MADA MPYA 3: KUHAKIKI KAZI YA FASIHI ANDISHI
MADA MPYA 3: KUHAKIKI
KAZI YA FASIHI ANDISHI
MADA NDOGO-1: MAENDELEO YA FASIHI ANDISHI.
A.Mwelekeo
wa kazi za fasihi andishi nchini Tanganyika na Zanzibar wakati wa ukoloni.
Kimaudhui Kazi nyingi za fasihi andishi nchini Tanganyika
na Zanzibar zilishughulikia masuala mbalimbali ya kimaisha lakini kazi nyingi
zilikuwa na mambo ya mila na tabia kama njia ya kufundisha maadili .vile vile
zilishughulikia utamaduni, mawaidha, dini, maadili mema na maonyo na kazi zilizopinga
ukoloni
Maandishi ya kwanza ya nathari yaliyotokana na waafrika
wenyewe na kama vile“Uhuru wa watumwa ‘(1934)
cha James Mbotela kinashughulikia uhusiano baina ya mataifa ya
magharibi na ya Afrika.Katika kitabu hiki mwarabu na muislam wanalaumiwa kwa
utumwa uliokuwepo Afrika Mashariki wakati mkoloni anasifiwa kwa kuleta uhuru japokuwa
utumwa ulitiliwa nguvu na ukoloni.
Kwa ujumla hadithi ya uhuru wa watumwa inaonyesha ubaya wa
biashara ya utumwa iliyoendeshwa na waarabu na papo hapo inaonyesha matukio
yaliyowapata watumwa mambo yaliyowaumiza na uchungu ulowapata watumwa hao.
Mwandishi anaeleza mateso ya watumwa kwa watumwa kwa uchungu
na mchomo mkali.Pia hadithi hii inawatukuza wakoloni wa Kiingereza, ikijaribu
kumfanya mwafrika akubali kutawaliwa.Hadithi hii inausuta utumwa wa kimwili uku
ukiusanifu ule wa akili na mawazo ambao ni utumwa ulio mbaya zaidi.
Baada ya mwaka 1949-1960
kazi nyingi za fasihi za Kiswahili hasa riwaya zilifuata mkondo wa ngano na
fasihi simulizi kama za Paukwa! pakawa…hapo
zamani za kale palitokea…..,kimaudhui fasihi simulizi zilijadili maadili ya
kufuatwa katika kujenga jamii inayofaa katika maisha.Mfano mzuri wa vitabu hivi
ni Adili
na Nduguze (1952) utenzi wa mwanakupona (1858) na Al-inkishafi (1890).
Katika Adili na Nduguze mwandishi alitumia visasili vya jadi ya
kiarabu kama vile matumizi ya majini anaonya dhidi ya uchoyo na kuhimiza moyo
wa wema, usamehevu na kutosheka.Katika utenzi wa mwanakupona,mama anatoa
mafunzo kwa binti yake.Humo ndani ya utenzi mwanamke anapaswa kujitazama kwa nyenzo
tatu
Ø
Yeye ni nyenzo ya starehe ya mume wake hivyo
inampasa ajitahidi mno kumfurahisha ili apate rehema zake, kwani Mungu hata acha kumtia hatiani kwa kutotimiza huu mume
atakapomkana mbele ya Mungu.
Ø
Inampasa mwanamke awanyenyekee wanaume wote
isipokuwa watumwa tu.Aonyeshe kilicho na heshima kubwa kwao.
Ø
Mwanamke ajione kuwa yu mmoja wa matajiri au
maskini (watumwa).Binti anayeandikiwa shairi hili ni tajiri naye anaaswa
asichanganyike na watumwa, watu duni waliodharauliwa duniani
Shughuli za kisiasa zilizopamba
moto miaka ya 1950-1960 ilisababisha
kuibuka kwa fasihi ya kisiasa ambayo wasanii wake walizitumia kumpinga mkoloni.
Shaaban Robert pamoja na matatizo yake yote, alionyesha
upinzani wake hasa katika riwaya zake za Kusadikika (1951) na Kufikirika
(1967) ambamo zaidi ya kuwatetea wajumbe mbalimbali walikuwa wakiutetea
uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Pia mwandishi anaitetea serikali ya kikoloni kwa kejeli
kubwa kwani ilikuwa inainyonya Tanganyika na Zanzibar kwa ajili tu ya kukidhi
“Ugumba na Utasa” wa mfalme na malkia.Ugumba na Utasa ambao Shaaban
Robert kautumia ni ishara tu ya
mahitaji ya wakoloni.
Katika “Kusadikika” mwandishi
anajali suala la haki ya watu dhidi ya uongozi kandamizi wa kiimla utawala usio
na kiasi wala mpaka ni utawala ambao hatimaye hukwamisha maendeleo ya nchi na
watu wake.Kwa sababu huwanyima watu
uhuru wa kufikiri na kuchangia katika maendeleo ya nchi yao kwa kutumia mbinu ya kejeli, tashtiti, misemo, nahau. Mwandishi amejitahidi
kufikisha lengo lake la kuonyesha hasara ya kuyakwamisha maendeleo ya nchi.
Ukombozi wa
kiutamaduni ni mwanzo tu wa ukombozi wa siasa na uchumi. Hata katika riwaya ya
Tafsiri ya hadithi ya ”Chinua
Achebe”Shujaa Okonkwo (1932) ambapo wamisionari walitangulia kuja ili
baadae watawala waje na kuiteka nchi yote. Hivyo wamisionari walishirikiana na
watawala katika kuwanyanyasa na kuwanyonya watu.
Mhusika wa zamani, hasa mhusika mkuu alikuwani halisi mwenye
sifa zisizo za kawaida ambaye alisanifiwa na msanii kwa makusudi mazima ya
kuumba. Mfano bora wa kuigwa na kumfanya awe kielelezo cha ukweli na ukamilifu
wa maisha na mwenye kupigania na kuleta mambo hayo bila kuwa na dosari. Mhusika
mkuu wa zamani alitafakari maisha ya jamii kwa njia ya matendo makubwa na lugha
teule. Mhusika huyo japo kuwa alijitokeza
kuwa mtendaji mkuu kiasi hicho lakini hakuwa na saikolojia wala hisia.
Sifa hizi za upungufu wa saikolojia na hisia katika mhusika mkuu wa zamani
ndizo zilizomtofautisha na mhusika mkuu wa kisasa.
Tofauti nyingine ya msingi ni ile inayohusu uhusianao kati
ya mhusika mkuu huyo na wakati.
Mhusika mkuu wa zamani kama vile wa kwenye hadithi ya kifasihi alijitokeza kama
mhusika mkuu wa wakati wote. Kwa msanii
wa namna hiyo wahusika, dhana za wakati
na ukweli uliokamilika zilikuwa katika hali ya kutobadilika wakati na ukweli
vilikuwa na vitu vilivyotitia pamoja.
Kwa jinsi hiyo maandishi ya kisanii yaliyopewa jukumu la
kuzibeba sifa hizo yalilengwa kuwa ni ya wakati wote, yasizeeke. Lakini kinyume
chake mhusika mkuu wa kisasa anayaona masuala yasiyotulia bali ni masuala
ambayo yana badilika pamoja na jamii. Na baadhi ya wasanii wa kisasa wanaona
kuwa, suala la ukweli uliokamilika kwa kiasi kikubwa ni ndoto iliyomo katika
vichwa vya watu tu, na wala si maisha
halisi.
Mhusika mkuu wa kisasa yuko katika wakati maalumu wa
kihistoria ambapo anayazamia maisha kwa undani na kuyatafakari. Lakini kadri
Shaban Robert alivyozidi kuandika kama Maisha
yangu na baada ya mwaka Hamsini(1966) Wasifu
wa Siti binti Saad(1967) Siku ya watenzi wote(1968) ndivyo alivyozidi
kuwapa wahusika wake sifa zinazokaribia au zinazoelekeana katika hali halisi ya
maisha. Hii ina maana kwamba mkabala wake ulizidi kuelekea katika hali ya
kueleza ukweli kwa kutumia mbinu za kisanii ambazo hazikutenga kazi ya Sanaa
kwa kiasi kikubwa na uyakinifu wa maisha.Kwa ujumla fasihi Andishi ya awali
ilihusu zaidi maadili na masuala ya kidini kama katika”Adili na nduguze”.
Pia mvutano ulikuwepo baina ya wakoloni na waafrika, Ulikuwa
unadhihirishwa katika baadhi ya kazi za fasihi Andishi za awali.Pia maandishi
mengine ya fasihi yalihusu matarajio ya jamii itakiwayo baada ya ukoloni, kama
katika kufikirika na kusadikika,
katika kipindi hiki tanzu za fasihi andishi zilizokuwapo ni riwaya na ushairi.
Baada ya uhuru, tamthiliya zote za Kiswahili zilizochapishwa zilikuwa
zimeandikwa na wakenya, watanzania, hawakujitokeza katika uwanja huu hadi baada
ya uhuru.
B: Mwelekeo wa kazi za fasihi
Andishi nchini Tanzania baada ya uhuru
Baada ya uhuru
kulikuwa na fasihi mchangamano ambayo ni vigumu kuiainisha hadi tukio kuu la
kutangazwa kwa Azimio la Arusha, kabla ya hapo fasihi kwa
kiasi kikubwa, ilikuwa ya kushangilia uhuru uliopatikana hasa katika magazeti
ambako mashairi na hadithi nyingi zilionyesha hoi hoi ya lelemama za uhuru.
Kwa upande wa mashairi, vitabu kama vile Utenzi wa uhuru wa Tanganyika(1967) na utenzi wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania(1968) viliandikwa wakati huo. Ni kipindi hicho cha uhuru utanzu wa
tamthiliya ulijitokeza kwa mara ya kwanza kwa upande wa Tanganyika na
Zanzibar.Mwandishi maarufu wa tamthiliya aliyejitokeza kipindi hicho Ebrahim
Hussein ambaye tamthiliya yake ya kwanza “Wakati
ukuta”(1969) ilichapishwa ikifuatiwa na tamthiliya ya “Kinjekitile”(1969)
Fasihi ya Kiswahili
imepevuka zaidi kwenye miaka ya 1970,karibu tanzu zote za
fasihi Andishi ya Kiswahili zimepata wawakilishi. Hali hii imepelekea kutokeza kwa fasihi za mkondo mbali mbali.
Kimaudhui,fasihi andishi nchini Tanzania baada ya uhuru
imejadili dhamira mbali mbali ambazo zinatokana na matukio mbali mbali ya kihistoria yaliyojitokeza
katika jamii yetu ya Tanzania.
Kipindi maalumu cha maisha kina matukio yake maalumu ambayo
huigusa jamii kwa uzuri au ubaya na kuwa dundo la moyo la kipindi hicho ndichi
kinachojenga kilele. Aidha tukio linapokuwa dundo la moyo la kipindi fulani cha
maisha huwa pia mada kuu(muhimu) ya wakati huo kwa jamii inayohusika.Mada hiyo
uweza kujitokeza kinagaubaga katika taaluma mbali mbali za jamii na fasihi
ikachukua nafasi muhimu.
Kihistoria masuala makuu ya miaka ya 1960 yalikuwa ni ukombozi wa bara la
Afrika na ujenzi wa jamii mpya baada ya uhuru. Masuala haya makuu yaliyojitokeza
katika fasihi andishi ya Tanzania wakati huo. Hivyo palitokea fasihi andishi ya
kisiasa na kifalsafa zilizojadili maisha, utawala na ujenzi wa jamii mpya.Kazi
nyingine za fasihi zilipingana na
ukandamizaji, ubinafsi pamoja na unyama
mwingine uliokuwa unafanywa.Pia zilieleza mkondo wa ubanadamu usawa na ustawi.
Baadhi ya kazi hizo ni za Shaaban Robert,
Utu bora mkulima (1987) na siku ya
watenzi wote(1968)
Kwa upande wa ukombozi, riwaya ya kiimbila “Lila na Fila” (1966) iligusa dhamira
hiyo kiishara. Tamthiliya ya E. Hussein”Kinjekitile” (1969),kaburi bila
msalaba (1969)ya Kaireth. Katika kipindi cha miaka ya 1960 ilitokea fasihi ya tabia n maadili ambayo
imejadiliwa maadili mema na maonyo.
Fasihi hii ya tabia na maadili inawakilishwa na J.M Somba “kuishi kwingi kuona mengi”(1968) “Alipanda upepo akavuna tufani” (1968)
Mathias Mnyapala “Diwani ya mnyapala”(1965)
S.A Kandoro “Mashairi ya Saadan”(1972), “Dwani
ya Akili Mali”(1967)
Aina nyingine ya fasihi iliyojitokeza katika kipande hiki ni
ile riwaya na hadithi fupi za upelelezi na za mapenzi. Fasihi ya aina hii
ilizuka kutokana na nguvu mbali mbali za jamii.Katika Tanzania, aina hii ya
fasihi ililetwa kwa mara ya kwanza na M.S Abdulla alipoandika riwaya ya “Mzimu
wa watu wa kale”(1959) na miaka ya 1960 aliandika riwaya ya “kisima cha giningi”(1968) akafuatiwa na
katalambula aliyeandika kitabu cha “Simu
ya Kifo”(1965)
Mwisho kazi za fasihi
zilizojitokeza miaka ya sitini ni fasihi ya mila na utamaduni inayowakilishwa
na M.S Farsy “Kurwa na Dotto”(1960)
F.Nkwera “Mzishi wa baba ana radhi zake”
(1968)
Mwaka 1967 Azimio la
Arusha lilitangazwa.Azimio hilo lilionekana kwa wanasiasa na wananchi wengi
kuwa ndio dira ya kuitetea jamii ya Tanzania katika maisha bora ya ufanisi na
maendeleo kwa hiyo kipindi cha miaka 5 hivi baada ya Azimio la Arusha kilikuwa
na fasihi ambayo ilitukuzwa maadili na amali zilizotokana na tamko Azimio la
Arusha.
Maudhui yaliyotawala fasihi ya kipindi hiki ni ujenzi wa
jamii mpya kwa kupitia nguzo ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kazi hizi
zilizosisita mabadiliko ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni,
zilizopigania jamii mpya. Ijapokuwa bila kuonyesha kimantiki (kiyakinifu) vipi
jambo hilolingewezekana.
Mfano wa kazi hizi ni:-Mashairi
ya miaka kumi ya Azimio la Arusha (1977),Mashairi ya Azimio la Arusha (1970),Utenzi wa zinduko la ujamaa (1972),Utenzi
wa kumbukumbu za Azimio la Arusha (1970),Matunda ya Azimio la Arusha (1980),Liwazo
la ujamaa (1978),Mtu ni utu (1971),Ndoto ya Ndaria (1976),Njozi za usiku (1970),Kijiji
chetu (1971) n.k
Pia kutokana na Azimio la Arusha pamoja na siasa yake iliyosisitizakuhusu umuhimu wa
vijiji na umuhimu wa kilimo, zilitokea kazi za fasihi ambazo zilihubiri kuhusu
maisha bora ya vijiji yaliyolinganishwa
na yale ya mjini.
Suala ambalo liliwahi kuongelewa na Shaaban Robert katika
riwaya yake ya “Utu bora Mkulima”(1968).
Sasa lilipata damu mpya katika kazi kama Penina
Muhando,”Hatia” (1971)
Balisidiya Shida (1975) Mnyampala, Ngonjera za ukuta (1968) Mbogo “Giza limeingia”(1980) mashairi mbali mbali katika magazeti n.k
katika kazi hizi mvutano baina ya mji na vijiji ambao ulileta matatizo ya wizi,
ujambazi, umalaya na mengine ya aina hiyo yalitolewa dawa moja, kurudi kijijini. Jawabu hili zaidi ya
kutokuwa sahihi kwani linakwepa kiini hasa cha tatizo papo hapo lilipotosha maana halisi ya kijiji
na kilichotakiwa kuundwa katika jamii ya Tanzania. Kijiji kilionekana kuwa
mahali pa kuwalundika wahuni walioshindwa maisha ya mjini.
Naye Madumilla (1988) anaonyesha kuwa katika kipindi
hiki cha 1970-1980 zilizojitokeza kazi ambazo zilitazama suala
lakujenga jamii mpya kwa kutafakari na kujiuliza na hata kwa mashaka na wasi
wasi pia. Hususani baada ya kubaini utata, mgongano ya kitabaka na ukuaji wa haraka
wa ubepari wa kimji. Mfano Kiu (1972) Kichwa maji (1974) Gamba la
nyoka (1979) Nyota ya Rehema (1978) Dunia uwnja wa fujo (1979).
Kwa ujumla miaka ya 1980 riwaya ya Kiswahili imeshuhudia
jaribio la muundo wa riwaya ya kifalsafa. Lakini kama ilivyogusiwa kwa kiasi
kikubwa mikondo ya riwaya imeendelea kuwa ile ile ya miaka ya sabini. Riwaya ya
ukasuku katika upande wa riwaya dhati imepotea. Badala yake kuwa riwaya
inayopevuka nakutumia ukweli wa mambo. Inayojaribu kubainisha migongano ya
kijamii katika vipengele mbali mbali vya maisha hususani cha kiuchumi.
Ijapokuwa waandishi wanafanya hivyo katika mkabala au mitazamo ya maisha
inayotufautiana.
-Mfumo wa vyama vingi
-Utandawazi
Kipindi hiki mfumo wa chama kimoja ulifutika na mfumo wa
vyama vingi ukaanzishwa hapa nchini ambapo uliambatana na kuoneshwa kwa utitiri
wa vyama vingi. Fasihi andishi ilijitokeza kipindi hiki inazungumzia mfumo wa
vyama vingi na athari zake kwa jamii yake. Mfano wa kazi hizo ni riwaya ya “Nyuma ya pazia” (1996), Kipanga (Khatibu)
na mashairi mbali mbali yaliyokuwa yanaandikwa kwenye magazeti.
Kwa upande wa utandawazi ambao unaenda unaenda samba samba
na ubinafsishaji wa soko huria umewaathiri sana waandishi wa fasihi ya
Kiswahili. Katika fasihi ya Kiswahili kwa mujibu wa Khamisi(2007) utandawazi
umesababisha kuzuka kwa fasihi mpya ya Kiswahili ambayo imezaliwa mwanzoni mwa
miaka ya 1990, muda mfupi baada ya neon utandawazi kuingia masikioni na kuzama
akilini mwetu kuanzia 1980.
