KI 311:SEMANTIKI NA PRAGMATIKI KISWAHILI
SEMANTIKI NA
PRAGMATIKI KISWAHILI
SEMANTIKI
Semantiki ni nini?
Wataalamu
mbali wanakubaliana kuwa:- Ni utanzu wa
Isimu unaochunguza maana katikalugha za binadamu.
:
Ni utanzu wa Isimu unaoshughulikia maana katikalugha. Taaluma hii hufanya kazi ya kuunganisha Tanzu
nyingine za Isimu.
Mofolojia
Ø ALAMA / ISHARA NA
MAANA.
Taaluma
ya Semantiki ni sehemu ndogo tu ya taalumapana zaidi iitwayo SEMIOLOJIA
(Semiolojia/Semiotiki)
Ø SEMIOLOJIA
Ni
taaluma inajikita katika kuchambua mfumo wa alama na Ishara kwa ujumla.
Semiontiki
huchunguza alama na Ishara za lugha za binadamu na maana zake. Inaangalia alama na Ishara zinavyotumika
katika kuashiria maana.
AINA
MBALI MBALI ZA ALAMA NA ISHARA
Kuna aina 3, Alama na Ishara.
Ishara hutumika kimbadala
i) Ishara
za usababisho (Index)
ii)
Ishara za ufananisho (Incons)
iii) Ishara nasibu (Sambolo)
ISHARA ZA
USABABISHI
Ni
Ishara ambazo kunakuwa na ufungamano wa kiusababisho kati ya ishara na
kinachoashiriwa
Mfano
Moshi - Ishara ya moto
Mawingu
–
Mvua
ISHARA ZA UFANANISHO
Ni
Ishara ambazo kunakuwa na ufanano wa kipicha kati ya ishara na kile
kinachoashiriwa
Mfano Mchoro wa Ke na Me
katika milango ya vyoo, michoro hiyo inatoa maana hapa ingia Ke tu au Me tu.
Kiti na kiti chenyewe, Meza na Meza yenyewe –
ukiona Ishara / Alama unapata picha ya kitu halisi.
ISHARA
NASIBU
Ndio
zinzo chunguzwa zaidi na taaluma ya semantiki kwani ndizo zinanzojikita katika
lugha. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja
kati ya ishara na kituchenyewe kinachoashiriwa hivyo uelewekaji wake hutokana
na mazoea ya jamii.
Alalma
nyingi za lugha zipo katika kundi hili.
Mfano Bendera - Nchi
Fulani
Rangi nyekundu - Upendo
au hatari
AINA ZA MAANA
Kwa
mujibu wa Leech (1981) ambaye ana ainisha aina 7 za maana.
1. Maana
ya Msingi (conceptual meaning) Denotative / cognitive)
Hii ndio maana kuu ya neno isiyobadilika
kutokana na mazingira.Aina hii ya maana hufafanuliwa kwa kuangalia nduni bainifu
zinazobainisha kitu kinachotajwa na neno husika.Nduni bainifu ni sifa za msingi
za neno au alama ambayo imetumika.Kwa lugha ya kisematiki nduni bainifu hujulikana
kama vijenzi emantiki.
Hivyo maana ya msingi ya neno Fulani hufafanuliwa
kwa kuangalia kuwapo au kutokuwapo kwa vijenzi semantiki ambavyo vinajenga
msingi wa kitu kinachofafanuliwa na neno hilo.
Mfano Mwanamke - + Binadamu / mtu
+ Mzima
+ Ke
·
Me
Mwaname - + Binadamu /
mtu
+ Mzima
+ Me
·
Ke
Shoga - + Binadamu
/ mtu
+ Mzima
+ Me
·
Ke
2.
MAANA DOKEZI (Connetative
meaning)
Ni ile maana ambayo hupatikana kwa njia ya
kitu kingine maana hii hutokana na sifa
kuu 3:-
a)
Sifa
ya Kiumba ya kitu
Sifa za umbo za kitu kinachodokeza maana ya
kitu kizima yaani sehemu ya kitu fulani inayo ashiria kitu kizima.
Mfano Ndevu - Mwanaume
Sehemu
to ya Me inafafanua kitu kizima ya Me.
Mimba - inaashiria Ke
Maziwa - Ke
Hivyo sehemu ya
kitu fulaniambayo inaishiria
b)
Sifa
za Kisaikolojia za kitu.
Mfano Huruma,
Upendo, Uvuilivu, Heshima Maneno hayu yanamrejelea Mwanamke.
c)
Mitazamo
ya watu kuhusu kitu hicho
Mfano Mwoga, dhaifu, Mwepesi kulia,
Asiye na msimamo - Mwanamke
* Kalam - Elimu
3.
MAANA MTINDO
Ni maana inayohusisha Muktadha wa
kimatumisi Inahusisa mitindo mbalimbali ya matumizi ya lugha. Baadhi ya mitindo hiyo ni mitindo ya
kilahaja, kiwakati, kieneo / Taaluma au famine kihadhi, kiuwasilishaji, Binafsi
n.k.
Kuna namna tunavyotumia lugha
kutegemea na mtindo
Mfano Juma
ni mshenzi wa hesabu
Maana ya
msingi ya Mshenzi ni tusi
4. MAANA HISIA
Ni maana inayotegemea hisia au mtazamo wa
msemaji kuhusu kitu anachokizungumza.
Maana hii hujengwa kwa namna mbili:-
(a)
Kwa
kutumia maana ya msingi au dokezi
- Unahusisha
maana ya msingi ya hivho kitu a unahusisha sifa za maana dokezi
Mfano Wewe Mwanamke kweli kweli
- Ke wa tofauti
- Jasiri
- Hodari
Lakini hapa anaonyesha hisia
Mfano Mume wangu amekuwa samba.
- Mkali
(b)
Kwa
kutumia njia isiyo ya moja kwa moja kutoa ujumba au hisia zako.
Mfano Wanafunzi
wanapiga kelele – unawambia ongezeni kelele kidogo
5. MAANA TANGAMANI (Collocational meaning)
Ni maana inayopatikana katika mktadha wa
kimatumizi kwa kuangalia jinsi maneno mawili au zaidi yanavyotangamana yaani
yanavyokubali kutumika pamoja ili kuleta maana fulani iliyokusudiwa.
Mfano Msichana
- Mrembo
Mvulana
Mtanashati
Usiku
wa Manane
Mchana Kutwa
Uwiku
Kucha
Mchana Kutwa
Kujifungua
Binaadamu
Kuzaa Mbwa
6. MAANA MWANGWI (Reflected meaning)
Ni maana inayopatikana kwa kuhusianisha
maana moja na dhana nyingine ya kitu kile kile yaani maana moja inaakisi maana
nyingine.
Mfano Ejaculate - Ejaculation
Erect - Erection
Hapa awali yalikuwa na maana zake mfano
Ejaculate - kuondoa
Erect - kusimamisha kama vile jengo. Maana hizi za msingi zilianza kupata maana
Mwangwi.
Maana mwangwi zimepata mashiko zaidi hadi
sasa
Mfano Tia, Simamisha, Panua, Comeka, Ingiza
Maneno haya yamepata maana mwangwi
ambazo zimekuwa na mashiko zaidi.
7. MAANA DHAMIRA (THEMANTIC MEANING)
Ni maana ambazo hutegemea kile ambacho
msemaji au mtoa ujumbe anakusudia kukipa umuhimu mkubwa au kukipa msisitizo
mara nyingi kwa kukitaja mwanzoni.
