NAFASI YA USHAIRI KATIKA FASIHI SIMULIZI NA FASIHI ANDISHI
NAFASI YA USHAIRI KATIKA FASIHI SIMULIZI NA FASIHI ANDISHI
USHAIRI wa Kiswahili una dhima kubwa mno katika Fasihi Simulizi na Andishi. Ushairi umetumiwa sana katika tanzu mbalimbali za fasihi kwa sababu mbalimbali.
Nyimbo kwa mfano zimetumiwa sana katika kuandika na kuwasilisha maudhui ya riwaya, tamthilia, novela na hata hadithi fupi.
Zaidi ya mambo mengine, matumizi hayo yana dhima ya kutambulisha wahusika, kujenga tamathali za semi, ishara, taswira, kuweka urari wa vina au mizani na kuonyesha ushiriki wa hadhira katika kazi nyingi za fasihi.
Dhima nyingine ya ushairi katika fasihi ni pamoja na kodokeza, kuibua maudhui na kukuza tanzu za fasihi ya Kiswahili.
FANI
Ushairi una dhima ya kujenga na kuhamisha mbinu mbalimbali za fani.
FANI
Ushairi una dhima ya kujenga na kuhamisha mbinu mbalimbali za fani.
Hili linathibitishwa na Mugyabuso Mulokozi (2002) anaposema kwamba tabia ya tendi ya kutumia au kuazima mbinu za kifani kutoka katika ushairi wa majigambo huhamisha udokezi na sitiari ambazo hutumiwa sana katika majigambo kwenda kwenye tendi.
Hapa tunaona wazi kwamba pale ushairi wa majigambo unapotumika katika utanzu wa utendi, labda na tanzu nyinginezo za fasihi simulizi, hujenga mbinu za kifani kwa kuhamisha mbinu zile zinazotumika katika ushairi wa majigambo na kuzipeleka katika utanzu husika ambao hutumia ushairi huo wa majigambo.
Zaidi ya kuhamisha sitiari na udokezi, ushairi wa majigambo pia huhamisha chuku na ucheshi, mbinu ambazo hutumika sana katika majigambo.
Vivyo hivyo, nyimbo kama mojawapo ya vipera vya ushairi zinapotumiwa katika riwaya, tamthilia au utanzu mwingine wowote, huhamisha mbinu za kifani zilizopo katika wimbo kwenda katika utanzu husika.
HADHIRA
Matumizi ya ushairi katika tanzu nyingine yanasaidia kuibua ushiriki wa hadhira. Ushiriki wa hadhira ndio msingi wa kazi yoyote ya fasihi simulizi.
HADHIRA
Matumizi ya ushairi katika tanzu nyingine yanasaidia kuibua ushiriki wa hadhira. Ushiriki wa hadhira ndio msingi wa kazi yoyote ya fasihi simulizi.
Sifa hii ni mojawapo ya sifa zinazoifanya fasihi simulizi kuwa hai. Hivyo, tunaweza kusema kwamba ushairi wa majigambo na ushairi wa Kiswahili kwa ujumla husaidia sana katika kuibua ushiriki wa hadhira katika tanzu nyinginezo za fasihi na hivyo kuzihuisha tanzu hizo husika.
MAUDHUI
Kazi yoyote ya fasihi hujengwa kwa maudhui na fani. Maudhui ni jumla ya mawazo yaliyomo katika kazi ya fasihi wakati ambapo fani ni mbinu zitumikazo kwa minajili ya kuwasilisha maudhui hayo.
MAUDHUI
Kazi yoyote ya fasihi hujengwa kwa maudhui na fani. Maudhui ni jumla ya mawazo yaliyomo katika kazi ya fasihi wakati ambapo fani ni mbinu zitumikazo kwa minajili ya kuwasilisha maudhui hayo.
Ushairi wa Kiswahili unapotumiwa katika tanzu nyinginezo za fasihi huweza kusaidia kuibua au kukazia maudhui yabebwayo na kazi husika ya fasihi.