Utandwazi ni neno dhahania lenye maana nyingi tata kutegemea
msisitizo wa anayelitumia. Pamoja na tofauti za maana na matumizi ya neno hili
wataalamu wakubliana kwamba ni neno linaloelezea mfungamano na uhusiano
uliojitokeza katika miaka mingi iliyopita, hasa katika biashara na uchumi.
Lakini pia katika utamaduni, miongoni mwa jamii tofauti za dunia . Mfungamano
na uhusiano uliojitokeza katika miaka mingi iliyopita hasa katika biashara na
uchumi, lakini pia katika utamaduni miongoni mwa jamii tofauti tofauti za
dunia. Mfungamano na uhusiano huu unaotufautishwa na mfungamano na uhusiano
mwingine wa aina hii uliojitokeza kabla, kwasababu utandawazi umepata kazi
kubwa ya kuwekeza mitaji na kuvuna faida kubwa kiuchumi kiutamaduni, ikisaidiwa
na maendeleo makubwa ya kiteknolojia yalipatikana karibuni hasa ya vyombo vya
habari vya masafa na wakati kiutamaduni. Utandawazi unausishwa na kuenea kwa
tamaduni za kimataifa (Marekani na Ulaya) kwa njia ya biashara (kama vile
vinywaji vya Cocacola, bia na pombe kali ambazo zamani zilikuwa hazijulikani).
Mtiririko wa muziki na taswira kupitia video, luninga, mitandao ya kompyuta na
simu,CD, DVD na VCD.
Kwa mujibu wa Khamisi(2007) fasihi ya Kiswahili ni kama vile
Nagona(1990), Mzingile(1990), Zirani na zraili(1999), Babu alipofufuka(2001).
Makundi wa soko huria(200), Baria- Adam(2002), Dunia yao(2005), Mkamaduma(2005)
zimeathiriwa sana na utandawazi wa kimagharibi, sifa moja kubwa ya kimaudhui
miongoni mwa kazi hizi ni ile ya kushughulikia kwa kina matatizo ambayo yana
kabili ulimwengu wetu leo. Ingawa bado riwaya hii inajishughulisha kwa kiwango
fulani na matatizo ya ndani ya nchi na jamii husika kwa kiasi kikubwa imekiuka
mipaka ya kitaifa na kuenea kwa kiasi kikubwa inachunguza si jamii ya Tanzania
tu bali dunia yote huku ikionyesha athari za utandawazi kwa jamii hizo.
Katika Babu alipofufuka (2001), Dunia yao(2003) na hata
Biria- Adamu (2002), Suala zima linaloshughulikiwa kifalsafa ni siasa. Nini
maana ya kuishi? Nini maana ya uhuru? Nini maana ya maendeleo? Nini maana ya
uraia wa mtu? Nini maana ya uzalendo? Kwanini kikundi kidogo cha watu wapange
maisha ya watu wengi katikavjamii fulani nan je ya jamii hiyo? Kuna dunia ngapi
katika dunia moja ya jamii fulani?
Mipaka ya dunia hizo ni miembamba au mipana kwa kiasi gani? Nini maana
ya kijo? Nini maana ya kuishi? Inawezekana mtu anayeishi akawa amekufa? Nguvu
zipi zinaongoza limwengu wetu? Zinaongoza kwa mslahi ya nani na kwa taathira?
Katika Bina – Adamu (2002) na riwaya nyingine. Nguvu zenyewe zinajieleza hivi
“Itakuwa vigumu kupambana nani?.....imewaingia akilini kabisa. Ninahusika
kwingi hata msipokuwepo kutakuwapo kwangu, Ndiko hata kwako kwangu….
Athari hizi za utandawazi katika jamii na maisha halisi
zimehitimishwa na Chachage, ambaye riwaya yake ya “Makuadi wa soko huria”(2002)
inavua nguo na kusambaratisha utandawazi na utetezi wake wa ndani.
Kwa jumla maendeleo ya fsihi Andishi nchini Tanzania baada
ya uhuru ni makubwa sana ukilinganisha na akati wa ukoloni. Tanzu zote za
fasihi Andishi, riwaya, hadithi fupi ushairi wa tamthiliya zimepanuka sana.
Vile vile kama waandishi wengi sana wa tanzu hizo na uandishi wao umekuwa
ukibadilika kuungana na mabadiliko mbali mbali yanayoitokeza katika jamii. Kila
tukio la kihistoria lililotokea katika jamii limezaa kazi zake za fasihi.
UHAKIKI WA
USHAIRI
USHAIRI
Mulokozi na kahigi (1982) Ushairi ni Sanaa inayopambanuliwa
kwa mpangilio maalumu wa maneno fasaha na yenye mwaliko kwa lugha ya mkato,
picha au sitiari au ishara katika usemi, maandishi au mahadhi ya umbo ili
kueleza tukio, wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisi fulani kuhusu
maisha au mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo
Kutokana na maana hiyo kuna mambo muhimu yanayojitokeza
katika ushairi:
Ø
Ushairi ni Sanaa yaani kazi iliyobuniwa na
mtunzi mahususi.
Ø
Ushairi una ufungamano na hisia.
Ø
Ushairi una mpangilio wa aina fulani kuanzia
kiwango cha sauti, neno, sentesi hadi ubeti.
Ø
Ushairi huchota hisia na tafakari zake kutoka
katika ulimwengu halisi wa maisha ya jamii na mara nyingi hufungamana na
falsafa ya jamii fulani.
Ø
Ushairi hutumia lugha ya mkato yenye kueleza
mambo mengine kwa maneno machache kwa kutumia mbinu za taswira na tamathali za
semi.
Ø
Ushairi huzingatia sana dhana ya ushairi
ulinganifu wa vitu kimuundo.
Ø
Ushairi una uhusiano na muziki (nidhimu) ngoma
na uchoraji (mchoraji) hutumia rangi na brash mshairi hutumia taswira na
maneno.
AINA (KUMBO) KUU ZA
MASHAIRI YA KISWAHILI
MULOKOZI(1996) Ameainisha aina tatu za ushairi waKiswahili.Aina
hizo ni:-
I)
USHAIRI
WA KIMAPOKEO
Ni mashairi na tenzi za kijadi
zenye kufuata kanuni za urari wa mzani na mpangilio wa vina vya mwisho au
kati.Katika ushairi wa kimapokeo kuna mambo ya msingi ambayo yanasemekana kuwa
ni mti wa mgongo wa ushairi wa Kiswahili.
Kwa mujibu wa wanamapokeo.Shairi la
Kiswahili lazima liwe na vina na mizani,mistari ubeti na kituo.
Katika utenzi
(aina pia ya ushairi wa kimapokeo) kuna kuwa na bahari katika mstari wake wa
mwisho.
Ushairi wa kimapokeo unaweza
kugawanyika katika sehemu kuu mbili yani Tenzin
na Mashairi
a) TENZI
Ni utungo ambao kimaudhui huelezea tukio fulani linalotokea
katika jamii au liliwahi kutokea.Pengine huweza kuwa maelezo juu ya wasifu wa
mtu fulani, jambo fulani la kihistoria au jambo lolote zito linaloelezwa kwa
maelezo marefu.Utenzi ni masimulizi marefu juu ya jambo fulani maalumu
Katika upande wa fani
utenzi una sifa za pekee kabisa
v
Utenzi unakuwa na beti nyingi kuliko yalivyo
mashairi au aina nyingine yoyote ya ushairi.Beti hizi zaweza kuwa 100, 200, 300
au zaidi kutegemeana na ufundi wa mshairi mwenyewe.
v
Utenzi huwa hauna mizani ndefu,tenzi zilizo
shamiri sana katika jamii hii ni zile zenye mzani nane nane katika kila mistari
zaweza pia kwenda zaidi ya nane kufikia kumi na moja lakini hazuii zaidi ya
hapo
v
Katika utenzi kila ubeti huwa na mistari minne, mistari
mitatu ya kwanza ikiwa ina vina vyenye urari sawa na ule wa mwisho ikiwa na
kina tofauti ingawa vina vya mistari mitatu ya kwanza huwa na vina vyenye urari
sawa lakini vina hivyo hubadilika badilika toka ubeti mmoja hadi mwingine.
v
Katika utenzi kina cha mwisho katika msitari wa
mwisho wa kila ubeti huwa hakibadiliki badiliki, kina cha mwisho wataalamu
wengi wa ushairi hukiita bahari kwa sababu huwa kimetenda na kuongelewa katika
utenzi mzima
Mfano wa tenzi:
S.Robert, Mapenzi bora.
A.Abdilatif, Utenzi wa maisha ya Adam na Hawa (1971)
J.K.Nyerere, Utenzi wa Injili kadiri ya utungo wa Luka (1996)
Mfano Utenzi wa Fumo Liyongo (13 BK)
Ubeti 6: Liyongo Kitamkali
Akabalighi vijali
Akawa mtu wa kweli
Na hiba huongeya
Ubeti 7: Kilimo kama utukufu
Mpana sana mrefu
Majimboni yu maarufu
Watu hujakumwangalia
Ubeti 10: Sultani pate Bwana,
Papo nae akanena,
Wagala mumemwona,
Liyongo kuwatokeya
b)
MASHAIRI
Shairi kama sehemu ya ushairi, ni
utungo ambao huelezea kwa ufupi mambo fulani kuhusu binadamu na mazingira
yake.Aghalabu mashairi huelezea mambo yanamhusu binadamu na maisha yake ya kila
siku.Mashairi ya kimapokeo yanapoandikwa hufuata kanuni za vina, mizani,
mistari, ubeti na kituo mfano:-
KUNTU SAUTI YA KIZA (FUNGATE YA UHURU-UK
38)
Nyuki ni mtanashati, umbo na zake
tabia,
Yeye yu kila wakati, vichafu
huvikimbia,
Mchana na kulati, hatui kwa
kukosea,
Kuntu sauti za kiza, Nyuki
hapendi vichafu.
Ni inzi na sio nyuki, Nadhafa
hajazoea,
Kwa uchafu ni ashiki, hawezi
kuuachia,
Vianzavyo humiliki, fahari
hujonea,
Kuntu Sauti za kiza, Nyuki
hanyoni vichafu.
U WAPI UZURI WAKO
U wapi uzuri wako, haupo
umepotea,
Ya wapi maringo yako, na hashuo
za dunia,
Leo upo peke yako, sote
tumekukimbia.
Sasa ni chano cha maji, watu
wajichanyatia,
Umekwisha ujuwaji, haya
zimekupatia,
Yale usoyatarajia kwako
yamekuhamia.
DAFINA
Paa ni kuruka angani, kama ndege
wa tiara
Paa ni mnyama porini, ni mwenye
nyingi, Papara
Paa ni kuteka mengine, moto uwako
imara
Paa ni toa migombani, Samaki atie
sura
Paa Pia ni la nyumba, makuti au
kurara
Mgodi wa Kiswahili ni dafina
isiyokwisha
2. USHAIRI WA MAIGIZO
Ushairi huu unahusisha ngonjera
na ushairi wa kidrama
v NGONJERA
Ni ushairi wa majibizano
ulioanzishwa na Mathias Mnyapara miaka 1960 ili kueleza siasa ya ujamaa na
kujitegemea kabla ya hapo ulikuwepo ushairi wa majibizano lakini ulikuwa
unatambwa tu.
Ø
Katika ngonjera kuna pande mbili zinazojibizana
kuhusu mambo fulani upande mmoja huwa sahihi na wa pili huwa umepotoka.
Lengo la mabishano ni kuushawishi
upande uliopotoka ukubaliane na upande wenye msimamo sahihi baada ya
kuelimishwa. Hili linapotokea ngonjera huwa imefikia kilele chake. Mfano wa
ngonjera ni Ngonjera za ukuta 1 na 2
(Mnyapara 1970-1972)
Ushairi wa kidrama ni ule unaotumika
katika baadhi ya tamthiliya. Ushairi huo ni sehemu tu ya mchezo wa kuigiza ni
mtindo wa kuandika mazungumzo ya wahusika katika tamthiliya hivyo hauwezi
kutenganishwa na hiyo fani ya tamthiliya. Kwa mfano tafsiri Shaspare, Mabepari
wa Verusi Julius Kaizari (Nyerere) 1969, Mfalme Epidope (Mushi 1971)
Mfano:
Juma: Naam na nitampa bure bila ya fidia
Pokeeni na Jeshika kutika kwa
Myahudi
Hati maalum ya hiba, baada ya
kifo chake
Ataacha kwenu nyingi, kila atakachokiacha
Baraka: Mabibi wema, mwaonyesha maana kwa walagai
Neema: Kunakaribia kucha, lakini nina hakika
Bado hamjaridhika, kabisa na
mambo hayo
Kwanza na twendeni ndani, kisha
huko tuhajiri
Nasi tutawajibuni, mambo yote
sawa sawa
(W. Shakespare, Mabepari wa virusi
1969)
Katika mfano huu ushairi huu una
mizani 16 kwa mshororo bila urari wa vina, kanuni ya utoshelezi imekiukwa wazo
la mshororo mmoja linaendelezwa katika mshororo unaofuata.
3.
USHAIRI WA
MLEGEZO / KISASA / MASIVINA
Ni mashairi yasiofuata urari wa
vina na mizani, Vina vinaweza kutoka lakini si lazima katika mistari. Pia
mapigo yanaweza kuwa sawa kwa idadi katika mfululizo wa vipande kadhaa lakini
si katika tungo nzima.
Mfano:
CHAI
YA JIONI
Wakati tunywapo chai hapa upenuni
Na kuwatazama watotowetu
Wakicheza bembea kwa furaha
Tujue kamba ya bembea yetu
Imeshalika na imeanza kuoza
Na bado kidogo tutaporomoka
Kulikuwa na wakati uinisukuma juu
Nikaenda zaidi ya nusu duara
Kulikua na wakati nilidaka
Ulipokimbia na kuanguka
Sasa tukisubiri ndoto tusizoweza
kutekeleza tena
Tumalize machicha ya chai yetu ya
jioni
Bila kutema tena na kuwa tabasamu
Baada ya hapo tujilambe lambe
utamu utamu
Uliobakia kwenye midomo yetu
Tukikumbuka siku ilee ya kwanza
Tulipoutana jioni chini ya mwembe
Tukifunga bembea yetu
Naye umbwa samba akikusubiri
Lakini kabla hatujaondoka kimya
kimya
Kukamilisha nusu duara iliyobakia
Tuhakikishe vikombe vyetu visafi
(Kazilahabi 1988)
VIJENZI VYA USHAIRI WA KISWAHILI
Ushairi wa Kiswahili unajengwa na
vipengele vifuatavyo:-
1.
Mpangilio
wa maneno
Maneno ya ushairi hupangwa ili
kuleta maana fulani, sauti za aina fulani au urari fulani wa mizani.
Katika shairi la Kazilahabi “Kisu
mdomoni” , kisu mdomoni (kiuchumi) uk 10 kuna mstari ufuatao.
“Ya nyuma sana nisijali ya mbele
sana niyakabili. Hapa neno “sana” limewekwa makusudi kati ya “nyuma” na
“nisijali” ili kupata maana mbili. Mambo ya zamani sana (ya nyuma sana) na
kutojali jambo neno (sana nisijali) kama neno sana kinga kuja baada ya nisijali
maana hizo mbili zisingalitokeza. Vivyo hivyo uwili huu wa maana tunaupata
katika kipande cha pili cha mstari huo “ya mbele sana niyakabili” kutokana na
mpangilio wa maneno.
2. Takriri
na Ridhimu au wizani
Takriri ni mbinu
ya kurudia rudia jambo kwa kusudi maalumu, vina na urari wa mizani ni aina ya
takriri. Mtunzi anaweza pia kurudia rudia maneno fulani au silabi fulani kwa
shabaha malumu. Kwa mfano katika shairi la “ Kufa moyo” Shaaban Robert anatumia
mbinu ya takriri kwa kurudi rudia kifungu cha maneno “ siku ya ………. Kwa
msisitizo:-
Siku ya panga
kufuta, mashujaa kwenda kona
Siku ya kuja
matata, kwa damu kwenda mdundo
Siku ya watu
kuteta, kufa moyo mfundo
Siku ya kung’ara
nyota za watenzi wa mtindo
(Shaaban Robert 1991 : 48-49)
Takriri hutumika
sana katika nyimbo na mashairi ili kutia msisitizo.
Ridhimu ni mapigo asili ya lugha
, kila lugha ina mapigo yake. Mawimbi ya sauti yenye kupanda na kushuka na
yanayofunga maana na mfuatano wa sauti usio na maana yoyote.
Ridhimu ya ushairi wa muziki
hutokana na mlingano wa vipande vya mapigo ya lugha au sauti . Katika muziki
vipande hivyo vya mapigoni lazima vilingane kabisa katika ushairi.Vinaweza
kupitana kidogo ili kupunguza maudhi masikioni.
3. Taswira
au Picha
Taswira ni mbinu
ya kuumba picha ya jambo katika mawazo ya msomaji au msikilizaji wa tungo hilo
kwa kutumia maneno. Picha ya maneno ikichorwa vizuri mtu huweza kuhisi, kuona,
na hata kunusa kile kinachozungumzwa.
Mfano:
Amina umejenga,
umekufa umetangulia
Kama ua
umefunga, baada ya kuchanua
Nakuombea
mwanga, peponi kukubaliwa
Mapenzi
tuliyofunga, hapana wa kufungua
(S. Robert Amina
1966: 3)
Katika ubeti huu, mshairi
analinganisha maisha ya mauti ya Amina kwa njia ya picha na ua mbalo limekuwa
likichanua na kisha likafunga au kunyauka.
4. Tamathali
za Semi
Tamathari ni
umithilishaji yaani uwakilishaji wa jambo kwa kulinganisha au kulifananisha na
jingine.Kwa mfano badala ya kusema “Juma alikuja mbio sana” Mshairi atasema
“Juma alikuja kama umeme” Tamathari nzuri hupanua, huyadumisha na huipa uhai na
uhalisia zaidi dhana inayoelezwa, huburudisha na kuzindua akili ya msomaji au
msikilizaji wa shairi na athari ya kudumu katika hisia na mawazo yake.
Tamathari
zinazotumika zaidi katika ushairi ni Tashbiha, tafsida, tashhisi, mbalagha,
kejeli, sitiari n.k.