Mfano 1. Mtoto
amevunja kikombe
2. Kikobe kimevvunwa na mtoto
3 Msichana yumo darasani
4. Darasani kuna msichana
Sentensi 1. Msisitizo ni
nani amevunja
2. Nini kimevunjwa
3. Nani yumo darasani
4. Wapi mahali alipo msichana)
Kwa
ujumla Aina za maana zimegawanyika katika sehemu kuu 2 :-
1. Maana ya msingi
2.
Maana ya ziada
DHANA ZA UTAJO, UREJELEO NA FAHIWA
Dhana
hizi zinauhusiano wa moja kwa moja na maana
UTAJO (Denotation)
Ni
uhusiano baina ya Leksimu au kipasho cha kiisimu (Expression kiyambo cha lugha)
na seti ya vitu ambavyo vinarejelewa na Leksimu Meza ni vitu vyote katika
dunia ambavyo kwa hakika vinaitwa Meza.Utajo wa Leksimu Nyumba ni
viu vyote katika dunia ambavyo kwa hakika vinaitwa Nyumba.
UREJELEO
Ni
uhusiano baina ya viyambo vya kiisimu au vya lugha na viwakilisho vyake duniani
wakati maalum wa semo au usemi wako. Ili uhusiano huo uwe na urejeleo lazima
uoneshe umahususi Mfano Kiti hiki, kiti cha miguu minne, meza ya mviringo.
Mfano Mwanamke huyu
Utajo
wa Leksimu nyumba Urejeo wake Nyumba ya msonge.
FAHIWA
Ni
seti ya mahusiano yaliyopo baina ya kiyambo kimoja na viyambo vingine katika
lugha au seti ya mahusiano katik ya neno
moja na jingine katika lugha .Mahusiano hayo huitwa mahusiano ya kifahiwa au
mahusiano ya Kisemantiki.
Mahusiano
ya kifahiwa ni kama vile Usinonimia, Unyume, Utata n.k.
Mfano
Pesa, hela, fedha - Maneno haya
yanauhusiano wa kifahiwa unaoitwa Usinonimia na maneno yenyewe yanaitwa
Sinonimia.Chini, juu Uhusiano wa Unyume.
Utajo
wa Urejeleo huhusu vipengele vya lugha na nje ya vipengele vya lugha lakini fahiwa
inhusu vipengele ndani ya lungha.
Tofauti
kati ya utajo na Urejeleo Utajo ni wa jumla lakini Urejeleo ni mahususi yaani wakati
maalum wa semo.Dhana hizi hutusaidia kufafanua maana katika lugha.
NADHARIA ZA
MAANA
Zipo
nadharia nyingi zinazojadili masuala ya maana.
Hii ni kutokana na:-
Dhana
yenyewe ya maana ni tata na telezi na ni vigumu kusema maana hasa nini?
Kuna
nadharia 4 ambazo tunaziteua
i) Maana kama kitajwa au kirejelewa
(referencial)
ii)
Maana kama dhana / Tasurira (Idiotional)
iii)
Maana kama mwitiko (Behavioral)
iv)Maana
kama matumizi (operational au contextional
than of meaning)
1. MAANA
KAMA KITAJWA AU KIREJELEWA
Nadharia
hii inadai kuwa maana ya umbo la kiisimu hurejelea kitu halisi kinachotajwa na
umbo hilo. Maana ni kitu halisi
kinachorejelewa na neno hilo au umbo hilo la kiisimu. Hivyo basi kama umbo lolote la kiisimu lina
maana basi lazima liwe na kirejeleo chake.
Nadharia
hii inasisitiza kuwa kama maumbo 2 yanatenelea kitajwa kile kile basi mambo
hayo yana maana moja.
Nadharia
hii inahusu hasa majina maalumu ambayo hutokwa kipekee na kuwakilisha kitu
halisi.
UBORA
i) Ni kweli kwamba
lugha ina kiambo ambacho tuaweza kupata maana kwa kuirejelea latika mazingira
halisi.
MAPUNGUFU
i) Sio kila Leksimu au kiambo chake japo maneno
mengi katika lugha yenye maana pasipo kuwa na verejeleo vyake . Mfano Viunganiuhi -
kwa, na, ya - vibaisahi hivi havina viwakilishi vyake.
ii) Tunaweza kuwa
na viamb matamko maweili au zaidi
yanayorjelea kitajwa kimoja lakini si lazima matamko hayo yawe na maana sawa.
Mfano
Mtu anaweza kuitwa /
kurejelewa kwa jina lake, cheo cha kazi, cheo cha uzazi n.k. nab ado akawa ni
mtu yule yule japokuwa maana za maneno yaliyotumika ni tofauti.
Mfano - Mwalimu
Kibiki
- Mwalimu wa DULE
- Mke wa Mbata
- Mwanachama wa UDASA
- Mwalimu
Mlezi wa CHAWAKAMA
- Mwenyekiti wa kikundi cha kina mama
iii) Kuna maneno ambayo hayarejelei kitu
kinachotajwa ingawa htumia tamko au jina la kitu hicho.
Mfano Kupe - John ni kupe
- kupe mduu
-
Unyonyaji
Utapaswa useme - John
ni mdudu anayeitwa kupe
iv) Kunamaneno yanayotaja vitu dhahania
hivyoni vigumu kurejea vitu halisi vinavyo rejelea kitu dhahania.
Mfano Shetani, Uchovu, Furaha, Huzuni,
Malaika
2. MAANA KAMA DHANA
Nadharia hii inadai kuwa maana au
taswira inayoibliwa na umbo hilo la kiisimu akilini mwa wana lugha pindi umbo
hilo la kiisimu litumikapo, yaani maana ni picha /Taswira zinazoibuliwa pindi
umbo la kiisimu linapotumika.
Hivyo badala ya kuhusisha maana na vitu
halisi moja kwa moja nadharia hii inahusisha maana na wazo ama Taswira. Viambo dhahania kama mallaika, shetani, upepo
hapa zinaweza kupata maana kwani mnaangalia kitu mmoja ana picha au Taswira
gani kujusiana na dhana hiyo.
Nadharia hii inaisitiza kuwa mawasiliano
hujafanikiwa pale ambapo maneno au kiambo huchochea mawazo sawa kati ya msikilizaji
na msemaji.
Hivyo hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati
ya neno au umbo hilo a kiisimu na kitajwa halisi lakini uhusiano upo kati ya
kitajwa na Taswira halisi aliyonayo mtu.
UBORA
i)
Kwa
kiasi Fulani maana hutokana na dhana na
ndio maana vitu dhahania huweza kupata maana.
UDHAIFU
i)
Nadharia
hii inaibua maswali mengi:-
Wakati mwingine
hutofanana
Nani huamua kuwa
dhana hiyo ni kweli kama ilivyotumika
ii)
Tunaweza
kuwa na dhana tofauti juu ya kitu kilekile
Maumbile
iii)
Si
kweli kwamba kila kiambo kina husishwa na Taswina mfano na, lakini, ingawa.
3. MAANA KAMA MWITIKO
Mwasisi wa nadharia hii ni
Bloomfield – alliasisi 1935
Nadharia hii imetokana na wana Utabia
(behaviourism) kama B.F Skinner, Parlon waliofanya utafiti kwa wanyama.
Misingi ya nadharia ni kwamba Tamko
huwa ni kichocheo ambacho huamsha mwitiko kwa msikilizaji. Nadharia inahusu hasa kila mtu anavyoitikia
katika nafsi yake yaani kila mtu anaposikia neno Fulani huibua hisia Fulani
ndani ya nfsi yake inayomfanya aitikie maana ya neno hilo.
