wazo hulegezwa mkazo wake wa kusisitizwa. Kilele cha chini hujitokeza wakati ambao msanii anaijenga kazi ya kifasihi na kuleta hisia iliyo kinyume na matazamio ya wengi. Msamiati wa Muda wa Fasihi ya Kiswahili39 unatoa mfano wa mhusika Kmjeketile wakati anapokabiliana na wakinzani wake, anakusanya wananchi wake ili wapigane na maadui hao. Lakini kinyume na matarajio ya wasomaji, Kinjeketile anakataa kwenda vitani. Mahali hapa ndipo panaonyesha kileie cha chini, ambacho istilahi yake iliyotolewa na BAKITA * ni mpomoko.
* BAKITA = Baraza la Kiswahili la Taifa
Vilele katika kazi za sanaa za kifasihi huundwa na wasanii kwa madhumuni mbalimbali, na kuweko kwa vilele hivi kumezua mawazo tofauti kwa wanafasihi. C.H. Holman40 kwa mfano anasema kuwa katika baadhi ya kazi za fasihi vilele vya chini huwa ni udhaifu wa kazi zao. Lakini katika kazi nyingine za kisanaa, hususan hadithi fupi za Kiswahili, kilele cha chini kimekusudiwa hivyo na msanii ili kuleta athari iliyokusudiwa naye. Hali hii ya pili hutokea katika hadithi fupi ambapo kipeo au kilele cha chini hutumiwa kuwa mbinu ya kuipa hadhira mshangao mkubwa, yaani taharuki. Sifa hii ya kitaharuki ni muhimu sana katika kazi ya sanaa ya kifasihi, ua hasa hadithi fupi.
Suala la Migogoro
Hadithi yoyote ile lazima iwe na migogoro. Migogoro katika hadithi husaidia kujenga aina mbalimbali ya misuko ya hadithi. Migogoro ni nini hasa? Migogoro ni mivutano ama mikinzano katika kazi za fasihi. Mgogoro unaweza kutokea ua kukuzwa na uhusiano uliopo kati ya mawazo mbalimbali na matendo mbalimbali. Mgogoro pia unaweza kuwa baina ya wahusika wawili, au unaweza uwe kati ya mhusika na mazingira yake au kati ya wazo na wazo41 Yote hiyo ni migogoro inayoweza kuwa katika kazi ya sanaa ya kifasihi.
Mgogoro katika kazi ya fasihi ni muhimu kwa sababu ndio unaojenga mvu-tano baina ya wahusika na kujenga maudhui yanayohitajika.
Migogoro inayojitokeza katika kazi ya fasihi inaweza kuwa katika mafungu makuu matatu. Migogoro hiyo ni ya kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa. Migogoro hiyo ikiangaliwa kwa undani inatokana ua utawalaji wa nyenzo za uzalishaji mali katika jamii. Kwa mfano kama kuna wale walionacho hawawajali wasionacho, wasionacho wataamua kudai haki yao kwa nguvu, na hivyo kuunda mgogoro wa kiuchumi.
Mgogoro mwingine ni ule wa kisiasa. Katika aina hii ya mgogora mtu anaweza kuwa hakubaliani ua siasa ya nchi yake na mwandishi wa kifasihi anamwonyesha kama mpinzani. Mgongano huu unaweza kuonyeshwa kama kitu kidogo kinachoenea kwa watu wengine kutokana na uwezo wa kipropaganda anaoweza kuonyesha na labda kuwa nao mtu huyo.
Mkondo mwmgine wa migogoro un akuwa katika kundi la utamaduni. Huko tunakuta migogoro kama ile ya mapenzi ndoa; Jini ua imani malezi na tabia nyinginezo.
Tukiondoa migoro hiyo tuliyoitaja na kuizungumzia hapo juu, kuna mgogoro mwingine muhimu ambao tunafikiri ni bora kuutaja hapa. Huu ni mgogoro wa mtu binafsi. Wakat: wote mhusika akiwa katika jamii anaonekana kuzongwa na hali mbili: kutenda au kutotenda. Hali hii itamjengea mivutano mbalimbali kila pale atakapokutana na mazingira fulani katika maisha yake. Kwa kuzingatia hilo, mwandishi wa hadithi fupi anatakiwa kuwajenga wahusika wake kwa kuzingatia pia aina hii ya migogoro.
Mianzo, Kiwiliwili, na Miisho ya Hadithi ya Hadithi Fupi
Tumesema msuko wa hadithi fupi umegawanyika katika sehemu kuu tatu, yaani nawanzo, kati, na mwisho. Lakini tulitoa tahadhari kuwa si kila hadithi fupi hufuata utaratibu huo kwa sasa kutokana ua mabadiliko kadhaa ya kisanaa yaliyokwisha tokea katika fasihi. Kama tulivyokwisha dokeza, ziko hadithi zinaweza kuanza ua mwisho, ukafuata mwanzo, na kumalizia na sehemu nyinginezo. Aidha, bado kuna hadithi zile zenye kuzingatia utaratibu wa mianzo ileile ya awali iliyosemwa na wakongwe wa Kiyunani akina Plato na Aristotle. Katika sehemu hii hatutaingilia mjadala juu ya mianzo hiyo, lakini tutataja vipengele hivyo vya mianzo katika hadithi fupi kama vilivyo kwa sasa, kwa kuzingatia kuwa zina asili ya kimapokeo ama ni za kisasa.