5. Hisia
za kishairi
Hisia hizi
hutokana na msukumo wa ndani wa moyoni alionao mshairi wakati anapotunga shairi
lake na hujidhihirisha katika uteuzi na mpangilio mzuri wa maneno yenye kuwakilisha
maudhui husika kwa mfano, maudhui ya huzuni hudhihirika katika maneno
yanayotumika ambayo aghalabu yanadokeza hali ya huzuni, vina vyenye sauti ya
kilio.Mfano ee, lel, lel, lel, ea, aa, ya n.k.
Mfano mzuri ni
shairi la Shaaban Robert la AMINA ambazo linaomboleza kifo cha mkewe.Hisia za
furaha pia huweza kuwasilishwa kwa njia hizo hizo
Mfano:-Shairi
la Cheka kwa furaha
Dhiki
ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?
Haya cheka ha! ha!, ndio ada duniani,
Basu cheka kwa! kwa!, usifike moyo wako.
(Robert, kielelezo cha fasihi 1968:16)
6. Lugha
ya mkato.
Shairi
huzungumza mambo wa ufupi kuliko ulivyo katika maongezi ya kawaida. Hivyo ni
muhimu kwa mtunzi kujua namna ya kueleza jambo kwa Lugha ya mkato.Hii
inawezekana kwa kutumia taswira na tamathali badala ya maelezo marefu.
7. Mchezo
wa maneno
Mbinu ya
kuchezea maneno hutumiwa na washairi ili kutoa maana ya kile kisemwako na
kuongeza utamu wa usemaji mara nyingi maneno yenye umbile moja lakini maana
tofauti hutumiwa kwa ajili hii mfano katika Shairi la M.Mulokozi la “wale,
wale” maana tatu za neno wake (yaani kundi la watu na hao watafune na kumeza
chakula “na” “wale”wale” kwa maana ya “hao hao” si wengine zinachezewa ili
kuleta ujumbe fulani.Mshairi anaona kuwa hakuna mabadiliko ya msingi
yaliyotokea .Kundi lile la walaji limerejea katika madaraka kadharika maneno
“kura” na “kula” yamewekwa sambamba ili kuonyesha uhusiano uliopo kati ya
uchaguzi (kupiga kura) ulaji.
Wale wale
Wale wale ndiyo wao
Bado wapo palepale
Wao wale wenye vyao
Na vya kwao vile vile
Wala kale wala leo
Kura huko kule kule
Mwendo huu ndiyo huo
Bado tupo pale pale
(Mulokozi 1990)
FANI
NA MAUDHUI
Ushairi kama Sanaa hujengwa na
mambo mawili ambayo ni fani na maudhui.Maudhui ni mambo yaliyomo
(yanayozungumzwa) ndani ya shairi na fani ni njia anazozitumia mtunzi kuyasawirisha
maudhui yake kwa hadhira yake.Fani na maudhui huingiliana hutegemeana na
kukamilishana.Ni mambo ambayo hayatunganiki, fani hubeba maudhui, na maudhui
huathiriwa na fani.Uwiano wa fani na maudhui ndiyo kigezo bora cha ndani cha
ubora wa shairi.
Katika fani kuna mambo
yafuatayo:- Muundo, mtindo, matumizi ya lugha na jina la kitabu katika kipengele
cha lugha kuna mpangilio wa maneno, tamathali za semi, methali, misemo, picha
n.k.
Maudhui ni mawazo yanayosemwa
ndani kazi ya Sanaa.Mada kuu inayayozungumziwa katika shairi huitwa
dhamira.Dhamira inapounganishwa na mtazamo wa mtunzi, Shabaha na ujumbe
hupatikana yanaweza kuhusu jambo lolote linalohusika.Maudhui yanaweza kuhusu
jambo lolote linalomkera mwanadamu kwa mfano maana ya maisha, mapenzi, mauti,
ndoa, elimu, kazi, dini, ukombozi, usaliti n.k.
UHAKIKI WA VIPENGELE VYA FANI
a)
Mtindo
wa mashairi
Masharti ya
Kiswahili yana mtindo mingi sana katika utungaji wake kwa hakika si rahisi
kutambua ama au idadi ya aina za utungaji wa ushairi, kwani hii hususani
kutegemeana sana na ufundi wa mtungaji mwenyewe.Baadhi ya mtindo ya utungaji wa
ushairi ni kama ifuatavyo
a) Mtindo wa pindu
Katika utungaji wa aina hii silabi mbil za mwisho wa
mstari hurudiwa rudiwa kwa mfano: kama mstari wa kwanza uliishia na neno
“fahamu” basi mstari wa pili utaanza na silabi mbili za mwisho, yaani “hamu”
wakati mwingine huitwa “Mkufu”
Mfano:
Zipokeeni Salamu, lamu kila na mvita,
Vita kwa wanadamu, damu zinawezachonyota,
Nyota
njema ni agumu, gumu jema kulipata,
Pata kwa kuyafuata, fuata mambo mazuri.
Zuri katika dunia, nia mama yanaleta,
Leta kila la sheria, ria huleta matata,
Tata
watu hujifia, fia ipo kwa kupita,
Pita usije kupita, pita katika mazuri.
(waniitila, kichocheo cha fasihi simulizi na andishi
Uk 224)
b) Mtindo wa msisitizo
Kuna msisitizo wa aina mbili, kuna msisitizo wa wima
na msisitizo wa ulalo
Msisitizo wa wima ni kule kuwa na neno moja likawa
linatokea mwanzoni na linarudiwa katika kila mistari wa shairi zima
Mfano: Ua
langu la moyo, nitunzo nipowe
Ua langu usinitunze, ua nitunze nitowe
Ua nikae shingoni, ua usinichambue
Ua la moyo ua, Ua lichanue kwangu
(Diwani
ya Akilimani 1973:63)
Msisitizo wa ulalo ni ule wa kutumia kibwagizo kama
kiini cha habari yote inayozungumziwa katika shairi lote na ikawa hicho
kibwagizo cha rudiwa rudiwa katika kila ubeti wa shairi
Mfano: Kokoni
kucha kuchile, risala enenda hima,
Kufika similatile, ulitimavu si mwema,
Kumbe nao watambule, haya ninayoyasema,
Iwapo kimya si chema, na maneno hayafai.
Sipendelei kusudi, na manji mno kusema,
Nendapo hijitahidi, kimya change hatuzamu,
Kanama sio mwadi, watu wengine si wema,
Iwapo kimya si chema, na maneno hayafai.
(fani
na taratibu za ushairi wa Kiswahili 1939:18)
c) Mtindo wa beti kubadilisha vina.
Iwapo katika ubeti wa kwanza kina cha kati kilikuwa
“na” na ile ile cha mwisho kilikuwa “ma” basi katika ubeti unaofuata kina cha
kati kitakuwa “ma” na kile cha mwisho kitakuwa “na”.
Mfano: Kila
shairi nalia, chozi latoka machoni,
Na ninyi mwangalia, wala hamniponzeni,
Mpenzi kankimbia, naudhika simwoni
Nirudie we mwandani, roho ipate tulia.
Nakuomba samahani, magoti nakupigia,
Nisamehe nuksani, zote nilo kutendea,
Naapa kwa yangu dini, kamwe sitayarudia,
Narudia we mwandani, roho ipate tulia.
d)
Mtindo wa
kubadilisha vina vya kati toka ubeti ili hali vile vina vya mwisho katika ubeti
vikibaki vile vile
Katika ubeti wa kina kina cha mwisho kilikuwa “za”
basi kina hicho kitaendelea kujitokeza ubeti mmoja hadi ubeti mwingine wakati
vile vya kati vitaendelea kubadilikabadilika.
Mfano:
Jalali wangu mchunga, nikidhi yako rehema,
Niweke natangatanga, nitabaruku kwa wema,
Niweke kwenye kiunga,cha malisho ya
uzima,
Na
majani ya rehema, na vijito vyenye raha.
Tabaruku moyo wangu, nisifikwe na zahama,
Pasinifike machungu, kwani u mwenye
hunena,
Nakutegemea tangu, wala sinayo tahuma,
Uniongoze kwa wema, nami nitakutukuza.
(fani
na taratibu za ushairi wa Kiswahili 1986:38-39)
e) Mtindo wa kidato
Katika muundo huu baadhi ya mistari na maneno yake au
silabi zake zina maneno machache au zimefupishwa tofauti na mistari mingine
ambayo huwa na silabi au maneno mengi.Ufupishaji huu wa maneno au silabi katika
baadhi ya mistari hufanywa kwa lengo maalumu.
Mfano:Tohara, kwa wanawake ni hatari
Madhara, kwa wake uke, hushamiri
Hasara, ya peke yake, hudhurika
Zinduka
(Wasakatonge 2004:02)
f) Mtindo wa kuhoji
Huu ni mtindo unaotumiwa na mwandishi wa kuuliza
maswali ambayo aidha majibu yake yako wazi au hayako wazi hivyo mtindo huu
unaweza kutumika kama tashtiti.
Mfano: Si
wewe?
Ukinijia mapema kama ukidayatema,
Nikawa kama wako baba na mama,
Kakulea kwa ugonjwa na uzima,
Ni wewe uso hisani.
Si wewe?
Niliyekunyima chungu kukutafutia tamu,
Kila kichota hakisishi hamu,
Ukazoa bila kufahamu,
Kuhujua kuichota,
Ni wewe ujilaumu.
(Fungate la uhuru 1996:42-43)
g) Mtindo binafsi
Huu ni mtindo ambao mwandishi anaweza kutumia nafsi ya
umoja au wingi au nafsi kundi kila nafsi ina maana yake kimaudhui.Nafsi moja
huzungumzia mambo fulani yanayomkabili mtu mmoja tu.Mara nyingi huwa ni maonyo,
mawaidha au sifa.
Mfano:
Umeshapwelea nchi kavu,
Wako werevu umekwisha,
Sasa tunatweta,
Utaabani,
Ni wewe ulo mrafi,
Si wewe?
(Wasakatonge 2004:21-22)
Nafsi nyingi hutokea pale mashairi anapozungumzia na
kundi fulani la watu huku na yeye akiwa mmojawapo.
Mfano:
Hatukubali tena,
Kwetu kurudisha ubwana,
Kwetu kuurejesha utwana,
Kwetu kuurejesha utumwa.
Hatukubali katu,
Ndani ya nchi yetu.
Hiyo huru.
(Wasakaonge
2004:30-31)
Lakini nafsi kundi hutoka pale ambapo mwandishi au
msanii anapozungumza na kundi la watu huku yeye akiwa ama msimulizi.Hutoa
masimulizi kama hadithi au hotuba fulani.
Mfano: Jua
kali ni wasakatonge.
Wao ni wengi ulimwenguni
Tabaka lisilo ahueni
Siku zote wako matesoni
Ziada ya pato hawaoni
Lakini watakomboka lini?
(Wasakatonge 2004:5)
h) Mtindo ambao unaruhusu kipande kizima cha
mstari wa mwisho wa ubeti kuweza kurudiwa, kikiwa ni chanzo cha huo ubeti
unaofuata:-
Iwapo mstari wa mwisho wa ubeti wa kwanza ulikuwa kama
“Uwanjani nayanena, leo wote wataona” Basi ule mstari wa kwanza na ubeti wa
pili utaanza na “leo wote wataona”
Mfano:
Chochote ulichonacho, kilikuwa kwa mwenzako,
Leo yeye hako nacho, kimesha hamia kwako,
Huenda utokwe nacho, kiende kwa mwingine
huko,
Kiumbe wacha vituko, sione ulichonacho.
Sione ulichonacho, ukaendesha vituko,
Na
upambwe chokochoko, mwishowe ni pukutiko,
Malao akupambacho, kilipambiwa mwenzako
Kiumbe wacha vituko,sione ulichonacho.
(Sheria
za kutungo mashairi na Diwani ya Amri 1967:30)
Kimsingi mitindo katika ushairi
ni mingi sana na hutegemea ufundi wa mshairi katika kuunda mashairi yake na
ushair unaweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa.
ii) Miundo ya Mashairi
Muundo ni neno pana ambalo
hujumlisha mjengo wa shairi yaani jinsi ulionekana.Mashairi yana mundo
mbalimbali kutegemea ufundi wa mshairi mwenyewe kimsingi Shairi linaweza kuwa
la kimapokeo au likawa Shairi huni (kisasa) Shairi la kimapokeo huwa na
mpangilio maalumu wa vina na mizani, silabi, vituo, beti n.k.Idadi ya mistari
huzaa aina mbalimbali za mashairi.
a) Muundo wa Tarbia
Kila ubeti wa shairi huwa na mistari mine na kila
mstari huwa na mizani kumi na sita (16) vile vile katika muundo huu kila mstari
unakua umegawanika katika viande viwili vilivyo na mizani sawa kila kipande
kukiwa na mizani nane.
Mfano:
Amkeni kumekucha, wakubwa hata wadogo,
Wadoho siku waacha, kwa kuogopa
kinyongo,
Kinyongo sikuficha, kukificha ni
uongo,
Mnapowacha madogo, na makubwa
mtawaacha.
Na wakubwa mtawaacha, mnapoacha
madogo,
Mfano kama kuchacha, chakula japo
kidogo,
Kidogo kinapochacha, kikubwa hakina
kingo,
Mnapowacha madogo, na wakubwa
mtawaacha.
(Masahiri
ya Saadani 1972:25)
b) Muundo wa Tathnia
Kila ubeti wa shairi huwa na mistari miwili muundo huu
unatiwa zaidi katika nyimbo si muundo ambao hutumika sana katika mashairi ya
kawaida ya kusomwa kam mashairi au ya kuimbiwa.
Mfano:
Mjamzito, umelazwa “Thieta”
Lazima kupasuliwa
Chake kitoto tumbo kinatweta
Hawezi
kujifungua
Mwili u moto, tumbo linamkeketa
Kwa
kite anaunguwa
Jasho na Joto, kiungo cha mpwita
Na
mauti yanamwita
Ni jambo zito, daktari kufata
Wauguzi
waameitwa
(Fungate la uhuru 1988:08)
c) Muundo wa Tathilitha
Kila ubeti wa shairi unakuwa na mistari mitatu
Mfano:
Kujitawala si kwema, kuliko kutawaliwa,
Kujitawala ni umma, kila yao kuamua,
Kujitawala si kama, wanguzi na
rushwa.
Kujitawala khatamu, na umma
kushikiliwa,
Kujitawala hukumu, makosa
kushitakiwa,
Kujitawala si sumu, mara kwa mara
kuuwa.
Kujitawala kisomo, kupiga kubwa
hatua,
Kujitawala kilimo, njaa na kuondoa,
Kujitawala si somo, njiani
kusimuliwa.
d) Muundo wa Takhimisa
Kila ubeti wa shairi unakuwa na mistari, mitano
Mfano: Hao
nyani wanaruka, mara hapa mara kule,
Hao nyani wanabweka, hawaoni soga
mbele,
Hao nyani wanaanguka, waingiwa na
ndwele,
Nyani wanababaika,misitu una upele
Msitu haukaliki, nyani wanahangaika.
Msitu wawaka moto, kufukuzwa hao
nyani,
Umeligundua pato, la nyani lenye
utani,
Moto waziona kwato, zilizoko
mapangoni,
Nyani
watupa watoto, hawakubaliki mwituni
Msitu haukaliki, Nyani wanahangaika.
e) Muundo wa Sabilia
Katika muundo huu mtunzi au mshairi anakuwa na uhuru
wa kuweka zaidi ya mistari mitano katika kila ubeti, ubeti unakuwa na mistari
sita na kuendelea
Mfano: Mmea
unapokuwa, huifurahisha mvua.
Lakini siposogea, hulisingizia jua
Uliamini ni mola, hata maji
kukupatia
Ulikubali kabila, haliishi bila mila
Mwanadamu kadhalika, kukua kufurahika
Huupenda uhakika, wa nyota yake
kufika
Umri wa kuridhisha, huhitaji
kujitwisha
Hapa, ukiufikisha, huona, kufanikiwa
Maisha ya hupenda, ni, mazuri ya
kwenda
Na siyo yenye kupinda, haya daima hupenda
(Diwani ya Mloka 2002:18)
f) Muundo wa mistari mine
Muundo huu unaweza kuwa na mizani nane au
pungufu.Muundo huu ni wa Abdilatifu Abdalla (1973) mfano ametumia katika
mashairi yake ya “Kamili wazi” “mnazi”
“Jana na leo na kesho” na “Njia
panda” mara nyingi huo mstari wa mwisho kina chake huwa ni sawa na kina cha
mwisho wa mstari mwingine katika ubeti wao
Mfano:
Kimbunga mji wa Siyu, kilichowahi kufika.
Si kwa yule wala huyu, ilikuwa
patashika
Kimeingoa mibuyu, minazi kunusurika
Nyoyo zilifadhaika
(Kimbunga 1995:01)
iii) Matumizi ya Lugha.
Hiki ni kipengele muhimu sana
katika kazi yeyote ile ya Sanaa ya kifasihi. Matumizi ya Lugha ndiyo
yanayofanya kazi fulani ionekane tofauti na nyingine au itofautishe kazi ya
Sanaa ya kifasihi na ile isiyo ya kifasihi.Luha ndiyo mzizi wa kazi ya fasihi
kwani fasihi ni kazi ya Sanaa inayotoa maudhui ya kutumia Lugha ya
maneno.Matumizi ya Lugha katika kazi ya fasihi yako ya aina mbalimbali
a) Methali, misemo na nahau
Mhakiki anapaswa avifahamu na ajue kuvichambua katika
ushairi.Vipengele hivyo vina kazi ya kufafanua maudhui ya kazi ya fasihi
METHALI
Ni kazi ya Sanaa ya kifasihi inayotumia mafumbo kwa
kwaida semi zote zina hakima ndani yake.Ubora wa hekima hiyo hutegemea muktadha
hali ambapo methali hutumika.Methali pia ina kazi ya kufurahisha, kutisha,
kuonya nakadhalika, waandishi hutumia methali katika kazi zao nani jukumu la
mhakiki kuzitambua hizo
MISEMO NA NAHAU
Matumizi ya misemo na nahau hushabihana na yale ya
methali.Misemo, misimu na nahau huzaliwa, hukua nap engine hufa
-Sekela
amenipaka mafuta kwa mgongo wa chupa (sekela amenipa sifa zilizostahili)
-Juma
katutangulia (Juma amekufa)
b)
Tamathali
za Semi
Mulokozi &
Kahigi wanasema kuwa tamathali za semi ni maneno, nahau au semi ambazo hutumiwa
[H1] na
waandishi wa fasihi ili kutia nguvu na msisitizo katika maana, mtindo, na
pengine sauti katika maandishi hayo.Tamathali za semi zinatumiwa pia [H2] kuipamba
kazi ya Sanaa ya kifasihi kwa kuongeza utamu wa Lugha.
