MASHAIRI YA CHEKA CHEKA MWANDISHI: Theobald A. Mvungi MCHAPISHAJI: EDP MWAKA : 1995
MASHAIRI YA CHEKA CHEKA
MWANDISHI: Theobald A. Mvungi
MCHAPISHAJI: EDP
MWAKA : 1995
UTANGULIZI
MASHAIRI
YA CHEKA CHEKA ni diwani
inayoongelea masuala hayo ni pamoja na uongozi mbaya,mapenzi duni,Ukombozi.Mwandishi
Theobald Mvungi amejadili kuwa kwa kinamasuala ya hayo na alipoanza
alipendekeza namna ya kukubaliana nayo;mfano katika shairi la CHANZO
CHA HUO UOZO amewashauri viongozi wa dini kuhimiza waumini watende
matendo mema na wamrudie Mungu badala ya kuhimiza michango kwa ujumla Mvungi
ametoa mchango mkubwa katika kujenga jamii mpya.
MAUDHUI
Maudhui ni mawazo
yanayozungumzwa na msanii wa kazi ya kifasihi pamoja mtazamo wa mwandishi au
msanii juu ya mawazo hayo.
A)
DHAMIRA
1.
UKOMBOZI
Mwandishi
anazungumzia suala la ukombozi kisiasa ambapo kupitia shairi lake la TAIFA
WAMELIZIKA,msanii anaonyesha namna wananchi wasivyo na uhuru katika
masuala mbalimbali,msanii anasema;
Ni sera zao tukufu, hangaiko la raia
Hao ndio maarufu, wajua kuhutubia,
Wajumbe mshiriki, katika huo uovu,
Pia
mshauri anaendelea kusema kuwa hakuna demokrasia ya kweli kwani watu wanaamriwa
kila jambo kama ubeti huu usemavyo,
Mezikwa demokrasia,chama kimoja ndio ngao
Watu hawana nafasi,kutetea nchi yao.
Mawazo ya ukakasi, mawazo ya mtitio,
Wapenda jibu mkato, wale waongo wa hoja.
Aidha mwandishi anaeleza kuwa ukombozi
wa kweli utatekelezwa endapo kutakuwa na mshikamano wa dhati baina ya viongozi
na wananchi, msanii amedhihirisha hayo kupitia shairi la MWINYI UMEWASHA MOTO:Angalia
usizimwe.Hapa mshairi anaeleza kuwa wananchi wanategemea viongozi katika kuleta
maendeleo, viongozi ni dira hivyo wapaswa wawe mstari wa mbele kwenye mambo ya
maendeleo.
Kwa
suala la ukombozi kiuchumi mshairi anasema ni vigumu kupata maendeleo kama viongozi
wataendelea kutumia madaraka kwa manufaa yao binafsi kama shairi la MTOTO
ASO RIZIKI lisemavyo;
Taifa wamelizika,mali zetu wamepora,
Tena hawa wasifika,tunawapigia kura,
Kwa hotuba wasifika,vitabu sura kwa
sura,
Uchafu ulivyojaa,dawa maji ya
tufani
2. MAPENZI
Mwandishi
amejadili dhamira hii kupitia mashairi mbali mbali kama vile NJIWA
KIUMBE
MTINI,katika shairi hili mshairi anasema katika mahusiano ya kimapenzi kuna
umuhim wa watu kuchnguzana na kupeana muda kwani papara husababisha
watu kutoa majibu yasiyo sahihi na kama mtu ana mapenzi ya dhati hatakata tamaa
asumbuliwapo na ampendaye.Katika ubeti huu msanii asema;
Matawi mkiyakwea,njia arukie
kule,
Si kwamba anakimbia, ni mbinu zake teule,
Tabu kaniongezea,hata
chakula nisile,
Vivyo hivyo katika shairi la PENZI
LISILO HESHIMA,mshairi anaonyesha namna mapenzi ya siku hizi yalivyogeuzwa bidhaa;
Penzi la umaskini, kwa hii yetu dunia
Ni penzi la nuksani,mpendwa hatapokea,
Mpendwa hamuelewani,kwa maneno ya kumwambia,
Mfukoni huna kitu,mpenda tahangaika.