Mianzo
Tutaigawa mianzo ya hadithi fupi katika mafungu mawili ya msingi. Mgawanyo huu umefanywa kwa kuzingatia mikondo ya hadithi hizo fupi zi nazoandikwa kwa Kiswahili ua ni za Kiswahili. Mianzo hiyo ni (a) ile inayotokana na mkondo wa hadithi za Kiswahili za simulizi, hadithi za kingano (b) mianzo ile inayotokana na mkondo wa hadithi za kubuni za kisasa.
Mianzo ya Hadithi za Simulizi
Hadithi za namna hii zina mianzo ya aina tatu inayofanana. Aidha, ziko tofauti ndogo kati ya mwanzo mmoja na mwingine. Mianzo hiyo hutanguliwa na kifungu cha maneno maalumu, ambacho kimsingi hutamkwa na kiongozi kama hadithi inatambwa, au inaweza ikasomwa tu katika hali ya kawaida kama inasomwa na mtu yeyote yule. Baada ya kumaliza utangulizi huo, kiwiliwili cha hadithi ndicho kinachofuata. Mfano wa mwanzo wa aina ya kwanza ni kama ufuatao:
Paukwa! (Kiongozi)
Pakawa! (Hadhira)
Paukwa! ... ...
Pakawa! ... ...
Baada ya kumaliza utangulizi huo, masimulizi ya hadithi nzima yanafuata. Kwa kawaida huanza ua: 'Hapo zamani za kale... Kuliondokea mtu ua mkewe... Siku moja Chura na Ng'ombe... Paliondokea..." na kadhalika.
Mwanzo wa aina ya pili ni kama ufuatao:
Hadithi, hadithi! (Kiongozi)
Hadithi njoo! (Hadhira)
Hadithi, hadithi! ... ...
Hadithi njoo! ... ... ...
Baada ya kitangulizi hicho, masimulizi hufuata kama ilivyoelezwa hapa juu kaitka kifungu cha kwanza.
Mwanzo wa aina ya tatu ni kama ufuatao:
Atokeani! (Kiongozi)
Naam Twaib! (Hadhira)
Kaondokea Chenjagaa
Kajenga nyumba kakaa
Mwanangu Mwanasiti
Kijino kama Chikichi
Cha kujengea kijumba
Na vilango vya kupitia...
Katika kifungu hiki kiongozi huanzisha kwa kusema: Kaondokea Chenjagaa na hadhira huungana naye na kusema kifungu hiki kilichosalia. Wakishamaliza kifungu hiki ndipo hadithi iliyokusudiwa husimuliwa. Wakati mwingine mianzo hiyo inaweza kuwa katika mfumo wa kishairi kama inavy-oonyeshwa katika mfano huu ufuatao, ambao umechukuliwa kutoka katika gazeti la Mambo Leo42
KAKA SUNGURA
NA NAMNA ALIVYOPATA NYAMA
Masbairi ya kukaribisha:
Njoo tusimulie jamani
Hadithi zile za zamani
Njooni tukakaa rahani
Kuzunguka moto
Hadithi zile za Mzee Ndovu
Hadithi kuondoa ucovu
Hadithi kututilia nguvu
Kuzunguka moto
Mzee Simba, Kaka Fisi
Mjanja kweli ya halisi
Kila jambo kudadisi
Hadithi tamu zile
Na Mzee Kobe, Catu, Nyota
Kutaja wote nitacoka
Sungura wote' kawapoka
Kwa zamani zile
Na Sungura yu mwerevu
Akili zake kweli mpevu
Kaka huyo mcekevu
Hadithi tamu zile
Basi tukakusanyika
Tutafurahia hakika
Mambo yalihadithika
Kwa zamani zile.
IKATOKEA siku moja ya kuwa wanyama wote wakafanya shauri la kujenga nyumba kubwa wapate kukaa humo salama. Kila mmoja alifanya bidii nyingi sana lakini Sungura (Kaka) alisema moyoni kama kupanda ngazi mara kwa mara hucosha sana, basi yeye akashughulika shughulika tu anakwenda huko na kupima, na kurudi huko na kupima, lakini hafanyi kitu kabisa na kila mara kama wengine wanafanya kazi zao, yeye alikwenda kulala tu. Basi nyumba ilikwisha na Kaka Sungura alicagua cumba kimoja katika ghorofa juu kabisa. Akafanya werevu na walipotoka wote kutembea yeye akacukua bunduki na mzinga, na pipa kubwa la maji macafu, akayaweka cumbani mwake juu.