Baadhi ya
tamathali za semi ni:-
Ø
Tashbiha
Hii ni tamathali ya ufananisha au mlinganisha wa vitu
viwili au zaidi katika tashbiha kama ilivyo katika sitiari huwa kuna vitu
vitatu vinavyofananishwa ambavyo wataalamu wameviita kuzungumzwa, kufananisha
na kiungo.Katika tashbiha hakuna maana dhahania bali kuna ulinganishaji wa vitu
viwili vilivyobayana.
Mfano: Kweli
ni sawa na radi, inapotoa kauli…
Kweli
kinywnani ikiwa sawa na moto wa nili
Kweli kama msumeno hukoreza sawa kweli
Ø
Tashhisi
(uhaishaji)
Washairi mara nyingine huweza kukipa kitu kisichokuwa
na uhai sifa za kitu chenye uhai, hasa sifa za binadamu, kisanaa maelezo ya
kitashhisi huwa na upekee unaomwingia msomaji akilini haraka, kwani si jambo a
kawaida, mathalani kuona mti “Ukimpungia mtu mkono” au “nyumba ikimkodolea
macho mgeni”
Mfano: kimya
hakineni jambo si kimya chawatazama…
Kimya chajazua mambo, pasiwe mwenye kusema.
Kimya kipimeni sana, msione kutosema.
Kimya hakichi kunena, kitakapo kusimama.
Kimya chaja watukana, na kizuwe yalozama.
Katika ubeti huu “kimya” (ambayo ni nomino dhahania)
kimepewa sifa za binadamu kinaweza kunena, kutazama, kuzua mambo, kusimama na
kutukana.
Ø
Metonumia
Hii ni tamathali inayotumia neno (au semi) kuwakilisha
neno, kitu, mtu au dhana nyingine yenye kuhusiana nalo neno hilo huweza
kutumiwa kwa kuwa dhana inayozungumziwa au kwa kuwa linataja ktu ambacho ni
sehemu na kuwakilisha cha kitu kingine kikubwa zaidi.
Mfano neno “kitambi” huweza kutumiwa kuwakilisha
tajiri au kabila “meno” huweza kuwakilisha kicheko
Ø
Mubalagha
Ni matumizi ya lugha yaliyotiwa chumvi ili kuongeza
utamu na kuleta athari fulani katika ushairi wa majigambo, tamathili hii
hutumika sana maana huo ni ushairi wa kujitapa na mtu mwenye kujitapa aghalabu
hujilimbikizia sifa. Mara nyingi mubalagha hutumika katika tenzi zenye
kusimulia habari za mashujaa.
Mfano: katika utenzi wa fumo Lyongo kuna mfano
unaokusudiwa kuonyesha ukubwa wa (kimo na umbo) na nguvu za Lyongo.
“Ruhu zikienda kishindo
Zima zao hukoma ondo
Huyo ni bwana wa kondo
Ashindaye jeshi miya
Ingawa wagala wanajulikana kuwa ni watu warefu akini
vimo vyao vilifika magotini tu (ondo) pia Lyongo
Ø
Kejeli
Ni usemi ambao maana ya ndani ni kinyume cha maanayake
halisi. Ni usemi wa kebehi ambamo kisemwacho na msemaji. Pia kejeli ni tukio
ambalo ni kinyume cha lile linatazamiwa au lililotakiwa na ambalo kutokea kwake
huwa ni namna ya dhihaka
Katika shairi la “Ibada na Haki” Shabaan Robert
anatumia usemi wa kejeli kukebehi watu wanothamini fedha kuliko dini.
Anasema hivi:
Huifanya fedha mungu wao
Itazame adha na Imani yao!
Na mwenye akili kama hana fedha
Hatajwi mahali ila kwa rakadha
Na kuadhiriwa kuwa mtu chini,
Tazama dunia ilivyo na dini
Katika mstari wa pili “Itazame adha na Imani yako!”
kuna kejeli, mshairi anachotaka kutuambia ni kwamba watu hao hawana adha wala
Imani katika mstariwa mwisho “Tazama dunia ilivyo na dini” Anakusudia kutuambia
“Tazama dunia ilivyo na dini kwa hiyo semi hizo ni kejeli
kinachosemwa ni kinyume na maana yake halisi kadha toka alama za mshangao!) zimetumika
kusisitiza hali ya kejeli.
MBINU ZA KISANAA
Kuna mbinu mbalimbali za kisanaa
ambazo hutumika katika kazi za kifasihi ya ushairi na ambazo mhakiki atatakiwa
azitambue na kuzifafanua mbinu hizo ni kama vile
Ø Takriri
Ni kurudia rudia
neno, sauti, herufi au wazo katika kazi ya Sanaa ya kifasihi.
Mfano: kweli kito mhabubu, mwenyezi nijaze kweli
Kweli siri ya ajabu, huwapa watu fadhili
Kweli chimbo la johari, linahimili la kweli
Kweli inatafakari, husema na kujadili
Katika ubeti huu
neno “kweli” limerudiwa rudiwa. Neno hili linasisitiza wazo kuu la mwandishi
Ø Onomatopea
Ni mwigo wa
sauti. Hutumiwa na washairi kutoa picha au dhana ya kile kinachowakilishwa au
kupambanuliwa na sauti hizo. Mfano tukisema “maji yalimwagika mwaaa!” neno
mwaaa! Ni onomatopea linawakilisha sauti au kishindo cha maji yanayomwagika.
Baadhi ya onomatopea ambazo zimekwisha kuwa sehemu za msamiati wa kawaida.
Mfano: pikipiki, bomboni, kata n.k.
Katika shairi la
“Cheke kwa furaha” Shabaan Robert ametumia onomatopea ili kuleta dhana ya
kucheka
“Dhiki ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?
Haya cheka ha! ha! ha! Ndiyo ada duniani
Basi cheka kwa! kwa! kwa! Usafike moyo
wote
Pamoja na malaika, wema mbinguni waliko
Maneno ha! ha!
ha! na kwa! kwa! kwa! Ni onomatopea
yanayotoa sauti ya kusikika ya sauti ya mtu anayecheka. Huu ni mpangilio
maalumu wa sauti ili kutoa picha ya kusikika ya dhana inayozungumzwa
Ø Mjalizo
Ni kuunganisha
maneno yanayofwatana bila kutumia viunganishi mfano: bila kutumia “na, kwa”
n.k. Mfano: Nilikaa, nikashangaa,
nikachoka
Niliimba, nikanuna, nikacheka
Ø Mdokezo
Hii ni mbinu ya
kisanaa ambapo mwandishi anaukatiza usemi fulani na kumuacha msomaji. Aghalabu
pana vielekezi vinavyoweza kumsaidia msomaji katika kukamilisha.
Mfano: wimbo la mauaji limezidi
Mashaka…ah! Shida tupu
Maneno…tena anyway…
Labda tusubiri.
Ø Tashtiti
Ni matumizi ya
maswali ambayo majibu yake kwa kawaida yanakuwa yameeleweka. Swali hili
linakuwa yameeleweka. Swali hili linakuwa kwa ajili ya msisitizo tu au
mshangao.
Mfano: Mtu anayemfahamu amekufa anauliza
-Adela ameachana nami?
Au mtu anayemfahamu amekutembelea
- Jamani hata Luiza naye kaja?
-Aisee ni wewe?
Ø Usambamba
Ni takriri ya
sentensi au kifungu vya maneno vyenye kufanana kimaana au kimuundo. Usambamba
huonekena sana katika ushairi simulizi
Shabaan Robert
amekitumia kipengele hiki mara kwa mara atika mashairi yake katika shairi lake
“kinyume” anasema
Tulifululiza mwendo lakini sana
twasita
Tulikwenda kwa mshindo lakini
sana twanyata
Katika mistari
yote miwili wazo linalosisitiza ni moja maneno tu ndiyo yanabadilika uwezo wao
wa zamani katika utendaji mambo unalinganishwa na udhaifu “wao” wa sasa.
c)
Taswira
au Picha
Dhana hii
hutumiwa kueleza neno, kirai au maelezo ambayo yanaunda picha fulani katika
akili ya msomaji. Taswira zinaweza kuwa za kimaelezo (yaani maelezo fulani
yanaunda picha) au za ki-ishara (zinazounda picha ambayo inaashiria jambo
fulani au imeficha ujumbe mwingine). Taswira huweza kuundwakwa matumizi ya
tamathali za semi hasa tashbiha na sitiari.
Kimsingi taswira
nyingi ni taswira za uoni (yaani zinamchochea msomaji kuona picha fulani)
Mfano: Neno lenye mzunguko, halipatikani mwisho,
Wa huku hafiki huko,wala halina
matisha.
Halishibishi huchosha, wala hapati utuvu,
Heri ya mtu ni kwenda, njia iliyonyooka.
Na milima akapanda, apendako akafika,
Mabondeni akashuka, mwituni akatumbua,
Na mzunguko wa dira, mwisho wake ni dinani
Hupati kupenda bara, na hushuki baharini
Tazama mashaka gani, njia ya dira si njia
Katika shairi
hili tunapewa picha tatu mahususi picha ya kwanza ni neno linalozunguka mshairi
anatuambia kuwa neno ambalo halifuati njia iliyonyooka neno lenye mzunguko
halifiki mwisho wake na halileti mradi uliokusudiwa “Halina malisho”
Hapa neno
limefanya kuwa kitu chenye uwezo wa kutembea na kuzunguka
Picha ya pili ni
ya mtu aendaye safari ngumu kwa ujasiri na moyo wa dhati akipanda milima na
kushuka na mabonde akipenya misitu na kuvuka mito hadi kufika kule anapokwenda.
Huyu ni mtu asiyeogopa matatizo anayeshikilia njia ngumu lakini nyoofu,
alimradi anajua kuwa itamfikisha kwenye lengo lake. Ni mtu anayepamana na
matatizo badala ya kuyakimbia mtu wa kwenda njia iliyonyooka
Piha ya tatu ni
dira, dira ni chombo kitumiwacho na mabaharia na wasafiri wengine kusahihisha
majira yao, wasipotee njia. Dira ni chombo cha mviringo na mshale wake aghalabu
huzungukia palepale ulipo, katu hautoki nje ya dira. Picha hii inasisitiza wazo
la mwandishi kuwa njia yenye kuzunguka haiwezi kumfikisha mtu kwenye lengolake.
Mshale wa dira huzunguka daima lakini haufiki kokote.
Picha hizi tatu
kwa pamoja zimefaulu kufikisha ujumbe wa mwandishi kuhusu maisha na namna ya
kuyakabili tuyakabili kwa juhudi na ujasiri na nia.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu ni vyema liwiane
na yale yaliyomo ndani ya kitabu hicho. Mfano: “Fungate la uhuru” (1988) jina
hili linawiana vipi na yale yaliyomo ndani ya kitabu hicho?
PICHA YA JALADA KATIKA UCHAMBUZI
Kazi ya kifasihi kuwa na picha au
michoro fulani kwenye majalada yao. Inawezekana majalada hayo yakawa na
uhusiano fulani na dhamira na maudhui ya kazi zinazohusika. Picha hizi huweza
kuwa kielelezo muhimu cha fani kwenye uchambuzi wa kazi ya kifasihi. Hata hivyo
si kazi zote za kifasihi ambazo zinaonyesha uwiano kati ya majalada yake na
yaliyomo.
UHAKIKI WA VIPENGELE VYA MAUDHUI
Maudhui katika mashairi
hupatikana baada ya mhakiki kupitia beti zote za shairi lile ili kupata ujumbe
wa shairi lazima itambidi mhakiki ajumlishe yaliyo katika beti mbalimbali za
shairi lile.
Kwa ufupi katika ushairi
uchambuzi wa maudhui mhakiki anapaswa kuangalia:
Ø DHAMIRA
Ni wazo kuu
katika kazi ya fasihi.
Ø UJUMBE
Ni mafunzo
mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazifulani ya fasihi.
Ø FALSAFA YA MWANDISHI
Ni wazo ambalo
mtu anaamini lina ukweli fulani unaitawala maisha yake.
Ø MSIMAMO WA MWANDISHI
Ni hali ya
mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili linaweza kuwa
halikubaliki na wengi, lakini yeye atalishikilia tu.
Ø MTAZAMO WA MWANDISHI
Ni hali ya
kuyaona mambo katika maisha kwa kuzingatia mazingira aliyonayo msanii mwenyewe
HATUA ZA UCHAMBUZI WA USHAIRI
Katika uchambuzi huu wa vitendo,
kielelezo tutatumia shairi la “Wauwaji wa Albino wapigwe vita” Shairi hilo
linasema hivi:
Kwa kweli inashangaza, ni mambo
hufikirika,
Ukijaribu kuwaza, wenzetu
wanatutukana
Albino wanaweza, kifo
kimeshawafikia
Ni wauwaji wabaya, vikali
walaaniwe.
Ni unyama wa kuzidi, albino
kuwashika
Huu wote ni ukaidi, utajiri
kuusaka
Tena ni kwa makusudi, maovu
umeyashika
Ni wauwaji wabaya, vikali
walaaniwe.
Mikononi wanawakata, kwa mashoka
na mapanga
Kuwasema sita sita, huu wote ni ujinga
Kwa vitisho wajikita, kusikiliza
waganga
Ni wauwaji wabaya, vikali
walaaniwe.
Albino tuwalinde, wamekuwa almasi
Wasakwa kila upande, sababu ya
ibilisi
Yatupasa tuwalinde, binadamu kama
sisi
Ni wauwaji wabaya, vikali
walaaniwe.
Majumba kuyabomoa, pande zote
kuzunguka
Damu isiyo hatia, kwa wingi
inamwagika
Mola inamlilia, hukumu ipo hakika
Ni wauwaji wabaya, vikali
walaaniwe.
Albino ni wenzetu, uzao wao ni
halisi
Acha tofauti zetu, tena tuwape
nafasi
Tujenge taifa letu, tuuache
ukakasi
Ni wauwaji wabaya, vikali
walaaniwe.
Ujinga na upumbavu, kuwaua albino
Wajawa maumivu, mikono na
visigino
Sahitaji utulivu, upole
mshikamano
Ni wauwaji wabaya, vikali
walaaniwe.
Zamu yako inakuja, mwisho wao
utafika
Wenyewe watajitaja, tena bila ya
mashaka
Sote tuwe na umoja, kufungua
mashtaka
Kuwasaka wauwaji, kusudi
wahukumiwe.
HATUA ZA KUCHAMBUA SHAIRI
1. Lisome
shairi zima toka manzo hadi mwisho ili upate picha ya jumla, kimaana na kiumbo
ya shairi hilo. Katika hatua hii kama shairi ni gumu linaweza lisieleweke, kwa
bahati shairi la “wauwaji wa albino wapigwe vita” linaeleweka bila tatizo
2. Rudia
kulisoma tena shairi hilo polepole, andika maana ya jumla unayoipata. Unaweza
kupata maana zaidi ya moja katika “Wauwaji wa albino wapigwe vita” maana ya
jumla inayojitokeza ni maombolezo ya mauwaji ya Albino
3. Huku
ukiwa na kalamu yako ya risasi, rudia kulisoma tena shairi hilo mstari baada ya
mstari. Pigia kila neno usemi, sentensi au kipengele kinachoelekea kuwa na
umuhimu au dhima maalumu ya kifani au kimaudhui.
Katika shairi
ili pengine utayapigie mstari mafungu ya maneno yafuatayo:
-Albino wanaweza kifo
kimeshawafikia
-Ni wauwaji wabaya vikali
walaaniwe
-wasakwa kila upande sababu ya
ibilisi
-damu isiyo hatia kwa wingi
inamwagika
-Albino ni wenzetu uzao wao ni
halisi
4. Jaribu
kufanya kisisisi maneno hayo yalyopigiwa mstari au kuorodheshwa katika hatua ya
tatu bila shaka yapo mambo ambayo undani wake hutauelewa katika hatua hii,
hivyo aghalabu itabidi
a)
Urejee mambo hayo yalivyotumika
b)
Urejee katika muktadha wa shairi hilo kama una
ufahamu kwa upande wa wauwaji wa Albino wapigwe vita, muktadha huo ni mauaji ya
Albino
Jiulize semi,
sentesi hizi zinasema/zinaonyesha au zinadokeza nini? Kwa nini mtunzi kaamua
kutumia maneno hayo na si mengine? Je yanahusiana vipi na maana ya jumla
uliyopata katika hatua ya pili.
5. Chunguza
vipengele vingine vya kisanaa na kimuundo alivyovitumia mtunzi. Jiulize kama
vinaoana na madokezo ya maana uliyoyapata katika hatua ya nne. Vipengele
unavyoweza kuchunguza katika hatua hii ni muundo wa shairi, vina, mizani,
wizani, takriri, milio ya maneno, tamathali n.k. kwa mfano hadhihirika kuwa
muundo wa shairi ni kijadi ambao hautuambii lolote kuhusu maana ya shairi hili
vifanye uchambuzi vipengele vya kisanaa ulivyovipambanua
6. Husisha
ufafanuzi wake hadi hatua hiina maana ya shairi iliyokwisha kujitokeza kuona
kama mambo hayo yanaoana barabara au bado kuna pengo au mkinzano.
Baada ya hatua
hii utakuwa umepata maana kamili ya shairi ambayo unaweza kuitetea kifasihi kwa
kurejea katika shairi lenyewe si lazima maana unayopata/unazopata ioane/zioane
na maana watakazopata wengine jambo muhimu ni kuwa na ushahidi wa kutosha
kuweza kutetea hoja zako.
Maana ambayo
umepata hadi sasa yaweza kuelezwa iwe:
Mshairi
anaomboleza mauaji ya Albino ambayo yanafanywa na watu mbalimbali kwa Imani za kishirikina
anaonyesha kuwa kuua binadamu wenzetu ni unyama na ni ukatili. Anamwomba Mungu
awaepushie Albino na mates ohayo.
7. Hadi
hatua hii umepata maana ya shairi lakini bado hujapata maudhui yake.
Ili kupata maudhui unatakiwa upambanue dhamir kuu ya/za shairi hili na uonyeshe
mtazamo wa mshairi kuhusu dhamira hizo. Katika shairi hili ni dhahiri dhamira
kuu ni “Mauaji ya Albino” mtunzi anasawiri tukio la mauaji ya Albino mwandishi
anaonyesha kuwa mauaji ya albino ni tukio lenye kuleta majonzi na kilio.
