JIPIME KIDATO CHA NNE
CHILDREN AND YOUTH DEVELOPMENT INITIATIVE CENTRE (CYDIC)
MTIHANI WA UTAMILIFU
(PRE-NECTA-1)
KISWAHILI
MAELEKEZO
1.Karatasi hii ina sehemu A,B,C,D na E
2.Jibu maswali yote katika sehemu A,B,C na D na maswali matatu kutoka sehemu E
3.Andika vizuri kwa mwandiko mzuri unaosomeka vizuri.
4. Andika jina lako vizuri na Epuka kufuta futa.
SEHEMU
A (Alama 10)
UFAHAMU
Jibu Maswali yote katika sehemu hii
1.
Soma shairi lifuatalo kasha jibu maswali yanayofuata;
Ima mwana wende kasi,ima usirudi nyuma,
Ima ukwepe sabasi,ima ukipite kima,
Ima ujivike lasi,ima ndiyo taadhima,
Ima mwanakwetu ima,dunia ni sarakasi.
Ima kasema mkwasi,ima uende kulima,
Ima njaa sikughasi,ima mgongo
inama,
Ima wekupe uasi, ima upate usalama,
Ima mwanakwetu ima, ima ndipo
utapasi.
Ima ndipo utapasi, ima mwanakwetu
ima,
Ima ujiunge nasi, ima tuujenge umma,
Ima usile najisi, ima ule cha
kuchuma
Ima mwanakwetu ima, ima emaye
hakosi.
Ima emaya hakosi, ima jikalifu
ima
Ima upweke tatasi, ima wewe na
mwajuma
Ima yoyomea kusi, ima usiuye nyuma
Ima wa ima faima, ima upate fulusi.
Ima mwanakwetu basi, ima usende
kinyume
Ima kazi ni libasi, ima inama kulima
Ima wacha udadisi, ima nakwambia ima
Ima usikae ima, kama kuishi wahisi.
Maswali
a)
Eleza maana ya
maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika
shairi ullosoma:
i.
Mkwasi
ii.
Utapasi
iii.
Jikalifu
iv.
Libasi
b)
Kwa kutumia
sentensi tatu (3), fafanua ujumbe wa mwandishi katika shairi hili.
c)
Msanii ana maana
gani anaposema “ima mwanakwetu ima, dunia ni kama sarakasi”.
2. Soma kifungu habari kifuatacho kisha fupisha habari
hii kwa maneno yasiyopungua hamsini (50).
Kijana anataji kuwa na rafiki ili aweze kuondokana na ukiwa pia ili
aweze kupata faraja. Aidha hayo yatajitokeza kwa sababu atafahamiana na
marafiki hao, vilevile atazoeana nao hasa kwa kupitia maongezi. Kijana huweza
kupata marafiki popote, kwa mfano miongoni mwa majirani zake, shuleni, kazini,
sehemu za ibada na hata awapo safarini. Lakini kijana anapaswa kuwa mwangalifu
katika kuchagua marafiki.
Katika makuzi yake kijana huwa karibu sana na rafiki zake ambao kwa
kiasi kikubwa huwa na nguvu, na ni rahisi kwa kwa rafiki kuambukizana tabia
ambazo zaweza kuwa nzuri au mbaya. Kawa hiyo ni jukumu la wazazi kumwelekeza
kijana na kumshauri kuhusuni yupi hasa rafiki mwema. Ni heri kukosa rafiki
kuliko kuwa na rafiki mlevi, mwongo, mwizi, mvivu, mvuta bangi au mtumiaji wa
madawa ya kulevya. Rafiki mzuri ni Yule mwenye tabia njema na busara ambaye
hutoa ushauri mzuri unaoweza kumsadia mtu kupata mafanikio katika maisha.
SEHEMU B (Alama 25)
Jibu maswali yote katika sehemu hiii
3.
Kwa kuzingatia
tungo ulizopewa, bainisha aina za maneno
i.
Juzi tulishiriki
maandamano ya amani.
ii.
Kucheza kwake
kunaburudisha.
iii.
