MADA 1 : FASIHI KWA UJUMLA NADHARIA YA FASIHI
MADA
1 :
FASIHI KWA UJUMLA
NADHARIA YA FASIHI
Nadharia ni Imani au kanuni
zinazofuatwa na watu Fulani au jamii katika kushughulikia jambo Fulani mahsusi.
Nadharia za fasihi ni muongozo au
kanuni zinazofuatwa na wataalamu (wanazuoni) mbalimbali katika kuteua fasili/maana
halisi ya fasihi.
Fasihi ni nini?
Wataalamu mbalimbali wamefasili/Maana ya dhana ya fasihi,
maana hizo ni kama zifuatazo:-
1. Fasihi ni kioo cha jamii (maisha),Kwa
maana kwamba mtu anaweza akajitazama akaona taswira yake na akajirekebisha .
Fasihi hii ina udhaifu kwani kioo hakiwezi kumweleza mtu jambo la kufanya ili hali yake iwe bora zaidi
. Pia si sehemu zote takazojiona kwenye kioo(F.Mkwera , 1978)
2.
Fasihi ni hisi,Fasili ina maana kuwa
lazima pawe na mguso fulani wa wahusika ndipo mtu aweze kuandika na kueleza
jambo fulani,’Sengo na kiango Wanasema “hisi
ni kama kuona njaa, baridi, joto, uchovu pengine kuumwa. Hapa swali la
kujiuliza ni kwamba, je fasihi ina maana moja kati ya hiyo? Uamuzi wa kutenda
jambo huja wakati umeguswa?. Je hizo hisia ziko wapi? Je mtu ambaye
haguswi sana moyoni hawezi kuwa mwanafasihi
mashuhuri? Je mwanamuziki ambaye huusifu
uzuri wa mwanamke anaguswa moyoni? Je mwandishi kama Shaban Robert, E. Kazilahabi wameguswa mara ngapi? Vile vile
kivipi waguswe Zaidi ya wengine? (Sengo
na Kiango) hivyo bado fasili hii ina udhaifu
3. Fasihi
ni mwamvuli wa mtu na jamii na utu na maisha ya hadhi na taadhima.Fasihi hii ina maana kwamba mwamvuli humkinga mtu
katika mvua na jua na fasihi huhifadhi na kukinga amali za jamii zisiharibike
maana hii ni nzuri kwani inasisitiza utunzaji wa kile kizuri kwa maana kuwa
jamii inachambua kuwa makini na kuona amali za jamii zinazohifadhiwa. Lakini
swali la kujiuliza ni kwamba jamii
itasaidiwa?
Jamii haitulii kama maji katika mtungi bali hubadilika mara kwa mara kutokana na
nguvu za migongano, hivyo kitu kipya huzaliwa na cha zamani hufa kwasababu
jamii haitulii, hivyo hakuna haja ya kuhifadhi amali za jamii chini ya
mwamvuli. Zipo mila na desturi zilizohifadhiwa na makabila mengi ambazo hazina
nafasi leo. Hali ya mabadiliko ya jamii kutokana na siasa, utawala, uchumi,
elimu, sayansi na teknolojia vyote hivi katika maendeleo vitatoboa mwamvuli na
kuziharibu amali zilizohifadhiwa (Sengo na Kiango 1973)
4.
Fasihi ni sanaa ya uchambuzi wa lugha yoyote
kadri inavyosemwa,inavyoandikwa na kusomwa,Hii ni kweli kuwa fasihi
lazima itumie lugha kwani lugha ndicho chombo muhimu kitumiwacho na fasihi na
si fasihi tu bali taaluma zote hutumia
lugha.Udhaifu wa fasili hii ni kwamba maana hii imejikita katika uchambuzi wa
Lugha kana kwamba hakuna vipengele vingine vinavyochambuliwa katika fasihi
zaidi ya lugha na hii ni sawa na kusema umeme ni waya wa shaba kwa vile umeme umepita
kwenye waya huo.Na hii ni si kweli kwani Hisabati,fizikia au historia si fasihi
ingawa hutumia lugha.
5.Fasihi ni kielelezo cha hisia
za mwandishi juu ya mambo yanayomwathiri yeye,kikundi au jamii nzima anamoishi
na kwamba lengo lake ni kustarehesha au kufunza wasomaji.Fasili(maana)
hii ni nzuri kwa ujumla lakini mapungufu yake ni kwamba imemuwekea mwandishi
kama chanzo pekee cha uumbaji wa Sanaa na hasa akili yake pia maana hii
imetokana na falsafa ya kidhaanifu kwa
kuhusisha uchambuzi wa mambo katika fikra bila
kutazama hali halisi ya maisha ya watu na vitu.
6. Fasihi ni chombo cha utetezi wa maslahi ya
tabaka moja au jingine na kwamba mwandishi ni mtumishi wake anayejijua au
asiyejijua atake asitake mwandishi huyu analengo au dhamira fulani anayotaka
kuionesha.Wasomaji wanaweza kuyakubali au kuyakataa maudhui ya kazi
yake na pengine jamii kufuatana na msimamo juu ya itikadi ya siasa (napengine
amali za jamii) inayotawala kwa kipindi kile
na jinsi mwandishi anavyooanisha maandishi yake na itikadi hiyo.
Fasili au maana hii ni nzuri sana kwani kwa kifupi ni kwamba
fasihi ni mojawapo ya silaha nyingi zinazotumiwa na tabaka moja kutetea maslahi
yake katika mapambano ya kudumu dhidi ya matabaka mengine.
Hitimisho kwa ufupi fasihi ni taaluma inayotumia Sanaa
maalumu ya lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii inayohusika.Fasihi hutueleza
uzuri wa maandishi au mazungumzo ambayo huonekana katika mashairi ,historia za
maisha ya watu ,tenzi,hadithi za kusisimua na insha mbali mbali.
DHIMA YA MWANAFASIHI KATIKA JAMII
Maana ya mwanafasihi/mtunzi wa kazi ya fasihi
Ni mtu yeyote anayejishughulisha na uandishi au utungaji wa
kazi za fasihi yaani fasihi andishi na fasihi simulizi.
DHIMA ZA MWANAFASIHI
1. .Kuelimisha jamii,Katika kuelimisha jamii mwanafasihi ;
(a)Huchambua
na kuchochea umma kuwafumbua macho,hufichua wazo au uchafu uliomo
katika jamii,wagandamizaji hufichuliwa na wagandamizwao hupewa muongozo sahihi
ili waitambue hali yao dhaifu.Mfano”Duka la Kaya”imechambua na kuchochea jamii
ili iweze kupambana na hali mbaya ya maisha.
(b).Kupiga vita kwa hali na mali mazingira yote ya ujinga,maradhi,njaa
na umaskini,Mfano mwandishi wa tamthiliya ya Hawala ya fedha
anapambana na maovu kama vile ujinga na uvivu na Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
anajadili na kupiga vita uzembe na
mengineyo.
(c).Kukosoa jamii,Mwanafasihi anaikosoa jamii katika vipengele
mbalimbali vya maisha.Mfano riwaya ya “ Vuta n’kuvute”inakosoa mila na desturi
zilizopitwa na wakati “Raha karaha na Mashairi ya Chekacheka”mwandishi wa
diwani hizi anaikosoa jamii ya Tanzania kwa mapana kama vile Uongozi
mbaya,kukithiri kwa rushwa n.k.
(d).Kutia hamasa na kumfanya mtu asikate tamaa,Mfano S.Kandoro
anaeleza hamasa ya wananchi waliokuwa wameungana kama “Siafu ili kumtoa nyoka
pangoni katika shairi liitwalo ‘Siafu wamekazana’’.Mwandishi kwa hamasa
amewaita waafrika njooni “au” kwetu ni kwa nini’.Hivyo ni wazi kuwa kazi hizi
zinajitahidi kuendeleza mapambano dhidi ya ukoloni mambo leo.
(e)Mwandisi anadhima kujenga misingi na fikra za usawa na demokrasia
miongoni mwa umma wa wakulima na wafanyakazi,Mwanafasihi huyu
huwatukuza wakulima na wafanyakazi pamoja na amali zao.
(f) Mwanafasihi hueneza mawazo na falsafa za jamii,Kwa mfano
katika shairi na ngonjera za Mathias Mnyapala ametangaza sana siasa ya ujamaa
na kujitegemea kwa kutumia ngonjera za UKUTA 1 & 2 vile vile riwaya kama
vile mfaa na utu,njozi za usiku,ndoto yandaria ,jero si kitu n.k zimetangaza
sana siasa ya ujamaa na kujitegemea hapa nchini Shaban Robert aliwahi kueneza
falsafa juu ya kweli kwa kiasi kikubwa katika mashairi yake.
(g)Mwanafasihi hutoa mwongozo kwa kuikomboa jamii kutoka fikra mbovu za
kugandamizwa,kunyonywa na kuonewa na kujikomboa ili iweze kupata haki na usawa,Mfano
Riwaya ya kiimbila “Ubeberu Utashindwa” na tamthiliya ya E.Mbogo “Tone la
Mwisho” G Husseni “Kinjekitile”
2.Kuburudisha,zipo kazi mbalimbali za fasihi
zinazoburudisha.Msomaji au msikilizaji wa fasihi huburudisha yaani husisimsha
mwili na akili na huvutiwa kihisia na kazi ya fasihi anayoisoma au
kusikiliza.Tabia ya msomaji au msikilizaji huweza kujengwa kutokana na mafunzo
na mifano bora ya matendo ya kuigwa anayoyapata katika fasihi.