Kwa mfano, ushairi wa Kiswahili unapotumiwa katika utanzu wa ngano, riwaya, tamthilia au hadithi fupi huweza kusaidia kudokeza maudhui yabebwayo na kazi husika ya fasihi.
Akifafanua dhima ya nyimbo katika hadithi fupi, Samwel (2012) anaeleza kuwa waandishi wa hadithi fupi huweza pia kutumia nyimbo na hivyo kuonyesha jinsi tanzu zinavyoingiliana, kukamilishana na kutegemeana.
Watunzi wa hadithi fupi hutumia mdokezo wa wimbo ili kuibua maudhui wanaoyakusudia. Mfano mzuri ni matumizi ya nyimbo katika hadithi ya 'Maeko’ (Mohamed Khelef Ghassany) katika diwani ya 'Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine’ ambapo nyimbo kadhaa zinatumika kufafanua dhamira na maudhui ya ulevi.
Wimbo wa 'taarab njia’ unaimbwa na Hamduni ambaye ni mumewe Jamila kila anapoelekea nyumbani kwake baada ya kuelewa.
WAHUSIKA
Ushairi wa Kiswahili husaidia pia katika kujua kazi husika yafasihi inatumia wahusika wa aina gani na wenye uwezo upi. Dhima hii huonekana hasa pale ushairi unapotumika katika utanzu mwingine.
WAHUSIKA
Ushairi wa Kiswahili husaidia pia katika kujua kazi husika yafasihi inatumia wahusika wa aina gani na wenye uwezo upi. Dhima hii huonekana hasa pale ushairi unapotumika katika utanzu mwingine.
Ushairi wa majigambo unapotumika katika tendi, hutambulisha na kujenga sifa mbalimbali za shujaa anayesimuliwa, matendo yake, chakula chake, mavazi yake na mambo muhimu yanayozingira maisha yake.
VIPERA
Ushairi pia huweza kukuza tanzu za fasihi. Inaelezwa na wataalamu mbalimbali kuwa matumizi ya nyimbo pamoja na matumizi ya vipengele vingine vya fasihi simulizi katika fasihi andishi yanakuza vipera vya fasihi hiyo.
VIPERA
Ushairi pia huweza kukuza tanzu za fasihi. Inaelezwa na wataalamu mbalimbali kuwa matumizi ya nyimbo pamoja na matumizi ya vipengele vingine vya fasihi simulizi katika fasihi andishi yanakuza vipera vya fasihi hiyo.
Matumizi hayo ya vipengele vya fasihi simulizi ndani ya fasihi andishi ambayo hayakuwapo hapo awali katika fasihi andishi ya Kiswahili, yameibua kile kinachoitwa majaribio katika fasihi na yamezalisha dhana ya 'fasihi ya majaribio’.
Hivyo, matumizi hayo yameibua riwaya ya majaribio, tamthilia ya majaribio nk. Matumizi ya vipera vya fasihi simulizi, ikiwa ni pamoja na ushairi simulizi (nyimbo), yamekuza fasihi andishi ya Kiswahili.
Matumizi hayo ya nyimbo hukazia kwa mfano maudhui yabebwayo na tamthilia husika na kubadilisha mtindo wa uandishi wa kazi hizo.
Wimbo uliopo katika tamthilia ya 'Nguzo Mama’ unabainisha jinsi jitihada za wanawake kujikomboa zinavyokwamizwa na wanawake wenyewe. Aidha, matumizi hayo ya nyimbo yanajenga picha, taswira na sitiari katika kazi hiyo ya fasihi.
Ushairi wa Kiswahili una dhima kubwa sana katika jamii ya Waswahili na pia kwa fasihi yao na ya jamii nyinginezo.
Hata hivyo, mbali na dhima kubwa ya ushairi wa Kiswahili kwa jamii na fasihi, ushairi wa huo, kama zilivyo tanzu na vipera vingine vya fasihi ya Kiswahili na fasihi ya jamii nyinginezo isipochukuliwa kwa tahadhari, huweza kuipotosha jamii kidhana.