THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL
ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION
EXAMINATION

121/1                                                   KISWAHILI 1
(Kwa Watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 3                                                                                Jumatatu 05 Mei 2003 Mchana

SEHEMU A (Alama 20)
HISTORIA
Jibu maswali moja (1) kutoka sehemu hii.
1. Kwa nini Kiswahili kimekua na kuenea zaidi nchini Tanzania kuliko Kenya na Uganda?
2. Kiswahili kabla ya Uhuru nchini Tanzania kilidumazwaje na hawa wafuataio?
   (a) Waingereza
   (b) Waarabu
   (c) Wajerumani
   (d) Wanadini
3. Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia katika shule za sekondari na elimu ya juu hapa nchini
    kumesababisha wananchi kugawanyika katika makundi mawili, wanaokubali na wanaokataa.
   (a) Wanaokubali wana hoja gani za msingi?
   (b) Wanaokataa wana hoja gani za msingi?

SEHEMU B (Alama 20)
SARUFI
Jibu maswali moja (1) kutoka sehemu hii.
4. Katika jedwali la hapo chini onesha aina ya tungo na viaina vyake katika kila kisanduku.



5. (a) Ni zipi patanisho za kisarufi zifuatazo zenye kosa?
- Kipofu kizuri                        Maji ni safi
- Kikapu kizuri                        Shule zuri
- Kifaranga mmoja                  Machungwa masita
- Kinyonga kimoja
- Kalamu izuri
    (b) Kwa nini upatanisho huo uliooneshwa katika 5(a) hapo juu una makosa?
    (c) Unatakiwa uweje?
6. (a) Tenga mofimu za maneno yafuatayo:
            (i) Starehe
            (ii) Shukuru
            (iii) Anakunywa
            (iv) Atasali
            (v) Atakuja
    (b) Kwa nini umetenga hivyo?
SEHEMU C (Alama 20)
MATUMIZI
Jibu maswali moja(1) kutoka sehemu hii.
7. Kwa kutoa mfano wa sentensi eleza matumizi matano ya kiunganishi “kwa”
8. Thibitisha kwamba lugha ya mazungumzo hutawaliwa na mada ya mazungumzo, mtu
     anayezungumza naye na mahali au sehemu wazungumzaji walipo.
9. Kwa kutumia mifano eleza maana, chanzo, aina na matumizi ya misimu kwenye Kiswahili.

SEHEMU D (Alama 20)
UTUNGAJI
Jibu maswali moja (1) kutoka sehemu hii.

10. Chagua mada moja kati ya hizi:
            (a) Andika barua kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi uliyomaliza darasa la saba,
                 ukimuomba akutumie cheti chako cha kumaliza elimu ya msingi. Jina na anuani yako
                 iwe: Maji S. Machungu, S.L.P. 75, Kuzimu.
            (b) Andika insha ya maneno yasiyozidi 400 na yasiyopungua 300 juu ya ajali ya treni ya
Powered by Blogger.