Mtazamo wake kuhusu mauaji ya Albino ni kwamba wanaofanya hivyo hawana utu
hivyo ni sawa na wanyama wa porini na anaonyesha kuwa kuwaua albino ni kinyume
cha utu
Mtunzi
anazungumzia pia dhamira ya ujinga. Mwandishi anaonyesha kuwa ujinga ni kikwazo
cha maendeleo ya jamii kwani wote wanaojihusisha na mauaji ya albino ni wajinga
na wanataka kupata utajiri kwa njia za mkato.
8. Katika
hatua hii mchambuzi ana uhuru wa kuithamini kusifu au kwaani. Baada ya
kulichambua na kulielewa vizuri shairi hilo katika hatua saba zilizotangulia
sasa unaweza kulitolea tathmini ya kifani na kimaudhui katika kufanya tathmini
ni muhimu kuzingatia muktadha wa wakati lilipotungwa na wakati wa leo.
Tathmini yako
itazingatia muktadha yote miwili unaweza kusema kuwa, shairi hilo lilipotungwa
ulikuwa na umuhimu wake leo labda umepungua kwa kuwa muktadha huo wa vifo vya
Albino umepita. Hata hivyo labda shairi limebaki na umuhimu wa kihisia na
kifalsafa kuhusu tatizo la maisha na mauti na ufumbuzi wake.
HISTORIA NA MAENDELEO YA KISHAIRI WA
KISWAHILI
Wataalamu wengi wanakubali kuwa
ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi hasa ngoma na nyimbo. Kabla ya karne ya
10 BK ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa na kugharura kwa ghibu bila
kuandikwa.
Kuanzia mwaka 1000 B, mambo
mawili yaliletwa na kuathiri ushairi, mambo hayo ni Dini ya kiislamu na
Uandishi wa hati ya kiarabu waswahili wengi walijifunza kusoma na kuandika hati
za kiarabu, hali hiyo ilienda sambamba na ustawi wa miji ya Pwani katika
biashara na majengo ya mawe mashujaa mashuhuri wa miji ya Pwani wanokumbukwa
katika tendi na masimulizihuenda waliishi katika hicho ni Fumo Lyongo wa
Shangapate kaskazini mwa upwa wa Kenya kati ya karne ya 8 na 9
Katika kipindi hiko washairi
wengi walitunga mashairi mengi kwa ghiba kwa sababu hayakukusudiwa kuhifadhiwa
kwa maandishi kwa kipindi kirefu ni tarihi na baadhi ya mswada hiyo imepotea.
Tungo zilizosalia ni Fumo Lyongo ambayo ilandikwa 1500 BK kutoka katika mapokeo
ya mdomo.
-“kumswifu” yanga au suifa ya
mwana ning utingo wa mwanzo kuhifadhiwa kwa maandishi.
Mwaka 1500-1700 BK kulikuwa ni
kipindi cha uvamizi wa maneno katika kipindi hicho tungo chache zilihifadhiwa
zikiwasifia maneno mashairi yaliyo wasifia wareno> mfano
-mzungu
mgeli} 1630
-Portugezi
Afala} 1630
Lakini tungo mashuhuri za wakati
huo ni:
·
Utendi wa Hamziyya (Seyyid Aidamis bin Athumani
1652)
·
Siri lasirari (Binti Lamba 1668)
·
Utendi wa Tambika (Taboka) {Mwango bin Athumani
1728}
-Siri Lasirari ni kisa cha kubuni
-Hamliyya ni tafsiri ya utendi wa
kiarabu kuhusu maisha ya Mtume Muhamadi
-Tabuta (tambuka) ulihusu vita
kati ya waislamu na warumi walikuwa chini ya mfalme Hela kali
1750-1900 kipindi cha waarabu
Sehemu kubwa za tendi mashuhuri
za wakati ambazo mpaka leo zipo ni:
·
Tendi za
dini na vitu
-
Utenzi wa Shufaka
-
Utenzi wa masahibu
-
Utenzi wa kijamaa
-
Utenzi wa mayasa na mikidadi
-
Utenzi wa Ras L Ghuli (unahusu vita vya waarabu
kati ya waislam na makafiri-{1855})
·
Tungo za
kitamaduni, mawaidha na Tumbuiza
Tungo hizi zilikuwa nyingi na zilikuwa katika
maandishi na zilihusu (maudhui yake) kueleza mandhari ya Afrika Mashariki mfano
tungo hizi ni:
-
Utenzi wa
Inkishafi (1810)
Mtunzi: Seyyid
Abdallah bin Nasri.
Utenzi huu unazungumzia matokeo ya uvamizi wa waarabu
na wareno ambapo matokeo yake ni kuporomoka kwa mji wa Pate.
-
Utenzi wa
Mwana kupona (1858)
Unahusu utamaduni na misingi ya Dini. Utenzi huu
uliandikwa kama wosia kwa binti yake na kwa kiasi kikubwa unahusu unyumba pia
ndani yake kuna mafundisho ya unyago kwa watu wa Pwani.
Kundi jingine kubwa ni mashairi
ya siasa kundi hili liliwakilisha/lilisimamiwa na akina Muyaka bin Haji wa
Mombasa. Huyo alifunga mashairi ya kupinga waarabu wa Oman
-
Suid bin Said (1810-1876)
-
Kibabina (1776-1834) na wengine.
Wote hawa walitunga mashairi yaliyohusu
harakati za kisiasa na kijamii za wakati huo, wa baadhi yao walifungwa au
kuuwawa gerezani kwa sababu ya kupinga kutawaliwa. Mchango mkubwa wa hawa ni
kuendeleza mashairi ya unne (tarbia)
Kwa ujumla katika kipindi hiki
mambo yaliyojitokeza katika maendelezo ya ushairi ni manne:
i)
Umbo la tarbia (unne) ulifika kilele
ii)
Utendi
iii)
Kanuni ya utunzi ziliwekwa wakati huo
iv)
Hati ya maandishi (Kiswahili n kiarabu)
ilisanifiwa kuzingatia sauti za lugha ya Kiswahili.
1885-1918 USHAIRI WAKATI WA UKOLONI WA KIJERUMANI
Ushairi wa wakati huo unaweza
kugawanyika katika makundi matatu.
i)
Ushairi wa kawaida-mashairi haya yalihusu
mawaidha, mapenzi na dini.
ii) Ushairi
wakusifu wakoloni- huu uliandikwa kwenye magazeti na vitabu mfano kitabu
maarufu cha Dr. C
Velter (1907)
Prose and Poesie der Sua heli
Kitabu hiki
kilisifu utawala wa kidachi
iii) Ushairi
wa upinzani.
Huu ulipinga
utawala wa kikoloni.
Mfano: utenzi wa
vita vya wadachi (H.Abdallah)
Utenzi wa vita vya majimaji
Katika kipindi
hiki mambo matatu yalitokea katika ushairi kwa upande wa Tanzania.
a.
Kuandika kwa kutumia hati ya kirumi hati hii
ulienea kwa kupitia Elimu kanisa na ilianza kutumiwa na watunzi baada ya hati
ya kirabu
b.
Utafiti kuhusu ushairi ulianza wakati huo na
wachambuzi maarufu walikuwa C.Velter Buttner na K.Mein holf n.k
Hawa walisaidiwa na waafrika kama vile Mohamed Kajunwa,
utenzi wa Fumo Lyongo Rev.Taylor ndiye aliyekusanya mashairi ya Fumo Lyongo.
1918-1961 UKOLONI WA KIINGEREZA
Kipindi hiki kiliambatana na
mambo matatu mapya:-
a)
Elimu
Hii ilieneza
lugha ya Kiswahili na ushairi katika maeneo ya bara kupitia shuleni maarifa ya
kusoma na kuandika. Hati ya maandishi ya kirumi ilienea kupitia elimu
b)
Kuanzishwa
kwa mashirika ya uchapishwaji.
Katika kipindi
hiki magazeti mengi yalichapwa kwa lugha ya Kiswahili na kusambazwa. Baadhi ya
magazeti yalikuwa na kurasa maalumu ya ushairi ambapo ulisaidia kuwakutanisha
watunzi kutoka Afrika Mashariki.
Mfano: Gazeti la
“Mambo leo” 1923 kupitia gazeti hilo watunzi maarufu kama S.Robert, Mdanzi
Hamasa, Mzee Waziri (kijana) walipata umaarufu kupitia mambo leo
Pia kuanzishwa
kwa shirika la wachapishaji vitabu Afrika Mashariki (E.A.L.B) kulisaidia sana
kukuza na kueneza Sanaa ya ushairi.
c)
Shughuli
za siasa za kudai Uhuru ziliibua ushairi wa kisiasa mnamo mwaka 1950-1960.
Mfano: S.Kandoro
alitunga mashairi mengi pia kipindi hicho ushairi ulikuwa wa aina.
1. Mashairi
yaliyosaili mfumo wa uchumi wa kikoloni. Matatizo ya kazi, umanamba, mshahara
mdogo n.k haya yote yalitolewa na gazeti la mamba leo.
2. Mashairi
yaliyohusu utaifa yalianza miaka 1930. Haya yalijiuliza mwafrika ni nani? kwa
nini mzungu yupo hapa?
Mfano: S.Robert- mashairi ya kutetea weusi mfano
Shairi la Rangi zetu.
S.Kandoro kwetu ni kwao kwa nini
Pia kulikuwa na mashairi ya kutetea Lugha.
S.Robert (Titi la mama li Tamu)
S.Kandoro (Kitumie Kiswahili)
3. Mashairi
ya kisiasa ambayo yalihimiza watu waungane ili waweze kujitawala wenyewe
S.Kandoro shairi la siafu wamekazana
4. Pia
kipindi hiki walitokea wachunguzi wengi sana wa ushairi wa Kiswahili.
Mfano: Withchens (1930), A.Wine, B.E.Damman
(1930-50) Lumbart, H.Cory W.Whitely n.k. “wazungu”. Waafrika Sr. Mbarak Hisway,
Hamis Kitumbey
USHAIRI BAADA YA UHURU
Baada ya uhuru ushairi ulisambaa
zaidi kutokana na msukumo wa kisiasa fani mpya mfano Ngonjera na mtiririko au
tungo huru zilizanziashwa ili kuzingatia mahitaji mapya ya kisiasa na kisanaa.
Ushairi wa Kiswahili baada ya uhuru ulikuwa wa aina kuu mbili
1.
Mashairi ya
kawaida: Haya yalitungwa sana magazetini na vitabu vya mashairi mbalimbali
vilichapishwa ambapo Dhamira za malezi, mapenzi , dini, mawaidha n.k.
o
Akilimali snow- white
o
Mwinyi khatibu- Mohamed
o
Andanenga
o
S.Kandoro
o
S.Robert
2.
Mashairi
ya kisiasa: Hapa kuna makundi mbalimbali ya mashairi ya kushangilia Uhuru.
Mfano: Utenzi wa uhuru wa Tanganyika
Utenzi wa jamhuri wa Tanzania
Utenzi wa uhuru wa Kenya.
a) Mashairi yanayojadili dhamira ya ujenzi wa
jamii mpya. Katika mashairi yao walisisitiza watu wafanye kazi ili kuinua
pato.
Mfano: S.Kandoro
katika shairi la kujitawala
J.K.Nyerere-chombo cha taifa
letu
b) Mashairi ya Ujamaa
Hayo yalitokea
baada ya Azimio la Arusha ambalo yalisisitiza siasa ya ujamaa na kujitegemea,
ambapo walipinga unyonyaji, ukupe, ukabila na ubepari. Walitukuza kilimo na
kuwashawishi watu kurudi shamba (kijijini)
Mfano: Mashairi
ya Azimio la Arusha (kamaji), Ngonjera za Matias Mnyapara, Mashairi ya miaka 10
ya Azimio la Arusha ( Abdulah)
Tatizo kubwa
lilijitokeza katika hiki ni ukasuku ambapo waandishi wengi walikariri hotuba za
viongozi bila kuzifanyia uchambuzi na kuziandikia mashairi.
c) Mashairi yaliyohakikii siasa yaliyokuwepo
na hawa walikuwa na mitazamo mbalimbali.
·
Wanauhalisia
Walihakiki dhana ya ujamaa na ukombozi na kuchambua
mafanikio ya matatizo yake hasa katika utekelezaji wa malengo ya Azimio la
Arusha. Waandishi hao ni E.Kezilahabi, E.Husein, Z.Mochiwa na T.A.Mvungi.
·
Washairi
wa Malengo wa kushoto
Hawa walikuwa na mambo yafuatayo walichukua msimamo wa
kufanya kazi na mkabala wa kitabaka katika kutolea tungo zao
·
Waliona
usoshalist kama suluhisho la matatizo yao.
Ili usoshalist upatikane waliona ni lazima kumwaga
damu (kutumia nguvu). Kundi hili lilikuw na K.Kahigi, na M.Mulokozi, Ally
Salehe, M.S.Khatibu, A.Abdullah na S.A.Mohamed.
Hivyo Sanaa hii ambayo ilianza upwa wa Kenya na
Tanzania katika kare ya 10-15 sasa imeenea Afrika Mashariki nzima hadi Rwanda,
Burundi na Kongo
MGOGORO KUHUSU USHAIRI WA KISWAHILI
Mgogogro huu ulianza mwisho mwa
miaka ya sitini (1968) na mwanzoni mwa miaka ya sabini. Mgogoro ulihusisha
pande mbili washairi wa kimapokeo (wasiokubali mabadiliko hawa walisisitiza
kuwa vina na mizani ni uti wa mgongo wa shairi la Kiswahili) wanamabadiliko
waliona kuwa si lazima shairi liwe na vina na mizani.
Sababu kuu zilizozua utata ni
mbili
i.
Maana ushairi kwa ujumla
ii.
Maana ya shairi la Kiswahili
Mvutano huu unahusisha na
mabadiliko ya kidunia yaliyotokea miaka ya Sitiari na Sabini katika Nyanja
mbalimbali za maisha hata kupelekea washairi nao kuhitaji mabadiliko katika
tasnia ya ushairi kwa upande wa fani
Msukumo huu wa kuleta mabadiliko
katika tasnia ya ushairi uliletwa na wanazuoni akina E.Kezilabahi, Jared Angira
na E.Husein wasomi hawa walijishughulisha na utunzi wa mashairi hivyo baada ya
kusoma fasihi za nchi mbalimbali waligundua kuwa vina na mizani ni wazo
zilizofuatwa na washauri wote duniani hivyo waliamua kuasi sharia hizo ili
kuleta mabadiliko ya kuondoa minyororo iliyowafunga kuhusu utungaji wa shairi
la Kiswahili kwa pamoja waandishi hawa waliweza kutunga mashairi mengi au tungo
zisizofuata niaza ya vina na mizani na pia waliungwa mkono na watunzi wengi
kama vile M.M.Mulokozi, K.K.Kahigi miaka ya themanini washairi wengi waliibuka
kuungana na kundi hilo. Mfano: Henry MhanikanaT.Mvungi
Madai ya wana mabadiliko kutunga
tungo zao yalikuwa kama ifuatavyo:
1. Mbinu
na njia za kutunga mashairi ya Kiswahili zilikuwa chache mno.
2. Kutunga
kwa kufuata taratibu za muundo wa tungo za Kiswahili (mapokeo) kuliwanyimia
uhuru walidai kuwa hakuna sharia za utunzi wa mashairi katika (diwani ya Amri)
(sharia za kutunga mashairi).
3. Muundo
wa tungo zao zisizofuata kaida ni wa kiasilia. Hii ina maana kwa ushairi wa
mwanzo haukuwa na mizani wala vina.
Kwa namna nyingine tunaweza
kusema kuwa mgogoro huo ulijitokeza baina ya wazee akina Kuluta Amri Saadam
Kandoro, Ustadhi, Andamenga, Shihabdini chira hdin n.k na vijana akina
E.Kezilahabi na Uanza.
KUHAKIKI RIWAYA
Riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni
yenye mawaidha, lugha ya nathari, mchanganyiko wa visa, wahusika kadhaa na
matukio yaliyosukwa kimantiki yenye kufungamana na wakati na kushabihiana na
maisha halisi.
SIFA ZA RIWAYA
1.
Urefu, Riwaya kwa kawaida huwa ndefu
ikilinganishwa na tanzu nyingine za kinathari kama vile hadithi fupi. Mfano wa
Riwaya ya Bwana Mnyombokera na Bibi Bagomoka (198 ) iliyoandikwa na Kiterezi,
Hii ina mamia ya kurasa
2.
Matukio,Riwaya humulika hali halisi
ya maisha ya binadamu ingawa matukio ya riwaya si lazima yawe ya kweli
yametokea, yanaweza kupatikana katika ulimwengu halisi wa binadamu matukio kama
vile rushwa, wizi wa mali ya umma, matabaka, uongozi mbaya, athari za pesa
katika ndoa na mapenzi na tatizo la usafiri Dar-es-salaam katika “Pepo ya mabwegwe” (1981) iliyoandikwa
na Mwakyembe, mambo yaliyoandikwa yamo katika jamii yetu kwa sasa.
3.
Muundo,Riwaya huwa na miundo
changamano ukilinganisha na kazi nyingine za kinathari. Riwaya inaweza kua na
muundo wa msago, rejea au rukia, wakati mwingine inaweza kuwa na muundo
changamano yaani inakuwa na muundo miwili katika kazi moja.
4. Mandhari
yake ni pana
Mandhari ya riwaya ni mapana na kikamilifu kwani
riwaya hushughurikia mawazo mengi, hujishughulisha na vipengele vingi vya
maisha ambavyo hupatikana katika nyakati na mahali tofauti kama vile shuleni,
mijini, vijijini, nyumbani, barabarani n.k. ili kushughulikia mazingira mapana
mwandishi hutumia kipindi kirefu cha wakati ikilinganishwa kazi nyingine kama
vile hadithi fupi ambayo huweza kuchukua kipindi kimoja tu kukuamilika.
5. Wahusika
,Wahusika wa riwaya ni wengi na waliokuwa zaidi. Riwaya hushughulikia
masuala mengi huwa na wahusika wengi wanaomwezesha mwandishi kukidhi haja hiyo
kuna wahusika wanaobadilika kwa lengo la kuonyesha hali halisi ya maisha kuna
wale wasiobadilika ili kutumiwa kukashifu au kuhimiza hali fulani n.k. Riwaya
ya Ziraili na Ua la faraja na Mkufya na Makuadi wa Soko Huira iliyoandikwa na
Chacha Gezina wahusika wengi.