Wanyama wakarudi na Kaka Sungura akaenda cini akakaa pamoja nao wakaongea mpaka Kaka Sungura akasema kama amecoka akapanda juu cumbani mwake. Basi alipofika juu akatoa kicwa dirishani akawaambia wale cini. "Je! ninyi, kama mtu mkubwa kama mimi anataka kukaa atakaa wapi?" Wale wengine uaceka wakaceka sana wakajibu. Kama mtu mkubwa sana kama wewe hawezi kukaa kitini basi afadhali akae cini." Kaka Sungura akajibu: "Vema, ninyi cini angalia nitakaa sasa." Basi akaishika bunduki akaipiga.
Wanyama wale wakashangaa sana, wakasikiliza, wakasikiliza, mpaka wakaanza kuzungumza tena. Halafu Kaka Sungura akatoa kicwa dirishani tena akasema. "Je! kama mtu mkubwa kama mimi anataka kupiga cafya atapiga cafya wapi?" Na wale wanyama wakajibu, "Kama mtu mkubwa kama wewe hana wazimu, atapiga cafya apendapo. Kaka Sungura akajibu. "Vema angalieni ninyi cini! nataka kupiga cafya sasa." Akapiga mzinga wake.
Looo, kila kitu kilistuka sana na wanyama wale Cini wakashangaa. Halafu kidogo wakasahau wakaanza kuongea tena, mara Kaka Sungura akatoa kicwa tena akasema, "Haya ninyi cini huko, kama mtu mkubwa kama mimi akitafuna tumbako yake ua akitaka kutema mate atatema wapi?"
Basi sasa wanyama wale cini wakakasirika kwa ucungu.
"Kama mtu mkubwa, kama mtu mdogo, tema mate upendapo."
Kaka Sungura akajibu. "Vema, hii ndiyo namna anavyotema mate mkubwa." Mara akamwaga maji yale rnacafu katika pipa lake yakashuka yakamwagika katika ngazi na katika vyumba cini na wanyama wale wote wakatoka mbio sana.
Basi Kaka Sungura akafunga mlango, akafunga madirisha yote akalala usingizi. Wale wanyama wengine waliojenga nyumba hawakurudi tena, wakamwacilia Kaka Sungura na nyumba yake.43
Maelezo juu ya mianzo ya hadithi za simulizi yanaonyesha ukweli kuwa katika hali ya kawaida hadithi hizi hutegemea sana masimulizi ya mdomo, kusikia kwa masikio, kuona vitendo vinavyofanyika ua uhusiano kati ya mtambaji/msimuliaji ua hadhira ili kukamilisha uhusiano wa kimaudhui uliokusudiwa kutolewa. Ufanisi wa hadithi unategemea uwezo wa mtambaji katika hadithi hizo za simulizi. Kwa hiyo, hadithi hizo zinapoandikwa zinakosa mambo muhimu kisanaa yaliyokuwa yakipatikana wakati wa masimulizi. Hali hii huifanya hadithi nzima kuonekana kuwa chapwa.
Mianzo ya Hadithi za Kubuni
Baada ya kuangalia mianzo ya "ngano" sasa tuangalie mianzo ya hadithi fupi za kisasa.
(1) Jina la Hadithi: WASUBIRI KIFO
Mwandishi: E. Kezilahabi
Kutoka: Uandishi wa Tanzania (J.P. Mbonde - Mhariri)
Kijiji cha Mkalala - kijiji ambacho kwa muda mrefu kilikuwa hakijapewa nafasi ya kuingia katika mashindano ya maendeleo - kilikuwa hakijulikani. Yamkini utafikiri hakikuwa katika ramani ya Mkurugenzi wa Wilaya - ramani ambayo ilikuwa...44
(2) Jina la Hadithi: NDUMILA KUWILI
Mwandishi: J. Rutayisingwa
Kutoka: Gazeti la Mzalendo (Gazeti la Chama)
Ali Gihaza alikuwa chumbani kwake akisoma kitabu wakati mtu alipobisha hodi mlangoni na kuuliza. "Wenyewe humu ndani mpo?" Gihaza alishtuka na kuweka kitabu mezani, akaitikia huku akiwa amekunja uso kwa fikra, "Tumo, karibu mpaka ndani."45
Mianzo hii miwili imeonyesha tofauti zilizoko kati ya hadithi za kingano na hizi za kisasa. Mianzo ya hadithi za kisasa inabadilika kufuatana na lengo la mwandishi na dhamira yake.
Kiwiliwili au Katikati
Mara baada ya mianzo hiyo, kinachofuata ni kiini cha hadithi nzima. Kwa mfano tukiangalia hadithi ya "Kaka Sungura ua Namna Alivyopata Nyama,'' mwanzo unajionyesha waziwazi, katikati napo pameonyeshwa na mwisho unaweza kutambuliwa kirahisi tu'. Ni muhimu kusisitiza hapa kuwa hadithi za asili za simulizi hazibebi sanaa kama ile ya kimasimulizi kutokana na ukweli kuwa mambo mengi yanayofanywa na watendaji hai hayawezi kufanywa kwa maandishi. Hili, tutalirejea tena hapo baadaye.
Miisho
Kama ilivyo katika mianzo, miisho ya hadithi fupi za Kiswahili nayo tunaweza kuigawa katika makundi mawili - ya simulizi na ya kisasa.
