JARIBIO LA MWEZI KISWAHILI 1 KIDATO CHA SITA














JARIBIO LA MWEZI
KISWAHILI  1
KIDATO CHA SITA
121/1
MUDA SAA  2:30
MAELEKEZO
1. Mtihani huu una sehemu nne (4).
2. Jibu maswali yote katika mtihani huu.
3. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali.
4. Andika majina yako yote kwa usahihi kama yalivyosajiliwa.
5. Swali lisilo na namba halitasahihishwa.











SEHEMU A (Alama 20)
UFAHAMU NA UFUPISHO
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kwa makini kisha jibu maswali  
     yanayofuata.

          Bibi aliwaita wajukuu zake wote na kukaa nao sebuleni kisha akawasimulia hadithi iliyoanza hivi: “Paukwa!” Watoto wakajibu “Pakawa” kisha akaendelea: “ Hapo zamani za kale palikuwa na kisiwa kimoja kikubwa sana kilikuwa na watu wengi sana wa kila aina. Kisiwa kilijaa matajiri na masikini, pia watu wa kisiwa hiki waliishi kwa raha mustarehe kwa kipindi kirefu.
          Punde kukatokea dubwana kubwa katika kisiwa kile na kukawa na kutafutana. Dubwna likaleta balaa kisiwani na kila aliyeguswa na dubwana alidhurika, watu wakatokwa mapele na ukurutu, wengine waliharisha na kufungwa nepi kama watoto wachanga! Nywele zilinyonyoka na hatimaye vifo vikafuatia. Ngoja watu wapukutike! Walipukutika ,wakapukutika na kupukutika kama majani ya kiangazi.
          Kila mtu akawa na lake la kusema, wengine jini,mara mzimu,na wale waumini wa dini mbalimbali wakasema hizo ni dalili za kiama. Basi wakubwa wakajikinga,wakaandikiana mabuku kupeana habari na kuitisha mikutano ya siri waliyoiita semina,walibandika mabango kupeana tahadhari,lakini maskini watoto wakaachwa wakiangamia na kuteketea wakubwa wakaanza kujitetea kuwa dini na mila haziruhusu. Oo!Mila na desturi haziruhusu. Basi vijana wakafichwa na kuachwa bila kupewa kinga yoyote ya kujinusuru na dubwana hili.
          Kumbe kufa kufaana waswahili walisema yalianzishwa mashirika chungu nzima yakidai yanawasidia waliokumbwa na dubwana hili, fedha zikamiminwa,vitambi vilitokea na majumba wakajenga huku vijana wakiendelea kukata kamba kwa maelfu! Ukatili gani huu! Kisiwa kiliendelea kuwa gizani. Watu hususani vijana walishindwa kutofautisha kati ya puto na kondomu.
          Kujitoa kimasomaso,mashirika yaliyoanzishwa yalianza kutoa elimu iliyoshauri watu kuwa waaminifu,wasubiri au wakishindwa watumie kondomu. Lakini ukweli unabaki palepale kwamba bado vijana walio wengi hawapewi elimu yoyote na wazazi wao kwa kuhofia kuvunja miiko ya mila na desturi za Kiafrika zinazoweka ukuta baina ya wazazi na watoto wao! Baada ya kumaliza hadithi yake bibi na wajukuu zake walitawanyika na kwenda kulala.

    Maswali
(a)  Andika kichwa cha habari hii
(b) Ni watu gani walioathiriwa na dubwana kwa kiasi kikubwa?
(c)  Unafikiri dubwana katika habari hii ni nini?
(d) Kwa nini mwandishi anailaumu jamii na hasa wazazi na viongozi?
(e)  Taja madhara yaliyosababishwa na dubwana katika habari hii (yasizidi manne)
(f)   Nini maana ya misemo au maneno yafuatayo:
(i) Walipukutika      (ii) Kufa kufaana   (iii) Kukata kamba 
(iv) Kuweka ukuta baina ya wazazi na watoto  (v) Hususani

2. Fupisha habari hiyo kwa maneno mia moja (100).

SEHEMU B (Alama 10)
SARUFI
Jibu maswali yote sehemu hii

3.         Andika sentensi zifuatazo katika wingi.
(a)     Mtoto mkaidi hatapewa zawadi.
(b)     Mimi nilimwona mwizi aliyevunja mlango wako.
(c)      Uzi ulioshonea shati langu unatoa rangi.
(d)     Mzabibu wangu haukuzaa zabibu nyingi.
(e)      Mzazi wangu anashiriki kulima shamba la kijiji.
(f)      Mkulima anashiriki kulima shamba la kijiji
(g)     Kile kilima kina mnyama mkali sana.
(h)     Huyu mchuuzi amenunua nazi hii wapi?
(i)      Mkono mtupu haulambwi.
(j)      Kito cha thamani hakipatikani kwa urahisi.

4. Vibadilishe vitenzi vifuatavyo viwe katika kauli ya kutendeka:
(a)     Badili
(b)     Kata
(c)      Komboa
(d)     Zuia
(e)      Fika
(f)      Zoa
(g)     Jenga
(h)     Remba
(i)      Tumia
(j)      Lima





SEHEMU C (Alama 05)
UTUMIZI WA LUGHA
Jibu swali la tano (5)
5.       Katika kila sentensi andika neno moja lenye maana sawa na maelezo ya
         sentensi husika.
(a)     Kifaa kitumiwacho kuwezesha watu kuona chaneli za televisheni.
(b)     Mtu anayefua na kupiga pasi nguo za watu wengine kwa makubaliano
          maalumu.
 (c)     Mtoto wa mwisho katika familia.
 (d)    Msururu wa watu wanaosubiri huduma fulani.
 (e)     Shimo kubwa litumiwalo kujificha wakati wa vita.


SEHEMU D (Alama 15)
TAFSIRI
Jibu swali la sita (6)
6. (a) Toa maana ya tafsiri

Powered by Blogger.