3.Kuhifadhi na kurithisha amali za jamii,Amali za jamii ni
pamoja na mila na desturi mtindo wa maisha,Imani, historia jiografia,visasili
na visakale ni urithi wa maarifa ya kijadi kwa mfano tiba, sayansi ya
kilimo,mbinu za uwindaji,ufundi wa aina zote n.k.Amali hizo huweza kuhifadhiwa
na kuendelezwa na mwanafasihi na hivyo kurithishwa kwa vizazi vijavyo.
Kwa mfano tamthiliya ya Kinjikitile inahifadhi mengi kuhusu
hali ya maisha wakati wa ukoloni wa kidachi,Kurwa na Doto (1969) ni
riwaya yenye kuhifadhi japo kwa kejeli,mila,desturi na itikadi za jadi za
waunguja,Riwaya ya Bwana Mnyombokero na Bibi Bugonoka;Ntuhanalwo na
Buliwali iliyoandikwa na Anicet
Kitereza imehifadhi mila,Imani,mtindo wa maisha,ufundi na taaluma mbalimbali za
jadi za wakerewe mengi yaliyoeleza humo siku hizi hayapatikani popote isipokuwa
katika riwaya hiyo, vile vile Mzishi wa Baba ana Radhi (1967)
kinaeleza mila na desturi za wapangwa.
Watunzi hasa nyimbo na visasili
hukoleza pia shughuli za kijadi za kiutamaduni kwa mfano
Ibada,matambiko,sherehe,katika shughuli za aina hiyo nyimbo licha ya kuwa
kiburudisho hubeba ujumbe wenye kuhusiana na tukio hilo.
4.Kudumisha na kuendeleza lugha,Kwa kadri lugha inavyotumiwa na
kufinyangwa na watunzi ndivyo inavyokuwa na kupevuka.Maneno mengi yatumiwayo
leo katika lugha mbalimbali yalibuniwa na kuenezwa na watunzi wa mashairi,riwaya,nyimbo
na tamthiliya katika Kiswahili.Mifano mizuri ni maneno mengi yahusuyo Sanaa ya
ushairi(vina, mizani, beti, mishororo, miwala, tathlitha, takhimisa, tarbia
n.k)
Katika jadi ya ushairi wa kiswahili inadaiwa kuwa ushairi
ulikua ni ghala ya maneno.Washairi walitumia maneno magumu au yasiyokuwa ya
kawaida makusudi ili kuyahifadhi ysipote.katika tamaduni nyingine kazi hiyo
hufanywa na kamusi pamoja na vitabu viitwavyo Hazina ya maneno kwa kuwa
waswahili hawakuwa na kamusi kazi ya kuhifadhi maneno ilifanywa na ushairi.
FASIHI NI SANAA.
Sanaa ni uzuri unajitokeza katika umbo lililosanifiwa umbo
ambalo mtu hulitumia kuelezea hisia zinazomgusa kwa kutoa kielelezo au
vielelezo vyenye maana maalumu.
Aina za Sanaa
i)
Sanaa za Uonyeshi,ni sanaa ambazo
uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa
na uzuri wake kuonyeshwa wakati wowote. mfano uchoraji, uchongaji, kutarizi,
ufinyanzi, n.k. Sanaa ambazo hututolea vitu kama vile picha, vinyago, nguo
zilizotarizwa, vyungu n.k.
ii)
Sanaa za Ghibu,ni sanaa ambazo uzuri
wake haujitokezi kwenye umbo linaloonekana kwa macho au kushikika bali katika umbo linalogusa hisia mfano ushairi,
uimbaji, upgaji muziki, n.k. Uzuri wa sanaa hizi umo katika kuzisikia.
iii)
Sanaa za Vitendo,ni sanaa ambazo
uzuri wake umo katika umbo la vitendo. Uzuri wa sanaa hizi umo katika umbo la vitendo, na ili
kuupata uzuri huu yampasa mtu kutazama vitendo vikifanyika. Umbo hili
linalazimisha kuwepo kwa mwanasanaa (mtendaji) na mtazamaji(Hadhira) wa sanaa
mahali pamoja kwa wakati mmoja, ama sivyo sanaa haikamiliki. Hali hii ndiyo
inayosababisha sanaa hizi za vitendo kuita sanaa za maonyesho kwa sababu
lazima wakati zinapototendeka awepo mtu wa kuonyeshwa, maana uzuri wake umo
katika vitendo vyenyewe.
SIFA ZA SANAA ZA MAONESHO
-
Dhana ya kutendeka (tendo)
-
Mtendaji (fanani)
-
Uwanja wa kutendea/jukwaa maalumu
-
Watazamaji (hadhira).
Hivyo sanaa za maonyesho ni dhana
zilizo kwenye umbo linalotendeka na ili
dhana hii itendeke inahitaji mtu wa kuitenda (mtendaji). Mtendaji huhitaji
uwanja wa kutendea hiyo dhana, na wakati akiitenda hiyo dhana wanakuwepo
watazamaji.
Tanzu za
Sanaa za Maonyesho
i)
Tambiko
Ni sadaka inayotolewa kwa miungu au mahoka, mizimu, pepo, n.k. wakati wa kusalia miungu.
Matambiko yalikuwa na umuhimu mkubwa katika jamii za babu zetu kuliko
siku hizi. Jamii ya asili ilipokabiliwa na matatizo yaliyowashinda kama vile
magonjwa, ukame, au kukosa mtoto, n.k. walifanya tambiko na kusali ili miungu yao
iwasaidie. Wakati fulani walifanya matambiko kwa ajili ya kuomba radhi au kutoa
heshima na shukrani.
Mara nyingi matambiko haya huandamana na kafara kama sadaka inayotolewa
na jamii kwa wahenga wao. Kafara inaweza kuwa ya kuku, kondoo, ng’ombe, mbuzi
au chakula. Katika jamii nyingi za Kiafrika kabla ya ukoloni walitoa kafara ya
binadamu.
Fani katika Tambiko
Ø
Sanaa
Katika tambiko sanaa inayotendeka ni ule ufundi wa kutenda vitendo kwa
ukamilifu kwa kutambika kwa kutumia ufundi wa aina fulani.
Ø
Wahusika
Wahusika wa tambiko ni wale wazee maarufu walioteuliwa na jamii kuendesha
shughuli hizi za matambiko. Si watu wote katika jamii huhusika.
Ø
Mazingira (Mahali)
Tambiko linaweza kufanyika porini, makaburini, njia panda, kwenye mti
mkubwa au mahali popote kutegemeana na aina ya tambiko lenyewe.
Umuhimu wa Tambiko
1) Hujenga
imani kama chombo cha kutatulia matatizo ya jamii. Jamii ya asili ilipokabiliwa
na matatizo ilifanya tambiko na kusali ili miungu iwasaidie kuondokana na
tatizo hilo.
2) Tambiko
husaidia kuendeleza mila na desturi za jamii.
3) Tambiko
hujenga na kuimarisha mahusiano miongoni mwa wanajamii.
4) Matambiko
huiongoza jamii katika mapambano dhidi ya matatizo mbalimbali yanayowakabili.
Hasara za Tambiko
1) Hujenga
dhana potofu katika jamii kwani watu huamini nguvu fulani bila kuwa na uhakika
au uthibitisho wa kisayansi.
2) Huleta
hasara kubwa kwa jamii kwani kafara ya tambiko inahitaji mnyama au chakula,
ambapo watu hutumia hela nyingi kuvipata vitu hivyo.
ii) Mivigha
Ni sherehe zinazofanywa na jamii katika kipindi maalumu cha mwaka. Mivigha
hufanywa kwa lengo la kufundisha jambo
fulani maalumu kwa maisha ya jamii. Sanaa za maonyesho katika kundi hili
zinahusu kuingizwa kwa mwanajamii kwenye kundi la watu wa aina fulani kutoka
kundi la watu wa aina nyingine. Mfano jando na unyago, harusi, kutawazwa chifu,
n.k.Katika jando na unyago mtu hutoka kundi la watoto kuingia kundi la watu
wazima, mtu aliyeoa anatoka kundi la makapera kwenda kundi la waliooa au
kutawazwa chifu, mtu anatoka kundi la raia na kuingia kundi la watawala n.k.
Kutoka
kundi moja kuingia kundi jingine ni hatua iliyopewa umuhimu mkubwa katika jamii
ya asili. Umuhimu huu uliambatana na madaraka mapya yaliyo mkabili mwanajamii
kuingia katika kundi jipya. Kila kundi la watu lilikuwa na madaraka fulani
mbayo kutekelezwa kwake ndiko kulikoleta maendeleo ya jamii .
Fani katika Mivigha
Ø
Sanaa
Sanaa katika mivigha ni ule ufundi wa kutenda kikamlifu na kiufundi
katika kudhihirisha yale yanayotendeka.