Kijana mlevi
amepata ajali.
iv.
Neema alikuwa
amekwisha kwenda kulima shambani.
v.
Wale vikongwe
wamepata ajali.
vi.
Mawazo haya si
yangu.
vii.
Amekwenda
shambani japokuwa ni mgonjwa.
viii.
Kikombe hiki
kitawekwa ukumbini jioni.
ix.
Mtoto mdogo
atakuja kesho shambani.
x.
Baba mdogo
ameleta zawadi nzuri nzuri sana.
4.
Unganisha tungo
zifuatazo kwa kutumia O-rejeshi
a)
Mafisadi
wametoroka. Mafisadi wamekwenda ulaya.
b)
Mbuzi
amenunuliwa. Mbuzi yupo zizini.
c)
Mchezaji
amesajiliwa. Mchezaji anacheza vizuri sana.
d)
Hukumu imetolewa.
Hukumu ni ya haki.
e)
Gari limeondoka
jana. Gari limepindukaleo alfajiri.
5.
Bainisha makosa
yaliyopo kwenye sentensi zifuatazo na uyasahihishe.
a)
Kuna baadhi ya
watu wengine wanaodhani dunia ni ya tambarare.
b)
Nimekuja hapa ili
kusudi niongee na nyinyi.
c)
Sijala tena
samaki wa kupika, hi ni mara yangu ya kwanza.
d)
Kwa kuwa nimeamka
sasa hivi, hebu unisubiri nikaoshe uso.
e)
Wakati huu aidha
yuko kazini au yuko mjini.
6.
Changanua
sentensi zifuatazo kwa kufuata maelekezo ya kila sentensi.
a)
Mwalimu
nafundisha darasani lakini watoto wake walikua wanaimba nyimbo nzuri sana
(mishale/mistari).
b)
Ng’ombe mweupe
aliyenunuliwa juzi jioni atachinjwa kesho alfajiri (Matawi)
c)
Walimu walikua
wanataka kwenda kucheza mpira uwanjani (jedwali)
d)
Wanafunzi
waliokuja jana wameondoka leo asubuhi na mwalimu wao ataondoka kesho jioni
(Matawi)
e)
Mtoto mwerevu,
mrefu, mweupe, amesafiri kwenda kagera leo asubuhi.
SEHEMU C (Alama 10)
MAENDELEO YA
KISWAHILI
7.
“Waingereza,
wajerumani, waarabu na wamisionari wanastahili kulaumiwa sana kwa kupotosha
uhalisi na kuduma lugha ya Kiswahili”. Thibitisha dai hii kwa hoja na mifano
kuntu.
SEHEMU D (Alama 10)
UANDISHI
8.
Andika kumbukumbu
ya kikao cha mahafali yenu ya kuhitimu kidato cha nne. Kikao hicho kilifanyika
tarehe 10/7/2017 katika ukumbi wa DIOMOND JUBILEE UPANGA.
SEHEMU E (Alama 45)
FASIHI KWA UJUMLA
Jibu maswali matatu katika sehemu hii, swali la kumi
na mbili ni la lazima.
9.
Kwa kuirejea
Tanzania ya leo fafanua jinsi waandishi wa tamhiliya mbili ulizosoma
walivyopambana na maadui wa jamii. Toa hoja nne kwa kila tamthiliya.
10.
Maranyingi
waandishi hutumia jazanda katika kazi zao lakini maudhui halisi ya jazanda hizo
ni maisha halisi ya mwanadamu. Thibisha dai hili kwa kutoa jazanda nne kwa kila
diwani huku ukirejea maisha halisi ya jamii yetu.
11.
Chagua wahusika
wawili mmoja toka kila riwaya kasha fafanua namna walivyochorwa kwa kuzingatia
mienendo na matendo ya binadamu halisi katika maisha ya jamii ya kitanzania.
Toa hoja tatu kwa kila mhusika.
12.
Uhai wa fasihi simulizi hutokana na sifa kadhaa,
kwa kutoa hoja tano madhubuti jadili dai hili.