Nadharia hii uliona neno kama
kichocheo na maana ni ule mwitiko hivyo maana ya kitu au Tamko fulani ule
mwitikio wa msikilizaji.
UBORA
i)
Kwa
kiasi fulani una ukweli kwa sababu mwitiko unaweza kutusaidia kupata maana.
UDHAIFU
i)
Namna
watu wanavyoitika si sawa wakati wote.
Watu huweza kutika tofauti tofauti kwa tamko hilo olo moja.
ii)
Yapo
maneno ambayo ni vigumu kupata miitikio yake
Mfano - Viunganishi
- na, kwa, ingawa, ni vigumu
kutenda tendo
lolote linalotokana na mneno hayo pia maneno dhahumia .
Mfano - Njaa
iii)
Nadhani
hii inakazia zaidi mwitiko na kusahau kuwa lugha ni chombo kinachohusisha jamii
nzima
4. NADHARIA YA MAANA KAMA MATUMIZI
Mwasisi wake ni Ludwig Wittegn
(1953).Katika kitabu chake “Philosophical
Investigation”.Alifanya mapinduzi makubwa katika kueleza maana.
Anasema ni kosa kubwa kuweka mipaka ya
maana kama ambavyo nadharia ya maana kama kitajwa, Maana na Mwitiko
zinavyofanya “Kwani kufanya hivyo ni sawa na kuweka mipaka ya thamani ya umbo
lenyewe la kiisimu. Kinachopaswa kuzinyatiwa ni matumizi yaani jinsi neno au
kiumbo cha kiisimu kinavyotumika. Haina
haja ya juuliza neno hili lina maana gani bali angalia neno hili linatumikaje.
UBORA
i)
Inasaidia
kuondoa uvulivuli wa maana za maneno kwa kujikita katika mktadha wa kimatumizi.
ii)
Nadharia
hii haibagui umbo lolote la kiisimu, maneno ambayo hayajengi, taswira, dhana
yeyote inaweza kupata maana kulingana na matumizi yake.
UDHAIFU
i)
Baadhi
ya wanaisiimu wanahoji kuwa Nadharia hii haiweki wazi mipaka ya kimatumiz. Je mipaka ya kimatumizi ni ipi?
ii)
Kuna
mamemo ambayo yanaweza kupata maana kabla ya matumizi.
Mfano vifaa vya kieledromic
vinavyogunduliwa, mfano Kinukushi – Fax
Je ni namna / Nadharia ipi ni Bora kwa
kueleza Maana?
SEMANTIKI YA MANENO
Tutajikita
kuangalia maana katika ngazi ya neno na sentensi
1. SEMANTIKI
YA MANENO VIKOA VYA MAANA
Dhana hii inahusu mahusiano na mpangilio wa
msamiati wa lungha. Maneno katika lugha
yeyote hayapo kiholele bali yapo katika
utaratibu au mpangilio maalum.
Wanasemantiki wanaamini kuwa “Maneno yangekuwa yanaonekana katika ubongo
wa binadamu basi maneno hayo yangeonekana yakiwa yamepangwa katika makundi
madogo madogo kulingana na jinsi maneno hayo yanavyohusiana.
Hayo makundi madogo madogo ya
kidhahania ya maneno yaliyojitenga kulingana na mahusiano yake ndiyo huitwa
Vikoa vya Maana.
Mfano wa Vikoa vya maana, kunakuwa
na Neno kuu na Memba wa kikoa hicho
Mfano Wanyama - Simba,
Pak, Mbwa, Kunguni
Matunda -
Embe, Pela, Nanasi
Nyani - Sokwe,
Kima, Tumbili, Komba, Ngedele
Mbwa - Mbwa,
Mbweha, Fisi, Mbwa mwitu
Embe - Dodo,
Embe maji, Ng’ong’o
Chungwa - Chungwa,
Limau, Chenza Ndimu
Kikao cha thamani za kukalia kiti,
sofa, kochi
Rangi - Nyeusi, Nyeupe, Nyekundu n.k.
SIFA ZA VIKOA VYA MAANA
i)
Maneno
yaliyo katika kikoa kimoja yanauhusiano wa kisiganifu yaani kuwa na ufanano
kimaana na kutofautiana pia.
Mfano Samani
inajumuisha vitu vyote vinavyotumika kukatia lakini ukiangalia kimoja kimoja na
matumizi yake vinatofautiana.
2. Kikoa kimoja kikubwa au kipana huweza
kuwa na vikoa vidogo vidogo vya maana ndani yake.
Mfano Wanyama
- mbali
mbali tunaweza kuchukua kikoa kidogo tukapata vikoa vingine.
3. Maneno katika vikoa Fulani hayana
mpangilio maalumu yaani hakuna utaratibu maalum wa neno lipi lianze na lipi
lifuate.
Angalizo : Upo mpangilio maalum katika Vikoa vya siku,
miezi, mwaka na vipimo mbalimbali.
MAHUSIANO YA KIFAHIWA
Mahusiano ya kifahiwa ni seti ya mahusiano
yliyopo baina ya kiambo kimoja na kingine au neno moja na jingine. Mahusiano ya kifahiwa yapo ya aina sita:-
i)
Usionimia
/ Usawe
ii)
Uantonimia
/ Unyume
iii)
Uhomonimia
iv)
Upolisemia
v)
Umenonimfa
vi)
Uhiponimia
USINONIMIA / USAWE
Ni mahusiano ya kimaana baina ya maneno
mawili au zaidi ambapo maana ya maneno hayo huwa ni sawa au hukaribiana.
Maneno yenye maana sawa au maana
zinazokaribiana huitwa Usawe au Usinanimia.
Mfano Pesa,
hela, fedha maneno haya yanauhusiano wa Usinonimia au Usonee kwani maana zake hukaribiana.
AINA ZA SINONIMIA
i)
Sinonimia za kimantiki /logica /
synomimes.
Ni sinonimia zinazotokea pale ambapo
leksimu mbili au zaidi huweza kubadilishana nafasi katika sentensi afifu zhote
pasipo kuathiri masharti ya ukweli ya sentinsi hizo.
Mfano -Lengo,
Kusudi, Nia, Dhumuni, Mama anatembea pole pole / Taratibu. Haraka haraka, Upesi upesi.
ii)
Sinonimia
Kuntu (Absolute Synomimes)
Ni Sinonimia ambazo hutokea pale ambapo
Leksimu mbili au zaidi huweza kubadilisha nafasi katika miktadha yote bila
athari yeyote ya maana. Watafiti wanakubaliana
kuwa hakuna lugha yeyote duniani yenye sinonimia kuntu.
Hivyo ni vigumu kupata maneno yenye maana
sawa kwa asilimia moja.
“Eneo moja wapo linaloaza kuwa na Sinonimia
kuntu ni eneo la Silabi”
Mfano Ving’ong’o
au Nazali wakati wote vinaweza kubadilishana
Sintaksia - Saruji
miundo
Fonolgia -
Mofolgia
Elimu viumbe - Baiologia
VYANZO VYA SINONIMIA / SABABU
Habwe ba jaranja
i)
Ukopaji
wa misamiati
Maneno yakiwa na asili tofauti huleta hali
ya Usinonimia.
Mfano Neno
Shule limetoholewa toka lugha ya kijerumani “Schule “ lakini kuna neno “Skuli “
hili limtokana na School la kiingereza.
Maneno haya yanatumika katika lugha ya
Kiswahili wengine wanatumia Skuli na wengine Shule/
ii)
Jinsia
Hutokana na maneno yanayolejelea ama
mwanmke au mwanaume.