Ø
Wahusika
Katika mivigha wahusika ni wa aina tatu:
a) Mtendaji/watendaji,ni
wale wote wanaoshiriki kutenda ile dhana ya kuwatoa watu kutoka kundi moja na
kuwaingiza katika kundi lingine. Vitendo hivyo huambatana na nyimbo, michezo
mbalimbali n.k.
b) Watazamaji
,ni wale wanaoingia kutoka kundi moja na kwenda kundi lingine. Hawa
ndio watazamaji, kwa sababu maneno, nyimbo, vitendo, ngoma, n.k. vyote
vinafanyika ili wao wavione na wajifunze na baadae watekeleze yale
waliyojifunza.
c) Waangaliaji,
ni wale wanaoangalia mambo yanayotendeka bila wao kushiriki katika
kucheza au kuimba au kutoa mafunzo, wanaangalia tu. Hawa kwa upande wa sanaa za
maonyesho sio watazamaji kwa sababu yale yafanywayo hayawasilishwi kwao.
Wakiwepo au wasiwepo bado vitendo vinatendeka tu bila maana yake kupotea. Hawa
wanaitwa “waangaliaji”
(d) Mahali /Mandhari,kwa upande wa mivigha
uwanja wa kutendea ni mahali sherehe zinapofanyika. Inaweza ikawa ndani ya
nyumba, au porini, kwenye uwanja wa nje ya nyumba,milimani au mapanngoni, n.k.
Umuhimu wa mivigha
1)
Mivigha hufundisha umuhimu wa kazi kama vile
kilimo, uwindaji, uhunzi, ufinyanzi, ushonaji, n.k.
2)
Mivigha huhimiza umuhimu wa ujasiri katika
maisha.
3)
Mivigha
hufundisha suala zima la unyumba na malezi kwa ujumla mfano umuhimu wa uzazi na malezi bora.
4)
Mivigha husisitiza umuhimu wa umoja na ushirikiano
katika jamii.
Hasara za Mivigha
1)
Hugharimu pesa nyingi sana ambapo huwaacha wenye
sherehe kwenye madeni makubwa.
2)
Sherehe huweza kusababisha ugomvi, chuki,
dharau, tamaa, n.k.
3)
Huleta ushindani na matokeo yake husababisha
baadhi ya watu wasio na uwezo hujiingiza katika wizi, utapeli, ujambazi, n.k.
3. Majigambo
Ni
masimulizi ya kujigamba kwa mtu kuhusu mambo ya kishujaa aliyopata kuyatenda
maishani mwake. Majigambo hayo husimuliwa katika lugha ya kishairi na
masimulizi yake huambatanishwa na vitendo vya mjigambaji mwenyewe.
Mtambaji anapotamba katika sanaa hii, kwa kawaida huwa na tabia ya
kujivuna au kujitapa kuwa yeye ni bora kuliko wengine wote.
Wakati wa utambaji mazingira humtawala fanani. Pengine fanani alikuwa
akitamba kuonyesha utukufu wake kwa mfalme wao. Au alikuwa akitamba wakati wa
kujiandaa kwenda vitani.
Fani katika Majigambo
Ø
Sanaa
Sanaa katika majigambo ni ule ufundi anaoutenda mjigambaji, kwa kujigamba
kwa ufundi huku akionyesha vitendo waziwazi alivyopata kuvitenda maishani
mwake.
Ø
Wahusika
Hapa kuna mtendaji na watazamaji
·
Mtendaji ,ni yule anayejigamba mbele
ya wenzake, yaani Yule anayejigamba kuhusu mambo yake ya kishujaa aliyoyatenda
maishani mwake.
·
Watazamaji,ni wale wanaotazama vitendo vinavyotendwa na mtendaji.
Ø
Mahali/Jukwaa maalum
Uwanja wa kutendea ni mahali popote ambapo majigambo yanaweza kufanyikia.
Hapa inaweza kuwa kwenye uwanja mkubwa ambapo sherehe hizo zinafanyikia au
kwenye ukumbi.
Ø
Matumizi ya Ngoma katika Majigambo
Majigambo vile vile yaliambatana na ngoma, wakati mwingine ngoma
zilichezwa na katikati ya ngoma mjigambaji mmoja alijitokeza na kuanza
kujigamba, alipomaliza alirudi kucheza ngoma na mwingine alijitokeza tena.
Umuhimu wa Majigambo
1)
Hudumisha utu wa mwanaume katika jamii.
2)
Hudumisha ari ya kuwa wakakamavu, shujaa na
jasiri katika jamii.
3)
Huburudisha jamii yaani mtendaji na
wasikilizaji.
Hasara za Majigambo
1)
Hukuza na kuendeleza ubinafsi kwani fanani
huonekana ni bora zaidi kuliko watu wengine.
2)
Mkusanyiko wa hadhira hutumia pesa au vyakula
kwa wingi, hivyo husababisha umasikini .
3)
Majigambo husababisha unafiki kwa sababu fanani
huonyesha mafanikio yake tu na sehemu alizoshindwa hagusii kabisa, kitu ambacho
si cha kweli katika maisha ya mwanadamu.
4
.Michezo ya Watoto
Ni
mchezo mbalimbali inayochezwa na watoto, na michezo hiyo hufungamana na hali ya
utamaduni, uchumi na siasa ya jamii inayohusika. Mchezo hii husaidia watoto
waweze kujifunza mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii yao. Kwa njia hii
watoto hujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji kama vile kilimo, kupika
chakula, kuwinda, n.k. Vile vile hucheza mchezo wa baba na mama. Hapa mtoto
mmoja anakuwa mama, mwingine baba na wengine watoto. Mchezo huu huakisi mambo
halisi ya nyumbani.
Fani katika Michezo ya Watoto
Ø
Sanaa
Sanaa katika michezo ya watoto wadogo ni ule ufundi wa kutenda vitendo
kikamilifu na kuonyesha ujuzi mkubwa katika utendaji huo
Ø
Wahusika
Kuna watendaji na watazamaji. Watendaji ni watoto wenyewe wanaocheza
michezo hiyo, yaani wavulana na wasichana. Idadi ya watendaji inategemea aina
ya mchezo wenyewe.Watazamaji ni wale wanaotazama mchezo huo. Hapa wanaweza wakawa watoto wenyewe ambao hawachezi
au jamii inayowazunguka watoto hao.
Ø
Mahali
Uwanja wa kutendea michezo ya watoto ni sehemu yoyote itakayochaguliwa na
watoto wenyewe kulingana na michezo unaohusika. Kwa mfano, wanaweza kucheza
uwanjani, chini ya mti, barabarani, chumbani, sebuleni, kando ya nyumba, n.k.
Umuhimu wa Michezo ya Watoto
1)
Huwasaidia watoto wadogo kujifunza mambo
mbalimbali yanayotokea katika jamii yao. Kwa njia hii watoto hujifunza shughuli
mbalimbali za uzalishaji mali, utamaduni na siasa ya jamii yao.
2)
Huwasaidia watoto kujifunza kuwa na ujasiri,
ushujaa, udadisi wa mbinu mbalimbali za kupambana na matatizo yanayojitokeza
katika jamii.
3)
Hurithisha
amali za jamii toka kizazi kimoja hadi kizazi kingine. Michezo hii hurithisha
mila na desturi za jamii fulani kwa kucheza michezo hiyo.
4)
Michezo hiyo huburudisha watoto. Katika kucheza
michezo hiyo, watoto huburudika na kustarehe.
5)
Huwasaidia watoto huimarisha viungo vya mwili
kwa watoto wanaocheza michezo hiyo.
Hasara za Michezo ya Watoto Wadogo
Ø
Watoto huweza kuumizana kutokana na michezo hii.
Ø
Ikiwa wazazi wa watoto hawa wana tabia chafu
kama ile ya kugombana, kutukanana ovyo, vivyo hivyo watoto hawa watarithi tabia
chafu kutoka kwa wazazi wao na wanaweza kuwaambukiza wenzao.
5. Utani
Ni hali ya kufanyiana mizaha
pasipo kuogopa na kushtakiana au utani ni uhusiano wa kutaniana au kufanyiana
masihara ambao ni tofauti na desturi za kutokuheshimiana. Madhumuni yake
makubwa ni kupunguza na kuondoa kabisa uhasama na chuki iliyokuwepo baina ya
makundi fulani ya watu.
Fani katika Utani
Ø
Sanaa
Sanaa katika utani ni ule ufundi
na uwezo wa kutaniana baina ya wahusika wanaohusika na utani huo.
Ø
Wahusika
Katika utani, washiriki wanaweza
kuwa mtu na mtu, familia na familia, kabila na kabila, ukoo na ukoo au nchi na
nchi.
Ø
Mahali
Uwanja wa kutendea inaweza kuwa
mahali popote ambapo utani unaweza kufanyika. Inaweza ikawa kwenye harusi,
msibani, kwenye pombe wakati watu wanakunywa, n.k.
Umuhimu wa Utani
1)
Kutoa maadili na mafunzo fulani kwa jamii.
2)
Kuimarisha umoja na ushirikiano miongoni mwa
wanajamii (kujenga undugu)
3)
Kuhimiza ujasiri na juhudi katika maisha.
4)
Kuhimiza upendo katika maisha.
5)
Hukuza na kuimarisha mila na desturi za jamii.
Hasara za Utani
1)
Husababisha ugomvi katika jamii.
2)
Huleta hasara za kuchukuliana vitu bila malipo.