6. Mtindo,Riwaya
hutumia mtindo wa wasimulizi, monolojia au dayolojia na nafsi zote tatu.
Mwandishi anaweza kuwa ndiye msimulizi au mhusika fulani akawa ndiye
anayesimulia au wahusika wakawa wanajibizana wao kwa wao.
Mfano: Njama (1981), Uchu (2000), Kikosi cha
Kisasi(1979) vya musiba ametumia zaidi mtindo wa monolojia na dayolojia kidogo.
AINA/TANZU ZA RIWAYA
Kuna michepuo miwili ya riwaya ambayo ni;
A.
RIWAYA YA DHATI
Riwaya dhati ni riwaya yenye kuchambua masuala mazito
ya kijamii, kutafuta sababu zake athari zake na ikiwezekana ufumbuzi wake. Ni
riwaya inayokusudiwa kumkera na kumfikirisha msomaji, sio kumstarehesha mtu.
MATAWI YA RIWAYA YA DHATI
1.
Riwaya ya
kijamii
Ni riwaaya inayosawiri maisha na matatizo ya kawaida
ya jamii. Matatizo haya huweza kuwa ya kifamilia, kiuhusiano wa kitabaka ya
kisasa ya kiutamaduni n.k. Utanzu huu ndiyo wenye idadi kubwa zaidi ya riwaya.
Mfano: -Shabaan Robert “Siku ya watenzi wote”
(1968)
-M.S.Moamed “Nyota ya Rehema” (1978)
-S.A..Mohamed “Dunia mti mkavu” (1980)
-E.Kezilahabi “Rosa mistika” (1971)
-J.N.Somba “Alipanda upepo Akavuna Tufan”
(1969)
-Alex Banzi “Titi la mkwe” (1972)
2.
Riwaya ya
kisaikolojia
Ni riwaya inayododosa nafsi ya mhusika, fikra, hisia,
mawazo, Imani, hofu, mashaka na matumaini na matamanio yake binafsi na athari
za mambo hayo kwake binafsi na labda jamii yake. Baadhi ya watunzi
waliojipambua katika utanzu huu ni
-E.Kezilahabi “Kichwa maji” (1974)
-M.S.Mohamed “Kiu” (1972)
-S.A.Mohamed “Tata za Asumini” (1990)
-K.G.Mkangi “Ukiwa” (1973)
3.
Riwaya ya
kitawasifu
Ni riwaya ambayo husimulia habari za maandishi tangu
kuzaliwa kwakwe hadi pale inapokomea au hadi kufa.
Mfano:
-Shabaan Robert “Maisha Baada ya miaka Hamsini” (1966)
-Maisha ya Hemed Bin Muhamed “Tipu Tipu”
(1950)
4.
Istiara
Ni riwaya ya mafumbo ambayo umbo lake la nje ni ishara
au kuwakilisha tu cha jambo jingine.
Mfano: -Riwaya
ya Nathanuel Swift (1926)
-Safari za Gulliver (Mfasiri F.Johnson)
(1945)
-Shamba la wanyama (Msafiri F.Mkwegere)
Ni ishara ya mfumo wa utawala wa dikteta wa kisovieti
wa enzi za Staliri. Yaelekea pia riwaya Shabaan Robert (1951) kusadikika ni
ishara kuhusu utawala na mabavu wa kikolono.
5.
Riwaya ya
kigano
Ni riwaya yenye umbo la mtindo wa ngano mathalani
huweza kuwa na wahusika wanyama, visa vya ajabu ajabu, mandhari ya kubuni na
visa vyenye kutendeka nje ya wakati wa kihistoria.
Mfano:
-Shabaan Robert (1952) “Adui na nduguze”
-J.K.Kimbila (1966) “Lila na fila”
6.
Riwaya
teti
Ni riwaya inayosimulia vituko na masahibu ya watu,
wapuuzi, walaghai, wajanja na kwa njia inayosisimua na kuchekesha. Aghalabu hao
huwa ni watu wanaovutia wa tabaka la chini na bapa. Matukio ya Riwaya hii
hayana msukumo ulioshikamana vizuri shabaha yake mojawapo ni kuziteta na
kuzikejeli tabia za matabaka na watu mbalimbali katika jamii.
Mfano:
-Hadithi za “Hekaya za Abunuasi na Hadithi nyingine (1915) imefanana na
vituko vya riwaya teti.
7.
Riwaya ya
wasifu
Ni riwaya inayoandikwa na mtu mwingine kuhusu maisha
ya mtu mwingine tangu kuzaliwa hadi kufa kwake.
Mfano:
-J.Makabarah “Maisha ya Salum Abdallah” (1975)
-S.Robert “Wasifu wa Siti bint Saad” (1967)
8.
Riwaya
chuku
Ni riwaya ya vituko na masaibu yasiyokuwa ya kawaida
ni riwaya isiyozingatia uhalisia mara nyingi masaibu ya Riwaya chuku huambatana
na mapenzi, mfano; baadhi ya hadithi za Alfu-lela-Ulela (1929) ni chuku katika
fasihi ya Kiswahili. Riwaya za Shabaan Robert za “Adili na Nduguze” (1952) na “Kusadikika”
(1951) zinaingia katika kundi hili.
9.
Riwaya ya
kihistoria
Hii huchanganya historia halisi na Sanaa kwa makusudi
ili kutoa maudhui fulani. Mara nyingi riwaya hii hujikita kwenye matukio makuu
ya kihistoria yalioathiri mwenendo na mwelekeo wa jamii au taifa linalohusika
na historia ya kubuni, matukio ya kweli na ya kubuni. Hata hivyo riwaya hiyo
inazingatia zaidi namna matukio makuu ya kihistoria yalivyomwathiri na
yalivyoathiriwa na matendo ya mtu binafsi aliyeyashiriki baadhi watunzi
mashuhuri wa riwaya za kihistoria ni
Mfano: -Olef
Msewa “Kifo cha ugenini” (1977)
-M.Karuthi “Kaburi bila msalaba” (1971)
-S.A.Shafi “Kuli” (1979)
-A.Lihamba “Wimbo wa Sokomoko” (1990)
-B.Mapalala “kwa heri iselemaguzi” (1992)
-G.Ruhumbika “Miradi Bubu ya wazalendo”
(1992)
10.
Riwaya ya
kimaadili.
Ni riwaya inayowapa watu maadili mema na wengine
maadili hayo ni ya kidini wausika wanakuwa na sifa za kudumu kama vile upendo
wa ukarimu.
Mfano:
-Shabaan Robert “Adili na Nduguze” (1952)
-M.Mnyapala “Mrina Sali na wenzake wawili”
(1961)
-G.Mhina “Mtu ni Utu” (1971)
11.
Riwaya ya
kimapinduzi
Ni riwaya inayojadili matatizo ya kisiasa katika
jamii. Riwaya hii ni mwelekeo fulani wa kuleta mabadiliko ya kisiasa katika
jamii.
Mfano: wa riwaya hizi ni “kuli” (1978), Kabwela
(1978), Mzalendo (1977) Ubeberu Utawashinda (1971) n.k.
12.
Riwaya ya
kifalsafa
Ni riwaya zinazojadili migogoro ya kimaisha kifalsafa.
Riwaya hizi hujuliza maswali kama vile
-
Ukweli ni nini?
-
Maisha ni nini?
-
Kifo ni nini?
-
Kuwepo na kutokuwepo ni nini? n.k
Muundo wa riwaya hizi ni wa kimchangamano au a
mviringo na wahusika huvunjwa vunjwa hivyo mhusika wa riwaya hizi ni wazo tu au
hawapo kabisa
Mfano:
E.Kezilahabi- “Nagona” (1987) Mzingile (1991)
S.Mohamed- “Kiza katika nune” (1988)
K.G.Mkangi- “Mafuta” (1984) n.k
13.
Riwaya
Barua
Ni riwaya ambayo sehemu yake kubwa husimuliwa kwa njia
ya barua wanazoandikiana baadhi ya wahusika.
Mfano: -Mariam
Ba “Barua ndefu kama hii “(1980) Msafiri Maganda
-Walter Tribisch “Nampenda mvulana. Barua
ya siri” (1964)
14.
Riwaya ya
vitisho
Ni riwaya yenye visa vya kutisha na kusisimua damu
mara nyingi visa hivyo huambatana na mambo ya ajabu au miujiza
Mfano:
-C.Mung’ong’o “Mirathi ya Hatari” (1977)
-N.J.Kuboja mbojo Simba-mtu (1971)
15.
Riwaya
pendwa
Ni riwaya iliyokusudiwa kuwastarehesha na kuburudisha
msomaji tu lengo hili kulihimiza kwa kusawiri visa na vituko vya kusisimuwa
damu
Mfano: Vituko vya majambazi na uhalifu, ususi na
mahaba ya waziwazi.
Riwaya pendwa huwa na mafunzo kidogo kama lengo la
ziada katika Tanzania aina hii ya riwaya ililetwa kwa mara ya kwanza na Abdull
alipoandika riwaya ya “Mzimu wa watu wa kale“ (1957/8) na miaka ya 1960
-
Katalambwa (1965) simu ya kifo
SIFA ZA RIWAYA
PENDWA
1.
Matumizi
makubwa ya taharuki na utendaji
Taharuki
hutumika kuelezea hamu kubwa anayokuwa nayo msomaji katika kujua yatakayotokea
katika hadithi fulani. Taharuki hutokea pale ambapo msomaji ana hamu kubwa au
anajua yanayoweza kutokea laikini hajui jinsi yatakavyotokea.
Riwaya pendwa ni
riwaya ya taharuki kwa sababu ya kimsingi ya fani yake hujiweka katika mbinu ya
kisanaa ya taharuki. Taharuki imepewa nafasi kubwa katika aina hii ya riwaya
kwa njia ya vituko vya kusisimua vinavyojibainisha kwa njia ya mkingano
iliyosukwa kwa namna ya ufundi usiokuwa wa kawaida.
Kwa upande wa
utendaji wahusika wake n hodari sana katika kutenda, katika kuwindana, kupigana
kwa silaha na mikono mitupu na kufanya matukio yake utendaji unaojitokeza humu
unaziteka nafsi za wasomaji wake.
2.
Hutumia
wahusika walewale.
Riwaya pendwa
inasifa ya kutumia wahusika walewale hivyo ikawa na uwezo wa kujiendeza katika
vijitabu kadhaa. Karibu kila mwandishi maarufu wa aina hii ya riwaya ameandika
vitabu zaidi ya kimoja. Sifa hiyo ya kuwatumia wahusika walewale imefanya
kijitabu kimoja katika mfuatano wa vitabu kadhaa vya mwandishi mmoja kionekane
kama tukio linalojitegemea katika mfululizo wa matukio. Ili kuustawisha na
kuwisisitiza mfuatano huo, baadhi ya waandishi wameweza hata kudondoa kazi za
nyuma katika kazi zao za baadae.
-
Abdallah “Kosa la bwana Musa”
-
Hofu (1988) musiba
-
Salamu Toka Kuzimu (1993) Mtobwa
-
Tutarudi na roho zetu?? (1987)
3.
Mhusika
mkuu hupewa sifa zisizo za kawaida
Mhusika mkuu
ameumbwa juu ya wahusika wengine anatawaliwa, hivyo ana sifa ya ubabe sifa ya
kuwa kielelezo chenye ukamilifu, yaani kutokana na dosari.
Mfano:
-
Abdallah “ Bwana Musa”
Mhusika mkuu ndiye mshindi hata apitapo katika taabu
na mashaka ya aina gani tunajua hatimaye ni mshindi katika mambo yake. Wahusika
hawa wakuu hutenda na kuendesha mambo yao kama miungu wadogo pasi na kukosea
hata wakawa wasioaminika.
4.
Mandhari
yake huundwa kwa namna ya pekee
Wasanii wa
riwaya pendwa wanatumia mandhari ya kitanzania au kiafrika, lakini sehemu kubwa
ya matukio ama imo ndani ya vichwa vya wasanii au filamu za upelelezi, uhalifu
na mapenzi za kigeni.
5.
Upangaji
holela wa matukio
Katika riwaya
pendwa kuna upangaji wa haraka wa mtiririko wa matukio kiasi kwamba sehemu
zingine zinakosa upatanifu na mantiki.
6.
Kuenzi
jinsia ya kike kama chombo cha anasa na uhalifu.
Riwaya pendwa
hua zina mapenzi ndani yake kana kwamba upelelezi au shughuli inayofanyika
haiwezi kusisimua bila mapenzi, yaani hazina dawa, dawa ya kazi ni mapenzi.
7.
Hutumia
lugha ya kila siku
Mara nyingi
riwaya pendwa hutumia mitindo wa masimulizi na monolojia na kwa kiasi kidogo
dayolojia. Lugha yake ni rahisi ya mazungumzo ya kila siku.
ATHARI ZA RIWAYA PENDWA
1.
Hudumaza
vipaji vya waandishi wetu kwani huiga kila kitu.
Kazi hizi
zinadhihirisha jinsi gani fasihi pendwa za kigeni pamoja na filamu zinaathiri
waandishi wetu. Riwaya pendwa ni matokeo ya mwigo ambayo yameathiri uasili wa
waandishi wetu katika ubunifu kimaudhui na kifani kazi hizi zinashindwa kabisa
kudhihirisha umahiri wa waandishi wetu katika kubuni kazi na sanaa zenye mawazo
yao wenyewe.
2.
Hufundisha
majangili na wahalifu mbinu mpya katika shughuli zao za kufanya uhalifu.
Riwaya pendwa
husababisha uhalifu katika jamii.Mfano: Athari mbaya za tamaduni za kigeni
zinazokuja kwa njia ya filamu na riwaya pendwa ni kama vile kuzuka kwa makundi
ya kiharamia hapa nchini ambayo yanavamia benki, baa, maduka na kuwaibia watu
kwa kutumia silaha mbalimbali.
3.
Hazichambui
kwa undani misingi ya matatizo ya jamii.
Riwaya hizi
haziingi kwa undani katika misingi ya matatizo ya jamii kama kuna tatizo
linalosababisha upelelezi je kiini chake ni nini? Riwaya hizi zinataja juu ya
wivu, tamaa, uovu wa aina hiyo bila kuyahusisha vilivyo mazingira ya jamii (mfano
filamu zinaitwa 24)
AINA ZA RIWAYA PENDWA
1.
Riwaya ya
Mahaba
Ni riwaya yenye
kusawiri uhusiano wa kimapenzi kati ya mvulana na msichana au mwanaume na
mwanamke. Siku hizi zipo zenye kusawiri mapenzi haramu pia.Kwa mfano: Mapenzi
baina ya watu wa jinsia moja (mashoga)
Mfano:
-
J.Simbamwene “Mwisho wa mapenzi” (1972)
-
J.D.Kiango “Jeraha la moyo” (1974)
-
S.M.Komba “Pete” (1978)
-
J.Simbamwene “Kweli unanipenda” (1978)
2.
Riwaya ya
Uhalifu/Ujambazi
Ni riwaya
zinazosimulia vituko vya uhalifu. Mfano: wizi, ujambazi, uuaji, magendo,
utapeli, n.k. Aghalabu polisi huhusishwa katika kuwasaka na kuwadhibiti
wahalifu hao.
Mfano:
-
J.Simbamwene (1972) “Kwa sababu ya pesa”
-
H.Katalambula (1975) “Buriani”
-
L.O.Omolo (1970) “Mtu mwenye miwani meusi”
-
S.J.Chadhoro (1972) “Kifo change ni fedheha”
-
Hammie Rajab (1979) “Ufunguo wa Bandia”
3.
Riwaya ya
Upelelezi
Riwaya hii
huelezea mambo mawili kosa au uhalifu na upelelezi wa uhalifu huo hadi mwalifu
anapopatikana.
Hivyo wahusika wake
ni wahalifu, wadhulumiwa (waliotendewa kosa) na upelelezi wakiwemo polisi.
Mtunzi wa kwanza wa riwaya ya upelelezi nchini Tanzania ni
M.S.Abdallah na
riwaya zake ni:-
-
Mzimu wa watu wa kale (1958)
-
Kisima cha giningi(1968)
-
Duniani kuna watu (1973)
-
Siri ya sifuri (1974)
-
Mwana wa yungi Hulewa (1976)
-
Kosa la Bwana Musa (1984)
Watunzi wengine wa riwaya ya upelelezi ni:-
-
H.Katalambwa na E.Ganzile
-
Simbamwene (1984) “Dimbwi la Damu”
-
E.Ganzele (1980) “Kijasho chembamba”
4.
Riwaya ya
Ujasusi
Ni riwaya ya
upelelezi wa kimataifa majasusi ni wapelelezi wanaotumwa na nchi, serikali au
waajiri wao kwenda katika nchi nyingine kuchunguza siri zao hasa siri za
kijeshi (silaha walizonazo) siri za kisayansi na kiuchumi n.k ili taarifa hizo
ziwanufaishe waliowatuma wakati Fulani hutumwa kwenda kuharibu silaha zao au
nyenzo za uchumi na maadui
Mfano wa riwaya
za ujasusi ni:-
-
E.Musiba (1979) “Kikosi cha kisasi”
-
E.Musiba (1981) “Njama”
-
K.M.Kassani (1982) “Mpango”
-
Mtobwa (1987) “Je tutarudi na roho zetu?”
-
Hammie Rajab (1984) “Roho mkononi”
UHAKIKI WA VIPENGELE VYA FANI
Vipengele vya fani ni kama vile:-
a) Muundo
Muundo hutumika
kueleza mpangilio wa kazi ya kifasihi. Mpangilo huu hujionyesha kwenye maumbo
ya kazi za kifasihi kama hadithi fupi au riwaya. Muundo ni namna au jinsi kazi
za fasihi inavyoonekana yaani umbo lake, ilivyogawanyika. Mfano sura, mfuatano
wa matukio yake (mtiririko wa matukio), msuko n.k. matukio yanaweza kufuatana
kwa njia sahihi nay a moja kwa moja (msuko sahahi) au yakawa na uchangamano
ambao unahusisha kwenda mbele na kurudi nyuma (msuko changamano)
b) Mtindo
Ni jumla ya
mbinu au sifa zinazomwezesha mandishi kuwasilisha ujumbe wake.Mtindo huelezea
jinsi mwandishi anavyoiunda kazi yake.Dhana hii inarejesha sifa maalumu za
mwandishi au mazoea ya mwandishi fulani ambayo hujionyesha kwenye fani yake.