3. DEMOKRASIA
Mwandishi
amejadili suala la kidemokrasia katika shairi la TAIFA WAMELIZIKA ambapo wanawatumia
wakunga na wajumbe mbalimbali wahudhurie vikao mbalimbali vya kujadili masuala
ya nchi,lakini wao wasiende kupiga porojo na kufanya mawazo ya wachache bali
wawasilisha mawazo ya wananchi Lakini Wabunge
na wajumbe husinzia wawapo mikutanoni badala ya kuchangia hoja zenye kuleta
tija kwa wananchi wanaowakalisha majumbani wengi hujali posho zao matokeo yake
mawazo ya wananchi hupuuzwa. kama ubeti huu usemavyo;
Mezikwa demokrasia,chama kimoja ndio ngao,
Watu hawana nafasi,kutetea nchi yao,
Mawazo ya ukakasi,mawazo ya mtitio,
Wapenda jibu
mkato,wale waongo wa hoja.
Msanii anawataka viongozi wakumbuke kutekeleza
majukumu au wajibu wao kwa ufanisi na
sio kwenda kusinzia wawapo mikutano kwani wao ni wawakilishi wa watu wao.
4.
MATUMIZI MABAYA YA MALI YA UMMA
Katika
shairi la GUNIA LA MIKUTANO,mwandishi ameonyesha namna ambavyo viongozi
wengi hutumia fedha za umma kinyume na utaratibu. mfano; kujilipa posho wawapo
vikaoni,hata vikao visivyo vya ulazima.Aidha huandaa sherehe mbalimbali
zinazohitaji fedha nyingi na ambazo haziwanufaishi wananchi.msanii anasema;
Sherehe zenye utamu,raha ya wachache humu,
Ni mateso kwa kaumu, wasoweza kujikimu,
Sherehe si kipaumbele, mwelekeo uwe kazi
5. UZEMBE NA UKASUKU
Katika
shairi la NI WAPI USHAURI msanii anakemea uzembe na kwamba watu hawafanyi
kazi kwa kujituma bali wanataka wasukumwe,kwa mtazamo wake msanii anaona
kufanya kazi kwa kusukumwa ni kama utumwa.Msanii anadhihirisha hili kwa
kuwatumia wanaohusika na usafirishaji mazao toka kwa wakulima ambao huzembea na
kufanya mazao yaoze mashambani ambapo hali hii huwakatisha tama wakulima ya
kuendelea na kilimo.Msanii anasema;
Wanawe idadi sita,wakulima maarufu,
Pamba mahindi ufuta,tena wana watiifu,
Fedha wanazitafuta,wanunue maradufu
Mazao yamo nyumbani,hayana mnunuzi.
Pia katika shairi la TUAMBAE
UKASUKU mwandishi anawaasa watu wanaoishi maisha yakufuata mkumbo kuwa maisha
ya namna hiyo hayafai. Katika maisha mtu anatakiwa kuangalia jambo gani lina
manufaa na lipi halina,lile lenye manufaa lifuatwe kwa lengo la kuboresha
maisha.Hapa msanii anawazungumzia washairi kuwa watunge mashairi yenye lengo la
kuleta maendeleo siyo kuwasifia viongozi wafanyapo mambo yasiyofaa
kuwasifia.Mwandishi anaona kuwa mshairi bora ni yule anayesema ukweli
asiyekubali kuwa kibaraka.Mwandishi anasema;
Mshairi uwe huru,upige yako mafumbo,
Usiwe kama kunguru,woga umejaa tumbo,
Na usitoze ushuru,hapo utakwenda kombo,
Wataka wanyonge,so wale waheshimiwa.
Mwandishi
anawataka waandishi na jamii kwa ujumla waishi kama vile walivyo na si kuishi
maisha ya kuigiza kwa lengo la kuwafurahisha watu fulani.
6. DINI
Mwandishi
katika diwani yake amezungumzia upotofu unaojitokeza kwenye madhehebu yetu ya
dini.mfano; Dini ya kikristo madhehebu ya wakatoliki na walutheri viongozi
huimiza sana michango badala ya kuimiza matendo mema kwa waumini.Watu
wanatakiwa kumrudia Mungu na kuacha dhambi,kuhimiza upendo na mshikamano badala
ya kutenda hayo waumini hujazwa chuki kwa kurundukiwa michango.Msanii anasema;
Nimechunguza kanisa,luteri na katoliki,
Viongozi nawaasa,roho hazimpi chuki,
Zile ibada za misa,watu wanajazwa chuki,
Padri hanalo jambo,ila kudai michango.
kupitia ubeti huo mwandishi wa shairi
la CHANZO
CHA HUO UOZO anaonesha namna maana ya dini inavyopotoshwa watu
wanachukizwa na kuchoshwa na michango na kuona kanisa kama sehemu ya maudhi
badala ya faraja.Mwandishi anawataka viongozi wa dini kuwasaidia waumini wao
waende mbinguni na sio kudai michango pekee.
7.