Mfano Hali
ya kutokuwa na uwezo wa kuzaa kwa m-ke ni Utasa na Ugumba kwa mwanaume. Msichana mrembo lakini Mvulana mtanashati
Mwanamke aliyefiwa na mume - Mjane
Mwanaume aliyefiwa na mke -
Mgaje
Mwitiko Abee na Naam
iii)
Tofauti
za kijiogorafia au Maeneo Wazungumzaji
wa lugha moja ambao wanaisi katika
maeneo tofauti ya kijiografia wanaweza kuwa na maneno tofauti yanayorejelea
dhana au kitu kile kile.
Mfano Zanzibar
- Markiti
Tanzania
bara - Soko
Tanzania
bara - Umeme
Kenya
- Stima
Tanzania - Bomba
Zanzibar
- Mfereji
Tanzania - Dala dala
Kenya - Matatu
iv)
Taaluma
au Uwanja
Taaluma mbili mbili huwa na maneno mbali
mbali yanayotumiwa kurejelea kitu au dhana ile ile.
Mfano katika
riwaya kuna Aya lakini ushairi kuna Ubeti, maneno hayo yote
hutejelea kitengo au mfululizo wa maandishi.
v)
Wakati
Baadhi ya Sinonimia huzuka kutokana na
wakati.
Mfano Habwe
na Karanja
Kuna neno kama soko kuna mahali liliitwa Utuku
Mfano Zamani
wanyonyaji - Mabepari kwa sasa Mafisadi
vi)
Urasimi
Tunarejelea neno lipi ni sanifu kuliko
lingine
Mfano Hela,
fedha, pesa – neno rasmi ni fedha
Mpumbavu, mjinga – yanaonekana
rasimi kuliko fara, bwege n.k.
vii)
Ujumla
na Umahususi yapo maneno ambayo hutumika
kwa jumla na wakati mwingine hutumika kwa umahususi
Mfano Hamu neno la jumla
kiu – kinywa, njaa.
viii)
Rika
au Umri
Tofauti za umri na rika, yapo maneno ambayo
yanaonekana ni ya kitoto zaidi mengine ni ya kiutu uzima.
Mfano Piga - mtu mzima / kutandika chapa – mtoto
ix)
Elimu
au Hadhi
Watu wenye elimu tofauti tofauti hutumia
maneno tofauti, wakati mwingine huwa ni kutofautisha.
Mfano neno Afya – kawaida na Siha – kitaaluma njema
x)
Dini
Dini tofauti huwa na maneno tofauti kwa
ajili ya kuelezea dhana zinazolingana hasa Waislamu na Wakristo
Mfano Dhana ya kujinyima chakula kwa
minajili ya kupata fadhila za kidini Waislam
- Saumu na Wakristo - Kwaresma
Mahali pa kuabudia Wakristo - Kanisa
Waislamu – Msikitini,
Sala - Swala
NAMNA YA KUBAINI
KAMA NI SINONIMIA KUNTU AU SIO KUNTU
Kuna mbinu kuu 2:-
i)
Kuangalia
miktadha mbalimbali ya matumizi husika ya Sinonimia
ii)
Katika
mazungumzo au katika maandishi
1. KUANGALIA MIKTADHA MBALIMBALI YA
MATUMIZI YA SINONIMIA HUSIKA KATIKA MAZUNGUMZO AU MAANDISHI
Mfano Fahamu, Jua, Elewa,
je maneno haya yanatumika kote
·
Nilielewa
atakuja, Nilifahamu atakuja
-
Muasherati, kahaba, mzinzi - utofauti kidogo kimaana
2. *
Kutunga sentensi kahaa tofauti kwa kutumia kila Sinonimia kwa sentensi
moja kishi kubadilisha nafasi ya kila Sinonimia katika sentensi hizo na kuweka
Sinonimia nyingine
Mfano -Shimo, Tobo, na Tundu
i)
Hamis
alichimba shimo.
ii)
Suruali
ya Festo ina tobo
iii)
Chandarua
change kima matundu mengi
iv)
Ni
rahisi ngamia kupenya kattika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika
ufalme wa Mungu.
Hizo ni Sinonimia lakini sio Sinonimia
Kuntu.
Shimo
- kubwa, Vifaa jembe n.k.
Tundu
- Dogo zaidi
UANTONIMIA / UNYUME
Ni uhusiano wa kimaana baina ya maneno
mawili ambayo maana zake ni vinyume yaani maana ya neno moja ni kinyume cha
maana ya neno jingine
Mfano Neno - Nenda - Rudi Cheka - Lia Kubwa - Dogo
Kuna aina kadhaa
AINA ZA UNYUME AU UANTONIMIA
i)
Unyume
kamilishani / complimentary or simple antonyms.
Ni Unyume ambao unampaka usiopitika ambapo ukanushi wa upande mmoja ni
unenetezi wa upande wa pili
Mfano Mwanamke
- Mwanaume
Hai - Mfu
Pata - Kosa
Kweli
- Si kweli
ii)
Unyume
kadilifu (Gradable)
Ni unyume ambao hamna mpaka usiopitika
hivyo huweza kuelezwa kwa makadirio yaliyopo baina ya pande mbili husika. Ukamohi wa upande mmoja si lazima uwe ni
unenko wa upande mwingine (wa pili) kubwa
- ndogo si lazima kinyume cha
kubwa iwe ndogo kwani inaweza kuwa ndogo wastani n.k.
Zito
- nyepesi inaweza kuwa nzito
wastani n.k..
iii)
Unyume
elekeana (Relational Antonyms)
Ni unyume unaokuwepo pale ambapo uhusiano
baina ya leksimu mbili katika jozi huwa ni wa kiuelekeano yaani Leksimu
nyingine kutegema na Uelekeo yaa upande ambako tendo linaelekewa.
Mfano Nenda - Rudi -
Uelekeo Fulani yaani tenda linaelekewa wapi
Panda - Shuka
Sukuma - Vuta
Kushoto - Kulia
Mbele - Nyuma
Juu - Chini
Chomeka
- Chomoa
iv)
Unyume
Rejezi au Tenduzi
Ni unyume ambao huhusisha Leksim ambayo
kwazo tendo la Keksim mojawapo kuweza kubadilishwa ili kurejelea kinyube chake.
Mfano Chomoa - Chomeka
Ezeka - Ezua
Ziba - Zibua
UHOMONIMIA
Ni hali au uhusiano ambao umbo moja la
kiisimu huwa na maana nyingi zisizohusiana.
Mfano Panda
·
Kusia
mbegu
·
Kwea
mlima au mti
·
Tawi
la mti
Kaku
·
Ugonjwa
wa vidole
·
Ganda
la yai
·
Ndugu
mkubwa wa kiume
UPOLISEMIA
Ni Sifa ya neno moja kuwa na maana nyingi
zinazohusiana, au ni hali ya neno kuwa na maana nyingi zinazo husiana yaani
maana inakuwa moja lakini inahusiana na vitu vingi
Mfano Mdomo
(N)
wingi wake midogo
i) Ni sehemu ya nje ya kinywa inayomwezesha
kiumbe kupitisha
kitu chakula.
ii) Uwazi wa kitu
kama chupa ya birika n.k.
iii) Kinywa
Kichwa
i) Ni sehemu ya mwili wa kiumbe hai
ii) Ni injini ya gari moshi inayokokota mabehewa
iii) Ni kiongozi wa
familia
iv) Mtu hodari sana katika masomo
UHIPONIMIA
Ni uhusiano wa kiwima baina ya Maneno ambapo fahiwa ya neno moja hujumuishwa
katika fahiwa ya neno jingine.Ina maana kwamba maana za neno Fulani ni sehemu ya
maana y neno jingine. Kuna neon moja jumuishi
na madogo madogo na ili uelewe maana ya neno kubwa lazima uhusishe maneno
madogo madogo.