Mazoea hayo ya mwandishi yanapambanua msanii huyu na wenzake kiasi kwamba
msomaji anaweza kusema hii ni kazi inayoandikwa na fulani kwa kusoma tu katika
mtindo wa riwaya kuna vipengele vifuatavyo
·
Matumizi ya Lugha
·
Usimulizi wa nafsi (Msanii anaweza kusimulia
matukio kwa kutumia nafsi ya 1,2 na ya 3)
·
Matumizi ya masimulizi (msanii hutoa masimulizi
yake juu ya mfululizo wa matukio kama yalivyotokea katika kipindi fulani cha
maisha ya wahusika. Msanii husema nini kilitokea jinsi gani kilitokea na mahali
ambapo hayo yalitokea
·
Matumizi ya monolojia ni masimulizi yanayofanywa
na mhusika mmoja katika hadithi au kazi nyingine za kisanaa katika mbinu hii,
hadithi inayojitokeza kama inasimuliwa na mhusika aliye hadithini. Mwandishi
anaonekana kuwa hayupo. Pia hadithi inaweza kujitokeza ikisimuliwa katikaa
nyakati mbalimbali.
·
Matumizi ya dayolojia, ni mazungumzo baina ya
wahusika wawili au zaidi katika riwaya.
·
Matumizi ya tanzu nyingine za kifasihi simulizi
kama vile nyimbo, mashairi, majigambo, hadithi matumizi ya barua n.k.
·
Uteuzi wa wahusika na ujengaji wa mandhari.
c) Wahusika
Ni viumbe wa
sanaa wanabuniwa kutokana na mazingira ya msanii. Hatua ya kwanza katika
utungaji wa kazi ya sanaa ni wazo, wazo kutokana na hali halisi anayoiona msanii
ili kueleza fikra rai au falsafa yake kuhusu kile akionacho anaichukua Lugha na
kuifinyanga.
Wahusika wake
pia huwaweka katika mandhari yatakayomsaidia kuwakilisha hoja zake kutokana na
vitendo, maingiliano na fikra zao kuna wasanii wanaotumia wanyama au wadudu
kama wahusika kwa lengo la kufikisha maudhui fulani kwa jamii au dhamira,
mitazamo yao, kwa jamii.
d) Mandhari
Ni mahali au
makazi maalumu yaliyojengwa na mtunzi na yanamatokeo, matukio mbalimbali ya
fasihi. Mandhari ni mazingira ya wahusika na matukio na inahusu mahali
wanamokaa wahusika na kuingiliana, mazingira ya kijamii na kiuchumi ya wahusika
hao na nafasi zao za kitabaka kufahamu mandhari kunatusaidia kuelewa hisia,
imani, tabia, na maumbile ya wahusika. Mandhari hutupatia mwelekeo kuhusu maudhui.
e) Matumizi ya Lugha
Lugha ina nafasi
kubwa sana katika fasihi kwa kuwa fasihi yenyewe ni sanaa ya lugha. Lugha hiyo
ndiyo nyenzo inayotofautisha fasihi na sanaa nyingine kama uchoraji, ufinyanzi,
udarizi n.k
Lugha ni nguzo
kuu ya kazi za kifasihi na uchunguzi wowote wa kazi hizo hauna budi kuangalia
suala la lugha kazi ya kifasihi
huyawasilisha maudhui yake,
dhamira yake kwa kutegemea lugha. Baadhi ya wahakiki wa fasihi wa kwanza
kuwa fasihi hutumia lugha kwa namna
maalumu, inayozoea lugha ambayo inajulukana kama lugha ya kifasihi. Katika
matumizi ya lugha kuna vipengele kama:-
Tamadhali za
semi, kama vile tashibiha, sitiari, tafsida, tashihisi, kejeli, mubalagha,
dhihaka n.k
·
Mbinu nyingine za kisanaa ni kama vile takriri,
tanakali sauti, mdokezo, tashititi, mjalizo n.k
·
Matumizi ya majali maana ya watu aghalabu huwa
na maana. Wasomaji wa riwaya ni vyema tuyachunguze majina na kuyahusisha na
matukio, dhamira, maudhui na ujumbe wa riwaya husika. Mfano wa riwaya ni “Adili
na Nduguze” (1952) mhusika Adili ni mwadilifu
·
Matumizi ya jazanda au Taswira ni mafumbo ambamo
ndani maana ya kitu imejificha na mfano katika riwaya ya “Dunia mti mkavu”
(1980) mvua inatumiwa kama jazanda na matumizi ya nguvu dhidi ya wananchi.
·
Uteuzi na mpangilio wa maneno. Lugha ni nyenzo
ya kimsingi ya msanii na jinsi anavyotumia huathiri jinsi msomaji
atakavyoisoma, kuielewa na kuathiriwa na riwaya fulani mfano wa matumizi ya
miundo fulani huweza kuathiriwa na maswala yanayozungumzwa.
·
Matumizi ya semi, kama vile methali, misemo, nahau,
misimu mafumbo n.k vipengele hivi vina kazi ya kufafanua maudhui ya kazi ya
fasihi
·
Matumizi ya taharuki. Hii ni mbinu inayotumiwa
na watunzi wa kazi za kubuni ili kutetea hisia na hamu ya msomaji ili kujenga
taharuki. Mtunzi husuka matukio yenye mshikamano na kutiririka kwa muwala ambao
unamfanya msomaji asiitue kazi hiyo hadi kikomo chake kazi yenye taharuki
haichoki kuisoma bali inaburudani ndani yake.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu ni vyema lisadifu
yale yaliyomo ndani ya kitabu. Mfano Je Shetani msalabani (1982) linasadifu
vipi yale yaliyomo ndani ya riwaya hiyo?
UHAKIKI WA MAUDHUI
Maudhui ya riwaya kama kazi
yoyote nyingine ya fasihi yaweza kuwa kitu, mtu, tukio au jambo lolote katika
maisha yetu. Maudhui hudhihirika baada ya kuangalia mambo mengi, mathalani
tukio mbalimbali
Kwa ujumla, maudhui ni muhimu
katika riwaya hasa ndiyo msingi wa riwaya kwa hivyo ni lazima tutegemee mambo
yaliyojitokeza katika ile riwaya yaani maudhui lazima itoke ndani ya riwaya na
sio nje.
Katika bahari hii ya maudhui, hatuna
budi kuichunguza jumuiya iliyozungumzwa.
Matokeo yote katika utunzi ule yatapimwa kwa mujibu wa hali ya jumuiya. Mhakiki
astahili kuichunguza jumuiya ili kuweza kuhukumu kama mtunzi amezingatia kutoa
hali halisi ya jumuiya yake.
Maudhui huwa ni ya aina
mbalimbali kwa ujumla huwa yanalenga migogoro na mikinzano katika jamii. Baadhi
ya maudhui ya kazi zote za riwaya na sanaa kwa jumla ni kama vile:-
-
Mgongano wa tabaka kati ya watawala na
watawaliwa
-
Migongano kati ya wenye elimu na wasiopata elimu
-
Migongano kati ya walio na mali na wasionayo
-
Migongano kati ya mwenye kupigania usawa kati ya
mume ne mke na wenye kupinga usawa huu n.k
Kwa ujumla maudhui hutupa
mafunzo, ujumbe na kutufahamisha falsafa
UHAKIKI WA TAMTHILIYA
Tamthiliya ni utungo wa kidrama
ambao ni aina mojawapo ya maandishi ya sanaa za maonyesho. Ni sanaa
inayoonyeshwa kwa vitendo katika sanaa hii ili mtu apate maadili au utamu
uliomo katika sanaa mpaka asome vitendo vya wahusika waliotumiwa na msanii na
kuvitafakari kwa makini.
Tamthiliya huonyesha matendo ya
wanajamii kwa njia ya kuigiza, maigizo ambayo hatimaye huweza kuonyeshwa kwenye
majukwaa katika sanaa za maonyesho wahusika wake huonyesha matendo waziwazi kwa
njia ya kuigiza. Wausika hawa huzungumzia nafsi zao wakati zamu zao za kuongea
zinapowafikia ili mradi kila mmoja hujaribu kuonyesha waziwazi kuridhika au
kutoridhika kwake kufutana na nafasi anayoiwakilisha katika jamii inayohusika.
Sifa za tamthiliya
Tamthiliya huwa na sifa za
kawaida za sanaa za maonyesho, sifa hizo ni:
i)
Dhana
inayotendeka
Dhana
inayotendeka ni kile kinachoongelewa katika tamthiliya na kinaweza kuwa cha
kubuni au cha kweli. Dhana inayotendeka kwa kawaida huhusu mzozo fulani
unaohusisha pande mbili. Kwa mfano, katika tamthiliya ya “Kilio chetu” (1995), dhana inayotendeka ni “Vita dhidi ya ugonjwa
wa UKIMWI”
ii) Kuwepo kwa mtendaji
Hapa ni wale
wanaotenda ile dhana, yaani wahusika. Ili tamthiliya ikamilike lazima wawepo
wale wanaotenda lile tendo ambao wanaitwa wahusika. Kwa mfano, katika
tamthiliya ya “Mashetani” (Hussein) watendaji wakuu ni: Juma na Kitaru na
watendaji wadogo ni: Mama Kitaru, Baba Kitaru, Daktari, Bibi, Mama Juma, n.k
iii) Kuwa na uwanja maalumu wa kutendea
Tamthiliya
huigizwa sehemu fulani. Hapa kuna jukwaa ambako wahusika wanaingiliana katika
uigizaji wao. Ukubwa au upana wa eneo hilo ni muhimu sio tu kwa athari, bali
pia kwa kuupitisha ujumbe fulani.
iv) Kuwepo kwa watazamaji
Hawa hutazama
dhana inayotendeka. Kwa tamthiliya iliyoandikwa, watazamaji hapa ni wasomaji,
yaani wale wanaosoma kazi hiyo ya sanaa. Kwa hiyo, tamthiliya inaingizwa mbele
ya watazamaji (hadhira).
v) Kusudio la kisanaa.
Hili hutupa
uhakika kuwa kinachotendeka hapo kimedhamiriwa kuwa sanaa na si kitu kingine
kwa mujibu wa kanuni za jamii inayohusika.
vi.
Muktadha
wa kisanaa
Ni sifa nyingine
ya tamthiliya. Muktadha wa kisanaa
unafafanua mazingira ya tukio hilo. Kwa mfano, ugomvi wa walevi kilabuni au baa
si sanaa za maonyesho kwa sababu muktadha wa tukio hilo haulipokei kama sanaa.
vii.
Tamthiliya
ni kazi ya kubuni kama kazi nyingine za kifasihi.
Hii ni muhimu
ili kutofautisha kati ya tendo la dhati katika maisha na tendo la sanaa.
viii.
Matukio
ya tamthiliya huigizwa kwa hadhira hai.
Hapa basi pana
mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wahusika, ambao ni vipaza sauti vya mtunzi
na hadhira.
ix.
Tamthiliya,
hadithi yake imegawika kimuundo katika matendo na maonyesho
Matendo na
maonyesho huonyesha matukio mbalimbali. Kila tendo huzingatia tendo moja kuu
ndani ya mchezo; na hugawanyika katika sehemu ndogo ziitwazo maonyesho. Onyesho
moja kwa kawaida huwasilisha tuko moja linalotendeka mahali pamoja.
x.
Mgogoro
wa tamthiliya huwa mwanzoni
Mwandishi hana
wakati wa kutoa maelezo mengi. Kwa mfano, katika tamthiliya ya “Kifo Kisimani “ ya Kathaka wa Mberia,
mgogoro kati ya Mtukufu Bokona na wanyonge unajitokeza mwanzoni
AINA ZA TAMTHILIYA
1.
Tanzia
Tanzia ni ile inayohusika na mambo yenye uzito,
kifikirika na kihisia katika maisha ya binadamu. Mhusika mkuu ambaye hupewa
sifa nyingi zinazovutia, hukabiliwa na shida au tatizo;tatizo ambalo linaweza
kumkabili mtu yeyote. Lakini namna anavyojitahidi kulitanua tatizo hili, namna
anavyopigana vita kushinda shida inayomkabili, hali ya ulimwenguni na tabia za
binadamu, zinamfanya asiweze kufaulu na mwishowe anashindwa katika vita hii.
Kwa mfano, tamthiliya ya “Mzalendo
Kimathi” (1978) “Kinjekitile” (1969), “Pungwa” (1988), “Kilio cha haki” (1981) ni mfano wa tanzia. Katika tamthiliya zote
hizi mhusika mkuu anashindwa na hata anakufa au anauawa, lakini kifo chake si
kile cha ajali barabarani, bali ni kifo kinachokuja baada ya mapambano marefu,
mapambano yanayochepuza hisia za ushujaa wa binadamu
2.
Ramsa (komedia)
Ramsa ni ile inayokusudiwa kufurahisha au
inayochekeshachekesha na yenye mwisho mwema. Aina hii ya tamthiliya ni kwamba
hutuchorea picha yakini ya maisha yetu, huwa haijaribu kuisawiri picha hiyo kwa
undani na uzito kama uleunaojitokeza katika tanzia. Mfano wa ramsa ni
tamthiliya ya Aliyeonja Pepo (1973)
3.
Melodrama
na vichekesho
Melodrama inafanana sana na tanzia, ingawa mara nyingi
mhusika mkuu wa meleodrama humaliza kwa ushindi, matokeo yake huwa yanasisimua
sana, na mwendo wa msuko wake huwa ni wa harakaharaka zaidi.
Vichekesho, kwa upande mwingine; huwa vinakusudia kutuonyesha vituko
vitakavyotuchekesha tu. Ujenzi wa wahusika huwa ni muhimu, matukio huwa
hayawekewi sababu zozote au sababu za kuturidhisha na msuko wake huwa hauna
uchangamano mzuri. Tamthiliya nyingi zinazoonyeshwa katika televisheni ni
vichekesho.
4.
Tamthiliya
ya kihistoria
Hii ni aina ya tamthiliya inayoelezea tukio fulani la
kihistoria katika jamii fulani. Msomaji wa tamthiliya hii huweza kukutana na
sifa za tanzia pamoja na tamthiliya chekeshi. Mhusika mkuu wa tamthiliya hii
mara nyingi huwa ni shujaa aliyejitoa mhanga kuipigania na kuitetea jamii yake
ili iweze kuondokana na matatizo yanayoiandama, hususani ya kisiasa na
kiuchumi.
Tukio la kihistoria linaloelezewa kwenye tamthiliya
hii huwa limeiathiri jamii husika kwa kiasi kikubwa na hivyo huwa si rahisi
kusahaulika. Vitabu vya tamthiliya vinavyoelezea matukio ya kihistoria ni kama
vile Kinjekitile, Mzalendo Kimathi,
Mkwawa wa Uhehe (1979) pamoja na Tone
la Mwisho.
UHAKIKI WA
VIPENGELE VYA FANI
Uhakiki wa tamthliya kimsingi
huzingatia kanuni na misingi ileile ya uhakiki wa Riwaya. Kuna mambo ya msingi
yz hizo tanzu mbili kufanana na kutofautiana. Mambo muhimu yanayochunguzwa
wakati wa kuhakiki fani ya tamthiliya ni:
a) Utendaji/tukio/tendo.
Kitu muhimu sana
katika ujenzi wa tamthiliya ni tukio. Kutokana na tukio moja, msanii anao uwezo
wa kuibua dhamira mbalimbali. Wataalamu wa taaluma hii husisitiza umuhimu wa
tendo au tukio katika tamthiliya kwa kusema “drama ni tendon a wahusika ni
tendo”
Tendo huanza
pale mhusika anapoulza, “Ninataka nini? Je, lengo langu ni nini?” Kwa kawaida,
aina ya tendo/tukio litaathiri matokeo ya tamthiliya itakayoandikwa.
Mwandishi
mwenyewe anapaswa kuamua juu ya aina ya tamthiliya anayotaka kuandika, lugha,
mtindo, wahusika au mandhari anayotumia. Kwa hali hiyo, uteuzi wa tendo/tukio
la kuandikia tamthiliya lazima uende pamoja na uteuzi mzuri wa vipengele
vingine vya kisanaa kama vile lugha, wahusika, mandhari, n.k.
b) Lugha
Lugha ndiyo
nyenzo kuu ya kazi ya fasihi. Dhamira na maudhui ya kazi ya kifasihi haziwezi
kuwasilishwa na kuwafikia wasomaji bila ya kuwako kwa lugha. Uchunguzi wa
matumizi ya lugha ni muhimu katika uhakiki wa tamthiliya. Je, mambo gani ya
kuchunguza hapa? Hapa tunachunguza:
-
Matumizi ya nahau na misemo.
-
Uteuzi na mpangilio wa maneno/msamiati.
-
Tamathali za semi. Kwa mfano, sitiari,
tashibiha, tafsida, tashihisi, n.k.
-
Mbinu nyingine za matumizi ya lugha. Kwa mfano,
takriri, tanakali sauti, majazi, mdokezo, mjalizo n.k.
-
Matumizi ya taswira na ishara mbalimbali.
-
Matumizi ya mkopo na kutohoa.
c) Wahusika
Katika
tamthiliya, wahusika ni nguzo muhimu sana. Wahusika si watu halisi bali ni watu
wa kubuniwa, wenye sifa muhimu za binadamu. Wahusika huwa na athari kubwa kwa
hadhira kutokana na sababu mbalimbali:-
-
Wahusika wanabebeshwa sifa nyingi tofauti ambazo
zinawakilisha maisha halisi ya watu hai.
-
Mwandishi wa tamthiliya hulazimika kumjenga
mhusika mmoja kwa kuvutia na kumpa mbinu za ki-drama, mambo ya kushangaza au
mbinu yoyote ile anayoichagua mwandishi. Kama tamthiliya inaigizwa jukwaani,
wale waongozaji wa tamthiliya hiyo wanaweza kuathiri mchezo huo pia. Kama
ilivyo katika riwaya, tamthiliya huwa na wahusika wakuu na wahusika wadogo.
d) Muundo wa tamthiliya
Muundo katika
tamthiliya humaanisha msuko wa vitendo na mgogoro kuanzia mwanzo wa mchezo,
kuingia kwenye kilele (upeo) na kuhitimisha kwenye ufumbuzi/masuluhisho ya
mchezo huo (mwisho). Kwa upande mwingine, muundo huonyesha mpangilio wa
maonesho kutoka mwanzo hadi mwisho wa tamthiliya.