SUALA LA UONGOZI
Mwandishi
amejadili suala la uongozi kwa kuonesha namna viongozi wetu wengi wasivyo
wasikivu na kutotekeleza wajibu wao.Mwandishi ameonesha namna ambavyo viongozi
wengi wanavyoweka ahadi ambazo hazitekelezwi,ahadi zao ni za kutaka madaraka
wakati wa kampeni za uchaguzi.katika shairi la MTOTO ASO RIZIKI mwandishi
ameonesha namna viongozi wanzvotusaliti.Msanii anasema;
Wasalitiwa mbali, wala si waamerika
Ni hawana wala mali, hatamu walioshika,
Weusi kwa kila hali, madaraka waloshika,
Si wote hilo ni wazi, lakini ni wamo wengi.
Katika shairi la MASHAIRI YA NGULU mwandishi
ameonesha namna viongozi wanavyojipendelea na kufanya dhuluma kwa wananchi,wakulima
na wafanyakazi hawatendewi haki wanadhulumiwa mazao na mishahara yao.Msanii
anasema;
Diwani unasaili,falsafa za kukwama,
Uongozi usojali,taabu za wakulima,
Wale wasio na hali,wanarudishwa nyuma,
Waporwa mazao yao,kwa hoja za ulaghai.
Tazama mfanyakazi,mshahara
wa mwezi,
Utani wa uchochezi,hautoshi hata
nazi
Ni vipi asiwe mwizi,nani asiye
mwizi?
Ujira wa moja juma, ati ndo
wa wote mwezi.
Katika ubeti huo hapo juu mwandishi
ametoa mfano wa dhuluma hizo wanazofanyiwa wakulima kwa kulaghaiwa bei wauzapo
mazao yao (bei hailingani na thamani ya mazao). Pia wafanyakazi wanapata
mishahara midogo ambayo haikidhi mahitaji yao na ndiyo maana wengi wanapokea
rushwa katika utendaji wao.
Vivyo hivyo katika shairi la MUWAPI
NAWAULIZA msanii ameeleza namna viongozi wanavyolala na kuacha baadhi ya
watu kufanya watakavyo. kwa mfano; Wafanyabiashara kupanga bei za mazao ya wakulima watakavyo kwa madai kuwa biashara
ngumu,Aidha wauzapo huuza kwa bei wazipendazo eti biashara huria.
Katika
shairi la RAIA SI MALI KITU Mshairi ameonesha kuwa viongozi
hawashirikishi wananchi katika kutoa maamuzi, mambo mengine huamuliwa na
viongozi na wananchi wanaambiwa tu kutekeleza.
Mwandishi anawataka viongozi kutekeleza wajibu
wao kwa ufanisi hasa ahadi wanazoahidi pindi wanapotaka uongozi.
FANI
A.
MUUNDO
Mwandishi
amegawa mashairi katika makundi mawili, mashairi ya kawaida na tena ambapo aina
zote kwa kuzingatia beti, vina, mizani na vituo.
Kwa
upande wa beti yapo mashairi yenye beti nyingi na yenye beti beti chache. Mashairi
yenye beti nyingi ni pamoja na LAZIMA WAUMINI lenye beti 10, RAIA SI MALI KITU lenye beti 9
na yenye beti chache ni KIMOYO lenye beti 4.
Mizani,mwandishi ameunga mkono mashairi kwa idadi ya mizani
ambapo mashairi ya kawaida yana mizani 16 kwa mgao wa 8¤8 kwa kila shairi, mfano shairi la MWENYEWE UMEWASHAMOTO.
Hao
wamekuzunguka,walaji hawako mbali,
Vipigo
vimetukuka,ndilo jina la awali,
Hawa
ndio wasifika,kwa hidhini na vibali,
Usoni
tadhani watu,lo aheri mbwa mwitu,
Kwa upandewa ametumia mizani nane (8)
kwa kila shairi, mfano shairi la SENG’ENGE
Nipishe
wewe seng’enge,
Nipishe
kando jitenge,
Nipishe
usinifunge,
Usiwe
haambiliki
Vina,kwenye mashairi ya kawaida kuna vina vya kati na
mwisho.Mfano shairi la CHATU MMEZA MATONGE.
Sipendi
yanatokea, shirika macho kufumba,
Kukataa
kusikiya, ya wapangaji wa nyumba,
Watu
walifikia, shirika la nyumba,
Ndilo
kimbilio lao, hawa wavuja majasho
Katika ubeti huo kuna vina vya kati “a”
na vina vya mwisho ni “mba” na upande wa tenzi huwa na vina vya mwisho. Mfano utenzi wa INDIRA
Sifazo
kwa jitihada,
Tuishi
kwa kawaida,
Kwetu
ukawa ushuhuda,
Takukumbuka
daima.