Miisho ya simulizi husisitiza raha ama kutoa taarifa ya maisha ya wahusika walioijenga hadithi. Kwa mfano:
a - Hapo ndipo wakaishi raha mustarehe
b - Hapo ndipo hadithi yangu inaishia
c - Huu ndio mwisho wa hadithi yenyewe
Miisho ya aina ya pili, ile ya hadithi fupi za kisasa ni tofauti kimsingi na hii ya hadithi za kimapokeo. Hata hivyo wakati mwingine athari za hadithi hizo za kimapokeo katika hadithi za kisasa inajitokeza sana. Mifano ya miisho ya hadithi za kisasa imetolewa hapa chini.
(1) Jina la Hadithi: WASUBIRI KIFO
Mwandishi: E. Kezilahabi
Kutoka: Uandishi wa Tanzania (J.P. Mbonde - Mhariri)
Walipotoka huko kilimani, mahali ambapo mifupa ya baba zao ilikuwa ikizikwa - walianza kufurukuta na kutafuta mayai ya utajiri, wakasahau kwamba katika kila jiwe la msingi wa majumba hayo kulikuwa kumelala mifupa ya baba zao maskini. Kwa hiyo wakawa watu wa maneno mengi na nadharia zisizokuwa ua mkia wala kichwa!46
(2) Jina la Hadithi: NDUMILA KUWILI
Mwandishi: J. Rutayisingwa
Gazeti la Mzalendo (Gazeti la Chama)
Kwamba nilimchukulia rafiki na papo hapo akawa rafiki wa mke wangu si jambo ambalo limetokea kwangu tu. Hutokea kwa wengi. Mimi namuombea apone ua nimemsamehe dhambi zake zote. Hatua yoyote ninayoweza kuchukua haiwezi kumfufua Sakina.47
Hii ni miisho ya hadithi fupi za kisasa. Kwa ujumla kuna athari tuliyoisema ya kimapokeo inajitokeza kwa kiasi fulani katika miisho hiyo. Aidha, bado kuna miisho ambayo haina athari za kimapokeo.
Tunaweza kuhitimisha sasa kwa kusema kifupi kuwa hadithi fupi za kisasa zina msingi wa kubuniwa. Mtu anayebuni na kuandika hadithi za aina hii anajulikana, na kwa hiyo kazi hiyo ya sanaa huwa ni mali yake.
Ngano kwa upande mwingine ni kazi ya sanaa yenye misingi yake katika mapokeo. Kwa muda mrefu ngano zimekuwa zikisimuliwa, na hivyo, kuhifadhiwa kichwani. Ingawa kwa sasa ngano huhifadhiwa kimaandishi, bado kuna mambo ya msingi ya kimasimulizi yanajitokeza katika hadithi hizo. Hadithi hizo zikichunguzwa zinafuata mikondo (pattern) katika usimulizi wake.
V. Propp48 anazigawa ngano kwa kuzingatia kazi ambazo hufanywa na wahusika waliomo katika ngano mbalimbali. Katika kusisitiza mikondo hiyo, Propp anasema kuwa:
· Katika ngano mhusika anatazamwa anafanya nini katika matukio yote
· Kimsingi, kazi za wahusika katika ngano ya aina fulani itabaki kuwa ileile hata kama anapewa jina jingine.
· Mfululizo wa matendo katika ngano za aina fulani unafanana
· Hata kama ngano huwa ua miundo tofauti, kimsingi zote ni za aina moja kwani zina lengo na tabia zinazofanana.
Baadhi ya wataalamu huzigawa ngano kwa kufuata dhamira. S. Kichamu Akivaga na A. Bole Odaga49 wamezingatia utaratibu wa aina hii. Kufuatana nao, kuna hadithi za ngano za visasili, hekaya, ishara, kharafa, viada na kadhalika. Mgawanyo huu unaelekea kukubalika na wataalamu wengi, wakiwemo F. Senkoro,50 Ndyanao Balisidya na Penina Muhando,51 na J. Berg Esenwein.52 Kwa vile kazi hizi ni za kimapokeo, hakuna mwenye haki nazo, isipokuwa jamii nzima.
Hadithi fupi za kisasa, zikilinganishwa na ngano, ni ndefu kidogo. Hii inatokana na mambo yanayoandikwa hadithini humo. Mambo hayo ni pamoja na kuwa na msuko ama muundo wa mtiririko wa matukio katika usimulizi wake. Masimulizi ya hadithi fupi yanazingatia uhalisia katika misingi ya muda na mahali maalumu.
Ngano husimulia kitu kilichokwisha simuliwa. Fanani anaweza kuongeza au kupunguza kitu katika usimuliaji lakini katika uandishi hawezi kufanya hivyo bila kupoteza uasili wa ngano inayohusika. Muda wake hauna mpaka (infinite past), hakuna uumbi mpana wa wahusika wake ua kadhalika.
Uzuri wa hadithi fupi unategemea uwezo wa msanii. Kama msanii ni mtaalamu na ana nyenzo zote za lugha, anaweza kutunga hadithi nzuri. Kinyume cha hapo, ataharibu. Ngano zinategemea hasa uwezo wa fanani wa kusimulia matukio ya hadithi.