3)
Huvunja au kuvunjiana heshima miongoni mwa
wahusika.
Kazi za fasihi zipo katika nyanja zifuatazo uchoraji, ususi,
fasihi, ufinyanzi, muziki, ufumaji, utarizi na maonesho.Nyanja hizi za Sanaa
zinaweza kuonyeshwa kwenye kielelezo hiki:-
Ufumaji
|
Muziki
|
Utarizi
|
Uchoraji
|
SANAA
|
Fasihi
|
Ufinyanzi
|
Uchongaji
|
Maonyesho
|
Ususi
|
Kila kipengele cha Sanaa kinatofautiana na kingine kwa umbo na matumizi. Fasihi ni
kipengele cha Sanaa kinachotumia maneno kuumba huo uzuri wa kisanaa.
TOFAUTI KATI YA FASIHI
NA TANZU NYINGINE ZA SANAA
1. Lugha
, kazi zote za kifasihi zinaundwa kisanaa kwa kutumia lugha inayotumika au
kuandikika. Lugha hiyo hubeba maana Fulani (ujumbe) kwa jamii Fulani.Hivyo
lugha ndiyo inayotufautisha fasihi na Sanaa nyingine. Kwa mfano, uchoraji
kipengele chake muhimu kalamu, rangi na kipande cha nguo au karatasi. Ufinyanzi
lugha yake ni udongo , uchongaji wa vinyago lugha yake ni gogo la mti n.k. Fasihi
si maelezo ya kawaida kawaida kama vile matangazo, taarifa ya habari au barua,
fasihi ni maelezo yenye mguso kisanaa. Kazi za kifasihi, huumbwa kimafumbo
hutumia nahau au misemo , methali, tamathali za semi, taswira na ishara mbali
mbali. Kazi za fasihi hufikirisha mtu huweza kutumia akili ili aweze kugundua
kazi ya kifasihi aliyosoma au kuisikia kuwa ina maana gani.
2. Wahusika,kazi
yeyote ya fasihi inakuwa na wahusika wake ambao matukio mbali mbali yanayohusu
jamii huwazungukia wahusika ni watu ama viumbe, waliokusudiwa wawakilishe tabia
za watu katika kazi za fasihi. Kwa upande mwingine wahusika ni muhimu sana
katika kutoa na kufikisha dhamira kwa hadira iliyokusudiwa na mwandishi.
3. Mandhari,
kazi ya fasihi inakuwa na mandhri ambayo huonyesha tukio linaponyika. Mandhari hiyo
inaweza kuwa ya kubuni au ya kweli.Mandhari husaidia kujenga hisia
inayokusudiwa na mwandishi.
4
. Utendaji, utendaji hasa katika
fasihi simulizi hushirikisha fanani na hadhira kwa wakati mmoja. Vile vile
utendaji humfanya fanani aweze kuonyesha baadhi yamatendo katika usimulizi
wake.
5
Fani na maudhui,kazi za fasihi zina
sehemu mbili yaani fani na maudhui na sehemu hizi zinafungamana. Maudhui ni
kile kinachosemwa na fani ni namna kinavyosemwa. Kazi nyingine za Sanaa vile
vile zinafanikisha ujumbe kwa hadhira lakini mbinu na vifaa vinavyotumika ni
sehemu ya fasihi. Kwa ujumla kazi za kifasihi, fani na maudhui yake ni ya hali
ya juu sana ukilinganisha na Sanaa
nyinginezo.
KWA VIPI FASIHI NI
SANAA ?
Usanaa wa fasihi hujitokeza
katikavipengele mbali mbali kama ifuatavyo:-
1.
Mtindo, Sanaa katika fasihi
hujidhihirisha katika namna kueleza jamii (mtindo) katika kueleza jambo
kunakuwa na aina fulani ya kiufundi ambao mwanafasihi huutumia katika kufikisha
ujumbe kwa jamii yake. Taarifa inayotolewa inaweza kufichwa katika fumbo, shairi,
kitendawili, tamthiliya au hadithi.
2.
Muundo (mpangilio maalumu wa matukio),katika
kazi ya fasihi, matukio yanapangwa kiufundi ili yaweze kuwasilishwa vizuri kwa
jamii husika. Matukio hayapangwi ovyo ovyo tu bali yanakuwa na mpangilio
maalumu.
3.
Utenzi mzuri wa lugha iliyojaa nahau,
misemo, methali, tamathali za semi,taswira na ishara mbali mbali
unaonyesha wazi usanaa wa fasihi. Lugha itumikayo katika fasihi ni ya kisanaa.
Ni lugha iliyopambwa na inayokusudiwa kuibua hisia za namna Fulani kwa hadhira
yake. Lugha hiyo inaweza kuchekesha, kukejeli, kubeza, kuchokoza, kutia hamasa
au kushawishi. Matumizi ya lugha yako ya aina tofauti, kuna tamathali za semi,
misemo, nahau, methali. Lugha ya wahusika hasa lahaja zao, uchaguzi wa
msamiati,ufundi wa kutoa maelezo hasa ya wahusika ya mandhari na matukio,
uteuzi wa lugha yenyewe itumiwayo.
4.
Uundaji wa wahusika, wahusika huwa
na tabia zinazotofautiana kati yao. Wanaundwa kiufundi sana na msanii anaweza
kuamua anataka wahusika wanaowakilisha tabia na matendo fulani tu katika jamii
na kwa hiyo atawaumba wahusika hao ili kukamilisha nia na lengo lake.Katika
kutofautisha tabia na hali za wahusika, mwandishi analazimika kutumia mbinu ya
kuwapa majina wahusika wake. Wahusika wanaweza kuumbwa kinafsi au kiakili na
kimwili. Kutokana na ujenzi wa aina hii mhusika huonyesha wasifu wake wa ndani
na nje au anaweza kuonyesha mabadiliko yake kila anapokutana na mazingira
tofauti.
5.
Ujengaji mzuri wa Mandhari, fasihi
hujengwa katika mazingira maalum. Mandhari husaidia sana kujenga hisia
inayokusudiwa na mwandishi. Mandhari yanajengwa kiufundi na mwandishi ili
yasaidie katika kujenga kazi nzima ya fasihi.
MADA NDOGO; MAENDELEO YA FASIHI
CHIMBUKO
LA FASIHI NA SANAA.
Kuna mitizamo mikuu minne ya kiulimwengu inavyotokeza katika suala la
chimbuko la fasihi .Mitazamo hiyo ni
kama ifuatayo;
1.
Mtazamo wa kidhanifu.
Mtazamo wa kidhanifu wa misingi yake katika kudhani tu kwa
hiyo kufuatana na mtazamo huu inaaminika kuwa fasihi na Sanaa kwa ujumla kutoka
kwa Mungu kwa hiyo mwanasanaa huipokea ikiwa imekwishapikwa na kuivishwa na
Mungu huyo.
Mtazamo wa
namna hii ulijitokeza tangu zamani sana wakati wanafalsafa wa mwanzo wa
kigiriki na kinenzi kama vile Socrafes Plato na Anstotle,walipoanza kuingia
katika ulimwengu wa nadharia ya Sanaa. katika uwanja wa nadharia ya
fasihi/Sanaa ya Kiswahili kuna mifano mingi ya wahakiki wa mwanzo waliokuwa na
mitazamo sawa naya wanafalsafa hao mfano F.Nkwera (1970), insha yake ya fasihi inadhihirisha uaminifu
wake wa mawazo ya kidhanifu kwa kudai “fasihi ni Sanaa ambayo huanzia kwa muumba
humfikia mtu katika vipengele mbalimbali -ni hekima ambayo mtu ameshirikishwa
apate kumtambua muumba wake”.
Nkwera ameungwa mkono na wahakiki wengine ambao wanasisitiza
mtazamo huu kwa kusema
“Mtengenezo ya Sanaa huonekana kuwa ni shughuli ya kiungu yenyekumwiga
Mungu ambaye ndiye msanii wa kwanza”
John Ramadhani pia katika makala yake ya fasihi ya Kiswahili
anasisitiza kuwa.
“Zaidi ya kwamba fasihi ni hisia vile vile kitengo cha mtu cha kubaini
kazi ya Sanaa ni uigaji wa Mungu ambaye ndiye mfalme wa Sanaa zote”.
Mawazo haya ya akina Nkwera,John Ramadhani na wengine
yamejaa mwangwi tu wa mawazo yaliyochakaa
ambayo yalikwisha kutajwa na kushughulikiwa
na wahakiki wa zamani tuliowataja kwa msimamo huu wa kidhanifu,Sanaa au
fasihi havijifinyangwi kwa jitihada za akili za mikono ya mtu bali
hupokelewa kutoka katika mikono mbayo mtu hana uwezo wa kuiona.
Udhaifu, mtazamo huu umepotosha maana halisi kwa kuchanganya Imani
na taaluma,pia unajaribu kumtenganisha msanii na jamii yake kwani unatoa
nadharia inayomwinua msanii na kufanya aonekane kuwa mtu wa ajabu aliyekaribu na Mungu kuliko watu
wengine wa kawaida.