Neno lenye maana pana huitwa neno jumuishi
nayale yenye maana finyu huita Haponimia
Ndizi Chungwa Embe Parachichi
Fahiwa ya neno Ndizi ni sehemu ya fahiwa ya
matunda hivyo ukitaka kuifasili ndizi utasema ni aina ya matunda, ili uweze
kuelewa maana ya ndizi, chungwa, embe, parachichi ni sehemu ya fahiwa ya neno
jumuishi ambayo ni Matunda
UMERONIMIA
Ni uhusiano ulipo baina ya Leksimu
inayotaja sehemu na ile inayotaja kitu kizima.
Mfano Mwili
-
Shingo
-
Kichwa
-
Mabega
-
Miguu
-
Tumbo
Meronimia inahusu kitu na sehemu zake,
nikitaka kujua kichwa ni nini nitarejelea sehemu mbali mbali za kichwa
MAANA KATIKA NGAZI YA TUNGO AU SENTENSI
Kuna vipengele 5
i)
Usawe
ii)
UtataUkinzani
iii)
Ukinzani
iv)
Upotoo
v)
Uziadu
– dufu
USAWE
Ni uhusiano baina ya sentensi mbili au
zaidi zenye kudhihirisha maana moja ya msingi.
Mfano Sikujua
kwamba usingeongea naye abadani
Sikufahamu kuwa usingezungumza naye
katu
Katika sentensi hizimaneno yanaetofautiana
lakini maana ile ile
-
Maelezo
yako yalikuwa magumu kueleweka
-
Ilikuwa
vigumu kuelewa maelezo yake
Katikasentensi hizi kinachotofautisha ni
mpangilio.
AINA ZA USAWE
i)
Usawe
wa kilekisika
ii)
Usawe
wa kimuundo
1.
USAWE WA KILEKSIKA
Ni Usawe unaotokana na sentensi mbili au
zaidi kuwa na maneno yenye maana ile ile ya msingi katika nafasi ile ile.
Mfano Sikujua kwamba usingeongea naye abadani
Sikufahamu
kuwa usingezungumza naye katu
Maneno yaliyotumika katika nafasi ile ile
yanabeba maana ya msingi
2.
USAWE WA KIMUUNDO
Hutokana na maana ya msingi ya sentensi
mbili au zaidi hubaki ile ile japo sentensi zina mpangilio tofauti. Hapa kinachozingatiwa saidi na muundo wa ile
sentensi.
Mfano Maelezo
yake yalikuwa magumu kueleweka
·
Ilikuwa
vigumu kuelewa maelezo yake.
Kilichotofautisha hapa ni mpangilio tu.
Mfano Hakuna
aliyelewa maneno yake ya ajabu
·
Maneno
yake ya ajabu hakuna aliyeelewa.
UTATA
Ni hali ambayo sentensi moja huwa na maana
au tafasiri zaidi ya moja au huwezi kuelewaeka kwa namna zaidi ya moja.
AINA ZA UTATA
i)
Utata
wa Kileksia / Kileksika
ii)
Utata
wa Kimuundo
UTATA WA KILEKSIA
Ni Utata unaosababishwa na matumizi ya
Homonimia na Polisemia
Mfano Baada
ya shida nyingi alifannikiwa kumleta Papa nyumbani
Papa - Mnyama
- Mkuu wa kanisa.
Siku hizi bei ya kanga na sh 10,000
- Ndege
- Nguo.
UTATA WA KIMUUNDO
Hutokana na jinsi sentensi ilivyo pangiliwa
au umbo la neno au kirai kuwa katika nafasi malumu katika sentensi.
Mfano - Wanawake na wanaume waangalifu
walikaa kando.
1. - Wanawake walikaa kando
- Wanaume waangalifu nao walikuwa kando
2. - Wanaume waangalifu na Wanaume
waangalifu walikaa
Kando
* Mtoto alilalia maziwa
- Alikunywa maziwa akalala
-
Alilala juu ya maziwa.
* Ananipenda
zaidi kuliko wewe
- Nyinyi nyote wawili mnanipenda
- Wewe unanipenda lakini mwenzio
ananipenda zaidi yako
UKINZANI
Ni hali itokeayo pendi kiyambo cha lugha
kinapokuwa na sifa Fulani na wakati huo huo hakina sifa hiyo.
Kiambo cha namna hii hunena kwamba mtu au
kitu Fulani kina sifa Fulani na wakati huo huo hakina sifa hiyo.
Mfano Mwanamke
Yule ni mwanamke kweli kweli
+
Me
- Ke
Bibi yangu nikijana kabisa.
+
Uzee
- Uzee
Yule kijana ni mwizi mtakatiu
+ Mtakatifu
- Mtakatifu
Huyu mtoto ni mtu mzima
+
Uzima
- Uto Uzima au
+
Utoto
- Utoto
Nilikwenda mbele nikarudi nyuma
+
mbele
- mbele
UPOTOO
Ni Ukiushi wa kisemantiki utokeao pindi
vijenzi semantiki viwili singanifu vinapounganishwa kueleziea jambo au kitu.
Mfano Alichora
barua kwa guu wa kushoto
·
Viatu
vyake vinacheka
·
Kaptura
yake inwasha taa
·
Kuchora
– haliendani na neno “barua” kifaa kinachotumika kuchora hakiendani na mguu (wa
kushoto)
·
Barua
– haichorwi
Viatu vyake vinacheka
*Matumizi holela ya maneno katika lugha
na husababisha upotoshaji
UZIADA
– DUFU
Ni urudiaji wa maneno usio wa lazima au
usiohitajika ambao hauifany sentensi kueleweka zaidi au haufafanui zaidi maana.
Mfano - Mke wangu ni mke wangu
·
Mwizi
ni mwizi tu
·
Mwanafunzi
ni mwanafunzi tu
·
Mwalimu
ni mwalimu
PRAGMATIKI
Ni tawi la isimu linalohusu maana kama
inavyowasilishwa na mzungumzaji na kutafsiriwa na msikilizaji
Progamatiki inahusu kitu kinacho maanishwa
zaidi a kile kinachosemwa au kuandikwa.
Progmatiki inahusu kinachomaanishwa na
mzungumzaji katika muktadha fulani na namna muktadha unavyosaidia kutafsiri
maana.
Progmatiki ni maana ktika mtagusamo
(meaning in interaction ) maana haijikiti katika maneno pekee wala haichukiliwi
na msemaji pekee na wala haitesemei utashi wa msikilizaji pekee. Kujenga maana ni mchakato chanamni
unaohusisha mnafaka baina ya msemaji, msikilizaji, muktadha wa mzungumzo pamoja
na maana ya msingi ya kilichosemwa.
Wanaisimu – Pragmatiki ni taaluma ambayo inhusu mahusiano yaliyopo baina
ya maumbo au alama za lugha na watumiaji wa maumbo au alama hizo.
Katika Pragmatiki suala la msingi ni
muktadha. Muktadha hutumanishi tu
mahali, sehemu au mazingira ambapo mazungumzo yatafanyika hivyo ni kipengele
kimoja tu katika vipengele vingi.
Muktadha inahusisha yafuatayo:
DHANA YA SKIMA (SCHEMA – SCHEMATA)
Skima ni ramani dhahania zilizopo akilini
mwa binadamu ambzo hutusaidia kupata na kuelewa taarifa mpya. Hizini ramani majumuni za maarifa au utambuzi
ambazo kila mtu anazo akilini mwake. Kwa
kawaida tunatumia skima mara zote tupatapo habari mpya, hivyo skima zetu
huboreshwa na kurekebishwa pindi tupatapo habari au maarifa mapya.