Hadithi Fupi za Kibarua
Suala la mianzo, katikati na mwisho katika aina hii ya hadithi halina uzito sana, kwani hadithi nzima huwa, inachukua muundo wa barua za kawaida. Mwanzo huwa ni salaam na maamkizi, halafu huja maelezo yake, na humalizia na mwisho. Barua ina misingi yake.
Hadithi fupi za aina hii huwa ni masimulizi yanayohusu barua ziandikwazo na mhusika mmoja au wahusika zaidi. Mwandishi huwatumia wahusika kuelezea hisia na vionjo mbalimbali, lakini vyote vinajengwa na kuunganishwa katika "mkufu" wa dhamira kuu moja au wakati mwingine zaidi.
Kwa mfano, hadithi ya So Long a Letter53 ni nzuri na imepata kushinda Noma Award.
Hadithi za aina hii inasemekana kwanza zilianzia huko Uingereza, ua mwanzilishi wa kwanza wa hadithi hizo ni mtu aliyejulikana kwa jina la Samwel Richardson('s).54 Baada ya hapo, waandishi wengine walifuata kuandika aina hii ya hadithi.
Hadithi za aina hii si nyingi katika Kiswahili. Mwandishi Agoro Anduru amepata kuandika hadithi za aina hii katika gazeti la Mzalendo.55 Mfano mwingine ni ule wa hadithi iitwayo "Barua kutoka Ufaransa" katika kitabu cha Chale za Kikabila.56
Kutokana na ukweli kuwa hadithi hizo ni chache, tumeona iko haja ya kuzihimiza. Katika diwani ya hadithi fupi ya kitabu hiki kuna mfano mmoja wa hadithi iitwayo "Uchungu." Tunategemea mfano huu utawasaidia wanafunzi na wale waandishi wanaokusudia kufanya hivyo.
Mfululizo wa barua hizo unaunda hadithi moja yenye mgogoro wa kimapenzi kati ya Dora Charles (msichana), na Richard m'Banza (mvulana). Mgogoro unaanza na kule kumwona Dora aigizapo mchezo wa Lina Ubani kule shuleni Kilakala. Changamoto ya mapenzi hayo inamfanya Richard m'Banza amweleze Dora nia ua lengo lake, ua kuwa ameshindwa kuvumilia bila kuwa ua Dora. Kinyume na matarajio ya Richard, Dora anapinga matakwa ya ndoa kati yake na Richard. Dora anasisitiza kuwa jambo hili haliwezekani kwa sababu yeye Dora ana mkataba mwingine wa mapenzi na mtu aitwaye Mm. Ni jibu la kusikitisha kwa Richard, na hadithi inaishia katika ushindi wa Dora na kushindwa kwa Richard. Tunaweza kuhitimisha mjadala wetu kwa kusema kuwa licha ya aina hii ya kuandika hadithi fupi za kibarua (ambayo imefafanuliwa zaidi hapa chini katika II) hutokea pia waandishi wengine wakaandika hadithi kwa kutumia aina nyingine za uandishi wa hadithi hizo fupi za kibarua. Aina hizo zimefafanuliwa hapa chini:
I. Hadithi ya Kibarua inayosimuliwa na mtu mmoja:
(i) Katika aina hii ya hadithi ya kibarua, mhusika ama mwandishi mmoja humwandikia mtu mmoja tu. Mfano kama huu uliwahi kuandikwa pia ua Agoro Anduru katika gazeti la Mzalendo (1982).57
(ii) Wakati mwingine mwandishi huandika hadithi ya kibarua kwa watu wawili au zaidi. Katika lugha ya Kiswahili hatujawahi kuwa na mifano ya aina hii ya hadithi.
II. Watu wawili au zaidi kuandikiana:
(i) Katika hadithi nyingine, watu wawili huandikiana barua wakijibizana kama ilivyofanywa katika hadithi ya Uchungu katika kitabu hiki.
(ii) Yawezekana pia watu wengi wanaandikiana barua katika aina nyingine ya barua, na wanaungwa na dhamira zinazotofautiana.
(iii) Wakati mwingine katika aina nyingine ya hadithi fupi za kibarua, mtu mmoja huandikiana na wahusika wengi ambao wote humwandikia yeye majibu.
III. Watu zaidi ya wawili husimulia ama huandika barua lakini hawajibizani:
Aina nyingme ya hadithi fupi ya kibarua ni ile ambayo huwa ua waandishi wengi wa barua hizo, ambao lakini hawajibizani. Aina hii ya masimulizi kwa kweli hufanana na aina ya I na II, bali hutofautiana na hii ya III kwa kipengele kuwa katika aina hii ya hadithi, hakuna kupeana ama kujibizana/kubadilishana mawazo kama zilivyo hadithi za I na II. Hata hivyo, inasisitizwa hapa kuwa kundi III linakaribiana sana na kundi I kuliko na kundi II.