2. Mtazamo
wa kiyakinifu
Kulingana na mtazamo huu Chanzo cha fasihi ni sawa na chanzo cha binadamu wenyewe yaani Binadamu
na mazingira yake ndio Alfa na Omega ya fasihi.Iwe kwa kuumbwa au mabadiliko
kuanzia chembe hai ambayo imepitia maendeleo kadha ya makuzi hata kufikia mtu
binadamu alioanishwa na kazi ili kuyabadili mazingira yake.Katika harakati zake
za kujiendeleza kiuchumi kila mara alijaribu hiki na kile alichokiona kinafaa
alikiendeleza Zaidi na kukidumisha katika hali hii hadithi(ngano),methali,vitendawili,nyimbo,tenzi(mashairi)
n.k vyote hivyo vilitungwa na kusimuliwa kwa madhumuni ya kufunza,kukosoa,kuadhibu,kuchokoza fikra
na kuliwaza jamii baada ya kazi.
Sanaa hii ilirithishwa toka kizazi hadi kizazi kwa njia ya
masimulizi na binadamu alivyozidi kujiendeleza kisayansi na kiteknolojia
akahifadhi taaluma hii katika maandishi.Ndiyo sababu tunasema chanzo cha fasihi
ni sawa na chanzo cha binadamu mwenyewe na jinsi binadamu alivyozidi na
atakavyozidi ndiyo taaluma hii ilivyokuwa na kuendelea.
3.
Fasihi inatokana na sihiri,Istilahi
Sihiri’ ina maana ya Uwezo au nguvu ya kimiujiza inayotumiwa na watu
kusababisha matokeo fulani.Watalaam hawa
wanadai kuwa chimbuko la fasihi ni haja
ya mwanadamu kukabiliana na kujaribu
kuyathibiti mazingira yake. Haja hiyo haikutimilika ipasavyo katika hatua zake
za mwanzo za maendeleo ya mwanadamu
kwani uwezo wa kisayansi na kiteknolojia wa mwanadamu wa wakati huo bado
ulikuwa kiwango cha chini sana.Hivyo Imani au miujiza ilichukua nafasi ya
sayansi na ugunduzi.Fasihi ilichimbuka kama chombo cha sihiri hivyo katika kujaribu kuyashinda
mazingira,Mfano Wawindaji walichora picha ya mnyama waliyetaka kumuwinda kabla
ya kwenda kuwinda,kisha walichoma mkuki au mshale kwa kuamini kuwa kitendo
hicho kitatokea kuwa kweli watakapo kwenda kuwinda. Nyimbo walizoimba wakati wa
kufanya sihiri hiyo ndiyo fasihi ya mwanzo.
Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba inachangnya dhima na chimbuko
kwani kutumika kwa nyimbo au ushairi katika sihiri hakuthibitishi kuwa sihiri
ndiyo chimbuko lake.Sihiri ni amali moja tu kati ya amali nyingi za wanadamu wa
mwanzo zilizotumia ushairi.
4.
Nadharia ya Mwigo,Wataalam wa
nadharia wanadai kuwa Fasihi imetokana na mwigo(Uigaji),Katika nadharia hii
inaeleza kuwa mwanadamu alianza kuwa mbunifu kwa kuiga maumbile
yaliyomzunguka.Hivyo sanaa za mwanzo mara nyingi zilijaribu kusawiri vitu
vilivyomo katika mazingira ,mfano wanyama,ndege,miti,watu.
Nadharia hii ni kale,ilianzisha na wataalamu wa kiyunani na walioieneza zaidi ni Plato (Republic) na
Aristotle (Poetics) Plato anahusisha
mwigo na dhana ya uungu.Anaeleza kuwa Maumbile na vilivyomo ni mwigo tu wa
sanaa ya kiungu.Sanaa ya Mwanadamu (Hususani ushairi) ambayo huiga tu mambo
hayo yaliyomo katika maumbile haiwezi
kuwa na ukweli au uhalisi wa kuwa inaiga
maumbile ambayo na yenyewe yanaiga kazi
ya Mungu.Hivyo alishauri aina fulani za ushairi zipigwe marufuku kwa sababu
zinapotosha ukweli.
Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba inasisitiza mno uigaji na kusahau
suala la ubunifu katika sanaa na fasihi.Kama wasanii wangeig maisha na
mazingira tu,sanaa yao ingepwaya sana na haingekuwa tofauti na picha ya
fotografia au maelezo ya matendo ya mazingira na matendo ya kila siku ya
mwanadamu.
FASIHI KAMA CHOMBO CHA UKOMBOZI
Ukombozi ni harakati za jamii yoyote zenye lengo la kuitoa
jamii hiyo kwa nguvu (kwa silaha) au kwa mazungumzo kutoka katika makucha ya
watumwa kisiasa,kiuchumi,kimawazo na kiutamaduni.Jamii inaweza kuwa ni ya
kitumwa kisiasa ikiwa haitakuwa na fursa ya kushika hatamu ya uongozi wao na
badala yake ikategemea uongozi kutoka kwa jamii nyingine jamii itaitwa ya
kitumwa ,kiuchumi,ikiwa haitakuwa na haki ya kuendesha njia mbalimbali za
uzalishaji mali.Pia jamii isiyoweza kufikiri na kuamua wala kutokuthamini
mawazo yake yenyewe na badala yake ikawa katika mgawanyiko wa ibada na itikadi
za kigeni ni jamii isiyo huru kimawazo vile vile jamii haitakuwa huru
kiutamaduni ikiwa itakosa kuthamini uaminifu,uumbaji na ugunduzi wake yenyewe
badala yake ikasujudu amali zilizo na chimbuko kutoka nje.Nyanja za ukombozi wa
jinsi fasihi ya Kiswahili ilivyozitazama mpaka leo
(a)Kisiasa
Ukombozi wa kisiasa unapatikanaje?
Unapatikana tu baada ya kupigania uhuru wa bendera kuwa ndio
wa kwanza kupatikana kwa nchi ambayo iko katika harakati za kujikomboa.Katika
maandishi ya mengi fasihi ukweli huu unajitokeza kwa mfano katika utenzi wa uhuru
wa kenya msanii anatuonyesha
juu ya vita vya kumng’oa mkoloni kutoka katika kiti cha uongozi kwanza
baada ya mwafrika kupandisha bendera yake mambo mengine yafuate vilevile katika
utenzi wa uhuru wa Tanganyika na utenzi wa jamhuri ya
Tanzania “mwandishi anasisitiza uhuru wa bendera ukielezwa kuwa kabla ya
ukombozi wa aina nyingine kufuata.
Kwa hiyo ukombozi huu wa mwanzo (uhuru wa bendera) husababisha
uhuru wa kisiasa wanchi kisha uhuru wa kisiasa huwa ni jukwaa la ukombozi wa
uchumi na mambo mengine,vitabu vingine vinavyozungumzia ukombozi wa kisiasa ni mzalendo,F.E.MK
Senkero) Ubeberu Utashindwa(J.K Kiimbila),Tone la Mwisho(E.Mbogo),Kinjikitile
na Mashetani(E.Hussein),Nuru mpya(R.Rufeshobya)
(b)Kiuchumi
Uhuru wa bendera ni sehemu ya mwanzo tu wa ukombozi wa jamii
nchi zinaweza kujidai ni huru kumbe uchumi wake bado ungali mikononi mwa nchi
nyingine.Nchi nyingi zinazoendelea bado ziko katika harakati hii ya kutaka
kujikomboa kiuchumi.Waandishi wengi wa fasihi ya Kiswahili wamezungumzia sana suala la uchumi katika mfano ‘’Mashairi ya Azimio la
Arusha’’ mwandishi anaonyesha na kushambulia unyonyaji ambao ni adui wa
uhuru wetu.
Vilevile waandishi wanasisitiza kufanya kazi kama njia ya
kuimarisha uchumi.Pia wameeleza kuwa unyonyaji unaweza kukomeshwa kwa
kutaifisha njia zote za uzalishaji mali na kuwa mikononi mwa umma. Pia Katika
tamthiliya ya “Bwana Mkubwa” (J.P Mbonde) mwandishi ameonesha
kuwa kwa sasa shabaha yetu sisi ni kupigana na ukoloni mambo leo ili kupata
uhuru kamili.Ukoloni mambo leo ni kikwazo cha ukombozi wa kiuchumi. Kwa sababu
ya ulegevu wa uhuru wa kisiasa nchi inaweza kuwa na mali lakini ikizembea kufanya kweli ipasavyo
yaweza kufanyiwa njama na ukoloni ndio maana upo umuhimu wa bidii katika kazi
na uzalishaji wa mali kisha linafuata swala la ulinzi wa mali hiyo.
Kuzikomboa njia za uzalishaji mali hakutoshi kwani kila hila
zao zisizoisha wakoloni wanaweza wakatupora mali hiyo tunapaswa kuwa
macho.Katika utenzi wa “Zindiko la ujamaa” mwandishi anaeleza
utaifishaji wa njia kuu za uchumi na uhalali wa utaifishaji huo. Mwandishi
anaonyesha kuwa utaifishaji huo ulifanywa si kwa kuwaona wakoloni kuwa wanadhuluma
bali kama njia moja wapo ambayo itaongeza kwenye ukombozi wa kiuchumi katika
jamii. Lengo moja ni kufuta ubinafsi ambao unapelekea tofauti za kitabaka na
badala yake manufaa ya umma kwa ujumla.