Vituo,mwandishi ametunga mashairi yenye vituo vitoshelezi
kwakuwa katika mashairi yake yote kila ubeti una kituo chake
B.
MTINDO
Mwandishi
katika mashairi yake yote yamezingatia urari
wa vina na mizani, pia ametumia mtindo na maelezo yaani anaelezea
ufahamu alionao juu ya jambo analozungumzia.Aidha ametumia mtindo wa nafsi
ambapo nafsi karibu zote zimetumika. Mfano
-“Mwinyi amewasha moto” (U-nafsi ya
pili umoja-wewe),
-“Tuambae ukasuku” (Tu-sisi nafsi ya
kwanza wingi),
- “lazima mniamini (nyinyi- nafsi ya
pili wingi) n.k.
C.
LUGHA
Mshairi
ametumia vipengele mbalimbalivya lugha ili kuifanya kazi yake na mvuto wa
kueleweka kwa hadhira, baadhi ya vipengele hivyo ni :-
TASWIRA/ PICHA
Mshairi
ametumia taswira mbalimbali yani zahisi,au za kuonekana.Mfano;
-Shairi la KUNA NINI HUKO NDANI inamaanisha
matumizi
mabaya ya madaraka ),
- CHATU
MMEZA MATONGE linamaanisha matumizi mabaya ya mali za umma, GUNIA LA
MIKUTANO (ufugaji wa fedha)
METHALI
Mshairi
ametumia baadhi ya methali katika mashairi yake mfano
-Taratibu ndio mwendo, katika shairi la MOYO,
-Umoja ni nguvu, katika shairi la KAZI
ZETU HARAKATI.
TAMATHALI
ZA SEMI
Mwandishi
ametumia tamathali za semi mbalimbali ili kuongeza mvuto kwenye kazi yake,
mfano
Ø
Tashibisha
Ni
tamathali inayolinganisha vitu viwili au zaidi kwa kutumia viunganishi.mfano
katika shairi la LAZIMA MNIAMINI mandishi anasema;
Mlevi
akakolea,kama tumbaku ya tozo
Miguu ikalegea, katika kuchezacheza,
Kaziongeza
bia, watu wakatumbuiza,
Watoto
wakirimu,mradi kiitikio,
vile vile katika shairi la MOYO
mwandishi anasema;
Moyo
nimeushauri, lakini umekaidi,
Moyo
kiburi hatari, mfanowe kama radi,
Moyo
mefumbata shairi, unayakwepa maradi,
Moyo
mwilini mwangu,jiradi tuwe pamoja
Ø Sitiari
Ni
tamathali inayounganisha vitu pasipo kutumia viunganishi.Mfano katika shairi la
INDIRA
Mwandishi anasema;
Mwenzetu
Gandi kwaheri,
Moyo
hutuna shwari,
Machozi
yetu bahari,
Gandhi
ulitudhamini.
Aidha katika shairi la UTU
UMEKUWA KIMA mwandishi anasema;
Dhuluma
ndio hekima,
Utu
umekuwa kima,
Hafai
huyo mnyama,
Jumlaye
ni uhuru.
Ø
Tashihisi
Ni
tamathali ivipavyo uwezo vitu visivyo binadamu kutenda matendo ya binadamu.
mfano, katika shairi la NJIWA KIUMBE MTINI mwandishi anasema;
Mmejaribu
kujongea,ndege awe mkononi,
Yeye
juu hurukia, na muomba samahani,
Nyimbo
anaziimba, nyimbo zachoma moyoni,
Basi
mie kaabani, njiwa akitabasamu.
Katika shairi ubeti huo njiwa amepewa
uwezo wa kumwimbia mwanadamu nyimbo kuomba msamaha na kutabasamu.Matendo hayo
kiuhalisia yanatakiwa yatendwe na watu sio ndege (njiwa).
Katika
shairi la MOYO unaambiwa uache jeuri na ukaidi na ujifunze busara.
MKATO WA MANENO
Baadhi
ya maneno yamekatwa katika diwani hii ili kupata urari wa mizani na vina.Mfano
maneno asotaka badala ya asiyetaka na walojonea baala ya waliojionea,
katika shairi la LAZIMA MNIAMINI na katika shairi la MOYO mwandishi anasema mekuwa
badala ya imekuwa.
Kwa
ujumla Mwandishi amejitahidi sana kutumia utenzi na utumizi wa lugha na hivyo
kufanya kazi yake iwe na mvuto.