Mandhari ya Hadithi Fupi
Kwa mujibu wa C.H. Holman,58 mandhari au mazingira ya kazi ya sanaa ni hali ya maumbile ilivyo na inavyoonekana. Wakati mwingine, hali ya mizimu na kuzimu kwa ujumla; ni mandhari pia. Mazingira hayo hutumika katika kujenga masimulizi ya riwaya, drama, hadithi fupi na kadhalika. Mambo muhimu yanayounda mandhari au mazingira ya hadithi ni pamoja na (1) mahali palivyo: hali ya milima na mabonde, mpangilio wa vitu katika chumba, milango na kadhalika (2) kazi ua utaratibu wa maisha ya kila siku ya wahusika (3) muda au wakati ambapo tukio linatendeka k.m. kipindi gani cha kihistoria, majira katika mwaka na kadhalika (4) mahusiano ua maisha ya jumla ya wahusika wa kazi ya sanaa, kama vile dini yao, akili na mawazo katika masimulizi ya kazi ya sanaa na kadhalika.
M.H. Abrams59 anaelezea juu ya mazingira ya hadithi au tamthilia kuwa "ni pale yalipowekwa kulingana na mfumo wa kihistoria. Mazingira ya kazi inayosimuliwa yanahusu mahali ambapo matukio yanatendeka."
Kwa upande mwingine, Kamusi ya Kiswahili Sanifu60 inasema kifupi tu kuwa mandhari "ni sura ya mahali, aghalabu ardhi, panavyoonekana."
Tukitathmini maana zote tatu zilizotolewa, maana ya Holman ni pana na imezama kwa undani katika kulifafanua suala zima la maana ya mandhari ama mazingira. Maana nyingine mbili zinazofuatia ile iliyotolewa ua Holman si pana sana. Kwa msingi huo, tutakapojadili dhana ya mazingira tutapenda kukubaliana na Holman zaidi kwa sababu hawa wengine mawazo yao yameisha jumuishwa katika maana yake.
Kwa msanii yeyote yule, mandhari anayoitumia inatakiwa izingatie ile misingi mmne iliyotolewa pale awali. Hadithi inaonekana kuaminika kama ina mismgi hiyo.
Ujenzi mzuri wa mazingira au mandhari una nafasi ya kuleta athari mbalimbali katika hadithi. Tunajaribu kufafanua athari hizo kama ifuatavyo:
(a) Mandhari kama kitu kinachodhibiti maelezo ya matukio katika hadithi fupi.
Maelezo mazuri na ya wazi kuhusu mahali ambapo hadithi inatendeka yanasaidia kuonyesha mwelekeo wa hadithi. Maelezo hayo kwa kawaida huonyesha kwanini mambo fulani huwa yanatokea baadaye katika hadithi hiyo. Angalia mfano ufuatao kwa ufafanuzi.
Katika kutafuta uhuru na furaha, Elena Chiku Ntale aliamua jambo la mwisho kulifanya katika nafsi yake: "Kuhama huko shamba kwenye maisha duni na ovyo na kwenda kula vya wajinga mjini." Alishaona viumbe wa kike na kiume waliowanda juu ya wingu furaha juu ya fedha. Yeye ndivyo alivyo- uona ulimwengu wa jijini. Shamba - mahali ambako hakuna raha - mahali ambako kumejaa sauti za kila aina za ndege mashambani, na mende, panya na mijusi majumbani, huku wakishindana kung'arisha macho kila wakipigwa na mwanga wa taa za vibatari vya wakazi wa huko shamba, wakazi wa mbavu za mbwa!" (Tazama Nyota ya Chiku, sehemu ya Diwani ya Hadithi).
Tukisoma maelezo hayo, tunaona uwiano uliopo wa mandhari na yale yanayotokea ama atakayoweza kuyafanya mhusika katika hadithi hiyo.
(b) Mandhari kama (nguzo) ya msuko na ujenzi wa wahusika wa hadithi fupi.
Wakati mwingine, mazingira ya hadithi fupi yakiwa yameelezwa vizuri yanasaidia kuimarisha msuko wa hadithi pamoja na uumbi mhusika/wahusika wake. Mazingira yakiumbwa ovyo, wahusika ua matukio yote yanaweza kuonekana ovyo. Mfano ufuatao unaonyesha mazingira yanavyoweza kushika-manisha matendo ya mhusika na hadithi yote kwa ujumla.
...Miguu yake ya kuchonga ilibeba kiwiliwili chake cha mwili mwororo bila wasiwasi. Mara pale miguu ilipoishia, kiuno cha ubapa na kinene kidogo kilikuwa kimebeta kwa nyuma. Utadhani cha mbuni, ndege wa fahari katika mbuga za Afrika! Tumbo lake lililokuwa limeteremka kwa chini kidogo halikuwa kubwa! Aidha, lilituna kwa mbele kidogo... Mabega yake ya kadiri yalining'iniza mikono ya mbinu huku katikati ya mabega hayo kukiwa kumehifadhiwa kifua chembamba chenye kubeba titi changa zilizotuna na kuwachungulia vijana wa kila aina - wenye kustahili na wasiostahili. Lakini wote waliziona... Utadhani titi hizo zilikuwa zikiwakonyeza! Na vijana wasivyokuwa na dogo, wakawa wanamtania na kumbeza ana titi chonge kama mdomo wakuku... Ukiwauliza wenyeji wa jiji la Mwanza juu ya msichana huyu wa damu mchanganyiko ya Kimalaba na Kingoni, watakuhadithia mengi..." (Tazama Nyota ya Chiku Sehemu ya pili ya kitabu hiki).