Ukombozi wa kiuchumi si utaifishaji wa njia za uzalishaji
mali tu na wala si kukomesha ukabaila na ubepari bali ni kuongeza juhudi katika
kazi mbali mbali ili kuongeza kiasi cha pato la kitaifa. Waandishi wengine
wanazungumzia ukombozi wa kiuchumi ni kama vile, “Nuru mpya” (G. R. Ruteshubya)
“Mashetani” (E. Hussein) “Sauti ya dhiki” (A. Abdallah) “Kasri ya mwinyi fuad”
(Shafi Adam Shoji) Zetu bora mkulima na wasifu wa sili binti saad(S. Robert).
C) Kimawazo
Ukombozi wa kimawazo ni uhuru wa
mtu katika upeo wa fikra pasipo kutegemea mtu mwingine. Hapa mtu aliye huru awe
anajiamini mwenyewe na awe mtu kama watu wengine. Awe mwenye uwezo wa kuwaza, kuamua
na kutenda, kuchanganua na kupanga kama watu wengine. Mtu aliye mtumwa wa
kimawazo anaweza kufananishwa na mnyama wa kufugwa. Mnyama wa kufugwa daima ni
mtumwa na bwana wake wakati wote huongojea amri kutoka kwa bwana wake.
Maandishi ya fasihi yanazungumziakwa
upana swala hili la uhuru wa mawazo . Katika riwaya ya “Njozi za usiku” dhana
hii ya utumwa wa kimawazo ipo ndani ya watu wengi ambao wanashikilia hasa baada
ya maajilio ya elimu iliyokuja pamoja na ukoloni na ikatumika kwa upotofu.
Katika riwaya hii msanii anaonyesha kuwa wale waliosoma walidharau kazi zote za
mikono, walifikiri kuwa kazi za mikono zinafaa kwa wale ambao hawakusoma. Wao
wanafikiri kuwa kazi ya mtu aliyesoma ni kushika kalamu na kuandika tu au
kuwasimamia ambao hawakusoma.Tangu uhuru wa Tanzania kumekuwa na harakati za
kufutilia mbal ukanganyifu wa namna hii katika mawazo ya watu. Mawazo ya namna
hii ndio yamekuwa yakiwafanya watu wengi wa hali ya chini waamini kuwa uchumi
walionao wamepewa na Mungu.
Vile vile kimawazo watu waliamini kwamba kila jambo
lilitokana na watawala wa kizungu lilikuwa ni bora kabisa. Kwa mfano hata
majina yliletwa toka Ulaya nay a kwetu
ya asili kuachwa. Haya yanajadiliwa wazi katika tamthiliya ya “Bwana mkubwa” (J.
P. Mbonde)
Katika ukombozi wa kimawazo kuna swala la ukombozi wa
mwanamke na swala la dini.Katika suala la ukombozi wa mwanamke watu wengi
wanalitazama kirahisi jambo hili. Wengi wanadhani kuwa mwanamke hana haki ya
kujibagua kutoka kwa wanaume na kujipigania haki yake. Watu hawa hawaelewi ni mapinduzi
gani ambayo hawa wanapigania.Katika fasihi ya Kiswahili Shaban Robert amewatetea
wanawake katika kazi zake mbali mbali ikiemo Diwani ya”Wasifu wa siti binti saad” na
siku ya watenzi wote. Shaban Robert amemtazama mwanamke kama mtu
anayestahili utu kama watu wengine
wowote wale.
Katika kitabu cha “Wasifu wa Siti binti Saad” msanii au
mwandishi anaeleza wazi jinsi jamii ilivyomfanya mwanamke kama chombo cha
kutunzwa utawani ili kiwe kizuri kipate kuwavutia wanaokitafuta na baada ya
kutoka utawani kikawa mikononi mwa mwanaume kikamtegemea kwa hiyo mwanamke
alikuwa ni mtu aliyechukuliwa kama hana wajibu wowote wa maana Zaidi ya kuwa
mtegemeaji. Lakini Shabn Robert aliona kuwa ( uk 23) “Ukimdumisha mtu leo utamuona juu
ya kilele cha utukufu kesho.
Mawazo ya mwandishi ni kwamba wanawake ni vyema watazamwe
katika hali zao za maisha katika ubaya na uzuri kama wanaume. Kuhusu suala la
dini linajitokeza katika riwaya ya “Kichwa maji” ambapo mwandishi anaona
dini imeanzishwa na waoga ambao hutawaliwa na milango yao ya fahamu badalaya
kutawaliwa na akili au bongo zao.
Jambo muhimu katika kumkomboa mtu kimawazo ni kwamba ikiwa
dini itaendelea kuwepo isiwe na mtazamo duni na finyu na athari zake ambazo alikuja
nazo mkoloni akidai kuwa tamaduni zetu ni za kishenzi. Sharti elimu ndiyo iwe
ya kutafakari na kugeuza mfumo wa maisha ya jamii.
Katika dini pia kuna madhehebu mbali mbali ambayo kati yao
kuna uhasama mkubwa, muislamu anadai kuwa yeye ni bora Zaidi kuliko mkristo na
mkristo anajiona yeye ni bora kuliko muislamu. Madhehebu yote haya yamechimbuka
huko mashariki ya kati…….katika kitabu cha “Bwana mkubwa” (uk 18-19”)……kwanini
basi mlitutenganisha katika vikundi vidogo vya madhehebu tofauti kati ya
wakristo na waislamu iwapo Mungu ni yule yule mmoja leo mnatueleza tuombe
kuungana, utengano alianzisha nani? na kwa faida ya nani?........mbona babu
zetu walimwabudu Mungu wao toka zamani kabla ya ujio wa wazungu.
Kwa ujumla dini imechangia kwa kiasi kikubwa sana katika
kudumisha mtu kimawazo na kumfanya atumie fahamu tu kwa hiyo katika kumkomboa
mtu kimawazo sharti suala la dini litupiwe jicho kali fasihi inazidi kuona
jicho lake.
(d)Kiutamaduni.
Kwa ujumla utamaduni wanchi zilizotawaliwa na ukoloni
umeathiriwa sana na ukoloni huo watu wa nchi hizo wanazipoteza kidogo kidogo
thamani za utamaduni zao.Katika fasihi ya Kiswahili ukweli huu wa mambo yameoneshwa
katika kitabu cha “Njozi za Usiku” mwandishi
wa riwaya hii ameelezea namna vijana wote hasa waliosoma hawataki kabisa kusikia
kuhusu mila na desturi zao (uk 51).Hadi leo vijana wengi wakiwa kwao (vijijini)
na ikatokea kwamba kuna ngoma za kienyeji zinachezwa wao husimama mbali au
kando wakitazama kwa dharau mambo yanayotendeka mbele yao.Wanaamini kabisa kuwa
ngoma hizo ni za kishenzi ngoma ambazo zinafaa kuchezwa na watu wasiosoma watu
wasio staarabika.
Katika riwaya ya “Kichwa maji” mwandishi ameonesha
jinsi isivyo kawaida kwa msomi au watu
wenye cheo serikalini kucheza ngoma za kienyeji lakini vijana hao hao mwanzoni
wasomi wenye mwazo ya kisiasa wakisikia sehemu fulani kuna mziki au disko
watajitahidi sana ili wasikose kufika huko.Kwa sasa kuna mtindo mwingine wa
kupaka madawa ya kujichubua ngozi waonekane weupe na wengine huvaa nywele za
bandia au maiti ili kuficha nywele zao za kipilipili.Huu wote ni utumwa wa
kimawazo kwa upande fulani watu hawa wanaamini kuwa uzungu ndilo shina la
maarifa, watu hawa hawajui kwamba kuna wazungu wengine ni maskini zaidi hata
kuliko sisi wenyewe.
Hivyo ili tujikomboe katika nyanja hizi ni lazima tuondoe
ubinafsi, uroho wa madaraka na ulevi wa madaraka hapa nchini.
MADA NDOGO; UHURU WA MWANDISHI/MTUNZI WA KAZI
ZA KIFASIHI
Dhana
ya uhuru wa mwandishi ni pana sana na inatazamwa kwa kuangalia vipengele kadhaa
kama ifuatavyo:
Mosi,uhuru wa mwandishi uko katika utashi,Bila utashi mwandishi
atakuwa mwoga na mwepesi wa kukata tamaa.Atayumbishwa haraka kutoka kwenye
msingi wa falsafa yake na Imani aliyo nayo juu ya mabadiliko yatokeayo katika
jamii.Makombora ya wahakiki na wanasiasa huweza kumyumbisha, lakini kwa
mwandishi mwenye utashi makombora hayo humkomaza.
Baadhi
ya waandishi walioonyesha utashi wao katika Afrika ni ‘Ole Sanyika na Ngugi wa Thiongo
waandishi hawa wameshambuliwa sana na wahakiki, lakini misimamo yao ni ile ile,
pia wamewahi kufungwa na walipotoka kifungoni hawakubadili misimamo yao na
wamekuwa hivyo kwa sababu ya utashi wa falsafa zao katika fasihi ya kiswahili,
waandishi wenye utashi wapo na msingi wa kuwepo kwao ni kutoyumbishwa na
matamshi ya jukwaani na wahakiki ambao hawajapevuka.