Skima ndizo ambazo hutusaidia kuelewa kile
ambacho kinasomwa katika miktadha mbali
mbali
Mfano Skima zinazohusu watu au tukio kama
vile harusi, akilini utajua ni tukio gani kulingana na jinsi tunavyopata
maarifa mapya.
Mfano Amina aliingia akajazi mahitaji
yake ya wiki nzima katika kapu lake na kuyapakia kwenye torori ambalo
aliliburuza mpaka alipoegesha gari, akapakia kapu garini na kwenda zake.
Katika hali ya kawaida tukio hili
linafanyika sokoni au supermaketi
- Uelewa
huu na maana hii ni kwa sababu ya skima ya sokoni au supermarket
NJIA ZA KUPATA TAARIFA MPYA ZIPO 3
1. Kupokea
na kuhifadhi
Ni kitendo cha kuchukua taarifa mpya na
kujaribu kuhifadhi bila kuifanyia marekebiso au mabadiliko yoyote. Unapopata taarifa mpya unaiimarisha au
kuiboresha skima yako.
2. Kupokea
na kuboresha
Hii hutokea pale uapatpo taarifa mpya na
kisha kuifanyia markebisho kwa sababu haiendani na skima yako iliyopo
3. Kuunda
Upya
Ni kitendo cha kutengeneza skima mpya pindi
hupokeapo taarifa mpya ili kuirekebisha au kuondoa Ukinzani uliopo akilini
mwako.
AINA ZA SKIMA
i)
Skima
ya mtu
ii)
Skima
ya kitu
iii)
Skima
ya tukio
iv)
Skima
ya dhima
1. SKIMA
YA MTU
Ni skima inayohusu sifa ya mtu fulani
mahususi kama inavyofahamika na mtu mwingine.
2.
SKIMA YA KITU
Ni skima inayohusu sifa za kitu fulani
mahususi kama zinavyo fahamika na mtu mwingine
Mfano Meza, Darasa n.k.
3. SKIMA
YA TUKIO
Ni skima inayohusu
mchakato shughuli au njia ya kutenda jambo Fulani
Mfano Msiba, Harusi
4. SKIMA
YA DHIMA
Ni
Skima inayohusu matarajio ya wanajamii juu ya dhima au wajibu wa mtu
fulani katika jamii hiyo.Kila mtu katika jamii ana dhima Fulani ambayo
wanajamii wanatarajia aihimize.
MCHANGO WA
WANAFALSAFA KATIKA TAALUMA YA PRAGMATIKI
Taaluma hii kwa kiasi kikubwa imeathiriwa
zaidi na michango ya wanafalsafa kuliko wanaisimu. Hii imewafanya watukujiuliza Pragamatiki ni
tawi la Isimu au falsafa.
Michango ya wanafalsafa 3 muhimu:-
i)
John
L. Austiri (1962)
ii)
John
R. Searie (1969)
iii)
Herbet
(H.P Grice.) Paul Grice (1975)
JOHN L. AUSTIN (1962)
-
Aliasisi na dharia ya
TENDO – UNENI John R. Searie
- Aliboresha
nadharia ya Tendo Uneni iliyoasisiwa na Austin.
H. P Grice
Ni mwasisi wa kanuni ya
ushirikiano katika mawasiliano.
KANUNI YA USHIRIKIANO KATIKA MAZUNGUMZO
HERBET
PAUL GRICE (1975)
Aliasisi kanuni ya ushirikiano katika
mazungumzo . Aliiasisi katika makala yake iitwayo “Logic and Compesation”
ilihusu Mantiki katika mazungumzo. Kwa
mujibu wa H. P. Grice “kanuni ya mazungumzo inasema “ “Toa mchango wako
katika mazungumzo kadri inavyohitajika
wakati wote uzungumzapo kwa kuzingatia lengo linalokubalika na mwelekeo wa
mazungumzo unaojihusisha nao”.
Hivyo H. P. Grice “Mawasiliano ni kitendo
cha ushirika ambacho kinahitaji jitihada za pamoja kati ya msemaji na msikilizaji”
Pia kuna kuwa na seti ya malengo ambayo
yanafahamika kati ya mzungumzaji na msikilizaji
- Kuna
kuwa na muelekeo wa mazungumounaoelekeza nini cha kusema nini si cha kusema
ktika mawasiliano.
VIKANUNI VYA KANUNI KUU YA USHIRIKIANO (Comperative Principles)
Inajengwa na vikanunu (axims) vidogo vidogo
4:-
1. Kanuni
ya kiasi (maxims of quantity)
Inasema “Toa taarifa inayohitajika
kulingana na lengo la mawasiliano, usitoe taarifa zaidi ya ile inayohitajika na
pugufu ya ile inayohitajika.
2.
Kanuni ya ukweli (maxims of
quality)
Inasema “Usiseme jambo lolote unaloamini
kuwa ni uongo” usiseme jambo uliloweza
kulidhibitisha.
3.
Kanuni ya Uhusiano (maxim of
relation)
Inasema “sema yanayohusiana
na mada au jambo linalozingumzwa”
4.
Kanuni ya Njia au Jinsi
(maxims of manner)
Inasema “Epuka maneno au miundo
isiyoeleweka. Epuka utata, sema kwa
kifupi , sema kwa mpangilio mzuri.
UKIUKWAJI WA KANUNI YA USHIRIKIANO
Pamoja na kwamba Grice anaisisitiza
kanuni ya ushirikiano kwa wasikilizaji
huivunja kanuni hii kwa kuvunja vikamini
vidogo vidogo.
Hali hii ya kutozingatia vikanuni vidogo
vidogo vya ushirikiano anapojitokeza msikilizaji hulipua na kunyamaa maana za
msemaji katika muktadha husika hat kama maan hiyo hikutamkwa na mzungumzaji.
Maana inayobaliwa na kung’amuliwa na
msikilizaji huitwa VIMANILIZI
VIMANILIZI (IMPLICATIVE)
Ni maana anyegundua msikilizaji hata
kama haikuelezwa bayana na msemaji, au
Ni yale yasiyosemwa ambayo tunagundua
kupitia yaliyosemwa, au
Ni kile kinachomaanishwa na msemaji ingawa
hakikusemwa bayana.
Mfano
1. Msemaji
A: Mzee
yupo?
B: Gari lake halipo
Kimanilizi hapa ni
hayupo - Angekuwapo na gari lake lingekuwepo
2. Niliposikia
kuwa mwanafunzi amejinyonga nilijua tu kuwa ametoka Iringa
3. A: Ninaonekanaje leo
B:
Kiatu chako kizuri
Maana
hujapendeza ila tu kiatu chako .
AINA ZA VIMANILIZI ZIPO 2:
i)
Vya
Mazungumzo
ii)
Vya
kaida
VIMANILIZI VYA MAZUNGUMZO
Ni vile ambavyo utokeaji na uelewakaji wake
hutegemea muktadha wake mazungumzo..
Ndio hasa hutokana na ukiukwaji wa kanuni
ya ushirikiano kwa kuvunja vikanuni vyake vidogo vidogo.
Mfano: - Mzee hapo juu
·
Naonekanaje
A - Tutakwenda
kwenye shoo ya Diamond Dar live jumapili usiku?