Maelezo hayo yanaonyesha kuwa ujenzi wa mhusika Chiku Ntale umesaidiwa sana na mazingira ya tabia na mahali alipo. Kwa hiyo, tunaweza kukiri hapa kuwa mandhari yanaimarisha ujenzi wa wahusika pia.
(c) Mandhari na uibuaji wa hisia katika hadithi fupi za Kiswahili.
Mwandishi anaweza kuyatengeneza mandhari ambayo yanapohusishwa ua wahusika na matukio yake huibua hisia maalumu kwa msomaji wake. Kwa mfano, katika tamthilia inayoigizwa, jinsi taa zinavyowashwa, jinsi maelezo ya mahali, hali ya nchi inavyoelezwa inaweza kuibua hisia. Tazama mfano wa andiko lifuatalo:
Baada ya mwito wa kuanzisha kijiji cha ujamaa huko Msota, kulitokea mldkimkiki mkubwa. Kukawa huku shoka lakata miti, jembe lang'oa magugu, mitungi na maji, ua mwiko ua kuta za nyumba. Si muda mwingi kijiji kikajengeka. Mawingu ya mvua yalipotuna, watu wakawa mashambani viakishika jemhe, kila siku hadi jua linapomezwa na mawingu. Wakati wa msinu ulipofika, watu wakaandamana sokoni na magunia ya nafaka. Baada ya kukunja noti; wananchi wakakimbilia madukant wakajinunulia mashuka ya Marekani, kanzu za China, na kofia za Japani. Wapenda mambo ya starehe wakanunua radio, asubuhi wakafurahia nyimbo wafunguliapo akina Salum Abdalla au akina MbarakaMwinshehe. Ili mradi kila nyumba ikawa ua furaha."61
Lugha iliyotumika katika masimulizi hayo inajenga mandhari bora pamoja ua kuibua hisia kwa msomaji wake. Mwandishi ametumia lugha fasaha, lugha ya ishara. Matendo yanayoelezwa na kusimuliwa yanawakilishwa vyema katika ishara hizo.
Matumizi ya vifaa katika ujenzi wa mandhari yanatakiwa yawiane ua wakati. Kama masimulizi hayalingani na mazmgira yake, hadithi ama kazi ya sanaa yoyote ile itapwaya. Kwa mfano, mwandishi anapoandika hadithi kuhusu Dar es Salaam, si busara kusema kuwa Jijt la Dar es Salaam lilijabarafu.kama kawaida yake. Hii si kweli, kwani kila mtu anajua kuwa Dar es Salaam hapawezi kuwa na barafu hata siku moja kutokana ua mazingira ya kijiografia ya Dar es Salaam.
Hitimisho
Katika sura hii tumejitahidi kuvichambua vipengele vya fani kwa undani kadiri ilivyowezekana. Tumejadili FANI ua vipengele vyake (...) hadithi fupi. Japokuwa mjadala umelenga hasa katika hadithi fupi, vipengele hivyo ni vya kawaida katika kazi nyingine za sanaa. Jambo la muhimu kufahamu ni kuwa wakati mwingine kunakuwa ua tofauti za mkazo au njia za matumizi ya vipengele hivyo vya kisanaa. Kwa kuunganisha mawazo yaliyotolewa na kufafanuliwa katika sura ya tatu, mawazo yaliyo katika sura ya nne yanakamil-ishwa zaidi. Wazo kwamba ili fani iweze kufanya kazi kama FANI isitenganishwe na MAUDHUI ni muhimu.
Kwa hiyo, mpangilio wa vitu kama mawazo, taswira, mandhari, (mazingira), wahusika, lugha na mengineyo unakuwa muhimu tu pale unapotumika ili kuleta maana dhahiri ya maudhui kwa ujumla. Hadithi yoyote inafanikiwa kifani kama fani na maudhui vinaoanishwa na kukamilishana vyema.
Mshikamano katika hadithi lazima upimwe kwa kuzingatia vipengele vya fani: msuko, wahusika, mazingira, mtindo, lugha na matumizi yake parnoja ua maudhui.
Maelezo
1. S. Robert, Kusadikika, EALB, Dar es Salaam: 1961.
2. Kama Na. 1.
3. P. Muhando na N. Balisidya, Fasihi na Sanaa za Maonyesho, TPH 1976: 69.
4. M.Msokile, Nitakuja kwa Siri, DUP, Dar es Salaam: 1982.
5. Kuna wahusika mbalimbali tunaoweza kuwaainisha katika fasihi ua hasa kwa upande wa hadithi, wakati wanaposimulia hadithi zinazohusika. Kwa mfano tuna wahusika wafuatao: Msimulizi tinde, msimulizi horomo, msimuhzi mkengeushi, msimulizi penyszi n.k. Kwa maelezo zaidijuu yajambo hili, soma Istilahi za Fasihi, katika kitabu hiki.
