NADHARIA YA USHAIRI

NADHARIA YA USHAIRI
Ushairi ni sanaa inayojipambanua kwa mpangilio maalum wa maneno fasaha na yenye muwala, kwa lugha ya mkato, picha au sitiari au ishara katika usemi maandishi au mahadhi ili kueleza jambo,wazo au tukio au hisi fulani kuhusu maisha, mazingira ya binadamu kwa namna inayogusa moyo.
Ushairi ni utanzu / fani mojawapo ya fasihi ambao umbo lake hutofautiana na tanzu nyingine za fasihi, mathalani tamthiliya na riwaya.
Utanzu huu una historia ndefu iliyojikita katika fasihi simulizi za jamii zilizohusika.Kutokana na historia yake ndefu ni jambo la kukubalika kuwa hapana budi kuwepo na mabadiliko ambayo yamechimbuka kutoka kipindi kimoja kwenda kingine.
Baadhi ya mabadiliko yaliyochimbuka katika ushairi ni hali ya kuwa na MASHAIRI HURU/ MASIVINA/ YA KISASA amabayo hayafuati  kanuni za kimsingi ambazo washairi wa awali WANAJADI/ WANAMAPOKEO wananazizingatia. Kuna aina mbili za ushairi
1.    Ushairi wa kimapokeo
2.    Ushairi wa kisasa
Mashairi ya kimapokeo ni yaale yanayoongozwa na kanuni za urari wa vina na mizani (hizi ni kanuni za kimuundo), mashairi haya huwa na:-
Ø Beti, kila ubeti una mistari mine (4)
Ø Mizani huwa ni 16 (8/8)
Ø Vina vya kati na mwisho
Ø Kituo  ( bahari, nusu bahari)
UFAFANUZI
Ø Beti ni kifungu cha maneno ambacho hupangwa katika mistari kwa idadi maalumu na huwasilisha wazo au sehemu ya wazo.
Ø Mistari ni idadi ya mishororo katika kila ubeti wa shairi. Yapo mshairi ya mistari tofauti tofauti, mfano
Tamolitha =- mstari mmoja
Tathnia -  mistari miwili
Tathlitha – mistari mitatu
Tarbia – mistari minne
Takhimisa – mistari mitano
Sabilia – mistari sita na kuendelea
·       Mizani ni idadi ya silabi kwa kila mstari wa shairi
Kwa kawaida mashairi ya kimapokeo huwa na mizani kumi na sita kwa mgao wa 8/8.
Ø Vina ni silabi zenye sauti za kufanana, silabi hizi hutokea katikati au mwishoni mwa mstari wa shairi. Mashairi ya kimapokeo huwa na vina vya kati na mwisho
Ø Kituo,ni mstari wa mwisho katika kila ubeti na shairi. Kuna aina tatu za kituo
·       Kituo bahari – hiki ni kituo kinachobadilika toka mwanzo hadi mwisho wa shairi.
·       Kituo nusu bahari – hiki ni kituo kinachobadilika nusu ya mstari na nusu haibadiliki.
·       Kituo kitoshelezi – hiki ni kituo ambacho hubadilika kila ubeti.
Mashairi ya kisasa ni mashairi ambayo hayafuati urari wa vina na mizani. Mashari haya hayana idadi maalumu ya mistari, mizani n.k.
USHAIRI WA KIMAPOKEO NA MASIVINA:
Kuna tofauti kubwa kati ya utenzi, shairi la kimapokeo na masivina. Nazo zaweza kuwa hivi;
Utenzi
Shairi la kimapokeo
Masivina
Utenzi hugawanyika katika beti zenye idadi sawa ya mistari.
Hugawanyika kama utenzi katika beti mbalimbali na katika idadi sawa ya mistari.
Kuna beti mbalimbali lakini idadi ya mistari inatofautiana mara nyingi kutoka kifungu hadi kifungu.
Kwa kawaida utenzi unagawanyika ama kuundwa na mistari minne katika ubeti.
Laweza kuwa na mistari miwili, mitatu na kuendelea katika ubeti kufuatana na matakwa ya msanii.
Si rahisi kutaja idadi ya mistari katika ubeti mmoja wa shairi kwani hutofautiana mara kwa mara.
Mistari hugawanyika katika mizani ambayo huwa kati ya 8 na 12.
Mistari hugawika katika mizani na mara nyingi huwa 16  nane kila upande.
Mizani huwepo lakini hutofautiana kutoka mstari hadi mstari.
Utenzi una vina vya mwisho vinavyofanana.
Lina vina vya kati vinavyofanana na vya mwisho vinavyofanana. Navyo vyaweza kufanana kwa shairi zima au la.
Urari wa vina haujipambabui sana kama ilivyo katika shairi la kimapokeo.
Beti zake hazijitoshelezi, mawazo yake yanaendelezana kutoka ubeti hadi ubeti.
Ubeti mmoja hujitosheleza hivyo waweza kuwa na shairi la ubeti mmoja tu.
Maana ya shairi hupatikana baada ya kulisoma shairi lote.
Kimsingi utenzi huwa mrefu kuliko shairi la kawaida nao mara nyingi huelezea tukio moja kwa kirefu sana.
Mara nyingi haliwi refu sana na linaweza kuwa na ubeti mmoja.
Mara nyingi huwa na urefu wa wastani. Yanafanana na mashairi ya kimapokeo.
Utenzi katika usimulizi wake mara nyingi huanza na dua au kumaliza na dua
Si jambo la muhimu sana ingawa baadhi ya wasanii hufanya hivyo
Dua halijitokezi katika masivina.




Sanaaa hii ya ushairi yaweza kujipambanua katika;
·       Tenzi
·       Nyimbo
·       Mashairi

·       Ngonjera.
Powered by Blogger.