B - Nina jaribio la semantiki Jumatatu
kimanilizi ni sitakwenda
A: Hilo
dirisha lililowazi linapitisha baridi kalli
B: (Haongei
kitu) – anafunga tu dirisha kwa kutenda)
Kwasababu
anang’amua maana ya msemaji A isiyo ya moja kwa moja.
Kimanilizi
ni fungu dirisha
A: Nimeishiwa
mafuta kabisa katika gari langu
B: Kituo
cha mafuta kiko pale kwenye kona.
A: Umeolewa?
B: Nina
watoto sita
Kimanilizi - Nimeolewa na kwa muda mrefu
- Amevunja
kanuni ya kiasi
A: Vipi
boom limeisha
B: Unauliza
makoji polisi?
A: Mume
wangu kati yangu na bia nani bora?
B: Ebu acha kufananisha mambo ya kijinga
na bia wewe. Kimanilizi – Bia ni bora
kuliko mke.
2.
VIMANILIZI KAIDA (CONVENTANAL)
Ni vile ambavyo upatikanaji, utokeaji na
uelewekaji wake hautegemei kwa kiasi
kikubwa muktdha wa mazungumzo.
Hazitegemei zaidi kanuni ya ushirikiano na
hivyo havitokani na ukiukwaji na uvunjwaji wa vikanuni ya kanuni hiyo badala
yake vimanilizi hivi hutegemea maana ya
kipagmatiki ipatiikanayo moja kwa moja kutokana na maneno fulani fulani yaliyotumika. Baadhi ya maneno hayo ni kama kikini, ingawa,
kwa hiyo, kwasababu japokuwa n.k.
Mfano - Amina ni mchaga kwa hiyo anajua sana
kutafuta hela. Kimanilizi - Wachaga
wanajua kutafuta hela
Kijana Yule ni mfupi lakini sio mbishi hata
kidogo.
Kimanilizi - Wafupi ni wabishi.
- Huyu wa sasa atakuwa mke mwema
kwasababu alizaliwa na kukulia kijijini.
Kimanilizi - Wanawake kutoka kijijini, ndio wema
- Katika harusi ya nuru hata James
alihudhuria
Kimanilizi - Haikutarajiwa James ahudurie katika
harusi hiyo.
NADHARIA YA TENDO UNENI (SPEECHPERIOD)
John Austin (1962) anajadili kuhusu Nadharia
ya TENDO – UNENI katika kitabu chake kiitwacho “How To Do Thing With Word”
(Jinsi ya kutenda kwa kunena). Ndiye
alituzindua kwamba tunweza kutenda matendo fulani fulani kwa kunena tu, yaani
kwa maneno usemayo.
Mfano: - Naahidi kuishi nawe katika shida na
raha.
Ingawa sentensi hizi zipo katika muundo wa
kimaelezo lakini zifanye kazi zaidi ya
kueleza au kuto taarifa ya jambo.
Sentensi hizi ni vitendo au sehemu ya vitendo ambavyo msemaji anatenda
kwa njia ya kusema.
Hii humaanisha kuwa kwa kusema tu sentensi
basi msemaji anakuwa ametenda tendo husika vipengele 2 muhimu:
(a) Sema
tendeshi (Pperfomantive Uherance)
(b) Vitenzi
tendeshi (Performative base)
SEMO TENDESHI
Ni zile ambazo kusemwa kwake ndio kutendwa
kwa vitendo vinavyodokezwa na vitenzi vilivyo tumika katika sehemu hiyo.
VITENDI TENDESHI
Ni vile ambavyo kusemwa kwake ndiyo
kutendwa kwa tendo lililobebwa na kitenzi hicho.
Mfano Ahidi,
Tangaza, onya, Batiza, Pinga, Alika, Kemea, Shauri, Shukuru,
Samehe n.k.
Hata hivyo ni vizuri kwamba si kitu kitenzi
ni tendeshi na si kitu semo ni semo tendeshi hivyo zipo semo na vitenzi ambavyo
si tendeshi kwa sababu kusemwa kwake si kutenda tendo lolote
Mfano: Ninafundisha darasani, Mwajuma
anasema - Hizi ni semo lakini si tendeshi
Soma, fundisha – si
vitendi tendeshi.
MASHARTI YA TENDO
UNENI
Austin anadai leunu
“Matendo Uneni haya kamiliki ati tu mtu Fulani ameona hivyo na
wala haya kamiliki tu kwa semo au vitenzi tendeshi tu
hivyo kuna masharti ambao
lazima yatimia
ndipo tendo uneni husika likamilike.
Masharti hapo katika makundi 3 na
kila kundi lina
masharti mawili.
KUNDI A
a) Lazima
kuwe na utaratibu wa kiulimwengu juu ya utendaji wa tendo hilo na
kwamba athari au
matokeo ya tendo hilo yajulikana mahali pote.
b) Mazingira
na watu wanaohusika katika uneni wa tendo husika lazima wawe
muafaka (rasimi)
Mfano
Hukumu - Atoe hukumu na awe mahakamani
KUNDI B
i)
Utaratibu
wa kutenda au kutekeleza tendo husika lazima ufatwe kwa usahihi.
ii)
Utaratibu
huo lazima ufuatwe kwa ukamilifu.
KUNDI C
i)
Aghalabu
wahusika lazima wawe na mawazo, hisia na dhamira ya kweli ya kufanikisha tendo
husika.
Mfano Naahidi
kukupa million moja mwishon mwa mwezi
- Unapaswa kutekeleza.
ii)
Iwapo
wajibu ambao unatakiwa kutimizwa baada ya tendo uneni unafahamika basi watu
wanaohusika wautimize au wautekeleze.
HALI MARIDHAWA KATIKA MATENDO UNENI
Austini anasema Mbali na masharti ya
matendo uneni, ili tendo uneni litimie lazima kuwa na hali maridhawa
Ni jumla ya vigezo au sifa ambazo teno
uneni husika huhitaji kukidhi ili tendo uneni hilo liwe halali au hilimivu.
a) Hali
za jumla
Hujumuisha wahusika kufahamu au kuelewa
lugha inayotumika.
b) Hali
zinazohusu muda au wakati yaani uzingativu wa muda ambapo tendo uneni
husika linapaswa
kutekelellzlllllllllwa na kukamilika.
Mfano Ahadi -
hukamilika baadaye
Amri
- muda huo huo
c) Hali
za kimaandalizi yaani mazingira au mamlaka ya msemaji katika kutimiza
tendo uneni husika.
d) Hali
zinazohusu dhamira zinahusu msemaji au wahusika kuwa na dhamira ya
dhati katika tendo
litendwalo
e) Hali
madhubuti yaani ubadilikaji wa ukweli wa mambo au ulimwengu baada ya
Uneni
ikilinganishwa na hali iliyokuwa kabla ya tendo uneni.
AINA ZA MATENDO UNENI
Austini (1962) aliainisha aina 3 za
matendo uneni:
i)
Kisemwacho
(semo) Locutionary act)
Huusu usemaji wa sentensi yenye maana
inayoeleweka na yenye kitu kinachorejelewa.
Mfano Ninakushauri
uacha tabia mbaya.
ii)
Lengo
la kusema (illocutionary act)
Huhusu lengo la msemaji atika kile
akisemacho
Mfano Ninakushauri
uacha tabia mbaya - Kuonya au kushauri
iii)
Athari
au matokeo (Perocutionary) ya semo.
Huhusu athari au matokeo ya kile kisemwacho
kwa msikilizaji.
Mfano Ninakushauri
uache tabia mbaya
- Athari itategemea
msikilizaji kama ataacha hiyo tabia au hataacha
Matokeo / Athari inaweza
kuwa yale yaliyokuwa yametarajiwa au kukusudiwa
au la
Ni majibu ya
msikilizaji kimwili kimaneno, kisaikolojia, kiakili n.n.