6. S.A.K. Mlacha, "Wahusika katika Riwaya za Kiswahili," (Makala), TUKI: 1983.
7. Kamusi ya Kiswahili Sanifu, TUKI - OUP, Dar es Salaam - Nairobi: 1981.
8. M. Msokile, Usiku Utakapokwisha, DUP, Dar es Salaam: 1990.
9. C. Kuhenga, Tamathali za Usemi, EALB, Dar es Salaam: 1975.
10. Mfano wangu.
11. KamaNa. 9.
12. C.H. Holman, A Handbook to Literature, Odyssey Press, New York. 1936.
13. M.M. Mulokozi ua K.K. Kahigi, Kunga za, Ushairi na Diwani Yeiu, TPH, Dar es Salaam: 1976
14. W. Blair (nawenzake), Literature, Scott, Foresman & Company: 1966.
15. F.E.M.K. Senkoro, Fasihi, PPC, Dar es Salaam, 1984. Katika kitabu chake hicho Senkoro anajadili pia dhana ya ucheshi inavyoweza kutumiwa kisanaa ili kuiimarisha kazi ya sanaa inayotumia lugha. Anasema kuwa ucheshi unaweza kutumiwa na msanii ili kujenga dhamira kuu, kufurahisha, kukejeli, ua kukebehi n.k. Kwa msingi huo, ucheshi ni kipengele muhimu sana kwa msanii kama atataka msanii huyo kazi yake iwe ua nguvu kisanaa.
16. Mfano wangu.
17. A. Abdalla, Sauti ya Dhiki, OUP, Nairobi Dar es Salaam: 1973
18. Mfano wangu.
19. Mfano wangu.
20. Kama Na. 15.
21. Kama Na. 12.
22. J.H.Mwansoko, "Mitindo katika Uandishi wa Kiswahili," (Makala ya TUKI: 1982).
23. Kama Na. 20.
24. Kama Na. 15.
25. E. Kezilahabi, Ushairi wa Shaaban Robert, EALB, Dar es Salaam: 1976.
26. BAMITA, Zaka la Damu, BAMITA, Dar es Salaam: 1976.
27. M. Msokile, Thamani ya Ukubwa, Meza Publications, Dar es Salaam: 1979.
28. E. Kezilahabi, "Wasubiri Kifo." Katika Insha J.P. Mbonde (mh) 1976.
29. G. Rwechuagura, Ufahamu wa Lugha ya Kiswahili, Heinneman, 1973.
30. Mfano wangu.
31. J.R.R. Mkabara, Mbio za Kipofu, Utamaduni Publishers, Dar es Salaam: 1981.
32. E. Kezilahabi, Rosa Mistika, East African Literature Bureau, 1972.
33. W. Blair (na wenzake), Literature, Scott, Foresman and Company, New York, 1966: 824.
34. P. Muhando na N. Balisidya, Fasihi ua Sanaa za Maonyesho, TPH, Dar es Salaam, 1976: 64-67
35. Kama Na. 15.
36. Kama Na. 7.
37. T.S.Y. Sengo, Mwalimu wa Fasihi (Mswada) (Haujachapishwa).
38. M.S. Abdulla, Mzimu wa Watu wa Kale, EALB, Dar es Salaam: 1962.
39. P. Mbughuni (Mratibu) Msamiati wa Muda wa Fasihi, TUKI, (1985).
40. Kama Na. 12.
41. Kama Na. 22.
42. Gazeti la Mambo Leo lilichapishwa Tanzania kwa muda mrefu kuanzia mwaka 1923. Hadithi nyingi zilichapishwa kwa jina la Mjomba Remus.
43. Hadithi hii imedondolewa kutoka Gazeti la Mambo Leo la mwaka 1925. Kiawahili kilichotumiwa wakati huo ni cha herufi -c- badala ya -ch- kama ilivyoonyeshwa.
44. E. Kezilahabi, "Wasubiri Kifo," katika Uandishi Tanzania:Insha (Mhariri: J.P. Mbonde).
45. J. Rutayisingwa, "Ndumila Kuwili," kutoka kwa mwandishi mweayewe.
46. Kama Na. 44.
47. Kama Na. 45.
48. V. Propp, Morphology of the Folktale, University of Texas Press, Austin + London: 1968 (3-16).
49. S. Kichamu Akivaga na A. Bole Odaga, 0ral Literature, HEB, Nairobi, 1985.
50. F.E.M.K.Senkoro, Fasihi Simulizi (Mswada) (1988).
51. Kama Na. 34.
52. Kama Na 8.
53. Kama Na. 12.
54. Mariam Ba, So Long a Letter, Heinemann, Kenya, Nairobi: 1980.
55. Gazeti la Chama cha Mapinduzi, huchapwa na Kiwanda cha Uchapaji cha Taifa.
56. S. Ousmane, Chale za, Ktkabila, TPH, Dar es Salaam, 1981
57. Kama Na. 12.
58. M.H. Abrams, A Glosary of Literary Terms, Norton University Libtary, New York: 1957.
59. Kama Na. 7.
60. C. Kuhenga, Tamathali za Usemi, EALB, Dar es Salaam: 1977.
Powered by Blogger.