SWALI: Toa tofauti tano kati ya mhusika mkuu wa zamani na mhusika mkuu wa sasa katika fasihi andishi

Mhusika mkuu wa zamani, alikuwa halisi na mwenye sifa zisizo za kawaida aliyesifiwa na msanii kwa makusudi mazima ya kuumba. mfano bora wa kuigwa na jamii.

Alikuwa kilelezo cha ukweli na ukamilifu wa maisha na mwenye kupigania na kuleta mambo hayo bila kuwa na dosari.

Mhusika mkuu wa zamani alitafakari maisha ya jamii kwa njia ya matendo makubwa na lugha teule.Mhusika huyo japo kuwa alijitokeza kuwa mtendaji mkuu kiasi hicho lakini hakuwa na saikolojia wala hisia. Sifa hizi za upungufu wa saikolojia na hisia katika mhusika mkuu wa zamani ndizo zilizomtofautisha na mhusika mkuu wa sasa.

Tofauti nyingine ya msingi ni ile inayohusu uhusiano kati ya mhusika mkuu huyo na wakati. Mhusika mkuu wa zamani kama vile wa kwenye hadithi ya kifasihi alijitokeza kama mhusika mkuu wa wakati wote. Kwa msanii wa namna hiyo, wahusika, dhanna za wakati na ukweli uliokamilika vilikuwa katika hali ya kutobadilika yaani wakati na ukweli vilikuwa ni vitu vilivyotitia pamoja.

Kwa jinsi hiyo maandishi ya kisanii yaliyopewa jukumu la kuzibeba sifa hizo yalilenga kuwa ni ya wakati wote, yasizeeke. Lakini kinyume chake mhusika mkuu wa kisasa anayaona maswala yasiyotulia bali ni masuala ambayo yanabadilika pamoja na jamii. Na baadhi ya wasanii wa kisasa wanaona kuwa, suala la ukweli uliokamilika kwa kiasi kikubwa ni ndoto iliyomo katika vichwa vya watu tu, na wala si maisha halisi.

Mhusika mkuu wa kisasa yuko katika wakati maalumu wa kihistoria ambapo anayatazama maisha kwa undani na kuyatafakari. Lakini kadiri Shaaban Robert alivyozidi kuandika katika Maisha yangu na Baada ya miaka hamsini (1966), Wasifu wa Sitti Binti Saad (1967) Siku ya Watenzi Wote (1968) ndivyo alivyozidi kuwapa wahusika wake sifa zinazokaribiana au zilizoelekeana katika hali halisi ya maisha. Hii ina maana kwamba mkabala wake ulizidi kuelekea katika hali ya kueleza ukweli kwa kutumia mbinu za kisanii ambazo hazikutenga kazi ya sanaa kwa kiasi kikubwa na uyakinifu wa maisha.

Kwa ujumla Fasihi Andishi ya awali ilihusu zaidi maadili na masuala ya kidini kama katika "Adili na Nduguze"
Powered by Blogger.