AINA ZA MATENDO UNENI ZILIZO BORESHWA NA
SEARLE (1969)
Ameboresha za Austina “Searle anasema kuna
aina nyingi za matendo uneni na labda hazina ukomo.
Hii ni kwasababu aina hizo hutegea lengo,
muktadha na hata lugha husika. Searle anapendekeza aina za ziada kama
zifuatazo:
i)
Ahadi
(Commisives)
Ni matendo uneni ambayo humfunga msemaji
katik utekelezaji wa kilichonenwa hapo
baadaye.
Mfano Ahidi,
Zawadia n.k.
ii)
Maelekezo
(Directives)
Ni matendo uneni ambayo hulenga kuchochea
jambo fulani lifanyike na msikilizaji kama atakavyo msemaji.
Mfano Amrisha,
Amuru, Omba, Onya, Shauri, Pendekez, Sihi n.k.
iii)
Hisia
(Expressives)
Ni matendo uneni ambayo huthirisha hisia
imani, mitazamo au mawazo ya msemaji juu ya jambo fulani.
Mfano Fariji,
Laumu, Samehe
iv)
Matamko
Ni matendo uneni ambayo kunenwa kwake
hubadili ukweli fulani wa mambo katika dunia.
Mfano Jiuzulu,
Taliki Talaka, Fungua (mkutano) au funga (mkutano,
hukumu, Oza,
Tangaza n.k.
v)
Uwakilisho
(Representatives)
Ni matendo uneni ambayo hueleza kile
ambacho msemaji huamini kuwa kweli au si kweli.
Hujumuisha maelezo – shadidio, na mahitimisho
Mfano Lulu
hakumuona Kanumba. Wasichana wa mjini
hawana mapenzi ya kweli.
DHANA ZA PRAGMATIKI
UDHANILIZI
Unahusu maana inayoibuliwa katika mktalha
ambao msemaji hudhani kuwa msikilizaji
ana taarifa za awali juu ya kile kisemwacho sasa.
Mfano Simu yangu ni ya kichina taarifa ya awali ni kwamba nina
simu
AINA ZA UDHANILIZI
1)
UDHANILIZI WA KWELI
Ni udhanilizi ambao hujikita katika ukweli
wa mambo ambapo jambo au tukio linalodhanilizwa huwa limetokea au imetendeka
kweli.
Udhanilizi huu una vitenzi maalum kama
vile:
Mfano Sikujua
kuwa Eli ni Mchumba
2)
UDHANILIZI USIOKWELI
Ni udhanilizi ambao hujikita katika taarifa
ambayo kinachodhaitizwa au kinachosemwa hakina ukweli wowote.
Mfano Niliota ni mekuoa.
Udhamilizi hajanisa
3)
UDHANILIZI ULIZI
Ni aina ya udhanilizi ambao hudhaniliza
kwamba kauli inayofuatia neno ulizi ni kweli
Mfano: - Lini ulializa chuo kikuu?
Udhamilizi: - Nilimaliza Chuo
kikuu.
- Mume
wako ameachalini kutembea na watoto wa shule?
Udhanilizi:
i)
Una
mume
ii)
Mume
wako anatabia ya kutembea na wanafunzi
UOLEZI
Ni uoneshaji maalum wa vitu, watu, mahali,
hali n.k. katika muktadha husika kwa kutumia maneno yaani violezi.
Ni tofauti na uoneshaji wa kawaida ambao
hutumia viungo vya mwili hususani vidole.
Kuna maneno maalumu katika lugha ambayo
hutumika kufanya ulejelezi wa kimuktadha, maneno hayo huitwa VIOLEZI
Mfano Viwakilishi
Yule, hapa, kule huyu n.k. maneno yatumikayo katika uolezi yaani violezi
aghlabu hayana maana ya kudumu bali kupata maana zake kutokana na kila
kinacholejelewa kutokana na muktadha husika.
Mfano Ukija
YEYE utamkuta PALE itabidi usubiri kwa dakika 40 kisha MIMI nikija
tutakwenda kuwaona ili tuwarejese HUKU nao watupatie KILE kingine.
AINA ZA UOLEZI
1)
UOLEZI NAFSI
Ni uolezi unaotumia viwakilishi vya nafsi
kama violezi vyake mfano katika kisu vipo sita
Mimi - Sisi
Wewe - Ninyi
Yeye - Wao
Mimi sipendi tabi hiyo
*
Mimi / Sisi hurejelea wazungumzaji
*
Wewe /Ninyi hurejelea
wasikilizaji
*
Wao / Yeye hurejelea mtu mwingine watatu ambaye ama hayupo mahali /
wakati wa mazungumzo au kama yupo basi hajihusishi moja kwa moja na mazungumzo.
2)
UOLEZI WAKATI
Ni ulejelezi wa kimuktadha unaohusu mda /
wakati wa utendekaji wa jambo,
violezi vyake ni
vielezi vya wakati ie Sasa, kesho, leo, baadaye, mtondogoo n.k.
Mfano Nitakuja kesho.
3)
UOLEZI MAHALI
Ni uolezi unaohusu
msemaji na msikilizaji kuhusishwa na mahali ambapo
mawasiliano
yanatokea.
Mfano hapa, huku, humu vinarejelea mahali
ambapo ni kirani na
Mzungumzaji.
wawili. Vipo violezi vya mahali ambavyo vinafahiwa ya
ndani ya mfano humu,
humo na mule
4)
UOLEZI MWELEKEO
Ni uolezi unaohusu nafasi ya kitu kimoja
kimwelekeo kikilinganishwa na nafasi ya kitu kingine .
Mfano Mbele,
Nyuma, klia, kushoto, juuu, chini
5)
UOLEZI JAMII
Ni uolezi ambao hutokea ambapo maana ya
tungo inategemea uhusiano wa kijamii kuweza kueleweka na uhusiano huu
hurejelewa na maneno fulani fulani hupata maana yanapotumika kwa kuhusianishwa
na watu wa kaida fulani katika jamii.
Mfano Mzee,
Mama, Bwana.
- Ndio mzee nimekuelewa ie hutumika kuonesha
heshima
- Samahani mama hivi kituo cha dala dala kipo
wapi?
- Ngoja tutamwendea kwa babu
·
Mtu
fulani mahususi anayetumika kutatua matatizo ya watu.
·
Kikombe - hurejelea
pombe
·
Kiti - Jamani
tuheshimu kiti – hurejelea mamlaka (mkutanoni)
DHANA YA UCHOPEZI
1) Ni
uhusiano wa sentensi mbili ambapo ukweli wa sentensi ya pili huridhishwa na
sentensi ya kwanza.
Mfano : Athumani
amemuoa Asha
: Asha
ameolewa na Athumani
: Mwalimu
amefundisha somo la Sintaksia
: Somo
la Sintaksia limefundishwa
: Jakaya
Kikwate ni Raisi wa Tanzania
: Tanzania
inaongozwa na Raisi
Ni
kama unahusisha sentensi
2) Kimantiki
hatuoni uhusiano wake wa moja kwa moja na taaluma ya pragmatic.
Mfano - Viongozi wengi wa Tanzania si
Waaminifu
- Tanzania ina viongozi ambao si
waaminifu.
Ili mawasiliano ya lugha yaweze
kufanyika maneno ya lugha yapangwe kwa mpangilio
maalumu.
Jadili kauli hii kwa mifano kuntu nay a kutosha.
KANUNI
Fonolojia
Barabara