Pili,uhuru wa
mwandishi umo katika kuwa na falsafa moja inayoeleweka, Falsafa ifanyayo maandishi ya mwandishi moja yawe na kitu
kijulikanacho kama lengo.Waandishi waliotajwa hapo juu yaani Ole
Sanyika na Ngugi wa Thiongo ndio wanaongoza kuwa na falsafa zao
zinazojulikana. Katika fasihi ya Kiswahili tunaona waandishi wachache wenye
falsafa zao inayojulikana wengi tulio nao wanaandika kufuatana na jambo fulani
au tukio la wakati huo bila kulinganisha leo ataandika juu ya mapenzi, kesho juu
ya upelelezi na kesho kutwa mapinduzi mwishowe anakuwa na orodha ndefu ya
vitabu visivyokuwa na lengo.Waandishi wachache tulio nao ambao wameelekea kuwa
na falsafa inayoongoza maandishi yao ni kama Shaban Robert, G.Kezilahabi na
Mohamedi Suleiman.Bila kuwa na falsafa maalumu ni rahisi sana mwandishi kuyumbishwa.
Tatu,uhuru wa mwandishi umo katika kuitawala vema
Sanaa yake,kama unaandika riwaya na hujui misingi ya Sanaa ya aina hiyo atajikuta
katika kikwazo,utajikuta uhuru wa kisanaa unaweza kujaribu, lakini kazi
utakayoitoa itakuwa hafifu.Kazi nzuri ya kisanaa ni ile inayounganisha vema
ubunifu na uhalisia.Mwandishi akielemea sana katika ubunifu anazua matatizo
mengine kazi ngumu aliyonayo mwandishi ni katika kupata barabara msitari
huo.Mwandishi mwenye vitabu vingi anaweza kuwa na kitabu kimoja tu
kilichoupatia vema mstari huo. Katika fasihi ya Kiswahili waandishi walioupatia
msitari huo tunao ni kama vile Ebraim Hussein,Penina Mhando,Mohamed
Suleiman, C.G Mng’ong’o na J.A.Safari.Msanii anayeweza kuitawala vema Sanaa yake anaunganisha vizuri Sanaa na
maudhui yake.
Mwisho, uhuru
wa mwandishi umo katika lugha anayotumia,ili msanii atawale vema Sanaa yake nilazima
ajue lugha anayotumia.Lugha ndicho kiungo maalumu kati ya Sanaa na kazi ya
kifasihi mwandishi kama hajui vema lugha anayotumia atajikuta hana uhuru wa
kukisema anachotaka kwa hiyo lugha ndiyo nguzo ya nne katika uhuru wa
mwandishi, waandishi wa Kiswahili
waliokwisha kutajwa wanakitawala Kiswahili sanifu,Kiswahili sanifu ndiyo
msingi wa fasihi ya Kiswahili.
Ni
kweli kuna uhuru wa mwandishi?
Uhuru
wa mwandishi ni nini?
Ni ile hali ya mwandishi wa fasihi kuwa huru na wazi katika kutoa
mawazo au hisia zake kwa jamii.Ni uhuru wa kuandika na kulikosoa tabaka lolote
katika jamii bila kupata matatizo yoyote.
Mwandisihi ni nani?
Ni
mtu yoyote atumiaye muda wake mwingi
kuandika na kuzungumzia jamii yake kwa njia ya maandishi.
Je kuna uhuru wa
mwandishi?
Kwa
ujumla uhuru wa mwandishi ni uhuru ikiwa hakufaulu kudhuru tabaka tawala hii ni
kwa sababu suala la uhuru wa mwandishi ni la kitabaka na lilianza pale jamii
ilipogawanyika katika matabaka kwa maana hii uhuru wa mwandishi unaamuliwa na
tabaka tawala
Kuanzia
enzi za utumwa, maandishi ya liyovumbuliwa katika fasihi andishi ya mwanzo ilikuwa ya wateule
wachache tu na wenye vyeo vyao.Hao mabwana, wamwinyi na mabepari walihakikisha
kila mbinu inatumika ikiwemo ya udhibiti wa maandishi ili kuendeleza na kulinda
utawala wao.
Naye B.Goya (1974-78) anasema kuwa mwandishi hana
uhuru kwa vyovyote vile kwa sababu yeye ni tokeo la jamii Fulani, kila jamii
ina mipaka yake ambayo mtu hatakiwi kukiuka kwa vyovyote vile mwandishi huyu
amebanwa na mipaka hiyo asivuke.Pindi avukapo mipaka hiyo atapambana na jamii
hiyo (tabaka tawala) vitabu vya mwandishi huyo vitapigwa marufuku au vitabu
vikitolewa havitanunuliwa au serikali itavikusanya na kuvifanyia mipango
mwingine. Katika Afrika kuna mifano
mingi ya udhibiti wa waandishi mfano mzuri ni mwandishi maarufu wa Kenya Ngugi
wa Thiongo ambaye kazi zake hasa ya “Ngaahika Ndeenda”(I will marry
when I want)- Nitaolewa Nitakapotaka, ilimgombanisha na vyombo vya dola
hadi akawekwa kizuizini, Ngugi ni mwandishi wa kwanza kufichua siri za mfumo wa
kibepari kwa watu wanyonge aliliuzi tabaka tawala la jamii yake ambalo
halikusita kutumia udhibiti na vyombo vyake vya Mabavu.
Baada
ya uhuru vitabu vingi sana viliandikwa kwa kudhibitisha maandishi mbalimbali
uliojitokeza waziwazi E.Kazilabi aliandika riwaya “Rosa
mistika”(1971),kitabu hiki kilipigwa marufuku kisitumike mashuleni na wala
kisiuzwe waziwazi madukani.Ilidaiwa na waliokipiga marufuku kuwa kilikiuka
maadili ya jamii kwa kueleza mambo ya aibu kwa wazi.Sura ya kumi ndiyo hasa
ilitolewa mfano wa uchafu wa kitabu hiki.Udhibiti huo ulifanywa na Wizara ya
Elimu na ulizusha maswali mengi kwa wasomaji.Wasomaji walianza kujiuliza, Je si
kweli uchafu uelezwao katika “Rosa mistika” umo ndani ya jamii ya
Tanzania? Je upotofu na uongozi mbaya ulifuchuliwa na riwaya hiyo hii si upo
kati yetu? Kwa baadhi ya wasomaji ilielekea kuwa suala la uchafu wa maelezo
yatokeayo kitandani baina ya wakuu wa chuo na wanafunzi wao lilitumika kama
kisingizio tu cha kudhibiti ukweli wa masuala mengine nyeti yaliyowagusa
viongozi yaliyowakilishwa na watu kama vile Bwana Maendeleo Deogratius
anayeshiriki katika kuwaharibu vijana.
Vitabu
vingine ambavyo havieleweki vinasema nini, maudhui, falsafa na ujumbe wa
mwandishi ni mashetani(E.Hussein) “Aliyeonja Pepo”(F.Topan) na “Ayubu” Paukwa
theatre Association.Na hivi viko kwa kukwepa mkono mrefu wa tabaka
tawala.
DHIMA YA UHURU WA MWANDISHI.
·
Mwandishi atakuwa huru kuikosoa
jamii au tabaka lolote litakaloenda kinyume na utaratibu wa jamii bila
matatizo.Mwandishi atakuwa huru kuonyesha dhuluma, ukatili na ujangili
unaofanywa katika jamii na tabaka lolote bila matatizo yoyote.
·
Kukiwa na uhuru wa mwandishi, msanii atakuwa na falsafa inayoeleweka pamoja na utashi wake.Hii
itamfanya mwandishi awe na msimamo unaoeleweka.Msimamo wake utamsaidia kuifundisha na kuielimisha
jamii bila uoga.Ataijiulisha jamii hali yake na ataonesha jamii njia za kufikia
haja na kutatua matatizo ya jamii bila uoga
·
Mwandishi atakuwa huru kutoa mwongozo katika jamii kwa
kuikomboa jamii kutoka katika fikra mbovu za kugandamizwa,kunyonywa na kuonewa
na tabaka tawala ili jamii ipate haki na heshima bila woga wa kuliondoa tabaka
ambalo ndilo lenye mamlaka yote katika jamii.
·
Uandishi wa kikasuku utapungua, waandishi au wasanii
huacha tabia ya kuwa vipaza sauti vya tabaka fulani katika jamii, wasanii
makasuku huandika mambo bila kufikiri na kurudiarudia mawazo yaliyokwisha semwa na wanasiasa
majukwaani bila fikra mpya kwa hali hii hupotosha jamii.Hivyo kunapokuwa na
uhuru wa mwandishi wa kutosha hali hii haiwezi kutokea kwa sababu mwandishi
ataandika mambo mbalimbali yanayojitokeza katika jamii na hataweza kujikomba au
kujipendekeza kwa tabaka tawala lenye mamlaka yote katika jamii.
·
Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi fasihi inakuwa chombo cha
kuikomboa jamii kiuchumi,kisiasa, kiutamaduni na kifikra (kimawazo). katika
jamii ya kitabaka fasihi ni mali ya tabaka tawala na hutumia fasihi kutetea na
kulinda maslahi yao.Hivyo inapokuwa mali ya jamii nzima inatumiwa na jamii hiyo
katika kuwakomboa wanajamii wote.
·
Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi, mwandishi anakuwa huru kuichokoza
na kuisukasuka (kuichochea) jamii bila matatizo yeyote.