Kwa ujumla,
tamthiliya inakuwa na mwanzo unaomwelekeza msomaji kwenye wahusika na migogoro
au mkinzano unaokuwa na kufikia upeo kasha msuko wa aina fulani kabla ya
kufikia ufumbuzi. Muundo unaweza kuwa wa moja kwa moja au muundo wa rejea.
e) Maelekezo ya jukwaani
Haya ni yale
maelezo ambayo huandikwa kwa mabano katika tamthiliya na huandikwa kwa hati ya
mlazo. Je, maelezo hayo hufanya kazi gani?
-
Hueleza mienendo na miondoko ya wahusika.
-
Hutoa maelezo kuhusu wasifu wa wahusika, mavazi,
lugha ya ishara za uso, n.k.
-
Hutoa maelezo kuhusu mandhari au mahali pa
mchezo.
-
Hufafanua matendo mbalimbali yanayotokea
jukwaani.
-
Hueleza wasifu wa mazingira na hata malebaya
wahusika.
-
Hutoa vielekezi vy jinsi ya kuandaa jukwaa kwa
ajili ya uigizaji
-
Hutoa tathmini ya matendo ya wahusika au lugha;
kwa kuonyesha wapi pana kinaya, n.k
f) Mandhari
Madhari hutumiwa
kuelezea sehemu ambako tendo fulani hutendeka. Neon hili huweza kutumiwa kwa
mapana kuelezea pia mazingira ya kisaikolojia ya tendo fulani. Mandhari huweza
kurejelea yale mazingira ya jukwaani na hata wakati wenyewe katika tamthiliya.
Mandhari yanaweza kuwa ya kubuni au ya kweli (halisi)
g) Upeo/kilele
Upeo ni sehemu
ya tamthiliya ambamo taharuki na
matamanio ya hadhira hufikia kilele.sehemu ambapo hadhira huanza kupata
suluhisho la mgogoro uliomo katika tamthiliya. Peo katika tamthiliya ni za aina
mbili upeo wa juu na wa chini
i.
Upeo wa juu ni ule ambao unakidhi
haja za hadhira au jamii inayoipokea. Katika sehemu hii, jamii hupata majawabu
muhimu ambayo tamthiliya huwa imeyachelewesha kwa kutumia mbinu kama vile za
taharuki, mbinu rejeshi, mtindo telezi, n.k. Sehemu hizi mara nyingi husisimua
hadhira kwa hali ya juu sana.
ii.
Upeo wa chini ni ule ambao haukidhi
haja ya wasomaji wa tamthiliya inayohusika. Katika baadhi ya kazi za tamthiliya
upeo wa chini huonyesha udhaifu wa kazi ya sanaa ya msanii anayehusika. Wakati
mwingine upeo wa chini umekusudiwa na msanii na huutumia sana katika hadithi
fupi na lengo kubwa huwa ni kuipa hadhira mshangao.
h) Jina la kitabu na jalada lake
Kama ilivyo
kwenye uhakiki wa riwaya, katika tamthiliya vilevile tunaangalia uhusiano wa
jian la kitabu na yaliyomo katika kitabu, hali kadhalika jalada na uhusiano
wake na maudhui ya kazi inayohusika.
i)
Mtindo
katika tamthiliya.
Tamthiliya
yoyote hupambanuliwa kwa mtindo wake ambao ni mazungumzo au dayolojia.
Mazungumzo/dayolojia hutumiwa kuelezea majibizano baina ya wahusika wawili au
zaidi waliopo kwenye jukwaa au katika tamthiliya maongezi au majibizano si kwa
ajili ya kujibizana tu. Hata hivyo ni muhimu kutambua kuwa, mazungumzo hayo si
mazungumzo tu, lazima yaendeleze tendo kuu katika tamthiliya. Mazungumzo ndiyo
nguzo ya kukuza dhamira na maudhui.
-
Mazungumzo mazuri yana uhalisia na uthabiti.
-
Mazungumzo sio maelezo tu bali yanaonyesha
matendo ya ndani.
-
Mazungumzo mazuri hukuza na kuendeleza tendo kuu
na msuko
-
Mazungumzo sio maongezi yanayovutia tu, lazima
yawe na lengo.
-
Ikiwa mazungumzo yanakuza na kuendeleza tendo
kuu, basi yanatekeleza jukumu la kidrama.
-
Mazungumzo yanaweza kutokea sambamba; kwa kuwako
kwa wahusika kadhaa jukwaani.
-
Mazungumzo na uzungumzi nafsi wa wahusika
huchukuliwa kama sehemu ya mazungumzo ya tamthiliya kwa sababu ya kuliendeleza
tendo kuu.
-
Mazungumzo huweza kuonyesha sifa zisizokuwa za
kawaida katika maongezi ya kila siku ikiwa mwandishi anataka kulimulika jambo
fulani.
-
Mazungumzo ya mhusika yanaweza kuyavunja
mtarajio fulani wa wasomaji au hadhira katika hali fulani kwa ajili ya
kupitisha ujumbe fulani.
-
Mazungumzo ndiyo njia kuu ya kuindeleza hadithi
iliyopo katika tamthiliya kwa kuwa mwandishi hana uhuru wa kutumia mbinu za
usimilizi, isipokuwa katika maelezo ya jukwaani. Tamthiliya yoyote
hupambanuliwa kwa mtindo wake ambao ni dayolojia.
Dayolojia ndiyo
mtindo mkuu wa tamthiliya nyingi.
Dayolojia ni
majibizano baina ya wahusika wawili au zaidi, ambao hujadili jambo fulani.
UHAKIKI WA MAUDHUI
Maudhui
hutujulisha lile lililomgusa mwandishi mpaka kuunda ile kazi yake. Hili
linaweza kuwa ni wazo tu au aliloshuhudia au hata likawa ni jumuisho la mambo
mengi.
Maudhui pia
hutuangazia jinsi jumuiya ya mwandishi ilivyo kwa kuwa fasihi ni kioo cha
jamii. Kupitia maudhui, tunaweza kugundua mazingira ya mwandishi yalivyo.
Mwandishi
hutumia maudhui yake kutudhihirishia mivutano, misuguano na pia maendeleo ya
jamii yake. Maudhui ndiyo lengo la mwandishi. Ndicho chombo chake cha kutuonyesha furaha na matatizo ya jumuiya
iliyomzingira na kuwathiri kimawazo. Kuathirika huku kwa mwandishi hasa
hujitokeza zaidi baada ya kusoma kazi zake nyingi.
Kwa hivyo, basi
maudhui ya kazi yoyote ile ya fasihi yatahusu mambo ambayo yalimsukuma
mwandishi hadi akaiunda kazi ile. Pia yatahusu mafunzo ambayo mwandishi
aliliengea hadhira yake. Zaidi ya haya, kwa kuwa maudhui hayatenganishwi na
mazingira na jamii, itambidi mwenye kuyachambua ayalinganishe na hali ya jamii
ya mwandishi katika vipengele mbalimbali vya maisha. Mathalani, itambidi
achunguze siasa, uchumi, utamaduni, n.k.
Mwanafasihi
mmoja, Senkoro (1981), amefafanua maudhui kama yanayojumlisha mawazo nap engine
mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma mtunzinama msanii hadi akatunga kazi fulani ya
sanaa. Huwa msanii huyo amekusudia hadhira yake ya wasomaji, wasikilizaji ama
watazamaji wayapate mawazo au mafunzo hayo. Kwa hiyo, haya twaweza kuyaita kuwa
ni lengo la msanii kwa hadhira. Mawazo na mafunzo haya hayazuki hivi hivi tu.
Kwa hiyo, kuna umuhimu wakati wa kuyachambua na kujadili yahusishwe na hali
halisi ya jamii.
Mhakiki
anachunguza maudhui ya kazi ya fasihi anaweza kuongozwa na maswali yafuatayo:-
-
Je, wazo kuu la msanii n nini?
-
Je, msanii ametazamia hadhira ya aina gani?
-
Je, kuna kundi lolote analoliunga mkono?
-
Je, kuna kundi analolibeza?
-
Je, msanii ameipa hadhira yake mbinu zipi za
kuitatua migogoro aliyoichunguza?
Katika
tamthiliya ya Kiswahili, kuna dhamira mbalimbali ambazo waandishi
wamezishughulikia kwa mujibu wa Mulokozi (1996). Dhamira hizo ni:-
1. Migongano ya kiutamaduni
Hizi zinonyesha mvutano kati ya utamaduni wa jadi wa
Kiafrika na utamaduni wa Kizungu au kati ya mji na shamba. Suala hili
limejadiliwa kwa dhati zaidi katika
-
E.Hussein “Wakati Ukuta” (1969)
-
E.Hussein “Kwenye Ukingo wa Thim” (1989)
-
P.Mhando “Hatia”
-
J.Ngugi “Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi” (1961)
-
H.M.Liyoka “Dunia Imeharibika” (1978)
-
C.Riwa na M.S.Masanja “Damu Imemwagika na Paulo!
Paulo!” (1976) n.k
2. Matatizo ya kijamii
Kwa mfano, mapenzi, ndoa, ufukara na urithi.
Karibu tamthiliya zote za mawazo
zilihusu kipengele hiki. Kwa mfano, Nakupenda
Lakini…(1957) na Nimelogwa Nisiwe na
Mpenzi (1961), zilizungumzia matatizo ya mapenzi yanayokumbana na vikwazo
vya kiuchumi na vinginevyo. Tamthiliya za Hyslope zilihusu matatizo ya urithi,
rushwa, fitina na tama. Tatizo la mimba limejitokeza katika Hatia, katika Mke Mwenza (1982), tunakutana na tatizo la wivu katika ndoa za
mitala.
3. Dini
Hizi ziko katika makundi mawili:
·
Tamthiliya za kanisani zenye kufundisha dini.
Kwa mfano, zile tamthiliya zinazoingizwa kanisani kukiwa na shughuli au sherehe
fulani.
·
Tamthiliya zinazochambua na kuhakiki asasi na
maundisho ya dini kifasihi. Hizi ni kama vile
-
F.Topan “Aliyeonja Pepo” (1973)
-
Muba-“Maalimu” (1980)
-
Mulokozi “Mkwawa wa Uhehe” (1979).
Hawa
wanaonyesha mikinzano iliyomo ndani ya mafundisho ya kidini, hasa pale
mafundisho hayo yanapogongana na maisha halisi, sayansi au mantiki. Tamthiliya
nyingine zinazoonyesha mgongano huo ni Kinjekitile
(1969) na Njia Panda (1981).
4. Ukombozi
Hizi zinazungumzia juu ya harakati za kumwondoa
mkoloni hapa Afrika. Mfano wa tamthiliya hizo ni Nkwera “Mkwawa Mahinya” katika
“Johari Ndogo” (1968), E.Hussein “Kinjekitile” (1969) na “Mashetani” (1971),
M.Mulokozi “Mkwawa wa Uhehe” (1979), E.Mbogo “Tone la Mwisho” (1981),
P.Muhando, N.Balisidya na A.Lihamba “Harakati za Ukombozi” (1972) na
M.S.Masanja “Damu Imemwagika na Paulo! Paulo!” (1976), n.k. Tamthiliya hizi
licha ya kujadili ukombozi wa kisiasa, vile vile zinajadili ukombozi wa
kiuchumi na kiutamaduni.
5. Ujenzi wa jamii mpya
Baadhi ya tamthiliya zinazojadiliwa zinazojadili suala
hili ni za Ngahyoma “Kijiji Chetu” na M.Rutashobya “Nuru Mpya” (1980). Hawa
walipendekeza marekebisho katika mfumo uliopo. Baadhi wameonyesha tu kuwa mambo
siyo sawa. Mfano: Mbogo- Giza Limeingia (1980)
na Hussein- “Mashetani” (1971) na
wengineo wanalitazama suala hili kitabaka na kuhimiza mapambano ya wafanyakazi
dhidi ya mabepari na ubepari- Kahigi na Ngemera- “Mwanzo wa Tufani” (1976) na Mazrui “Kilio cha Haki” (1981).
6. Uke na matatizo ya kijinsia
Hawa wanaonyesha hali duni ya mwanamke katika jamii ya
sasa, kutafuta sababu za hali hiyo na kupendekeza ufumbuzi. Baadhi ya
tamthiliya hizo ni P.Muhando-“Nguzo Mama” (1982), Ngozi-“Machozi ya Mwanamke”
(1977), Mulokozi-“Mkwawa wa Uhehe” (1979), Mazrui “Kilio cha Haki” (1981), E.Mbogo “Tone la Mwisho” (1981), E.Hussein
“Kwenye Ukingo wa Thim” (1989).
7. Uchawi, uganga na itikadi za jadi
Suala hili limejitokeza katika tamthiliya kadhaa. Kwa
mfano, Mhanika-“Njia Panda” (1981), Mbogo “Ngoma ya Ng’wanamalundi” (1988),
Hussein “Kinjekitile” (1969) na Kitsao “Mfarakano” (1975). Kwa ujumla, uganga
na itikadi za jadi katika tamthiliya hizi husawiriwankama amali muhimu za jamii
zifaazo kutatua baadhi ya matatizo ya kimaisha.
8. Tatizo la ugonjwa wa UKIMWI
Hawa wanaonyesha madhara yanayotokana na ugonjwa wa
UKIMWI kwa jamii. Tamthiliya hizo ni Ushuhuda
wa Mifupa (1990), Mwalimu Rose (2007),
Orodha (2006) na Kilio Chetu (1995).
TOFAUTI KATI YA TENZI NA MASHAIRI
Tenzi na mashairi hutofautiana,
hasa katika vipengele muhimu vifuatavyo:
1. Muundo,tenzi hutumia muundo wa tarbia
tu katika beti zake ambapo mashairi yana uhuru wa kutumia miundo mingine
tofauti kama vile tathlitha, takhmisa n.k
2. Urefu,tenzi kwa kawaida huwa ni ndefu kwa vile hutokea zikiwa katika mtindo
wa usimulizi, na hivyo kuwa na beti nyingi sana ili kkamilisha usimulizi wa
kisa ambapo mashairi kwa kawaida hutumia beti chache
3. Vina,tenzi zina vina vya mwisho tu;
hazina vina vya kati ambapo mashairi yana vina vya kati na vya mwisho.
4. Urefu na mistari ,tenzi mistari yake ni
mifupi; haigawanyiki katika nusu ya kwanza nay a pili, mashairi yake ni mirefu;
na hugawanyika mara mbili, nusu ya kwanza na nusu ya pili (huitwa vipande).
5. Idadi ya mizani, tenzi katika mistari yake huwa na mizani nane tu,
mashairi huwa na mizani 16 katika mistari yake.
6. Kituo,kituo cha tenzi
hubadilikabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Kituo cha shairi kinaweza
kubadilika au kutokubadilika.
KANUNI ZA UTUNZI WA NGONJERA
Ngonjera ni tungo za kishairi
zinazowasilishwa kwa kutumia mazungumzo ya majibizano baina ya watu wawili au
zaidi. Mazungumzo hayo huwa na mjadala wa malumbano yenye lengo la kutoa ujumbe
maalumu kwa wasikilizaji
Katika majibizano hayo, mhusika
mmoja hueleza jambo fulani kwa ubeti mmoja, mhusika wa pili naye hujibu kwa
kupinga au kuunga mkono hoja za mhusika aliyetangulia. Mwishoni mwa ngonjera
wahusika hao huwa wanaondoa tofauti zao na kuwa na msimamo mmoja. Hali hiyo
hutokea pale mhusika mmoja anakubali kulegeza msimamo wake na kukubaliana na
mtazamo wa mwenzake.
Kanuni za utungaji wa ngonjera
hazitofautiani na kanuni za utungaji wa mashairi ya kimapokezi. Ngonjera sharti
iwe na kichwa, beti, vina, mizani, muwala, utoshelezi, kituo na urari wa
mistari ya beti. Ngonjera pia, hutakiwa kutumia lugha ya kisanaa kama ilivyo kwa
mashairi.
Mfano wa ngonjera: Mwenye nyumba na mhitaji
MWENYE NYUMBA: Nakwambieni
jamaa, vya nyumbani mwangu visa,
Mpangaji amekaa, huu mwezi wa tisa,
Mpangaki ana baa, atoapo zangu pesa,
Hivi sasa nimenusa, nataka
kumfukuza.
MHITAJI: Taibu maneno yako, yananipata
kabisa,
Mimi mhitaji kwako, chumba sina
nimekosa,
Sema kodi iliyoko, unayopokea sasa,
Name nitakupa pesa, upate kumfukza.
MWENYE NYUMBA: Kwa hesabu
iliyoko, mimi sipati halasa,
Thelethini ndizo ziko, alipazo Bwana
Musa,
Kinipa sitini zako, atatoka hivi
sasa,
Himiza unipe pesa, nipate kumfukuza.
MHITAJI: Sitini ni hizi hapa, pokea ni
kama posa,
Na kodi hasa talipa, daima bila
kukosa,
Tena Wallahi naapa, kulipa sitakutesa,
Nenda kafanye mkasa, upate kumfukuza.
(Kutoka: Ngonjera za UKUTA, uk 86-87)
TOFAUTI KATI YA NGONJERA NA MASHAIRI
Ngonjera hutofutiana na mashairi
katika vipengele vine, navyo ni wahusika, namna ya uwasilishaji, kituo, na
matumizi ya lugha.
1.
Wahusika,ngonjera
hutumia wahusika wanaojibizana. Wahusika hao wanaweza kuwa wawili au zaidi, ambapo shairi hutumia
mhusika mmoja tu anayezungumza au anayetoa mawazo yake pasipo kujibizana na
mtu.
2.
Uwasilishaji,
ngonjera huwasilishwa kwa njia ya uzungumzaji wa kujibizana, mashairi
huwasilishwa kwa njia ya uimbaji.
3.
Kituo,ngonjera
huwa na vituo tofauti kwa vile kila mzungumzaji huwa na ktuo chake, lakini
shairi huwa na kituo kimoja tu na hata kama kitabadilikabadilika huwa hakilengi
kuonyesha mtazamo wa ukinzani wa mada inayojadiliwa kama ilivyo kwa vituo vya
ngonjera.
4.
Matumizi
ya lugha, ngonjera hutumia sana lugha rahisi lakini mashairi hutumia sana
lugha ya kuzama.