Mwandishi atachokoza jamii ya wakulima na wafanyakazi kufikiri ili waweze
kulichunguza tabaka tawala kwa jicho pevu na kutoa hadharani uozo uliopo katika
kunyonywa, kupuuzwa,kuonewa, kugandamizwa na kunyanyaswa na tabaka tawala
·
Mwandishi atakuwa huru kuelimisha na kuishauri jamii katika
mambo muhimu yanayojitokeza katika jamii bila woga.Mwandishi ataishauri jamii
kuhusiana na mambo kama vile afya, elimu na ichague mambo gani yanafaa
kuhifadhiwa na yapi hayafai vile vile msanii anakuwa huru kuirekebisha jamii
bila woga kwa kuangalia yapi ni mazuri na yapi ni mabovu yanayotendeka katika
jamii
MADA NDOGO;MASUALA YA KIITIKADI NA DHANA YA UDHAMINI
KATIKA KAZI ZA FASIHI
Maana ya Itikadi
Itikadi ni Imani ya watu au jamii
fulani juu ya kitu fulani. Itikadi kisiasa ni mfumo wa mawazo na Imani ambao
umewekwa na tabaka tawala/ tawaliwa au tabaka lolote lenye nguvu katika jamii
inayohusika ikiwa na lengo la kulinda, kutetea na kuendekeza matakwa na maslahi
yake. Utaratibu huo unaambatana na umilikaji wa njia kuu za uchumi na umilikaji
wa mapato ya ziada yatokanayo na jasho la wazalishaji mali hizo, nyenzo za
kitaaluma kama vile elimu ni nyenzo zisaidia kuimarisha itikadi kama vile dini
vinatumika kutetea utaratibu uliowekwa na tabaka tawala.
Kimsingi kuna mitazamo miwili ya kiitikadi:-
i)
Itikadi inayotetea na kulinda maslahi ya watu
wchache tu katika jamii (utumwa, ukabaila na ubepari)
ii)
Itikadi inayotetea na kulinda maslahi na matakwa
ya watu wengi katika jamii (ujima na ukomunisti).
Vile vile tunapojadili juu ya itikadi katika fasihi na usemi kwa ujumla
pia tunaongelea juu ya utabaka uliopo katika jamii inayohusika . Kuna matabaka
ya aina mbili:-
a)
Tabaka tawala
b)
Tabaka tawaliwa
v
Tabaka tawala linamiliki vyombo vya dola na kwa
kutumia vyombo hivyo na kwa kutumia waandishi, tabaka tawala linaunda,
linaendeleza na kutetea maslahi yake.Vile vile tabaka tawala lina nguvu za
kiakili na za kielimu kwa manufaa yao. Mwandishi kwa ujumla hawezi kuepukana na
mfumo huo wa kitabaka. Tabaka fulani huwadhamini waandishi kwa njia mbali
mbali.
UDHAMINI
Ni hali ya watu au shirika fulani kutoa fedha kwa ajili ya
kugharamia kitu fulani . Mdhamini au wadhamini ni kundi la watu wenye shabaha
zinazofanana wenye kusimama kama ufadhili wa mradi fulani. Katika fasihi hawa ni
wale wanaosimamia makundi maalumu kipropaganda na kiitikadi.
AINA ZA UDHAMINI
Kuna udhamini wa aina
mbili:-
i)
Udhamini wa ushawishi
ii)
Udamini wa nguvu
Ø
UDHAMINI WA USHAWISHI
Ni aina ya udhamini ambao mdhamini huwashawishi na kuwanunua
waandishi au wasanii. Matokeo yake ni kwamba msanii anafungwa na matakwa ya
mdhamini.
Ø UDHAMINI WA NGUVU
Huu ni udhamini unaotumia vyombo
vya dola kama vile jeshi, polisi, magereza kumdhamini mtunzi au mwandishi n.k.Hakuna
hiari katika udhamini wa nguvu, kila kitu kinaendeshwa kama vile mashine tu.
Kwa ujumla mwandishi akidhaminiwa kwa nguvu za serikali huwa kama kasuku
aimbaye na kuutukuza mfumo wa maisha uliopo katika jamii hata kama roho na moyo
wake viko mbali sana na mfumo huo. Lakini msanii anapodhaminiwa kutetea umma, lazima
kutakuwa na madhara yake katika jamii yake inayohusika.
Mwandishi wa fasihi katika kila nchi atakuwa na udhamini
unaolingana na mazingira yake kwa mfano katika nchi ya Tanzania, mwandishi
anaweza kuandika kwa udhamini wa jamii yake inayohusika.Mdhamini anaweza kuwa mtu
binafsi mwenye fedha, shirika, chombo cha serikali, chama fulani au kundi la
mataifa kwa ushirikiano. Pia mdhamini ni mwakilishi wa wenye mamlaka juu yake,
kwa mfano katika serikali yaTanzania chuo kikuu ni mwakilishi wa serikali na
serikali ni mwakilishi wa tabaka tawala. Hivyo msanii anayedhaminiwa na chuo
kikuu ambacho ni chombo cha serikali hatimaye anajikuta anafanya kazi ili
kuendeleza maslahi ya tabaka tawala.
SABABU ZA UDHAMINI
Ø
Uhaba wa fedha kwa waandishi za kuendeshea
shughuli zao za uandishi katika uandishi wa kazi za fasihi. Pesa zinahitajika
kwa ajili ya kununulia karatasi, kalamu, uchapaji n.k.
Ø
Kulinda na kutetea maslahi yawadhamini wao. Hii
inatokea zaidi kama mdhamini ni wa tabaka tawala. Kama tabaka linalo tawala ni
la mabepari kazi za fasihi zitatetea tabaka hilo.
Ø
Kujulikana au kuipendekeza. Baadhi ya waandishi
hudhaminiwa kwasababu ya kutakakujulikaa na kwa upande mwingine mdhamini
anawadhamini waandishi kwa lengo hilo.
Ø
Kupata fedha za haraka. Hawa huandika vitabu
vyenye kujaa wahusika wakuu, mafundi wa kufanya mahaba, kutumia madawa ya
kulevya na kufanya mapenzi kwa kutumia mipira ya kiume na kike bila kujali
staha utamaduni wa jamii yake. Mwandishi anachojali hapa ni pesa na sio matakwa
ya jamii yake.
Ø
Kulazimishwa na tabaka tawala. Waandishi hawa wanakubali
udhamini huo kwa kuogopa udhabiti wa kazi zao na tabaka tawala. Waandishi hawa
wakikataa udhamini huo kazi zao zitadhibitiwa na kupigwa marufuku zisisomwe au
kuchapishwa kabisa.
ATHARI ZA UDHAMINI
Ø
Mwandishi anayedhaminiwa anatakiwa kuandika yale
tu ambayo mdhamini wake anayataka. Msanii hatakuwa na uhuru wa kuandika kitu
chochote na kwa njia anayotaka.
Ø
Mapana ya
uandishi wake kidata, kigiografia na kimaudhui huamuliwa na mdhamini na kutegemea
mahitaji yake na kiwango cha fedha alichonacho mdhamini.
Ø
Ufafanuzi
wa data na maudhui ya kazi ya fasihi lazima ulingane na mtazamo wa itikadi ya
mdhamini.Hii ina maana kuwa mwandishi wa kazi ya fasihi hawezi kufanya
ufafanuzi wa data na maudhui mwenyewe bila kumshirikisha mdhamini.
Ø
Matokeo ya
uandishi wa kazi za fasihi mara nyingi ni mali ya mdhamini na hutumia
kuendeleza maslahi yake mabayo sio lazima yalingane na malengo ya mwandishi.
Ø
Wasanii au
waandishi wengi kutokana na kudhaminiwa huanza kuandika kazi zao kwa
kupenda pesa hii huwafanya waandishi kuwa makasuku kwasababu ya kuandika yale
tu yasemwayo na mdhamini wake bila kuyafanyia uchambuzi wa kina.
Ø
Udhamini
hukuza utabaka katika jamii, hapa tunakuwa na tabaka la wenye nacho
(mdhamini) na tabaka la wasionacho (msanii) mdhamini humnyonya msanii.
Ø
Kuzuka kwa
fasihi pendwa (riwaya ya pendwa).Hapa waandishi huandika kazi zao kwa lengo
la kupata pesa za haraka, huandika riwaya pendwa ambazo zina soko kubwa hapa
nchini hasa kwa vijana na wakati huo huo riwaya hizo hazifunzi lolote jamii Zaidi
ya kuburudisha.
Ø
Huchochea
rushwa, hii ni kwa sababu waandishi wengi wanataka udhamini huo na matokeo
yake wale wanapata udhamini huo lazima watoe chochote (rushwa) kwa mdhamini.
UMUHIMU WA
UDHAMINI
·
Husaidia waandishi chipukizi katika kuchapisha
kazi zao.
·
Husaidia waandishi katika kufanya utafiti wa
mambo mbalimbali yatakiwayo katika Sanaa hiyo ya fasihi.
·
Husaidia jamii kupata kazi mbali mbali za
kifasihi.
·
Husaidia kuleta ushindani wa ubora wa kazi
katika soko la kazi za fasihi.
·
Husaidia kuinua vipaji hasa vya waandishi
chipukizi.